RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU!!
Baada ya nusu saa tangu azinduke mlango wa chumba hicho ulifunguliwa na taa zikawaka Norbert aliingia akiwa na uso wenye tabasamu, Scott alipomuona alishutuka sana hadi Norbert mwenyewe akagundua.
"hatimaye upo katika uwanja wangu wa nyumbani Scott" Norbert aliongea huku akitabasamu.
"Kaila wewe ni mwandishi wa habari msafi utanikamataje hapa wakati nimekuja kuisadia nchi yenu" Scott aliongea.
"umekuja kuisadia nchi yetu sio? Kwanini uliingia kinyemela kupitia ziwa Viktoria tena kwa boti iliyoibiwa huko Urusi, si ungetumia njia halali" Norbert alimwambia Scott mambo ambayo yalimfanya ajione amenasa kabisa.
****
"We Kaila unataka nini kwani?" Scott aliuliza swali ambalo halina maana kwa Norbert.
"nataka niilinde nchi yangu dhidi ya mabazazi" Norbert aliongea huku akitabasamu.
"sasa mabazazi wenyewe mi mmojawapo au unanipakazia tu?" Scott aliuliza kwa jeuri.
"wewe ni bazazi mdogo nsmuhitaji yule bazazi mkubwa" Norbert aliongea
"Sijui usemacho wewe" Scott aliongea kijeuri kwa mara nyingine
"Kiufupi namuhitaji Brown Stockman aliyewatuma" Norbert aliongea kwa ustarabu huku akimtazama Scott kama anaongea na rafiki yake wa karibu.
"Simjui huyo" Scott aliongea kwa kujiamini.
"hapo umekaa kwenye kiti cha umeme na nikiwasha swichi tu utapigwa shoti mpaka ufe, ukweli wako ndiyo uokozi wako Scott" Norbert aliongea huku akimsogelea Scott.
"Sina ukweli mwingine zaidi ya huu niliokwambia" Scott aliongea kwa kujiamini huku akimtazama Norbert ambaye alikuwa akitabasamu tu wakati wote.
"ohoo! Vizuri basi ngoja tuone utaongea nini la ziada" Norbert aliongea akiwa ameisogelea swichi iliyopo ukutani halafu akaiwasha, Scott alianza kupigwa shoti hadi akawa anajihisi anakaribia kufa lakini hakutaka kuuunyanyua mdomo wake kutamka neno lolote. Shoti ilipozidi kuwa kali ilimbidi atafute mbiu apumzike na adhabu hiyo, alipiga kelele kuashiria yupo tayari kusema ukweli ili Norbert azime swichi ya umeme. Swichi ilipozimwa alijiinamia akihema kwa muda na alipoinua kichwa alitukana matusi mazito ambayo hayawezi kusitirika hata kwa turubai, matusi hayo yanaweza kumfanya mtu yoyote wa kawaida achukie ingawa kwa majasusi kama Norbert ulikuwa ni wimbo tu ambao ulihitajiwa kubadilishwa tu masikioni mwao. Matusi yote ya Scott yalimfanya Norbert atabasamu tu kisha akamsikitikia kutokana na jeuri yake, aliamua kutoka nje ya chumba hicho kwa muda mfupi na aliporejea alikuwa amebeba nyaya zinazotumika kuchaji betri za gari ambazo huwa na vibanio vya chuma sehemu inayopitisha umeme. Akichomeka zile nyaya kwenye umeme kisha akamsogelea Scott hadi mbele yake, tabasamu pana ndiyo lilikuwa limeutawala uso wa Norbert na mikunjo ya hasira za maumivu ndiyo ilikuwa imeutawala uso wa Scott hadi akawa mwekundu kutokana na weupe wake wa kizungu. Norbert alimvua nguo zote Scott na akabaki kama alivyozaliwa kisha akaweka vibanio vile vya kuchaji betri la gari kwenye kifua cha Scott zilipo chuchu zake za kiume, shoti kali iliingia kwenye mwili wa Scott na akajikuta akipiga makelele kama mtoto mdogo huku akimsihi Norbert amuachie lakini hakuachiwa aliendelea kupigwa shoti vilevile. Alipokuja kuwa ameanza kuishiwa nguvu na mapigo ya moyo yalikuwa yakimuenda kwa kasi sana, pamoja na kuwa katika hali hiyo bado aliendelea kuporomosha matusi mazito tu baada ya kuachiwa.
"Sasa ngoja nizibane hizu korodani zako ili ujue unacheza na mtu mwenye roho ya aina gani" Norbert aliongea huku akigusa korodani za Scott na sehemu ya juu ya kibanio na kupelekea shoti imshtue sana hadi akawa anamtazama Norbert kwa macho yaliyojaa uoga, Norbert alinyanyua vibanio vya zile nyaya akavifungua akawa anavisogeza kwenye korodani ili abane. Alipofikisha vibanio jirani na korodani tayari Scott alikuwa ameshajisaidia haja ndogo bila ya kujitambua na alikuwa akitetemeka sana.
"haya ongea ukweli mwenyewe" Norbert alimwambia akiwa amesitisha zoezi lake la kutesa, Scott bila ya kuleta ubishi alitiririsha maelezo ambayo yalikuwa hayajulikani na Norbert zaidi ya kuwa siri katika kundi lao.
****
Siku hii ilikuwa ni siku ya kutokwenda shule kwa Moses na ilikuwa siku ambayo alijaa majuto kwa kile kilichomkuta siku iliyopita, aliamua abaki chumbani tu akiwa na mawazo na hofu ya kuharibika kwa penzi lake kwa kitendo alichokifanya Annie cha kufanya nae mapenzi bila ya ridhaa yake baada ya kumlewesha. Kutokana na kitendo hicho alimuona Annie kama ni bundi aliyetumwa kuja kumletea mkosi katika mapenzi yake na alitokea kumchukia zaidi ya anavyomchukia kwa dhamira yake ya kutaka kumfanya mtumwa wa ngono. Hakuwa tayari kwa jambo hilo na moyoni alikuwa anawaza jinsi ya kumuepuka Annie na hakutaka kuwa naye kabisa, mbinu zote za kumkomesha Annie zilimuishia na ikabidi aombe ushauri kwa rafiki yake kipenzi ambaye ndiye angeweza kumsaidia katika hilo. Aliamua kumpigia simu Hilary na kumtaarifu kuwa ana tatizo kubwa na alihitaji ushauri wake kwa namna yoyote, Hilary ambaye naye hakwenda shule kwa usalama wake akumuahidi atakuja hapo kwao ili amsaidie kwa tatizo linalomkabili. Ahadi ya Hilary kwa rafiki yake ilikuwa ya kweli na aliitimiza kwa kufika nyumbani kwao Moses akiwa na mlinzi wake binafsi aliyepewa na baba yake, Moses alimueleza kila kitu Hilary bila kumficha chochote juu ya kilichomtokea.
"Mmmh! Mwana hapo kweli huyu malaya kashika mpini wewe umeshika makali, ukileta ubishi unakatwa" Hilary aliongea huku akisikitika kwa jambo alilofanyiwa Moses.
"Ni kweli man ndiyo maana nikakuita wewe unipe ushauri niondokane na adha hii" Moses aliongea akionesha wazi amechanganyikiwa na machozi yalikuwa yakimlenga machoni mwake.
"Usihuzunike mshkaji wangu kama mimi mtu wako wa ukweli wa toka tupo baby class St'marry, sasa hivi tupo wote form six siwezi kukuacha nitaendelea kuwa nawe tu. Sisi marafiki wa kuzikana haina budi kusaidiana" Hilary alimfariji Moses kwa maneno yaliyomfanya atulie na kuchanganyikiwa kwake kukaisha hapohapo.
"we unanishauri nifanyaje maana sitaki kumpoteza Beatrice hata kidogo?" Moses alimuuliza.
"kama yeye kamwaga mboga sisi tunamwaga ugali tuone nani mjanja" Hilary aliongea kimafumbo.
"enhee! Hebu funguka bwana nikuelewe" Moses aliongea.
"ujue huyu anataka mashindano ya kupuliza matarumbeta wakati anauguza mgonjwa wa presha ngoja tushindane naye, yeye akipuliza tarumbeta tu kaua mgonjwa wake" Hilary aliongea kwa mafumbo zaidi ambayo safari hii yalieleweka kwa Mosea na kumfanya atabasamu na huzuni ikamuondoka kabisa.
"mwana hapo umetoa sumu kali inabidi nimsambazie kabisa" Moses aliongea huku akitabasamu.
"Yaani yule gashi pamoja na ukicheche wake wote jambo hilo ukimfanyia anasanda mwenyewe, usikubali akupeleke sehemu nyingine yoyote kama zimempanda mwambie aje hapa home halafu we mpeleke chumbani ukiwa umetegesha macho kama manne hivi halafu akiondoka unishtue nije" Hilary aliongea kwa kutumia misimu iliyojaa maneno yasiyo rasmi ambayo yalieleweka kwa Moses.
"poa poa mtu wangu nakuaminia ndiyo maana nikakuita maana hukosi mbinu kama professional coacher" Moses aliongea huku akitabasamu na kupelekea Hilary acheke.
"yaani Mwana hii kitu tukiifanya tunaua ndege wawili kwa jiwe moja" Hilary aliongea huku akigongesha ngumi yake na ngumi ya Moses kwa mtindo unaoitwa tano, waliamua kuachana na habari hiyo wakawa wansongea mambo mengine ya kawaida kabisa huku wakicheka.
Wakiwa katikati ya mazungumzo simu ya Moses iliita na alipoitoa aliona ni namba ngeni kabisa, aliipokea na kusikiliza mpigaji ni nani akajikuta akiweka spika kubwa isikike hata kwa Hilary.
"NAKUJA TENA KAMA JANA ILA LEO NAHITAJI UNIFANYIE KITU SPECIAL KWA UFUNDI WAKO MAANA WE NI MTAMU SANA" Ilisikika sauti ya Annie katika simu ya Moses.
"ok" Moses aliitikia akakata simu halafu akamtazama Hilary.
"Macho si yapo man kule stoo?" Hilary alimuuuliza
"ndiyo yapo ya akiba mshua aliyanunua kitambo sana akiwa hai" Moses alijibu.
"tukayafunge fasta akija mchezo uanze" Hilary aliongea akainuka akielekea stoo na Moses akamfuata, ilikuwa ni kazi ya dakika kumi waliyoitumia wakawa wamemaliza kufanya kile walichokikusudia na Hilary akaondoka kabla hata Annie hajafika.
Muda mfupi tangu Hilary aondoke Annie alifika akiwa amependeza sana na akapitiliza moja kwa moja chumbani kwa Moses ambapo alimkuta akiwa anamngojea akiwa amejipumzisha kitandani, Annie alipoona hivyo alipanda kitandani naye akaionekana ana kiu ya mapenzi na akaanza vurugu zilizopelekea kutokee mpambano usio na uwanja uliochukua masaa mawili. Baada ya hapo alioga akaondoka zake akimuacha Moses akishangilia kwa kufikia nusu ya mpango wao walioupanga na Hilary, aliziangalia kamera alizozitegesha yeye na Hilary chumbani kisha akampigia simu Hilary na kumtaarifu juu ya kukamilika kwa mpango mzima walioupanga. Hilary alipopata taarifa hizo alirejea nyumbani kwao Moses akiwa na tarakilishi ndogo na akapitiliza hadi chumbani kwa Moses alizitungua kamera akatoa mikanda yake akaiunganisha na kifaa kilichounganishwa na tarakilishi aliyokuja nayo. Aliifanya kazi iliyomchukua nusu saa kisha akamuonesha Moses ambayo ilimridhisha kabisa.
"Hapa ataomba poo mwenyewe" Moses aliongea huku akicheka.
"wewe akikuletea ujuaji mtumie picha tu azione akiwa anajifanya kichwa ngumu tunasambaza video yenyewe akionekana anazini na mdogo wake wa tumbo moja" Hilary aliongea.
"man we mkali wa kuedit nimekukubali, unajua nilidhani nitaonekana mimi kwenye hiyo video kumbe umempachika yule bwiga" Moses aliongea.
"kitu kidogo kwangu hichi, cha msingi wewe fungua blog mapema" Hilary aliongea.
"poa " Moses aliongea kisha akagongesha ngumi na Hilary wakawa wanaongea maongezi mengine yaliyojaa utani.
****
Baada ya kuondoka nyumbani kwao Moses aliamua kwenda kwa mzee Bernard ili akaonane na shoga yake Victoria, siku hiyo Annie alikuwa na furaha zaidi ya siku zote baada ya kupata uhakika wa mpango wake kufanya kazi baada ya Moses kukubali mwenyewe kufanya naye mapenzi. Hakujua kama amechimba kisima kirefu kilichomzidi kimo na hana ngazi ya kupandia ilihali kimeanza kujaa maji, alichojua yeye ni kwamba amempata Moses na hawezi kutoka katika mtego wake akihofia kuharibu penzi lake kwa Beatrice.
"akijifanya majanja tu namuonesha Beatrice picha ili apigwe kibuti na namtishia kuzisambaza mtandaoni akinikataa, najua hawezi kutoka ameingia kwenye cheni ngumu isiyoweza kutolewa hata kwa tindikali" Annie alijisemea maneno hayo akiwa yupo getini kwa mzee Bernard akisubiri geti baada ya kupiga honi, geti lilifunguliwa akaingiza gari ndani hadi kwenye maegesho halafu akashuka akaingia hadi ndani akamkuta Mama Beatrice akiwa sebuleni.
"Karibu mwanangu" Mama Beatrice akimkaribisha Annie huku akiinuka akakumbatiana naye.
"asante mama shikamoo" Annie aliitikia ukaribisho huo kisha akamuamkia Mama Beatrice.
"marahaba, za huko utokapo?" Mama Beatrice aliitikia salamu.
"salama tu mama yangu, mwenzangu nimemkuta?" Annie aliongea.
"Vicky yupo huko juu chumbani kwao anaongea na mdogo wake" Mama Beatrice alimwambia.
"Haya mama ngoja nimuangalie" Annie alisema huku akielekea chumbani kwao Beatrice na Viktoria.
"haya mwanangu" Mama Beatrics alisema huku akitabasamu, Annie alienda hadi chumbani kwao Viktoria akamkuta akiongea na Beatrice wakiwa wapo kitandani.
"Wooow! Shosti karibu" Viktoria alimlaki Annie kwa kumkumbatia
"asante Shostisto wangu, Bite vipi" Anjie aliitikia ukaribisho huo kisha akamsabahi Beatrice.
"safi" Beatrice aliitikia akionesha kutofurahishwa na ujio wa Annie.
"shosti kaa basi ngoja nikakuchukulie kinywaji maana kwenye friji la humu ndani vimeisha" Viktoria aliongea kisha akanyanyuka akatoka nje ya chumba akawaacha Beatrice na Annie, Baada ya Viktoria kutoka humo ndani Annie na Beatrice walitazamana kwa muda huku kila mmoja akionekana kumchukia mwenzake moyoni, Annie alipitazamana na Beatrice aliachia tabasamu la kinafiki lakini Beatrice alizidi kukunja sura.
"Annie hivi kwanini wewe king'ang'anizi hivyo?" Beatrice aliuliza huku akiwa ameikunja sura yake.
"sikuelewi kabisa unaongea nini?" Annie alijifanya kutoelewa kinachoongelewa na Beatrice kutokana na kutokuwa na uhakika kama Beatrice anatambua kama anamtaka Moses.
"Mdada mzima upo chuo tena umri mkubwa unajikusanya kabisa unakuja kumtongoza boyfriend wangu isitoshe unatambua kabisa ninampenda, hivi huoni haya kumfuata Moses hadi kwao unamtongoza kabisa" Beatrice aliamua kumwambia ukweli kutokana na kutopendezwa na tabia ya Annie hasa baada ya kusikia kutoka kwa Moses siku ile aliyompiga Andrew.
Annie aliposikia maneno hayo akimuangalia Beatrice kwa dharau halafu akamuambia, "we ulitaka nifanye nini kama mwanaume nampenda, ulitaka nikuachie? Ha! Ha! Bibie sahau hilo hukumuumba mpaka unikataze namna hiyo. Nampenda na nitampata tu".
"loh! Jitu zima halina haya yaani umalaya wako wote unalazimisha penzi usipopendwa, Mxiuuuuuuu! hovyoo fuata malaya wenzio" Beatrice naye aliongea kwa dharau.
"Ha! Ha! Jitupe bibi, umalaya wangu na bwana wako huyo aliyekuvunja huo ukuta namchukua hatoki mbele ya mbele ya shepu kama hili. He! He un..." Annie naye aliongea kwa dharau huku akiachia kicheko, alishindwa kumalizia kauli yake baada ya mlango kufunguliwa na Viktoria akaingia akiwa ana bilauri yenye kinywaji. Beatrice na Annie waliweka sura zenye tabasamu ghafla kama walikuwa wakiongea kwa furaha.
"naona mnacheka wenyewe mashosti tuambizane basi mnacheka nini na mimi nicheke" Viktoria aliongea huku akimpa bilauri yenye kinywaji Annie.
"mmmh! Nawe kila kitu ujue, hii ni siri yetu mimi na Bite tu" Annie aliongea huku akitabasamu kiunafiki akimtazama Beatrice usoni.
"nijuzeni kidogo tu Mashostito wangu" Viktoria aliongea.
"sis hii yetu sisi tu utaijua baadaye usihofu" Beatrice naye aliongea.
"mh! Haya nificheni tu, halafu Annie leo umetoka kwa mshefa maana jicho hilo si kawaida" Viktoria aliuliza la kizushi kwa Annie ambalo lilimfanya Annie atabasamu kisha akakiri kwa kutikisa kichwa.
"yaani mwenzangu hapa nina uchovu maana nimekutana na dume la simba huko, nikitoka hapa home kulala" Annia aliongea huku akitabasamu.
"mmh! Bibi wewe sikuwezi" Viktoria aliongea.
Marafiki hawa waliendelea kuongea kwa furaha huku wakigongssha mikono huku Beatrice akiamua kutoingilia maongezi yao, baada ya nusu saa Annie aliaga akaondoka kwao akiwaacha ndugu wawili aliowakuta wakiendelea na maongezi yao. Muda huo anaondoka hapo ndiyo muda ambao Moses na Hilary walimaliza kazi ambayo ingekuwa ni dawa tosha kwa Annie akae mbali na Moses na Beatrice.
****
USIKU
BUNJU
DAR ES SALAAM
Baada ya Norbert taarifa zote za Brown Stockman kupitia kwa Scott aliamua kurudi tena kwenye nyumba ile ile akiwa na sura yake halisi kabisa akiacha kutumia sura za bandia kama alivyofanya alipokuja kuwaua Campbel na Christian, alifika katika uzio wa nyumba hiyo akiwa na silaha zote muhimu na zisizoonekana ambazo hutumiwa na majasusi kama yeye. Siku hiyo alivaa shati nyeusi lenye vifungo vya kung'aa kama fedha na suruali nyeusi, alipofika kwenye uzio wa nyumba hiyo aliuruka kwa sarakasi adimu kuonekana kwa mtu wa kawaida na mara nyingi huonekana na kwa watu wenye ukufunzi wa mchezo wa Ninjutsu pekee. Alipotua ndani alitua kwa sehemu ya nyuma ya vidole vya nyuma vya miguu kisha akajibiringisha upesi kuepuke kusikika kwa sauti yoyote ya kishindo. Alibiringira hadi pembeni ya ukuta wa nyumba kisha akatulia gizani kwa nusu dakika akiangalia mazingira yalivyo, aliporidhika pako kimya akasogea taratibu ulipo mlango wa kuingilia ndani kisha akanyonga kitasa cha mlango huo taratibu lakini ulionekana umefungwa kwa ndani. Mlango huo ulionekana ulikuwa umefungwa kwa ndani na ikamlazimu atumie ufunguo malaya kufungulia mlango huo kisha akaingia ndani baada ya mlango kufunguka, aliufunga vile kisha akaanza kutembea taratibu kwani ndani kulikuwa na giza kutokana na taa kuzimwa.
Norbert alipopiga hatua tano tu tangu alisikia sauti ikimuambia"karibu sana" kisha akapigwa na kitu kigumu kisogoni hadi akapoteza fahamu hapohapo.
*mzee wa kazi hatiani
* Annie achimba kisima kirefu bila ya kuwa na ngazi.

ITAENDELEA!!
No comments:
Post a Comment