RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI!!
Dereva teksi huyu aliongeza mwendo na alipokaribia Tegeta alivua kiatu cha mguu wa kushoto makusudi, hali ya hewa ya humo ndani ilibadilika ghafla ikawa ni harufu ya uvundo mzito iliwa imetawala.
"mmh! Gari yako iko nuka harufu baya baya" Scott aliongea kiswahili kibovu cha kuigiza huku akibana pua kutokana na harufu hiyo.
"Usijali bosi ngoja nikuwekee airfresh kuiondoa hiyo" Dereva aliongea huku akifungua mkebe uliokuwa pembeni yake akatoa chupa ya uturi wa kuweka harufu nzuri katika gari, aliupuliza ule uturi sehemu mbalimbali hadi harufu za uvundo wa viatu ikatoka.
"bosi hapo vipi?" Alimuuliza Scott baada ya kupuliza uturi huo.
"hapo safi kabi.." Scott alijibu lakini alidhindwa kumalizia sentensi yake akajikuta amepitiwa na usingizi mzito wa ghafla.
"Scott umekwisha wewe" Dereva wa teksi aliongea huku akizidi kuongeza mwendo wa gari kuitafuta Mbezi akiiacha Tegeta.
****
Yule dereva teksi alipofika kwenye makutano ya barabara ya Mwenge alikata kona kulia kufuata barabara ya Sam Nujoma hadi Ubungo kisha akafuata barabara ya Mandela baada ya kuvuka mataa ya Ubungo hadi Uhasibu. Alivuka mataa ya uhasibu akaingia barabara ya Kilwa iliyompeleka hadi mtoni kwa Aziz Ally kwenye mzunguko uliopo karibu na sheli ya Oilcom, aliingia kushoto akaifuata barabara iendayo Kurasini. Alipoingia Kurasini alienda hadi mbele ya nyumba moja yenye geti kubwa kisha akapiga honi mara moja, geti lilifunguliwa na mtu mwenye mwili wa kimazoezi akaingiza gari ndani hadi sehemu ya maegesho halafu akashuka akaenda kumtoa Scott akamkokota kumuingiza hadi sebuleni.
"mpeleke basement haraka" Yule dereva alitoa amri kwa mtu aliyemfungulia geti.
"bosi" Yule mtu alitii amri halafu akambeba Scott begani kwake akaondoka naye, yule dereva teksi alipohakikisha Scott yupo mikononi mwake alishika kidevu chake kwa nguvu akavuta kwa juu na ngozi ya usoni mwake ikavulika kama na akaonekana ana sura nyingine kabisa tofauti na ile ya kizee. Norbert ndiye aliyekuwa anaonekana muda huu baada ya sura ya plastiki kuivua, alienda ndani kubadilisha nguo baada ya kuona kazi yake imekamilika.
MASAA MAWILI YALIYOPITA
Asubuhi ya saa kumi na mbili kasoro Norbert alikuwa tayari ameshafika maeneo ya Bunju akiwa na muonekano wake wa kawaida kisha akaenda kwa mzee Kitwisho akavaa sura ya bandia pamoja na nguo nyingine, alipohakikisha amebadilika kwa kiasi kikubwa alichukua dawa fulani iliyokuwa kwenye kichupa kidogo mithili ya dawa ya mafua ya kupaka jirani na matundu ya pua. Aliipaka hiyo dawa jirani na matundu ya pua na kwenye sehemu ya mdomo wa juu ambayo huota masharubu, halafu akachukua kopo la pafyumu ya ndani ya gari ambayo imechanganywa na dawa ya nusu kaputi maarufu kama Klorofomu. Alipokamilisha kila kitu alichukua mfuko mdogo wa lailoni wenye kimiminika cha rangi ya njano akautia kwenye soksi yake halafu akavaa viatu vyake, aliingia ndani ya gari kisha akaondoka hadi jirani na nyumba waliyopo vijana wa Brian kisha akaegesha gari pembeni sehemu iliyojificha akakaa akasubiri hadi geti lilipoanza kufunguliwa akatoka Scott ndipo alipolisogeza gari jirani na geti. Scott alipunga mkono kusimamisha Norbert akakanyaga breki akasimamisha.
" peleka mimi Msasani" Scott alimwambia
"30000 tu" Norbert akitumia lafudhi ya kizaramo alijibu.
"twende" Scott alisema kisha akaingia ndani ya gari ya gari, Norbert aliondoa gari kwa akingia barabara ya Bagamoyo na alipofika mbali kidogo aliupasua ule mfuko mdogo wa nailoni aliouweka kwenye soksi yake kisha akavua kiatu makusudi. Harufu ya humo ndani ya gari na ikawa ni harufu mbaya kama ya uvundo wa ndani ya kiatu.
"mmh! Gari yako iko nuka harufu baya baya" Scott aliongea kiswahili kibovu cha kuigiza huku akibana pua kutokana na harufu hiyo.
"Usijali bosi ngoja nikuwekee airfresh kuiondoa hiyo" Norbert aliongea huku akifungua mkebe uliokuwa pembeni yake akatoa chupa ya uturi wa kuweka harufu nzuri katika gari ambayo ina mchanganyiko wa kemikali za dawa ya nusu kaputi(Klorofomu), aliupuliza ule uturi sehemu mbalimbali hadi harufu za uvundo wa viatu ikatoka.
"bosi hapo vipi?" Alimuuliza Scott baada ya kupuliza uturi huo.
"hapo safi kabi.." Scott alijibu lakini alidhindwa kumalizia sentensi yake akajikuta amepitiwa na usingizi mzito wa ghafla.
"Scott umekwisha wewe" Norbert aliongea kwa ghadhabu, dawa hiyo ya nusu kaputi haikumdhuru Norbert kwasababu alikuwa amepaka ile dawa ya kuizuia isiingie katika pua zake ambayo ni ile aliyopaka jirani na matundu ya pua iliyofanana na dawa ya mafua ya kupaka.
****
Majira ya saa sita mchana gari aina ya Toyota altezza iliegeshwa jiranj na nyumbani kwao Moses, mlango wa gari ilifunguliwa na Annie akaonekana akishuka akiwa amevaa gauni fupi la rangi nyeupe pamoja na viatu vya rangi hiyohiyo. Alionekana mrembo kuliko kawaida kutokana na gauni hiyo kumpendeza kuliko kawaida na miguu yake iliyojaa vema ilimfanya azidi kuwa mrembo sana, hata mwanaume aliye rijali akipishana naye lazima macho yake yavutika kumuangalia chini ya mgongo wake kwa umbo zuri la kibantu alilokuwa nalo. Uzuri aliokuwa nao ndiyo uliompa ujasiri wa kuzidi kumfuata Moses akijua atavutika kwake kwa namna yoyote kwani karibu kila mwanaume huwa anapata misukosuko kila akimuona, kwa hakika Annie alisahau ule usemi wa avumaye papa baharini wengine wamo. Hakutambua kama wazuri wengine wamo tena ndani ya dunia hii yeye alijiona ni mwanamke mzuri hata zaidi ya Beatrice anayependwa na Moses hivyo suala la kumpata Moses kwake lilikuwa linawezekana kwa namna yoyote.
Annie alitembea hadi getini ambapo akimkuta akiwa amekaa sehemu yake ya kazi.
"mambo" Alimsabahi mlinzi
"safi tu mrembo nikusaidie nini?" Mlinzi aliitikia salamu kisha akamuuliza shida yake.
" Moses nimemkuta?" Annie aliuliza
"Ndiyo yupo ila bosi Kennedy amesema mgeni yoyote asiingie humu ndani kwa usalama wa Moses.
"Jamani kwani mimi kuja hapa ni mara ya kwanza hii mpaka useme mi mgeni" Annie aliongea kwa sauti ya kulalamika huku akimpa mlinzi hela.
" natambua hilo lakini.." Mlinzi aliongea lakini alishindwa kuimalizia kauli yake baada ya kupokea pesa ya Annie, alifungua geti na Annie aliingia ndani.
"ingia ndani muulize dada wa kazi atakutajia alipo" Mlinzi alimwambia Annie huku akifunga geti, Annie alienda hadi ndani ya nyumba akamkuta mfanyakazi wa ndani hapo nyumbani akiwa anaangalia luninga.
"karibu" Mfanyakazi wa ndani alimkaribisha.
"asante, za hapa?" Annie aliuliza
"salama tu" Mfanyakazi alijibu.
"vipi mwenyeji wangu yupo?" Annie aliuliza.
" unamuuliza kaka Moses?" Mfanyakazi aliuliza
"yeah! Namuulizia Moses" Annie alijibu
"yupo gym anafanya mazoezi" Mfanyakazi alimwambia
"he! Ni wapi?" Annie aliuliza
"fuata korido hadi mwisho utaona mlango, fungua mlango na utaona ngazi zinaelekea chini. Shusha ngazi hizo hadi chini halafu ingia chumba cha pili baada ya Maabara" Mfanyakazi alimuelekeza.
"asante mdada" Annie huku akimpatia hela mfanyakazi halafu akafuata njia aliyoelekezwa na msaidizi huyo wa kazi, aliifuata hadi kwenye chumba alichoelekezwa akamkuta Moses akiwa anafanya mazoezi kifua wazi katika vifaa mbalimbali vya mazoezi vilivyopo humo ndani. Annie alibaki akimuangalia Moses kwa jinsi anavyotunisha musuli ya mwili wake wakati akifanya mazoezi hadi mwili wake ukaanza kumsisimka, alijikuta amemsogelea Moses hadi nyuma yake na kuanza kumpapasa sehemu ya mgongo na kupelekea Moses asitishe kufanya mazoezi amuangalie mtu aliyemshika ili amtambue. Alipoiona sura ya Annie uso wake ulimbadilika na kuwa usio na furaha kuliko hata alivyokuwa awali, Annie alitabasamu tu pale alipomuona Moses akiwa kifua wazi kwa mara ya pili.
"unataka nini Annie?" Moses aliuliza akioneshwa kukerwa na ujio wa Annie.
"nakutaka wewe ndiyo maana nipo hapa" Annie alijibu kwa madaha
"hivi wewe una masikio ya kenge husikii mpaka utoke damu" Moses aliuliza kwa taratibu.
"hata ya kenge yana nafuu Moses yakitoka damu yanasikia ila yangu mimi hayasikiii kwa chochote ndani ya dunia dhidi ya matakwa ya moyo wangu, Moyo wangu ukipenda no body can stop to follow kitu inachokipenda" Annie aliongea huku akimsogelea Moses hadi akawa anatazamana naye uso kwa uso.
"Moyo wangu katika kupenda siku upo static hivyo haubadiliki, na usitegemee kama moyo wangu utakuwa dynamic utbadilika uje ukupende wewe baadaye. Sahau hilo" Moses aliongea akiwa yupo makini akimuangalia Annie ambaye alikuwa yupo karibu yake hadi muda huo, Annie aliposikia maneno hayo aliinama chini kama vile anasikia aibu kumuangalia Mosea usoni halafu akatoa kitambaa cheupe mfukoni akawa anakipeleka usoni kwa Moses. Moses aliuzuia mkono wa Annie kwa nguvu huku akimtazama usoni kwa umakini na kumfanya Annie aangalie chini, aliuachia mkono na mara ya pili Annie akakileta kile kitamba usoni mwake Moses akakizuia tena.
"nakuona unatokwa jasho na taulo lipo mbali, kuna vibaya nikikufuta jasho ili nikupunguzie usumbufu wa kulifuata taulo" Annie aliongea.
"nashukuru lakini ningependa nitumie taulo langu" Moses aliongea.
"please Moses niachie nikufute kwani kuna ubaya gani nikikufuta" Annie aliendelea kung'ang'ania kumfuta Moses jasho lililokuwa linamvuja usoni mwake.
"fine futa halafu uondoke kama huna cha ziada" Moses alijikuta akukubali ili kuondoa mabishano ambayo yangetokea kama angemkatalia, Annie alishika kitambaa akaanza kumfuta kuanzia shavu la kushoto kwa madaha sana tena taratibu sana. Kitambaa kilikuwa kikavu alipoguswa nacho Moses tena chenye ubaridi usio wa kawaida ambao ulimshangaza sana lakini aliamua kunyamaza, Annie aliendelea kumfuta taratibu sana na alipomfuta usoni sehemu za puani jambo lingine lisilotarajiwa lilitokea kwa Moses. Taratibu uchovu wa ajabu ulianza kumnyemelea Moses na usingizi wa ghafla ukaanza kumpata, alijitahidi asilale lakini mwisho wake alilala bila kutarajia mwenyewe,
Alikuja kuamka baadaye na alipoangalia saa alikuta ni saa kumi alasiri na ikamfanya akurupuke kwanj hakujua ilikuwaje mpaka akalala hivyo, alipoamka alihisi mwili wake una uchovu mkubwa sana na njaa kali ilikuwa inamsumbua. Alisimama alajikuta amevaa nguo tofauti ns zile alizokuwa amevaa awali alipokuwa anaamka asubuhi, alipovuta kumbukumbu nguo hizo alivaa saa ngapi alishindwa kutambua kabisa ni muda gani.
"kwanza tangu lini nikalala hadi muda huu si maajabu haya" Moses alijisemea huku akinyanyuka kitandani na aliposimama miguu alihisi haina nguvu lakini alijilazimisha kutembea hivyohivyo hadi sebuleni akaenda kukaa kwenye kochi.
"Dadaa!" Moses alimuita msaidizi wa kazi kwa sauti kubwa.
"abeee!" Sauti ya Msaidizi wa kazi ilisikika ikiitika kutoka katika moja ya chumba katika nyumba hiyo, baada ya sekunde kadhaa Msaidizi wa kazi alikuja hadi sebuleni akamkuta Moses akiwa amekaa kwenye kochi.
"Kaka Mose unajisikiaje hadi sasa hivi?" Msaidizi wa kazi alimuuliza Moses.
"mbona unaniuliza hivyo?" Mosesnaye alimuuliza swali badala ya kujibu swali.
"Kaka wewe si ulizimia huko gym wakati unatoka kuoga kwenye bafu la huko gym" Msaidizi wa kazi alimueleza Moses maelezo yaliyozidi kumchanganya Moses.
"Nimezimia?!" Moses aliuliza kwa mshangao.
"Ndiyo kaka yule mdada aliyekuja leo ndiye ameniambia umeteleza ukajigonga ulipokuwa unatoka kuoga tena akanitaka nije nimsaidie kukuleta huku chumbani kwako" Msaidizi wa kazi alizidi kumueleza, Moses aliposikia hivyo kumbukumbu zake ujio wa Annie zikamrudia kichwani mwake hadi pale alipofutwa jasho akajikuta amepata usingizi wa ghafla.
"tena amaniambia ukiamka nikupe maziwa unywe ili mwili wako upate nguvu" Msaidizi alizidi kutiririka zaidi.
"nizimie halafu nikiamka nipewe mziwa? Maziwa yanahusiana nini na kuzimia?" Moses alijiuliza nafsini mwake kisha akasema, "haya nipatie hayo maziwa". Msaidizi wa kazi aliondoka kisha akarudi na bilauri ya kioo yenye maziwa hadi juu akampatia Moses kisha akaja kukaa kwenye kochi hilo pembeni yake.
"kaka nikuambie kitu" Alimwambia Moses.
"sema tu nakusikiliza" Moses alimpa uhuru wa kuongea hicho anachotaka kukiongea.
"kaka unajua yule mdada anakupenda sana" Msaidizi wa kazi aliongea
"halafu wewe naona umekosa la kuongea" Moses aliongea na kusababisha msaidizi wa kazi acheke, Moses alitishia kumpiga msaidizi akakimbilia kochi jingine huku akicheka.
"kaka tuache utani unajua alivyoondoka mara nyingi anapiga simu na akiulizia hali yako" Msaidizi wa kazi aliongea.
"Sasa ndiyo ujikusanye uje kuniambia hivyo" Mosea alimwambia
"Ndiyo tena alikuwa ana wasiwasi huyo" Msaidizi wa kazi aliongea.
"hebu wacha hiyo habari kwanza pokea simu" Moses alimwambia msaidizi wa ndani ambaye aliinuka hadi mahali ilipo simu ya mezani isiyo na waya akaipokea halafu akaongea, "hallo....ndiyo amemka........huyu hapa". Alimkabidhi simu Moses kisha msaidizi wa kazi akarudi kukakaa kwenye kochi alilokuwa amekaa hapo awali.
"hallo" Moses alisema alipoweka simu sikioni, masikioni mwake alisikia sauti ya Annie ikimuambia jambo ambalo aliishia kukunja sura kutokana kukerwa nalo sana.
"Moses wewe ni mtamu zaidi ya asali tena mwenye ladha ya utamu kuliko chochote, kwa mara ya kwanza nimeonja penzi lako ukiwa usingizini hadi kiu yangu iliyopanda baada kuuona mwili wako ikaisha. Nimekuogesha nikakuvisha nikamuita huyo dada akanisaidia kukubeba hadi chumbani kwako ukiwa hujitambui kutokana na kunusa Klorofomu niliyoiweka kwenye kitambaa ambacho nilikusudia kumteka nacho shemeji yako ili Beatrice aachane na wewe" Sauti ya Annie iliyokuwa ikimkera Moses ndiyo ilisikika katika masikio yake.
"Malaya mkubwa wewe" Moses alijikuta ameropoka mbele ya msichana wa kazi.
"ohooo! Sawa mimi malaya na nitakufanya wewe uwe malaya kwa kutembea na mimi pamoja na Beatrice ambaye umemtoa usichana wake, ukikataa jua mtaachana na Beatrice kwani wakati nastarehe na mwili wako nilipiga picha kadhaa tukiwa wawili tena kama tulivyozaliwa. Nitamtumia Beatrice na huo ndiyo utakuwa mwisho wa uhusiano wenu" Annie aliongea kwenye simu kisha akakata simu.
"ooh! Shit!" Moses alisema kwa jazba kisha akaibamiza simu chini halafu akainuka kwa kasi akaenda chumbani kwake akafunga makomeo yote, Msaidizi wa kazi alibaki akimshangaa tu.
****
BUNJU
DAR ES SALAAM
Kutoonekana kwa Scott ilikuwa ni pengo jingine lilizidi kuwachanganya makomandoo wa kizungu ambao wa po watatu hadi muda huo kutokana na wenzao wawili kufa na mmoja kupotea, jioni ya siku hiyo Jameson, Obrsn na Calvin walikaa kikao kizito na wakajadili juu ya suala hilo kwa upana kisha wakaliwasilisha kwa Brian ambaye aliwaahidi kuingia mwenyewe kazini kwani anahisi kuna mkono wa simba unapita katika mipango yake. Baada ya kusikia uingiliwaji wa kazi hiyo na bosi wao walipata ahueni kidogo kwani walijua mtu mwenye uwezo mkubwa anafanya nao kazi hivyo itatimia tu.
"huyu ibilisi anayetusumbua ni nani?" Obren aliuliza baada ya suluhu ya kikao chao kupatikana.
" hatumjui wote, yaani hapa tupige msako tumdake si unajua yule dogo ana wiki mbili wafanye graduation na ana mwezi afanye mtihani wa taifa sasa tukichelewa tu akimaliza necta itakuwa ngumu kumpata" Jameson aliongea
"sasa inabidi tufanikishe upesi kabla mambo hayajaharibika ndugu tena tukipata huyo aliyewaua wenzetu ndiyo atajuta kwani tutakamfanyia yeye na hii ncho yake kama watapona basi hawatasahau" Calvin aliongea.
"wale virusi hawana dawa na wataisha kama kuku wenye kideri hadi huyu anayetuulia wenzetu" Obren aliongea, wazungu hawa walionekana wanaogelea katika mkondo wa maji sasa nguvu umewashinda wameomba msaada.
****
Asubuhi ya siku iliyofuata Scott alijikita akiwa yupo kwenye chumba chenye giza sana kikiwa hakina hata dirisha moja, mazingira hayo yalimshangaza kwani hakukumbuka mara ya mwisho alikuwa wapi. Alipojaribu kuinuka alijikita hawezi hata kusogea kwani mikono yake ilikuwa imefungwa na kitu cha chuma ambacho hakukijua ni nini, alikuwa amekalishwa kwenye kiti cha chuma na mikono na miguu yake ikiwa imefungwa katika kiti hicho. Baada ya nusu saa tangu azinduke mlango wa chumba hicho ulifunguliwa na taa zikawaka Norbert aliingia akiwa na uso wenye tabasamu, Scott alipomuona alishutuka sana hadi Norbert mwenyewe akagundua.
"hatimaye upo katika uwanja wangu wa nyumbani Scott" Norbert aliongea huku akitabasamu.
"Kaila wewe ni mwandishi wa habari msafi utanikamataje hapa wakati nimekuja kuisadia nchi yenu" Scott aliongea.
"umekuja kuisadia nchi yetu sio? Kwanini uliingia kinyemela kupitia ziwa Viktoria tena kwa boti iliyoibiwa huko Urusi, si ungetumia njia halali" Norbert alimwambia Scott mambo ambayo yalimfanya ajione amenasa kabisa.
*Simba ndani ya mtego wa panya kanasa hatoki
*Annie amtumia Moses kimapenzi baada ya kumnisisha nusu kaputi.
No comments:
Post a Comment