Thursday, December 17, 2015

SHUJAA SEHEMU YA KUMI NA TATU







RIWAYA: SHUJAA


MTUNZI: Hassan O Mambosasa

SIMU:+255713776843
+255762219759



WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



            ILIPOISHIA

"yaani umeaga wote ila mimi hujaniaga" Beatrice aliongea kwa sauti ya chini ambayo haikusikika na wakina Andrew ambao walikuwa wanawatazama.

"sio hivyo" Moses aliongea akiwa anatazamana uso kwa uso na Beatrice. Beatrice alimtazama Moses kwa macho malegevu kisha akafanya tendo ambalo lilikuwa mwiba kwa Andrew alipoliona, alimbusu Moses kwenye papi za mdomo kwa sekunde kadhaa kisha akamuachia huku akiwa amegusanisha paji lake la uso na la Moses.

"I love you too" Beatrice alimwambia  Moses kwa hisia tena kwa sauti ya juu kidogo hadi Andrew akasikia kutoka pale alipo.



ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI YAKE



SEHEMU YA KUMI NA TATU!!

 ****

 Maumivu aliyoyasikia ni zaidi hata ya kujibonda na nyundo kwenye kidole cha mwisho, mwanamke anayempenda akimtakia mwanaume mwingine neno ambalo alihitaji atamkiwe yeye. Moyoni alihisi amefanyiwa hatia na Beatrice kwa kuweka moyo wake kwa kijana mwingine, machozi taratibu yalishuka kwenye kutoka machoni hadi mashavuni kwa aliloliona mbele ya macho yake. Andrew alijikuta analia bila kutoa sauti na machozi ndio yaliashiria kulia kwake, lilikuwa ni jambo lisilopingika kwa kuwa macho yake yalipendezwa na moyo ukajihitaji mahala usipohitajika. Moyo wa mtu mwingine ndiyo ulihitajika mahala ambapo moyo wake ulipahitaji, mapenzi ya dhati juu ya mtu asiyempenda ndiyo yaliyokuwa yanamtesa.

"mwana hapa kubali kushindwa tu" Mmoja wa marafiki zake aliongea huku akimshika Andrew.

"upendo wangu ni nuru kali kama ya jua ambayo hutoka tu kuonesha siku mpya  hauzuiliki, yale naona ni mawingu yanataka kuzuia upendo wangu na hayatoweza. Yatayeyuka tu yawape faida wakulima" Andrew aliongea kwa hisia machozi yakimtoka huku mwili ukimtetemeka akiwa anaangalia upande aliposimama Moses na Beatrice pamoja na Irene na Hilary ambao tayari walikuwa wameongezeka na muda huo walikuwa wakiongea kwa furaha wakiwa wamekaa juu ya gari ya Moses.

"hakuna atakayeninyima haki ya kupenda nilipopenda maana mimi ni jua na nina haki yoyote mbele ya dunia ndani ya ulimwengu wa sayari zote. Nitapendwa na nitampata" Andrew aliongea huku machozi yakizidi kumtoka kwa uchungu alionao kwa alichokiona. Machozi yake sasa hivi yalizuiwa na kitambaa cheupe kutoka kwa dada yake aliyewasili muda huo, Annie alijawa huruma na hali aliyonayo mdogo muda huo.

"Machozi yako haya hayafai kuanguka  kisha yanyonywe na sakafu hii ya vigae iliyopo eneo hili kwa kitu ambacho utakipata, Andrew Iam your sister nipo siwezi nikakuacha uumie hivi  young bro. Remember what am I told you we have to do something for our happiness(kumbuka nilichokuambia tunatakiwa tufanye kitu kwa ajili ya furaha zetu) Annie alimwambia Andrew akiwa na sura ya huruma, Andrew aliikubali kwa kutikisa kichwa chake kisha akamkumbatia dada yake.

"tuondokeni jamani maana muda umeenda na mdogo wangu akibaki hapa atazidi kuumia" Annie aliongea huku akimvuta mkono Andrew kuingia ndani ya gari baada ya kufungua mlango, wote waliingia ndani ya gari kisha wakaondoka eneo hilo.

****

Baada ya kuongea kwa muda mrefu na wapenzi wao, Moses na Hilary iliwabidi waage ili waweze kuondoka kwani Irene alikuwa analala kwa akina Beatrice na wao tu ndio waliokuwa wanarudi makwao.

"girls muda umeenda jamani tunahitaji kuondoka" aliongea Hilary huku akiangalia saa yake ya mkononi.

"Mmmmh yaani shem ungejua huyu mwenzako natamani hata alale hapahapa" Beatrice aliongea huku akiegemea kifua cha Moses.

"He! Hee! Yaani kuanza kupenda ni tabu tupu, si umuachie shem wangu akapumzike kesho mtafutane tu" Irene aliachia kicheko kisha akaongea

"Hey baby mimi ni wako tu usiwe na wasi, nipo kwa ajili yako ingawa muda huu inahitajika niende kwani sina mamlaka ya kukaa na wewe hapa unapoishi chini ya wazazi" Moses aliongea kisha akambusu Beatrice mbele ya Hilary na Irene, alienda kukumbatiana na Irene pia kama ishara ya kuagana. Moses aliingia garini akimwacha Hilary awe dereva wakati wa kurudi huku macho yake yakiwa kwa Beatrice. Ndani ya siku hiyo alijiona ni mtu alipewa kitu cha kipekee ndani ya dunia hii, kupenda kwa mara ya kwanza na kupendwa na anayempenda ndiyo kulimchanganya na kumfanya awe hachoki kumtazama kipenzi cha moyo wake. Hadi Hilary anaondoa gari katika eneo la maegesho kuelekea getini bado alibaki anamtazama Beatrice, walipoliacha geti la nyumba hiyo ndio ukawa mwisho wake wa kumtazama.

****

Asubuhi ya siku iliyofuata ilikuwa ni asubuhi ya ibada kwa wakristo na siku ya furaha kwa watu wote, mapumziko ya siku hii ndiyo yaliyoifanya siku iwe na furaha na watu kupata wasaa wa kupumzika na familia zao. Uzuri wa siku hii ulikuwa mchungu kwa Andrew ambaye alikuwa na kidonda kibichi katika moyo wake, kifungua kinywa siku hiyo kilionekana hakina ladha kutokana na kuumia moyo. Kujifungia chumbani kwake na kulia ndiyo aliona kunafaa kuliko kitu chochote, kujisingizia ugonjwa ndiyo sababu pekee aliyoona inafaa kwa siku hiyo ili aweze kuepuka udadisi wa macho ya wazazi wake. Majira ya saa nne asubuhi Annie aliingia chumbani kwa Andrew akamkuta akiwa na hali hiyo, huruma ilimuingia hata yeye mwenyewe  kiasi cha machozi kukaribia kumtoka kutokana na kumpenda sana mdogo wake. Akiwa amesimama mbele ya kitanda alichokaa Andrew alizidi kumuonea huruma mdogo wake, aliamua kukaa kitandani karibu yake.

"Andrew we ni mwanaume sasa ukilia na mimi nifanyeje" Annie alimwambia.

"dada inauma we acha tu, mtu unayempenda kumwambia mwingine anampenda mbele ya macho yangu" Andrew aliongea huku akifuta machozi.

"mimi mwenyewe naumia pia ila sijalia kama wewe, penzi ni kulipigania sio kulililia Andrew" Annie alimwambia.

"sister kwanza unaumia kivipi maana sijakupata" Andrew aliongea

"kwanza hebu nikuulize...hivi ukilia ndio Beatrice anajileta hapa halafu akwambie anakupenda?" Annie alimuuliza ili kupoteza swali aliloliuliza, Andrew alitikisa kichwa kukataa.

"sasa kama hajileti kulia kuna faida gani mdogo wangu, si ungekuwa unatafuta njia ya kuupata moyo wa Beatrice. Wake up Andrew  kulia ni  udhaifu tosha" Annie alimwambia.

"sasa wewe unataka kuniambia nifanye nini ili niupate moyo wa Beatrice"  Andrew alimuuliza.

"sepatation between Moses and Beatrice ndio chanzo cha furaha yako na furaha yangu pia" Annie aliongea.

"what do you mean unaposema hivyo"  Andrew aliuliza.

"I love Moses and you love Beatrice, their separation ni our happiness" Annie aliongea.
"kwahiyo unapanga plan hiyo kwakuwa unampenda yule mpuuzi" Andrew aliongea akiwa amekunja sura.

"mind your tongue Andrew, you don't know how much  I love that boy(chunga ulimi wako Andrew, hujui kiasi gani nampenda yule mvulana)" Annie aliongea akiwa amebadilika sura yake ikionesha kuchukia kutokana na mdogo wake kumuita Moses mpuuzi. Annie aliendelea kumuambia, "kitendo cha Beatrice kuwa na Moses inanifanya nimchukie sana ingawa nj mdogo wa best yangu, lakini sijamuita mpuuzi kama wewe unavyomuita kipenzi cha moyo wangu".

"ok sister nimekuelewa plan ni ipi sasa" Andrew alishusha pumzi kusha akaongea.

"dirty game on them is our happiness, so lets play(mchezo mchafu ni furaha yetu ,kwahiyo tuucheze)" Annie aliongea huku akinyoosha mkono wake mbele.

"Lets play, but tutaanza vipi?" Andrew aliongea huku akiushika mkono wa dada yake sehemu ya nyuma ya kiganja halafu akauliza.

"usiwe na wasiwasi kuhusu hilo, leo twende Mangrove beach tukapunge hewa maana naona una mawazo sana ingawa umeacha kulia. Nitampigia simu Victoria aje na Beatrice"  Annie aliongea huku akinyanyuka kitandani akijiandaa kuelekea mlango, kauli hiyo ilimfurahisha sana  Andrew na akajiona amepata nafasi nzuri ya kuwa karibu na Beatrice. Huzuni yake aliyokuwa nayo awali ilianza kumuondoka na tabasamu mwanana likaanza kumjia usoni mwake, alitamani hata kumshukuru dada yake mara mia kwa alichomfanyia lakini akaona haitoshi.

"Sister thank you" Andrew alimwambia Annie aliyekuwa yupo akiwa anatoka nje, Annie alipopewa shukrani aligeuka kisha akamtazama Andrew halafu akamwambia, "you are so handsome ukiwa una smile Andrew, ndio maana dada yako nafanya chochote kuhakikisha unakuwa unasmile ili uwe unavutia. Amini tabasamu lako linamvutia yoyote young bro hata Beatrice ingawa moyo wake ndiyo unahitajika uufanye ukuvutie wewe." Annie aliondoka humo ndani akimuacha mdogo wake akiwa na furaha sana. Maneno yake ndiyo yaliyomfanya Andrew ajione ni binadamu miongoni mwa wanadamu, Andrew aliinuka kisha akaenda kufunga mlango halafu akaenda hadi kwenye kioo kikubwa cha kujitazama kilichopo chumbani kwake. Aliamua kujitazama upya kwa mara ya pili huku akijaribu kutabasamu katika kioo hicho, tabasamu lake lilimvutia yeye mwenyewe pia na hapo ndipo akaafikiana na maneno ya dada yake pia.

"Iam so handsome than Moses ingawa kavutika kwa Beatrice, sasa nitahakikisha  ninamvutia na mimi ili niweze kumnyang'anya tonge mdomon" Andrew aliongea peke yake.

****
        
                 MAJIRA YA ALASIRI

         MANGROVE BEACH AND HOTEL
                         MSASANI


Hii ni hoteli iliyopo ufukweni mwa bahari ya hindi katika peninsula iitwayo Msasani, hoteli hii ambayo huchukua watu wanaopumzika ufukweni hapo pamoja na watu ambao wanahiraji huduma za kihoteli. Hoteli hii ni kubwa sana na ni mojawapo kati ya hotel tano zinazomilikiwa na tajiri asiyefahamika kwa raia zaidi ya watu wake wa karibu na uongozi wa juu wa hoteli hizo. Majira ya saa tisa alasiri hoteli hii ilipata wageni wa sehemu mbalimbali na wenye asili mbalimbali, wazungu, wahindi, watu weusi pamoja na wengineo walikuwa wapo katika hoteli hiyo yenye huduma bora. Upande wa ufukweni kulikuwa na watu mbalimbali wakipunga upepo mwanana wa bahari ya hindi, Victoria, Beatrice, Annie na Andrew nao walikuwa wapo kwenye ufukwe huo wakiongea mambo mbalimbali. Annie, Victoria na Andrew walikuwa wapo katika mavazi ya kuogelea na Bearrice alikuwa yupo katika mavazi ya kawaida tu, wote kwa pamoja walikuwa wamekaa kwenye kitambaa kikubwa walichokitandaka jirani na viti viwili vitumikavyo kwa ajili ya kupumzika watu wanaogelea.

"Bite ndiyo umegoma kuogelea sio" Annie aliuliza.

"sitaki kuogelea leo jamani" Beatrice aliongea.

"hapo Mose akija akikwambia mkaogelee je utakataa" Victoria aliuliza swali ambalo kwake aliliona la masihara lakini katika mioyo ya Andrew na Annie lilikuwa ni mwiba mkali ulioingia katikati ya mioyo yao. Swali hilo halikujibiwa na Beatrice zaidi ya kuinama chini kwa aibu na kupelekea Victoria acheke, Annie alitoa tabasamu la uongo ili aonekane amefurahishwa na utani aliuouliza rafiki yake.

"vipi leo anakuja kweli au umenidanganya tu" Victoria aliuliza.

"don't worry he'll be hare" Beatrice alijibu pasipo kutambua kuwa anaupasua moyo wa mtu kwa kisu butu na chenye kutu, Annie naye alijisikia wivu sana aliposikia maneno ya Beatrice kutokana na kumpenda Moses. Nafasi ya kumuambia Victoria aje na Beatrice mahala hapo  ilikuwa ni kuja kumuweka karibu na mdogo wake ikiwezekana autue mzigo wa upendo kwa Beatrice, aliamini kabisa kuwa mdogo wake anaweza kumpindua Moses ndani ya muda mfupi tu akipewa nafasi ya kufanya hivyo. Annie aliamua kumkonyeza Andrew kisha akamuomba Victoria waende kuoga ili nafasi ya kufanya hivyo ipatikane, Victoria pasipo kujua kinachoendelea aliamua kukubaliana na ombi la shoga yake kisha wakaelekea kwenye maji moja kwa moja.

"bahari tulivu kama hii yenye kupendeza ni mahususi kwa ajili ya kuogelea, nashangaa wewe hutaki kuogelea" Andrew alianza kuongea.

"sina mood ya kuogelea leo"  Beatrice aliongea.

"Mood unaweza ukawa nayo ila yahitajika uipe moyo ili uweze kuitekeleza" Andrew aliongea huku akiweka uso wa tabasamu.

"mmh nakwambia  mood sasa naona unabisha" Beatrice aliongea huku akitabasamu.

"siyo kama nabisha nabisha bali maneno yako hayatoki moyoni mwako" Andrew.

"umejuaje?!" Beatrice aliuliza.

"anyway tuachane na hayo, umeona hivi viatu?" Andrew aliongeakisha akauliza  huku akinesha kidole vilipo viatu vya wazi vya Beatrice vilivyopo pembeni mwa eneo walilokaa.

"yeah! Nimeviona" Beatrice alijibu.

"je kikiwa kimoja kina maana gani?" Andrew aliuliza.

"hakina maana vinahitajika viwili ndiyo viwe na maana"  Beatrice alijibu.

"ikiwa kiatu  kikiwa kimoja hakimaanishi chochote ndiyo binadamu hivyo hivyo akiwa peke yake hamaanishi chochote na huitaji mwenzake ili kukaonekana ana maana, binafsi nimekuwa ni mfano wa kiatu na moja ya jozi yangu imekuwa ikitumika sambamba na kiatu tofauti. Beatrice wewe ni kama jozi moja ya kiatu kwangu yaani kama mimi ni wa upande wa kulia basi wewe ni wa kushoto na wewe kama ni wa upande wa kulia basi mimi ni wa kushoto, nilipokuona kwa mara ya kwanza kupitia picha yako kwenye sinu ya dada nilitokea kukupenda na nilishika kiganja cha mkono wako kwa mara ya kwanza jana usiku moyo ulihitaji kuwa nawe. I love you Beatrice and I need you."  Andrew aliamua kueleza hisia zilizopo ndani ya moyo wake kwa Beatrice. Maneno hayo yalimfanya Beatrice ashushe pumzi kisha akamtazama Andrew halafu akamwambia, "remember when eyes are not admire heart does not desire, you are handsome boy but you are not my cup of tea. Moses is my everything in my heart, I love him and I can't be with you(kumbuka macho yasipopendelea basi moyo hautahitaji, wewe ni mvulana mzuri lakini wewe si chaguo langu. Moses ndiyo kila kitu changu katika moyo wangu, ninampenda na siwezi kuwa nawe".  Maneno hayo hayo yalimchoma Andrew na akaamua kujikaza kiume hada alipokumbuka kauli yake aliyomwambia asubuhi.

"penzi ni kulipigania sio kulililia Andrew" Maneno ya dada yake yalimjia kichwani mwake na kumpa ustahimilivu wa kuweza kuhimili maneni ya Beatrice bila kutoa chozi.

"penzi langu kukubaliwa nawe ndiyo tiba ya maradhi yangu kukataliwa nawe ndiyo kuongeza maradhi yangu, naomba unielewe Beatrice nakupenda" Andrew alizidi kubembeleza kwa huruma.

"Andrew ni mara ya pili tunaonana na kwa muda huo wote ningekuwa nimevutika na wewe ningekuwa nimekupa kipaumbele tangu mara ya kwanza tunaonana, but Moses nilimpenda na hata kabla hajanitamkia ananipenda na nilifanya juhudi za kuhakikisha anajua kama nampenda nikafanikiwa na sasa nipo naye. Laiti kama ningekuwa nakupenda wewe ningekuwa kwako na ningeonesha hisia za kukupenda kwako si kwake. Pia utambue mo..". Beatrice aliongea maneno ambayo yalikuwa ni mwiba kwa Andrew, alipotaka kuendelea kuongea alikatishwa na simu yake ya mkononi ilipoita. Jina la mpigaji lilimfanya atabasamu halafu akaipokea.

"My love umefika....upo wapi.....ok nakuja" Beatrice aliongea kisha akakata simu halafu akamgeukia Andrew aliyekuwa kajiinamia halafu akamwambia, "Andrew  bado unavutia wewe ni mzuri  na una uwezo wa kuwa na msichana mrembo zaidi yangu, tafuta anaekupenda na si kung'ang'ania asiyekupenda." Beatrice aliongea maneno hayo ambayo yalimuumiza Andrew kisha akasimama, "dada akija mwambie nimeenda kumfuata Moses". Aliondoka hapo akimuacha Andrew akisindikiza kwa macho hadi alipopotea katika upeo wa macho yake, kooni alijisikia kama kuna kitu kizito kimekwama ambacho kinamuumiza na machoni aliona kama ukungu umeanza kutanda katika macho yake kisha kimiminika kikaanza kuteremka kwenye macho yake taratibu. Aliamua kujifuta kisha akawajiweka katika hali ya kawaida wakati dada yake na Victoria walipokuwa wanarudi mahala hapo, tabasamu lake alilirudisha kama ilivyokuwa awali ili aifiche huzuni yake.

 "Bite yupo wapi?" Victoria aliuliza.

"ameenda kumfuata Moses" Andrew alijibu jibu ambalo lilikuwa linamuumiza moyoni mwake alipolitamka, Annie naye aliishia kubinua mdomo huku akiangalia pembeni.

****

Beatrice alimkuta Moses akiwa ameegemea gari yake ya kifahari aina ya hummer akiwa amevaa mavazi ya kuvutia, siku hiyo Moses alikuwa kavaa fulana inayombana mwili wake ya rangi ya bluu na pensi ya rangi ya bluu huku mguuni akiwa amevaa raba za rangi nyeupe. Mkononi alishikilia miwani ya jua yenye rangi ya bluu kwenye kioo na ufito wa rangi nyeupe, siku hiyo alipendeza sana kuliko hata aluvyowahi kuonekana na Beatrice. Macho ya Beatrice yalipouona muonekano huo yalisababisha hadi mdomo wake uachie tabasamu pana, alimkimbilia Moses halafu akamkumbatia kwa nguvu kjsha akambusu mdomoni mwake.

"umependeza mpenzi" Beatrice alimsifia.

"si zaidi yako my queen, vipi upo na nani huku?" Mosea  aliongea.

"nipo na dada pamoja na Annie na mdogo wake"  Beatrice aliongea akiwa amejilaza kwenye kifua cha Moses.

"mpo upande gani mpenzi?" Moses aliuliza.

"Ufukweni honey"  Beatrice alijibu.

"ok mpenzi twende receiption kisha tuingie swimming pool ya juu ghorofa ya kumi ya hoteli, wenzako utawaita w waje" Mossa aliongea kisha akamshika mkono Beatrice, aliingia hadi mapokezi katika hoteli hiyo ambapo kulikuwa na mhudumu wa kiume.

"floor ya kumi kuna wateja" Moses aliuliza.

"hakuna wateja kwa leo" Mhudumu alijibu.

"ok kwa muda huu hadi saa kumi na mbili nitapahitaji mimi na wenzangu" Moses alimwambi Mhudumu huku akimpa kadi yake ya benki, Mhudumu alipoiangalia kadi hiyo alistuka kidogo kisha akamrudishia Moses kadi yake. Alipotaka kuongea Moses akimkzia sura na kupelekea anyamaze, Moses alimchukua Beatrice hadi kwenye lifti ya ghorofani  halafu wakaingia. Lifti hii iliwapeleka hadi ghorofa ya  kumi kisha ikafunguka milango baada ya kupiga kengele, Moses alitoka huku akiwa amemshika Beatrice kiunoni kisha wakaifuata korido ndefu iliyowapeleka kwenye bwawa la kuogelea  la kisasa. eneo la juu la bwawa hilo lipikuwa wazi huku pembeni kukiwa kuna uzio mnene upande wa mashariki  na pande zilizobaki kulikuwa  ukuta wa ghorofa kuashiria ghorofa bado linaendelea. Sehemu hiyo ya bwawa la kuogelea ilijengwa kwa namna ya kuvutia na inaonekana ni sehemu iliyowazi baada ya kipande cha ghorofa kukatika.

"welcome my queen" Moses alimwambia Beatrice.

"thanks my king, leo nilitaka nisiogelee ila kwa ajili yako mpenzi nitaogelea" Beatrice aliongea kisha akamkumbatia Moses.

****

Sauti ya mlio wa ujumbe mfupi wa maneno ndio ilisikika katika simu ya Victoria, ujumbe huo ulifunguliwa na mwenye simu halafu akusoma, alipomaliza aliwaangalia Annie na Andrew halafu akawaambia "jamani chukueni vitu mnifuate".

"vipi kuna nini?" Annie aliuliza.

"twendeni mtajua huko huko" Victoria alijibu huku akijifunga mtandio kiunoni mwake. Annie na Andrew waliamua kumfuata bila ya kujua chochote na waka wanapoenda. Walienda hadi ndani ya hoteli kisha wakaingia kwenye lifti iliyowapeleka hadi ghorofa ya kumi, walipofika hapo walipokelewa na mhudumu aliyevalia sare maalumu ambaye aliwaongoza hadi sehemu ambayo waliyokuwa wanaenda. Mwisho wa safari hiyo ilikuwa kwenye bwawa la kuogelea ambapo walimkuta Moses na Beatrice wamevaa mavazi ya kuogelea, wapendanao hawa walikuwa wamelala kwenye kiti kimoja cha kupumzika jirani na bwawa la kuogelea.

"karibuni" Moses aliwakaribisha

ITAENDELEA

No comments:

Post a Comment