Thursday, February 1, 2018

TENDAGURU SEHEMU YA SITA


RIWAYA: TENDAGURU
NA: HASSAN O MAMBOSASA
MAHALI: TANZANIA NA MAREKANI



<><><>SEHEMU YA  SITA<><><>


     Aliwasili langoni ambapo kuna walinzi waliyokuwa na kifaa maalum cha kukagua, hapo walimkagua  kuhakikisha hakuwa na hatari yeyote ile. afisa kutokana na ukaguzi wa hapa aliamua kuacha silaha yake garini, hivyo anajitosa mikono mitupu.




_____________TIRIRIKA NAYO
    Walinzi maalum waliyovalia sare za rangi nyeusi ambazo zina muundo wa sare za kijeshi, waliziba njia ya kuingilia lango pale tu alipolikaribia. Mmoja alibebea kifaa cha kukagulia huku mwingine akijiandaa kupeleka mkono kiunoni ikiwa kutatokea lolote lile, haya yote aliyaona lakini hakuonesha kuyajali zaidi ya kupiga hatua zake kuwasogelea gadi hao. Alipofika usawa wa yule aliyeshika kifaa cha kukagulia alinyoosha mikono na kuweka umbile la msalaba, alitoa wasaa mzuri kwa Mlindaji huyo kuweza kufanya wajibu wake.

       Kifaa  maalum chenye kunasa vitu vyenye asili ya chuma na asili ya madini mengine yanayokaribiana na chuma,kilipitishwa mwilini mwake kwa mwendo wa taratibu. Alitulia vivyo hivyo pasipo kuleta tukio lolote, hadi anamaliza hakikutoa mlio wa aina yeyote ule kama kulikuwa na hatari mwilini mwake. Alijulikana wazi ni mwenye usalama na hakukuwa nalengo lingine la kumzuia hapo, kwani  ukumbi huu haukuwa unabagua wateja zaidi ya kuwaruhusu baada ya kulipa gharama zao.

      Alivuka kikwazo hicho ambapo alikutana na kikwazo kingine kilichopo jirani na mlango tu kwa ndani, hichi hakikuwa kikiwepeka kwani alichangia haswa mapato ya kiserikali kupitia hapa ingawa anatambua wazi humo ndani kunafanyika ufuska. Ni katika ukumbi ambao haukuwahi kufungiwa hata siku kutokana na kiasi kikubwa cha pesa ambacho serikali kinapata kupitia kodi, kuwepo kwa tabia zisizofaaa kulibaki tu uvumi jambo ambalo lilikanwa kutokuwepo uhakika wake. Inspetka Mtela alijikuta akitumia pesa nyingi kwenye ofisi ndogo ya kulipia kisha akapewa kadi malum, alipatiwa pia pamoja na risiti yake ya malipo aliyoyafanya. Hii aliitupia macho kwa sekunde kadhaa baada ya kuishuhudia inatoka ndani ya mashine ambayo huunganisha wenye miradi na mamlaka ya mapato, alitikisa kichwa baada ya kupokea kisha akajongea kuufuata mlango wa pili ambao ungemuingiza kabisa eneo lililopo klabu hiyo.

      Kwa mara ya kwanza maishani mwake alijikuta akiingia kwenye eneo ambalo limesheheni uhuni wa kila aina, kusipo na staha hadi kudhaniwa hakukuwa ndani ya nchi hii. Mwangaza hafifu uliyomoo humo ndani ambao ulipambwa zaidi ya muziki mzito. Haukumzuia kuweza kuona jinsi wasichana wadogo walivovaa nusu utupu wakicheza kwenye majukwaa huku wakitunzwa pesa. Wengi wa wanaume  walionekana kushangilia kwa kitendo hicho, upande mwingine aliona  wanaume wakiwa wapo baoni wakicheza nao huku wanawake wenye umri mkubwa wengi wakiwa wanawashngilia hasa pale walipotoa vizuizi vya miili yao.

       Alitikisa kichwa kwa kuliona hilo na ikambidi ageuka upande mwingine ambao kulikuwa na makochi pamoja na meza ndogo yenye vinywaji, hapo ndipo nusura abaki mdomo wazi kwa kile alichojionea. Hakutegemea kabisa kama anejionea kitu kama hicho, alijizuia tu asioneshe kuwa hayo ni mageni kwake kuepusha kutiliwa shaka na watu. Hapo aliwaona wanaume kwa wanawake wakiwa wamepeana nafasi huku wakimaliza haja zao bila ya  chembe ya haya kwenye nyuso zao, hakika kulijaa laana humu ambazo hakuwahi kuziona walau siku moja na hiyo mara ya kwanza anazitia machoni.

      Aliwapita hao na akaona eneo ambalo kuna mlango wenye pazia la kutengenezwa na mbao ndogo mno pamoja na kamba, kwenye sitiri hiyo ndipo aliona ile alama aliyokuwa akiisaka kwa udi na uvumba. Hii ilimfanya hata asiwe na  lengo la kutazama wale wenye laana ambao wapo kwenye kukufuru yule aliyewaumba, alipiga hatua huku akipishana na watu mbalimbali. Hii ilimfanya apigane vikumbo na baadhi ya watu hadi anafika mlangoni hapo, alishusha pumzi na akaingia ndani kwa kusogeza pazia lile, huku alikutana   mambo tofauti yaliyokuwa yakifanyika kule. Kitendo cha kuingia aliona kundi kubwa la watu wakiwa wamezunguka meza moja wakicheza kamari, alipozidi kuzungusha mboni  zake za macho alifanikiwa kuona mengi zaidi ya hayo. Upande mwingine aliona mashine kadhaa  za kuchezesha kamari zikiwa zimekaliwa na watu, alipozidi kukipa wajibu kifaa chake cha maoneo. Aliona meza kubwa ambayo nyuma yake kuna na kabati kabati kubwa lenye vileo pamoja na majokofu, mbele za meza hiyo  kuliwekwa viti virefu na baadhi ya viti hivyo vilishapata wakaliaji waliyokuwa wakipata vinywaji..

        Inspekata Mtela alijongea hadi kwenye meza hiyo kisha akaketi kwenye kiti, alitupa macho kwenye kabati lile huenda kuna kinywaji kilaini angeweza kukitumia kuweza kuzuga hapo lakini hakuona cha namna hiyo. Vyote vilivyokuwa vipo machoni mwake ni pombe kali ambazo zilitofautiana kiwango tu na za hali ya chini zikiwa ni bia za nchini Tanzania ambazo ni gharama za chini kuliko bia zote zinazotoka Wilayani Ilala na Temeke. Mwanamzalendo huyu alijikuta akiagiza bia ya kilimanjaro hakuwa  mtumiaji kabisa wa bia, tena hakuwa na lengo la kuinywa hata kidogo. Nia yake ni kuzuga nayo wakati akizungusha macho kutazama mandhari aliyopo huenda angeweza kubaini lolote lile, aliwekea kinywaji chake mezani ambacho hakuhitajika kulipa baada ya kufanya malipo yote kule mlangoni. Yeye  alichukua kadi ile aliyokabidhiwa ambayo anayo mkononi  na kuipitisha kwenye mashine kisha akaweka namba za siri  alizoambiwa pale mlangoni.

       Aliwekewa hadi bilauri ambayo aliitumia kumimina kinywaji hicho kisha akakitolea macho kwa sekunde kadhaa, alipokea ukaribisho kutokwa kwa binti aliyefanya kazi hiyo ambaye ndiye mwenye jukumu la kuhudumia wateja. Yeye alimpa tabasamua tu na hakunyanyua mdomo wake. Akiendelea kuzuga hapo na bilauri yake aliweza kuona mengi yanayotendeka humo, ilipita dakika kadhaa akiwa hajatia mdomo kwenye kinywaji kile hadi yule Mhudumu akaanza kumshangaa. Hili lilimfanya atie mdomo kwenye bilauri yake kwa mara ya kwanza, alikutana na ladha ambayo hakuwa akiipenda hata kidogo ila alijikaza tu kisabuni asiweze kujulikana kuwa hakikumpendeza.

         Robo saa baadaye eneo hilo aliingia Mzungu aliyevalia suti akiwa ameongozana na  vijana wanne wa kiafrika, huyu alijongea hadi kati ya eneo hilo. Kufika kwake hapo kulifanya eneo ambalo mwanzo kulikuwa na mlango uliyokuwa umefunikwa na pazia, kuonekane vioo vikichomoza kwa pembeni za kuziba hapo. Muziki ule mnene uliyotoka ukumbi mkubwa haukusikika tena zaidi ya kusikika minong'ono ya watu wakicheza kamari pamoja na kunywa, Mtu yule mwenye ngozi nyeupe alisogea na wale watu hadi eneo ambalo kulikuwa na meza kisha akapanda juu. Alipiga makofi mara mbili kwa nguvu na ukimya ulifuata kwenye eneo hilo, baada yahapo alishuka chini alipopata umakini wa watu juu yake.

 "Nikifika mimi huwa kuna jambo tu na pia dharura kama ilivyo hivi sasa, huwa sijitokezi mara kwa mara nafikiri wazoefu wa hapa wanajua. Eneo hili ni sawa na kichuguu hivyo kuna ulinzi wa nje pamoja na ulinzi wa ndani, ulinzi wa ndani wote unaongozwa na mimi na nikijitokeza basi kuna jambo ambalo si la kawaida kabisa" Mzungu huyo aliongea kwa kiswahili fasaha kabisa.

"Ndiyo maana nipo hapa kukiwa na wanachama watupu na pia kuna mwanachama mgeni ndani yake" Aliposema  hivyo aligeuza macho kule alipo Inspekta Mtela akiwa yupo na bilauri yake mkononi.

"Ni yule pale na ndiye aliyetufanya tufike hapa, sijui anaweza kutumbia wallet yake ipo wapi?" Mzungu alisema hukua akitazama Mwanausalama aliyeingia humo ndani kwa lengo la kupeleleza.

        Afisa huyu wa polisi aliweka tabasamua na kisha kapleleka mkono mfuko wa nyuma huku akijiinua kidogo, aliingiza huko akiwa na lengo la kuikuta pochi yake. Loh!  Haikuwepo na badala  yake alikuta kipande cha karatasi gumu ambacho kimekunjwa mithili ya pochi, hichi kilionekana dhahiri baada ya yeye kukitoa nje akijiamini ana kile ambacho walikihitaji wale. Salalleh! Hapo ndiyo moyo wake ulipopiga sarakasi ingawa sura yake ilitulia violevile kama hakuwa ameona cha ajabu chochote, wote walimtazama yeye na hapo ndipo yule Mzungu alipoingiza mkono kwenye mfuko wa koti la suti. Alitoka na pochi ya rangi ya  kahawia kisha akaionesha juu, akiwa bado ana mchanuo usoni mwake aliifungua kisha akatoa kitambulisho kilichomo ndani yake akakionesha hadharani.

"Mmeonaa! Ni Askari huyu tena Askari mpelelezi" Kauli hiyo ilipotlewa wale watu weusi waliyoingia sambamba naye walitoa bastola na kumuelekezea kwa haraka.


       Hili Inspekta ililimfanya azungushe macho kwa haraka kutazama kila pande na kisha akashikilia shingo ya chupa ya bia    kwa nguvu, alishajiwa na kitu kingine cha kufanya baada ya kuzungusha mboni zake. Ndiyo maana alishikilia chupa kwa uimara, kabla hatimiza wazo hilo alihizi kitu kikigusa sehemu yake ya kisogoni. Hajatulia sawa alihisi  mlio wa bunduki wa aina ya Shotgun kukokiwa. Mwenye kushika  silaha hiyo alitokea upande ule ambao yupo Mhudumu wa kike aliyekuwa akifanya kazi ya kuhudumia watu, bado hakutaka kushindwa namna hiyo alijaribu kujisogeza kando kidogo lakini bunduki ile ilikandamizwa zaidi kumuusia asifanye ujanja.

"Tulia kama ulivyo, eneo hili huwa hawafiki Polisi daima sasa utatuleza kwanini ulifika hapa" Suati ya Mhudumu  wa kike yule aliyempa kinywaji ndiyo aliisikika, hakika aliwezwa haswa kwa kuwekwa kati.

"Daima sura ngeni ikiingia humu ndani ni lazima ipekuliwe kijanja bila ya yeye kujua, ndiyo maana tukawaweka wataalamu wa kuiba poshi za watu hapo ndani na ndiyo walifanya kazi hiyo. Afisa  ingekuwa ni mtu mzuri kwetu basi ungerudishiwa kila kitu chako lakini kwa kuwa wewe ni mbaya kwetu, so sorry umejileta mwenyewe  pabaya. Mkamateni" Mzungu alipomaliza kutoa kauli zake na kuweka amri, Inspekta Mtela alikamatwa kwa haraka sana kisha akashikiliwa kinguvu huku akiongezwa na silaha sehemu ya paji lake la uso. Aliondolewa humo ndani na kisha mlango ule wa kioo ulifunguliwa tena,  sauti nzito ya muziki ilirudi kama awali.

****

                SAA KUMI ALASIRI

      Muda huu  likuwa ni kwa miadi kati ya Missinzo na yule Mzee mwenye uongozi kwenye kampuni ya usafirishaji haramu, ni ndani ya eneo la kurasani kwenye  eneo ambalo lina ghala lisilotumika. Huko walikutana wote  wawili nje na kisha mwenyeji akamsihi waingie ndani waweze kujadili vizuri, kijana huyu hodari mwenye akili nyepesi alikataa kitendo hicho mara moja.  Hakuwa akiaminiana naye kiasi cha kuweza kukubali jambo kama hilo, tena ndiyo kwanza wamekutana siku hiyo, uliwekwa mvutano kidogo katika kuwekeana ushauri lakini mwishowe hawakuingia.

      Iliwabidi watoke kwa pamoja hadi kwenye hoteli mojawapo iliyopo maeneo  hayohayo, hapo waliingia na Mzee yule aliomba chumba maalum cha mkutano akalipa pesa zote. Waliongozana moja kwa moja hadi kwenye chumba hicho wakiwa wawili tu na hapo ndipo Missinzo kidogo alijiwa na amani lakini hakutaka kujiaminisha kwa asilimia zote kuwa  kuna usalama. Silaha zaidi ya moja kwenye mwili wake aliziweka tayari kwa lolote lile ambalo lingejitokeza, haswa muda huo ambao amevaa suti ndiyo kabisa aliweza kuzificha silaha mbili kwapani huku nyingine zikiwa  ikiwa mguuni. Hapo alijiwekea asilimia mia moja kuwa usalama upo na utaendelea kuwepo, waliketi kwenye meza moja ndefu wakiwa wapo wawili tu na hapo Missinzo aliweka mkoba aliyokuja nao mezani kisha akatoa karatasai moja gumu ambalo lina  mchoro wa uliyochorwa kwa mbinu za kijeshi zaidi.

"Aisee kweli ninajadiliana na mtu mwenye kulijua jeshi, ni ramani ya kivita ya jeshi hili" Mzee alisema.

"Ni mmoja kati ya watu hatari niliyopo nchini kwa ajili ya kazi hii, na huu ndiyo mchoro mzima kuanzia watakapoingia nchini hadi kufika Kongo na kufanya tukio kisha kupotea kwao. Sasa inabidi mtambue kuwa nyinyi kwenye mpango kazi yenu inaanza hapa" Alisema huku akiweka kidole kwenye ramani ile.

"Sawaswa Israel, sasa weka kinagaubaga itakuwaje ndani ya mpango wetu"

"Mtahitajika kufika uwanja wa ndege kwani wageni hao watafika kama watalii hao ingawa wana rangi nyeusi, pia madereva wengine kutoka kwenye kampuni yenu wanahitajika kufika mpaka wa Tanzania na Kenya uliyopo mwishoni mwa mkoa wa Tanga. Hawa watapokea mzigo wa silaha na vitendea kazi vingine ambavyo vingetumika kwa  ajili ya shughuli hiyo"

"Sasa hapo nimekupata vilivyo kijana mpango upo vizuri, je kuhusu wanausalama waliyopo njiani sisi  tunahusika kwenye kuwafanya wasiwe na kauli?"

"Haswa nyinyi mnahusika na hilo ndiyo maana nikawa hapa kupitia nyinyi kwani mnajulikana  sana  na baadhi ya magari yenu huwa hayakaguliwi kabisa"

"Hilo inabidi muongeze kabisa kiasi chetu cha ziada kwani serikali ya sasa si kila askari yupo hivyo, kuna wengine ni sawa na jiwe hawashawishiki hivyo  kama tupo eneo la porini tunawamaliza hukohuko"

"Worry out about that kila nitakupadvance na kisha tunamaliza kazi yetu baada ya nyinyi kumaliza kazi yenu,ndiyo jinsi tunavyoenda katika wajibu huu daima"


"Ok hilo si tabu basi kila kitu kimemalizika na kwakuwa   sisi jukumu letu ni kujilinda na wanausalama basi ngoja tuanze na kujilinda hivi sasa kwani itakuwa ni vizuri zaidi" Mzee huyo aliposema kauli hiyo mlango ulifunguliwa kwa nguvu na kisha watu wenye silaha  za moto wapatao wanne  walionekana wakielekeza kule alipo Missinzo jirani kabisa na mwenyeji wake.


"Israel Missinzo jua unacheza na mtandao mpana sana, ulitegemea hautojulikana kutokana  mbinu  zako hizi mbovu. Hakika umejulikana wewe baada ya kuchukua picha za kijana wetu  pale Airport kila akipokea wageni, ukaamua kujileta na kwangu uweze kunichimba vilivyo" Mzee huyo alisema.

"Israel Missinzo kijana mwenye kufanya kazi kitengo cha IT  kwenye wizara ya maliasili na utalii kama kizugio chako, ilihali ni afisa  wa TISS wa kuaminika aliyepachikwa huko na Mkurugenzi mkuu karibu sana ndani ya vijana wa  Tendaguru hill" Sauti kutoka nje ailisikika na  kisha mlio wa viatu ulifuatia, alitokea yule kijana wa chumba cha kuongezea kamera kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere aliyempatia picha.

"Si rahisi  namna hiyo" Missinzo alisema.
    
       Kuona hatari ipo mbele yake Missinzo kwa kasi ya ajabu alijiangusha kwenye kiti alichokalia kisha akafyatua  kiti ambacho aliketi yule Mzee  naye akaenda chini bila ya kutarajia. Wakiwa huko chini alimdaka na kubiringita naye kuelekea uoande mwingine kutoka ule waliyokuwa awali, meza kubwa iliyopo humo ndani iliwasadia kumkinga vilivyo. Maswi pamoja na wenzake walibaki  wameduwaa na kabla hawajapata uamuzi mwingine wa kuchukua, Adui yao alisimama juu akiwa amemkaba yule Mzee huku bastola ikiwa kichwani.

"Fanyeni ukichaa, na mimi nifanye utahira" Missinzo alisema  kwa kijeuri.

ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment