Thursday, November 24, 2016

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA KUMI NA MOJA




RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA



______________+18__________________



        SEHEMU YA KUMI NA MOJA!!

     Mguso wa kiganja chake kwenye paja ulisababisha  Josephine ageuke kukitazama kiganja cha Norbert kisha akainua macho juu kumtazama Norbert, macho ya Josephinee yalikutana na macho ya Norbert ambayo yalikuwa ysmeshazungumza kitu ingawa kwake ilikuwa ngumu sana kukiri kuwa ameelewa lugha ya macho ya Norbert kutokana na kutotaka kuonekana mrahisi.

    Lugha ya macho ya Norbert ilipozidi kumsihi atoe maana Josephine aligeuka pembeni kutokana na aibu, alirudisha macho chini aliutazama mkono wa Norbert uliokuwa pajani kisha akashusha pumzi akamuangalia Norbert usoni akajiandaa kutamka neno.


****


              "Norbert" Josephine alifungua kinywa chake akiwa anashindwa kuyatuliza macho katika uso wa Norbert, aliita jina la Norbert kisha akashindwa kustahimili kutazamana na macho ya huyo anayemuita.

    Norbert naye alinyanyua nyusi moja akiashiria yupo tayari kusikiliza huo wito wa Josephine, kimya kilipozidi na hakuambiwa chochote juu ya wito alianza kuvitanua vidole vyake na kuvibana juu ya paja la Josephine akasababisha mwenye kiungo hiko amuangalie tena usoni akiwa na macho malegevu kuliko ilivyokuwa hapo awali.

                 "Norbert" Josphine alitamka tena huku akizidi kulegeza macho huku pumzi akiachia kwa nguvu, wito wake wa mara ya pili ulibidi uitikiwe kwa sauti na Norbert badala ya kuinua nyusi kama alivyofanya awali huku kiganja chake kikiendelea kufanya utafiti usio rasmi juu ya paja la Josephine

                 "sema bibie" Norbert aliitika huku akimtazama Josephine usoni ambaye alishindwa kustahimili kutazamwa huko akaangalia pembeni.

                 "aaah hamna" Josephine alikosa cha kusema baada ya kumuita Norbert na pumzi zake zilianza kumuenda kwa nguvu ya mithili ya mtu aliyekimbia umbali mrefu, macho yalizidi kulegea na mkono wa Norbert muda tayari ulianza kusafiri safari isiyo rasmi kwa mwendo wa taratibu  zaidi hata wa mwendo wa msafara wa harusi.

     Kusafiri kwa mkono huo kuleweka vituo viwili katika mwili wa Josephine ambao ulikuwa na ulaini usiokuwa wa kawaida, kituo cha kwanza kabisa kilikuwa ni kwenye kiuno kilichobeba miguu ya mwanadada huyo chenye ulaini usio wa kawaida, mkono huo ulianza kazi ya kutalii hapo kwenye kiuno kwa kufanya kazi mithili ya kukamua jipu. Mkono mwingine wa Norbert uligusa sehemu ya jirani ya redio ya gari ukawasha kiyoyozi kisha ukasogea  jirani na mlango wa dereva ukavuta vitufe viwili vilivyosababisha vioo vya giza vipande juu taratibu sana.

     Josephine hakuwa amelitambua hilo alibaki amefumba macho kwa hisia huku akizidi kupungua nguvu za mwili wake na hatimaye akaegemea upande aliiopo Norbert, alikutana na bega la Norbert ambalo aliliegemea kisha mdomo wake ukagusa shingo ya Mwanaume huyo ukiambatana na muhemo wa pumzi zilizoonesha kutojiweza baada ya kufanyiwa ukorofi na mkono wa kiume.

      Msisimko wa ajabu ulitoka shingoni mwa Norbert akajikuta  akiachia mkono kule kiunoni lakini Josephine alimzuia asiuachie kutokana na  ladha aliyokuwa akiipata baada ya mkono huo kuwepo katika kiuno chake ukifanya utalii. Hakutaka kubishana na Josephine aliuacha mkono huo ufanye kazi yake iliyokuwa awali huku mkono mwingine ukikishika kidevu cha Josephine na kumfanya atazamane uso kwa uso na Norbert huku macho yake yakionekana ni  mtu aliyezidiwa kilevi kisichonyweka mdomoni mwa mwanadamu.

     Alitazamana na Norbert kwa shida sana na hatimaye akawa anataka kutazama pembeni lakini Norbert alimuwahi kwa kudaka papi za midomo yake juu ya midomo ya Josephine kwa muda  kisha akaachia akamtazama, Josephine alijikuta akileta mdomo wake tena baada ya Norbert kuacha kumpiga busu hilo ambalo ni maaarufu sana kutumiwa na wafaransa. Alipokelewa mdomo wake huo na hapo shughuli ya kubadilishana shurubati ya mdomoni ikaanza kwa taratibu  na hatimaye ikakolea hata wakajisahau kama wapo barabarani, mikono ya Norbert muda huo tayari ilikuwa ipo kifuani ikifanya utalii mwingine uliozidi kumletea wazimu usio rasmi katika mwili wa Josephine kusababisha atoe miguno hafifu wakati kinywa chake kikiwa kimekutana na kinywa cha Norbert.

    Habari ya uwepo wao barabarani ilikuwa imeshahaulika kabisa na walijihisi wapo kwenye ulimwengu wao wa peke yao tu, magari tayari yalishaanza  kutembea  lakini wao waliendelea kuzama ndani ya dimbwi lenye kina kirefu lisilo hata na kimiminika chochote  ingawa lilikuwa linamfanya mtu yoyote asiweze kufanya kitu kingine cha kawaida.
 
     Walikuwa wamezama kwenye dimbwi la huba ambalo lilikuwa ni kero kwa wengine  baada ya gari hilo kutosogea. Walikuja kushtuliwa na kugongwa kwa kioo ndipo Norbert akaangalia mbele kwa jicho upande akimuacha Josephine akiwa anaendelea kuburudika na shurubati iliyomo kinywani mwake.

      Macho ya Norbert kwa mbele yalishuhudia magari yakiwa yapo umbali wa mita takribani kumi na ikamlazimu kuweka gia kwani hakuwa amelizima, aliutoa mdomo wake mdomoni mwa Josephine kisha akakata kona ya haraka akageuza gari akawa anaelekea mjini huku mkono wake mmoja ukirudi katika mwili Josephine ambaye alikuwa amejiegemeza begani kwake. Aliuvuka mzunguka wa Clock tower kisha akaendelea mbele akaingia kushoto katika barabara ipitayo katika mtaa wa Aggrey, alienda na barabara hiyo hadi alipofika katika makutano ya mtaa wa Jamhurii na mtaa wa Aggrey.

     Hapo aliegesha gari  jirani na hoteli ya New avon na alishuka kwa harska kisha akaenda kumshusha na Josephine ambaye alishuka kwa uvivu mkubwa na aliposhuka tu alimuegemea  kifuani mwake, mkono wa Norbert mmoja ulimshika Josephine kiunoni na mkono mwingine ulishika funguo ambayo aliminya kitufe cha kufunga milango kwenye gari na kupelekea taa za pembeni za gari ziwake.

     Wote kwa pamoja waliingia hadi mapokezi wakakutana na msichana ambaye hakuwapokea kwa uchangamfu sana na alikuwa akimtazama Norbert kwa jicho baya sana, Norbert alichukua chumba hotelini hapo kisha akapanda  ghorofani na Josphine kilipo chumba alichochukua ambacho kipo ghorofa ya pili ya hoteli hiyo.


****


    Upande mwingine Moses alikuwa yupo katika nyumba ya shirika la EASA yenye kutumika kama makazi maalum kwa wapelelezi wa EASA(East Africa Security Agency), alikuwa yumo ndani ya chumba cha chini ya ardhi cha nyumba hiyo ambacho hutumiwa kwa kazi maalum. Mbele yake kulikuwa kuna viti viwili vya mateso vilivyokuwa vimefungwa watu wenye mavazi maalum ya Special force wa jeshi la polisi, pembeni yake kulikuwa kuna meza iliyofunikwa kitambaa cheupe ikionekana ilikuwa imebeba kitu ambacho hakikutakiwa kuonekana kabisa kwa watu waliofungwa kwenye hivyo viti.

    Moses alikuwa akiwatazama watu wale mmoja baada ya mmoja kisha akawasogelea akiwa na tabasamu pana usoni mwake, aliwashika kila mmoja shavu kama watoto wa kike na kusababisha atukanwe matusi mazito sana mengine yaliwahusu wazazi wake. Matusi hayo yalimfanya atabasamu kisha akasogeza meza iliyofunikwa mbele yao akaifungua tararibu mithili ya mtu anayefungua meza yenye chakula kulichoandaliwa kwasababu maalum, vifaa mbalimbali vya mateso vilionekana kwenye meza hiyo ambavyo hutumiwa kutesa watuhumiwa wakubwa wakiwa wapo chini ya ulinzi.

               "Matusi yenu kwenu ni kama wimbo uburudisho ambao muda si mrefu utakuwa wa huzuni kwenu" Moses alipngea huku akivaa mipira ya kitabibu iloyopo kwenye meza hiyo kisha akauliza, "ni nani aliyewatuma?".

     Swali lake hilo halikujibiwa na badala yake alitukanwa matusi mazito  sana na wale mateka wake, matusi hayo yakimfanya atabasamu kwa mara nyingine kisha akachukua kifaa kinachofanana na koleo la kukatia nyaya ingawa kilikuwa kina makali zaidi. Alimuendea mmojawapo aliyekuwa jeuri zaidi akabana shati alilolivaa akavuta hadi likachanika kisha amtazama kwa tabasamu, jeuri ya mtu huyo wa Special force ilionekana kwani alirusha mate ambayo yalimpata Moses kwenye nguo zake kisha akaachia matusi mfululizo.

    Moses aliposikia matusi hayo alitabasamu zaidi kisha akachukua lile koleo akaanza kufinya taratibu ngozi ya mtu huyo kuanzia shingoni hadi kifuani akatoa vipande vya ngozi , damu ilianza kumtoka yule akari aliyejifanya jeuri na maumivu yakafuata lakini hakuthubutu kunyanyua mdomo na ndiyo kwanza alizidi kutukana matusi ambayo kwa muda huo yalikuwa ni kama wimbo kwa Moses.

             "muda wako wa kuwa mnyonge umefika sasa ngoja uwe mnyonge" Moses aliongea kisha akaacha kumbana na koleo akarudi kwenye meza yenye vifaa vya mateso akachukua mkebe mpana uliokuwa umefungwa akaja nao hadi mbele ya askari huyo aliyejifanya mjeuri sana.

     Aliufungua mkebe huo na ndani ukaonekana unga mwingi mwekundu sana ambao hakuna kiumbe angethubutu kuweka pua zake karibu na unga huo pasipo kumletea madhara, unga wa pilipili ambao hutumiwa sana na wahindi au kwa wauza maembe ndiyo ulikuwa mbele yake.

     Moses alimuonesha unga huo yule askari kisha akamsogelea askari mwingine wa pembeni akampiga karate ya  kisogoni akazirai kisha akasema, "hupaswi kusikia mwenzako kajibu nini". Alimfuata yule askari wa kwanza aliyemkata shingoni mwake akachukua ule unga akaanza kuumwaga taratibu kwenye vidonda vyake huku akitabasamu, makelele ya maumivu kutoka kwa askari hakuyajali hata kidogo ndiyo kwanza alizidi kutabasamu huku akiendelea kimimina pilipili hiyo kifuani akitokea shingoni.

          "nani aliyekutuma?" Moses aliuliza tena huku akitabasamu akiitazama pilipili iliyobaki ndani ya mkebe, askari alikaa kimya huku akisikiliza maumivu hali iliyomfanya  Moses amuone ni jeuri na akarudi kwenye meza ya mateso akauweka mkebe na koleo la awali akachukua koleo jingine jembamba zaidi akaja nalo hadi osle alipo askari huyo.

           "Huwa siulizi swali mara tatu nitaendelea mpaka ujibu hilo swali nililokuuliza" Moses alisema kisha akalishika koleo alilikuja nalo kwa nguvu halafu akamminya askari sehemu ya  mwisho wa taya hadi akafungua mdomo wake bila kupenda, aliliingiza koleo hilo mdomoni akabana jino moja kisha akaling'oa akamuacha askari huyo akiendelea kuugulia maumivu.

    Moses hakusitisha zoezi lake aliendelea kumng'oa meno  mengne hadi ya mbele yakaisha kabisa lakini askari huyo hakufungua mdomo wake kuongea chochote na ndiyo kwanza jeuri ilizidi akajaribu kumtemea mate yenye damu Moses. Kitendo kikimfanya Mosea ang'oe hadi meno yaliyofuata na yakabaki magego tu kwa yule askari na bado alijifanya kichwa ngumu hakutaka kunyanyua mdomo wake kuongea chochote.

           "Sasa nimeharibu showroom  yote ya mdomoni tuone atakupenda bibie gani na uwazi huo kama ukuta uliovunjwa" Moses aliongea kisha akarudi kwenye meza yenye vifaa vya mateso akachukua mkebe wenye  unga wa pilipili, alirudi akamsogelea yule askari akamfungua mdomo kinguvu na akauinamusha mkebe huo ili kumlisha unga huo mdomoni.

    Askari huyo alionesha uso wa huruma akawa anatikisa kichwa kukataa asilishwe unga huo ambao ungeenda kwenye vidonda vyake, Moses alisitisha zoezi lake kisha akamtazama akasema "una dakika mbili za kuongea au  niendelee na kazi nyingine".
Askari huyo mapigo ya moyo hadi muda huo yalikuwa juu kwa kuhofia pilipili ambayo angelishwa kinywani mwake na Moses, ujanja tayari ulikuwa umeishia kwenye mfuko wa nyuma wa suruali yake na hakuwa na ubavu tena wa kuleta jeuri kwa kuhofia kulishwa pilipili ilihali ana vidonda mdomoni mwake vya kung'olewa meno bila ganzi. Alifunguka kwa kila kitu juu ya aliyemtuma hadi akamaliza jinsi mpango mzima ulivyokuwa, maneno hayo yalimfanya Moses ashushe pumzi kwani huo mpango huo na yeye ulikuwa unamuhusu.

                "Kwahiyo wote tulioendesha Operesheni fagio la chuma kifo ilikuwa ni haki yetu?" Moses alimuuliza yule askari.

               "Ndiyo tulivyoambiwa na jukumu tulilopewa, tuliwekwa makundi tofauti ya kuweza kuwaua nyote mliosababisha binamu wa Kaminshna auawe. Wengine walitumwa nyumbani kwako na wengine nyumbani kwa M.J Belinda kwenda kuwaua na wengine tulitumwa kuja kumuokoa Lion mikononi mwa Norbert" Askari yule aliongea huku akivumilia maumivu yaliyopo mdomoni mwake.

                "je kiini cha mpango huo ni nini ukiacha hiyo ya kutuangamiza sisi?" Alimuuliza huku akimtazama kwa umakini sana.

                "Sijui kiini ni nini sisi Kamishna alitupa kazi tu na alituambia iwe ya siri kama kikosi chetu kilivyokuwa cha siri, hatuhoji kingine kwani hatukuwa ns haki ya kupinga amri  za mkubwa wetu" Askari huyo alijibu kisha akamtazama Moses kwa huruma sana.

                 "Ngoja huyo mwenzako aamke aongee tofauti na wewe nitabandika ile pasi ya mateso iliyopo pale mezani kwenye korodani zako" Mosea alisema  huku akimuonesha yule askari ilipo pasi ya umeme kwenye meza ya mateso, yule askari alimuangalia kwa huruma lakini haikumfanya abadili uamuzi wake.

       Moses alichukua simu yake akabonyeza baadhi  ya vitufe vilivyopo kwenye simu yake akaipata namba ya Norbert akampigia, simu iliita kisha ikakatwa kisha  ukaingia ujumbe mfupi wa maneno kwa Norbert.

      Gawaza alipofungua ujumbe huo na kuusoma alijikuta akicheka kisha akasema, "jamaa huyu umalaya utammaliza kwa kweli", alitoka humo kwenye chumba cha mateka akafunga mlango akazima taa akaondoka.


****


     Muda ambao Moses anampigia simu Norbert tayari alikuwa ameshafika kwenye mlango  wa chumba cha hoteli alicholipia, ilipoita simu alitumia mkono mmoja kuitoa kukata kisha akaandika ujumbe mfupi  huku mkono mwingine ulikuwa upo kiunoni mwa Josephine.

   Aliingia ndani na Josephine  kisha akafunga mlango kwa ufunguo  na hapo ndipo akaanza uchokozi mwingine katika mwili wa Josephine akiwa yupo nyuma yake amemkumbatia, alitumia wasaa huo kwa kukichezea kiuno cha Josephine huku midomo yake ukiwa ipo shingoni ikifanya utalii wa ghafla ambao ulimpa kichaa cha ghafla Josephine hadi akaishiwa nguvu akabaki akikishika kichwa cha Norbert kama aliyetaka kukitoa huku akichezea akichezea kidevu cha Norbert kilichobeba ndevu ndogo zilizokatwa vizuri kwa mtindo wa kupendeza.

          "ooosiii! Norb....ert" Josephine alilalamika huku akizidi kumuegemea Norbert kwa nyuma kutokana na kuishiwa nguvu, utundu wa Norbert katika mwili wake alishindwa hata kusimama akawa anaelekea kudondoka ikambidi Norbert ambebe huku  wakiwa wamekutanisha ndimi zao akaenda kumtupia kitandani huku akiendelea na utundu wake.

     Alikuwa juu ya kifua cha Josephine akifanya utalii usio rasmi katika wa mrembo huyo ambao ulaini na joto lake ulizidi kumtia hamasa aendelee na utalii huku akipunguza stara za mrembo huyo pamoja na stara zake, ndani ya robo saa tangu waingie walikuwa wapo kama walivyoingia duniani na utundu uliendelea baada ya muda mrefu kisha wakaanza kile kilichowafanya wawepo humo ndani katika mazingira hayo.

    Iliwachukua masaa takribani mawili wakawa tayari wamemaliza kile kilichowafanya wawepo humo ndani, wote kwa pamoja walijipumzisha huku wakiwa na tabasamu pana usoni mwao na wakawa wanaongelea kile kilichokuwa kikifanyika muda mfupi uliopita, walipongezana kwa kila mmoja kuonesha ushirikiano kwa  mwenzake huku wakiwa wamekumbatiana kwa upendo wa hali ya juu kama walikuwa wana muda mrefu tangu wajuane.

     Haukupita muda mrefu Josephine alipitiwa na usingizi papo  hapo kitandani akamuacha Norbert akiwa amejilaza pembeni yake akiusanifu mwili wake ambao muda huo haukuwa nakificho chochote kitachozuia usiuone moja kwa moja.

     Norbert alibaki akitabasamu alipouangalia mwili wa Josephine kisha akajikuta amepeleka mkono akashika moja ya mapambo ambayo ukubwa wake ulikuwa umeongezeka kutokana na  Josephine kifudifudi, alipoendelea kuyashika mapambo hayo mhemko mpya ulimuanza na alitamani kumuamsha Josephine lakini alisita baada ya simu yake ya mkononi  kutoa mlio wa kuingia ujumbe mfupi wa maneno na ikamlazimu aichukue simu yake ausome ujunbe huo.

     Ujumbe huo ukimfanya asikitike kisha akamtazama Josephine aliyekuwa amelala akambusu shavuni, alivaa nguo zake akaiacha simu yake kitandani akatoka chumbani humo akaelekea chumba cha tatu kutoka chumba alichopo. Aligonga katika chumba hicho mara mbili kisha akasubiri kidogo, mlango wa chumba hicho ulifunguliwa akaonekana yule msichana aliyekuwa yupo mapokezi akiwa yupo ndani ya mavazi maalum ya kulalia. Sura ya msichana huyo ilipomuona Norbert ilibadilika na kuwa isiyo na furaha hata kidogo, Norbert hakujali hilo suala yeye aliingia ndani kisha msichana huyo akafunga mlango.

              "Nor hivi kipi hukipati kwangu?" Msichana huyo alilalamika akimtazama Norbert kwa sura yenye kuonesha hakuwa amependezwa na tabia yake.

              "Nor nimekupa mwili wangu nimekupa mapenzi yangu lakini bado tu huridhiki hadi umeamua kumleta mwanamke mwingine katika hoteli hii ambayo nafanya kazi na umelipa chumba kwa ajili yetu tukutane...Aaaargh! Nor nifanye nini ujue nakupenda mpenzi wangu" Msichana huyo alizidi kulalamika huku machozi yakianza kumtoka, Norbert alimsogelea kwa taratibu huku akimtazama usoni na alipomfikia karibu akamshika bega.

               "Jamila" Norbert aliita akiwa ameshika bega lake na mkono wa pili akaupeleka shavuni mwa binti huyo.

               "niache huko" Jamila alisema kwa ukali sana kisha akautoa mikono mikono ya Norbert kwa nguvu akaendelea kulalamika, "Norbert kwanini unanifanyia hivi jamani nimechoka nasema nimecho....".

       Jamila alishindwa kuendelea tena kulalamika baada ya Norbert kumuwahi kwa kukutanisha papi za midomo yake kwa nguvu sana na akawa anapata shurubati kwa nguvu, Jamila alileta upinzani kutokana na kutotarajia jambo hilo lakini upinzani wake ulizidiwa na nguvu alizonazo Norbert katika kumdhibiti asifurukute.

       Haukupita muda mrefu sana tangu midomo yake ikitutane na midomo ya Norbert kwa ghafla tayari alikuwa amelegea na akashindwa kutoa upinzani na badala yake akatoa ushirikiano kwa Norbert, aliendelea kufanya  hivyo huku akimpapasa Norbert kufuani mwake na akiwa amekolewa kabisa na kitendo alichokuwa akikifanya Norbert.

       Maruhani yake ya kike yaliyokuwa yamelala tayari yalikuwa yameshaamka kutokana na zoezi hilo, Norbert alipotoa mdomo kinywani Jamila aliuleta mdomo wake karibu akionesha kuhitaji kuendelea na zoezi hilo. Norbert aliamua kuendelea na zoezi hilo ambalo analijua kuwa ni udhaifu mkubwa sana kwa Jamila kwani huamsha vilivyo lala, haikupita muda mrefu tayari Jamila alikuwa hajiwezi kabisa  hata macho yakawa yanafunguka  kwa tabu sana huku mihemo ikawa inamtoka akionesha kazidiwa.

        Norbert alitumia wasaa huo kumpeleka kitandani huku akiendelea na uchokozi, Jamila alionekana kuzidiwa zaidi hadi akafungua shati la Norbert akalivua halafu akadaka vishikizo vya suruali vilivyopo juu ya zipu akiwa na papara sana.

               "dah! Hawa wanawake wataniua kama natumia mafuta vile" Norbert alisemea moyoni  huku akidaka mikono ya Jamila isifungue vishikizo vya suruali kwa kuhofia kuzua mapya, alikuwa katoka kutimiza hitaji la Josephine   hivyo angefungua suruali angejua kila kitu kwani hakuwa amejisafisha kabla ya kuja humo ndani.

                "Nor please usinitese", Jamila alilalamika huku akikazanania kufungua suruali ya Norbert.

               "subiri kwanza mpenzi mimi ni wako tu usiwe na papara" Norbert alimuambia Jamila huku akiitoa mikono yake akaendelea kufanya utundu wake huku akipunguza vizuizi vinavyofanya mwili wa Jamila usionekane vizuri kwake, baada ya muda mfupi tayari na yeye alikuwa amepunguza vizuizi katika mwili wake akawa hana tofauti na Jamila. Waliianza safari nyingine iliyowachukua saa kadhaa wakawa wameshamaliza wakiwa wamechoka hasa Norbert ndiyo alichoka zaidi kwani alikuwa ameangusha magogo mawili bila kupumzika.

                "Asante Nor" Jamila huku akihema kwa nguvu sana.

                "huna haja ya kushukuru ni haki yako hii" Norbert alimuambia huku akivaa nguo zake kwa haraka kwani hadi muda huo tayari giza lilishaumeza mwangaza wa jioni.

               "Nor unaenda wapi sasa au kwa huyo kimada wako?" Jamila aliuliza huku akikunja sura kwani hakupendezwa kuondoka na Norbert muda huo.

               "Aaah! Jamila mpenzi wangu mbona wivu hivyo acha nimuwahi yule siyo kimada wangu nipo kazini" Norbert alimulalamika Jamila.

               "Etii upo kazini! Ndiyo mshikane viuno pale receiption? Haya mwandishi wa habari naona ulienda kutafuta habari kitandani na yule mwanamke" Jamila alikuja juu huku akimbania pua na hapohapo Norbert akabadilika uso wake ukawa usio na furaha hata kidogo.

               "Unajua nini? Sasa kulala na wewe kitandani inaonekana umevuka mipaka hadi unafikia hatua ya kunitusi sasa tusijuane" Norbert aliongea kwa hasira akamaliza kuvaa nguo zake akataka kuondoka, Jamila hakuweza kustahimili kuona jambo hilo kutokana na kutekwa sana na Norbert kihisia tangu waanze uhusiano wao usio rasmi. Alikimbilia Norbert akamkumbatia kwa nyuma huku akilia, Norbert alimtoa mikono yake kisha akageuka nyuma kumtazama.

                "Nisamehe mpenzi wangu ilikuwa ni hasira tu" Jamila huku machozi yakianza kumtoka kisha akaendelea kusema,"nakupenda sana Norbert ndiyo maana nakuwa hivi".
Jamila alipomaliza kuongea alibaki akimtazama Norbert ambaye alisimama akimuangalia, alipoona Norbert hajibu kitu aliamua kupiga magoti akiwa hivyohivyo mtupu aombe msamaha huku machozi yakimtoka.

      Norbert alimtazama Jamila kisha akashusha  pumzi akamuinua pale chini alipopiga magoti akamkumbatia. Aliamua kumfuta machozi akamuambia, "kilio chako ni zaidi ya msiba kwangu hivyo sipendi kukiona mpenzi wangu, kosa lako wewe kwangu msamaha hutoka haraka sana  hata kabla hujalikiri mbele yangu. Nakupenda sana mpenzi wangu".
     
       Jamila aliposikia maneno hayo amani ya moyo ikarudi na alitabasamu akambusu Norbert mdomoni, Norbert alitabasamu alipopewa busu hilo kisha akampiga kibao cha kalio Jamila cha uchokozi kilichosababisha Jamila ashtuke halafu amtazame Norbert.

                  "Afuuu Nor unaanza sasa wakati mwenzako nimechoka sana kazi yako siyo ndogo" Jamila aliongea kisha akambusu Norbert kwa mara ya mwisho akamuambia,

                  "haya mpenzi wahi".

       Norbert hakuchelewa alitoka upesi chumbani humo akimuacha Jamila ndani na alirudi katika chumba ambacho alikuwepo Josephine amelala, alipoingia ndani hakumkuta Josphine zaidi ya kusikia maji yakiwa yanamwagika bafuni na kitandani aliikuta simu kama alivyoiacha. Norbert aliichukua simu yake akawasha kioo ili aingize namba zake za siri atoe loki, alipoingiza namba za siri kwenye simu yake picha ya Josephine ikaja kwenye kioo kwa ghafla ikitoa tangazo na mfano kwenye mfumo wa simu juuvya kuchezewa simu yake.

                 "intruder selfie" Norbert aliongea huku akiitazama picha ya Josephine ambayo ilipigwa moja kwa moja na siku bila Josephine kujua.





TUKUTANE IJUMAA PANAPO UHAI NA AFYA NJEMA




HAIRUHUSIWI KUNAKILI RIWAYA HII KWA NAMNA YOYOTE PASIPO RIDHAA
YA MTUNZI






No comments:

Post a Comment