Thursday, December 29, 2016

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE







RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________


SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE!!
.
       "What! Kamudu msaliti ni wewe!" Rais Zuber aliongea kwa mshangao alkini alijikutra akinyoosha mikono juu haraka baada ya Kamudu kumuelekezea bastola yake aina ya revolver yenye uwezo mkubwa sana, watu wote waliomo humo ndani nao walitoa silaha zao wakamuelekezea Kamudu. Kamudu aliishikilia bastola hiyo kisha akamtazama kila mmoja aliyekuwa amemuolekezea bastola, alimeza funda moja la mate kisha akakaza mikono yake barabara na kidole kkwa kimeshika kifyatulio.

          "Fanyeni ujinga na mimi nifanye upumbavu!" Kamudu aliongea kwa hasira huku midomo yake ikimcheza.

_________________
_______________________TIRIRIKA NAYO
_________________


              "Ohoo hamjanielewa siyo, shusheni silaha zenu na mtoe magazine nje mzimwage risasi zote la si hivyo  napasua kichwa chake huyu"  Kamudu aliongea kwa nguvu hadi mishipa ya kichwa ikawa inamtoka, wanausalama wote hawakuwa na sababu ya kupinga sharti hilo.
   Wote kwa pamoja walishusha silaha chini kisha wakatoa vibeba risasi ambavyo walivifungua wakamwaga risasi zote mezani hapo na bastola wakaziacha mezani hapo.
             "rudini nyuma hatua tano kila mmoja kutoka hapo kwenye meza" Kamudu alitoa amri nyingine, wanausalama hao wakafanya kama walivyoambiwa na lakini Moses hakunyanyua mguu wake kurudi nyuma aliendelea kusimama palepale alipokuwepo awali.
            "Professa ndiyo husikii siyo" Kamudu alimfokea Moses huku akikaza kidole chake katika sehemu ya kufyatulia risasi, hilo halikumtisha Moses hata kidogo yeye ndiyo kwanza alitabasamu kama alikuwa hajaelewa kile alichoambiwa na aliketi kwenye kiti.
   Hali hiyo ilimshangaza kila mmoja hata rais mwenyewe ambaye uhai wake uikuwa ukihitajka kwa gharama yoyote ile, wote walibaki wakimtazama kwa mshangao kwani ilikuwa ni kinyume cha kazi yake ya kuhakikisha mheshimiwa hadhuriki akiwa yupo karibu naye. Kupinga jambo hilo haikutarajiwa hata na Rais Zuber mwenyewe ambaye alichoka kabisa akaona Moses alikuwa hamtakii mema, alishajikatia tamaa ya kutoka hai ikiwa Moses alikuwa akipinga amri hyio. Alibaki akiikodolea macho bunduki aina ya revolver kubwa ambayo Kamudu alikuwa ameishika akiona siku zake za kupumua zilikuwa zikihesabika kutokana na ukaidi wa Moses, alifumba macho yake mwenyewe huku akisubiri muujiza utokee wa kupona ama apigwe risasi ya kichwa.
                 "Moses fanya kama anavyokuambia tafadhali" Rais Zuber alimuambia Moses akiwa amefumba macho, Moses alitabasamu tu na hakutii jambo alilokuwa ameambiwa na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya uliznzi na usalama.
                  "Mheshimiwa muache apasue tu kichwa chako kama ana uwezo wa kufanya hivyo lakini humu hatoki" Moses aliongea huku akiegemea mgongo wa kiti mikono akiwa amefumbata kifuani mwake.
                  "Professa  unasema nini wewe" Kamudu aliuliza kwa mshangao sana baada ya kusikia maneno hayo ambayo hakuyatarajia kuyasikia.
             "Mpige risasi sasa unasubiri nini ila sifanyi kama uanvyoniambia" Moses aliongea, Kamudu aliposikia maneno aliona liwalo na liwe.

     Aliamua kuminya kifaytulio cha risasi akitarajia mlipuko wa bastola ndiyo utasikika lakini aliambulia kusikia mlio wa vyuma  vya ndani ya bastola tu, alishtuka haswa baada ya kusikia hivyo na aliamua kuminya tena kifyatulio hicho cha bastola lakini mlio ulikuwa ule risasi haikuwa na kitu. Hapo Moses ndiyo alicheka zaidi huku akimtazama Kamudu kwa dharau kuu, Kamudu alijikuta akiishiwa mbinu na akaona njia nzuri ilikuwa ni kumrukia Rais Zuber na kumkaba ndiyo angeweza kusalimika na balaa hilo.

    Wakati akiifikiria mbinu hiyo tayari Rais Zuber alishatoka mbio mahali alipokuwa amesimama akazunguka meza hiyo kwa upande mwingine akakimbilia eneo alilokuwa yupo Moses,  mpango wa Kamudu ulifeli papo hapo kutekelezeka kwani wanausalama wenzake waliruka kwa haraka kutoka eneo walilokuwepo wakamdaka na kumbana mikono wakamlaza  chini kwa nguvu. Walimbana mikono kwa nguvu hadi akawa amefumba macho kwa maumivu, muda huo ndiyo Moses alinyanyuka kwenye kiti alichokuwa amekaa akatumbukiza mkono wake kwenye mfuko wa kombati lake la kijeshi.
    Alitoa risasi  kumi na mbili akazimwaga mezani kisha akatabasamu, alisogea pembeni ya meza kwenye kiti hiyo kisha kajongea hadi eneo ambalo Kamudu alikuwa ameshikiliwa barabara na vijana wake waaminifu. Moses alipomfikia alichuchumaa mita kadhaa kutoka pale alipolazwa chini kifudifudi kisha akatabasamu kama kawaida yake, alimtazama mwanausalama yule msaliti kwa jinsi alivyokuwa ameuma meno kwa maumivu baada ya kubanwa mikono kwa mbinu hatari ya judo.
                 "Kamudu kosa kubwa ulilolifanya ni kweka bastola yako mguuni, ukarudia tena kosa kwa kuweka kinasa sauti chako sambamba na mkanda wa suruali wako.
    
   Ukafanya kosa jingine kukaa hapa kwenye kwenye meza suruali yake ikapanda juu bastola nikaiona, ukafanya tena kwa kwa kukitoa kinasa sauti na kukitupa chini kijanja zaidi uliposikia mheshimiwa akiulizia mwenye kinasa sauti. Hapo nilikujua wewe ni msaliti njkaitoa risasi hiyo bastola yako bila ya wewe kujua halafu nikakizima hicho kinasa sauti" Moses alimuambia jinsi alivyofanya mpango wote ambao ulidhoovisha mbinu yake ya kutaka kutoroka, maneno hayo yalimfanya Rais Zuber atoe tabasamu usoni mwake baada ya kuona alikuwa na vijana makini sana waliokuwa wakihakikisha usalama wake unakuwa sawa kwa usiku na mchana.
              "Nakuambia Moses mshachelewa nyinyi alhamisi leo jua kesho kutwa jumamosi  jeshi lililopo hapo nje linaingia humu ndani kumtoa huyo unayemlinda" Kamudu aliongea kwa hasira.
               "Labda niwe mfu Kamudu, jeshi la nchi na anga lipo upande wetu tuone hao wa majini watavamia kwa nguvu ya namna gani ikiwa majeshi yote ya  anga na nchi kavu bado yapo chini ya  Amiri jeshi na Meja jenerali Belinda" Moses aliongea akimsikitikia Kamudu.
               "Na bado tu huyo atatoka humu aingie mzee Philbert Ole siku ya jumamosi" Kamudu  aliongea kijeuri zaidi.
               "Ohoo ndiyo mliomtorosha siyo sasa tunaanza na wewe utakuwa mfano, mpelekeni chini huyo" Moses alitoa  amri na Kamudu alinyanyuliwa kwa nguvu akatolewa humo ndani na wanausalama wakabaki ADC na Rais Zuber pekee tu. Moses alipokamilisha amri hiyo alikakamaa mbele ya Rais Zuber kiheshima.
                 "Well done my boy, nafurahi kuwa na mtu kama wewe" Raiis Zuber alimpongeza Moses ambaye alitoa tabasamu tu. 

****

    Subira huvuta heri lakini ikizidi muda mwingine heri kusubiri hutakuwa tayari, ngoja ngoja siku zote huumiza matumbo ingawa harakahraka haina baraka. Ndivyo ilikuwa kwa kwa kundi la Mzee Ole tangu walipotoka Santos na Benson kwenda kumsaka Norbert hawakuwa wamerudi hadi muda huo, waliweka subira ii wavute na lakini heri hiyo waliyokuwa wakiisubiri  ilikuwa mbali. Wakangoja vitoke vizuri kwa kuwatuma hao lakini kungoja huko kuliwachosha kabisa, hawakufanya haraka katika kungoja huko lakini muda unavyo zidi ndipo walipozidi kuwa na harak zaidi  ya jambo walilokuwa wakilingojea litimie. Muda nao ulikuwa haugandi ulizidi kuyoyoma pasipo Benson naSantos kutokea eneo hilo, walisubiri wakachoka na hatimaye wakavunja amri ya kutowapigia simu wapigiwe wao kazi ikiwa kamli.
   Walipopiga simu zao zilikuwa zikiita sana pasipo kupokelewa jambo lililozidi kuwatia hofu wote wawili, kutopokelewa kwa simu hizo kulisababisha Thomas  na Wilson waitwe na waambiwe juu ya hali hiyo iliyojitokeaza ghafla ambayo wao walikuwa hawaielewi. Hawakujijua kwamba walikuwa wamesalia watu watu watano na wawili tayari walikuwa wameshamalizwa na Norbert, kwa haraka zaidi wao waliagizwa kwenda kuwafuatilia wenzao. Thomas na Wilson walikwenda  hukuwakitumia programu ya simu ya kusaka simu za wenzao zilipo.
   Thomas akiwa na Wilson walifuata uelekeo wa simu hizo ambao uliwapeleka moja kwa moja hadi kwenye  uzio wa mabati ambao ulikuwa ukitumiwa kuegeshea magari ya wafanyakazi mbalimbali wa kampuni zilizopo katikati ya mji wakiwa wanaelekea maofisini , hapo alikuta umati mkubwa wa watu ukiwa nje ya uzio huo huku sehemu ya lango la uzio huo kukiwa na utepe pamoja na maaskari waliokuwa wapo kwenye sare. Iliwabidi waegeshe gari mbali na hapo kisha wakaenda kukaa kwenye kibanda cha fundi viatu ambapo walikuwa wamejikusanya watu wakiwa wanjadili, walipokaa kwenye kibanda hicho walijifanya hawajuani kabisa ambapo Wilson alikaa pamoja na kundi hilo la watu na Thomas akaenda kukaa jirani na fundi viatu ambapo watu walimpisha kutokana na rangi yake. Thomas akiwa ni mzungu pekee kwenye kundi hilo alivua viatu vyake kisha akamkabisdhi fundi viatu ambaye alivichangamkia kwa haraka, Wilson alijiingiza kwenye kundi la watu kama mpita njai ambaye alikuwa akitaka kujua kilichotokea eneo.
              "jamani mimi mpita njia kuna nini hapa mbona askari wengi?" Wilson baada ya kufika kwenye hio kundi la watu.
              "Dah kaka nchi hii imeisha ndugu, si watu wawili wameuliwa humo ndani mmoja ni mzungu fulani ana nywele ndefu mwingine black" Kijana mmoja alimuambia Wilson.
               "duh nchi yetu inapoelekea sipo" Wilson alijifanya kushangaa lakini moyoni alikuwa akihisi tayari washapoteza wenzao wawili.
               "Yaani ikulu imezungukwa na wajeda leo hii na mengine yanatokea sijui mzungu wa watu alikuwa kawakosea nini hao wauaji, yaani doh nasikia wamefumua kichwa na mwenzake black kaharibiwa miguu kabla hajauliwa" Mwingine alidakia akijifanya kuijua zaidi habari hiyo kwa kutumia maneno ya kuambiwa.
                "Ndugu zanguni sina amani ya kukaa eneo hili tayari mshanitisha" Wilson aliongea huku akijifanya kaogopa habari hiyo na aliamua kuondoka eneo hilo mara moja, alielekea moja kwa moja alipokuwa ameegesha gari kisha akaingia ndani ya agari akatoa simu yake akabonyeza baadhi ya namba akaiweka sikioni.
                  "Haloo kamishna nafikiri unayo ripoti ya watu wawili waliouawa leo hii.... sasa tulikuwa tunataka utuhakikiashie je hao ni Santos na Benson......sawa nasubiri" Wilson aliongea baada ya simu hiyo kupekelewa na Kamishna  Wilfred kisha akakata alipoambiwa asuburi, alikaa ndani ya gari kwa muda mfupi tu Thomas naye akarejea akiwa amegwaya kwa taarifa aliyokuwa ameisikia juu ya mauaji yale.

    Ingawa hawakuwa na uhakika nayo tayari mioyo yao ilishaanza kuingiwa na wasiwasi waliposikia wasifu wa watu hao waliouawa, waliamua kuwasha gari na kuondoka eneo hilo baada ya simu walizokuwa wakizifuatilia kuwa zipo katika eneo lenye polisi wengi sana. Walitumia njia ya mkato ambayo ilienda kuwapeleleka mahali ilipo barabara ya Bibi Titi Mohamed mita kadhaa kutoka Vilipo vyuo vya CBE na TPSC, hapo waliingia upande wa kulia wa barabara hiyo kulekea ilipo mahakama ya Hakimu mkazi KIsutu. Walienda kwa mwendo wa kasi sana kutokana na barabara hiyo kuwa tupu ambapo iliwachukua dakika tayari wakawa wameivuka mahakama ya Kisutu na sasa walikuwa wapo kwenye makutano ta barabara ya Bibi Titi, barabara ya Ally Hassan Mwinyi na barabara inayopita kwenye mtaa wa Ohio jirani kabisa na hoteli ya Serena. Wakiwa eneo hilo simu ya Wilson iliita kwa kutetemeka mfukoni mwake na ikambidi aipokeee kwani yeye hakuwa dereva wa gari hilo, Wilson kwa haraka aliipokea simu hiyo huku akimua cha Thomas akitenda haki kwenye usukani wa gari hilo.
                  "Ndiyo Kamishna......ndiyo nakusikiliza......unasema! Oh! Shit! Tukutane baadaye Msasani tuweze kujua jinsi ya kujipanga tena upaya yasiwe mabaya... Ok in the evening" Wilson alikata simu kisha akaweka mikono mashavuni mwake kwa taarifa aliyokuwa ameisikia kutoka kwa Kamishna, alimuangalia Thomas ambaye alikuwa akimtazama kwa jicho la kuibia ili asiweze kupoteze umakini akiwa barabarani kwani tayari mataa ya eneo hilo yalikuwa yamesharuhusu.
                  "Leta ripoti Nourther" Thomas alimuambia Wilson huku akibadilisha gia kutokan na  gari hiyo kutokuwa na mfumo wa gia wa moja kwa moja.
                   "Benson na Santos hatupo nao tayari, ndiyo hao waliouawa eneo lile" Wilson aliongea kwa sauti ya kinyonge sana kutokana na taarifa hiyo aliyoipata.
                   "Ooooh! Man! Norbert anatumaliza tu, nakwambia nikimtia mikononi mwangu namkata vipange vipande" Thomas aloongea kwa hasira huku akipiga  mikono yake kwa nguvu sehemu ya pembeni ya usukani wa gari hilo, hakutetereka kwa taarifa kiasi cha kushindwa kuliongoza gari vibaya ingawa taarifa hiyo ilikuwa ni pigo kubwa kwake kwa kuwapoteza watu muhiomu kama hao  kwenye kundi lao.
 
   Hatari ya N001 hakika alianza kuiona ni kubwa kuliko anavyofikiria na  wakiwa wamemuacha akiendelea kufanya anavyotaka basi ingekuwa hatari kwao zaidi, sasa aliona suala la kutumia akili zaidi kuliko nguvu katika kazi hiyo ndiyo lilikuwa likihtajka zaidi. Aliamini kama wakitumia akili basi N001 anaweza kuwa mikononi mwao kwa mara nyingine na na asiweze kuwatoroka tena, Thomas hakujua kama alikuwa ni mtu aliyekuwa anapigwa na baridi usiku na anakuja kukumbuka kuwa alikuwa ana shuka tayari mapambazuko yalikuwa yameshawadia. Jambo hilo katika kulifikiria kulitenda tayari walikuwa wameshachelewa kabisa katika kuendeleza mapambano na Norbert.

****

    Baada ya kutoka kuongeza pengo jingine kwa kundi la L.J Ibrahim Norbert aliongoza gari lake hadi nyumbani kwa Norene ambapo aliliingiza ndani moja kwa moja hadi katika eneo la maegesho, alishuka akiwa hatamaniki kutazamwa na mtu msafi ingawa alikuwa bado anatamanika kupendwa na mwanamke aliyekuwa anampenda. Aliingia  moja kwa moja hadi ndani ambapo alipitiliza hadi chumbani, alitumia dakika kadhaa huko chumbani kwenye bafu la ndani kujisafisha kisha akatoka akiwa amevaa suti zingine akiwa hana tai safari hii. Alitoka hadi sebuleni halafu akapitia jikoni  ambapo alimkuta Norene akiwa anapika. Hapo Norbert alimkumbatia kwa nyuma Norene kisha akambusu shingoni mwake, aliendela kumfanyia uchokozi mwingine katika mwili wake kama ilivyo kawaida yake wakiwa pamoja.
                 "Nor shida yako niunguze tu naona, kwanza niambie mbona mapema huvyo na umebadili nguo ghafla au ushapita sehemu zako nini?" Norene aliongea huku akiendela kupika
                 "Swali la kurudi mapema inabidi nikuuulize hata wewe pia kwanini umerudi mapema, sehemu yangu ya kupitia ni hii tu ipi nyingine?" Norbert aliongea huku akiwa bado amemkumbatia Norene kwa nyuma.
                 "Mh1 Haya  mshindi wewe bwana, nimerudi mapema baada ya kupewa ujumbe wako na CE na si vinginevyo. Nimemkufuata kule ofisi yako mpya nimekukosa ndiyo maana nikaamua nipite nyumbani moja kwa moja" Norene aliongea
                  "haya niambie kibabu huyo ana jipya gani au ndiyo uzeeee umeanza kumpeleka vibaya" Norbert aliongea
                   "nafikiri hali iliyochafuka Magogoni umeiona ndiyo hiyo umeitiwa, yaani nimepiga simu yako mpaka nimechoka we umeizima" Norene aliongea
                   "Yaani acha tu huko nimetibua hali ya hewa ndiyo maana nimeizima kabisa nifanye kazi kwa ufanisi zaidi, also kuhusu hiyo ishu nipo pamoja na Belinda na Gawaza kabla hata hajaniambia naona itakamilika haraka iwezekanavyo" Norbeet aliongea
                  "Sawa mume wangu ila ujichunge tu  ukumbuke mimi na mwanao bado tunakuhitaji na hiyo kazi ni ya hatari sana" Norene alipoongea maneno hayo alikuwa na sura ya unyonge sana.
                  "worry out malikia wangu kama niliweza kuifanya kazi ya hatari ugenini nikaimaliza nitashindwaje kufanya hii nyumbani" Norbet alimtoa wasiwasi Norene huku akikaa kwenye meza nyembamba ambayo huwa inawekewa  vyombo na majiko wakati wa kupika.
                 "Ok unatoka kwanza au unasubiri msosi?" Norene aliuliza
                   "Ooooh! Kitamu kinapika vitamu nitatokaje wakati sijala vitamu vilivyoandaliwa na kitamu, sinyanyui mguu hapa mpaka nile vitamu"
                 "Mhh! We nawe kwa maneno sikuwezi kabisa"
                    "uandishi wa habari upo kwenye damu,  kuwa na maneno ni sawa na gari la taka kuwa na harufu"
                   "aha! Ha! Ha!  Ha! Ha! Ha! Mwanaume wewe sikuwezi"
                     "unaniweza sana ndiyo maana uliniweka sawa bila kuchezesha msuli wowote" Norbert alipoongea maneno hayo Norene alinyanyua mwiko kwa haraka akamtisha Norbert kumpiga nao, Norbert aliinuka kwenye meza hiyo akasogea kando upesi huku akicheka.
                     "Nyoo lione jogoo pori mkubwa  wee ndiyo unayowaza hayo tu jianaume wewe"
                   "sasa ulitaka niwaze yapi wakati hadi leo yananitia uchizi na ukiyazisha nitaanza kuokota makopo" Norbert alipoongea maneno hayo Norene alishindwa hata kugeuza uso wake kumtazam na aibu ya ghafla ilimuingia akabaki akitazama sufuria ambayo ilikuwa na maakuli yakiwa ynachemka huku mwiko ulioushika ukifanya kazi ya kugeuza maakuli hayo.

   Kimya kifupi kilitanda hapo jikoni wakati Norene akiwa ndiyo anamalizia kupika chakula hicho cha mchana, Norbert asliutumia muda huo kufungua simu yake ambayo alikuwa hajaigusa kutokana na kuwa ndani ya kazi ambayo haikumstahiki kuigusa simu hiyo. Baada ya muda mapishi yalikuwa tayari na na yalipelekwa kwenye meza ya chakula yakiiwa kwenye vyombo maalum, Norbert na Norene walipakua kila mtu sahani yake na walianza kula huku wakiwa wanatazaman tu kama ndiyo walikuwa wanaonana kwa mara ya kwanza. Kilikuwa ni chakula ambacho wote kwa pamoja walikifurahia kutokana na furaha waliyokuwa nayo katika uhusiano wao, walikula kwa taratibu sana kama walikuwa akitamani kisiishe kwa haraka kutokana na ladha iliyokuwepo ndani ya chakula hicho.
              "Ama kweli Mungu amenipa bahati mja wake" Norbert aliongea huku akipeleka kjiko cha chakula hicho mdomoni, kauli hiyo alipoitoa iliambatana na tabasamu pana katika uso wake ambalo lilimfanya Norene amtazame kwa macho malegevu kabisa.
               "Kanijalia mrembo mwenye kila sababu ya kuitwa mke bora kwangu na mama bora kwa mtoto wangu" Norbert aliongea maneno ambayo yalimfanya Norene atabasamu.
               "Halafu Nor tutaendelea kuwa hivi mpaka lini unajua mama kanipigia simu anauliza kuhusu ndoa" Norene aliongea kwa kulalamika.
                "Kila kitu mipango tu mama Jerry ngoja kibarua kiishe halafu tutaongea vizuri" Norbert aliongea muda huo tayari alikuwa ameshamaliza kula, alinyanyuka kwenye kiti chake akaenda mahali lilipo eneo maalum la kunawia mikono akanawa kisha akarudi mezani ambapo alimpiga busu Norene la shavuni.
               "Wacha niwahi" Alisema akataka kuondoka lakini Norene alimkamata koti la suti akamzuia.
                "Khaa!  Haraka gani hiyo we jogoo pori ndiyo  hata maji usinywe hebu rudi hapa" Norene  aliongea, Norbert hakuwa na pingamizi aliamua kururdi akachukua bilauri ya maji iliyopo hapo mezani akanywa kwa haraka kisha akaondoka kutoka nje.
 
   *SANTOS NA BENSON HATUNAO
*TAARIFA IKIWAFIKIA WALIOWATUMA WATAKUWA KWENYE HALI GANI
*MSALITI IKULU MIKONONI, JE IKUU ITASALIMIKA

KUYAJUA YOTE HAYO USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA YA RIWAYA HII NA ZINAZOENDELEA PIA


  



No comments:

Post a Comment