Friday, December 18, 2015

SHUJAA SEHEMU YA KUMI NA NNE

RIWAYA: SHUJAA


MTUNZI: Hassan O Mambosasa

SIMU:+255713776843
+255762219759



WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



            ILIPOISHIA

Sauti ya mlio wa ujumbe mfupi wa maneno ndio
ilisikika katika simu ya Victoria, ujumbe huo
ulifunguliwa na mwenye simu halafu akusoma,
alipomaliza aliwaangalia Annie na Andrew halafu
akawaambia "jamani chukueni vitu mnifuate".

"vipi kuna nini?" Annie aliuliza.

"twendeni mtajua huko huko" Victoria alijibu hukuakijifunga mtandio kiunoni mwake. Annie na Andrew
waliamua kumfuata bila ya kujua chochote na wakawanapoenda. Walienda hadi ndani ya hoteli kisha
wakaingia kwenye lifti iliyowapeleka hadi ghorofa ya kumi, walipofika hapo walipokelewa na mhudumu
aliyevalia sare maalumu ambaye aliwaongoza hadi sehemu ambayo waliyokuwa wanaenda. Mwisho wa
safari hiyo ilikuwa kwenye bwawa la kuogelea ambapo walimkuta Moses na Beatrice wamevaa
mavazi ya kuogelea, wapendanao hawa walikuwa wamelala kwenye kiti kimoja cha kupumzika jirani
na bwawa la kuogelea.

"karibuni" Moses aliwakaribisha


ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI YAKE


SEHEMU YA KUMI NA NNE!!
"He!  Hee! Eti leo sitaki kuogelea jamani, heee kwa kidume umeogolea mwenyewe" Victoria alisema kimasihara huku akicheka huku wenzake alioingia nao wakibaki wanawaangalia Moses na Beatrice kwa macho yenye husuda, Andrew aliona ndiyo kaumizwa kuliko vyovyote ingawa alizidi kujawa na hari ya kumpata Beatrice ili awe wake. Umbile la Beatrice lile alilokuwa analiona kwenye nguo sasa alikuwa analiona kwa ufasaha baada ya Beatrice kuvaa nguo za kuogelea, moyo wake uliumizwa kwa kuona akiwa amekaa kiti kimoja na mtu mwingine tena akiwa amelalia kifuani kimahaba. Kila alipomtazama Beatrice aliona kama anamfanyia makausudi kwa kujilaza kifuani mwa Moses ili amuumize roho, maumivu aliyoyapata moyoni yalisababisha hadi kichwa kianze kuuma. Annie naye alipoona mwili wa Moses mwili wote ulimsisimka kwa hisia, nafasi aliyokuwa nayo Beatrice alitamani iwe yake kutokana na kuwa na upendo wa dhati kwa Moses. Kifu cha Moses ambacho kilifunikwa na shati alipokiona kwa mara ya kwanza, leo ameweza kukishuhudia kwa macho yake mawili.

"mmmh! Umeanza tayari" Beatrice aliongea kumuambia dada yake.

"nimeanza nini wewe dogo kwani uongo? Halafu Moses hivi mdogo wangu umemlisha nini" Victoria aliuliza.

"hilo swali ingepasa nimuulize yeye kuwa mimi amenilisha nini, sichoki kumuwaza kila saa" Moses aliongea.

"He! Hee! Kumbe wote mmechizika
 mioyoni, mnapendezana sana" Victoria aliongea.

"nawe ukianza tutakesha hapa hebu jumuikeni basi" Beatrice aliongea kuwakaribisha wote wajumuike katika kuogelea na kunywa pamoja nao, Annie muda wote huo alikuwa kabaki palepale alipo huku macho yake yakiwa hayachoki kuwaangalia wapendanao waliopo mbele yake, Andrew naye kuna jambo lilimsumbua sana moyoni mwake mbali na wivu aliokuwa nao kwa Moses. Maneno ya dharau aliyomtolea Moses jana ndiyo yaliyokuwa yakimsuta katika nafsi yake na hakutegemea kama Moses atakuwa na uwezo wa kumpeleka Beatrice sehemu ambapo hana uwezo napo na kama akijaribu kwenda yeye mwenyewe basi itamgharimu kiasi kikubwa cha pesa ambacho ni sawa kuimaliza akiba ya pesa aliyonayo ingawa ni mtoto wa kigogo, eneo hilo la hoteli ambalo ni maalum kwa walionazo ndiyo lilimfanya ajutie dharau zake.

"wengine mbona mmesimama jamani karibuni" Moses aliwakaribisha kwa mara nyingine, Annie na Andrew walishtuka kidogo waliposikia sauti ya Moses ikiwakaribisha kwa mara ya pili mahala hapo. Wote walisogea hadi katika bwawa la kuogelea kisha wakaketi kwenye viti vya kuogelea vilivyopo jirani na wenzao, wivu wa kumuona Beatrice akiwa pamoja na Moses na  kuuona mwili wa Moses kiufasaha ndiyo uliomsababisha  Annie abaki akishangaa. Jambo hilo pia lilikuwa likimtafuna mdogo wake pia ingawa alijitahidi kuvumilia.

"guys be free agizeni mnachotaka" Moses aliwaambia wote waliopo hapo baada ya wahudumu wa hoteli hiyo kufika eneo hilo, Annie na Andrew walisita lakini mwisho wake waliagiza kile wanachokitaka kwa wahudumu wao. Macho ya kuibia ndiyo aliyoyatumia kumtazama Moses kutokana na kuwa na hisia naye, Andrew naye alikuwa anaona kama moyo wake unatobolewa na visu vya moto kila akiwaona Moses na Beatrice wakiwa pamoja.

****

Wakati  Moses akiwa pamoja na mpenzi wake katika upande mwingine wa hoteli ya Magrove kulikuwa kuna casino kubwa iliyopo katika ghorofa ya tano ya hoteli hiyo. Casino hiyo ilijaa watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha wakiburudika kwa burudani za aina mbalimbali wanazozipenda huku wengine wakicheza kamari kama sehemu ya burudani, mziki mkubwa ulikuwa ukisikika ndani tu ya casino hiyo kutokana na uwepo wa vizuia sauti kutoka nje ya ukumbi huo. Jirani kabisa kabisa ya majokofu marefu ambapo ndipo baadhi ya watu ambao hawataki kukaa kwenye viti vya kawaida hupenda kukaa hapo kwenye stuli ndefu huku wakipata vinywaji vyao, eneo hilo kulikuwa kuna stuli nyingi sana zilizo tupu huku badhi zikiwa zimekaliwa na watu. Scott na Campbel nao walikuwa baadhi ya watu waliokaa kwenye stuli hizo wakipata vinywaji huku macho yao yakiangaza kila upande kwa umakini mkubwa, katika kutazama kwao huko macho yao yaligota katika mlango wa vioo vya giza ulioandikwa 'STAFF ONLY' ambao ulikuwa ukitumiwa na wafanyakazi wa hoteli tu katika kuingia humo Casino kufanya huduma kwa wateja. Campbel ndiye aliyekuwa anautazama mlango huo kwa umakini zaidi kuliko hata Scott, baada ya dakika kadhaa za kuutazama huo aliinuka kwenye stuli ndefu aliyokuwa ameikalia kisha akamtazama Scott aliyevaa kofia aina ya cap

"Hey! Scott niazime kofia yako mara moja kuna ishu nimeiona" Campbel alimwambia Scott.

"hii hapa" Scott alimwambia Campbel baada ya kuivua kofia  huku akimpatia, Cambel aliipokea kofia hiyo kisha akaivaa halafu akamwambia, "tukutane kwenye parking ya magari kwenye gari letu baada ya nusu saa na nisiporudi ndani ya muda huo basi ujue nimekwama". Campbel alipomaliza kuongea na Scott alielekea katika mlango unaotumiwa na wafanyakazi wa hoteli hiyo wenye vioo vya giza kisha akaufungua, mlango huo ulimtoa nje ya casino kwa upande mwingine kabisa na huko alikutana na wafanyakazi wa kawaida ambao hawakuwa na uwezo kumuuliza chochote juu ya uwepo katika eneo la wafanyakazi. Kila mfanyakazi aliyepishana naye aliishia kumshangaa kutokana na kuonekana eneo la wafanyakazi wa kawaida, baadhi ya wafanyakazi walipomuona waliendelea kufanya kazi na hata waliookuwa wanapiga soga waliacha mara moja wakijua labda ni mmoja wa mabosi wapya wa hoteli hiyo. Campbel naye alijivika ujasiri usoni mwake kisha akafuata korido ndefu hadi kwenye lifti moja iliyopo jirani na chumba cha wafanyakazi wanachotumia kubadilishia nguo pindi wanapoingia au wanapomaliza zamu, aliingia kwenye lifti hiyo kisha akabonyeza kitufe cha kushuka chini kabisa kwenye vyumba vya chini ya ardhi katika hoteli hiyo. Lifti aliyopanda naye ilitia amri kisha ikaanza kushuka kuelekea chini kwa mwendo wa taratibu, ilipokaribia chini Campbel alifungua juu katika chumba cha lifti halafu akapanda hadi akatoka nje ya chumba hicho cha lifti. Giza la eneo lenye kamba zinazoshikilia lifti ndiyo lilimkaribisha na ikamlazimu abaki hapo juu ya lifti hadi ilipofika mwisho wa safari yake, alishuka juu ya lifti hiyo kisha akaelekea katika upande ambao aliona kuna taa nyeupe ikiwaka katika chumba ambacho kna kioo kigumu sana. Alipofika alitoa kikata vioo kilichopo katika funguo zake kisha akakata kioo  kupande cha kumtosha yeye kupita, aliingia ndani  kupitia sehemu aliyoitoboa na akatokea katika chumba chenye makasha mengi yenye nembo za kuwekea za kemikali. Eneo hilo kwa kulitazama ungelitambua kama ni chumba cha maabara kinachotumika kutunzia kemikali mbalimbali, Campbel alilitazama eneo hilo kwa uangalifu kisha akaenda hadi ulipo mlango wa kuingia katika chumba hicho. Aliufungua mlango kwa taratibu huku macho yake yakiwa  makini kuangalia kama kuna mtu eneo analotaka kupita, ukimya wa eneo hilo ulimdhihirishia wazi kutokuwepo kwa mtu katika eneo hilo na angeweza kupita. Alitokea kwenye chumba chenye vifaa mbalimbali vya maabara  pamoja na tarakilishi mbalimbali za zinszotumika kwa katika kufanya majaribio ndani ya maabara pamoja na vitu mbalimbali, aliamua kupekua kila kitu humo ndani na hakuambulia chochote kitakachoweza kumsaidia katika kazi yake au kupata chochote kitachomuongoza katika kutafuta kitu alichotumwa. Aliamua kuangaza macho yake ndani ya chumba hicho ambacho ni maabara na akavutika na kitu kimojawapo kilichopo humo ndani, mlango mwingine ulioandikwa PRIVATE ndiyo ulimvutia na akataka kuna nini ndani yake. Aliuendea mlango huo na akajaribu kuufungua lakini ikashindakana kutokana na ukosefu wa kitasa cha kufungulia, pembeni ya mlango kulikuwa kuna sehemu ya kuweka kiganja ili kuufungua mlango huo. Campbel alipoiona sehemu hiyo ya kuweka kiganja cha mkono aliishia kutukana kisha akarudi hadi sehemu aliyoingilia halafu akapita kwenye tundu la kioo alilolikata kutokea nje, aliamua kuondoka kurudi alipotoka kwa uangalifu iama alivyoingia awali.

****

Vinywaji viliendelea kunyweka na kuogelea kukachukua nafasi katika  bwawa la kuogelea, Moses na Beatrice ndiyo waliokuwa wakifanya michezo mbalimbali ya kimpenzi na mingine ua kitoto kutokana na furaha waliyonayo katika mioyo yao ya kuwa katika ukurasa wa kimahusiano. Furaha ilitawala baina yao muda wote huo walipokuwa pamoja, furaha hii pia ilikuwa ipo ndani ya moyo wa Victoria baada ya kumuona mdogo waka akiwa  furaha katika kufungua ukurasa wa mapenzi katika maisha yake. Moses naye alikuwa katika furaha ya kumpata binti mrembo kama Beatrice, michezo waliyokuwa  wakiicheza ndani ya maji  ilikuwa ni kama watoto kimtazamo na ilikuwa ni kiburudisho tosha kwa mtu apendaye kuona wawili hawa wakiwa na furaha.  Laiti kama ungebahatika kuwaona ungetambua wawili hawa ni wenye furaha na hata wewe mwenyewe ungefurahi kuwaona wanavyocheza kimahaba na kama usingefurahi basi ungekuwa na wivu juu yao, Annie na Andrew walikuwa wakicheka kwa kijino upande tu lakini nafsini mwao walikuwa wakiungua kwa wivu  dhidi ya wawili hao.

"baby nahitaji kwenda barthroom nisindikize" Beatrice alisema huku akishika ngazi za bwawa la kuogelea ili atoke nje.

"ok baby" Moses alijibu huku akiwa nyuma yake.

"hebu leteni fimbo yaani nyinyi watoto mnaenda pamoja hadi hadi maliwatoni" Victoria aliongea kiutani.

"ushaanza tayari yaani huishiwi maneno" Beatrice aliongea.

"Shem usihofu namchunga kiduchu tu asiibiwe, kuwa na imani na mimi" Moses aliongea.

"dogs never protect  the meat between  his or her teeth(mbwa hawezi kulinda nyama kati ya meno yake)" Victoria aliongea na kupelekea Moses acheke akiwa yupo nje ya maji tayari.

"mhudumu muoneshe maliwato ilipo" Moses alimwambia mhudumu wa kike aliye karibu na eneo walilopo, Beatrice alivaa vazi maalumu la watu waliotoka kuoga lililositiri mwili wake kisha akafuatana na mhudumu huyo. Moses aliamua kukaa kwenye kiti akimsubiri Beatrice akiwaacha Victoria,Annie na Andrew wakiwa wapo ndani ya maji wakiogelea. Baada ya muda Annie naye alitoka ndani ya maji akisema anahitaji kupumzika na akawaacha Victoria na Andrew wakiogelea, Annie alienda kukaa katika kiti kilicho jieani na Moses huku akijilaza kihasara na kupelekea vazi la kuogelea liakisi maungo yake nyeti.

"nafikiri karatasi yangu niliyokuwekea kwenye mfuko  uliipata" Annie alimuuliza Moses kwa sauti ya chini.

"ndiyo nimeipata" Moses alijibu.

"sasa mbona hukunipigia wakati nimekupa namba yangu kupitia karatasi hilo" Annie aliuliza.

"Nikupigia ili iweje wakati sina shida wala jambo litakalonifanya nikupigie?" Moses alisema akionesha kukerwa na swali la Annie, hadi muda huo alishatambua  kitu anachokitaka binti huyo ambaye ni mkubwa kiumri kwake.

"Moses hujui jinsi gani naumia juu yako" Annie kwa sauti ya chini na ya kinyonge.

"Annie hadi hapa ulipokaa na vituko vyako nishajua unachohitaji na unajua Beatrice ni nani kwangu" Moses aliongea.

"I don't care about that, I love you and I care about my love to you(sijali kuhusu hilo,nakupenda na ninajali kuhusu upendo wangu) Annie aliongea.

" I care about that and I don't love you(ninajali kuhusu hilo na sikupendi). Pia utambue mimi sio kama hao wengine unaowajua"  Moses aliamua kuwa muwazi kwa Annie na akaweka msimamo kama mwanaume anayejielewa. Annie alimtazama Moses kwa huruma kisha akasema, "naomba unielewe Moses nakupenda" Annie aliongea.

"Haiwezekani........kisura umerudi" Moses alimwambia Annie kisha akaachana na mada hiyo baada ya Beatrice kurejea.

"yes My love, tukaogelee" Beatrice alimwambia Moses huku akimkumbatia, wote kwa pamoja walielekea kwenye bwawa la kuogekea wakimwacha Annie akiwa anatazama kwa jicho lenye husuda.

****

Campbel alifanikiwa kutoka kwa kutumia njia nyingine iliyompeleka hadi kwenye maegesho ya magari yaliyopo ghorofa ya pili ya hoteli hiyo, aliingia kwenye gari aina ya toyota verossa ya rangi nyeusi iliyopo katikati ya magari mengine yaliyopo kwenye mstari mmoja katika maegesho. Scott alikuwa yupo ndani ya gari akimsubiri kama walivyoahidiana.

"vipi huko umebahatika kupata fununu yeyote" Scott aliuliza.

"aisee hili eneo kuna maabara chini yenye mlango wenye unaofunguliwa na alama za vidole na unaonekana ni wa siri sana" Campbel aliongea.

"Mmmh  hilo eneo hilo nina wasiwasi nalo maana hoteli kama hii kuwa na maabara ujue kuna jambo, virus tunaowataka wapo hapahapa" Scott aliongea.

"tuongee kwanza na Tasu boy halafu tupange mikakati ya kuja kuingia hapa" Campbel aliongea.

"hilo ndiyo la muhimu kwani muonekano wa mazingira unayoyasema security system ni kubwa inaonekana" Scott aliongea.

"sawa tuondoke zetu" Campbel alimwambia Scott ambaye alikuwa yupo kwenye usukani, Scott aliwasha gari kisha akaliondoa taratibu kuzunguka mzunguko unaolipeleka chini ya ghorofa.


****

Jioni ilipowadia wote kwa pamoja waliamua kurudi makwao kwa kutumia usafiri uliowaleta mahala hapo, Moses aliamua kurudi kwa usafiri wake, Beatrice na Victoria waliamua kurudi kwa usafiri wao, Annie na Andrew hvyohivyo nao waliamua kurudi kwa kutumia usafiri uliowaleta. Annie na Andrew siku hiyo waliiona chungu kuliko hata siku zote za maisha yao, kukataliwa kwa kila mmoja kulikuwa ni maumivu kwao, wote kwa pamoja waliona kuna haja ya kutumia njia ya ziada katika kuharibu uhusiano huo ili waweze kupata wanachokitaka kutoka kwao. Mchezo mchafu ndiyo uliyokuwa umetawala vichwa vyao na si vinginevyo, mpango mzima ulikuwa umesukwa na watoto hawa  wa waziri na walihakikisha unatekelezeka kwa kutumia nguvu ya mshirika wa baba yake.

"Andrew unakumbuka nilichokuambia" Annie alimwambia mdogo wake akiwa ameshikilia usukani wa gari.

"Yeah! Nakumbuka na ulikuwa sahihi sasa tutauanzaje mchezo" Andrew aliuliza.

"tutamtumia my ex boyfriend naamini atatusaidia" Annie aliongea.

"nani? Tasu boy, hivi dada unafikiri atakubali akufanyie mpango wa kumnasa mwanaume mwingine kwa kumtumia yeye hebu fikiria tena kwa mara ya pili kuhusu hilo" Andrew alisema.

"Andrew niachie mimi kila kitu na usijali kuhusu hilo, nitamwambia ni kwa ajili yako ila si mimi" Annie alifafanua.

"hapo sawa" Andrew aliongea.


Huyu ndiye Annie Kabaita kama wengi wanavyomjua na mtoto wa waziri Kabaita, yupo chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka wa mwisho. Tabia ya kupenda mwanaume mzuri atakayemwona mbele ya macho yake hajaiacha tangu alipoingia katika ulimwengu wa mapenzi, kimuonekano ni mrembo pia mwenye sura ya upole ingawa moyoni ni shetani asiyehitajika kuwepo katika uso wa dunia. Binti huyu alikuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Tasu boy ambaye ni kibaraka wa Brian pia ni mshirika wa kibiashara na waziri Kabaita ambaye ndiye baba yake mzazi. Tangu mara ya kwanza alipomuona Moses alitokea kumpenda na alikuwa  tayari kuachana na tabia zake za kupenda wanaume, kitendo cha Moses kumpenda mwanamke mwingine ambaye ni tofauti na yeye ilikuwa ni maumivu tosha kwake na alihitaji kuyatuliza kwa namna ya kipekee. Lengo la kumtumia Tasu boy ilikuwa ni kuvuruga uhusiano wa kimapenzi uliopo baina ya Beatrice na Moses kwa kigezo cha kutafuta furaha ya Andrew, mpango huo ameshausuka na sasa anatafuta njia ya kumuhadaa Tasu boy hadi akubali.

****

Beatrice na dada yake walifika nyumbani kwao majira ya saa moja jioni kisha wakapitiliza hadi chumbani kwao wakiwa na furaha kupita maelezo. Dada mtu alifurahi baada ya mdogo wake kuwa na furaha na mdogo mtu alifurahi kwa kupata mtu anayempenda katika maisha yake, vicheko na matabasamu ndiyo yalitawala katika nyuso zao nzuri. Hakika kupendwa unapopendwa ni furaha na kuwa na unayempenda ni raha, Beatrice kapenda na yeye kapendwa alipopenda sasa yupo katika raha na furaha. Furaha ya Victoria ni kumuona mdogo wake yupo katika furaha na akiwa hana furaha basi  na yeye hatakuwa na furaha,  ndugu hawa waliopishana umri walikuwa wapendana na wapo karibu kama wamelingana umri.

"Bite kuna kitu nilisahau kukuambia nimekiona leo" Victoria alimwambia mdogo wake.

"wakati asubuhi ninatoka chumbani nilimuona Ojojo huyu mlinzi akiwa na picha zako na Moses mkiwa eneo la parking.

"my God! Nimekwisha dady akizipata" Beatrice aliongea kwa mshtuko.

"nimemnyang'anya kamera yake pamoja na picha zote alizowapiga kisha nimeziba mdomo na laki mbili, hivyo kesi nimeiua" Victoria aliongea.

"Thanks sis, umeniokoa namuogopa Daddy na sitaki Moses wangu apatwe na matatizo" Beatrice aliongea huku akimkumbatia dada yake.

"nilikwambia kuwa careful maana hawa walinzi wa Daddy ni wambea we umeenda kumpiga kiss mkaka wa watu kule eneo la parking, utampa matatizo young sis" Victoria alimlaumu.

"ok, nimekuelewa sis nitakuwa makini" Beatrice aliongea, wao wakiwa wamekaa chumbani kwao hawakutambua kama kama baba yao alikuwa amerejea kutoka na sauti yake ndiyo iliwafanya watambue kama yupi ndani ya nyumba.

"Beatrice!, Victoria!" sauti ya mzee Bernard ilisikika ikitokea sebuleni.

"my God daddy amerudi" Victoria alisema huku akiinuka kitandani kisha akasema, "yes daddy". Wote kwa pamoa kuelekea sebuleni ambapo walimkuta sebuleni, Victoria alimkimbilia halafu akamkumbatia Mzee Bernard huku Beatrice akisimama mbali halafu akakunja sura yake kuashiria amekasirika.

"whats wrong Beatrice come and give hug to daddy(nini tatizo Beatrice njoo na umkumbatie baba)" Mzee Bernard aliongea baada ya kumuona Beatrics kasimama.

"You left yesterday in the morning and you know its my birthday(umeondoka jana na unajua ni siku yangu yaa kuzaliwa)" Beatrice aliongea kwa kudeka.

"ooh! My daughter please forgive me(ooh binti yangu tafadhali nisamehe) ni kazi tu ilinihitaji na ndio inayotulisha na kutuvesha wote. I know it was your birthday, that's why I bought gift for you. You have  to smile and give hug to daddy so as to get your gift(najua ni ilikuwa ni aiku yako ya kuzaliwa, ndio maana nimenunua zawadi kwa ajili yako. Unatakiwa utabasamu na umkumbatie baba ili  upate zawadi yako) Mzee Bernard aliongea kuonesha upendo kwa binti yake, Beatrice alitabasamu kisha akaenda kumkumbatia baba yake huku akisema, "I love you daddy(nakupenda baba)".



ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment