Thursday, December 22, 2016

MJUE PROFESSA AMANDINA LIHAMBA



MJUE  PROFESSA AMANDINA LIHAMBA


Professa Amandima Lihamba



   Natumai mu wazima na mnaendelea vyema na majukumu ya ujenzi wa taifa. Leo  katika siku nyingine ndani ya blogu ya Maridhawa, ni vyema tukawajulisha juu ya wanafasihi katika kipindi
chetu cha Wanafasihi wetu. Kama ilivyo  ada ni lazima tuwafanye  walau watu wang’amue juu ya uwepo wao. Uwepo wa fasihi nchini  pamoja na  Sanaa zingine basi hao  ninaweza kusema wamechangia kwa namna moja ama nyingine kutokea kwake. Ni wajibu wetu  kwa jamii nzima iweze kuwafahamu watu hawa adimu mno, waliyoweza kuisogeza mbele sehemu ya Sanaa nchini Tanzania. Ukianza kuzungumza taaaluma ya Sanaa, ni aghalabu sana kutotajwa hawa watu. Mkiwa msemaji wake ni mtu ambaye hajajua vyema historia ya Sanaa nchini Tanzania,  basi hilo huweza kutokea.

     Siku ya leo aliyepamba ukurasa wetu wa Wanafasihi wetu, si mwingine bali ni Professa  Amandina Lihamba. Mwanafasihi, muigizaji na pia mwongozaji wa filamu mwenye upeo mkubwa  sana katika fani hiyo. Mmojawapo wa waigizaji mwenye uzoefu mkubwa, lakini asiyepewa kipaumbele sana na waigizaji wa filamu nchini, hata kutakwa ushauri. Hakika ni lulu kwa soko la filamu nchini ambayo haiangaliwi kwa jicho la upekee. Penye miti hapana wajenzi


     Professa huyu alizaliwa mwaka 1944, mkoani Morogoro nchini Tanzania. Alipata shahada yake ya uzamivu(PHD) katika chuo kikuu cha Leeds nchini Uingereza. Mwanamama huyu kazi zake  kipindi cha awali hapo zilikuwa zikielezea mitazamo ya kisiasa hapa nchini Tanzania,  ikiwemo kipindi cha Azimio la Arusha. Aliweza kulichambua azimio hilo jinsi lilivyo na matokeo yake, akiwa kama Mwanasanaa aliweza kutunga kazi nyingi  za Sanaa zenye kuakisi kuhusu siasa nchini Tanzania.
  Katika tasnia ameweza kutoa filamu mbalimbali na zenye mawazo pevu, kwa jamii yote. Filamu hizo ni kama:

      Hivi sasa Professa huyu  anapatikana chuo kikuu cha Dar es salaam katika idara ya Sanaa  za maonesho, amewahi kuwa Mkuu wa wanafunzi (Dean of Students)  na mwanchama wa baraza la chuo hicho.

Huyu ndiye Professa Amandina Lihamba

(MAKALA HII BADO NI MBEGU)

No comments:

Post a Comment