Friday, June 24, 2016

SHUJAA SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

RIWAYA: SHUJAA


MTUNZI: Hassan O Mambosasa

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA!!

"He! Kulikoni mbona unasonya hivyo hadi humu ndani tunakusikia?" Mama Andrew alimuuliza Annie baada tu ya kuingia humo ndani na kumfanya Annie ashtuke ingawa hakuonesha kama kashtuka.
"mama huyo mwanao mimi dada yake ananigeza bibi yake kwa jinsi anavyonitania" Annie alilalamika kwa maigizo na kumfanya mama yake acheke.

"si mnataniana wenyewe wala sihusiki maana na wewe unamgeza babu yako mkiwa nyumbani" Mama Andrew akiongea huku akicheka.
"shoga wanao wanapendana sana inaonekana hadi wanataniana hivyo?" Mama Beatrice alimuuliza Mama Andrew
"yaani shoga hawa wanapendana sana hadi nikiwaona wanataniana na kucheka huwa nafurahi sana" Mama Andrew alijibu huku akitabasamu na Annie naye akatabasamu

****

Hakika ya waswahili walinena usilolijua ni usiku wa kiza, usemi huo hawakukosea kuutunga kwani ulikuwa na maana kubwa sana katika maisha ya kila siku. Mtazamo wa mama Andrew juu ya maelewano ya wanae ulikuwa ni tofauti kabisa na hali halisi ya maelewano yao yalivyo, kiupande wake aliona maelewano ya wanae ni nuru kumbe yalikuwa ni giza totoro zaidi hata ya giza linaugubika msitu wenye  miti mingi baada ya mwangaza kuondoka. Alikuwa akihesabu namba ni tisa kwa jinsi anavyoiona kumbe ni sita kwa jinsi inavyoonekana, hakika hakutambua uhasama uliopo katika mioyo ya watoto wake na laiti angelitambua angeweza kuwa na hali mbaya kutokana na msongo mawazo.
"ni furaha kubwa sana kuwa na watoto wanaopendana kama watoto wako na wangu" Mama Beatrice alimuambia mama Andrew.
"hakika shoga maana ni furaha sana hasa ukiwaona wakiwa pamoja wanafuraha kama walivyo wanangu" Mama Andrew aliafiki maneno ya Mama Beatrice akitolea mfano zimwe wa mahusiano ya watoto wake pasipo kujua kilichopo upande wa pili wa mahusiano hayo, muda wote huo Mama Andrew akijisifu juu ya mahusiano ya watoto wake Annie alikuwa anatabasamu kinafiki ili ijulikane ni kweli.
"Hata mimi napenda sana nikiona wanangu jinsi wanavyopendana na kuwa pamoja ila ukosekanaji wa mmojawapo naumia sana, Vicky wangu sijui kawakosea nini mpaka wamfanyie hivyo" Mama Beatrice aliongea kisha akaanza kulia tena.
"Shoga usilie atapatikana" Mama Andrew alianza kumfariji Mama Beatrice huku akimkumbatia , Annie naye aliungana na mama yake katika kumbembeleza Mama Beatrice huku akiwa na mazito moyoni mwake aliyoyahimili mwenyewe.
"Kiherehere cha mwanao tu kupenda vinavyopendwa ndiyo kumeleta haya yote" Annie alijisemea huku akimbembeleza Mama Beatrice.

****

UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU NYERERE

DAR ES SALAAM

Wakati Mama Beatrice akibembelezwa na Mama Annie upande mwingine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere kijana mwenye  suti nyeusi na kofia aina ya Fedora yenye rangi nyeupe na utepe mweusi alikuwa yupo karibu kabisa na eneo ambalo wageni wanaowasili ndiyo huonekana, kijana huyo alikuwa amekaa kiutulivu sana hadi pale muda wa wageni kutoka ndiyo aliinuka akawa anaangaza kwenye eneo ambalo wageni wanaonekana. Kundi kubwa la watu waliowasili hapo uwanja wa ndege lilianza kuonekana likitoka na ikambidi kijana huyo asogee awe makini sana katika kutazama wageni hao hadi alipomuona msichana mrembo na mrefu aliyevaa suruali ndefu nyeusi iliyomkaa kisawasawa kiasi cha kuonesha umbo lake akitoka akiwa amebeba mkoba tu wa mkononi tu. Msichana huyo alivaa blauz nyeusi juu na koti jekundu la kike la suti lililomkaa vyema, usoni alikuwa amevaa miwani ya jua ya kisasa na miguuni alikuwa amevaa viatu virefu ambavyo alivimudu vyema.
Kijana huyo alipomuona huyo msichana mrembo alimfuata taratibu hadi alipotoka nje kabisa katika eneo lenye teksi, msichana huyo alipotaka kuita teksi kijana huyo alimshika mkono kisha akamuambia, "vizuri kwa kuja tuondoke. Sauti ya huyo kijana ilitambulika vyema na msichana huyo  ambaye alimtazama tu kisha akamuuliza, "Nor vipi mbona hivyo?"
"Hil hebu acha maswali twende kwenye gari tuondoke hapa" Yule kijana alimuambia yule msichana huku akianza kuelekea upande wenye magari binafsi mengi yaliyoegeshwa hapo uwanjani. Msichana naye bila hiyana alimfuata hadi kwenye gari aina ya Suzuki escudo ya rangi nyekundu akaingia upande wa pili baada ya kijana huyo kufungua milango. Baada tu ya kuingia kwenye gari yule kijana alitoa kofia yake aliyovaa na sura yake ikaonekana dhahiri, hakuwa mwingine ila ni Norbert Kaila mpelelezi wa siri wa shirika la upelelezi la Afrika ya mashariki(EASA).
"sikiliza Hilda ni hivi mambo yamefikia pazuri penye ugumu nitakueleza yote tukifika" Norbert aliongea kumuambia yule msichana ambaye ni Hilda Alphonce mpelelezi wa siri wa shirika la upelelezi la  Afrika ya mashariki (EASA) akitokea Rwanda.
"Ok tuondoke hapa basi" Hilda alisema huku akifunga mkanda wa kiti alichokuwa amekaa, Norbert aliwasha gari akaliondoa kwenye maegesho ya uwanjani hapo taratibu.
"halafu kuna kingine nimekisahau kukuambia" Norbert aliongea huku akitabasamu akiwa ameshika usukani w gari macho yake yakiwa makini kuangalia mbele.
"kipi hicho?" Hilda aliuliza huku akimtazama Norbert.
"leo bora umekuja tu nizimue damu maana ilikuwa imepooza" Norbert aliongea huku akimtazama Hilda kwa jicho la kuibia asiweze kupoteza umakini barabarani.
"Loh! Lione unawaza jimai tu kila muda, mwanaume wewe kama jogoo" Hilda aliongea huku akimsukuma Norbert na kidole cha shahada.
"kazi na dawa ndiyo mpango bibie" Norbert aliongea huku akimtazama Hilda kwa tabasamu ambalo huwa ugonjwa mkubwa kwa kina dada.
"hebu endesha huko usije ukagonga" Hilda alingea huku akimshika kidevu Norbert akiuelekeza uso wa Norbert mbele.
Baada ya dakika takribani ishirini tayari Norbert na Hilda walikuwa wamefika Temeke mahali anapoishi Norbert, waliposhuka ndani ya gari ndipo Norbert alipoanza uchokozi katika mwili wa Hilda kutokana na kumtambua vyema huyo binti hasa udhaifu wake. Norbert alizungusha ulimi katika shingo ya Hilda na kupelekea binti huyo wa kitusi ajihisi kama amegusa waya wa umeme usio na magamba.
"Nor bwana, hebu twende ndani" Hilda aliongea kwa sauti dhaifu akionekana kuishiwa nguvu kabisa kwa mambo anayofanyiwa na Norbert, wote kwa pamoja  waliingia ndani na wakaelekea hadi chumbani. Ukaribisho wa aina yake ulifanywa na wote wawili ambapo mgeni alimkaribisha mwenyeji kwa mapokezi ya kipekee na tofauti na wageni wengine wanavyokaribishwa pindi wafikapo nyumbani kwa wenyeji wao. Kama ni kinywaji hichi alichopewa mgeni huyu kilikuwa ni cha kipekee hakikutuliza kooo na kama ni chakula basi nacho kilikuwa cha pekee ambacho hakikumshibisha mgeni ingawa kilipendelewa sana na huyu mgeni.

****

Wakati Norbert akimkaribisha mgeni wake nyumbani kwake kwa namna tofauti na wageni wengine wanavyokaribishwa, upande mwingine tena mbali kabisa na nyumbani kwa Norbert kulikuwa na sekeseke ndogo iliyokuwa ikikaribia kutokea lakini ugeni wa waanzishaji wa sekeseke hiyo ndiyo chanzo cha kufa kwa sekeseke hiyo kistarabu.
Baada ya Moses kukaa kwa muda mfupi bustanini akiwa nampenzi wake pamoja na marafiki zake, haja ndogo ilimbana na ikamlazimu kwenda chooni ili kuondoa adhaa ya iliyokuwa inamsumbua kwenye kibofu chake.
"Jamani nina short call ngoja niingie ofisi muhimu mara moja" Moses aliwaambia wenzake kisha akambusu Beatrice shavuni akamwambia "I'll be back my queen".
"okay my king" Beatrice alijibu huku akitabasamu, Moses alitoka akaelekea kwenye maliwato za nje zilizopo nyuma ya nyumba hiyo ili akakidhi haja ya kuondoa taka mwili iliyokuwa ikimpa usumbufu sana, aliingia ndani akakidhi haja zake kisha akatoka akawa anataka kurejea alipomuacha mpenzi wake lakini akajikuta akivutwa nguo aliyovaa kwa nyuma na ikamlazimu kusimama na alipogeuka nyuma alikutana na Annie akiwa anatabasamu.
"finally nimekupata" Annie aliongea kwa madaha huku akijisogeza karibu na Moses kisha akaweka mikono shingoni kwa Moses lakini iliwahiwa kutolewa.
"Hivi unataka nini wewe?" Moses aliuluza akionekana kukerwa kabisa na mambo ya Annie anayomfanyia.
"nakutaka wewe hapo na si kingine, nakupenda Moses" Annie aliongea huku akijisogeza karibu na Moses na akataka kumbusu bila ridhaa yake, Moses alimsukuma Annie kisha akaangalia  pande zote asije akawa anaonekana. Bahati nzuri maliwato hizo zilikuwa zipo eneo ambalo si rahisi kuonekana na mtu katika nyumba hiyo, alipoona hajaonekana alirudisha  uso wake eneo alipo Annie akionekana kukerwa kabisa na tabia yake.
"Jibu ni lile sikupendi na sikuhitaji umri wako wewe kwangu ni dada yangu hivyo niheshimu kama mdogo wako" Moses aliongea kwa utaratibu akuzuia jazba isimpande.
"laiti ningekuwa dada yako nisingethubutu kukupatia huu mwili ukautumia Moses" Annie aliongea.
"kwanza umenifanyisha mapenzi kilazima pili na unataka kuwa na mimi sahau hilo kabisa, si kila anayeonjeshwa karanga ni mnunuaji wengine hujikuta tu. Sasa kama ulitegemea ulivyonifanyisha mapenzi kilazima nitanogewa sahau hilo kabisa, Beatrice ndiyo kila kitu kwangu nampenda hata kama ikiwa hivyo" Moses aliongea huku akimtazama Annie kwa dharau.
"Fine jiandae zile picha namtumia kwa Whatsapp tuone nani mjanja" Annie aliongea kwa hasira.
"na wewe jiandae ile blog yenye video yako naipublish tuone mjanja, moyo huu ni wa Beatrice tu na si vinginevyo" Moses naye alimjibu kwa hasira.
"Fanya ujinga mimi nifanye upumbavu, huyo malaya wako atazidi kulia zaidi ya pale nakua..." Annie alishindwa kumalizia kauli kauli yake baada ya kibao kikali kutua kwenye shavu lake kutoka kwa Moses.
"Tena ukirudia kumuita Beatrice malaya nitakufanyia kitu kibaya  sitoogopa huo mguu wa kuku unaotembea nao" Moses aliongea kwa sauti ya chini yenye hasira.
"Mosea unanipiga?!" Annie aliongea kwa mshangao.
"Aaah! Nimekupapasa tu" Moses alimuambia kwa dharau kisha akaanza kuondoka taratibu.
"maumivu niliyoyapata mimi kuna mwingine tutashare naye" Annie alimuambia Moses ambaye hakumsikiliza aliendelea kuondoka.
    Moses alipoamuacha Annie alipitia kibarazani ili aelekee bustanini alipowaacha wenzake, alipokaribia sehemu ya mbele ya nyumba ya akina Beatrice alikutana uso kwa uso na Andrew aliyeonekana alikuwa anamngoja kwa hamu. Andrew alikuwa ameifumbata mikono yake kifuani na Moses alipomkaribia alitabasamu kwa dharau akamuambia, "vita haijaisha Moses".
"Kwahiyo?" Moses alimuuliza kwa dharau.
"hii alama hapa jichoni mwangu inanikumbusha hasira zangu nilizonazo juu yako, ulinipiga ngumi siku ile pale kwenu mbele ya vijana wangu. Sasa napenda nikuambie hivi game is on na itakuwa off mpaka Beatrice awe wa kwangu" Andrew aliongea huku akitabasamu kama vile alikuwa anaongelea jambo la furaha.
"Beatrice hawezi kuwa wako na sahau kabisa kuhusu hilo, cha kukusaidia ni kukuambia mapenzi hayalazimishwi niachie mpenzi wangu fuata yako na ukitaka vita utajiumiza tu" Moses aliongea kisha akampiga kikumbo Andrew akaondoka akimuacha na hasira zake hadi akafikia kutaka  kuchomoa silaha yake kiunoni lakini alijikuta anashindwa baada ya mkono wake kudakwa kwa nguvu na mtu ambaye alikuwa nyuma yake. Alipogeuka alikutana na dada yake akiwa anamtazama kwa hasira, Andrew naye alipomuona ndiyo hasira zilizidi.
"fanya ujinga nikafanye upumbavu" Annie alimuambia kisha akamsonya akaondoka.
"hutamlinda kila muda" Andrew alimuambia Annie kwa hasira kwa sauti ya chini aliyoisikia, Annie alisimama akamtazama juu hadi chini mdogo wake halafu akamsonya kwa nguvu.
"asiyekupenda unamlinda?" Annie alimuuliza kisha akaondoka akisonya tena

****

   TEMEKE
 BAADA YA MASAA MAWILI


Baada ya ukaribisho wa namna yake aliofanyiwa Hilda na mwenyeji wake wote kwa pamoja walikwenda kuoga kisha wakakaa sebuleni kwa namna ambayo haihitaji elimu ya ziada kutambua kama ni wapenzi kwani kwani mkao waliyokaa inatosha kuwajua kama wao ni wapenzi. Ingawa ni wafanyakazi wa shirika moja lakini tangu wapangiwe kazi moja ya kupeleleza juu ya kupeleleza upotevu wa tani saba za dhahabu zilizoibiwa bandari ya Mombasa nchini Kenya ambapo waliingia kama waandishi wa habari katika mji wa Mombasa. Ilipomalizika kazo waliyopangiwa waljikuta kwa mara ya kwanza wakivunja amri ya sita kati ya amri kumi za Mungu kwa imani ya kikristo na dhambi yenye kutetemesha arshi ya Mungu muweza. Kuanzia hapo wakawa ni wapenzi wasio rasmi kutokana na kazi yao na maadili yake.
"Nor halafu hujanieleza sababu iliyokufanya uje airport kwa kujificha" Hilda alimuambia Norbert huku akimlalia kifuani.
"Yaliyonipata ni makubwa Hil yaani nilifanikiwa kumjua Brown Stockman ila wakati naendelea na upelelezi wangu nikajikuta nimenaswa katika himaya yake Bunju nikazimishwa. Nimekuja kuamka nimejikuta nipo katika himaya yake nyingine iliyopo katikati ya msitu wa Sao hill Iringa, kutoka mpaka nikafika huku Dar ni baada ya mbinu za kuniokoa nilizozitumia nikapora pikipiki" Norbert alieleza yaliyomkuta kisha akaendelea, "sasa habari ya kuja kwako niliipata kupitia ujumbe mfupi ulioingia kwenye saa yangu kutoka branch ya Rwanda, hivyo nilitaka nikupokee na sikutaka wale watu wajue kama mimi nipo mjini maana mtandao wao ni mkubwa".
"Hata mimi huyo mtu nimekutana naye kwenye ATM ya benki ya Barclays tawi la kigali akitumia ile kadi ya ATM yake tunayoijua, nimemfuma nikacheza naye  ndombolo ya solo akakimbia" Hilda akamuelezea Norbert.
"wacha wee ndombolo ya solo na mauno umempatia" Norbert alianza kumtania Hilda na kupelekea Hilda amtazame huku kanuna.
"halafu Nor unanitania too much, sasa hivi utani tuweke kando yule mtu ni hatari sana yaani tukileta mzaha hatumpati na kazi yetu hii isiyo na ratiba itaharibika nakuambia" Hilda alimuambia Norbert huku akijitoa kifuani mwake na kuketi pembeni.
"kama nilivyokuambia tumefikia pazuri penye ugumu na ni kweli, Brown amefanya plastic surgery hivyo ana sura ya bandia kwa sasa anajiita Brian Mcdonald mfanyabiashara mashuhuri Afrika  mashariki hii tena inaonekana anavaa invicible gloves zenye alama nyingine za mikono hivyo ametengeza hati ya kusafiria nyingine. Tushamjua ni yupi ila ugumu upo kwenye kumkamata tu huyu mtu inabidi tukune kichwa haswa" Norbert aliongea kumueleza Hilda mahali alipofikia katika kazi yake.
"vizuri, sasa basi inabidi tufanye kazi hiyo kwa pamoja kama makao  makuu walivyoamuru, uzito wake ushaonekana ndiyo maana nguvu ikaongezwa. Sasa basi inabidi tumalize kazi ambayo waliishindwa M16 wa Uingereza, KGB wa Urusi na FBI ya Marekani katika kumtia nguvuni nadhani file na rekodi za ulipofikia unazo, tuanze kazi mapenzi tuweke pembeni" Hilda alisisitiza.
"twende downroom ukaone kila kitu" Norbert alimuambia Hilda  huku akimshika mkono wakafuata ukumbi mrefu wa nyumba hiyo uliowapeleka hadi kwenye mlango ambao waliufungua wakaingia kwenye chumba chenye vitu visivyotumika maarufu kama stoo. Ndani ya chumba hicho Norbert alifungua mlango wa kabati moja la nguo ambapo ndani kulikuwa na mlango mwingine, aliufungua huo mlango pia ngazi zenye kuingia chini ya ardhi zilionekana. Alitangulia kuingia na Hilda akafuata kwa nyuma, taa za humo ndani zilijiwasha zenyewe na ngazi zikawa zinaonekana vyema, wote walishuka hadi sehemu yenye meza na kabati kubwa sana.
"Karibu downroom yangu" Norbert alimkaribisha Hilda sehemu hiyo halafu akaendelea "kila kitu kipo humu tutakachokitumia kwa ajili ya kazi kuanzia mafile hadi vitendea kazi vyote".
"Nashukuru sana, naweza kuona mafaili ya uchunguzi wa awali?" Hilda aliongea.
"bila shaka inawezekana" Norbert alisema kisha akabonyeza kitufe kilichopo mezani meza ikafunguka, alitoa faili moja lililotuna akampatia Hilda huku akimuambia "kila kitu kipo humo ndani".
Hilda alilipokea faili akalifungua akaanza kulisoma kidogo halafu akasema, "nahitaji muda wa kutosha wa kulipitia hili ili kazi ianze mara moja".
"Hamna shida nenda nalo juu upitie kila kitu halafu tupange tutaanzia wapi" Norbert alisema huku akitoka na Hilda akawa nyuma yake mkononi ana faili.

****

Baada ya chakula cha pamoja baadhi ya marafiki wa Beatrice waliondoka nyumbani kwao wakawaacha Moses, Hilary na Irene wakiwa na Beatrice ambapo nao ilipokaribia alasiri waliondoka waliondoka wakimuacha Beatrice akiwa mpweke na walimuahidi kumtembelea  mara  kwa mara. Muda mfupi baadaye Mama Andrew na wanae waliondoka nyumbani kwa mzee Bernard wakamuacha Beatrice na mama yake wakiwa na wafanyakazi wao pekee tu. Upweke ulirudi kama awali ndani ya nyumba hiyo.
Annie baada ya kutoka hapo nyumbani kwa mzee Bernard Mutashobya aliagana na mama yake  alienda moja kwa moja hadi ilipo maskani ya vijana wake ambapo ndiyo mahali alipomfunga Victoria, alipofika ndani ya eneo hilo vijana wake walimfungulia kwa heshima na utiifu.
"yule fisi kala?" Annie aliwauliza vijana wake.
"hapana Madam, tumempa chakula hataki kabisa" Mmoja wa vijana wake alisema.
"khaa! Nyie endeleeni na kazi huyo niachieni mimi" Annie alisema kisha akaingia ndani ya nyumba iliyopo ndani ya jengo hilo ambalo ndiyo amemfungia Viktoria, alipoingia ndani ya jengo hilo alipokelewa na sauti ya Viktoria akilalamika afunguliwe. Sauti hiyo ndiyo ilimzidisha hasira akaenda hadi kwenye alichomfungia Viktoria ambacho hakina tofauti na chumba cha anacholala nyumbani kwao, alipofungua tu na kuingia ndani ya chumba hicho alifunga mlango kisha akaanza kumpa kipigo Viktoria hadi alipochoka akabaki anamtazama kwa hasira.
"Annie rafiki yangu nimekukosea nini mimi?" Viktoria aliuliza huku akilia kwa uchungu.
"hujanikosea kitu ila mdogo wako kapenda nilipopenda ndiyo kosa lake linalokufanya uteseke, pia tabia ya kupiga makelele humu haitakiwi na nikisikia unagoma kula nakata pua hiyo. Chukua chakula na ule upesi sasa hivi" Annie aliongea kwa ukali na Viktoria akasogea hadi kwenye meza iliyopo humo chumbani akachukua chakula akaanza kula.
"nilimuahidi Moses maumivu ya kibao alichonipiga nitashare na mtu mwingine ndiyo maana nimekupa kipigo wewe, tena mdogo wako asipomuacha Mosea nitakuua halafu nitamteka mama yako pia nitamuua. Sitaki nimteke yeye sababu nitamkosa Moses moja kwa moja" Annie aliongea kwa hasira sana.
 
*kazi ipo



ITAENDELEA




MWENYE KUIHITAJI RIWAYA HII HADI MWISHO ANAWEZA KUWASILIANA NA MTUNZI KUPITIA NAMBA ZAKE HAPO JUU KWA NJIA YA UJUMBE MFUPI TU WA MANENO NA SI KUPIGA. HUKO UTAIPATA YOTE.



KWA RIWAYA ZAIDI LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK AMBAO NI:




      Riwaya Maridhawa
       Riwaya Maridhawa
      Riwaya Maridhawa
       Riwaya Maridhawa
        Riwaya Maridhawa

No comments:

Post a Comment