RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA!!
Baada ya dakika ishirini ving'ora vya magari ya polisi vilianza kusikika vikitokea niia iendayo Mwenge, viliposikika kwa karibu vijana hawa wa makundi yote mawili walipanda magari wakatokea kuelekea njia iendayo Bagamoyo kwa kasi sana. Baada ya wao kuondoka yule kijana aliyewasaidia kina Moses alinyanyua kiti cha dereva akakiweka sawa kisha akawasha gari.
"msiinuke kaeni hivyohivyo maana hii ni hatari kwenu" Aliwaambia kina Moses ambao walianza kuinua vichwa vyao juu, Yule kijana aliweka gia kisha akatembea pembeni ya barabara hadi akalivuka eneo la tukio. Aliingiza gari barabarani kisha akaondoka kuelekea Mwenge baada ya kuliacha mbali eneo ambalo awali liligeuka uwanja wa vita.
****
Kizazaa kilichotokea eneo la tukio ilikuwa ni la kihistoria ambalo halijawahi kutokea katika nchi hii yenye amani, wengi walifananisha tukio lile na matukio katika nchi ya Somalia yenye vikundi vya wanamgambo walio na uhasama. Wananchi kutoka sehemu mbalimbali walioshudia tukio lile walikuwa wakielekeza lawama zao kwa polisi kwa kuchelewa kufika eneo la tukio na kusababisha kuuawa kwa raia wasio na hatia waliokuwa wakipita njia, ilikuwa ni tukio la aina yake ambalo lilivuta hisia za wengi hasa baada ya kujua ndani ya gari aina ya landcruiser prado kulikuwa kuna wanafunzi wanne ambao hadi muda huo walikuwa hawajulikani walipo. Mashuhuda wa tuko hilo waliona hadi gari la wanafunzi hao lilipogonga nguzo ya umeme, walilifananisha tukio hilo na utekaji nyara ambao ulitaka kutokea lakini ulivurugwa na kikundi kingine na watu wenye silaha na hapo ndipo vita ndogo ndani ya nchi hii ikaibuka na milio ya risasi ikarindima. Hakuna mtu aliyejua kwamba wanafunzi hao walikuwa wameokolewa na mtu aliyekuwa ameegesha gari kando ya barabara, taarifa ilipotolewa shule ya sekondari ya Neema trust majina ya wanafunzi hao yalipatikana mara moja na mawasiliano na wazazi wao yalifanyika haraka iwezekanavyo. Mzee Bernard Mtashobya, Mzee Wilson baba yake Hilary, mzee Fortunatus baba yake Irene na Kennedy mjomba wake Moses wote walipewa taarifa za kupotea kwa vijana wao ndani ya siku hiyo. Wote kwa pamoja walijikuta wakichanganyikiwa kwa taarifa hiyo karibu kila nyumba ilitawaliwa na kilio huku wazazi wa kiume wakihangaika katika kuhakikisha watoto wao wanapatikana kwa kutumia uwezo wao wa kifedha katika kuwahimiza askari wa jeshi la polisi watilie mkazo suala la kutafuta vijana wao. Majira ya saa mbili usiku wazazi wote walikutana nyumbani kwa mzee Bernard na wakawa wanalijadili suala hili linalowakabili la kupotea kwa watoto wao, ilikuwa ni kikao ambacho wazazi wa kike walikuwa hawahusishwi na kiliwahusu wazazi wa kiume wa Beatrice, Hilary, Irene na mlezi wa Moses ambaye ni mjomba wake. Mjadala uliendelea katika kufanya mikakati ya kuhakikisha vijana wao wanapatikana kwa namna yoyote kwani imani yao kwa jeshi la polisi ilikuwa tayari imepungua, wakiwa katikati ya kikao simu ya mezani ya nyumbani kwa mzee iliita Bernard iliita na ikalazimu kikao kisitishwe kwa muda ili mzee Bernard akapokee simu hiyo. Mzee Bernard alienda kuipokea simu hiyo kisha akazungumza, "Ndiyo Wojojo.......ni nani huyo mgeni aliyepo getini.....mwandishi wa habari?......aaargh usimruhusu aingie", Mzee Bernard alipomaliza kusema hivyo alikata simu kisha akarudi kwa wenzake kuendelea na kikao.
"vipi mzee mwenzangu mbona hivyo?" Mzee Fortunatus alimuulixa Mzee Bernard baada ya simu kurudi kwenye kikao.
"aaaargh! Si mwandishi wa habari wa kujitegemea yupo getini anataka kuonana na mimi" Mzee Bernard alisema kwa hasira.
"yupi ni Kaila nini?" Mzee Wilson alidakia
"ndiye huyohuyo mzee mwenzangu, unafikiri ana cha maana zaidi ya kutaka kutuhoji aharibu mipango yetu" Mzee Bernard alisema kwa hasira.
"tena ni bora hata ulivyomzuia kwani yule kijana ni mchokonoaji wa mambo sana" Mzee Wilson aliongea.
"tena umefanya vizuri sana kwa kumzuia mzee wangu, haya wazee wangu tuendeleeni na kikao tuachaneni na habari za Norbert Kaila" Kennedy aliongea kuwarudisha wazee wake kwenye kikao, walipotaka kuendelea na kikao simu ya mkononi ya Mzee Bernard ikaita na ikambidi aitoe aangalie jina la mpigaji.
"aaaargh! Kaila huyu anataka nini kwangu sasa hivi?" Mzee Bernard aliongea kwa hasira.
"hebu usiikate pokea uweke loudspeaker tumsikie anasemaje" Kennedy alishauri na Mzee Bernard akatii kama alivyoambiwa.
"nafikiri mimi ndiyo msaada wako ikiwa utaniruhusu niingie, sipo kikazi bali nipo kimsaada zaidi" Sauti ya Norbert ilisikika kisha simu ikakatwa, wote waliokuwa kwenye kikao hicho walitazamana kwa sekunde kadhaa kishaa wakaafikiana Norbert aruhusiwe aingie ndani. Mzee Bernard alimpigia simu mlinzi akampa amri ya kumruhusu Norbert aingie ndani kisha wote kwa pamoja wakatoka hadi kwenye maegesho wakawa wanamsubiria Norbert aweze kuingia.
Gari aina ya Nissan patrol yenye vioo vya giza iliingia hadi kwenye maegesho ya magari ya nyumba hiyo kisha milango ya mbele ikafunguliwa, Norbert na kijana aliyevalia sare nadhifu za jeshi la polisi walishuka wakakutana na mzee Bernard akiwa na wazazi wenzake wakiwa wanamsubiri.
"habari za jioni wazee wangu" Norbert aliwasabahi akiwa na sura ya tabasamu.
"sema shida yako Kaila" Mzee Bernard alifoka kwa hasira.
"kutaneni na inspekta John Faustin wa kituo cha kati nimekuja naye ili kuja kutatua shida yenu" Norbert aliongea akitabasamu huku akimtambulisha Inspekta John.
"kijana ujue usituchezee akili sema kilichokuleta sisi tuna kikao cha muhimu, na kama umekuja kutuhoji kuhusu watoto uondoke kabisa" Mzee Wilson alifoka kwa hasira, Norbert aliposikia maneno hayo ya kukaripiwa alishusha pumzi kisha akageuka kuangalia gari walilokuja nalo. Alionesha ishara kama anaita mtu milango ya nyuma ya gari aliyokuja nayo ilifunguliwa, macho ya wazazi hao yaliwatoka kwa mshangao kwa kuwaona watu waliofungua milango na wakishuka kwenye gari hiyo walikuwa ni watoto wao waliokuwa wanawatafuta.
"mpo salama sasa mnaweza mkaenda kwa wazazi wenu" Norbert aliwaambia kina Moses ambao walikimbilia upande walipo wazazi na walezi wao, wazazi wote walijikuta wakitokwa na machozi ya furaha baada ya kuwaona watoto wao waliokuwa wamewapa kiwewe kwa kutoonekana baada ya kutokea tukio la kurushiana risasi . Norbert na Inspekta walipohakikisha wanafunzi wamefika mikononi mwa wazazi wao waoiamua kuondoka kwani maneno walikuwa wanaambiwa ni ya kuudhi kabisa.
"Kaila hapana usiondoke, najua kama nimekuudhi mimi na wenzangu. Samahani kijana wangu na karibu ndani kwani wewe ni msaada tosha kwetu kwa kuteletea watoto wetu" Mzee Bernard aliongea kwa ustarabu kutokana na kitendo alichomfanyia Norbert.
****
Muda ambao furaha ilikuwa imetawala ndani ya nyumba ya mzee Bernard ilikuwa ni karaha katika nyumba ya Komredi, vijana waliokuwa katika pambano la kutupiana kwa risasi ndiyo walikuwa wamesimama mbele ya Andrew na Komredi walikuwa wameinamisha macho yao chini baada ya mpango waliokuwa wanaenda kuufanya kuwa umefeli. Andtew macho yake yalikuwa yamemuiva kwa hasira huku akiwa anavuta msokoto mnene wa bangi kwa fujo, macho yake yote yalikuwa yapo kwa vijana hao ambao hadi muda huo walikuwa hawana la kujitetea.
"mna la ziada la kuniambia litakalofanya nikawaelewa juu ya kushindwa kwenu kufanya kazi" Andrew aliuliza huku midomo ikimtetemeka kwa hasira.
"Bosi Gotta haikuwezekana kumuua kwa muda ule kwani Junior aliyekuwa anamlenga alipigwa risasi na hawa majamaa waliotuvamia na nilimuachia Doku nikijua atamaliza" mmoja wa wale vijana alijitetea.
'PAAAAA!' mlio wa bastola ulisikika na yule kijana aliyekuwa anajitetea alianguka chini kama mzigo.
"haikuwezakanaa! Nani mwingine anasema haikuwezekana kwani risasi nyinyi hamuna? Haya wewe unayefuata niambie kwanini ulishindwa kumpiga risasi wakati kwa mujibu wa maelezo ya mwenzako wewe ndiyo ulikuwa karibu na
Junior?" Andrew alimuuliza mwingine huku akinyoosha bastola kumlenga akiwa hasira sana.
"Mkuu ningempiga risasi jua ningempiga Beatrice mwanamke unayempenda kwani vurugu zilipoanza Beatrice alimkimbilia Moses" Kijana mwingine ambaye ndiye Doku aliongea bila kuweka hofu yoyote, maelezo yake yalimfanya Andrew kushusha bastola yake kisha akasema "wewe ndiye mwenye sababu ya msingi ya kukufanya ushindwe kumlemga yule mbwa na risasi na hii pia ndiyo sababu inafanya niwasamehe wote sasa basi nahitaji vuguvugu ikitulia mumteke yule rafiki yake kwani ndiye atakayefanikisha nimpate Beatrice".
'PAA! PAA! PAA! PAA! PAA! PAA! PAA!' sauti ya bastola ilisikiia huku wale vijana waliobaki wakianguka chini kama mizigo, Andrew aligeuza macho yake akamtazama Komredi alimuona akipuliza shimo la kutolea la risasi la bastola ambalo lilikuwa linatoa moshi huku akitabasamu.
"Komredii! Umefamya nini sasa mbona unapunguza jeshi letu?!" Andrew aliuliza kwa hasira huku akimtazama Komredi.
"yoyote anayefeli misheni aliyopewa mbele ya Komredi hatakiwi kuwa hai hata kidogo na kifo ndicho anachostahiki. Jeshi bado lipo kubwa wewe panga plan hiyo itafanywa na jeshi lingine" Komredi aliongea akimtazama Andrew kisha akawaambia walinzi waliopo pembeni yake, "toeni hiyo mizoga mkaifukie mabwepande sasa hivi".
****
Upande wa kambi ya vijana wa Annie napo mambo yalikuwa si shwari hata kidogo, uso wa Annie ulikuwa umeiva kwa hasira hasa alipopata taarifa ya kufeli kwa mpango wake aliowatuma vijana wake. Vijana wote walikuwa wameinamisha macho yao chini wakishindwa kumtazama bosi wao kutokana na kushindwa kuifanya kazi aliyowatuma, wote walikuwa wapo kwenye chumba cha mkutano kwenye kambi yao nyingine iliyopo Bagamoyo.
"ok, mna sababu ya kunieleza itakayonifanya niwaelewe kwanini mlishindwa kufanya kazi ndogo ya kumteka Beatrice wakati kazi nzito za kusafirisha biashara yangu mnazifanya" Anni aliongea
"Madama maadui zetu walishatuwahi kwa kutangulia kufika kabla yetu sisi na hata tulipofika walikuwa tayari wamewazunguka na bunduki walikuwa wamemuelekezea Moses, hivyo ilitubidi kupambana ili wasimdhuru Moses" Kiongozi wa kundi la wahalifu waliokuwa wakirushiana risasi na kundi la Andrew aliongea, maneno yake yalimuingia Annie na akajikuta anatabasamu kwa kazi waliyoifanya vijana.
"vizuri sana mmefanya jambo la maana sana kumuokoa Mosea kundi dhidi ya hilo ambalo nina uhakika wametumwa na Andrew, umesema walikuwa wanatumia gari ya aina gani?" Annie aliongea.
"Ford rangers" Mkuu wa wale vijana alijibu.
"vioo vyake vina picha za chui?" Annie aliwauliza
"Ndiyo madam tena rim ya matairi yake ina umbo la fuvu katikati" Mkuu wa kikosi cha aina alizidi kufafanua.
" shit! Komredi na Andrew wapo pamoja sasa wameianza vita mimi naendeleza, Beatrice nitamnyonga huku wanamuona hivihivi" Annie aliongea kwa hasira baada ya kubaini gari waliyokuwa wanatumia maadui zao ni mali ya Komredi na alijiwekea asilimia mia kuwa yupo pamoja na Andrew kwani yeye ndiye mwenye ugomvi na Moses.
****
Furaha ilirejea tena baada ya huzuni yenye mchanganyiko wa wahka kuifukuza kutokana na kutoonekana kwa watoto wao, wazazi kwa pamoja walikusanyika katika sebule ya mzee Bernard huku wazazi wa kike wakihusishwa kwa mara ya kwanza katika kikao hicho. Shukrani za dhati zilienda kwa Norbert baada ya kufanikisha kupatikana kwa watoto wao wakiwa wazima ingawa walikuwa wana michubuko midogo iliyosababishwa na kashikashi za tukio lililowakumba, Beatrice, Moses, Hilary na Irens nao walizidi kumshukuru Norbert kwa kufanikisha suala la kuwaokoa katika uwamja wa vita vya ghafla.
"Kaila na Inspekta John asanteni sana kwa kufanikisha kupatikana kwa watoto wetu" Mzee Bernard aliwashukuru Norbert na Inspekta John kwa kufanikisha kupatikana kwa watoto.
"mzee wangu usijali ni jukumu letu kusadiana kama wanadamu" Norbett aliongea
"sasa nyinyi nyote kwa usalama wenu inabidi msiende shule wala kokote mpaka hali itulie" Mzee Wilson aliwaambia kina Moses
"kabisa mzee mwenzangu hata wakianza kwenda shule inahidi tuwawekee ulinzi hawa" Mzee Fortunatus aliongea
"jamani wakulindwa haswaa ni huyu Moses kwani yeye ndiye aliyetaka kuuliwa" Inspekta John aliongea na kusababisha Kennedy amtazame Moses kisha akamuuliza, "kuna yoyote unamtambua?".
"hapana Anko hakuna ninayemtambua ingawa nilisikia wakimtaja jina la mtu aliyewatuma tu" Moses alijibu, kauli hiyo iliwafanya wote wamtazame Moses.
"aliyewatuma ni nani?" Kennedy aliuliza.
"Anaitwa Gotta" Moses aliongea na kupelekea Kennedy aume meno yake kwa hasira huku wazazi wengine wakiachia miguno. Kennedy alinyanyuka na akawa anatembea hsna uelekeo maalum alikuwa akitembea sebuleni kwa kwenda mbele na kurudi nyuma bila hata kujulikana anaenda wapi, alipokuja kusitisha kutembea alisema "hapa wa kulindwa ni Moses tu hawa wengine wapumzike hali ikutulia waende shule ila muwe makini nao tu".
"Kijana kwanini unasema hivyo?" Mzee Fortunatus alimuuliza Kennedy.
"hili ni jina ni mara ya pili nalisikia jina hilo likituma watu kumfanyia fujo mpwa wangu tangu nianze kuishi nae" Kennedy aliongea kisha akamtazama Moses kwa umakini halafu akasema "hadi hapo nadhani mshaona kwamba anayetafutwa ni yeye kwani mara ya kwanza aliumizwa na akakaa nyumbani karibu nusu wiki". Maelezo hayo yalizua ukimya wa muda mfupi sebuleni hapo na kila mmoja alikuwa akiwaza lake, ukimya huo ulikuja kuvunjwa na Mzee Wilson ambaye alisema "inawezekana ikawa ni kweli kwani Hilary wiki mbili zilizopita aliniambia kuhusiana na tukio la kugongwa kwa gari ya nyumbani pamoja na kupigwa kwa huyu kijana".
"Moses baba kwani una ugomvi na mtu" Mama Beatrice aliuliza kwa mara ya kwanza tangu anakaa sebuleni hapo pamoja na wazazi wenzake.
"hapana mama sijawahi kuwa na ugomvi na mtu" Moses alikataa huku akificha tukio la yeye kuwa na ugomvi na Andrew kwa kuhofia kuulizwa chanzo cha ugomvi wao.
"nafikiri kijana anahitaji alindwe na hawa wengine pia walindwe kwani bado nina mashaka sana na hawa watu" Mzee Bernard aliongea, jambo hilo lilikubaliwa na wazazi wote na ikawa ndiyo suluhisho la kikao chao. Baada ya kikao kuisha kila mzazi alimchukua mwanae na kuondoka nae wakiwaacha wenyeji wao tu, Norbert na Inspekta John nao walindoka kwenda kuendelea na shughuli zao.
****
SIKU ILIYOFUATA
BUNJU
DAR ES SALAAM
Uchunguzi wa kutafuta mahali ambapo virusi vinavyotafutwa na Brian ulikuwa unaendelea kwa kikosi cha Mambas ambao sasa hivi wamebakia wanne kutokana na wenzao kuuawa walipobaki nyumbani katika siku walipoenda kuongea na bosi wao mijini, asubuhi ya siku hii ya leo Scott aliamua kwenda kwenye hoteli ya Mangrove kuangalia mahali ambapo virusi vinaweza kupatikana. Aliwaaga wenzake akatoka getini ambapo alikutana na teksi ikiwa inapita na ikamlazimu aipungie mkono isimame kwani hakuwa anatumia gari siku hiyo kwa sababu za kiusalama. Teksi hiyo ilisimama naye akafungua mlango akakaa kiti cha nyuma kisha akaongea kiswahili kibovu, " peleka mimi Msasani".
"30000 tu" dereva wa teksi mwenye lafudhi ya kizaramo alijibu.
"twende" Scott alisema na dereva akaondoa kuelekea ilipo barabara ya Bagamoyo, aliingiza gari barabara ya Bagamoyo akiwa anapiga uruzi za wimbo huku akimtazama Scott kwa jicho la kuibia katika kioo cha kati. Dereva teksi huyu aliongeza mwendo na alipokaribia Tegeta alivua kiatu cha mguu wa kushoto makusudi, hali ya hewa ya humo ndani ilibadilika ghafla ikawa ni harufu ya uvundo mzito iliwa imetawala.
"mmh! Gari yako iko nuka harufu baya baya" Scott aliongea kiswahili kibovu cha kuigiza huku akibana pua kutokana na harufu hiyo.
"Usijali bosi ngoja nikuwekee airfresh kuiondoa hiyo" Dereva aliongea huku akifungua mkebe uliokuwa pembeni yake akatoa chupa ya uturi wa kuweka harufu nzuri katika gari, aliupuliza ule uturi sehemu mbalimbali hadi harufu za uvundo wa viatu ikatoka.
"bosi hapo vipi?" Alimuuliza Scott baada ya kupuliza uturi huo.
"hapo safi kabi.." Scott alijibu lakini alidhindwa kumalizia sentensi yake akajikuta amepitiwa na usingizi mzito wa ghafla.
"Scott umekwisha wewe" Dereva wa teksi aliongea huku akizidi kuongeza mwendo wa gari kuitafuta Mbezi akiiacha Tegeta.
*Mmmh!
*ndugu wa damu ndani ya ugomvi mzito kisa mapenzi
*kama ni moto wa nyikani naweza umezidi kupamba zaidi lakini kwa hii riwaya sijui nisemaje,.
ITAENDELEA!!
No comments:
Post a Comment