Saturday, December 24, 2016

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU






RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________




SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU!!                                                                                                                                

     Majira ya saa tisa kasoro robo misafara hiyo tayari ilikuwa imeshawasili katika eneo la Pugu ambalo kulikuwa kumefungwa maturubai na viti kwa ajili ya kuketi viongozi mbalimbali, dakika kumi baadaye gari lililobeba mwili wa Jenerali Kulika liliwasili na watu aote walisimama wakati jeneza liliwa linashushwa ndani ya gari hilo. Maaskari wa JWTZ walewale wenye vyeo vya Brigadia jenerali
yaani bibi na bwana pamoja na nyota tatu katika mabega yao walilibeba jeneza hilo kwa mwendo wa pole kuelekea katika eneo lenye shimo lililojengewa pamoja na kuwekea mbao juu. Walitembea kwa mwendo huo hadi walipolifikia shimo hilo la kaburi wakaweka jeneza juu yake katika mbao, maaskari hao walisogea pembeni  ya shimo hilo kikakamavu  kisha watu wakaketi katika viti vyao kusubiri taratibu zingine zinazofuata.

____________
____________
_____________
    ________


    Kikundi cha maaskari kilichokuwa pembeni kilikuwa kimejipanga mstari mmoja ulionyooka huku mikononi mwao wakiwa wameshika bunduki aina ya SAR56, kikundi hicho kilinyanyua bunduki zao juu kiutiifu baada ya kupokea amri kutoka kwa kiongozi wao kisha wakazielekeza angani. Walipiga risasi angani kisha wakazishusha chini kihatua wakifuatana na amri ya Kiongozi aliyekuwa amewapa amri ya kuzinyanyua na kuzipiga angani, walisimama mguu pande baada ya kuzishusha silaha hizo wakiwa wametulia kiutiifu. Walikuwa kama wamegandishwa na theluji jinsi walivyotulia na hata kama nzi atatua jirani na pua wasingetingishika wala kuhangaika kumtoa kwa jinsi walivyojawa na roho ya kijasiri na kikakamavu, gwanda zao za mabaka walizovaa amabazo ziliwafanya wapendeze ndiyo zilizidi kupendezesha utulivu waliokuwa nao baada ya kupiga risasi angani.

   Askofu mkuu wa kanisa katoliki alisogea jirani na lilipo jenza na akendelea na utaratibu mwingine uliokuwa ukitakiwa kwa ajili ya  maziko ya Jenerali Kulika kama ilivyokuwa imepangwa kwa mujibu wa ratiba ilivyo, akiwa katika mavazi yake maalum ambayo hutambulika nayo katika sehemu za ibaba askofu huyo aliiongoza ibada hiyo hadi alipomaliza kisha jeneza likanyanyuliwa na wanajeshi waliokuwa wamelibeba hapo awali wakaliweka katikati ya shimo palipokuwa pamewekwa mbao maalum kulizuia lisianguke shimoni.Wanajeshi hao walizungushia jeneza hilo kamba kisha mbao zilizowekwa juu ya kaburi zilitolewa. Walilishuusha jeneza chini taratibu, lilifikishwa hadi mwishoni mwa sakafu ya kaburi hilo iliyokuwa imesakafiwa kwa utaaamu mkubwa sana. Hapo waanajeshi walitoa kamba zilizokuwa zimelishikilia hilo jeneza kwa kuzvuta kwenda juu kisha wakarudi kusimama kwa ukakamavu mkubwa.

   Askofu aliyekuwa akiongoza ibada nzima aliongea maneno ya kiroho kisha akatupa udongo kaburini kwa utaratibu mno,alipomaliza aliruhusu watu wengine kutupia udongo kaburini hasa viongozi wa juu wa serikali wakiongozwa na rais Zuber ambaye alikuwa ameongozana na ADC akiwa amevaliwa magwanda ya kijeshi tofauti na nguo za kisherehe alizoeleka kuonekana nazo naye  alifanya zoezi hilo la kutupia udongo kaburini. Rais Zuber alipotupa udongo kaburini viongozi wengine walifuata kisha mwishoni ubao ukafunikwa juu ya kaburi, kutokana desturi iliyojengeka miongoni mwa waumini wa dini ya kikristo wa kutofukia kaburi zaidi ya kufunika juu na ubao kisha zege linafuata. Jenerali Kulika  hakufukiwa pia,baada ya zoezi hilo kukamilika maaskari wenye bunduki mikononi mwao walipewa amri na walizinyanyua juu kwa mara nyingine kisha wakapiga risasi hewani. Baada ya tukio hilo viongozi mbalimbali wa kitaifa walianza kuondoka tararibu eneo hilo  kisha viongozi wa kijeshi wakifuatia wakiongozwa na L.j Ibrahim. Viongozi hao wakijeshi wakiwa wamekuja na magari yaliyofanana walianza kuondoka mmoja mmoja, kisha watu wengine wa kawaida wakafuatia kwa kuondoka eneo hilo.


****

    L.J Ibrahim akiwa amekaa kiti cha nyuma kwenye gari yake baada tu ya kuondoka eneo la maziko  alito simu yake akabonyeza baadhi ya namba kisha akaiweka sikioni, alisubiri kwa muda mfupi kisha akaanza kuoongea baada ya simu yake kupokelwa na mtu aliyekuwa akimpigia.

                   "nipe ripoti Boy....kazi imeenda kama ilivyopangwa?....pongezi kwako Boy uje jioni kuchukua malipo ya kazi yako" Alipomaliza alikata simu kisha akatoa tabasamu lililoashiria wa kile alichokuwa amekipanga

                   "buriani Belinda" Alijisemea moyoni huku akiwa na tabsamu pana usoni mwake.

    Muda huo tayari gari lilikuwa linakaribia kufika maeneo ya uwanja wa ndege kwenye njia inayotoka uwanja wa ndege kuingia barabara ya Mwalimu Nyerere,gari aina ya landcruiser lilionekana likitaka kuingia barabrani pasipo kutambua kulikuwa na gari ya mnadhimu mkuu wa majeshi ilikuwa inapita. Hali hiyo ilisababisha achomeke mbele ya gari la L.J ibrahim kimakosa,Dereva wa gari alilokuwa amepanda L.J Ibrahim alijitajidi kulikwepa gari hilo pasipo kupunguza mwendo na akafanikiwa kulikwepa lakini alipoendelea na safari alikuwa na wasiwasi mkubwa sana.

                 "mtu wa aina gani huyo asiyetambua kuwa gari ya three satrs general inapita hadi achomekee simamisha gari tukamtie adabu kutokana na nidhamu yake mbovu" L.J Ibrahim alifoka kwa hasira huku akimtazama  dereva wake amabaye alikuwa akitetemeka lakini hakugeuza gari kama alivyoambiwa hali iliyompelekea L.J Ibrahim apandwe na hasira.

                  "we Koplo Himu nimekuambia geuza gari husikii!!" L.J Ibrahim alifoka kwa hasira huku akimtazama dereva wake ambaye alikuwa akitetemeka hadi jasho jembamba lilikuwa likitoka kichwani ingawa kulikuwa na kiyoyozi ndani ya gari.

                   "mkuu kuna tatizo" Koplo Himu aliongea kiuoga.

                    "Damn hilo ni tatizo lako mimi halinihusu nimekuambia punguza mwendo na ugeuze gari au unapinga amri ya senior officer wako" L.J Ibrahim alifoka kihasira alipoona dereva wake hatii amri aliyompatia.

                    "Mkuu breki hazikamati nitageuzaje gari, hata huyo aliyechomekea mbele ya gari yetu nimemkwepa kwa mwendo mkali si kwamba niliamua hivyo bali breki zilikataa na nikafanya hivyo na hapa ninavyokuambia bado haikamati na mwendo haupunngui" Koplo Faimu alijitetea huku akimtazama mkuu wake kwa uoga kutokana na hofu aliyokuwa nayo bada ya kugundua tatizo lililopo kwenye gari waliyokuwa wanaitumia.

                     "nini?!" L.j Ibrahim aliuliza huku aiwa amegwaya kutokana nna taarifa aliyokuwa amepewa na dereva huyo, swali lake la mshangao halikujibiwa na dereva wake ambaye alikuwa akiiwazia roho yake kwa jinsi gari ilivyokuwa ikikaribia makutano ya barabara ya Tazara.

                      "Imekuwaje ikawa hivyo kwani gari hamkulifanyia uchnguzi wakati yanatoka kambini?!" L.J Ibrahim aliuliza huku akiwa hatulii kwenye kiti alichokuwa amekikalia, ujasiri wote wa kijeshi uliikuwa umemuisha na hakuwa na ujanja kabisa.

    Akiwa na kiwewe baada ya kuambiwa maneno hayo na dereva wake alifungua mkanda wa kiti  kisha akawa anaangalia kushoto na kulia kama mtu aliyepatwa  na wazimu, haja ndogo ilimbana kwa ghafla pasipo kutarajia kama ingembana.

                       "mkuu nilikuambia hi gari naona kama siyo lakini ukaniita nimechanganyikiwa kisa nyota tatu zilizopo kwenye gari hii ona sasa" Koplo Himu alimlaumu  mkuu wake.

     Maneno hayo yaliposikiwa na L.J Ibrahim alishika kichwa chake kwa mikono miwili kama mtu aliyesahau jambo muhimu kisha akamtazama Dereva, kumbukumbu zake zilirudi nyuma kwa haraka hadi aple muda ambao alikuwa akitoka kwenye maziko. Maneno ya Koplo Himu wakati aKitilia mashaka gari walilokuwa wamepanda yalimrudioa kwenye kichwa chake lakini alijikuta anakataa kisha akakunja sura akamtazama Koplo huyo kwa hasira.

                       "tahira wewe mbona ufunguo wa gari ni huohuo" L.J Ibrahim alimuambia kwa hasira.

                      "mkuu kumbuka funguo zinafanana na zina vibango vya aina moja zote" Koplo Himu alijitetea huku akijaribu kwa uwezo wake wa udereva aliongoze gari hilo.

                      "kufanana siyo kuingiliana wewe pimbi" L.J Ibrahim alifoka.

                     "mkuu nina wasiwasi yule dereva wa Madam Belinda alinibadilishia funguo" Koplo Himu aliongea huku akihangaisha usukani kukwepa magari yaliyokuwa yameanza kwenda taratibu kutokana na kuwa nusu kilomita kutoka eneo lenye mataa, taarifa ya gari yake kupita eneo hilo haikuwepo kwa maaskari wausalama wa barabarani.

    L.J Ibrahim wenyewe kwa uamuzi wake alimuamuru dereva wake asipitie njia ya mkato ya Tabata ambayo  ilikuwa imepangwa kutumiwa na misafara ya jeshi. Mpango alioupanga ndiyo ulimfanya asipite njia hiyo ili baadaye aje kuusikia kwenye vyombo vya habari ukiwa umetimia. Sasa aliona hatari ya kuchezewa mpango na mtu aliyekuwa amempangia njama hiyo, maneno ya Koplo Himu yalimpa taarifa kabisa ya kuharibika kwa mpango huo na akaona ajiokoe yeye na nafsi yake kwa kutumia mazoezi ya kijeshi aliyokuwa nayo.

    Kwa haraka kabisa alitoa kibanio cha mlango gari lake lilipokuwa limekwepa gari lililokuwa upande wa kulia. Alifungua mlango wa kushoto na alijitupa kwa umahiri mkubwa katika mtaro wa maji machafu uliokuwa mkavu hapo barabarani huku akimuacha Koplo Himu ndani ya gari akiwa anahaha na usukani wa gari. Kujirusha kwake kulimfanya atue vibaya  akaumia lakini hilo hakulijali zaidi ya kujali kuokoa maisha yake kutokana na ajali mbaya iliyokuwa ikikaribia kumpata.  Tukio hilo lilishuhudiwa na watu waliokuwa wakitumia sehemu ya wapitas kwa miguu ambao walimshangaa kwa jinsi L.J Ibrahim alivyojirusha kimaridadi,  yeye hakuwajali alijiweka sawa kisha akatoka ndani ya mtaro huo huku akiwa ameuma meno kwa maumivu aliyoyapata baada ya kuangukia vibaya ndani ya mtaro.

     L.J Ibrahim aliingia sehemu ya watembea kwa miguu na alianza  kutembea kwa haraka kuepuka watu wasije wakamkariri sura, aliinamisha uso wake chini na alienda hadi ilipo stendi ya pikipiki akapanda moja ya pikipiki ambaye dereva wake alikuwa aeshikilia usukani kama anajiandaa kuiwasha. Alimpa amri dereva mahali pa kwenda bila kuongea chochote na dereva wa pikipiki alitii amri hiyo kwa kuiwasha pikipiki akaiondoa kufuata uelekeo wa Jeti rumo.




MAMBO YALIVYOKUWA
   Muda ambao mazishi yalikuwa yakifanyika Norbert alibanwa na haja ndogo ambayo ilimshinda kuistahimili ikambidi aende kuitoa, aliamua kutembea kueleka vilipo vyoo vya dharura viliwekwa mita takribani tatu kutoka yalipoegeshwa magari ya wakubwa wa  kijeshi. Kuelekea kwenye vyoo hivyo ilimbidi ayavuke magari ya wakubwa wa jeshii  ili aweze kuvifikia. Akiwa anayakaribia magari ili ayavuke alimuona mtu akiwa yupo chini wa uvungu wa gari ambalo alilitambua ni la M.J Belinda kutokana na kuegeshwa karibu na gari lenye tatu ambalo ni la  L.J Ibrahim. Norbert alijikuta akiwa na hamu ya kuangalia kile anachokifanya yule mtu ilihali haja ndogo ilikuwa imembana, alijibana  miguu yake ili mtu mzima asije akaadhirika na akakaa jirani na eneo hilo yalipo malori ya kijeshi.

    Yule  mtu alipotoka uvunguni mwa gari la M.J Belinda alitokomea nyuma ya vyoo akiwa yupo makini na wala hakutambua tayari alikuwa amewekewa umakini na mtu aliye makini, alipopotea kwenye upeo wa macho ya Norbert alikuwa tayari amempa wasaa mwingine Norbert kufanya kile alichoona kipo sahihi. Alitumia akili nyepesi aliyonayo kwa kutoa nyota moja kwenye gari la L.J Ibrahim alilokuja nalo maalum kwa mazishi akaihamishia kwenye gari la M.J Belinda ambalo lilikuwa likifanyiwa uchokozi na yule mtu aliyekuwa yupo uvunguni mwake. Alipomaliza alishika sikio lake la kulia akaweka vizuri kinasa sauti kilichopo ndani ya sikio lake,  halafu akatumia muda huo kumpa taarifa Moses ambaye ni dereva wa M.J  Belinda kwa siku hiyo.
            "mliwekewa utelezi muangukie kwenye shimo la umauti katika hii gari, sasa fanya kila unachoweza ubadilishe funguo ya gari la Thrree star general uichukue wewe kisha  utumie gari lake" Norbert alipotoa taarifa hiyo ndipo alipokumbuka haja ndogo iliyokuwa imembana na akatimua mbio kwenda chooni.

****
    Baada ya Moses kupokea taarifa hiyo kutoka kwa Norbert alimfuata Koplo Himu ambaye alikuwa ameshika funguo za gari mkononi akizichezea hana akiwa habari yoyote, alimsogelea Koplo Himu alipokuwa amesimama huku akiangalia nyuma mithili ya mtu  aliyekuwa amezubaishwa na jambo ambalo lilimfanya ashindwe kutazama huko aelekeapo. Akiwa na funguo za gari mkononi alimkumba kikumbo Koplo Himu na kupelekea funguo za gari alilokuwa akiliendesha zianguke sambamba na funguo za gari la L.J Ibrahim ambazo zilikuwa mikononi mwa Koplo Himu.
             “Afande unawaza nini hadi huangalii mbele unapoelekea?” Koplo Himu alimuuuliza Moses huku akiokota funguo zilizokuwa zimesalia chini baada ya  Moses kuwahi kuokota funguo za gari  analoliendesha pasipo yeye mwenyewe kutambua.
             “afande acha tu cheki yule mtoto kule mbele” Moses aliongea huku akiomnyooshea kidole msichana mrembo aliyekuwa amevaa kitambulisho cha waandishi wa habari shingoni mwake, Koplo Himu alipomuangalia msichana huyo na jinsi alivyo mrembo alikiri ana haki ya kuwa na kiwewe namna ile hadi afikie hatua na kutoangalia upande anaoelekea.
               “afande aisee pale sikulaumu mtoto mkali yule hata ukigongwa na gari kwa kumuangalia bado sitakulaumu aisee, mungu kaumba bwana acha apewe sifa mtoto anavutia balaa yule kama  kizingiti cha msalani hajawahi kukivuka tangu aje duniani” Koplo Himu aliongea huku akijishika kidevu chake akimtazama yule mwandishi wa habri wa kike kwa tamaa kubwa.
               “ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Afande hata wewe umeona mtoto anakimbiza yule” Moses aliongea akicheka huku akingongeshana ngumi na Koplo Himu halafu wakatazama kama kuna mtu aliyekuwa akiwatazama, waliporidhika hakukuwa na mtu anye watilia umakini wowote walicheka tena kwa nguvu.
                “Sasa afande wacha mimi niende chooni mara moja maana kuonana na mdada huyo ilikuwa ajali tu nikiwa naenda chooni nikajikuta nimekatikiwa ghafla na haja ndogo lakini sasa hivi imerudi tena kwa fujo” Moses alimwambia Koplo Himu huku akigongesha naye ngumi.
                 “Poa afande mazishi yakiisha omba namba kabisa usimkose mtoto yule mkali” Koplo Himu alimuambia  Moses ambaye alikuwa ameshaanza kuondoka taratibu, alimsindikiza na neno la utani,”aisee mjeda unatikiswa na urembo tu jamaa yangu kama ni vitani halafu adui yako itakuwaje si kuuliwa tayari”
                 “Aaah! Afande pale usinilaumu aisee kama ni vitani labda niwe nimechemkwa na damu ndiyo nitammaliza lakini hivihivi tu sina moyo huo,cheki mtoto yule yaani angekuwa ni mkuu  wangu wa kazi ningepiga kwata mbele yake bila yeye unipa amri ya kufanya hivyo” Moses alizidi kutumbukiza maneno ya utani baada ya kubaini ni mada anazozipenda Koplo Himu ambaye aliishia kucheka huku akimtazama Moses amabye alikuwa akiishia mbele ya upeo wa macho yake.
     Moses baada ya kuachana Koplo Himu alielekea moja kwa moja katika upande wenye vyoo ambako ndiyo Norbert alikuwepo, huko alimkuta Norbert akiwa ameegemea moja ya vyoo vya chuma vilivyowekwa kwa muda akiwa anatafakari jambo. Alimfuata hadi pale alipo akasimama mbele yake akamuonesha funguo za gari, alitoa tabasamu na Norbert akajibu kwa kutoa tabsamu pia halafu akamuonesha alama ya dole gumba.
                  "good umecheza ndani ya mstari sasa wacha cha moto kiwawakie wenyewe kwa ujinga wao wanaoufanya" Norbert alimuambia Moses huku akitabasamu.
                   "wamewasha moto wacha sisi tutie mafuta ukolee zaidi waungue wenyewe siyo tuhangaike kuuzima, ukiwakolea watahangaika kuzima wenyewe ili mambo yasiwe mabaya kwao kumbe ndiyo wanajiharibia zaidi" Moses aliongea huku akiachia tabasamu kama alivyoachia Norbert baada ya kujua kila kitu kilikuwa kimeenda ndani ya mstari kama walivyokuwa wamepanga baada ya kuona mchezo mchafu walioelekea kuchezewa na ambao waliamini kabisa ulitokana na hila za maadui zao wasioitakia mema nchi ya Tanzania. Baada  ya  kuhakikisha kila kitu ipo sawa Moses alirudi alipokuwa awali huku Norbert akiwa anaangalia  usalama wa eneo hilo la maegesho ya magari. Alikaa jirani na eneo hilo kutokana na nafsi yake kumlazimisha aendeleaa kukaa eneo hilo, nafsi  ilimshauri awe na subira na yeye  aliifuata nafsi kwa kuwa na subira hivyohivyo.

    Haikupita muda mrefu yule Mtu  aliyekuwa akichokonoa gari la M.J Belinda alirejea akiiwa  ni mwenye  kuhangaisha macho yake katika eneo la maegesho ya magari hayo,macho yake yalitua kwenye gari la M.j Belinda ambalo tayari Norbert alikuwa amelibadilisha na kuonekana ni gari la Luteni jenerali. Mtu huyo aliweka mikono kichwani kwa haraka akijua alikuwa amekosea kazi aliyokuwa akiifanya,   alijipekua haraka mfukoni akatoa spana  akiwa na lengo la kwenda kusahihisha pale alipokosea wakati alipotumwa na mkuu wake.
     Aliwaza kusahihisha hilo suala haraka sana lakini hakutambua kwamba tayari alishachelewa kwani Norbert alikuwa tayri ameshamuweka katika anga zake, alipopiga hatua moja mbele aliguswa bega na Norbert ambaye tayari alikuwa ameshajongea hadi nyuma yake. Yule mtu alipogeuka nyuma wala hakupata hata nafasi ya kumuona huyo aliyemshika begani, kitendo chake cha kugeuza shingo nyuma alikutana na pigo la haraka la kijasusi ambalo hupigwa kwa kubonyeza shingo ya mlengwa. Pigo hilo ambalo Norbert alilitoa kwa wepesi mkubwa sana lilimfanya yule mtu apoteze fahamu papo hapo na akawa anadondoka, Norbert aliwahi akauweka mkono wake begani mwake mithili ya mtu anayembeba  mtu aliyezidiwa ambaye hawezi kutembea.

   Alimkokota kwa haraka kuelekea kuelkea nyuma ya vyoo ambako kulikuwa na miti mingi iliyopandwa kwa  ukaribu, alimuweka chini ya mti mmoja akimuelekeza kwenye shina mti katika upande ambao siyo rahisi kwa mtu  kumuona akitoka katika upande wa eneo la maziko labda atokee katika upande wa huko kwenye miti ndiyo angeweza kumuona kwa urahisi kabisa. Alimpekua mifukoni mwake akatoa vitu mbalimbali ikiwemo kitambulisho cha mpiga kura na kadi ya benki ambapo vyote vilikuwa na picha iliyoandikwa kwa jina lake huyo mtu'
              "Richard Mabina" Norbert alilisoma jina la huyo mtu ambaye hakuwa na fahamu kabisa na wala hakuwa na utambuzi wowote utakaomuwezesha kujua kama alikuwa ametajwa jina lake na  mtu ambaye alikuwa naye kwa ukaribu sana, Norbert hakuridhika upekuaji alioufanya akamsachi zaidi huyo mtu akamkuta na simu ya mkononi ya kisasa. Alichukua simu ya huyo akaibonyeza kitufe cha kuwasha kwa haraka ili aweze kuipekua lakini ilikuwa imefungwa kwa mchoro maalum(pattern)
               "Shit!" Norbert aliongea huku akiuma meno kwa hasira, alijifikiria kwa sekunde kadhaa kisha akajipekua mifukoni mwake akatoa kichupa kidogo kinafanana na kichupa cha unga maalum wa kujipodoa(poda), alifungua mfuniko wa chupa hiyo na ndani pakawa na mfuniko mwingine wenye matobo madogo.

   Norbert aliinamisha kichupa hicho kwenye kioo cha simu na akaanza kukitingisha na kupelekea unga wenye rangi ya kijivu utoke kidogokidogo umwagike kwenye kioo cha simu hadi ukafunika kioo, alipomaliza alifunga kichupa hicho kisha akakirudisha mfukoni, halafu akainamisha kioo cha simu na uleunga ukamwagika wote chini. Alipomaliza kuumwaga unga wote chini alimtazama Richard ambaye alikuwa hana fahamu kisha akaachia tabasamu, alirudisha macho yake kwenye kioo cha simu na kukuta ule unga ulikuwa umebakia  umechora mchoro maalum wa kufungulia simu ambapo ndiyo ulimfanya aachie tabsamu lake la ushindi wa kufanikiwa kufanya kile alichotaka kukifanya. Bila kupoteza muda aliufuaitisha mchoro  ule kama ulivyotokea kwenye kioo, alikosea kwa mara ya kwanza na ikamlazimu aufuatishe kinyume na jinsi alivyokuwa akiufuatisha hapo awali. Hatimaye simu ikafunguka naa Norbert akaanza kupekua kile alichokuwa akikitafuta kwenye simu hiyo, alitikisa kichwa kama mtu aliyekuwa ameafiki jambo wakati akizidi kuipekua simu hiyo hasa katka sehemu za ujumbe mfupi wa maneno.


*Mambo yamekuwa mambo
*Mtego kutegeana mazishini
*nini kitachojiri?!


USIKOSE SEHEMU YA ISHIRNI NA NNE AMBAYO NDIYO ITAKUWA NA MAJIBU YA  MITEGO MTEGEANO.

 KAMA UKIIHITAJI RIWAYA HII KUANZIA MWANZO AU HAPA ILIPOISHIA. WASILIANA NASI KWA SMS KWENDA NAMBA +255762 219759

No comments:

Post a Comment