RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
SEHEMU YA ISHIRINI!!
Wakati Boyka ambaye ni msambazaji wa madawa wa kuaminika akiwamaliza wazungu wawili kati ya sita waliotumwa na Brian, nyumbani kwa akina Moses kulikuwa kuna mambo mengine kabisa. Baada ya wote kuingia ndani Hilary na Irene aliingia katika chumba cha wageni na Moses pamoja na Beatrice waliingia katika chumba cha kulala cha Moses, Beatrice aliingia kwa kusita na hatimaye akaingia moja kwa moja hadi kitandani akaketi. Moses alipoingia tu aliuficha ule mkoba wa baba yake aliondoka nao halafu akaenda kukaa kitandani na Beatrice.
"ooh! Joto sana" Beatrice aliongea huku akifungua vifungo vitatu vya shule na kusababisha sidiria laini aliyoivaa ndani ionekane, Moses alibaki akimuangalia Beatrice chini ya shingo hadi kifuani.
****
Mapigo ya moyo yalianza kumuenda mbio baada ya kuona kifua cha Beatrice kikiwa kimeonekana, Moses alirudisha macho na kumtazama Beatruice alipoyatoa kifuani mwake. Tabasamu lililochanua mithili ya ua ndiyo lilipokea macho ya Moses alipoyasafirisha kutoka kifuani hadi kwenye uso wa Beatrice, Moses naye alijikuta akitabasamu huku akizidi kumsogelea zaidi Beatrice hadi akawa yupo karibu yake uso kwa uso. Beatrice aliyafumba na kufumbua macho na kufumbua huku akitazzma papi za midomo ya Moses akionesha uso wenye aibu kwa mbali, Moses alipoangaliwa hivyo kwake ilikuwa ni ishara tosha kwake iliyomulisha ni nini mpenzi wake anataka atimiziwe. Moses alitimiza kile ambacho mpenzi wake anataka ambacho kilianza hata kumuhamisha yeye katika ulimwengu huu na akajikuta yupo katika ulimwengu mwingine wa yeye na mpenzi wake. Uchokozi wa aina mbalimbali usiokasirisha wala kukera ndiyo ulifuata hapo kitandani kiasi cha kumfanya Beatrice awe hajiwezi na wala hakutambua ni muda gani alitolewa visitiri mwili wake na Moses hadi akajikuta akiwa viwalo vya maficho pekee, alibaki akiwa hajiwezi hata kidogo na alikuwa akimuangalia Moses kwa macho yaliyo na umbo la mwezi ambao upo nusu kutokana na kutojiweza kabisa na ujanja aliozidiwa na Moses. Alibaki akigumia kama mtu mwenye kiu sana anayekunywa maji kuondoa kiu inayomsumbua, Moses siku hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa kuwa na mwanamke katika hali kama hiyo ingawa alikuwa akifanya vitu kama vile ni mzoefu katika nyanja hiyo inayopendwa na kila mwanadamu. Wasaa mwingine ulifika katika mchezo wao huo ambao ulihusika kwa kutoa viwalo vya vificho, Moses alishika kiwalo cha kificho cha juu cha Beatrice akakitoa bila wasiwasi na akawa anajiandaa kiwalo cha chini ili akitoe vilevile. Upinzani mkali alikutana nao pindi alipogusa kiwalo cha chini na akahitajika atumie mbinu mbadala kukivuka kikwazo hiko.
"Moses please stop(Moses tafadhali acha)"Beatrice aliongea huku akiizuia mikono ya Moses kwa namna isiyotumia nguvu, Moses hakusita aliendelea na kile alichokuwa anakifanya bila hata kujali maneno ya Beatrice.
"Moses Iam afraid (Moses ninaogopa) sijawahi kufanya hivyo" Beatrice alilalamika kwa sauti yenye ulegevu huku akitumia nguvu kidogo katika kumzuia.
****
KITUNDA
DAR ES SALAAM
Ndani ya nyumba moja kubwa ya kizamani inayofanana na kiwanda katika eneo hilo, ilikuwa ni ghala isiyotumika ambayo sasa imegeuka kuwa makao ya kundi la wahalifu waliokuwa wapo mbali na bosi wao kwa miaka kadhaa tangu aache kuwa pamoja nao. Bosi wao huyo ni msichana mdogo aliyekabidhiwa kundi na mmoja wa wapenzi wake wa zamani baada ya kufariki katika ugomvi na kundi la wapinzani wao, Annie ndiye aliyekuwa bosi wao ambaye hakuwa nao kwa miaka kadhaa sasa amerejea akiwa na hasira kali sana za kunyimwa nafasi ya kuwa na Moses katika mahusiano. Muda huo wakati Moses na Beatrice wakiwa wapo katika ulimwengu mwingine wa kihisia katika chumba cha Moses yeye pamoja na vijana wake walikuwa wakiweka kikao ndani ya nyumba hiyo ambayo ndiyo makao ya vijana wake.
"madam tunafurahi kurejea kwako katika uongozi kwani tulikuwa hatuna dira katika maisha yetu kwa miaka hiyo ambayo ulikuwa haupo" Mmoja wa vijana wake aliongea
"msijali sasa tupo pamoja nimerudi kwenye kazi na pia ni muda wa kumshikisha adabu binti wa huyu mhaya mwenye sifa na jeuri ya pesa" Annie aliongea huku macho yake yakiwa ni mekundu kwa hasira kutokana na balaa lililomkuta asubuhi ya siku hiyo.
"madam mhaya yupi tuambie fasta maana tumemisi kuona damu kwa siku nyingi" Mwingine aliongea huku akimtazama Annie kwa macho makubwa yenye hamu ya kutaka kufahamu kinachoendelea.
"Bernard Mutashobya nafikiri mnamfahamu kabisa, sasa binti yake yule mdogo nataka atekwe mara moja tena atakuwa ni mke wenu kila siku akiwapa maraha humuhumu ndani" Annie aliongea akiwatazama vijana wake wa kazi ambao walikuwa wamejawa na matabasamu usoni mwao kwa kusikia suala la kumteka msichana mrembo pia awe kiliwazo cha miili yao.
"Madam kwahiyo unataka kutuletea bikra humu ndani awe mke wetu maana yule mtoto nasikia hajaguswa kabisa" Mwingine aliongea akiongea huku akitabasamu sana kuliko wenzake.
"of course tena inabidi mumteke haraka kabla mwanaume wa moyo wangu hajapasua boma lake ili mulipasue nyinyi awezwe kuachwa na mpenzi wangu ili niwe naye, pia leo ndiyo siku ambayo nitafungua mzigo uliopo kwenye ghala ya kusini ambayo niliifunga nilipoacha majukumu. Sasa basi mjiandae kufanya kazi mpate utajiri huku mnamleta hapa yule malaya mpenda wanaume wanaopendwa na wenzie, ngoja nikachukue ufunguo muanze kazi mara moja ya kutafuta wateja" Annie alisimama kwenye kiti alichoketi kisha akapeana na vijana wake halafu akaondoka.
****
Baada ya ushawishi alioutumia Moses anafanikiwa kile kilichokuwa kinampa hofu Beatrice na pia alifanikiwa kuuvunja ukuta mwembamba uliokuwa unalinda boma lake lisiweze kuingiliwa, kelele pamoja na maumivu vyote vilimtoka Beatrice na akajikuta anamng'ata Moses kutokana na maumivu aliyokuwa anayasikia. Moses alipomaliza Beatrice alioneksna kuwa na maumivu makali ambayo yalimfanya Mosea amuonee huruma na ikambidi ambembeleze mpenzi wake, Beatrice muda huo alikuwa amempa mgongo Moses akiwa hataki hata kumuangalia usoni hivyo Moses ikamlazimu amshike bega kumgeuza.
"Moses niache usinishike!" Beatrice alisema kwa ukali huku akiutoa mkono wa Moses begani kwake.
"Mpenzi" Moses aliita kwa taratibu huku akimgeuza Beatrice taratibu.
"Nimekwambia niache huko umeniumiza unanishika ili iweje" Beatrice aliongea akionesha wazi kukasirika, ilikuwa ni wakati mgumu kwa Moses kwani hakuwahi kukutana na hali kama hiyo katika maisha yake na hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kukumbana na hali kama hiyo, ilimbidi amtulize Beatrice kwa kumpa maneno matamu hadi alipokaa sawa ndipo akamsaidia kumnyanyua na akampeleka bafuni akajisafisha akavaa nguo zake. Walitoka hadi sebuleni wakishikana kutokana na Beatrice kushindwa kutembea vizuri, mwendo wake ulikuwa ni wa kuchechemea ingawa aliweza kujimudu kutembea. Hilary na Irene nao hawakukawaia kutoka katika chumba cha wageni, walitoka hadi sebuleni wakakaa kidogo halafu wakaungana na Beatrice katika kumuaga Mosea kisha wakaondoka.
****
USIKU
KIGALI
NCHINI RWANDA
Taarifa za kutumika kwa akaunti ya Brown anayetafutwa na mashirika mbalimbali ya kijasusi ya barani Ulaya nazo zilifika katika makao ya EASA nchini humo, mpelelezi mwenye namba HI002 anayeitwa Hilda Alphonce alikabidhiwa jukumu la kumtafuta gaidi huyo kwa upande wa Rwanda. Taarifa za kuangaliwa matumizi hayo kwa umakini ndiyo zilikuwa zimetolewa kwa matawi ya Barclays ya nchini Rwanda, usiku wa siku hiyo Hilda akiwa kwenye gari yake akipita barabara ya KN9 akitokea kwenye shughuli zake. Akiwa jirani na tawi la benki ya Barclays alipokea simu ikimtaarifu akaunti ya gaidi Brown ilikuwa inatumika muda huo katika tawi la Kigali, hiyo ilikuwa ni taarifa njema kwa Hilda alisimamisha gari yake kando ya barabara kisha akatembea kuelekea mahali ambapo mashine za kutolea pesa (ATM) zilipo. Siku hiyo Hilda alikuwa kavaa suti ya kike yenye muundo wa suruali na silaha yake ya kisasa ilikuwa katika koti la suti tayari kwa lolote, alitembea kwa tahadhari kwa kuangalia kila upande hadi jirani na sehemu ya kutolea pesa ambayo ilikuwa imezungushiwa vioo. Alipofika hapo alimkuta mwanaume mrefu mwenye asili ya barani Ulaya ambaye alikuwa akitoa pesa kwenye moja ya mashine zilizopo sehemu iliyozungushiwa vioo, Hilda aliingia hadi ndani ya vioo kabisa kisha akatazama kila upande kujiridhisha kuwa hakuna mtu mwingine huku macho yake yakiwa makini kabisa kumtazama aliyepo mbele yake ambaye ndiye aliyemtilia shaka kwa mujibu wa maelezo aliyopewa yanayohusu kutumika kwa akaunti ya gaidi Brown. Hakutaka kumchelewesha alichomoa akmuelekezea bastola kisha akamuamuru "tulia hivyohivyo na unyooshe mikono juu kisha upige magoti, vinginevyo namwaga ubongo wako" . Yule mtu ambaye Hilda mwenyewe alikuwa ana uhakika ni Brown alicheka kidharau kisha akasema, "mwanamama hivi unajiamini nini?", halagu akanyoosha mikoni juu kwa maringo mithili ya kinyonga atembeapo eneo lenye amani. Hilda alimsogelea kwa tahadhari sana ambayo haikuzaa matunda ya kujihami na kumtia nguvuni kwani huyo mtu ambaye sura yake haikufanana na Brown alirusha teke lenye kasi na kuipangua bastola ya Hilda bila hata yeye mwenyewe kutarajia kitu kama hicho. Bastola yake ilipigwa teke ikaanguka pembeni na akawa hana bastola tena, yule mtu alileta pigo la nguvu la judo kumlenga Hilda kifuani lakini alipiga hewa baada ya Hilda kusogea pembeni kulikwepa pigo hilo. Hilda naye hakutaka kuchelewa kwani alivyokwepa teke hilo alikuwa yupo karibu na adui yake ambaye alishtukishwa na ukaribu wa Hilda aliofika, Hilda alipokuwa karibu hapo alichia ngumi mfululizo zilizompata yule adui yake za uso kisha akampiga teke la miguu yote lilimtoa nje ya sehemu ya ATM kwa kuvunja kiooo kilichopo hapo. Kengele hatari ya hapo benki ililia baada ya mvunjiko huo na mtu aliyekuwa anapambana na Hilda alipotea ghafla katika mazingira ya kutatanisha baada ya kuvunjika kioo hicho na hata Hilda alipotoka kumuangalia hakumkuta kabisa alikuwa kama kapotea mithili ya mchawi. Hilda alipomkosa alirudi ndani akachukua bastola halafu akaondoka hadi kwenye gari lake, alipoingia ndani ya gari walinzi ndiyo walifika eneo la tukio wakakuta vipande vya vioo tu. Hilda alipokuwa ndani ya gari alitoa simu yake akabonyeza vitufe kadhaa kisha akaiweka sikioni akaongea, "hakikisha mkanda wenye picha ya nilichokifanya unautoa kwa ajili ya usalama zaidi". Alikata simu kisha akawasha gari akaondoka.
****
Brian baada ya kuongea na vijana wake Scott, Jameson, Calvin na Obren, aliamua kupanda ndege uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere kuelekea jijini Kigali nchini Rwanda hakutaka kukaa Tanzania na alitaka kuwaachia vijana wake wa kundi la Mambas waifanye kazi aliyowatuma. Baada ya saa matatu aliwasili na alihitaji kulala hotelini kwani giza lilikuwa limeshaingia tayari, hivyo ilimbidi atumie kadi yake ya zamani kutokana kusahau kadi yake nchini Kenya anapoishi. Hivyo ili asigundulike kwa sura anayoitumia muda huo aliamua kuvaa sura nyingine kisha akaenda kutoa peaa katika tawi la Barclays la jijini Kigali, alipomaliza kutoa hela ndipo alipokutana na sekeseke la kupambana na mwanamke asiyemjua hadi akatoroka kwa kutumia mbinu ya kijasusi akihofia kunaswa na maaskari kwani mwanamke aliyepambana naye alionekana ni jasusi kabisa.
Alipoondoka eneo la hapo benki alipokea simu kutoka Dar es salaam ikimjulisha vifo vya vijana wake wawili katika nyumba aliyowawela kule Bunju, habari hiyo ilimtia hasira na akaamua aende mwenyewe kuongeza nguvu. Siku hiyo hiyo alikata tiketi kwa njia ya mtandao kisha akajitayarisha kwa ajili ya safari siku inayofuata.
****
Siku zote msokota nywele kwa siku ya kwanza lazima kichwa kimuume kwani haikuwa mazoea yake na akizoea hatasikia maumivu na hata mvaa hereni kwa siku ya kwanza lazima sikio limuume na akija kuzoea maumivu huondoka, ndivyo ilivyo kwa mwanamke aliyevunjwa boma lake lazima apate maumivu lakini akizoea maumivu hamna tena na itakuwa kiburudisho kwake. Baada ya wiki
mbili kupita Beatrice alikuwa tayari ameshazoea jambo hilo na kwake haikuwa maumivu tena, mapenzi kati yake na Moses ndiyo yalizidi kuchanua sana, uhusiano wao ulimfurahisha hata dada yake Beatrice. Katika kipindi hicho hofu dhidi ya Andrew ilikuwa imeshawatoka na hakuna hata mmoja aliyekuwa na habari nao, katika kipindi hicho pia ndipo balaa jingine lilitokea maeneo ya Mbezi Afrikana. Ilikuwa ni siku ya Ijumaa wakati Moses, Beatrice, Irene na Hilary wakitoka shuleni wakiwa wapo ndani ya gari moja, siku hiyo Moses alikuwa kashika usukani wa gari akiliongoza kurudi wakitoka shule. Walipokuwa maeneo ya Mbezi Afrikana ambalo si mbali sana na shule yao mlio wa bunduki aina ya SMG kisha gari yao ikayumba ikatoka kutoka barabarani ikagonga nguzo ya umeme, eneo zima lilijaa makelele huku na kule baada ya risasi kupigwa hewani. Gari aina ya ford ranger ilionekana ikiegeshwa katikati ya barabara ikiwa imejaa kundi kubwa la wanaume wenye miili mikubwa, vijana wapatao wanne walishuka kwenye gari wakaenda hadi kwenye gari waliyomo kina Mosea na kuwatoa wote waliwakuta wakiwa hawajapatwa na tatizo lolote. Waliwakamata kwa nguvu wakawa wanawapeleka katikati ya barabara na walipowafikisha waliwaelekezea bunduki kila mmoja ya kichwa, Beatrice na Irene muda huo walikuwa wanatetemeka sana kama wamefungiwa kwenye chumba chenye baridi.
"Mosea ni nani kati yenu?" Mmoja kati ya wale vijana aliuliza huku akikoki bunduki.
"Mimi hapa" Moses alijibu huku akitetemeka baada ya kusikia bunduki aliyoelekezewa Beatrice ikikokiwa.
"Gotta kasema tumuue fasta, Dani mwaga ubongo wake fasta tusepe kabla nzi wa serikali hawajatimba" Mmoja wa wale vijana aliongea kumuambia aliyemuwekea bunduki Moses. Aliyemuelekezea bunduki Moses alitaka kumalizia kazi yake aliyotumwa hivyo aliweka kidole katika sehemu ya kufyatulia risasi na alipotaka kufyatua milio mingine ya risadi ilirindima kutokea upande wa njia inayotoka Mwenge, baadhi ya vijana waliowazunguka Moses walianza kuanguka chini milio hiyo ya bunduki iliposikika. Moses alipoona hivyo aliwakumba kikumbo wenzake wakaanguka chini kisha akawaashiria wenzake wabiringite kuelekea kwenye mtaro na wote wakatii ingawa walikuwa wanaumia, barabarani gari aina ya toyota hiace ilionekana ikiegeshwa katikati ya barabara upande wa numjia iendayo Mwenge kisha vijana wenye bunduki aina ya SMG wakashuka wakipiga risasi mfululizi upande walipo wale vijana waliotaka kumuua Moses. Yalikuwa ni majibizano ya risasi baina yao yaliendelea na kusababisha eneo lote liwe kama uwanja wa vita, Moses na wenzake walitambaa kwenye mtaro wakatoka nje ya barabara kisha waliiendea gari aina ya Suzuki iliyokuwa imeegeshwa pembezoni ili wapate sehemu ya kujificha. Eneo zima la lilikuwa linanuka baruti kutokana na majibizano hayo ya risasi yaliyosababisha maafa kwa mali za raia na hata kuua baadhi ya raia waliokuwa wapo pembezoni mwa barabara na jirani na eneo hilo kwa upande wa nyuma kwa upande wa mbele ya nyuma ya eneo la mashavu, mashambulizi hayakuwaathiri kina Moses kwasababu walikuwa pembeni wakiwa wamejibana kwenye ubavu wa gari waliyoikuta pembeni upande nwa barabara. Wakiwa wamekaa hapo milango ya gari hiyo iliyokuwa ndiyo ficho lao ilifunguliwa kwa upande waliopo.
"ingieni ndani na mlale kwenye viti" Ilisikika ikitokea ndani ya gari ikiwapa amri nao wakatii bila shuruti. Waliingia ndani ya gari wakamkuta kijana wa makamo ambaye ni sawa na kaka yao akiwa amejilaza kwenye kiti cha dereva kilichonyooka kuelekea nyuma, wote kwa pamoja walijilaza humo ndani ya gari wakiwa wanatetemeka sana kutokana na tukio hilo. Milio ya risasi iliendelea kurindima kati ya makundi mawili ya vijana ambao kwa kuwatazama tu ungejua kama ni majambazi au wahalifu, maganda ya risasi yalikuwa yamemwagika barabarani huku baadhi miili ya vijana miongoni mwa makundi haya ikiwa imezagaa barabarani baada ya kutokwa na uhai kwenye mapigano hayo. Baada ya dakika ishirini ving'ora vya magari ya polisi vilianza kusikika vikitokea niia iendayo Mwenge, viliposikika kwa karibu vijana hawa wa makundi yote mawili walipanda magari wakatokea kuelekea njia iendayo Bagamoyo kwa kasi sana. Baada ya wao kuondoka yule kijana aliyewasaidia kina Moses alinyanyua kiti cha dereva akakiweka sawa kisha akawasha gari.
"msiinuke kaeni hivyohivyo maana hii ni hatari kwenu" Aliwaambia kina Moses ambao walianza kuinua vichwa vyao juu, Yule kijana aliweka gia kisha akatembea pembeni ya barabara hadi akalivuka eneo la tukio. Aliingiza gari barabarani kisha akaondoka kuelekea Mwenge baada ya kuliacha mbali eneo ambalo awali liligeuka uwanja wa vita.
*Balaaa limeanza
No comments:
Post a Comment