MJUE PROFESSA PENINA MHANDO MLAMA
Professa Penina Mhando Mlama |
Awamu
nyingine ya kipindi chetu cha Msanii
wetu katika blogu yetu Maridhawa, ni wajibu wetu kukujulisha juu ya watu muhimu kwenye
fasihi hii ya lugha ya Kiswahili. Ambao wana mchango mkubwa kisanaa na hadi
kitaaluma. Hakika Tanzania ni yenye hazina nyingi katika Sanaa amabazo zimekuwa
hazijulikani miongoni mwa Watanzania wenyewe, au hata Wanafasihi wa kizazi hiki
wamekuwa hawawatambui watu hawa ambao ikitajwa historia ya sanaaa ya lugha.
Basi katu huwezi kuwaacha kuwataja,
wasomi mbalimbali wa somo hili wamekuwa wakiwaimba mashule pasipo kuwajua hao ni kina nani. Hivi leo ukimuuliza Mtu
fulani aliyesoma ngazi ya juu ya elimu ya
shule ya upili, katu hawezi acha kukutajia majina ingawa si wote wanaowajuia
kiundani watu hawa. Siku ya leo tuna
Mama yetu, bibi yetu,wifi yenu, shangazi yenu na wengine ni dada yenu katika
kipindi hiki.
Anaitwa Professa Penina Muhando akiwa na jina
la Mlama kama jina la mwisho kutokana na Mwanamke kutumia jina la mume wake daima.
Alizaliwa mwaka 1948 huko Berega mkoani Morogoro nchini Tanzania.
Mhando alipata shahada ya Sanaa ya ukumbini, shahada ya ualimu na pia shahada
ya uzamivu(PHD) katika lugha na sayansi
ya lugha(linguistiki) katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Baadaye alipandishwa
kuwa Professa kisha mkuu wa idara ya
Sanaa za ukumbini katika chuo hicho.
Mhando likuwa ni mmoja wa kundi la waandishi wa tamthiliya katika kipindi
mwishoni miaka ya 1960, ambaye aliibuka kutokana na matokeo ya azimio la Arusha
mnamo mwaka 1967. Kipindi ambacho falsafa ya Ujamaa ikawa
ndiyo falsafa inayoongoza nchi, kipindi hicho Sanaa za ukumbini zilikuwa
zikikatishwa tamaa sana pale zinapochezwa
tamthiliya za kigeni. Waandishi wa ndani
wakawa wameamriwa kutumia Sanaa zao ili kueneneza falsafa ya ujamaa kwa
watu wa Tanzania kuwaonesha watanzania kuwa
hiyo ndiyo njia pekee ya kimaendeleo. Mhando alipatwa na njia panda katika
kutumia kingereza au Kiswahili, kutumia
kingereza kingemuwezesha kutumika kazi zake sehemu mbalimbali duniani lakini
siyo Tanzania ambapo wengi wao hawatumii lugha hiyo. Kiswahili vilevile
kingemuwezesha kutumika nchini tu, mwishowe akaamua kuandika kwa lugha ya
Kiswahili.
Kazi za awali za Mhando ni kama vile
Haitia
(Guilt, 1972),
Nguzo Mama(1982),
Lina Ubani(1984)
Mitumba
Ndui(1989)
Mhando ni miongoni mwa waandishi waliyokuwa
wakiakisi utaifa wa kiafrika,ni mmoja wa
waanzilishi wa harakati za Ukumbi kwa maendeleo (Theatre for development)
ambao walitaka watu watumie tamthiliya
ili kuhusisha mambo muhimu katika maisha yao na jamii yao.
Mnamo mwaka 2013, aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) na Rais Jakaya
Kikwete kwa muda wa miaka mitatu. Hivi sasa bado ni Professa wa chuo kiku
cha Dar es salaam, huyu ndiye msaani wetu kwa siku ya leo
HUYU NDIYE PROFESSA PENINA MHANDO MLAMA
(Nakala yetu hii bado ni mbegu)
TUKUTANE JUMA LIJALO SIKU YA ALHAMISI, MAJIRA KAMA HAYA
TUKUTANE JUMA LIJALO SIKU YA ALHAMISI, MAJIRA KAMA HAYA
No comments:
Post a Comment