Tuesday, December 27, 2016

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA




RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________



SEHEMU  YA ISHIRINI NA SITA!!
                 "nasema niachie mimi huyu mshenzi nimtie adabu" Benson aliongea kwa hasira huku akilia.
                  "Come on Benson huyu reporter ana kosa gani?!" Thomas alimuuliza kwa sauti ya juu, muda huo huo saa ya Norbert iliyokuwa ipo mikononi mwa Santos ilitoa mlio kisha ikawaka taa
kwenye kioo, Santos alipotazama kwenye kioo alikutana na  taswira ya mkono wa binadamu ikiwa umeonesha alama ya dole la kati apamoja na maandishi yaliyoandikwa 'LOSER'.
                    "Damn Norbert!" Santos aliongea kwa hasira huku akiibamiza saa hiyo kwenye marumaru.

__________
_____________TIRIRIKA NAYO
__________

    Wote walibaki wakimtazama Santos baada ya kuipigiza saa hiyo  kwenye sakafu ya nyumba hiyo waliyopo hadi ikavunjika kioo, sauti ya kvunjika kwa saa hiyo iliwafnya wote wanyamaze kwa ghafla na macho yao wakayaelekeza  kwa Santos ambaye alikuwa akiitazama saa hiyo kwa hasira sana baada ya kuivunja. Santos aliiongezea saa hiyo kwa kuikanyaga na kiatu chenye soli ngumu hadi ikavunjika sehemu zingine zilizosalia, alipomaliza kuivunja hiyo saa alinyanyua uso wake akawatazama wenzake waliokuwa wakimshngaa.
    Alipowatzama wenzake alitaka kuongea jambo ila akasita akabaki akiwa amefungua mdomo wazi kama alikuwa anataka kupiga muayo,  alinyanyua mkono juu kwa ishara wamsikilize lakini  hakuongea neno lolote. Hasira za kushindwa kutekeleza mpango wao ndiyo zilikuwa zikimtafuna hadi akawa katika hali hiyo, alikuwa akipigana na hali ya kuwa na hasira ilia arudi katika hali ya kawaida ndiyo maana alishindwa kuzungumza hadi pale hasira zake zitakopopoa.  Hasira bado ilikuwa ikimchemka ndani ya kichwa chake hadi akaweka mkono wa kuume kichwani kama alikuwa akiizuia isizidi kumchemka kichwani mwake, wote waliobaki waligeuza macho kumtazama yeye kwani walikuwa wakimtambua kama mtu mwenye hasira sana na hasira zake zikimpanda huweza kufanya jambo baya lolote. Benson aliacha kufanya vurugu zake kwa kuhofia angeweza kumtibua kabisa Santos akiwa amependwa na hasira namna hiyo, wengine waliosalia bado macho  yao yalikuwa yapo kwa Santos kumuangalia angefanyaje baada ya kuwa na hasira hivyo.
                     "Nyinyi .........." Santos aliwatukania mama zao wote kisha akaendelea, "tukikaa hapa na kuanza kujilaumu inasadia nyinyi, ndiyo atarudi hebu nyanyukeni tukajipange tena acheni us....". Santos aliwafokea wenzake kwa kujilaumu pasipo kufikiria hata yeye mwenyewe alikuwa akijilaumu pia, hasira zilimpelekea yeye kuwa namna hiyo.
     Alipoona wenzake wanamtzama tu kwa mshangao aliachia msonyo mkubwa sana kisha akatoka akaanza kutembea kuelekea sebule ndogo ya kulia chakula, alipofika kwenye sebule hiyo iliyokuwa haina samani alilisogelea dirisha akashika vyumba vinavyowekwa kabla ya kubandikwa kioo kwa nje. Hapo aliinamisha kichwa chake chini kwa sekunde kadhaa na alipokiinua alitazama nje kupitia hapo dirishani, alipoacha kutazama nje aligeuza shingo nyuma kuwatazama wenzake akawaona bado walikuwa wakimshangaa vile vile ilivyokuwa.
                     "Mnashangaa nini nyinyi? Katupeni mzoga huo tuingie kazini " Santos aliwaambia kwa ukali kisha akageuza shingo kuangalia nje kama alivyokuwa awali huku akiwa ameuma sehemu ya juu ya papi za midomo yake

****
USIKU WA SIKU HIYO

BARABARA YA OBAMA
     Ilpotimu majira saa sita usiku eneo la ufukwe wa bahari ambapo kupo mkabala na Ikulu kulipata kufikiwa na watu ambao ni nadra sana kufika eneo hilo, ardhi ya eneo hilo ilianza kutetemeka na hatimaye Nyambizi kubwa zipatazo kumi zikaibuka ndani ya maji  umbali mita takriban hamsini kutoka ndani ya maji. Nyambizi hizo zilijifungua kwa juu na kisha zikatoa  vyuma vipana mfano wa njia za kupandishia gari kwenye ndege, taa kubwa kutoka kwenye nyambizi hizo ziliwashwa  kisha magari ya  kijeshi aina ya hummer na jeep zilizojaa wanajeshi ambazo zipo wazi juu zikaanza kutembea kutoka ndani ya nyambizi hizo zikifuata njia maalum ya vyuma hivyo ambavyo vilikuwa vimewekwa  kapeti fano wa barabara.
     Magari yote yalikuja kusimama pembeni ya barabara ya Obama yakawa yanatazamana na ikulu, wanajeshi nao waliokuwa na silaha wakiwa wamevaa magwanda na kofia ngumu vichwani mwao walishuka kwa haraka kisha wakapiga goti moja wakiwa wameelekeza silaha zao ilipo  ikulu. Kikosi cha wanajeshi waliopo kwenye magari kiliposhuka chini chote vifaru vyenye rangi ya kijani kibichi navyo vilifuatia vikiwa na  maaskari wengine wanaokimbia kwa miguu wenye silaha wakiwa wanavifuata kwa nyuma, vifaru hivyo navyo vilienda kujipanga mstari mmoja nyuma ya magari ya jeshi kwa umbali wa hatua takribani tano. Baada ya hapo kisha walishuka askari maalum waliokuwa wapo ndani ya magari ya mizigo ya jeshi wakiwa wamebeba mizigo mikubwa sana, askari hao walienda kushuka upande mwingine ambapo vifaru vilikuwa havijafika kisha mizigo mikubwa iliyokuwa ipo ndani ya gari ikashushwa kwa kutumia mtambo maalum unaofungwa nyuma ya kichwa cha magari hato ya mizigo. Mizigo hiyo ilifunguliwa kisha askari hao wakaanza kuchakarika kwa kazi maalum iliyokuwa imewaleta hapo, ndani ya muda mfupi tayari mahema ya kijeshi yalikuwa yameshafungwa na maaskari hao.
     Saa sita kamili usiku ilipotimu  kukatimia kwa siku mbili kufikia  siku ya mapinduzi iliyosemwa,  maaskari  wa jeshi la maji tayari walikuwa wamejaa eneo hilo walikuwa wakitishia amani ya raia wa kawaida na halikufaa kupitika kabisa. Kutotumiwa kwa barabara ya Obama majira ya usiku kulifanya raia wa kwaida wasiweze kujua kile kilichokuwa kikiendelea eneo hilo kwa muda huo. Wanajeshi hao hawakuwa wamefunga jicho tu siyo kulala tu, macho yao yalikuwa makini kuiangalia ikulu kama amri ya kiongozi mkuu ilivyowataka kufanya hivyo. Ikulu yote ilikuwa imezungukwa na wanajeshi hao kwa kila pande na hakukuwa na nafasi nyingine ya mtu aliyekuwa yupo ndani ya ikulu kutoka , silaha zote za wanajeshi hao ikiwemo mizinga na bunduki za kila namna zilikuwa zimeelekea katika kila upande wa Ikulu.

****
    Ndani ha ikulu hali ilikuwa tete kwa Rais Zuber baada kuona kikosi hicho kizito cha jeshi la maji kupitia mitambo maalum iliyopo hapo ndani, alitoa amri kwa vikosi vinavyohusika na usalama wake kukaa jirani na uzio wa Ikulu kwa pande zote huku wengine wakiwa wamekaa juu kwenye mapaa ya ikulu wakiwa na risasi maalum za udunguaji. Pamoja na ulinzi huo wa usalama wa taifa waliokuwa wamevalia suti nyeusi wakiwa silaha bado aliona hakuwa na usalama na aliingia wenye chumba maalum cha kuongoza mitambo yenye kuhakikisha usalama wa ikulu nzima unakuwepo na akabaki akiangalia jinsi maafisa wa usalama wanavyochakarika na kazi yao.  Usingizi wote ulikuwa umeshamuisha na alimuacha mke wake akiwa amelala chumbani yeye akabaki akiwa anatazama wingi wa wanajehi hao kupitia kioo cha tarakilishi, alijikuta akichachawa alipoangalia silaha nzito ambazo yeye hajawahi kuziona akiwa kama amiri jeshi mkuu tangu aingie madarakani.
                 "Tanzania haina nyambizi kubwa kiasi hiki na wala sina taarifa ya kuongezwa kwa Nyambizi katika jeshi la maji" Rais Zuber alisema huku akizitazama Nyambizi hizo.
                 "Mheshimiwa inamaana huna taarifa za umiliki wa silaha nzito kama hizi katika jeshi" Kiongozi mkuu wa chumba cha kuongozea mitambo aliuliza.
                  "Ndiyo sina taarifa hizo hata  General Kulika kabla hajafariki aliwahi kusema  Tanzania jeshi lina Nyambizi za kawaida na alikuwa ananishauri ziongezwe kubwa mbili kwa usalama zaidi wa nchi hii upande wa majini, Nyambizi zilizokuwa zipo nilioneshwa siyo hizi kabisa" Rais Zuber aliongea huku akihema kwa wasiwasi.
                  "Hebu niunganishe na Meja jenerali Belinda kwa simu nisikie anasemaje kuhusu huu uvamizi unaotaka kufanywa ili wanipindue" Rais Zuber alimuambia kijana wa usalama wa taifa aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha kuzunguka kilichokuwa  kipo jirani na mitambo mingi ya tarakilishi, kijana huyo alipopokea amri alibonyeza namba zilizopo kwenye kibonyezo cha tarakilishi kwa haraka sana halafu akasita baada ya kuona kialama maalum kilikuwa kimetokea kwenye kioo. Alijizungusha kwenye kiti hicho cha kuzungukaakageuka nyuma yake alipokuwa Rais Zuber kisha akavua spika maalum za masikioni alizokuwa amezivaa, aliijipangusa na viganja vyake usoni kisha akashusha pumzi akiwa anamtazama Rais Zuber.
                   "Kuna nini?" Rais Zuber aliuliza
                   "Mheshimiwa simu zote zakutoka zinatoka na kuingia ndani ya ikulu tayari wameziua kupitia mtambo maalum ambao wanao wao" Yule kijana alimuambia
                    "Ohhh! No!" Rais Zuber alitoa sauti ya kukata tamaa kisha akaweka mikono kichwani kwa sekunde kadha na alipoitoa mikono hiyo kichwani alisema,"hata wao ukiwasiliana nao huwezi"
                   "ngoja nijaribu" Yule kijana aliongea kisha akakigeuza kiti chake akaangalia upande wenye tarakilishi, alibonyeza vitufe vingi vilivyokuwa chini ya kioo cha taraklishi hiyo kisha akasema "tunao uwezo wa kuwasiliana nao tu".
                   "Ok niunganishe nao" Rais Zuber alisema  akasogea nyuma ya kile kiti cha yule kijana karibu na kioo kikubwa cha tarakilishi kimojawapo, Yule kijana alifanya ujuzi wake na kioo hicho kikatoa alama mistari iliyokuwa ikizunguka duara huku kukiwa na maandishi 'connecting'. Baada ya muda sura ya mwanajeshi mtu mzima mwenye cheo cha Meje jenerali akiwa amevaa  gwanda pamoja na kofia ya rangi ya nyeupe  ilionekana, Rais alipoona sura hiyo kwenye kioo moja kwa moja alimtambua kama huyo ni msaidizi wa L.J Ibrahim.
                 "Mugiso" Rais Zuber aliita huku akitazma kwenye kioo cha tarakilishi.
                 "Yes Mr President" Meja jenerali  huyo aliongea.
                 "mimi si mkuu wako kijeshi, kwanini unaleta vikosi kunizunguka" Rais Zuber alilalamika
                  "wewe ulikuwa ni mkubwa  wangu lakini kuna mkubwa wangu mwingine ajaye atakayeingia hapo kwa sasa,  hivyo wewe siyo mkubwa wangu tena na ni amri kutoka kwa three star general baada ya kutopata majibu yako kwanini mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa amuue four star general na kwanini leo hii ukaonana na mtuhumiwa halafu usimkamate" Meja jenerali Mugiso aliongea.
                  "Come on Mugiso! Moses ni innocent katika hilo usifanye usichokijua" Rais Zuber aliongea
                  "sina uamuzi mwingine zaidi ya huo nilioambiwa na future general, maamuzi yatabadilika iwapo atatoa tamko yeye. Kutokuwa na hatia kwa Professa Gawaza kamuambie yeye ndiyo aamue. Kwa sasa ni hayo tu, nikutakie usiku mwema Mheshimiwa kesho kutwa ndiyo siku ya wewe kutoka hapo" M.J Mugiso aliongea na hapo mawasiliano yakakatika, Rais Zuber alichanganyikiwa zaidi na maneno hayo akajikuta hana uamuzi mwingine wa kutoa juu ya suala hilo.


(3)MFUNIKO
     Asubuhi iliyofuata habari kubwa iliyokuwa imetawala ndani na nje ya nchi ilikuwa ni hiyo ya kuzungukwa Ikulu na wanajeshi wa jeshi la Maji, hali hiyo ilizua hofu pia miongoni mwa raia na kuepelekea hata wananchi wa kawaida washindwe kulikaribia eneo la Ikulu kwa uoga waliokuwa nao baada ya wingi huo wa wanajeshi wenye silaha nzito. Watu pekee waliokuwa hawana hofu ya kupita eneo hilo walikuwa ni waandishi wa habari ambao walifika na kurusha habari juu ya tuko zima la kuzungukwa kwa ikulu, Helikopta za mashirika mbalimbali ya habari zilikuwa zikizunguka juu kuchukua matukio yaliyokuwa yakiendelea katika eneo hilo. Hadi jua linachomoza hakuna alyekuwa ndani ya ikulu ambaye aliweza kutoka nje kutokana na kuzingirwa huko pia amari waliyopewa wanajeshi hao ya kuhakikisha hatoki mtu ndani ya ikulu. Vyombo vya habari mbalimbali viliendelea kuripoti kuhusu suala hilo ambapo bado ilikuwa haijaeleweka chanzo cha kuzungukwa namna ile ikulu, jitihada za waaandishi wa habari katika kusaka chanzo cha  kuzungukwa kwa ikulu hiyo ziligonga mwamba kabisa na hakuna aliyeweza kupata ufafanuzi juu ya suala hilo.
   Ilipotimu majira ya saa nne ndipo Meja jenerali Mugiso aliweza kuonekana akitoka ndani ya hema la kijeshi lilipo eneo hilo akiwa ameongozana na wanajeshi wenye nyota mbili wapatao wanne, Meja jenerali aliendea hadi kwenye gari la kijeshi ambapo aliingiza mkono ndani ya gari hiyo akavuta kipaza sauti kilichokuwa na waya mrefu. Alikiweka kipaza sauti umbali wa sentimita takribani mbili kutoka ulipo mdomo wake kisha akaongea, "hili ni ombi kwa sasa wala si amri kwa wote mliopo ndani ya ikulu takatifu, mnaombwa kutoka wenyewe ndani ya ikulu na mjisalimishe tuwakamte kabla rais mpya mtarajiwa hajaingia jumamosi asubuhi. Leo siku ya alhamisi mnaombwa kutoka wenyewe kabla hatujatumia nguvu kuwatoa humo, Rais uliyemaliza muda leo kabla ya miaka kumi haijaisha unapewa siku ya leo na kesho tu usiwepo humo ndani"
    Meja jenerali Mugiso baada ya kutoa tangazo hilo alimkabidhi kipaza sauti mmoja wa maluteni kisha akaanza kutembea kurudi kwenye hema kuu lililowekwa eneo hilo, waandishi wa habari walimkimbilia lakini waliwahi kuzuiwa na wanajeshi wasifike anapoelekea.
               "General tunahitaji kuzungumza na wewe machache" Mmoja wa waandishi wa habari alipaza sauti na waandishi wa habari wengine wakiwa wameshika vipaza sauti walimuita Meja jenerali Mugiso jambo ambalo lilimfanya arudi tena hadi pale walipozuiwa akawaamuru maluteni wale wawaachie.
               "General inamaana muda wa urais ni miaka miwili tu hadi umuambie mheshimiwa amemaliza muda wake?" Maswali yalianza
               "General je kipi chanzo cha kuwaamuru vijana wako waizunguke ikulu?" Mwandhishi wa habari mmoj aliongea huku akimnyooshe mkono wake uliokuwa na kipaza sauti.
                "je ni sahihi kumuamuru  mkubwa wako kijeshi atoke ndani ya ofisi yake?" Mwandishi wa haabri mwingine alimtandika swali akiwa bado hajalijibun swali la kwanza.
                "Je kupanga kumuondoa rais anayependwa na wananchi namna hii huoni kama itawapa picha mbaya sana hasa upande wenu?" Mwandishi wa habari mwingine alimpa swali akiwa hajajibu mengine, maswali mengi yalikuwa yamemuandama Meja jenerali Mugiso ambaye alikaa kimya hadi pale waandishi wa habari waliponyamaza ndiyo akanyoosha mkono kama aliyekuwa akitaka kutoa kiapo huku mdomo akiwa ameacha wazi akitafuta neno la kuongea.
                  "Sijawa msemaji mkuu wa jeshi mwenye mamlaka ya kuongea maneno hayo, hii ni amri nadhani mkaulize uongozi wa juu yangu ndiyo utawapa jibu" Meja jenerali Mugiso aliongea kisha akaanza kupiga hatua kuondoka.
                 "Ikiwa utapewa amri ya namna hii juu ya mkeo na uongozi wa juu upo tayari kuifanya?" Swali jingine kutoka kwa mwandishi wa habari aliyekuwa yupo katikati ya kundi la waandishi wa habari kulimfanya M.J Mugiso asite kuendelea na safari kisha akageuka nyuma akarudi hadi pale uso wake ukiwa haupo kawaida.
                  "Nani aliyeuliza swali hilo?" M.J Mugiso aliuliza na hapo waandishi wa habari wakamtazama yule mwenzao aliyekuwa ametulia wala asioneshe hofu yoyote, mkono wa mwandishi huyo wa habari aliyeuliza hilo swali ulinyooshwa na kupelekea wanajeshi wale maluteni wapite katikati ya waandhi wa habri wakamkamata mwandishi huyo wakamvuta mbele kwa nguvu, M. J Mugiso alipomuona mtu aliyeuliza swali hilo alijikuta akiwambia wale maluteni waliokuwa wakijiandaa kumpiga wamuache.
                    "Norbert Kaila ndiyo adabu uliyofundishwa kwenu hiyo?" M.J Mugiso alimuuliza swali
                    "General ni swali kama swali jingine ikiwa wewe unafuata amri za mkubwa je upo tayari kutii amri juu ya mkeo unayempenda?" Norbert aliuliza swali hilo ambalo lilimfanya M.J Mugiso amtazame kwa hasira halafu akaondoka akihofia kumuadhibu habari ile isambae na kulichafua jeshi kwa kutesa mwandishi wa habari.
                    "hakikisheni mwandishi wa habari yoyote havuki eneo la kivukoni kuanzia muda huu, tumeelewana?!" M.J Mugiso alitoa amri, wale maluteni walitoa heshima kwa ukakamavu baada ya mari hiyo kisha wakaanza kuwaondoa waanhishi wa habari ndani ya eneo hilo kwa nguvu.

   M.J Mugiso alirudi ndani ya hema ambapo alienda hadi kwenye eneo maalum ambalo lilikuwa na mitambo mingi ya kisasa ya mawasiliano ikiwa imepangwa kwa ustadi mzuri, kwenye kioo cha moja tarakilishi kwenye mitambo hiyo kulikuwa kuna sura ya L.J Ibrahim ikiwa inamtazama yeye baada ya kuingia eneo hilo. M.J Mugiso alitoa saluti baada ya kuiona taswira ya mkuu wake kisha akasimama kikakamavu akitoa amri, alitulia akimsubiri mkuu wake aongee na hapo mkuu wake alianza kuongea.
                    "vizuri kwa kazi uliyoiongoza kwa msaliti anayeishi ikulu sasa basi kuna la ziada unatakiwa ulifanye, nimeona kupitia luninga mwandishi wa habri anakudhalilisha sasa hakikisha vijana wanamtia nguvuni ili aje kulipia kwa kauli zake zisizo na adabu" L.J Ibrahim alitoa amri ambapo M.J Mugiso alipiga saluti kisha kisha akachukua simu ya upepo akaongea, "hakikisheni mnamkamata Norbert Kaila aingizwe ndani ya Submarine haraka tumeelewana!"
                     "Mkuu" Sauti kwenye simu ya uepo iliitika kwa adabu, baada ya hapo kioo cha mawasiliano ya ana kwa ana baina ya M.J Mugiso na mkuuu wake kilikata mawasiliano na ramani ya eneo la ikulu ikatokea.

****

     Wakati hayo yakiendelea  L.. J Ibrahim na Mzee Ole walikuwa wakiyatazma kupitia kwenye luninga huku wakiwa wamepambwa na matabasamu katika nyuso zao, walijua tayari walikuwa wakikaribia kuimaliza kazi hata Norbert angekuwa na uwezo gani asingeweza kumuokoa Rais Zuber na balaa lililokuwa likielekea kumkumba. Mvinyo ndiyo ulikuwa umetawala katika meza yao huku wakiwa na faraha sana katika nyuso zao, walikunywa kwa kufurahi wakijua kuwa nchi ya Tanzania tayari ipo kwenye mikono yao na  Mzee Ole alikuwa akirudi madarakani na wao waweze kugawana fungu la pesa walilokuwa wameahidiwa. Muda huo ulikuwa ni muda mfupi tu tangu L.J Ibrahim atoe amri ya kukamatwa kwa Norbert  baada ya kumuona kupitia kioo cha Luninga akimuuliza swali M.J Mugiso, waliendelea kufuarahi huku wakinywa kwa pamoja chupa ya mvinyo kwa kutumia bilauri tofauti. Walikuwa wakiongea na kucheka kwa furaha sana kila walipokuwa wakiiangalia Luninga jinsi ilivyokuwa ikirusha matangazo juu ya kinachoendelea Magogoni. Hakika hatua ya ushindi wa mwisho ndiyo waliiona ilikuwa wakiikaribia kuifikia na vikwazo vilikuwa vikiondoka kimoja baada ya kingine, walibadilisha chaneli mbalimbali za luninga bado habari ilikuwa ni ileile hata walipoweka chaneli za nje ya nchi.
               "aisee kazi imekwisha nasubiri wale vijana wa nusu komandoo wamtie mikononi Kaila tuje tummalize nina uhakika hatatoka" L.J Ibrahim aliongea
               "Kabisa General" Mzee Ole aliitiki, muda huuohuo simu ya upepo iliyokuwa ipo jirani yao ilianza  kukoroma na hapo L.J Ibrahim aliichukua m kwa haraka.
               "Enhee nipeni habari, Norbert mnae hapo" L.J Ibrahim aliuliza
                "Hatujamuona mkuu hata waandishi wa habari wenzake wanasema hawajui ameelekea wapi?" Sauti ya M.J Mugiso ilisikika kwenye simu hiyo ambayo ilimfanya L.J Ibrahim aondokwe na furaha papo hapo.
                "Wajinga nyinyi!" L.J Ibrahim alifoka kwa hasira.

*NJOZI YA MAPINDUZI IMEANZWA KUOTWA

*RAIS NDANI YA KUTI KAVU KISA MOSES

*NI MTAFUTANO TU


USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA KUUONA MTAFUTANO HUO, TUOMBEANE UZIMA NA AFYA TU MKIMBIZANO TUUONE.



*Mtafutanoo

No comments:

Post a Comment