Sunday, January 1, 2017

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA



RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________



SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA!!

    Msafara huo wa magri ya jeshi ulipita barabara ya kilwa  yote hadi ulipofika bandari ukaelekea ulipo mzunguko wa barabara unaounganisha barabara  inayoenda kariakoo na inayoelekea stesheni katika mtaa wa Gerezani. Magari hayo kwa mwendo uleule yaliyokuwa yakienda yaliingia barabara ya inayopita mtaa wa gerezani kisha yakaipita hadi stesheni yakanyoosha barabra moja kwa moja hadi posta ya zamani pembezoni mwa bahari, yaliipita posta ya zamani yakaelekea kivukoni ambapo yaliingia hadi barabara ya Obama kulipokuwa kuna wanajeshi wengine wa kikosi cha maji waliokuwa tayri wapo eneo hilo.


___________
______________TIRIRIKA NAYO
____________

    Kuingia kwa kikosi hicho cha jeshi la ardhi katika barabara hiyo ya Obama iliyopo mbele ya Ikulu kwa  mita kadhaa kuliwafanya wanajeshi wote waliokuwa wameizunguka Ikulu kurudi nyuma kidogo ili kuwapisha wenzao, walikuwa washapata taarifa ujio wao katika eneo hilo hivyo waliwapisha kwa hatua kadhaa nyuma na magari hayo yaliyokuwa yamebeba vifaru yakaegeshwa hapo barabrani. Magari mengine yaliyokuwa yamekuja hapo yalishusha wanajeshi wengi wa jeshi la ardhini wakiwa wapo kamili kila idara kama walikuwa wanaenda  vitani, wanajeshi hao wote waliposhuka walikaa kuangalia mbele wakiwa wameizunguka kama amri waliyopewa  na mkuu wao.
    Vifaru vizito vilivyokuwa vipo ndani ya magari makubwa ya mizigo ya jeshi navyo vilishuka taratibu kisha vikapanga mstari mmoja  mbele ya ikulu kama walivyokuwa wameagizwa, makombora yote yalikuwa yameelekezwa ikulu ikiwa ni sehemu ya kutimiza mpango waliokuwa wamepewa. wanajeshi wote wa jeshi la maji waliokuwa wameizunguka ikulu walikaa nyuma ya  wenzao waliokuwa wametangulia mbele kwa amri ya mkuu wao M.J Mugiso ambaye aliamini wote walikuwa wapo upande mmoja wa kutaka kumuondoa rais Zuber madarakani. Hawakutambua kama kikosi hicho kilikuwa kimetumwa kwa kazi nyingine tofauti na kazi yao waliyokuwa wamepewa hapo, laiti kama wangelitambua hilo basi wasingeweza kuwapisha hapo kwa ajili ya kuwaweka wao mbele kwani ni hatari sana  kwa kazi yao hiyo. Muda huohuo  ndege za kivita zenye makelele mengi sana zilipita eneo hilo kwa kasi sana na zikiwa na kazi ya kuizunguka ikulu tu  jambo ambalo lilisababisha watu waliomo ndani ya ikulu hiyo kuwa katika hali ya woga sana kila wakizitazama ndege hizo, ndege hizo ambazo mara nyingi huonekana sana katika maonesho ya sherehe za uhuru au muungano na zilipita hapo kwa tano mfululizo  kisha zikarudi katika kambi ya jeshi la anga Dar es salaam.
   Kiongozi wa vikosi vyote vilivyoingia eneo hilo alikuwa ni meja kutoka kambi ya jeshi la ardhi mbagala, meja huyo tayari alikuwa amefika eneo hilo sambamba na vikosi alivyokuja navyo eneo hilo akiwa ndiyo mtoaji wa amri kuu kwa hao. Uwepo wake eneo  ulimfanya M.J Mugiso atoke hadi kwenye eneo la jirani na njia inayoelekea lilipo lango la kuingia katika ofisi ya waziri mkuu ya hapo ikulu, M.J Mugiso alienda hadi eneo hilo ambapo kulikuwa kuna hema maalum ambalo tayari lilikuwa limewekwa na wanajeshi wa jeshi la ardhi kwa ajili ya kamanda wao waliokuja naye hapo. M.J Mugiso alipofikia eneo la jirani na hema  hilo alipokea saluti nyingi kutoka kwa wanajeshi ambao walikuwa wapo nje ya hema hilo, alipoingia ndani napo alipokea saluti kwa kila mmoja hadi kiongozi wa kikosi hicho ambaye alikuwa yupo ndani ya hema hilo akiwa amekaa sehemu moja na wanajeshi waliokuwa wataalamu wa masuala ya tarakilishi na mawasiliano kwa ajili ya kikosi cha anga.
               "Meja Kiboni" M.J Mugiso aliongea mbele ya meja huyo
               "Mkuu" Meja Kiboni ambaye ndiye kiongozi wa jeshi la ardhi kwa eneo hilo aliitikia.
                "Nafikiri ushapewa taarifa zote kuwa mpo chini yangu kwa siku hizi mbili za kumuondosha msaliti wa ikulu" M.J Mugiso aliongea kwa tabasamu.
                "Hapana mkuu sijapewa taarifa hizo, taarifa nilizopewa hadi naleta kikosi eneo hili ni kuwa niwe nasikiliza amri kutoka kwa kamanda mkuu wa  kikosi mkuu Belinda tu na si vinginevyo" Meja Kiboni aliongea maneno ambayo yalimfanya M.J Mugiso afinye uso wake kwa kutoamini.
                 "Meja taarifa zilizopo kutoka kwa Luteni Jenerali ambaye ndiye General mtarajiwa ni kwamba mtakuwa chini yangu nyote kwani mimi ndiye mkubwa hapa na pia ndege zote za kikosi cha anga zitaenda kutua kwenye nyambizi za kikosi cha maji ambapo kuna uwanja tayari upo kwa ajili yao" M.J Mugiso aliongea
                  "Mkuu taarifa niliyoambiwa ni hiyo tu siyo nyingine, nimeonywa nisifuate amri ya yoyote pasipo  mkuu Belinda kuipitisha amri hiyo kwa makamanda wangu wakuu tu" Meja Kiboni aliongea kisha akamgeukia mwanajeshi mwenye nyota mbili mabegani mwake ambaye alikuwa yupo karibu na vioo vingi vya tarakilishi ndani ya hema hilo.
                   "Unganisha video call kwa Mkuu Belinda haraka sana" Alimpa amri mwanajeshi huyo mwenye cheo cha luteni kisha akayarudisha macho alipokuwa M.J Mugiso.
                  "Sir" Luteni huyo alitii mari kisha akafanya kazi yake mara moja na ndani  muda huo kioo cha tarakilishi kilionesh alama za vidoti vikiwa vinazunguka duara huku maandishi ya kingereza yaliyosomeka 'waiting' yakitokea juu yake. Maandishi hayo yalipotoka sura ya M.J Belinda ilionekana kwenye koo hicho akiwa ameva nguo za kijeshi kasoro kichwani hakuwa na kofia, Meja Kiboni na M.J Mugiso walitoa saluti kwa alipoiona sura ya M.J Belinda kwenye kioo hicho.
                    "Belinda" M.J Mugiso aliongea akikitazama kioo hicho.
                    "Mugiso: M.J  Belinda aliitikia
                     "Mbona unaenda kinyume na amri ya mkuu Ibrahim si umeambiwa majeshi yote yawe chini yangu katika operesheni hii" M.J Mugiso alimlalamikia M.J Belinda
                     "Majeshi yaliyopo chini ya komandi yangu hayawezi kuwa chini yako hata siku moja Mugiso, wewe ni msadizi kwenye kikosi chako na mimi ni mkuu katika kikosi changu. Unapokea amri mimi natoa amri" M.J Belinda aliongea
                     "Aaah! Belinda inamaana unapinga amri ya three star general tuwe wote kwenye operesheni hii" M.J Mugiso aliongea.
                      "Amri ya kuwa wote katika eneo hili itakuwa palepale lakini si vikosi vyangu kuwa chini yako hiyo haipo kwangu. Vikosi vyangu vipo chini ya komandi yangu tu nafikiri umenielewa Mugiso, hao hawawezi kupinga amri niliyowapa" M.J Belinda aliongea
                      "Khaaa! Nini?!" M.J Mugiso aliuliza kwa hasira  sana.
                      "sisi wote ni two star general Mugiso lakini kuwa wote cheo kwenye cheo kimoja haimaanishi kwamba   hakuna mkubwa kati yetu, umenikuta kwenye cheo hiki hivyo mimi ni mkubwa ni wako tu ndiyo maana ukasaluti pamoja na Kibona ulipoiona sura yangu muda mfupi uliopita. Hivyo huna haki ya kuingilia maamuzi yangu katika misheni hii, kikosi nimeleta  hapo lakini kipo chini ya amri zangu hata kama sipo na hadi kesho  nitakapofika kitakuwa kipo chinii ya amri yangu vilevile"   M.J Belinda aliongea maeno hayo ambayo yalimkera sana M.J Mugiso lakini yalikuwa ni kweli tupu kuwa alikuwa ni mdogo kicheo kwa M.J Belinda, kuwa wote mameja jenerali hakukumaanisha kuwa hakukuwa na mkubwa kati yao.
                     "Kiboni fuata amri zangu kama nilivyokuambia tumeelewana" M.J Belinda alimsisitiza  Meja Kiboni kisha akaendelea, "Mugiso huna haki ya kuvunja amri hii na kuuifuata unapaswa kuanzia muda huu, tumeelewana".
     Maneno hayo yalikuwa ya kukera sana kwa M.J Mugiso lakini hakuwa na ulazima zaidi ya kuyafuata tu kwani aikuwa ni mdogo kwa M.J Belinda ingawa wote walikuwa wapo cheo kimoja kimoja, hakuitikia kwa kinywa chake aliposikia amri hiyo yeye alipiga saluti tu kiukakamavu kisha akatoka ndani ya hema hilo pasipo kuongeza neno lolote. Alikuwa amekasirirka sana kwa jinsi alivyokuwa akitarajia ni tofauti na aliyoyakuta huko, aliondoka moja kwa moja kurudi katika eneo alilokuwa hapo awali kwenye hema la wana maji ili kuendelea na taratibu zingine.

****

    Mlango wa kuingilia sebuleni ulipofunguliwa ndipo watu wote walipopata na ahueni kidogo baada ya mtu waliyokuwa wakimsubiri kuwa tayari ameshafika katika eneo hilo, waligeuza nyuso zao zisizo na dalili yoyote ya furaha kumtazama Kamishna Wilfred ambaye alikuwa ni amechelewa katika kikao hicho kuilichokuwa kifanyike muda mfupi kabla na kuchelewa kwake ndiyo kulikifanya kikao hicho kuchelewa kuanza.
                 "Mniwie radhi jamani nilikuwa nimekumbwa na mambo kifamilia ndiyo maana nikachelewa kufika ndani ya eneo hili" Kamishan Wilfred aliongea huku akielekea kwenye kochi lililokuwa tupu akaketi.
                  "hakuna kilichoharibika kamishna nadhani tuendelee na kikao chetu sasa hivi" Mzee Ole aliongea
                   "Ok jamani nafikiri mnaona mambo yanavyozidi kuwa mabaya zaidi inabidi tutafute jinsi gani ya kuweza kuyatatua la si hivyo mpango wetu utaegemea tu kwenye vkosi vya jeshi vilivyokuwa vimeizunguka ikulu  tu, nadhani mnatambua jinsi gani Norbert ambavyo amezidi kuwa hatari kwetu na tumejaribu kumteka zaidi ya mara ya mbili akatuzidi akili" Wilson aliongea
                     "Enhee! Tena kamishana kuna jambo nilisahau kukuambia kuhusu huyu Norbert, kwa taarifa nilizozipata huyu ndiye aliyemuua ndugu yako Kitoza akishirkiana na mpelelezi mwingine hatari kutoka Rwanda Hilda Alphonce katika usiku ile ambayo Kitoza na Eagle walikuwa wawaue Zuber na wenzake kama nilivyowaagiza nikiwa bado nipo ikulu" Mzee  Ole alimpa taarifa mpya kabisa Kamishna Wilfred.
                   "Nadhani unaona ni jinsi gani huyu mtu alivyo hatari Kamishna hatunao Reginald Kitoza mpelelezi hatari na aliyekuwa mkuu wa TISS ambaye ni mwenzetu, Benson, Benjamin na Santos hata Eagle ninja aliyeaminika  na kaka pia alouawa naye. Hapa huyu mtu ni hatari sana sasa inabidi tumpunguze kasi yake ya kufanya kazi ili achelewe na mpango wetu ufanikiwe kwa haraka, uharaka wake katika ujasusi wake ni hatari kwetu" Wilson alizidi kumuambia Kamishna
                    "Ok nimewalewa sasa tufanyeje? Na huyu nataka nimuue mwenyewe kwa mkono wangu kulipa kisasi cha ndugu yangu mwenyewe" Kamishna Wilfred aliongea kwa hasira aliposikia habari hiyo.
                     "Kumuua peke yako bali tutamuua sote nataka kulipa kisasi cha Benjamin pia" Josephine naye alidakia akionekana ni mwenye hasira sana
                    "Cool down Leopard Queen.....Taratibu Kamishna huyu mtu hauliwi tu kama kuku wa kizungu anayeandaliwa kutayarishwa nyama na mpishi, huyu mtu inabdi kwanza tumpunguze kasi then Mzee Ole arudi ikulu ndipo tuongeze nguvu ya kumtafuta tumuue" Thomas aliongea
                    "Enhee! Hilo ndiyo la muhimu kabisaa, na mimi ndipo nitakapopata wasaa wa kulipa fadhila zaungu kwa marehemu Kitoza kwa kuhakikisha huyu mtu anakamatwa na umuue kwa mkono wako ukishirikiana na Leopard Queen   maana yeye pekee ndiye aliyetutia hasara tangu nikiwa madarakani halafu  akaja kumpa kisa cha jinamizi mtunzi wa riwaya Hassan Mambosasa aandike akisema ni sehemu ya utafiti wake kama mwandishi wa habari" Mzee Ole aliongea
                     "Naye huyu mwandishi wa riwaya dawa yake inachemka kwa sasa maana ndiyo aliifanya nchi hii imchukie kaka yangu" Wilson aliongea
                     "Wilson hebu achana na huyo novelist sisi tudili na huyu mtu maana akizimwa basi huyo novelist hatokuwa na jipya" Thomas  aliongea
                     "Kabisa Thomas, sasa kamishna  inabidi umuwekee zengwe ashindwe kufanya kazi yake vizuri then niingie ikulu tumpe adabu kisawasawa" Mzee Ole aliongea
                     "Worry out future president, kuhusu kesi mbaya tu hapa nyumbani kwake kesho tu mtapata matokeo sasa hivi nikitoka naenda kufikiri kesi ya kumpakazia tu" Kamishna Wilfred aliongea.
                      "Tena huyu mtu zikianza ndoa ya jinsia moja aanze yeye kuwa mke kisha huyo rais kwake anayekataa dola milioni 600 kusaini mkataba kwa kujifanya mzalendo ndiyo afuate" Mzee Ole aliongea.
                      "wacha wenye kutaka fedha kama sisi tuendeshe life tupige kazi, kamishna tunakutegemea  kwa hilo our future IGP kaka akiingia ikulu tu. Chulanga hana chake yule" Wilson aliongea
                        "General mbona upo kimya hivyo siku ya leo?" Mzee Ole aliacha kuchangia kikao hicho akamuuliza  L.J Ibrahima ambye aikuwa amekaa kimya tu hajachangia chochote tangu kuikao hicho kianze.
                          "Hapana tupo pamoja jamani, nilikuwa natafakari juu ya mpango wetu wa kuhakikisha majeshi yote yawepo ikulu maana naona kimya" L.J Ibrahim aliongea
                           "kwani bado tu air force na wa ardhini hawajafika tu au  wameasi amri tayari" Wilson aliuliza, L.J Ibrahim alipokuwa akijiandaa kujibu swali hilo simu yake ya mkononi iliita na alipoitoa kuangalia mpigaji wake alijikuta akitabasamu.
                          "Enhee! Simu ndiyo hii nilikuwa natarajiwa kupigiwa kuanzia muda huu" Alongea na wote wakaka kimya kumuacha aipokee simu hiyo, L.J  Ibrahim aliipokea simu akaongea "sema kijana... anhaa ok ok nashukuru kwa taarifa yako"
      L.J Ibrahim alikata simu kisha akawatazama wenzake akiwa amejawa na tabsamu halafu akaongea, "tayari kikosi cha jeshi la ardhi chenye vifaru, mizinga na wanajeshi kimetoka kambi ya mbagala, huyu mtu aliyenipigia ni kijana wangu yeye ameuona msafara huo  ukimalizia kulivuka daraja la reli ya tazara linalopita Mtoni mtongani".
      Kauli hiyo ilowafanya wote watoe matabsamu ya furaha na hata ikawasahulisha juu ya vifo vya wenzao ambavyo vimetokea masaa akdhaa yaliyopita ndani ya siku hiyo, kikao hicho hadi kinafikia muda huo bado kikosi cha jeshi la ardhi kilichotoka Mbagala kilikuwa hakijafikia kabisa magogoni. Kilikuwa bado kipo njiani wakati mkutano huo ukiwa unaendelea, baada ya mpango huo waliompa kamishna Wilfred autekeleze kukamilika Kamishna Wilfred alisimama kwenye kochi kisha akaaga.
         "Jamani wacha niwahi mara moja maana nimemtoroka wife hiyo ishu ya kifamilia sijaisolve bado" Kamishna Wilfred aliongea huku akimpeana mikono na kila mmoja, wote kwa pamoja walisimama baada ya kikao hicho kufikia tamati. Walitoka nje kumsindikiza Kamishna hadi alipokuwa ameegesha gari lake pasipo kutambua kuwa ndiyo walikuwa wakimpa ushahidi zaidi Norbert ambaye alikuwa akifuatilia kila hatua yao na hata ajenda yao waliyokuwa wakiipanga tayari alikuwa ameisikia baada ya kuondoka katika eneo alilokuwepo hapo awali na kusogea jirani na nyumba hiyo baada ya kuichezea mchezo mchafu mitambo ya ulinzi ya mahala hapo.

****

    Baada y Norbert baada ya kuzishinda nguvu kamera za ulinzi za eneo hilo kwa kutumia mionzi mikali ya darubini yake, aliweza kuzifanya zisimuone kwa muda  ambao atakuwa katika eneo hilo. alizunguka nyuma  ya nyumba hiyo na akapanda juu ya paa kisha akatembea taratibu hadi  kwa juu kwenye kibaraza kirefu cha nyumba hiyo ambacho kiikuwa kipo karibu na sebule waliyokuwa wamekaa kina Thomas. Alipofika kwenye kibaraza hicho aliweza kutega kinasa sauti jirani na dirisha la sebule hiyo ambapo aliyanasa maongezi yote yaliyokuwa yakiendelea ndani ya nyumba hiyo hadi yanamalizika, Kamishna Wilfred aliposindikizwa na wenzake wote hadi mbele ya baraza yeye alitumia darubini yake kama kawaida na kuwapiga picha wote bila wao kujijua. Norbert  picha nyingi alimpiga mzee Ole ambaye ndiyo kwanza alikuwa anamuona tangu aliposikia amelipuliwa na bomu kule njia ya kwenda Tabata siku chahce zilizopita, baada ya kupiga picha hizo alitulia huko juu hadi Kamishna Wilfred alipoondoka na wote walipoingia ndani ndipo naye alishuka kwa ujanja mkubwa wa mafunzo ya kininja aliyokuwa nayo.
    Alikimbia kwa kukanyaga vidole ambapo hakutoa sauti hadi kwenye eneo alipokuwepo awali kwenye miti mingi, alipita katika njia ya tofauti na eneo alilokuwa amepita hapo awali kuhofia kuwakanyaga tena walepaka  hadi  kwenye mti mwingine wenye majani marefu kisha akachuchumaa chini kwa ghafa baada ya kusikia uruzi mtu. Alisikia vishindo kama ilivyokuwa awali kisha vishindi hivyo vikasimama, uruzi uliendelea kuvumana Norbert akaendelea kuchuchumaa katika eneo lenye majani mengi kama pori fulani hapo. Alikuwa amekaa kwenye eneo ambalo alijuta kwanini asingekaa kwenye enoe jingine, majuto yake na kutaka kuhama katika eneo hilo yalichelewa kwani alimshuhudi yule mlinzi akifika pale kwenye majani akitazama pande zote kisha akayarudisha macho yake kwenye majani yale ambapo alikuwa amejificha Norbert. Mlinzi yule alizima tochi kisha akafungua mkanda wa suruali ya suruali yake na ndiyo hapo Norbert alijuta kwanini alichuchumaa kwenye majani mengi kama hayo, kimiminika kilianza taratibu kunyeshea majani hayo na kumlowanisha Norbert begani kwake ambapo alitulia tu ingawa ilikuwa ni zaidi ya maudhi kufanyiwa vile. Aligeuzwa choo na yule mlinzi ambaye alikuja hapo baada ya kumfungulia geti Kamishna Wilfred  kutokana na kubanwa haja ndogo kwa ghafla akaona tabu kukimbia kuelekea chooni wakati sehemu yenye faragh ipo karibu, Norbert alivumilia maudhi hayo  hadi yalipoisha na mlinzi yule ambapo aliondoka eneo hilo kwa kasi kurudi getini ambapo palikuwa ni mbali kidogo.
    Kitendo cha mlinzi kupotea katika  eneo hilo hakuwa na muda wakusubiri tena alirudi hadi pale ukutani akapanda kwa kutumia vifaa alivyopandia kwa haraka sana akatoka nje ya uzio wa nyumba hiyo  pasipo kujulikana na mtu yeyote. Harufu ya haja ndogo mbichi ndiyo ilikuwa ikitoka kwenye bega lake la kushoto lakini hakuwa na jinsi aliendelea kuivumilia kwani hakuna jinsi, shati ake lote kuanzia begani hadi kifuani lilikuwa limelowana haja ndogo ya yule mlinzi ambayo ilikuwa inatoa harufu ya pombe. Norbert alijikaza akaivumilia harufu hiyo na alitembea hadi pale Bar alipoliacha gari lake, alipofika alitoa ufunguo wake na moja kwa moja aliingia ndani ya gari lake. Kitendo cha kwanza baada ya kuingia ndani ya gari yake hiyo ilkuwa ni kuvua shati lake hilo lililogeuzwa choo na kuvaa koti la suti pekee, aliwasha gari yake akaingia barabrani na kuondoka eneo hilo ambapo mitaa kadhaa baada ya kuingia barabarani aliegesha gari pembeni.  Alilichukua shati lake na akatoa silaha zote zilifungwa kwenye shati hilo kisha akalitupa nje na akaendelea na safari yake akiwa tayari ameshapata vitu muhimu ingawa kwa mara ya kwanza alijikuta akigeuzwa choo na mwanaume mwenzake.

****

    Wakati kabla hata Norbert hajatoka juu ya paa la nyumba ya Wilson na kuzunguka kisha na kupetelea kwenye miti mirefu iliyokuwa imepandwa kama pori, Kamishna Wilfred alikuwa na  ari kubwa ya kuhakikisha anampa kesi Norbert itakayomfanya aishi kama digidigi. Akiwa ndani ya gari baada ya  kuagana na wenzake aliendesha kwa kasi kwa lengo la kumuwahi mkewe na  pia kuweza kufanikisha mpango wake huo aliokuwa ameupanga vizuri. Baada ya kutoka nje ya ngome ya Wilson na kuigia barabarani aliendesha gari kwa kasi sana awahi nyumbani kwake, gia za gari lake hilo alibadilisha na kuweka nyingine awahi kufika Kawe alipokuwa akiishi. Baada ya kuimaliza Msasani Kamishna Wilfred alijikuta akiishiwa tumaini la kuishi kwani alipokea ugeni mwingine tofauti ambao ulikuwa bado haujajitambulisha kuwa umewasili tayari eneo hilo. Ugeni ulikuja kumjulisha kuwa tayari ulikuwa eneo hilo baada ya kuhisi kitu cha baridi kikimgusa nyuma ya shingo yake bila ya kutarajia. Kamishna Wilfred alikuwa hajatambua kitu hicho kilikuwa nini na alipeleka mkono kukigusa lakini kitu hicho kilimkandamiza haswa, alijikuta akiongeza mwendo na kisha kufunga breki kwa ghafla baada ya kutambua kuwa alikuwa amewekewa bastola kisogoni mwake.  Gari yake ilisimama kwwa nguvu sana lakini yule aliyekuwa amemshikilia hiyo bastola hakutetereka hata kidogo, bastola hiyo iliendelea kutulia palepale kisogoni mwake vilevile.
                 "Nimefunga mkanda kamishna unafikiri nitaaanguka kwa hiyo breki na bastola inidondoke" Alisikia sauti isiyokuwa ngeni ikimuambia





*JASUSI YAHITAJI MOYO HADI KUGEUZWA CHOO
*MPANGO WA KUMNASA NORBERT UNASUKIKA LAKINI MTEKELZAJI YUPO MATATANI, JE ATAPONA?
*JESHI LA ARDHI NA ANGA NDANI YA IKUU CHINI YA MARI YA M.J BELINDA, JE NINI KITAFUATIA

KUYAPATA MAJIBU YA HAYO MASWALI USIKOSE KUFUATILI SEHEMU ZINAZOENDELEA ZA RIWAYA HII  YA KUSISIMUA





No comments:

Post a Comment