RIWAYA: WAKALA WA GIZA
MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA
SIMU: +255713776843
+255762219759
WHATSAPP: +255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA
______________+18__________________
SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI!
Kamishna Wilfred alikuwa hajatambua kitu hicho kilikuwa nini na alipeleka mkono kukigusa lakini kitu hicho kilimkandamiza haswa, alijikuta akiongeza mwendo na kisha kufunga breki kwa ghafla baada ya kutambua kuwa alikuwa amewekewa bastola kisogoni mwake. Gari yake ilisimama kwwa nguvu sana lakini yule aliyekuwa amemshikilia hiyo bastola hakutetereka hata kidogo, bastola hiyo iliendelea kutulia palepale kisogoni mwake vilevile.
"Nimefunga mkanda kamishna unafikiri nitaaanguka kwa hiyo breki na bastola inidondoke" Alisikia sauti isiyokuwa ngeni ikimuambia
















































