Monday, June 20, 2016

MJUE PROFESSA ABDULRAZAK GURNAH

Abdulrazak Gurnah(kazaliwa 1948)




    Siku nyingine tena baada ya kurudi kwa nguvu nyingi mno tangu tulipopata changamoto za hapa  na pale ambazo zimetuweka nje ya fani yetu kwa muda mrefu mno. Leo hii  na kuendelea kwa kila jumatatu ndani ya
blogu hii tutawaletea kipengele hiki cha Wanafasihi wetu, tutajadili na kuwaelezea  wanfasihi mbalimbali ambayo ni wazawa wa nchi ya Tanzania.


  Shilingi yetu ya kuchagua yule apaswaye kujulikana na hadhira ya watanzani imemuangukia Professa Abdulrazak Gurnah (1948– ), huyu ni mmoja wa waandishi wa riwaya nchini Tanzania ambaye kwa sasa yupo nchini Uingereza. Alizaliwa  nchini Tanzania  mnamo mwaka 1948 huko Zanzibar.anajulikana haswa kwa kuandika kuandika kitabu cha  Paradise, Desertion na By the sea.  Aliingia nchini Uingereza kama mwanafunzi  mwaka 1968 ambapo kwa sasa ni Professa katika chuo cha Kent.


     Professa ni mmoja kati ya waandishi wachache wa kitanzania wanaotumia lugha ya kingereza kwenye kazi zake za kifasihi, mwanafasihi huyu asilimia kubwa ya riwaya zake zimeeangalia kipindi  cha baada ya ukoloni wa Afrika. Mbali na uandishi pia ni  mhariri mzuri wa kazi za kifasihi  na amehariri idadi kadhaa ya miswada na ripoti kuhusu fasihi.


Kazi zake ni ikiwemo:

Huyu ndiye mwanafasihi wetu kwa siku ya leo, pia ni Professa katika elimu ya elimu juu akiwa amefundisha vyuo kama vile  Bayero University Kano, University of Kent.

No comments:

Post a Comment