Tuesday, November 29, 2016

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA KUMI NA SITA





RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________


SEHEMU YA KUMI NA SITA!!
    Mtu huyo ndiye aliyekuwa anawasubiri hapo jambo ambalo haliwezekani, haikutokea kwa mtu kama huyo mwenye msimamo mkali amsubiri Askofu Valdermar tena akionekana ni mchangamfu sana.

     Norbert alibaki kutoamini kwa mtu huyo kusalimiana na Askofu Edson kisha akawapungia mkono yeye na vijana wa askofu, kitendawili  kizito kilitanda ndani ya ubongo wake juu ya hali hiyo.

             "Sheikh Ahmed" Alibaki akijisemea moyoni huku akimtazama  mtu huyo ambaye alikuwa amevaa mavazi ya kiislamu, alikuwa akitazamana na mtu huyo mwenye asili ya kiarabu ambaye amefuga ndevu nyingi sana kidevuni mwake. Akiwa ndani ya kanzu safi nyekundu pamoja na kiremba cheupe chenye kizibao chekundu,  sehemu ya uso ilitangaza kwamba mtu huyo anaingia sana nyumba ya ibada  lakini mambo aliyoyaonesha yalimtia shaka Norbert.


****


     Sheikh Ahmed Al-Baggara  muumini mkubwa wa dini ya kiislamu na kiongozi mkubwa wa dini ambaye amekuwa akisimamia misimamo ya dini, kiongozi huyu anatambulika na ulimwengu kuwa kiongozi wa dini mwenye msimamo mkali kutoka nchini Iraq ambaye alijiapiza kutokaa wala kuongea na mkristo baada ya kutokea mtafaruku wa kidini uliohusisha kikundi cha watu waliukashifu uislam.

     Kiapo cha Sheikh huyu kilienda sambamba na kushika kitabu kitukufu  cha kiislamu ili kuonesha kuwa alikuwa anamaanisha kuweka kiapo hicho, aibu iliyoje ilikuwa kwa kiongozi huyu ambaye sasa hivi alikuwa  ameshuhudiwa na macho ya Norbert akiwa anafanya tofauti na kiapo chake. Ingawa hakuwa muumini wa dini wa kiislamu Norbert alibahatika kuwa mtu anayeijua dini hiyo ambayo siyo imani yake kutokana na kazi yake, miiko mbalimbali ya dini hiyo juu ya uvunjwaji kiapo aliitambua vilivyo yampasa mtu kufunga siku tatu mfululizo.

    Hiyo ilikuwa ni sehemu ya sheria ya dini ya kiislamu lakini kwa Sheikh huyu wa Iraq anayetambuliwana dunia kwa ajili ya misimamo yake hiyo haikuwahi kutokea akavunja kiapo kama anavyoonekana hapo, Norbert alibaki akimtazama  Sheikh huyo akiingia ndani ya chumba cha hoteli akiwa amefuatana na Askofu Valdermar. Vijana wa Askofu nao walichukuliwa wakaenda kupewa vyumba vingine kila mmoja, Norbert naye alichukuliwa  akaenda kupewa chumba kingine ambacho hakikuwa mbali sana na kilipo chumba ambacho waliingia Askofu Valdermar na Sheikh Ahmed.

     Kitendawili kingine kingine kilijitega katika kichwa cha Norbert ndani ya siku hiyo na hapo ikamlazimu abebe vifaa  vyake vya kazi visivyoonekana, alijifunga vifaa hivyo kwenye mavazi yake kisha akabaki chumbani humo akiwaza juu ya Askofu Valdermar. Hapo alipata uhakika alikabidhiwa kumlinda asiyehitajika kulindwa dhidi ya mhalifu wa kimataifa, kazi aliyopewa na ofisi yake aliona haistahiki kufanywa kwa mtu mwenye kila aina ya shaka. Askofu mwenye kushirikiana na muuaji Benson na askofu mwenye kushirikiana na Sheikh aliyeweka kiapo mbele ya watu baada ya kukashifiwa mtume wa Mungu rehma na amani ziwe juu yake. Askofu ambaye aliwahi kutoa kauli nzito juu ya imani ya uislamu leo yupo na kiongozi wa dini ya kiislam aliyekuwa anajilikana kwa jinsi anavyowachukia wakristo,

     Norbert alibaki akifikiria hilo muda huo aliobaki hapo ndani na hapo onyo zito  likaja kichwani mwake juu ya hao watu. Wasiwasi wa uwepo  wa kitu kingine kinachowafanya viongozi hao kidini wawe pamoja ndiyo ulimjia Norbert, hamasa ya kuujua ukweli unaowafanya viongozi hao wa kidini wawe pamoja tayari ulishamuingia ndani ya mwili wake hadi vinyweleo vyake vikamsisimka. Wahka wa kutaka kuingia kazini tayari ulikuwa umeshaingia kwenye damu yake, kiherehere cha kuingia katika kazi yake tayari kilikuwa kimeivamia damu yake lakini alikizuia ili asifanye papara katika kazi yake hiyo.

      Muda huo aliopo peke yake chumbani aliutumia  humo aliutumia kujikagua silaha zake kuanzia bastola aliyoichomeka mguuni akaifunika vizuri na suruali yake, aliiangalia kamera ndogo aliyoichomeka kwenye nguo yake ambayo alitaka akusanye ushahidi utakaomsaidia kutegua kitendawili kinachomsumbua kichwani mwake. Alikuwa akijiandaa kuuvaa na upande  mwingine ambao haukuujua ulikuwa umejiandaa namna gani, bahati nasibu ndiyo alikuwa akiicheza ingawa mwenyewe alitambua na alihitaji umakini wa hali ya juu.


****


    Upande wa pili katika hoteli hiyo ya Singita Grumeti katika chumba cha hadhi ya kitalii kutokana na mapambo ya kitalii na muundo wa chumba hicho kilichojengwa kiasili zaidi, samani za gharama zilizojengwa kiasili ndiyo zilionekana kuzidi kupendezesha chumba hicho. Mojawapo wa samani zilizopo humo ndani samani moja ilionekana kupata purukushani isiyo ya kawaida kutoka kwa viumbe   wawili waliopo juu yake, samani hiyo iliyobeba godoro la kisasa ilikuwa katika mtikisiko usio wa kawaida.

     Kitanda hicho ambacho kilibeba  wenye laana kiliendelea kuvumilia hao waliolaanika wamalize laana yao ambayo iliwahi kusababisha wanadamu wa kale kuangamizwa, kitanda hicho kiliumia zaidi kwa kubebeshwa laana hiyo ya waliyolaaniwa. Kitanda hicho kilisononeka muda wote ambayo waliopo juu yake  wakifanya laana hiyo, ilikuwa si mara ya kwanza kitanda hicho kubeba watu waliokuwa wakichoshana miili yao ingawa hakikuwahi kuhuzunika  hata mara moja.

    Siku hiyo kitanda hicho kilisononeka kwa kubeba viumbe wa jinsia moja waliokuwa wakipashana miili yao kwa namna isiyotakiwa, miguno  ndiyo ilikuwa imetawala kwa kiumbe mmoja na mihemo ndiyo ilikuwa imetawala kwa kiumbe  mwingine. Hawakuwa wengine isipokuwa Askofu Valdermar na Sheikh Ahmed ambao walikuwa watupu kama walivyozaliwa wakifanya laana kwa kutumia njia iliyoharamishwa na Mungu muweza, walikuwa wakiitana mume na mke katika kipindi hicho wakichakarika katika kuzidi kumuasi Muumba aliyesababisha wakapata elimu ya dini kwa ajili ya kuwaongoza waumini wengine wawe kwenye mstari ulionyooka.

    Aibu! Aibu! Aibu iliyoje kwa  hawa wanadamu wawili waliouvaa uwakala wa nuru kumbe ni mawakala wa giza, wanafanya mambo yanayoamrishwa kufanywa na mawakala wa giza huku wakiwa na alama zinazowaonesha wao ni mawakala wa nuru. Mavazi ya kiaskofu yalikuwa yapo kwenye sehemu maalum ya kutundika nguo yakishuhudia uharamu huo, msalaba uliokuwa umewekwa mezani pia ulikuwa ni shuhuda mambo hayo. Kanzu safi, kilemba na kizibao navyo vilikuwa vimstundikwa sehemu maalum vilikuwap vikishuhudia mambo hayo huku tasbihi ya kutaja majina ya muumba ikiwa ipo mezani ikishuhudia mbebaji wake akifanya haramu.

     Ama kweli uchamungu siyo mavazi wala kutembea na vitu vya dini muda wote bali uchamungu ni usafi wa roho, Sheikh Ahmed na Askofu  Edson hawakustahiki kuitwa wachamungu hadi muda huo kutokana kuwa ni wachafu zaidi hata ya kinyesi katika roho zao. Laiti wangelikuwa uchafu basi hata kuhifadhiwa katika tundu la choo hawakustahiki kwani walikuwa wamekizidi kinyesi kwa uchafu, hata baharini pia panapowekwa uchafu mkubwa hawakustahiki kuhifadhiwa na ardhini pia lau kama wangehifadhiwa basi ardhi ingesononeka kwa kutupiwa uchafu mkubwa usiostahiki kutupiwa. Walikuwa wakionekana ni watu ambao hawatakaa hata meza moja kuongea masuala ya kidini kwa jinsi walivyo tofauti kiimani, kumbe walikuwa ni watu waliokuwa wakijuana  tangu muda mrefu na walikuwa wameshafanya muungano usio rasmi.


    Askofu Achim Valdermar na Sheikh Ahmed Al-Baggara walikutana nchini Uingereza mara ya kwanza miaka kadhaa iliyopita, Sheikh Ahmed alikuwa yupo ziarani na nchini humo na Askofu Valdermar alikuwa yupo katika mapumziko.  Askofu Valdermar kipindi hicho tayari alikuwa shoga wa kutupwa na aliyekubuhu katika ushoga na alikuwa akiwatumia wanaume maalum wanaofanya mapenzi ili kujiingizia kipato, kwa mara ya kwanza alipomuona Sheikh Ahmed alijikuta amevutika kutokana na utanashati alionao na hapo akatamani awe naye ili aweze kuonja raha za mwanaume wa kiarabu. Sheikh Ahmed naye kwa kipindi hicho alishakomaa katika kufanya usodoma kwa wanawake na alikuwa amejaribu kwa mwanaume mmoja na hapo akatamani aendelee zaidi kutumia wanaume baada ya kuona tofauti yao na wanawake aliowazoea huko kwao.

    Wawili hawa waliazisha uhusiano wakiwa nchini humo na hatimaye baada ya mwaka mmoja wakafunga ndoa  ya kisheria nchini humo kwa siri, tangia hapo walianza kuitana mume na mke pasipokuwa na haya na ndiyo hadi muda bado wapo kwenye ndoa hiyo ya kishetani. Hao ndiyo wanandoa wa jinsia moja ambao walikuwa hawatambuliki na umma zaidi ya kutambulika na watu wachache tu.

      Baada ya kumalliza tendo hilo wote kwa pamoja waliingia bafuni wakaoga, walipotoka tayari kiza ndani ya eneo kilikuwa kimetanda kuashiria mwangaza wa jioni ulikuwa umeshaingia na walienda kula chakula.

     Hali ambayo Askofu Valdermar hakuitarajia sura ya Sheikh Ahmed ilikuwa ni ya hasira kwa ghafla pindi tu walipomaliza kula, alijitahidi kumuuliza juu ya tatizo lililomsibu kwa mahaba  makubwa na hapo ndipo akajua kilichokuwa kikimsibu.

                  "Huyu kijana mweusi ni nani na kwanini uongozane naye?" Sheikh Ahmed aliuliza kiswahili fasaha.

                 "Ni mmoja wa watumishi wa kanisa  nimevutiwa sana kuongozana naye katika safari hii ili isijulikane kama mimi ni mwenyeji ndani ya nchi" Askofu Valdermar aliongea.

                 "Khaa! Sitaki kusikia huo upuuzi naondoka kwenda Musoma mjini na helikopta, nikirudi awe mfu tayari nakujua wewe unapenda sana vijana wa aina ile. Silaha zipo Scorpio na Spider watakusaidia kuhusu hilo" Sheukh Ahmed aliongea huku akivaa nguo.

                "Naenda nikirudi nitamchinja mwenyewe kwa mkono wangu ikiwa nitamkuta akiwa bado anapumua, sasa kama umeanza kuwa na mapenzi naye sitokuacha hai. Chagua umuue kwa risasi au bomu, ukishindwa nakuja kumuua mimi kwa kumchinja" Sheikh Ahmed aliendelea kuongea kwa sauti ya chini iliyojaa hasira huku akimalizia kufunga kizibao, Askofu Valdermar hakujali maneno yake alinyanyuka na kwenda kumsaidia kuweka vizuri kizibao. Alipomaliza alikutanisha mdomo wake na mdomo wa Sheikh Ahmed, alidhamiria kumtoa hasira Sheikh Ahmed lakini hasira zake zilikuwa palepale.

               "Msimamo wangu huwa haubadiliki nikirudi namchinja kwa jambia langu" Sheikh Ahmed aliongea kwa msisitizo kisha akaondoka, wivu wa mapenzi kwa mwanaume mwenzake tayari ulishaanza kumtafuna kwani alimtambua vyema huyu anayemfanya mke wake huwa ana tabia ya kutamani vijana wengine.

     Mawazo hayo ya Sheikh Ahmed yalikuwa ni kweli sana kwani Askofu Valdermar alimteua Norbert kuwa mwenyeji wake kwa lengo hilo, alikuwa amevutiwa na mwili wa Norbert pamoja na utanashati wake ambao unawatesa sana wanawake. Ndiyo maana akamteua ili tu aje kuonja ladha ya penzi haramu kwake,  alitaka amtumie kisha amkate kauli. Adhma yake tayari ilikuwa imeshagundulika na Sheikh Ahmed na akaona alikuwa ana hatiati ya kumkosa Norbert, ili kufanikisha jambo lake aliamua kuwapigia simu vijana aliongozana nao kisha akawaambia kila kitu.

****

     Norbert akiwa chumbani kwake alizama katika fikra sana hadi mbabe wa wababe asiyezuiwa hata na wenye bomu akaja kumdhibiti, akiwa amejilaza kitandani vile vile akiwa chali mbabe huyo alikuja kumdhibiti  akiwa hivyo hivyo baada ya kuzidiwa na uchovu. Ulikuwa ni usingizi ndiyo ulimpitia baada ya uchovu wa safari pamoja na kulala kwa mitego alivyofanya usiku uliopita amlinde Askofu Valdermar, pia hakuwa amepata muda wa kutosha wa kumpumzika tangu alipofanya mapenzi na wanawake wawili kwa siku moja zaidi ya kulala masaa  machache tu ndiyo maana usingizi ulimuonesha ubabe wake kwa njia nyepesi sana.

    Miguu sehemu ya magoti hadi kwenye unyayo ikiwa ipo nje ya kitanda na mwili ukiwa upo ndani ya kitanda, hadi Sheikh Ahmed anaondoka bado yeye alikuwa amezama usingizini. Muda ambao Askofu Valdermar anawaitwa vijana wake ambao wanatambulika kama watumishi wa kanisa aliokuja nao ambao ni Scropio na Spider bado Norbert alikuwa amelala, alikuja kuamshwa na mlango wake kugongwa ambapo alikurupuka akijibua sarakasi kisha akaweka kiganja chake ulipo mguu wake alipoficha bastola yake.

     Mlango ulipogongwa  kwa mara ya pili alijicheka mwenyewe kwa kurupuka kitandani akijua kavamiwa aliposikia sauti hiyo,  mlango uligongwa tena kwa mara ya  tatu hapo akaenda kuchungulia kwenye kioo maalum  kilichopo mlangoni akamuona mgongaji wa mlango huo. Alishusha pumzi kisha akajiangalia kama kila kitu kipo sawa halafu akafungua mlango, mlangoni alimuona kijana wa askofu ambaye ndiye Scorpio akiwa amevaa mavazi mengine ya kiraia ysliyomka vyema.

                "You are needed(unahitajika" Scorpio alimuambia.

                "Ok Lets go" Norbert alijibu kisha akawa anafunga mlango huo.

               "First of all change your clothes like us (awali ya yote badilisha nguo kama sisi)" Scorpio alimuambia Norbert huku akimuonesha mahali alipokuwa amesimama Spider ambaye alikuwa mbali na mlango, Norbert alitikisa kichwa kukubali kisha akaingia ndani akatumia dakika kadhaa kubadili nguo akihamisha zana kwenye nguo nyingine.

     Alipomaliza alitoka akaongozana na Scorpio pamoja na Spider, walielekea moja kwa moja chumbani kwa Askofu Valdermar. Norbert akiwa hana hili wala lile ingawa akili yake haikuhama  aliingia ndani  akakaribishwa kuketi kitandani badala ya kwenye kochi, yote yakiendelea Spider alikuwa amesimama mlangoni na Scorpio alikuwa amesimama jirani na Norbert ambaye alikuwa amekaa sambamba na Askofu Valdermar kwenye kitanda. Maajabu mengine alianza kuyaona hapo baada ya Askofu Valdermar kujilegeza kama mwanamke kisha akaanza kumshikashika Norbert akitaka kulazimisha kubadilishana kimiminika cha kinywani, Norbert alikataa akaanza kumrudisha Askofu Valdermar.

                "What is the meaning of this Bishop(Nini maana ya hii Askofu)?!" Norbert aliuliza huku akimzuia Askofu Valdermar.

                "Iam a gay my son and I like you( Mimi ni shoga mwanangu na ninakupenda)" Askofu Valdermar aliongea huku akipeleka mkono wake kwenye zipu ya suruali ya Norbert akashika kwa juu, kauli hiyo ilimshangaza sana Norbert ingawa mshangao wake haukumtoa kwenye maigizo aliyokuwa anayafanya.

                 "What! Ohh! Jesus Christ I can't do that Bishop, is against the God's rules. God created Adam and Eve not Adam end Steve, means man and woman not man and man (Nini! Ohh! Yesu Kristo siwezi kufanya  hivyo Askofu ni  kinyume cha sheria za Mungu. Mungu kanuumba Adam na Hawa siyo Adam na Steve, inamaanisha mwanaume na mwanamke na siyo mwanaume na mwanaume)" Norbert alimuambia  Askofu Valdermar kwa msisitizo zaidi.

                  "Saints are not yet born in this generation my boy, even you are not Saint (Watakatifu bado hawajazaliwa kwenye kizazi hiki mvulana wangu, hata wewe sio mtakatifu)" Askofu Valdermar aliongea.

                  "Yes Iam not, but you are cursed and Iam not cursed. Thats the difference, evil spirit (Ndiyo mimi siyo, lakini wewe umelaanika na mimi sijalaanika. Hiyo ni tofauti, pepo mchafu" Norbert alisema kwa kujiamini kisha akanyanyuka kwenye kitanda ili aondoke lakini alishindwa hata kupiga hatua akabaki kasimama hivyo hivyo, kitu cha baridi kilikuwa kimgusa juu ya sikio lake la kulia.

      Alipotazama upande wa kulia kwa kutumia jicho lake aliona bastola iliyoondolewa usalama okiwa imeshikwa na Scorpio, kicheko cha kejeli kutoka kwa Askofu Valdermar ndiyo kilifuata. Norbert alibaki akiwa ameganda vile vile mithili ya mtu aliyekuwa yupo kwenye mkanda wa video uliogandishwa, alibaki vilevile huku akitembeza macho kwa Askofu Valdermar akayarudisha kwa Scorpio halafu akayapeleka kwa Spider ambaye alikuwa yupo mlangoni akiea na tabasamu pana mikono kaweka nyuma.

                   "Kijana hutaki siyo sasa utafanya kilazima" Askofu Valdermar aliongea kiswahili kwa mara ya kwanza mbele ya macho ya Norbert ambaye alionekana kushangaa.

                   "Ha! Ha! Ha! Ha! Unashangaa kusikia naongea kiswahili? Kiswahili ni mojawapo wa lugha ninayoongea na Tanzania ni mojawapo wa nchi ninazitambua na mwenyeji sana. Nimekuambia kistarabu hutaki sasa utanifanya kwa lazima, jua nchi hii ikiwa chini yetu hii ni sheria ilimpunguze kuzaliana. Sasa utaanza kufanya wewe kabla nchi haijapinduliwa" Askofu Valdermar aliongea.

                    "Siwezi kufanya hivyo" Norbert alisema kwa jeuri huku akikagua kosa lolote linaloweza kujitokeza  kwa wapinzani wake, hakuona kosa lolote kwani maadui zake walikuwa makini sana na hapo akaamua atumie mbinu nyinginr kwani maadui zake alishabaini hawawezi kumuua eneo hilo pasipo kugunduliwa.

                    "Mtumishi wa Mungu Albert upo kwenye Jack Shaw sasa hivi usiniite Bishop Valdermar, kifo ni haki yako ukatae ukubali. Unakataa ushoga kama rais wako alivyokataa kusaini mkataba aupitishe nchini kwenu ili mpate maendeleo" Askofu Valdermar aliongea huku akimtazama Norbert kwa dharau sana, Norbert alipatwa na mshtuko mwingine baada ya kubaini alikuwa yupo chini ya mikono ya Jack Shaw anayejiita Achim Valdermar pia alipobaini lengo lake kwa Tanzania.

                    "Nipo tayari kufa nikauone ufalme wa Mungu lakini siyo kufanya ushetani unaotaka niufanye" Norbert alizidi kuonesha jeuri huku akipindisha mdomo, jambo hilo lilimkera sana Jack Shaw akataka kumpiga pigo ambalo lingemlegeza lakini alisita baada ya hali nyingine kujitokeza kwa Norbert muda huo pasipo wao kutegemea. Norbert alinyanyua kinywa chake ili azungumze lakini alionekana kushindwa kabisa, alionekana akihangaika kuvuta hewa kwa shida kisha akaanza kukohoa kwa mfululizo huku akiwa amejiinamia. Jack Shaw na vijana wake walibaki wakimshangaa tena Scorpio akabaki akimuangalia huku akiwa amepoteza umakini ingawa bastola  yake ilikuwa imemuelekea Norbert.

              "Kumbe ana  pumu huyu si atanifia mgongoni kwangu" Jack aljongea huku akimtazama Norbert aliyekuwa anakohoa mfululizo, hawakujua kama walikuwa wamefanya kosa kubwa mbele ya mtu mwenye akili nyingi za kufikiria kama Norbert. Hawakujua kama tayari Norbert alikuwa amecheza na akili zao kwa kufanya hila ya kujifanya amebanwa na pumu kumbe macho yake yalikuwa makini kumtazama Scorpio aliyekuwa na silaha mkononi, Scorpio tayari alikuwa amefanya kosa kwa kushughulika kumuangalia Norbert anayejifanya anakohoa kama ana pumu na hapo ikawa nafasi ya pekee kwa Norbert.

      Alifanya jambo ambalo hawakulitarajia kwa kujiinua juu kwa kasi kisha akaupiga mkono wa Scorpio ulioshika silaha, alienda sambamba na kuachia ngumi  nzito ya upper cut(ngumi hii hupigwa kwa chini ya kidevu) aliyoinuka nayo ambayo ilipiga kwenye eneo la chini ya kidevu cha  Scorpio hadi akaaanguka. Ngumi hiyo nzito ilienda sambamba na teke ya kisigino maarufu kama shukrani ya punda, teke hili lilimlenga Jack Shaw(Askofu Valdermar) lakini lilikosa lengo baada ya Askofu Valdermar kuhama eneo alilokuwepo kwa kasi ya ajabu.

     Norbert alipokosa lengo na pigo ake alijianda kuleta pigo jingine lakini alijikuta akiwahiwa kwa namna ya tofauti, kabla hajatoa pigo hilo mlio wa bastola ikitoa kikohozi hafifu kama cha mtoto mdogo ulisikika na hapo akahisi bega lake  likivamiwa na kitu kilichopenya ndani zaidi. Norbert hakutaka utaalamu kujua kwamba risasi ndiyo ilikuwa imevamia bega lake ingawa maumivu yalikuwa bado hayajaanza kusikika, damu kwa taratibu zilianza kumtoka na akaacha kupambana hapo hapa aliposikia kicheko kutoka mlangoni  eneo alilokuwa amesimama Spider.

      Muda huo huo Jack Shaw naye akaanza kucheka kwa nguvu, Norbert alipotazama kule mlangoni alimuona Spider akiwa ameitoa mikono yake aliyokuwa ameificha nyuma ambayo ilikuwa ilionekana ikiwa imeshika bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Moshi hafifu ulionekana kutoka ndani ya bastola hiyo na hapo akatambua kuwa aliyempiga risasi alikuwa ni Spider, hapo maumivu yalianza kuja kwenye bega lake kwa taratibu na akashika sehemu iliyokuea imeumia ili damu isitoke. Ujanja wa kujinasua ulikuwa umemuisha kwani alishabaini Jack Shaw aliyekuwa anapambana naye hakuwa mtu wa ksmawaida pamoja na watu wake pia, ilimbidi awe mpole tu huku akishikilia sehemu aliyokuwa ameumia.

      Hiyo ilikuwa nafasi kwa Jack Shaw ambaye aliachia teke kali lililotua kwenye bega la Norbert lililopigwa  risasi, Norbert aliyumba kurudi nyuma baada ya kushindwa kustahimili uzito wa teke hilo. Huko nyuma alikutana na teke jingine la kuzunguka lenye uzito mkubwa kutoka kwa Scorpio ambaye tayari alikuwa ameinuka tangu apigwe ngumi na Norbert, teke hilo lilimpeleka hadi chini kisha vicheko vikazidi.

                     "Kijana huwezi kuingia kwenye mikono ya Jack Shaw ukatoka ukiwa hai hata siku moja na ukijifanya mjanja utaumia kama ulivyoumia sasa hivi, ndiyo maana nimekuambia siri yetu nikijua hutoki salama. Haya nieleze wewe ni nani hadi uwe na ujanja kiasi hicho eti unajifanya una pumu hadi utake kunipiga. Jack ni ninja wewe hapigwi  kijinga namna hiyo" Jack aliongea kwa dharau sana, Scorpio ambaye alikuwa anatokwa na damu mdomoni alipomuangalia Norbert aliamua kumfuata kwa hasira hasa alipokumbuka ngumi nzito ya Norbert iliyotua kwenye kidevu chake. Alianza kumpiga mateke mfululizo ya mbavu ambayo yote yalimpata Norbert, alizidi kumpiga sehemu mbalimbali  za mwilini mwake  hadi pale Jack Shaw alipokuja kumzuia.

                        "inatosha! Mzibeni hilo jeraha tutoke naye hadi porini tukamuue" Jack Shaw aliongea  huku akimzuia Scorpio.

                        "Kanipiga ngumi hadi nimejing'ata ulimi huyu" Scorpio aliongea kwa hasira akataka kumuongeza pigo jingine lakini Jack Shaw alimzuia na  kumsukuma pembeni.

                       "Mume wangu anarudi muda si mrefu  na team nyingine na amesema hataki kumuona akiwa mzima na akimkuta anamchinja, mzuieni jeraha tukamuue msituni huyu" Jack Shaw aliongea na vijana wake wakafanya kama alivyowaagiza wakabeba na silaha ya kumuulia, walitoka na Norbert humo ndani huku wakitembea naye kiurafiki hadi kwenye gari moja ya hoteli hiyo ambayo waliilipia hela.

      Walimuingiza ndani ya gari Norbert huku wakimdhibiti asifanye ujanja wowote, safari ya kuondoka hotelini hapo kuelekea  katikati ya mbuga ya Serengeti. Waliiingia ndani kabisa ya msitu wa Serengeti hadi eneo lenye mwembamba  ambapo  walimfunga mikono na miguu kwa kutumia pingu  pasipo hata kumpekua zaidi, walipomaliza walitoa bomu aina ya C4 ambalo huwa na saa pamoja na baruti ambazo hufungwa mithili ya karoti na walilitega muda wa kulipuka.

                        "Albert mwana wa Mungu wasalimie huko mbinguni maana ndani ya dakika tatu bomu hili ninaloliweka mbele yako litasambaratisha viungo vyako vyote" Jack Shaw aliongea huku akimuita kwa jina la bandia alilojiita Norbert, wote kwa pamoja walicheka kisha wakaingia kwenye gari wakaondoka  kwa umbali wa mitaa takribani mia tatu halafu wakasimama. Walisubiri kwa muda wa dakika tatu hadi waliposikia mlipuko mzito wa bomu ukitokea walipomfunga Norbert, hapo walijua kazi yao imeshaisha na waliondoa gari kwa mwendo wa kasi.


*Ohhh! No Kaila





TUKUTANE TENA JUMATANO PANAPO UHAI NA AFYA NJEMA





HAIRUHUSIWI KUNAKILI RIWAYA HII KWA NAMNA YOYOTE PASIPO RIDHAA YA MTUNZI









No comments:

Post a Comment