Wednesday, December 28, 2016

SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA



RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________


SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA!!
    Walikuwa wakiongea na kucheka kwa furaha sana kila walipokuwa wakiiangalia Luninga jinsi ilivyokuwa ikirusha matangazo juu ya kinachoendelea Magogoni. Hakika hatua ya ushindi wa mwisho ndiyo waliiona ilikuwa wakiikariia kuifikia na vikwazo vilikuwa vikiondoka kimoja baada ya kingine, walibadilisha chaneli mbalimbali za luninga bado habari ilikuwa ni ileile hata walipoweka chaneli za nje ya nchi.
    
             "aisee kazi imekwisha nasubiri wale vijana wa nusu komandoo wamtiemikononi Kaila tuje tummalize nina uhakika hatatoka" L.J Ibrahim aliongea
                 "Kabisa General" Mzee Ole aliitikia, muda huohuo simu ya upepo iliyokuwa ipo jirani yao ilianza  kukoroma na hapo L.J Ibrahim aliichukua m kwa haraka.
                "Enhee nipeni habari, Norbert mnae hapo" L.J Ibrahim aliuliza
                  "Hatujamuona mkuu hata waandishi wa habari wenzake wanasema hawajui ameelekea wapi?" Sauti ya M.J Mugiso ilisikika kwenye simu hiyo ambayo ilimfanya L.J Ibrahim aondokwe na furaha papo hapo.
                 "Wajinga nyinyi!" L.J Ibrahim alifoka kwa hasira.


_________
________________ TIRIRIKA NAYO
_________

                   "Mkuu katupotea kwenye mazingira ya kutatanisha"
                     "Ye kawa mchawi kwahiyo atawapoteaje namna hiyo? Kama si uzembe ni nini?"
                   "Hapana mkuu nahisi huyu mtu ana namna"
                     "Pumbavu sitaki kusikia hayo nasema kamata hao waandishi wenzake wote ndiyo watajibu alipokuwepo, mtamuachaje mtu anayedhaiisha ofisa wa jeshi fanya haraka nataka hao waandishi wa habari wawe chini  ya ulinzi mara moja"
                    "Mkuu"
                        "ndani ya robo saa nataka nisikie ukiripoti tayari hao waanDishi wapo chini ya ulinzi tunaelewana?!"
                     "Mkuu"
    Baada ya hapo L.J Ibrahim alikata mawasiliano na akamtazama Mze Ole ambaye alikuwa akifuatilia maongezi hayo kwa umakini mkubwa sana, alishusha pumzi kisha akasikitika kwa jinsi walivyokuwa wakkihangishwa na Norbert. Mivnyo aliokuwa na anaunywa aliuacha mara moja na akasimama na mikono akaweka kiunoni, alipigapiga chini kiatu cha jeshi alichokuwa amekivaa huku akiwa amekunja sura yake kwa jinsi wanavyohangaishwa na Norbert.
                        "General huna sababu ya kumlaumu Mugiso, kumbuka tunapambana na mtu zaidi ya komandoo"
                        "Natambua hilo Ole lakini nao ni wazembe vilevile yaani mtu tunamuona hapa kwenye tv muda ambao tunawatuma wamkamate na hadi anaondoka kwenye usawa wa kamera hii ya televisheni ya taifa wangekuwa tayari wameshamkata"
                      "No no Norbert ni mtu mwenye akili sana huenda alishahisi hayo"
                        "Ole kumbuka wale ni special force wa jeshi la maji unafikiri watamkosaje mtu kama yule"
                         "General kumkamata huyu mtu na kumuua inabidi tutumie akili na siyo kupanic, sasa hivi anatuchezea akili kwa kupanic kwetu unafikiri tukiendelea kupanic si ndiyo atatuvua nguo za ndani kabisa huyu"
                     "Ok nimekuelewa unashauri tufanyeje?"
                     "Wapigie kina Santos huyu mtu hayupo mbali na hapo nahisi'
                         "ok" L.J Ibrahim alikubali kama alivyoambiwa na alitoa simu yake ya mkononi akwapigia hao watu alioambiwa.

****
NDANI YA IKULU
    Rais Zuber tayari alikuwa ameshachanganyikiwa kwa jinsi wanajeshi hao walivyokuwa wameizunguka Ikulu pasipo kuacha nafasi hata ya  mtu aliyemo humo ndani kutoka nje bila kukamatwa, yote aliyokuwa akiyapanga humo ndani ilivuja kwa muda mfupi tu na kumfikia L.J Ibrahim ambapo alizidi kuchanganyikiwa kuhusu suala hilo. Harufu ya usaliti tayari ilianza kumzonga kwenye pua zake hadi kichwa kikawa kinamuuma, tayari alishaanza kuhisi kuwepo kwa msaliti humo ndani ya ikulu aliyekuwa akifanya mambo yote yawe mabaya. Jambo hilo lilimtatiza  sana na ndani ya muda mfupi aliitisha kikao cha wote waliomo huko ikulu kuanzia wanausalama na hata ADC, akiwa mwenye sura ya kuchanganyikiwa  hakuweza hata kuweka kalio  kwenye kiti muda wote alikuwa amesimama akiwatazama wote wa eneo hili.
               "mnaweza kunipa maelezo ya hichi ninachowauliza?" Rais Zuber aliongea kwa nguvu, wote walikaa kimya wakwa wanamuangalia kwa umakini.
                "nahitaji kumjua mtu anayevujisha habari kati yenu hapa, haiwezekani mipango yote niliyoipanga asubuhi hii igundulike upesi tu kwa Ibrahim. Nani msaliti kati yenu!?" Rais Zuber aliuliza kwa hasira sana, akiwa anawatazama wale maofisa wa usalama wa taifa pamoja na mmoja wa jeshi simu yake ya mkononi iliita muda huohuo. Alipoangalia jina la pigaji alikuwa ni L.J Ibrahim, aliipokea simu hiyo na akaiweka sautu kila mtu akawa anaisikia.
                 "Ha! Ha! Ha! Ha! Zuber naona unahangaika kumtafuta msaliti sasa hivi siyo, haitasaidia kitu!" Simu hiyo ilikatwa na hasira zilimzidi sana Rais Zuber akaingiza mfukoni akatoa simu nyingine alibonyeza namba moja tu akaiweka sikioni akaongea, "njoo haraka chumba cha mkutano na vifaa vyako vyote".
    Aliwaangalia wanausalama wote wa humo ndani kisha akauliza, "simu zote mmeziacha nje sasa nani ana kinasa sauti humu ndani?
     Swali hilo liliwafanya wanausalama wote waanze kutazamana mmoja baada ya mmoja lakini hakuna aliyetoa jibu kumjibu, hasira zaidi zilimpanda Rais Zuber hadi akawa anahema kwa nguvu sana huku akiwatazama wanausalama hao ambao walikuwa  waaaminifu kwa kipindi chote alichokuwa nao. Siku hiyo baada ya kupokea simu kutokka kwa L.J Ibrahim ikimkejeli kwa mpango wake aliuongea muda huohuo, hapo ndipo alijua kuwa kuna mtu alikuwa akisababisha L.J Ibrahim ajue yote hayo kupitia kinasa sauti ambacho hakujua mtu huyo alikuwa amekiweka mahala gani. Kila aliyekuwa akimtazama uso wake haukumpa shaka naye na hapo ndipo alizidi kupagawa hakujua nani alikuwa amehusikana huko kuvujisha taarifa zake, aliwatazama watu wote na hatimaye macho yake yakatua kwa ADC wake aliyekuwa amevaa sare za kijani za jeshi la wananchi akiwa mtulivu sana asiyeonekana kama ana hofu yoyote  katika uso wake. Alimnyooshea kidole ADC huyo aliyekuwa akitembea naye katika sehemu mbalimbali akiwa nyuma yake na alikuwa ni mmoja kati ya watu aliokuwa akiwaamini, akiwa na uso wake wenye shaka juu yake alimuashiria asimame naye akatii na kusimama kisha akatoa saluti.
                   "Sina haja ya saluti yako, niambie kwanini unavujisha mambo kumpelekea msaliti wa taifa hili? Tangu uingie wewe asubuhi hii ya leo ndiyo siri zetu humu zimekuwa zikivuja. Sasa niambie kitoe kinasa sauti au aje mhusika akinase kilipo" Rais Zuber aliongea huku akimtazama ADC wake aliyekuwa amesimama kikakamavu akiwa anamtazama.
                    "Kamuti hatuna mwanajeshi mwingine humu ndani zaidi yako sasa nataka nijue ulipita vipi wanajeshi hao waliokuwa wameizunguka Ikulu nzima hadi ufike hapa kama hawakuwa wamekutuma toa kinasa sauti chako upesi" Rais Zuber aliongea  kwa kufoka, muda huohuo mlango ulifunguliwa na mtu mwenye suti nyeusi akiwa amebeba  kitu mfano wa fimbo aliingia humo ndani a. Rais Zuber alipomuona huyo mtu alitoa tabasamu la kihasira kisha akasema, "anza na ADC".
        Mtu huyo alimsogelea ADC  akamuamuru anyooshe mikono naye akatii bila shuruti yoyote, alimpitishia hiyo fimbo ambapo ilito sauti katika kila sehemu kutokana na kuwepo kwa vyuma na madini ya fedha juu ya nguo zake. Aliipitihsa mashine hiyo hadi miguuni lakini hakukuwa na cha ziada kilimchotoa sauti, baada ya kumaliza aliitazama fimbo yake hiyo iliyokuwa na kioo maalum kama cha saa ya mkononi na hakukuwa na dalili ya uwepo wa kinasa sauti chochote mwilini mwake.
                    "Mheshimiwa hana chochote zaidi ya vifungo, vyeo, nishani na mkanda ambavyo ndiyo vimefanya mashine hii itoe sauti" Alijibu huku akikisoama kioo cha kifimbo hicho alichoingia nacho.  
                    "Haya kila mmoja anyanyukea apekuliwe" Rais Zuber alitoa amri na wote wakatii wakaweka silaha zao mezani wakapekuliwa lakini hakikupatikana kinasa sauti hicho, hapo ndipo alipozidi kuchnganyikiwa  akawa hajui nini cha kufanya.  Aliwatazama kila mmoja lakini nafsi yake ilishindwa kumjua aliykuwa anahusika na hio suala, wakati akiendelea kujifikira umbile la mtu aliyekuwa amevaa amgwanda ya kijeshi alionekana akitoka ndani ya uvungu wa meza hiyo kwa taratibu sana na kwa maringo. Wanausalama wote walichukua silaha zao na wakamuelekezea kwa haraka sana, mtu huyo ambaye alikuwa amevaa kofia ya kijeshi iliyofunika uso wake kwa asilimia nyingi alitoka taratibu tena kwa maringo.
                   "Tulia hivyohivyo" Wanausalama wote waliongea huku wakimnyooshea silaha zao.

****

      Baada ya kuwapiga chenga mbaya wanajeshi waliotuma na M.J Mugiso, Norbert aliamua kutoka hadi maeneo ya Posta mpya akitumia njia za mkato mbalimbali ambapo alitumia mwendo mfupi akawa ameshafika. Alizunguka nyuma ya benki ya CRDB mtaa wa Azikiwe  kwa kupitia katikati ya sheli ya mafuta ya mfuta iliyopo pembezoni mwa benki hiyo, alipoimaliza sheli hiyo alivuka barabara kisha akafuata njia inzyoelekea ilipo shule ya sekodari ya wasichana ya Kisutu. Alitembea kwa umbali mfupi tu kisha akaingia kwenye lango la eneo lililokuwa limezungushiwa mabati lilipo pembezoni mwa barabara hiyo.
     Alitokea kwenye eneo lenye magari mengi yaliyokuwa yameegeshwa kwa mpangilio maalum, hapo alitembea hadi usawa wa mwisho wa eneo hilo ambapo kulikuwa na gari lake alilokuwa amekuja nalo eneo hilo. Alipolikaribia gari lake hilo alijipekua mfukoni kwa lengo la kutoa funguo lakini alisita baada ya kukitazama kioo cha giza kilichokuwa kwenye gari, alijirusha pembeni kwa haraka baada ya kuona kile alichokuwa amekiona kwenyekioo cha  gari hilo kikiwa nyuma yake. Kitendo cha yeye kutoka eneo hilo kwenye gari lake kulitokea tundu la haraka sehemu ya chini kidogo ya kioo, Norbert alipotua chini baada ya kujirusha alijibiringisha kuelekea chini ya magari mengi yaliyokuwa yameegeshwa kwa ustadi mkuba halafu akatulia akawa akitazama eneo ambalo lipo gari lake.
    Aliwashuhudia Santos na Benson wakifika haraka eneo hilo wakiwa bastola zilizofungwa viwambo vya kuzuia  sauti kila mmoja. Walipofika hapo kila mmoja alikuwa akitazama pembezoni ya gari hilo na magari mengine lakini hawakufanikiwa kumuona Norbert, waligawana kla mtu upende wake kwenda kumtafuta Norbert kisha wakaanza kutembea kwa taratibu huku risasi zao wakiwa wamezielekeza  mbele kwa tahadhari. Norbert alikuwa akiwatazama kila mmoja upande aliokuwa ameelekea ndipo na yeye akafungua kiatu  akatoa bastola ndogo ambayo huwa anaichomeka kwenye kiatu chake, alifungua na soksi yake akatoa kiwambo cha sauti ambacho alikifunga kwenye bastola hiyo.
    Alipomaliza  alitambaa hadi  mwisho wa uzio wa mabati wa eneo hilo palipokuwa kuna gari aina ya toyota landcruiser ikiwa imeegeshwa. Alijiinua kwa haraka akajibana pembezoni mwa  gari hilo kisha akatulia tuli bastola akiwa ameshika kwa tahadhari sana, alijibana eneo kwa muda hadi aliposikia mlio wa kukanyagwa kwa chupa ya plastiki ya maji ndipo akachungulia kule ulipotokea mlio ule. Machoyake yliweza kumshuhudia Benson akiwa anaelekea usawa wa lango la kuingilia eneo hilo akiwa amempa mgongo, Norbert kwa kasi ya ajabu alimuelekezea bastola yake na akaruhusu risasi mbili ambazo zilitoka zikaenda kutua mapaja ya Benson.
                "Aaargh!" Benson aliachia ukelele wa maumivu akaenda chini moja kwa moja huku akiwa ameshikilia sehemu za uvunguni mwa mapajani mwake baada ya risasi hiyo kutua kwenye mfupa wake, ukelele huo ulimfanya Santos ajitokeze hadi pale alipo Benson akamkuta akiwa anatokwa damu nyingi miguuni.
       Kujitokeza huko naye alikuwa amefanya kosa kwani  eneo hilo Norbert hakuwa ameondoka alilokuwa hapo awali, alikuwa akimshuhudia jinsi anavyohangisha macho yake kutazama kila pande kumtafuta lakini hakuwa amemuona baada ya Norbert kujibana palepale alipokuwa awali.  Santos akiwa anashangaa hali ya Benson alirudiwa na akili ya  kujihami ajikinge na adui yake lakini wakati anarudiwa na akili hiyo tayari alikuwa ameshachelewa kwani Norbert aliikoholesha bastola yake ikatoa risasi ambayo ilienda moja kwa moja na kupiga bstola aliyokuwa ameishika, Santos alipoangalia mahali ilipotokea risasi hiyo hakumuona mlengaji yeyote kwani Norbert tayari alikuwa ameshajibana tena katika eneo alilokuwepo awali.
      Santos alisimama hapohapo akiwa hana la kufanya baada ya bastola yake kumuanguka mitaa kadhaa kutokana na nguvu ya bastola ya Norbert kuisukuma mbali, aliganda hivyo kwa muda mfupi na alipoona kimya alipiga hatua moja kuifuata bastola hapo ndipo akaganda na hatua hiyohiyo moja hakuongeza ya pili baada ya mchanga kutifuka mbele ya mguu wake. Alijua moja kwa moja ilikuwa ni risasi ile imekita ndani ya udongo na ilikuwa ni onyo asiendelee kupiga hatua zaidi, aliganda hivyohivyo kama alikuwa amegandishwa baada ya mkanda wa video kusimamishwa na muangaliaji.
             "Geuka nyuma" Sauti ya Norbert ilimpa amri lakini hakuitekeleza mara moja akabaki akiwa amesimam vilevile, Norbeert hapo aliikoholesha bstola yake risasi ikatua kwenye ardhi  katikati ya miguu ya Snatos.
    Hapo Santos aligeuka nyuma akawa anatazamana na Norbert kwa umbali wa mita kadhaa, usawa wa bastola wa Norbert ulikuwa umemuelekea yeye ambapo angefanya kosa lolote basi basi bastooa hiyo ingekohoa kikohozi kingine na kummaliza moja kwa moja.
             "PIga hatua kumi na tano mbele" Norbert aliongea pasipo kumjali Benson aliyekuwa ameishiwa nguvu akiwa amejilaza na bastola ikiwa ipo pembeni, Santos alipiga hatua hizo kumi na tano alizoambiwa akawa amefika umbali ambao ulikuwa ni wa takribani mita moja kutoka aliposimama.
     Baada ya kufika umbali huo ambao ulikuwa jirani kabisa na Norbert alibaki akiwa ameganda vilevile akimtazama, hapo Norbert alishusha bastola yake akaichomeka nyuma ya suruali yake kisha akamtazama Santos huku akiwa ametabasamu usoni mwake. Santos iliposhushwa silaha hiyo aliona ndiyo nafasi pekee ya kuitumia, alijifyatua kwa haraka akaja na mateke mawili ambayo yalimpata  Norbert akaenda moja kwa moja chini.
             "Nyanyuka pusi mweusi wee!" Santos aliongea akimtazama Norbert ambaye pamoja na kupigwa na mateke hayo alikuwa akitabasamu tu, Norbert alijifyatua kiufundi akasimama wima kisha akasimama kizembe kabisa huku akimuita Santos aje ambaye hakusogea badala yake alimtazama Norbeert mkwa umakini akawa anapiga mahesabu ya jinsi ya kumkabili. Akiwa anamtazama Norbet kwa umakini akipanga jinsi ya kumkabili alijikuta akikunja sura kwa nguvu baada ya Norbert kumuonesha kidole cha kati, Santos hapo uvumilivu ukamshinda na alipiga mateke mengine ya miguu miwili lakini safari hii yaliambulia patupu baada ya Norbert kuhama pembeni kwa kasi kubwa.
               "Usitegemee lile pigo la kimama niilokuachia litanipata tena" Norbert alisema huku akikaa kimapigano halafu akawa anamtazama  Santos ambaye alikuwa amejiweka sawa akimtazama Norbert kwa hasira.
     Mpambano baina yao uliwekwa na wote walikuwa wakipigana kwa umakini mkubwa sana, Santos alimfuata Norbert kwa kurursha ngumi mfululizo ambazo zote zilipiga hewa kwa jinsi Norberty alivyokuwa akizikwepa. Aliendelea kurusha mateke ya nguvu ambayo yalipanguliwa na Norbert ambaye hakuwa ameshambulia hata mara moja, Santos alitumia uwezo wake wote wa kupigana katika kuleta mapigo mbalimbali lakini  hakuna hata moja lililompta Norber zaidi ya yote kuishia kwenye hewa. Alibadili mfumo wa kiupiganaji akawa anatumia judo katika kupigana lakini yote haikufua dafu dafu kwani Norbert naye alikuwa akiifahamu judo vyema na aliingia kwa judo naye katika kuizuia judo, mtindo wa judo wa kuangushana Santos alitumia lakini haukufua dafu hata kidogo katika kupambana na Norbert.
   Alipomshika Norbert na kumuangusha  nayeye alifuata chini kwani Norbert naye alimshika wakanguka wote, walikuwa wakibingirishana chini katika eneo hilo. Muda huo wakiwa wanapigana hapo Benson ambaye alikuwa ameishiwa nguvu baada ya damu nyingi kumtoka alifumbua macho kwa shida akawa anatazama  kule ambapo  mwenzake anapambana na Norbert, ukungu mzito ulikuwa umetanda kwenye macho yake lakini alipoweza kumuona Norbert kwa mbali alinyanyua bastola yake ili amlenge aweze kulipa kisasi cha ndugu yake.
    Benson alifyatua risasi muda ambao Norbert na Santos walikuwa wakibingirishana pale chini baada ya Norbert kuwa upande aliolenga, risasi yake alipokuwa anataka kuifyatua tu Norbert tayari alikuwa ameshaiona. Norbert alifanya tendo la haraka kwa mbinu ya mchezo wa judo akamgeuza Santos upande aliokuwa yeye ambapo risasi hiyo ilifumua kichwa cha Santos papo hapo, huo ndiyo ukawa mwisho wa Santos na Benson alipoteza fahamu papo hapo. Walimuacha Norbert tu ambaye alisimama wima kisha akajikung'uta vumbi hadi lilipopungua kwenye nguo zake ambazo bado zilikuwa ni chafu ndipo alipomsogelea Benson pale alipokuwa amezimia, alimtazama Benson kwa dharau kisha akamkanyaga na soli za kiatu chake kooni akammaliza kabisa. Aliondoka hadi kwenye gari lake akaingia ndani akawasha na kuondoka eneo hilo kwa kasi asiweke ushahidi zaidi, nyuma aliacha masalia ambayo  ni pigo sana kwa kina L.J Ibrahim.

****

    Mwanajeshi yule aliyotoka chini ya meza alivua kofia yake taratibu pasipo kujali  amri ya wanausalama hao wanaomlinda Rais, alipoivua kofia wote kwa pamoja waliiona sura ya Moses akiwa anatabsamu tu mkono mmoja akiwa amekunja ngumi. Wanausalama walipomuona ni Moses  walishusha silaha zao kasoro mmoja tu ndiye aliyekuwa akimnyooshea silaha yao huku akimtazama kwa wasiwasi mkubwa sana, Moses alimtazama mwanausalama huyo kwa sekunde kadhaa kisha akakunjua ngumi aliyokuwa ameikunja akatoa kinasa sauti akamrushia rais Zuber ambaye alikidaka akabaki akimtazama kwa wasiwasi.
              "Muulize huyo aliyeninyooshe silaha huku wenzake wakiwa wamezishusha kuhusu hiyo hardware, kwanini aitupe chini ulipogundua msaliti yupo humu" Moses aliongea huku akimtazama mwanausalama huyo aliyekuwa amemnyooshea silaha, Rais Zuber alipatwa na mshangao wa ghafla akabaki akimtazama Mwanausalama huyo aliyekuwa akimuamini kupitiliza.
                "Mheshmiwa jana nilipoaga kuwa naondoka sikuondoka bali nilirudi hapa kwa siri kwa msaada wa mtu mmoja tu miongoni mwa vijana wa wangu waaminifu, msaliti wako ni huyo hapo Kamudu" Moses aliongea.
                 "What! Kamudu msaliti ni wewe!" Rais Zuber aliongea kwa mshangao alkini alijikutra akinyoosha mikono juu haraka baada ya Kamudu kumuelekezea bastola yake aina ya revolver yenye uwezo mkubwa sana, watu wote waliomo humo ndani nao walitoa silaha zao wakamuelekezea Kamudu. Kamudu aliishikilia bastola hiyo kisha akamtazama kila mmoja aliyekuwa amemuolekezea bastola, alimeza funda moja la mate kisha akakaza mikono yake barabara na kidole kkwa kimeshika kifyatulio.
                  "Fanyeni ujinga na mimi nifanye upumbavu!" Kamudu aliongea kwa hasira huku midomo yake ikimcheza.

BASTOLA YA MSALITI YAMUELEKE MHESHIMIWA RAIS, JE NINI KITATOKEA WANAUSALAMA WATAFANYA UJINGA?         USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE NDIYO YENYE MAJIBU YA SWALI HILO


No comments:

Post a Comment