Sunday, December 25, 2016

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE


HERI YA CHRISMAS  KWA MASHABIKI WETU WOTE WENYE  KUSHEREKEA SIKUKUU HIII

RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________



SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE!!!
Alipomaliza kuumwaga unga wote chini alimtazama Richard ambaye alikuwa hana fahamu kisha akaachia tabasamu, alirudisha macho yake kwenye kioo cha simu na kukuta ule unga ulikuwa
umebakia  umechora mchoro maalum wa kufungulia simu amabapo ndiyo ulimfanya aachie tabsamu lake la ushindi wa kufanikiwa kufanya kile alichotaka kukifanya. Bila kupoteza muda aliufuaitisha mchoro  ule kama ulivyotokea kwenye kioo, alikosea kwa mara ya kwanza na ikamlazimu aufuatishe kinyume na jinsi alivyokuwa akiufuatisha hapo awali. Hatimaye simu ikafunguka naa Norbert akaanza kupekua kile alichokuwa akikitafuta kwenye simu hiyo, alitikisa kichwa kama mtu aliyekuwa ameafiki jambo wakati akizidi kuipekua simu hiyo hasa katika sehemu za ujumbe mfupi wa maneno.

____________________________
______________________________________________

      Aliyajua mambo mengi kupitia simu hiyo kutokana na mtumiaji wake kutokuwa makini katika kutumia simu hiyo katika kazi zake, mtumiaji wa simu hiyo alikuwa ametumia sehemu ya ujumbe mfupi wa maneno katika kupanga mikakati yake ya hatari ambayo tayari ilibainika na Norbert. Simu hiyo alifungua mtandao wa whatsapp akapitia sehemu mbalimbali akapekua ambapo alisikia sauti ya mhusika akiwa ameirekodi na kuituma wakati anawasiiana na mwanamke ambaye Norbert hakumtambua, aliporidhika na upekuzi wake alimtazama Richard ambaye hakuwa na fahamu akiwa bado alikuwa kwenye usingizi mzito wa nusu kifo. Akiwa bado anamtazama usoni simu ya Richard ilitetemeka mara mbali kisha ikatulia na ikatetemeka tena, Norbert kwa haraka aliweza kubaini simu hiyo ilikuwa imewekwa mtetemo pasipo kuwa na sauti. Kwa haraka aliitoa simu hiyo akaipokea kisha akaiweka sikioni akatulia kimya akawa anasikiliza, aliweka utulivu  wakati akisikiliza simu hiyo ambapo mengi aliyajua.
                   "Rich mbona kimya vipi hiyo kazi tayari ulivyohakiki?!" Norbert aliposikia swali hilo ndiyo akavibana viungo vyake vya kutolea sauti akaanza kuongea, alikuwa ameshaijua sauti ya mpigaji huyo
                     "ndiyo bosi tayari kazi imekwisha" Norbert alijibu huku akiongea kwa kuiga sauti ya Richard.
                      "welldone boy jioni njoo upokee ujira wako urudi garage ukaendelee na kazi" Sauti hiyo ilimuambia
                    "sawa bosi nashukuru" Norbert alizidi kumuiga Richard.
                       "Hooow! Belinda will dead so soon, Ooops! Rich tutaonana baadaye" Sauti hiyo amabyo ilikuwa ni ya adui mkubwa  wa taifa Mzee Ole ilisikika vyema kwa Norbert na kisha simu yake ikakatwa, Norbert aliizima simu hiyo kisha akaifuta kwa kitamba kuondoa alama zake za vidole zisibaki katika eneo hilo. Aliitumbukiza simu kwenye mfuko wa suruali ya Richard kisha akafuta sehemu zote alizokuwa ameshikakatika nguo za vitu vya Richard halafu tarattibu akaondoka eneo hilo akiwa tayari ameshamaliza kazi yake.

****
    Baada ya mazishi kuisha viongozi mbalimbali wa kitaifa waliondoka eneo hilo kwa zamu kwa mujibu wa ratiba ilivyo, alianza kuondoka Rais Zuber ambaye ndiye alikuwa kiongozi mkuu kisha wengine wakafuatia. Mwishoni kabisa ikawa ni zamu ya viongozi wajeshi kuondoka eneo hilo kwa mujibu waratiba ilivyo, muda huo ndiyo muda ambao Moses alitiliwa shaka na Koplo Himu kutokana na gari aliyobadilisha funguo. Moses aliwahi mapema kwenye eneo la maegesho ya magari akaingia ndani ya gari lile ambalo tayari hadi kibango maalum kilichokuwa na jina la M.. Belinda kilikuwa kimehamishiwa katika hilo gari, baadaye Koplo Himu alifika akasogea hadi ilipo gari hilo akataka kufungua lakini Moses aliwahi kumuona akashusha kioo cha gari  akiwa na uso wa tabasamu.
               "vipi afande umechanganya gari nini?!" Moses alimuuliza huku akimtazama kwa tabasamu.
               "hamna afande labda nikuulize wewe maana nilikuwa nimepaki hili gari hapa" Koplo Himu aliongea akiwa na ameshaanza kuona hali tofauti katika eneo hilo.
              "Aaah afande hebu litazame gari vizuri" Moses alimuuliza Koplo Himu ambaye alianza kulikagua gari hilo na akaridhika lilikuwa ni la Meja jenerali na siyo luteni generali.
              "Dah! Kweli afande nimechanganya si unajua haya magari yanayotolewa maalum kwa  kutumiwa na wakuu  kwenye mazishi yanafanana balaa yaani madereva tunayatambua kwa vibango hivyo vinavyobandikwa jina la mkuu anayepanda gari hilo...vipi  lakini umeshaomba namba ya mtoto yule" Koplo Himu alikubali  baada ya kuona hana sababu ya kupinga kisha akamuuliza Moses kuhusu namba ya yule mwandishi wa habari wa kike.
               "Daha mbona tayari kitambo sana nasubiri kazi iishe nianze kubonga naye" Moses alijibu huku akifungua mlango wa gari baada ya wakuu wa jeshi kuanza kujongea eneo hilo wakiwa wapo tayari kuondoka, Koplo Himu naye aliondoka haraka hadi lilipo gari lenye nyota tatu akiwa  amesimama jirani na gari hilo.

    L.J Ibrahim akiwa yupo mbele ya wakubwa wengine wa kijeshi waliokuwa na kofia tofuati kabisa kutokana na sehemu za jeshi walizopo, kuna aliyekuwa na kofia ya rangi ya kahawia ambaye ni mkuu wa JKT. Pia alikuwepo mwenye kofia ya rangi ya bluu iliyopauka, nyingine zilikuwa zina rangi kijani kibichi ambazo ni za JWTZ kikosi ch ardhi.
  
   M.j Belinda ambaye pekee kati ya mameja jenerali wa jeshi ndiyo alikuwa na kofia ambayo ilikuwa na rangi ya kipekee, yeye alikuwa amevaa kofia yenye rangi nyekundu kwasababu alikuwa ni komandoo huku sehemu ya juu ya mfuko wa kombati la kijeshi kukiwa na mabawa ya ndge mawili yakiyojengwa kwa madini ya fedha. Wakuu wote wa jeshi walisogea mahali yalipo magari yao ya kijeshi, madereva waliwapigia saluti kisha wakawafubgulia milango waingie ndani ya magari hayo. Askari wa usalama barabarani wenye pikipiki walishasogea eneo hilo kwa ajili ya kuwa kitangulizi kwa kila gari kasoro gari la L.J Ibrahima amabaye alikataa kufuatana na pikipiki ya askari yeye peke yake, misafara mingine iliyosalia iliondoka taratibu eneo hillo na ikapiga ving'ora kwa nguvu baada ya kufika barabara kubwa huku kasi ikiongezeka. Hivyo ndivyo L.J Ibrahim aliwapanda  manyunyu ya mvua akavuna mafuriko, hakutambua kwamba mchimba kaburi huanza kuingia yeye kwanza ndiyo achimbe kaburi hilo. Hapo aliingia ndani ya kaburi alilochimba ili azikwe mwingine ambalo lilimgharimu sana, kaburi ambalo nusura limfukie yeye mwenyewe kwa  kuchimba urefu mkubwa bila kujua mchimbiwaji alikuwa anafukia.

****

IKULU, MAGOGONI

    Gari ya kijeshi yenye nyota mbili ilionekana ikisogea kwenye geti la ikulu likiwa limefuatana na pikipiki ya askari wa usalama wa barabarani, geti la ikulu lenye nembo ya taifa lilianza kujifungua kwa mtambo maalum baada ya kuruhusiwa na walinzi waliokuwa wapo  kwenye chumba cha mitambo. Gari hilo liliingia ndani ya ikulu hadi eneo maalum la kuegesha huku king'ora cha pikipiki ya askari kikiwa kimezimwa, mashine ya gari hilo ilipozimwa tu Moses alionekana akishuka kwa haraka hadi kwenye mlango wa nyuma wa gari hilo.
     Alifungua mlango wa gari hilo kisha akapiga saluti huku askari wa pikipiki ambaye alikuwa tayari ameshashuka kwenye pikipiki yake akipiga saluti naye, ndani ya gari hilo M.J Belinda alishuka akiwa mavazi yake ya kijeshi ambayo yalimkaa vyema kiasi cha kulionesha umbile lake la kirembo ambalo ni tofauti na balaa alilo nalo katika mafunzo ya kijeshi. Moses alifunga mlango baada ya kushuka kwake mwanajeshi mrembo kisha akatembea akimfuata kwa nyuma yake hadi eneo maalum ambapo waliwakuta usalama wa taifa wakiwa wanwasubiri wake ajili ya kuwapeleka kuonana na Rais, maofisa hao wa usalama wa taifa walikakamaa kiheshima pasipo kunyanyua mkono kupiga saluti kama sheria ya kijeshi ya nchi hii katika utoaji saluti ilivyo.
     Ndugu msomaji askari yeyote haruhusiwi kutoa saluti ya mkono ikiwa hakukamilika kimavazi kuanzia kichwani hadi miguuni, ikiwa hatakuwa na kofia tu kichwani mwake basi haruhusiwi kupiga saluti ya  mkono zaidi ya kukakamaa huku akiwa amebana mikono. Ndiyo maana hawa maofisa wa usalama wa taifa walikakamaa tu hawakutoa saluti ya mkono kwa Meja jenerali Belinda kwa mujibu wa sheria hiyo ya kijeshi, ni miongoni mwa wanausalama hivyo kufuata taratibu ilikuwa ni lazima kwao.
    Maofisa hao wa usalama wa taifa walimuongoza M.J Belinda na Moses hadi kwenye chumba maalum ambacho Rais Zuber alikuwa akiwasubiri baada ya kuutambua ujio wao, walipoingia ndani ya chumba hicho walimkuta Norbert  tayari ameshawasili  akiwa amekaa kwenye kiti mkabala na Rais Zuber. Wao kwa pamoja walitoa saluti kwa Rais Zuber kisha wakaenda kuketi kwenye viti vilivyo jirani na Norbert kwa upande wa kushoto na kulia, walielekeza nyuso zao mbele ambapo walikuwa amekaa Rais Zuber akiwa na shauku ya kutaka kujua kile walichokuwa nacho wanausalaa hao kutoka vitengo tofauti ndani ya nchi ya Tanzania.
                "naam two star general, Norbert na.....Sajenti Matumbo" Rais Zuber aliongea huku akimtazama kila mmoja katika uso wake na alipofika kwa Moses aliyekuwa na sura ya bandia usoni hakuweza kumjua na alisoma tu jina lililokuwa kwenye kibango maalum ambacho kilikuwa kikining'inia kwenye mfuko wa kombati la juu.
                "Mheshimiwa hapa unaotuona tumeomba kuonana na wewe kutokana na jambo zito ambalo litakaribia kuikumba nchi hii ikiwa tu tutachelewa kulizima, kwanza kabla sijalielezea jambo hilo napenda nikutambulishe kwa huyu unayemfahamu kama Sajenti Matumbo ni Moses  Gawaza nafikiri unamfahamu" Norbert aliongea huku akimtazama Moses ambaye alivua sura ya bandia aliyokuwa ameivaa usoni mwake, Rais Zuber alishtuka baada ya kumuona Moses eneo hilo ambalo hakutarajia kumuona kabisa lakini Norbert alimuashiria atulie.
                "Mheshimiwa nafikiri suala la wewe kuliongoza taifa kwa matakwa ya wananchi tunalitambua na hilo ndiyo linakufanya upendwe na wanachi wote, upendo huu wa wananchi wako pia umekufanya uwe unachukiwa na watu waliokuwa wakitaka ufuate matakwa yao kwa maslahi yao binafsi na si maslahi ya taifa. Nikupongeze kwa msimamo wako juu ya masuala ya kimaendelo ya hapa nchini, sasa naomba nirudi kwenye nia ya sisi kuwepo hapa" Norbert aliongea kwa utulivu mkubwa kisha akasitisha kuongea, aligeuka kushoto akamtazama Moses kisha akageuka kulia akamtazama M.J Belinda  halafu akayarudisha macho yake kwa Rais Zuber.
                "Kabla ya kuanza kutokea mauaji ya viongozi wa dini kwa sumu aliyotengeneza professa hapa, nadhani uliwahi kugoma kusaini mkataba wa kupitisha ushoga na usagaji ndani ya Tanzania, Sasa huo mkataba uliugomea Mheshimiwa ndiyo chanzo cha kutokea haya yote yaliyokuwa yakiendeshwa na mapacha wawili ambao mmojawapo tayari ni marehemu kwa sasa. Watu hawa walipanga njama ya kuwatumia viongozi wa dini katika shghuli zao na walifanikiwa kwa hilo kwa kumtumia Marehemu Askofu Edson  aende kuomba dawa ya Quamtanise kwa Profess Gawaza kwa kigezo cha msaada uliokuwa ukihitajika na waluteri wa Italy, hatimaye walifanikiwa kuipata sumu hiyo hatari ndiyo wakaanza kuitumia kwa kumuangamiza Askofu Edson yeye mwenyewe kisha wakaangamiza viongozi wa dini mbalimbali. Hila zote hizo walitaka wawafanye wananchi wakuone wewe kama kiongozi wa nchi umeshindwa kazi hata kuviamuru vyombo vya dola, hila hiyo waliipitisha kwa mara ya kwanza wakaiona inafaa lakini baadaye waliiona haifai wakaanza kuua viongozi wa jeshi hasa walio kikwazo chao wakitumia hiyo sumu ili waweze kumsingizia Professa Gawaza ni msababishi wapate sababu ya kuweza kuipindua serikali yako" Norbert alieleza kwa kirefu zaidi, maelezo hayo yalimfanya Rais Zuber atikise kichwa kuwa ameyasikia barabara, alisimama kwenye kiti alichokaa akaanza kutembea kulizunguka eneo ambalo lilikuwa na meza na walivyokuwa  wameielekea kwa pamoja. Aliyafikiria maelezo yote aliyopewa kwa upana zaidi kisha akarudi kwenye kiti.
               "Okay! Nimeyaelewa maelezo yako ambayo yapo kama kisa chenye kusimulia, pia ningehitaji ushahidi zaidi ingawa maelezo yako yanafanana na ukweli" Rais Zuber aliongea huku akimtazama kila  mmoja
                "hilo siyo tatizo mheshimiwa, ushahidi ni huu" Norbert aliongea huku akijisachi mfukoni akatoa kadi ya kumbukumbu ya simu iliyokuwa ipo ndani ya kadi kubwa inayoweza kuingia kwenye tarakilishi, alimpatia kadi hiyo Rais Zuber ambaye aliipokea akaenda kuichomeka kwenye kioo kikubwa cha luninga kilichopo mahala hapo. Luninga iliwaka na hapo akapata nafsi ya kushuhudia kile kilichomo ndani ya kadi hiyo ya kumbukumbu, ilimchukua muda mrefu kweza kukimaliza kitu hicho ambacho ndiyo kilimfumbua macho kujua mengi yaliyopo nyuma ya pazia.
      Baada ya kumaliza kuangalia ushahidi huo Rais Zuber alisema, "hongereni sana vijana wangu najivunia kuwa na watu kama nyinyi katika utawala wangu"
      Maneno hayo yaliwafanya kina Norbert waachie matabasamu kisha wakatikisa vichwa kuonesha wapo pamoja na kauli hiyo ya Rais Zuber, walimtazama Rais ambaye alikuwa akijiandaa kutoa kauli nyingine baada ya kuwapa pongezi vijana wake wazalendo waliokuwa wakihangaika uhakikisha nchi ya Tanzania na hata watanzania kwa ujumla hawadidimii.
                       "Sasa basi napenda niwaambie kwamba suala hili nitalifanyia kazi mimi kama amiri jeshi mkuu wa majeshi yote, Mnadhimu mkuu wa jeshi Luteni jenerali Ibrahim Salim ambaye ndiye mkuu pia wa majeshi ya majini nitamfukuza kazi na pia nimshtaki" Rais Zube aliongea kwa hasira
                       "no no hapana mheshimiwa hiyo siyo njia nzuri ya kulitatua hilo jambo kumbuka yule ndiye mwenye mwanajeshi wenye cheo kikubwa nchini, sasa akikaidi amri na kupindua nchi je" Moses aliingiia
                       "Hata kama nisipofanya hivyo ana siku tatu kati ya siku saba alizoniahidi atapindua nchi sasa ya nini tumuache" Rais Zuber alikinzana na kauli ya Moses.
                       "kumfukuza na kumuweka ndani huyu mtu jua wananchi hawatakuwa na imani na wewe hasa hawa vijana wafuata mkumbo wa mitandaoni, utaonekana unataka kuzima balaa la Professa Gawaza hivyo utajiweka pabaya katika uongozi wako mheshimiwa" M.J Belinda aliongea.
                       "okay maneno yenu yana ukweli ndani yake mnanishauri nifanye nini?" Rais Zuber aliwaomba ushauri.
                       "Cha kufanya wewe ni kutulia tu hili suala liacha mikononi mwa N001 yupo kazini tayari, nakuahidi hayo mapinduzi yaliyopangwa hayatatokea kamwe ikiwa N001 tayari ameshaingia kazini" Norbert aliongea
                       "Inabidi aongezewe nguvu huyo N001 akishirikiana na vijana hawa wa TISS nafikiri kazi itakwisha" Rais Zuber aliongea
                      "Worry out mheshimiwa, kila kitu kipo under control" Moses alimuambia
                      "okay nimewaelewa" Rais Zuber alikubaliana nao.
                         "Sawa mheshimiwa sisi hatuna la ziada tunahitaji kuendelea na kazi" Norber aliongea huku akisimama, alipeana mkono na Rais Zuber huku M. Belinda akisimama akatoa saluti na Moses akiwa anavaa tena ile sura ya bandia aliyoivua.
                           "Okay msisite kuwasiliana nami" Rais Zuber aliongea, Norber pamoja na wenzake ndani ya eneo hilo baada ya kufikisha taarifa ile ambayo ilikuwa ni muhimu rais kuipata kwa muda

****

MSASANI
    Pikipiki aina ya bajaj boxer ambayo inatumika kukodishwa kwa ajili ya usafiri alimaarufu kama bodaboda ambayo ilikuwa imembeba L.J Ibrahim  ilisimama mbele ya geti kubwa lenye uzio mrefu, L.J Ibrahim alishuka kisha akampa dereva wa pikipiki hiyo noti mbili za shilingi elfu kumi  akamuashiria aondoke. Dereva wa pikipiki alitii amri akaondoka ndipo L.J Ibrahim aksogelea geti dogo la nyumba hiyo ambalo lilifunguliwa tu alipolikairibia baada ya mlinzi kumuona kupitia mtambo maalum. Aliingia ndani ya nyumba hiyo  bila kumsemesha chochote mlinzi huyo, alikaza mwendo hadi ilipo nyumba  ya kifahari ambapo alifika barazani akausogelea mlango akaufungua kwa nguvu akaingia ndani kama alikuwa anavamia na kupelekea wenzake waliopo sebuleni wake kukaa kitahadhari kisha kila mmoja akamuelekezea bastola wakijua ni adui yao.
                  "kuwa makini  bwana uingiaji gani huo General je tungekupiga risasi" Wilson alimuambia, L.J Ibrahim aliposikia kauli hiyo aliwatazama wote kwa zamu kisha akatikisa kichwa kwa masikitiko
                  "vipi General kwema huko?"  Mzee  Ole  alimuuliza baada ya kumuona ana hali tofauti.
                  "Jamani mambo yameharibika ile gari mliyomtuma Richard akate breki nimefanyiwa mchezo mchezo mchafu nikaipanda mimi" L.J Ibrahim aliongea
                  "what?! Huyu ni N001 tu hakuna mwingine anayeweza kufanya haya" Benson naye alidakia huku akiwa ameuma meno kwa hasira.
                   "dereva wangu akabadilishiwa funguo bila ya kujijua na nyota moja ya gari yangu ikatolewa ikaenda kuchomekwa kwenye gari la Belinda, kwahiyo tukaipanda ile gari"  L.J Ibrahim aliongea
                   "damn! Hivi huyu N001 ni nani mpaka atusumbue vichwa namna hii?!" Santos kwa mara ya kwanza aliongea huku akipiga ngumi yake ya kushoto kwenye tumbo la kiganja chake cha kulia.
                   "Sasa hapa jamani tunapambana na mtu tusiyemfahamu inabidi tuwe makini sana la si hivyo tutaisha wote" Mzee Ole aliongea
                   "First of all inabidi tumfahamu huyu mtu na mtu peke anayeweza kutusaidia tukamjua huyu mtu ni Leopard Queen pekee akahojiwe sasa hivi atakuwa kaamka" Thomas kwa mara ya kwanza aliingilia
                   "Ok nyinyi kamuhojini mimi napumzika hapa nimeumia sana" L.J Ibrahim aliongea kisha akajitupa kwenye kochi, watu wote walikuwa waliokuwa na shauku ya kutaka kumfahamu N001 waliondoka sebuleni hapo wakimuacha pekee akihema. Alikuwa haamini kama ameweza kupona katika janga lile ambalo hadi muda huo lilikuwa limemkumba dereva wake, alibaki akiwa na hasira juu ya N001  ambaye alikuwa akiwafanyia michezo ya kiakili bila ya wao kumjua hata kwa sura jinsi alivyo.

NDANI YA WODI MAALUM YA SIRI
    Josephine alionekana akiwa amekaa kitako kwenye kitanda huku akijifikiria  baada ya kujiwa na wenzake waliokuwa wana shauku ya kujua kile alichokuwa akikijua yeye, ilikuwa ni masaa kadhaa tangu ahamishwe kwenye nyumba hiyo akitolewa kule nyumbani kwake Keko alipokuwa amelazwa kwa dharura. Pia ilikuwa ni saa moja tangu arejewe na kumbukumbu zakevizuri tangu alipopoteza fahamu, uchungu juu ya kumuacha Benjamin katika hali ambayo ilikuwa si rahisi kupona ndiyo ulikuwa umemjia muda wote ambao kumbukumbu zake ziliporudi.

    Alijikuta akilia kutokana na moyo mdhaifu wa kike aliokuwa nao na mapenzi pia aliyokuwa nayo kwa Benjamin, muda huo ambao wenzake walikuja kumuona tangu arudiwe na kumbukumbu zake vizuri, Josephine alipomuona Benson akiwa mzima hana jeraha lolote aliweza kumtambua kama shemeji yake. Aliwaangalia wote waliokuwepo hapo kwa zamu lakini hakuiona sura ya Benjamin mpenzi wake, machozi taratibu yalianza kumtoka akajua mpenzi wake atakuwa amefikwa na jambo  baya baada ya kuanngushwa katika meza ngumu ya kioo na Norbert
                “Benjamin wangu yupo wapi?” Aliwauliza wenzake huku akiwatazama kwa zamu kila mmoja katika nyuso zao lakini hakupata jibu la swali hilo alilowauliza, alianza kuwatazama kila mmoja lakini kila aliyetazamwa alitazama chini kasoro Benson machozi yalianza kumlenga katika macho yake baada ya kutoneshwa habari za kifo cha ndugu yake.
                “Sitamwacha mzima yule mshenzi lazima nimuue kwa mkono wangu” Josephine aliongea kwa hasira akawa anajaribu kuinuka kitandani lakini kizunguzungu kilimzidi akarudi kuketi, maneno hayo yalimfanya Benson aanze kulia kimya kimya akawa anahema kwa hasira huku akimtazma shemeji yake.
                 “Niambie Leopard Queen nani kamuua kaka yangu? N001 ndiyo nani huyo” Benson aluliza huku machozi yakimtoka
                 "N001 ndiye aliyemuua Benjamin wangu" Josphine alijibu huku akijifuta machozi, kisha akaanza kufikiria tukio zimalililotokea hadi Benjamin akauawa na Norbert. Alikumbuka busu refu alilopigwa na Norbert kabla hajapigwa na ktako cha bastola, maneno ya Norbert aliyomuambia yalijirudia kwenye kichwa chake na hapo ndipo hasira dhidi ya Norbert ilipozidi akbaki akihema.
                 "N001 ndiyo nani Leporard Queen hebu tueleze tumjue akalipe ushenzi wote alioufanya" Benson alimsihi Josephine
               "ni Norbert Kaila" Josephine alijibu kisha akaanza tena kulia.
               "what!"  Wote kwa pamoja walijikuta wakiropoka kwa mshangao.

*N001 agundulika
*Rais mpango aufahamu


USIKOSE SEHEMU YA ISHIRNI NA TANO AMBAYO NDIYO ITAKUWA NA MAJIBU YA VITA HIVI VYA WAZALENDO NA WASALITI

*Mtafutanoo

 

No comments:

Post a Comment