Friday, December 30, 2016

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA






RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________


SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA!!
                "Kila kitu mipango tu mama Jerry ngoja kibarua kiishe halafu tutaongea vizuri" Norbert aliongea muda huo tayari alikuwa ameshamaliza kula, alinyanyuka kwenye kiti chake akaenda mahali lilipo eneo maalum ya kunawia mikono akanawa kisha karudi mezani abapo alimpiga busu Norene la shavuni.
   
              "Wacha niwahi" Alisema akataka kuondoka lakini Norene alimkamata koti la suti akamzuia.
                 "Khaa!  Haraka gani hiyo we jogoo pori ndiyo usinywe hata maji usinywe hebu rudi hapa" Norene  aliongea, Norbert hakuwa na pingamizi aliamua kururdi akachukua bilauri ya maji iliyopo hapo mezani akanywa kwa haraka kisha akaondoka kutoka nje.


_____________
_____________________TIRIRIKA NAYO
_____________

****
KAMBI YA NGERENGERE
MOROGORO

    Kikao cha dharura kilikuwa kimeitishwa ndani ya chumba cha mkutano katika ya kambi hiyo ambayo ndiyo kambi kubwa ya  jeshi la anga pamoja na nchi kavu, maofisa wa juu ya kambi hiyo walikuwa wameitwa kwenye hicho na mkuu wa majeshi hayo yote mawili alikuwa ametoka jijini Dar es salaam mara moja kuja kufanya kikao na wakubwa wa kambi hiyo kutoa uamuzi wake uliohitaji ufafanuzi zaidi . M.J Belinda ndiyo alikuwa amewasili ndani ya kambi hiyo baada ya kupokea taarifa kutoka wakuu wa vikosi vya anga na ardhi waliopo chini yake katika kambi hiyo, alikuwa ameingia ndani ya kambi hiyo muda mchache tu uliopita akitumia helikopta maalum ya jeshi. Taarifa aliyoipata ndiyo ilimfanya aje kwa haraka katika kambi hiyo kuja kutoa uamuzi wake kwa wanaejshi hao waliopo chini yake, ilikuwa ni lazima aje kutoa taarifa hiyo.

    Alishuka ndani ya uwanja  wa ndege wa kambi ya Ngerengere ambao upo chini ya jeshi la wananchi wa Tanzania muda mfupi uliopita,  alipitiliza hadi ndani kwenye chumba hicho cha mkutano ambacho tayari wakuu wa kambi hiyo walikuwa wameshakaa wakimsubiri. Muda huo alikuwa tayari ameshapokea heshima zote kama mkuu wa vikosi vyote viwili kwa wanajeshi hapo, alikuwa amesimama katika kiti chake kilichokuwa kimekaa  kwenye upana wa meza yenye umbo la mstatili. Wanajeshi wote waliosalia walikuwa wamekaa kwenye viti vyao vilivyopangwa sehemu ya urefu wa meza ndefu ambayo ilikuwa ndani ya chumba hicho cha mkutano. Wote  macho yao yalikuwa yapo kwa  mkuu wao  aliyekuwa amekaa kimya baada tu ya kikao hicho kuanza humo ndani, alikaa kimya kwa sekunde kadhaa pasipo kusema chochote akitazama tu amaofisa hao wa ngazi za juu wa vikosi vya anga na ardhi.
             "Nadhani hamjajua kwanini nimekuja kutoa uamuzi mwenyewe badala ya kuridhia tu kwa simu kuwa vikosi viende kuongeza nguvu katika kuizunguka ikulu kama mkuu alivyokuwa amewapa amri makamanda wangu wakuu wa vikosi hivi" M.J Belinda alianza kuongea
              "ok kabla sijaendelea napenda  niwasikilize Bridagia Hugo kamanda mkuu wa jeshi la anga la Brigadia  Maswe kamanda mkuu wa jeshi la ardhini ndiyo niwape sababu ya mimi kuja kutoa maaamuzi mwenyewe. Ok Kamanda Hugo unakaribishwa" M.J Belinda aliongea kwa mara nyingine na alipomaliza aliketi kwenye kiti chake huku akiiweka vyema kofia yake nyekundu katika kichwa chake, mwanajeshi  mrefu aliyekuwa   cheo cha Brigadia jenerali ambaye alivaa sare za jeshi la anga zikiwa ni za rangi ya bluu iliyopauka alisimama akatoa saluti kwa M.J Belinda. Huyo ndiye alikuwa kamanda wa kikosi cha anga ndani ya kambi hiyo Brigadia Hugo.
               "Mkuu nusu saa iliyopita nimepata taarifa ya kupeleka kikosi cha anga kombania tatu chenye ndege zilizo na silaha ziende kwenye basement ya dharura  iliyopo ndani ya Nyambizi amabazo wanazitumia kwa sasa jeshi la maji ili ziongeze nguvu katika kuizunguka ikulu kwani bado ilikuwa na silaha kubwa sana za kumuhami mheshimiwa ambaye niliambiwa ni msaliti, nilipopata taarifa ilinibidi nikujulishe kamanda mkuu mwenye kamandi kuu kabla sijachukua uamuzi wowote na ndiyo hapo nikakujulisha. Ni hayo tu" Brigadia Hugo aliongea kisha akaketi chini alipomaliza kuongea, mwanajeshi mwingine mwenye cheo brigadia ambaye alikuwa mtu mzima kiumri alisimama kisha akatoa saluti kwa M.J  Belinda. Huyo ndiye alikuwa Brigadia Jenerali Maswe.
             "Mkuu muda huohuo anaouzungumza afande Hugo dakika kadhaa mbele yake yaani....dakika ishirini zilizopita nimepokea amri  kutoka kwa mkuu Ibrahim nitoe amri kwa Kamanda kikosi cha Mbagala  kipeleke kombania nne zikaongeze nguvu ya kumuondoa mheshimiwa rais Ikulu kwani bado silaha ambazo zinatumika kumuhami ndani ya ikulu zilikuwa na nguvu zaidi hivyo niliambiwa niongeze kikosi atoke mwenyewe kwa hiyari baada ya kuona amezidiwa kiuwezo na silaha zetu. Nikiwa askari niliyekuwa chini yako niliamua kutoa taarifa kwako mwenye kamandi kuu kwanza kabla sijachukua uamuzi wowote na ndiyo nikakupa taarifa hiyo, ni hayo tu" Brigadia Maswe aliongea kisha akaketi chini, baada ya wakubwa hao wa majeshi yote mawili waliopo chini ya M.J Belinda kuongea M.J Belinda alisimama kisha akatoa flash ya tarakilishi akaenda hadi kilipo kioo cha tarakilishi ndani ya chumba hicho cha mkutano akaichomeka.
                 "Kabla ya sijatoa maamuzi inabidi tuangalie nani msaliti  kati ya Mkuu Ibrahim au amiri jeshi wetu mheshimiwa rais" M.J Belinda aliwaambia na hapo kioo hicho cha tarakilishi kikaanza kuonesha picha za matukio mbalimbali ambayo wakuu hao wa jeshi walikuwa hawayatambui, ilikuwa ni ule mkanda aliourekodi Norbert  akiwa ndani ya shughuli nzima na mkanda ule aliokuwa akihojiwa mzungu yule aliyekiri kila kitu juu ya mpango haramu uliokuwa umewekwa. Kimya ndani ya chumba  hicho cha mkutano kimya ndiyo kilichukua nafasi katika muda ambao mkanda huo ulikuwa ukiendelea huku kila mmoja akisikitika kwa kile ambacho alikuwa akikishuhudia, hadi mkanda huo unamalizika tayari  kila mmoja alikuwa katika hali ya kutomamini kwa kila kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia. Walikiri kwamba walikuwa sahihi sana katika kusikiliza maamuzi ya Kamanda wao kwanza kabla hawa timiza maamuzi ya mnadhimu mkuu wa jeshi nchini, walikua wameujua usaliti wote uliokuwa ukifanywa na Mnadhimu mkuu wa jeshi hadi mkanda huo ulipomalizika.
                     "Nadhani mmejionea wenyewe sasa inabidi mjiulize tunafuata amri za senior mkuu au junior wake kicheo katikaa jeshi, kama tunafuata amri za senior ambaye ni mheshimiwa Rais basi tutamlinda na kama hatufuati amri zake na tukafuata za junior wake ambaye ni mnadhimu mkuu basi tutamshambulia. Wangapi wapi upande wa rais kabla sijatoa uamuzi" M.J Belinda alingea kisha akauliza swali ambalo lilifanya wakuu wote wa kambi hiyo waliopo ndani ya chumba hicho cha mutano kunyoosha mikono yao juu, wote walikuwa wapo tayari kufuata amri ya mkubwa kuliko na mwenye haki ya kulindwa ambaye ni rais Zuber.
                      "Vizuri sana makamanda, nimetumia njia hii ili mkubali wenyewe kwa mioyo yenu kuliko kutumia cheo changu kuwapa amri najua haitokuwa sawa katika jambo kama hili. Sasa basi uamuzi ni huu, vikosi alivyoviagiza msaliti wa nchi hii vitatoka kama alivyopanga ila havitakuwa upande wake bali ni kwenda kuilinda ikulu tu. Tena silaha ziongezwe zaidi kumlinda rais wetu mpendwa, ni muda wa fagio jingine la chuma nadhani kauli mbiu yake mnaijua." M.J Belinda aliongea
                     "FAGIO LA CHUMAAAA!" Alipomaliza kutoa uamuzi wake alipaza sauti ndani ya chumba hicho cha mkutano huku akiwa amenyoosha mkono wake wa kulia juu aliokuwa amekunja ngumi
                       "FAGIAAAAAAA!" Makamanda wote waliitikia kwa pamoja wakinyoosha mikono yao  ikiwa imekunjwa ngumi pia.
                         "Kufagia kuanze kwa mara nyingine"  .M.J Belinda alipotoa kauli hiyo alitoka dani ya chumba hicho cha mkutano huku makamanda wote wakisimama na kutoa saluti kwake kukubali kwa moyo mmoja amri yake ambayo ipo upande wa kiongozi mkuu wa majeshi na kuiasi amri ya Mnadhimu mkuu aliyekuwa ni msaliti wa jeshi.

****

      Muda ambao kikao kilikuwa kinaisha tayari Norbert alikuwa yupo ndani ya neo la Msasani akiwa  amefika jirani na mtaa wenye maghorofa mengi sana ndani ya peninsula hiyo, aliegesha gari  jirani na bar moja iliyokuwa imeungana na nyumba ya kulala wageni. Akiwa ndani ya eneo hilo alikuwa akiwaza jinsi ya kutafuta eneo ambalo walikuwa wapo kina Wilson ndani ya  Msasani, maneno ya yule mzungu aliyemtesa siku chache ziizopita juu ya kufikia kwao sehemu ambayo ni peninsula ndiyo yalimuongoza hadi eneo hilo. Norbert alikuwa anajua wazi kuwa hakuna peninsula yeyote ndani ya jiji la Dar es salaama isipokuwa Msasani tu, hiyo ndiyo ilikuwa ni penisula pekee ndani ya  jiji la Dar es slaaam. Ndugu msomaji peninsula ni eneo la ardhi ambalo limezungukwa na maji pande tatu na upande mmoja ukiwa haujazungukwa na maji, jijini Dars es salaam eneo hio liikuwa ni Msasani tu ambayo ndiyo pekee ilikuwa imezungukwana maji ya bahari pande tatu na hakukuwa na eneo jingine lililokuwa limezungukwa na maji namna hiyo zaidi ya hilo tu.
     Norert alitambua wazi kambi ya maadui wa taifa lake analolipighania walikuwa wapo ndani ya eneo hilo na siyo jingine, alikuwa na tatizo moja tu la kutojua maadui hao walikuwa wapo ndani ya jengo gani katika eneo hilo la Msasani ambalo ni kubwa lililokuwa limesheheni majengo mbalimbali ya kifahari. Akiwa ndani ya bar hiyo aliagiza kinywaji kisicho na kilevi cha grand malt  akawa anakunywa kwa taratibu sana huku akitafakari juu ya mahali pa kuanzia, alikuwa amekaa kwenye kiti na ikambidi anyanyuke aende kwenye eneo lenye viti virefu kwenye meza nyembamba iliyopo mapokezi hapo Bar maarufu kama kaunta. Alitembea kwa mwendo wa taraatibu na alipofika akakaa kwenye kiti kimoja kirefu akaweka chupa ya kinywaji chake kwenye eneo lenye meza nyembamba ambayo watu huweka bilauri na vinywaji vyao, alitupa macho mbele akamkuta msichana mrembo sana akiwa amevaa nguo maalum za kazi akmtazama kwa tabasamu tu alipoketi kwenye kiti hicho kirefu.
                 "Sema mrembo" Norbert alimwambia msichana huyo huku akimbania jicho  halafu akatoa tabasamu lake ambalo ni kilevi kwa wasichana..
                  "Sina usemi handsome wa mapoz na masmile" Mhudumu huyo alimuambia Norbert huku akitabsamu.
                     "Utakosaje la kusema wakati kila kitu chako kinazungumza mrembo, kukuangalia tu nimepata mengi ya kuongea"
                   "Mh!"
                    "Amini hivyo ulimi unayatoa yaliyopo ndani ya moyo"
                   "Haya bwana mshindi wewe"
                    "bado sijawa mshindi kwa watoto kama nyinyi nafikiri Nouther ndiyo mshindi kwenu kwa kila wakati"
                  "Tena huyo mtu usimzungumzie kabisa simpendi sana yule mkaka"
                   "Mh!  Kwani unamjua tajiri kama yule"
                     "Hee! Msasani hii nani asiyemjua yule mkaka aliyekuwa mdogo wa rais yule aliyefungwa gerezani"
                    "Duh! Kumbe maarufu hivi"
                       "ni zaidi ya maarufu huyo mtu yaani Masaki  anamiliki nyumba nne za ghorofa mtaa wa Mwaya karibu na Supermarket  ya Shirjee i na anaringa sana yule, hapa Msasani kwenyewe mtaa wa tatu hapo ana linyumba lipo kimya mda wote kama gofu yaani halieleweki sijui wapangaji wamemdodea"
                     "mwenye hela lazima aringe kwa alichonacho life yenyewe fupi hii"
                        "kuwa na hela siyo lazima uringe handsme, mbona wewe unaonekana una hela na huringi"
                     "nina hela wapi au suti zinakudanganya mrembo, mjini kupendeza tu"
                     "mh! Nimekuona tangu unaingia na gari lako lile pale parking"
                     "Kuwa na gari siyo kuwa na hela mrembo"
                       "Haya mshindi wewe ila yule mkaka akija hapa ana kazi ya kutuita malaya sisi wahudumu anafikiri kila mtu anafanya kazi hii ni malaya"
                       "(akitabasamu)Dah kweli anakosea mrembo kama wewe kukuita malaya ningekuwa mimi kaka yake ningemchapa fimbo"
                        "Mh! Una vituko wewe(kicheko kinamtoka baada ya kusikia kauli hiyo ya Norbert)"
                         "Kweli hiyo we mrembo kabisa hebu leta mkono wake nikuoneshe" Norbert mhudumu huyo ambaye alimpa mkono bila kusita, kwa haraka aliubusu mkono wake kisha akatoa tabasamu pana.
                         "sifa hii stahiki ya kugusa papi za midomo yangu kwenye mkono wako ni kwa ajili ya msichana mrembo tu, wewe ni mrembo zaidi ndiyo maana nimegusa papi zangu za midomo hapo usifuate maneno ya yule mwenye dharau juu ya warembo kama wewe" Norbert aliongea kihisia zaidi na mwishoni akamalizia na tabasamu.
                       "(akiangalia chini) We nawee hadi naona aibu yaani"
                          "usiogope ni kawaida tu, naitwa Norbert ukipenda niite Kaila sijui mrembo unaitwa nani?" Norbert aliongea hukua akimpatia mkono wake, mhudumu huyo naye alimpatia mkono wake kwa madaha sana.
                           "(akishikana mkono na Norbert) Martha, enhee Norbert kama nishawahi kulisikia hili jina mahali. Enhee! Norbert Kaila huyu mwandishi wa habari ni wewe nini?"
                        "Hujakosea ndiyo mie hapa nipo mbele ya macho yako"
                        "(akitoa macho kutoamini) Woow! Nafurahi kukufahamu"
                           "Mimi nina zaidi ya furaha kukufahamu Martha tatizo muda unakimbia ningependa unipatie namba yako ya simu maana nina zaidi ya jingine zito kuliko huku kukufahamu"Norbert aliongea huku akitoa simu yake ya mkonnoni kisha akampa Martha ambaye aliandika namba zake kisha akapiga na simu yake iliyopo kwenye mfuko wa sketi yake ikaanza kuita, alimrudishia Norbert simu yake ambaye aliitia mfukoni.
                           "Sasa Martha ngoja niwahi mahali" Norbert aliaga huku akinyanyuka kwenye stuli ndefu aliyokuwa amekalia.
                        "Haya Norbert (akimpungia mkono Norbert)"
    Norbert kwa haraka zaidi alitoka ndani ya bar hiyo akiwa na kile alichokuwa akikitafuta ambacho kingempa mwangaza wa mahali pa kuanzia katika kazi yake, alienda kwenye maegesho ya magari ndani ya bar hiyo na akaingia ndani ya gari ambayo aliiondoa kwa mwendo wa wastani barabarani akielekea kwenye nyumba ambayo alikuwa ameambiwa na Martha baada ya kumchimba kiundani pasipo yeye mwenyewe kujijua. Ndani ya dakika tano alikuwa mtaa wa tatu kutoka pale bar lakini nyumba ile aliyoambia hakujua ipo upande gani hadi muda huo, alizunguka katika mitaa hiyo kuitafuta nyumba hiyo lakini hakuiona kabisa.
    Norbert hapo aliamua kwenda kwenye duka la vinywaji baridi baada kuegesha gari mbali na hapo akiwa na lengo la kumchimba muuuzaji wa vinywaji hivyo awze kujua nyumba hiyo ilipo, alifika kwenye duka hilo ambalo lilikuwa limewekwa dawati ambalo alilikalia huku akihema sana akionekana ni mwenye kuchoka sana. Alikaa kimya sana katika benchi hilo ikiwa ni mbinu pekee itakayomuweszesha kupata jibu la kile anachokitaka, alitulia kwa muda mrefu sana hadi pale muuzaji wa duka hilo alipomfuata  mahali alipo.
                "Kaka mbona upo kimya kama nyumba namba 134, nakusubiri wewe nikusikilize nikupe huduma" Muuza duka huyo alimuambia.
                "Ofuuuu! Nimechoka sana nipe koka nitulize koo" Norbert aliongea kichovu kisha kamuuliza huyo muuzaji "ukimya wangu umenifananisha na nyumba namba 134 kwani ina nini?"
                 "Braza inaonekana wewe mgeni mahala hapa hata nyumba ya Nourther huijui ile ambayo ina ukuta mrefu  sana ipo pale kona karibia eneo moja  lenye nyumba za kupangisha" Mhudumu huyo alimuambia huku akifuata kinywaji alichoagizwa.
                "Aaah kaka we acha tu nimekulia hapa jijini lakini hata sehemu zingine sizijui ndiyo sembuse huku ugenini nlipokuja mara moja" Norbert alimuambia
                 "Kweli aise wewe mgeni hapa" Muuzaji huyo alikiri ugeni wake akiwa tayari ameleta kinywaji hiko kwenye  dawati alilokuwa amekalia Norbert.
                  "jiji kubwa kaka hili siwezi nikajua kila mtaa" Norbert aliongea huku akipiga mafunda ya soda aliyoiagiza kwa haraka sana alikuwa ana hamu ya kinywaji hikohiko kwa muda mrefu sana kumbe ilikuwa ni moja ya hila zake za kumfanya muuzajia huyo asiwe na maswali katika ubongo wake ikiwa ataondoka eneo hilo.

     Baada ya muda alikuwa amemaliza soda yote  alimrudishia muuzajichupa yake kisha akakaa kwenye dawati hilo kwa sekundee kadhaa akisanifu mazingira ya eneo hilo ambayo hayakuwa mageni sana kwake ila kutokana na kuwa yupo ndani ya kazi ilimbidi ajifanye mgeni wa mazingira hayo. Muda huo tayari alasiri ilishatokomea na sasa muda wa jua kushuka ndiyo ulikuwa ukielekea, mwangaza wa jioni wa eneo hilo ulimfanya azidi kuwa na hari ya kujua kile alichokuwa akitaka kukifahamu kila  alipokuwa akiyatazama mazingira hayo ambayo yalikuwa ndiyo yamemfanya awepo eneo hilo kikazi zaidi akisaka maskani ya wabaya wake.
     Alikaa  kwenye dawati hilo kwa muda  mrefu baada ya kumaliza soda hiyo akawa na kazi ya kuangalia mwangaza tu wa neeo hilo ambao ulikuwa ukiondoka  taratibu sana, Norbert aliutazama mwanga huo huku akitamani sana uondoke kwa haraka ili aweze kutimiza kile kilichomleta eneo hilo ambacho aliona akikifanya muda ambao mwangaza huo basi asinge kifanya kwa ufasaha kabisa. Hatimaye muda wa kuingia kwa giza uliwadia ndipo Norbert alinyanyuka kwenye dawati hilo akamuaga mwenye duka baada ya kumlipa pesa yake kisha kaanza kuembea kwa mwendo wa taratibu sana kuelekea kwenye eneo ambalo alikuwa ameegesha gari lake  mbali kidogo na duka hio la vinywaji baridi.

    Alipofika aliingia ndani ya gari na taratibu aliondoka ndani ya eneo hilo akiwa ainaifuata nyumba namba 134 katika mtaa huo ambayo ndiyo alikuwa ameambiwa na muuazaji wa vinywaji baridi wa eneo hilo, aliendesha gari kwa umbali wa mita dhaa ndipo akaona kona kali ya barabra iliyokuwa imejenga umbo la U kutokana  na uwepo wa ukuta mrefu uliokuwa  upo pembezoni kwa barabara. Norbert alikuwa akiipita ukuta wa  huo huku akisanifu vizuri kwa jinsi ilivyokuwa na ukimya mkubwa sana kuliko kawaida, ilikuwa ni  uzio mrefu sana ambao laiti mtu angeuona kwa mara ya kwanza asingedhani hiyo ni nyumba bali angedhani ni shule au taasisi. Ukimya wa eneo hilo ambalo ndani ya uzio wa ukuta huo kulikuwa na miti mingi ya kupandwa iliyo mirefu kuliko ukuta ilikuwa ikiifanya eneo hilo lizidi kuwa na ukimya wa kutisha unaoweza hata kumuogopesha mwizi asiindani ya eneo hilo.
   Norbert akiwa ndani ya gari lake akiifuata barabra hiyo yenye kona kali aliweza kuliona lango kuu la kuingia ndani ya nyumba hiyo likiwa na mitambo maalum ya kuzuia wezi kwa juu, lango hilo la eneo hilo pia lilikuwa ni lango kubwa sana ambalo lilikuwa halina hata nafasi ya mtu kuweza kuona nje. Kulikuwa na barabara iliyokuwa ikitoka barabara ya magari kwa urefu wa mita thelathini ndipo ulifikie lango hilo lililokuwa na mataa pamoja na mlango mwingine mdogo unaotumika kwa watu wanaoingi kwa miguu. Mazingira yake na jinsi ukuta ulivyokuwa mrefu ndiyo ulimpa hamasa Norbert kuweza kuifuatilia zaidi nyumba hiyo, baada ya kuisanifu vizuri nyumba hiyo aliamua kupitiliza na gari lake akaenda hadi mtaa unaofuata hadi sehemu yenye bar. Norbert aliegesha gari mahali hapo kisha akavua koti la suti yake akatoka ndani ya gari, alifunga milango vizuri na akaingia ndani ya Bar hiyo.

*N001 SASA ANAELEKEA KWENYE NGOME YA WISON ILIYOKUWA IMEWEKA MAFICHO YA KAKA YAKE NA WENGINEO, JE ATAFIKIWA KUTOKA? USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI NDIYO INA JIBU LA JAMBO HILO

*MTU KAZINI

TUKUTANE SIKU INAYOFUATA PANAPO MAJALIWA, TUWE PAMOJA


No comments:

Post a Comment