Saturday, December 31, 2016

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA THELATHINI




RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________


SEHEMU YA THELATHINI!!

Kulikuwa na barabara iliyokuwa ikitoka barabara ya magari kwa urefu wa mita thelathini ndipo ulifikie lango hilo lililokuwa na mataa pamoja na mlango mwingine mdogo unaotumika kwa watu wanaoingi kwa miguu. Mazingira yake na jinsi ukuta ulivyokuwa mrefu ndiyo ulimpa hamasa Norbert
kuweza kuifuatilia zaidi nyumba hiyo, baada ya kuisanifu vizuri nyumba hiyo aliamua kupitiliza na gari lake akaenda hadi mtaa unaofuata hadi sehemu yenye bar. Norbert aliegesha gari mahali hapo kisha akavua koti la suti yake akatoka ndani ya gari, alifunga milango vizuri na akaingia ndani ya Bar hiyo.



__________________TIRIRIKA NAYO
     Sauti ya muziki wa dansi ndiyo ilimpokea alipovuka kizingiti cha bar hiyo, ilikuwa ni muziki maridadi mojawapo wa bendi ya muziki wa dansi nchini ambayo ilikuwa ipo namba moja kwa kuporomosha burudani na kuzikonga nyoyo za  mashabiki kila wakiusikiliza muziki wao. Muziki huo ulipenya vyema kwenye masikio ya Norbert lakini haukumshawishi kukaa katika eneo hilo lililokuwa limesheheni mabinti warembo pia, macho yake yalitua kwa mabinti ambao wengine walimtolea tabasamu alipowataza lakini hakushughulika nao. Norbert alipitiliza moja kwa moja hadi mlango wa nyuma wa bar hiyo huku akiacha macho ya baadhi ya wasichana yakiwa yapo kwake kutokana na utanashati wake, alipotoka kwenye mlango wa nyuma wa bar hiyo alifuata uchochoro mwembamba unaotenganisha uzio wa ukuta wa bar hiyo na ukuta wa jengo la Bar hiyo.
  
     Uchochoro huo ulikuwa mrefu sana ambao ulikuwa na kona mbili ambazo njiani Norbert alikutana watu wawiliwawili wakiwa wapo kibinafsi zaidi katika  mwanga hafifu uliopo kwenye uchochoro huo, hadi anamaliza kona za uchohcoro huo tayari alishashuhudia mambo yaliyotosha kuikomaza akili ya mtoto ikiwa atayatazama. Alipozimaliza tu hizo kona za uchochoro alitokea pembeni ya lango la kuingilia katika bar hiyo, alitoka huku akilitazama gari lake lilipo akaliona lilikuwa lipo mahala salama. Norbert alitembea kwa miguu kufuata njia ile aliyokuwa amepita kwa gari wakati akiitalii nyumba ya Wilson ambaye anajulikana sana kwa jina la Nourther. Alitumia muda wa dakika takribani tano tu tayari akawa ameshafika kwenye uzio wa jumba hilo kwa upande wa kushoto, Norbert alitembea kama alikuwa mpita njia wa kawaida ambapo giza ambalo tayari lilikuwa limeshaanza kuingia lilimpa uwezo mkubwa kujiamini akiwa anatembea mahali hapo.

     Norbert aliendelea kutembea pembeni ya uzio huo hadi alipolivuka lango la kuingia hapo ndani akiwa ameangaia vizuri mazingira ya kuingia hapo langoni yalivyo kwa mara ya pili, mita takribani kumi za urefu wa ukuta huo tangu alipite lango hilo aliwea kuingia eneo lenye miti mingi sana iliyopo nje ya ukuta huo. Norbert aliingia katikati ya miti hiyo iliyokuwa ipo jirani na ukuta huo kisha akaupanda mmmojawapo hadi sehemu ambayo ilikuwa ni rahisi kuona kilichopo ndani ya nyumba hiyo iliyo kimya, aliangaza kila pande za ndani ya eneo hilo akisaidiwa na mwangaza kutoka kwenye taa mbalimbali zilizopo hapo ndani. Aliweza kuona eneo ambalo lilikuwa karibu na ukuta huo lilikuwa limezungukwa kwa idadi nyingi ya miti humo ndani mithili ya kulikuwa kuna maonesho maalum ya  wanyama au kulikuwa kuna upandwaji wa miti ya mazao ya misitu iliyokuwa ikitunzwa kwa manufaa ya mmiliki, umbali wa mita zaidi ya hamsini aliweza kuiona nyumba ya kifahari sana ikiwa imezungukwa na mataa mengi yaliyowezesha mazingira yake kuonekana sawia kwake. Ilikuwa ni nyumba iliyokuwa kubwa sana ambayo ilikuwa ina bustani nzuri za maua kwa pembeni yake kwa kila upande ambazo ziliifanya ionekana kama hoteli ya kisasa.
   Nyumba hiyo ilikuwa imetawaliwa na ukimya mkubwa sana ambao ulikuwa ukiifanya ionekane ni ya kipekee sana . Norbert akiwa juu ya mti huo aliendelea kusanifu mazingira ya nyumba hiyo lakini hakuridhika na usanifu wake wa macho ya kawaida tu alitaka aisanifu kwa vizuri zaidi, aliamua kuingiza mkono mfukoni akatoa kitu mfano wa kalamu mbili nene za kuwekea alama (marker pen).  Vitu hivyo ambavyo vilikuwa vimegandana alivivuta vikaachana kwa umbali wa sentimita kadhaa, ilikuwa ni darubini maalum ya kijasusi ambayo ni vigumu sana kufahamika kwa mtu yoyote kutokana na muundo wake ulivyokuwa. Norbert aliiweka darubini hiyo jirani na macho  yake kisha akaelekeza upande wa nyumba hiyo, aliweza kuyaona mazingira ya nyumba hiyo kwa ukaribu zaidi ambapo aliona vitu mbalimbali ambavyo ingekuwa ngumu sana kuviona na macho yake ya kawaida tu. Darubini hiyo iliyokuwa na uwezo wa kugundua ilipo mitambo mbalimbali inaweza kuonesha  nyumba hiyo kwa nje kwa usalama walio ndani, kupitia uwezo huo wa darubini Norbety aliweza kugundua kuwa kulikuwa kuna kamera nyingi za ulinzi ambazo nyingine zilikuwa zimefungiwa kwenye taa mbalimbali hasa maeneo yenye miti iliyo karibu sana na nyumba hiyo.
 
    Norbert pia aliweza kuona kuwa nyumba hiyo ilikuwa na ulinzi mkubwa katika sehemu za getini tu na sehemu zingine kulikuwa kukilindwa na mitambo maalum ya kuwaonesha wezi  ndani ya nyumba hiyo ikiwa wataikaribia. Norbert kwa kutumia darubini hiyo iliyokuwa na uwezo wa kupiga picha alipiga picha mandhari ya humo ndani ya nyumba kisha akashuka juu ya mti huo aliokuwa ameupanda, alitazama mazingira ya pembeni ya nyumba hiyo pindi aliposhuka tu kisha akafungua suruali yake sehemu ya miguuni ambapo alikuwa amevaa soksi ndefu sana  ambazo sehemu ya ugokoni mwa mguu kulikuwa kumetuna kama mchezaji wa mpira akiwa amevaa kifaa cha kulinda mguu wake. Norbert alishusha soksi zake hizo alizokuwa amezipandisha kama machezaji mpira kisha akatoa vitu mfano wa soksi ambavyo alivivaa mikononi. Baada ya hapo aligusa ukuta nyumba hiyo akaanza kupanda mithili ya mjusi anavyopanda kwenye ukuta kwa kutumia vifaa hivyo ambavyo vilimpa wepesi sana katika kupanda ukuta huo hadi juu ambapo kulikuwa na nyaya malum za umeme  kwa ajili ya kuzuia wezi. Alizivuka nyaya hizo kwa umakini mkubwa sana kwa kutumia soksi gnumi ambazo zilikuwa na asili ya mpira kwa upande mmoja ambao haungizi umeme, alipozivuka nyaya hizo alishuka ukutani taratibu kisha akatua sehemu yenye majani kama alikuwa anakanyga ardhi kwa hatua moja na kumfanya asitoe kishindo wakati anatua. Alitazama pande zote kwa upande wa kulia na kushoto na mbele yake kisha akaziweka mfukoni soksi alizopandia ukuta halafu akaanza kutembea kwa mwendo wa tahadhari, alipita katikati ya miti iliyopandwa ndani ya nyumba hiyo kwa tahadhari kubwa akikwepa sehemu zote ambazo kulikuwa kuna kamera za ulinzi alizoziona kwa darubini yake yenye uwezo uwezo wa kuvuta mionzi ya kamera.
 
   Akiwa katikati ya miti hiyo alitoa darubini yake kwa mara ya pili kisha akataazama mazingira ya hapo ndani kwa mara nyingine, alitazama kwa umakini mazingira ya kule ndani ya nyumba akaona kulikuwa kama alivyopaona kwa mara ya kwanza. Alirudisha darubini yake kisha akajiweka sawa aweze kusogea mbele lakini alisita baada ya kuhisi kitu kikimtambaa katikati ya miguu yake, hapo Norbert aliganda kama sanamu huku akivuta hisia hisia kile kilichokuwa kikimparza kwenye miguu yake ni nini. Akiwa yupo katika hali hiyo alisikia vishindo vya mtu akija katika eneo alilopo huku akipiga uruzi, Norbert alitazama pande zote zinazomzunguka hapoo akaona muale wa tochi ukiwa unatembea huku ukimulika chini kuashiria mmulikaji alikuwa akimulika njia yake aliyokuwa akikanyaga ili asiweze kukanyaga kile kisichotakiwa kukikanyaga katika njia yake ndani ya majani hayo ya kupandwa. Norbert aliona hatari ya kukutwa eneo hilo lakini alipopiga hatua moja alijikuta akiharibu mambo zaidi, alikanyaga kitu ambacho hakutarajia kama ndiyo kilikuwa kikimparaza kwenye mkiguu yake.
             "NYAAAAAAAUUU!" Sauti ya paka ilisikika kwa nguvu sana baada ya Norbert kutuliza kiatu chake kwenye mkia wake, paka huyo ndiye alikuwa akimparaza kwenye eneo miguu yake akamfanya asimame kwa ghafla huku akivuta hisia juu ya kilichopo miguuni mwake. Mlio wa paka huyo ulifanya vishindo vile vilivyokuwa vikisikika vizidi kuwa vizito kuashria mtu aliyekuwa akitoa vishindo hivyo alikuwa akikimbia.

****

     Wakati Norbert akiwa yupo kweye haitiyati ya kudakwa na mlinzi yule ndani ya uzio wa nyumba hiyo  ambayo alikuwa nayo umbali wa mitaa zaidi ya hamsini, hali ilikuwa si shwari kabisa kwa umbali wa mita hamsini toka pale alipo. Ndani ya nyumba hiyo ambayo alikuwa yupo mbali nayo kwa mita hizo hamsini, Thomas na wenzake wote waliobakia walikuwa wamechanganykiwa haswa kwa taarifa za vifo vya wenzao waliotumwa kwenda kumdhibiti Norbert. Walikuwa wamekaa sebuleni wote kwa pamoja jioni hiyo, kila mmoja mkono ulikuwa shavuni mwake kwa kupokea taarifa hiyo,walikuwa wakimsubiri mmoja wao aliyebaki ambaye alikuwa awasili muda huo kwa ajili ya kikao.
     Ukimya ndiyo ulikuwa umetawala ndani ya eneo hilo la sebuleni ambalo lilikuwa la kupendeza sana lakini sura zao zilichangia kuifanya sebule hiyo isipendeze hata kidogo na kuonekana ni ya kuchukiza sana. Samani za kisasa ambazo zilikuwa za kupendeza ikiwa wenye nyumba hiyo watakuwa na sura zenye  kupendeza, hazikuweza kuependeza kutokana na sura za wenye nyumba hiyo kutokuwa za kupendeza hata kidogo kutokana na sura za wenye nyumba hiyo kutokuwa za kupendeza. Si L.J Ibrahim wala Mzee Ole,Thomas, Wilson au Josephine aliyekuwa na sura yenye kupendeza kati yao kwa taarifa hiyo ambayo ilikuwa ikiwatia hasira sana juu ya Norbert. Luninga ya kioo bapa ya kisasa iliyokuwa imefungwa ukutani ikionesha haikuwa hata na hadhira aliyokuwa amevutika kuiangalia kutokana na taarifa hiyo, ilikuwa ikitoa sauti pamoja kuonesha picha kwa mandhari ya humo ndani isiyo na uhai lakini si kwa viumbe vyenye uhai maana hakuna hata mmoja aliyekuwa ameitilia maanani hiyo televisheni. Wote kwa pamoja walikuwa wakimgojea kwa hamu mwenzao mmoja ambaye alikuwa hajafika tangu alipotoa ahadi yupo njiani  waweze kuanza kile kilichowafanya wawe pamoja, baada ya muda kioo cha luninga kilitoa mistari ya rangi kama zifanyavyo chaneli za televisheni zikifungwa.

   Sauti ya kengele pamoja na kubadilika kwa picha baada ya kutokea kwa rangi hiyo ndiyo vilifuata, picha iliyofuata kwenye kioo cha luninga hiyo ilikuwa ni ya mandhari ya getini ambapo ilionesha gari aina ya toyota landcruiser nyeusi ikiwa getini mwa nyumba hiyo. Kuonekana kwa picha hiyo wote kwa pamoja walinyanyua shingo zao wakitazama kioo cha luninga hiyo huku wakiwa na sura zenye ahueni baada ya subira yao kufikia kikomwe, gari hiyo iliganda kwa muda wa dakika moja getini hapo pasipo kufunguliwa kwa geti hilo.
                 "Huyu mlinzi yupo wapi mbona hamfungulii kamishna aingie hajui kama tunamsubiri yeye future IGP wetu tu"  Wilson aliongea kwa hasira hukua akikitazama kioo hicho.
               "Usiwe na papara mdogo wangu huenda ameenda kujisaidia ni binadamu huyo kama wwe hubanwa na haja pia" Mzee Ole alimuambia Wilson kwa upole, muda huohuo alipomaliza kumtuliza hasira mdogo wake geti lilianza kufunguka na gari hiyo iliyopo getini ikaingia ndani kwa mwendo wa wastani sana.

****

     Vishindo vilipokaribia zaidi Norbert alifanya kitendo cha upesi zaidi cha kujirusha juu akadaka tawi la  mti ambalo alilishikilia  vyema akajivuta juu akatulia, sekunde chache baadaye alimuona mtu aliyevaa sare maalum  za walinzi akifika hapo chini akiwa amebeba tochi kubwa. Mtu huyo alimuona kupitia mwangaza wa tochi aliokuwa akioumulika chini ya miguu yake kila akitembea, mtu huyo alipofika aliangaza  kwa kumulika kwenye eneo alilokuwa amesimama Norbert awali na alimuwezesha Norbert kuona idadi kubwa ya paka wa kizungu nwenye manyoya mengi wakiwa wamelala kwa pamoja kwenye majani huku wengine wakicheza.
             "Khaaaa! Yaani hii mipaka kumbe inapigana yenyewe bwana" Mlinzi huyo aliongea baada ya kuona alikimbia mbio nyingi zisizo na tija na akataka kuendelea kumulika maeneo ya pembeni ya eneo hilo lakini alisita baada ya mlio wa kengele maalum kusikika mfukoni mwake, aliingiza mkono kwenye mfuko wa gwanda lake la ulinzi akatoa kitu mfano wa simu akakitazama na kisha akaghairi kumulika maeneo ya jirani na hapo akatimua mbio kurudi getini.
   Muda huo ndiyo muda ambao gari ya Kamishna Wilsfredi ilikuwa ipo getini na kifaa maalum kilichokuwa kipo mfukoni mwa mlinzi huyo ndiyo kilimjulisha kupitia mitambo maalum iliyokuwa imeunganishwa na kifaa hicho iliyopo getini, nyumba hiyo ilikuwa ikilindwa na mitambo ya kisasa sana ambayo hata kwa baadh iya taasisi muhimu haikuwa nayo kabisa ndani ya nchi hii. Mitambo hiyo inayotumika kuilinda nyumba hiyo ni mitambo iliyoletwa kwa agizo maalum la Sheikh Ahmed kiongozi mkuu wa mpango mzima, mitambo hiyo iliiingia Tnazania kwa njia za panya na hatimaye ikaja kufungwa ndani ya nyumba hiyo na mafundi maalum walioletwa baada ya Wilson kujitolea nyumba yake iwe sehemu ya mpango huo. Ilikuwa imeandaliwa kwa siku nyingi nyumba hiyo ndiyo maana ikafungwa mitambo maalum  ambayo inaipa nafasi ya pili kati ya nyumba zenye ulinzi mkali ndani ya nchi ya Tanzania baada ya Ikulu ya Rais. Ulinzi wa nyumba hii haukuwa ukijulikana kama ni mkubwa kiasi hicho zaidi ya kujulikana na watu wachache tu wenye maslahi ya aina moja tu, ilikuwa ni nyumba inayoweza kujiongoza yenyewe katika suala la kugundua uvamizi wowote uliokuwa ukikairibia usawa wa vifaa vyake vilivyokuwa vimetegeshwa katika pande mbalimbali.
   Baada ya mlinzi kutoweka maeneo ambayo Norbert yupo alienda moja kwa moja kufungua geti akihofia kupewa lawama na hata kibano kwa kuchelewa huko kuufungua geti, baada ya geti hilo kufunguliwa gari aina ya toyota landcruiser nyeusi ambayo ndiyo ilionekana kwenye luninga sebuleni walipo kina Thomas ililivuka geti hilo kwa taratibu sana kisha ikongeza mwendo kupita katika barbara ya lami iliyokuwa imejengewa ndani ya nyumba hiyo. Norbert alikuwa ameshaiona gari hiyo na alishuka kwenye mti aliokuwa ameupanda kwa taratiubu sana kisha akaanza kwenda kwa mwendo wa wastani ulio na tahadhari kubwa sana, alikuwaa kilifuatilia gari hilo lililoingia getini hapo kwa umakini mkubwa sana  ambapo muda huo lilikuwa likiuzunguka mzunguko maalum uliokuwa ukiunganisha njia tatu toafati zilizokuwa zikielekea sehemu tatu tofauti ndani ya nyumba hiyo iliyokuwa kubwa sana mithili ya hoteli.

   Aliifuatilia gari hiyo hata baada ya kuupita mzunguko ikawa inaendelea mbele kuifuata nyumba waliyopo kina Thomas, kutokana na kasi ya gari hiyo ilipelekea iwahi kufika kabla hata Norbert hajasogea karibu zaidi. Hali hiyo ilimfanya Norbert atoe darubini yake palepale alipo kisha akawasha sehemu maalum ya kupigia picha,aliiweka darubuni hiyo jirani na macho yake akiwa bado yupo katika eneo lenye mitimingi ndani ya nyumba hiyo. Aliivuta karibu zaidi hiyo gari ambayo muda huo mlango wa dereva ulikuwa umefunguliwa, aliweza kumshuhudia Kamishna Wilfred akitoka ndani ya gari hiyo akionekana ni mwenye haraka zaidi. Norbert aibonyeza kitufe cha kupiga picha akampiga picha huku akitoa tabasamu kwa kuweza kupata ushahidi zaidi wa kazi yake, hadi Kamishna Wilfrd anaingia ndani ya nyumba  tayari alikuwa ameshampiga picha nyingi sana kwa haraka. Wepesi wake wa uandishi wa habari aliutumia hapo katika kubonyeza viufe vya kamera darubini hiyo kupata picha nyingi zaidi, baada ya kumaliza kuzipiga picha hizo aliibusu darubini yake kisha akasogea pembeni zaidi ya eneo alilopo ambapo aliweza kuona dirisha la sehemu ya mbele ya nyumba hiyo lakini hakuweza kuona na wala kupata kila kitu alichokuwa akikihitaji na ikambidi atumie akili ya ziada.

****
MBAGALA KIZUIANI
     Maeneo ya mbagala Kizuiani mbele ya kituo cha daladala cha magari yanayotoka mjini kwa mitaa kadhaa kulikuwa kuna mwanajeshi aliyenyoosha bendera nyekundu yenye kitambaa chenye kung'aa kikimulikwa na taa. Mwanajeshi huyo alikuwa amesimama mbele ya makutano ya barabra ya kilwa na inayoenda jeshini, magari yote ya barabara hiyo ya yalisimama baada tu bendera hiyo nyekundu kunyooshwa muda huo wa jioni na kupelekea foleni iwe kubwa sana katika barabara ya Kilwa. Upande wa mita kadhaa mbele kwenye sehemu ambayo kulikuwa kuna uwazi ambao unaruhusu magari yanatoka mjini kuingia upande wa kulia karibu na ofisi za TRA Mbagala napo kulikuwa na mwanajeshi mwingine aliyekuwa ameshika bendera nyekundu akizuia magari yanayotoka Zakhem yasipite eneo hilo. Ilikuwa ni jambo la ajabu sana kwa kutokea kwa jambo hilo katika eneo hilo ambalo kulikuwa kuna njia ambayo ilikuwa ikielekea kwenye kambi ya jeshi.

   Watu walijiuliza juu ya kutokea kwa hali hiyo lakini walipata majibu baada ya kuona miale ya rangi ya machungwa ikitokea kwenye ile barabara inayoelekea jeshini. Miale hiyo ilikuwa ni ving'ora vya magari makubwa sana ya kubeba mizigo ya jeshi ambayo yalikuwa na idadi kubwa sana na yaliingia kwenye barabara hiyo ya Kilwa kuelekea upande wa Zakhem, magari hayo yalikuwa yamebeba vifaru vizito sana vya jeshi ambavyo viliyafanya yatembee kwa taratibu sana. Umati wa watu waliokuwa wapo karibu na eneo hilo walibaki wakishangaa vifaru hivyo vizito ambavyo hawakuwahi kuviona vikiwa vimebebwa na magari hayo katika mazngira kama hayo zaidi ya kuviona kwenye maonesho ya kitaifa. Ubebwaji wake kwenye magari hayo ilikuwa ni  kuhofia kuharibu  pindi vitakavyotembea kwenye barabara ya lami. Magari hayo makubwa yalipoisha tu yalifuata magari ya wazi ya jeshi aina ya hummer yaliyokuwa yamejaa wanajeshi walio na silaha za kizita, magari hayo yaliingia barabrani kwa kasi kubwa zaidi huku wanajeshi hao    waliojichora usoni mwao wakishangilia kwa nguvu. Ilikuwa ni hali iliyozua maswali sana lakini watu walipoungaanisha tukio la kuzungukwa kwa ikulu na hilo la wanajeshi waliona ni uongezwaji wa nguvu ya kuzunguka ikulu. Haikuishia hapo magari yenye mizinga mizito nayo yaliingia katika barabara hiyo yakiwa na ving'ora juu, yaliingia yakiwa yamebeba wanajeshi wa kikosi maalum cha wapiga mizinga.
   Baada ya msafara huo uliochukua muda mrefu sana kuingia barabrani kuisha magari kama kawaida yaliruhusiwa kuendelea namatumizi ya barabra kwa upanmde wa magari yaliyokuwa yakirudi mjini jioni hiyo, barabara iliyokuwa ikitoka Mbagala kuelekea mjini bado ilifungwa kwa kutangulia gari ya kijeshi iliyokuwa ikitoa amri kwa magari mengine kuwekwa pembeni. Msafara huo wa magri ya jeshi ulipita barabara ya kilwa  yote hadi ulipofika bandari ukaelekea ulipo mzunguko wa barabara unaounganisha barabara  inayoenda kariakoo na inayoelekea stesheni katika mtaa wa Gerezani. Magari hayo kwa mwendo uleule yaliyokuwa yakienda yaliingia barabara ya inayopita mtaa wa gerezani kisha yakaipita hadi stesheni yakanyoosha barabra moja kwa moja hadi posta ya zamani pembezoni mwa bahari, yaliipita posta ya zamani yakaelekea kivukoni ambapo yaliingia hadi barabara ya Obama kulipokuwa kuna wanajeshi wengine wa kikosi cha maji waliokuwa tayari wapo eneo hilo.


ITAENDELEA!!


UKIITAKA HAPA ILIPO HADI MWISHO UNAWEZA KUIPATA KWA SHILINGI 3000,MAWASILIANO YAPO HAPO JUU. MAWASILIANA NASI KWA UJUMBE MFUPI(SMS) KWA MAELEZO ZAIDI

No comments:

Post a Comment