Monday, December 26, 2016

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO



RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________



SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO!!
              "N001 ndiye aliyemuua Benjamin wangu" Josphine alijibu huku akijifuta machozi, kisha akaanza kufikiria tukio zimalililotokea hadi Benjamin akauawa na Norbert. Alikumbuka busurefu alilopigwana Norbert kabla hajapigwa na kitako cha bastola, maneno aliyomuambia yalijirudia kwenye kichwa chake na hapo ndipo hasira dhidi ya Norbert ilipozidi akbaki akihema.
    
          "N001 ndiyo nani Leporard Queen hebu tueleze tumjue akalipe ushenzi owte alioufanya" Benson alimsihi Josephine
               "ni Norbert Kaila" Josephine alijibu kisha akaanza tena kulia.
               "what! Wote kwa pamoja walijikuta wakiropoka kwa mshangao.

__________________
_______________  TWENDE PAMOJA SASA
_________

    Walijikuta wakiwa hawaamini maneno ya Josephine na walibaki wakitazamana tu kisha wakapeana ishara ya macho kila mmoja, waliporuudisha macho yao kwa Josephine walikuwa na sura ya huruma kila mmoja  jambo ambalo lilimshtua Josephine akawa haelewi walikuwa wamekumbwa na nini. Josephine aliwashangaa sana  watu hao kwa jinsi walivyokuwa wakimtazaama kihuruma, macho yake yalipotua kwenye uso wa  Benson ambaye alikuwa na uchungu aliuona ukiwa tayari umepotea katika uso wake na huruma ndiyo ilikuwa imemtawala.
               "jamani kuna nini mbona hivyo siwaelewi?!" Josephine aliwauliza, swali lake  lilimfanya Benson asogee karibu  aye zaidi akakaa kwenye kitanda kisha akamshika viganja vya mikono yake kwa upole.
               "Josephine" Benson alimuita kwa kutumia jina lake na si jina la kikazi, Josephine alipeleka kichwa juu kuitika huku akimtazama usoni   Benson.
                "Are you sure(una uhakika) ni Norbert?"  Benson aliuliza kwa upole, Josephine hakujibu kwa kinywa chake zaidi ya kuinua kichwa juu kisha akakirudisha chini kukubali.               
                "Mkumbuke mliniambia nimuwekee mtego ili tumnase, sasa ndiyo mtego kauruka na kunipiga risasi ya bega halafu akamuua Benjamin kwa kumuangusha juu ya meza" Josephine alifafanua baada ya kukiri kuwa ana uhakika . Tena alizidi kueleza,
                "baada ya hapo ndipo akaniambia niwafikishie salamu  nyinyi kuwa N001 hakamatwi kijinga namna hii".
     Wote walipoyasikia maelezo hayo hawakuwa na sababu nyingine ya kupinga na walimuona Josephine hakuwa amechanganyikiwa kama ilivyo awali bali alikuwa anasema ukweli mtupu, hawakujua kama kwenye maelezo yake kulikuwa na uongo tayari aliuongezea waoa waliamini moja kwa moja kwamba alikuwa akiongea ukweli mtupu  katika maneno hayo. Hasira dhidi ya Norbert ndiyo zilizidi kuchukua nafasi,  hakika walichotwa kabisa na uongo jumlisha ukweli ambao Josephine aliwaambia  katika maelezo yake.
                "Huyu mtu anaonekana ni hatari kiasi gani hadi kawazidi ujanja wote kwa pamoja" Thomas aliongea baada ya kuyasikia maelezo hayo.
               "Hapana huyu hana uhatari wowote bali ni mviziaji tu na hawezi kuvizia  tena mbele yetu ni lazioma afe mara moja" Santos aliongea kwa kujiamini kabisa
                "tena nitamuua kwa mkono wangu mwenyewe huyu" Benson aliongea huku akitetemeka kwa hasira alizonazo
               "Benson najua una hasira sana ila huyu mtu anahitaji kuchezewa mchezo kama anavyotuchezea mchezo inabidi tufanye nini mnajua" Thomas aliongea huku akiwatazama kila mmoja, wote walijawa na shauku ya kutaka kusikiliza wanachotaka kuambiwa , walimtazama kwa shauku ya  kutaka kusikia hiyo njia ambayo wangeitumia kumnasa mtu hatari kama huyo.
    Thomas aliitamka mbinu hiyo ya kumnasa Norbeert kwa sauti ya chini ambayo ilisikiwa na wenyewe tu, hata mimi mwandishi sikupata hata wasaa wa kuisikia mbinu hiyo aliyoibuni mzungu huyo bingwa wa mbinu katika kikundi chao. Mwandishi nilipata kushuhudia jinsi wakinong'ononezana kwa suti ya chini tu juu ya mpango huo ambao walikuwa umumebuniwa na Thomas ndani ya muda mfupi tu,usiniulize nimeonaje wakipanga mpango ila tambua nimeuona nimeuina ndiyo maana nikuwasilidha kwa maandishi.

****

                                              SAA MOJA BAADAYE

   Norbert akiwa yumo ndani ya nyumba ya shirika la EASA alipokea simu kutoka mmmoja wa marafiki zake wa karibu ambayo ilikuwa ni ya muhimu kwa taaluma yake ya habari, ilikuwa ni simu ilimjulisha juu ya mkutano uliotakiwa kufanyika nyumbani kwa Mnadhimu mkuu wa jeshi ambao ungehusisha waandishi wa habari na  Mnadhimu huyo wa jeshi baada ya kumalizika mazishi ya Jenerali Kulika. Norbert alijiandaa haraka akiwa amebeba vifaa muhimu ikiwemo kamera yake ya kazi pamoja na mapambo amabyo huyatumia kama tahadhari, aliingia ndani ya gari yake akimuacha Moses ndani ya eneo hilo na aliondoka kuelekea Mbezi beach nyumbani kwa L.J Ibrahim aliposikia kuwa Mnadhimu mkuu wa jeshi alikuwa ameitisha mkutano wa pili wa waandishi  wa habari.
    Ndani ya nusu saa tayari alikuwa alikuwa ndani ya Mbezi Beach akiwa na amevaa suti nadhifu, alielekea moja kwa moja mtaa amabao alikuwa anaishi L.J Ibrahim ambapo alipiga honi katika geti la nyumba ya kisasa. Mlinzi wa getini alitoka hadi nje baada ya kusikia honi hiyo na alipobaini aliyekuwa akipiga honi hiyo alikuwa ni Norbert aliruhusu gari hilo liingie ndani kwa kufungua geti. Norbert aliingiza gari hadi kwenye maegesho ya magari ambapo alikuta magari mbalimbali yaliyobandikwa mabango ya matangazo ya televisheni na redio mbalimbali, hapo alipata uhakika kuwa kulikuwa na mkutano huo humo na ikambidi abebe vifaa vyake vya kazi kashuka garini akafunga milango.
    Aliposhuka tu garini alimkuta mwanajeshi mwenye sare za kijeshi ambaye alimpokea kisha akamuashiria aelekee upande wa mlangoni wa nyumba ya L.J Ibrahim, Norbert aliongoza njia huku akivaa kitambulisho chake vizuri ili aweze kutambulika kama mwandishi wa habari. Alipiga  hatua zake taratibu huku mwanajeshi akiwa nyuma yake kuhakikisha anafika kwenye mkutano maalum, mkutano amabo ulikuwa tofauti na yeye alivyotarajia. Alivyopiga hatua takribani sita tangu ashuke garini alihisi kitu kigumu na chenye ubaridi kikigusa shingo yake kwa nguvu, Norbert alisita ghafla akataka kugeuka  lakini alizuiwa na mkono mgumu wa mwanajeshi aliyempokea kugeuka nyuma.
               "weka shingo hivyohivyo nguchiro wewe na uongoze njia" Mwanjeshi yule alimkaripia, hapo Norbert alijua taayri alikuwa ameingia katika hatari, hakuwa na  la kubisha ingawa alitambua mwanajeshi huyo hawezi kumuua kwa muda huo hata kama akileta ubishi.

     Alitembea huku akiwa ameshika vifaa vyake vya uandishi wa habari, alipokaribia mlangoni yule mlinzi alimpekua kisha akamuamuru afungue mlango. Norbert alifungua mlango bila kubisha na akaingia ndani kisha yule mwanajeshi akaufunga mlango kwa nyuma, alitokea kwenye sebule pana iliyokuwa imetolewa samani na kuifanya iwe kama nyumba ambayo wakazi wake walikuwa wakitaka kuhama. Humo ndani aliwakuta L.J Ibrahim. Benson, Thomas, Santos na Wilson wakiwa wamesimam na kila mmoja akiwa na bastola mkononi wakimngojea kwa hamu kubwa sana, hakika alikuwa ameingia mtegoni bila yeye kujijua kabisa. Pembeni katika kona moja ya sebule hiyo kulikuwa kuna kiti ambacho alikuwa amefungwa mtu ambaye alikuwa hatambuliki kiurahisi kutokana na uso wake kujaa damu kuashiria  alikuwa amepigwa sana, ilikuwa ni jambo amabalo hakulitarajia kwa muda huo na tayari uoga mdogo alikuwa nao ndani ya moyo wake baada ya kuwa ameingia katika anga za watu ambao alishawahikuwatororka zaidi ya mara moja.
               "Smart guy Norbert Kaila a.k.a N001 karibu katika mdomo wa kifo" L.J ibrahim aliongea huku akitabasamu, ukairibisho huo usio na amani ulisikika vyema kwa Norbert lakini hakuonesha hali ya uoga usoni ili asiwape nafasi maadui zake wazidi kumvuruga asipate wazo la kujitetea.
       Aliachia tabsamu zito sana kisha akaanza kuwatzama kila mmoja kwa tabsamu pana mithili ya bibi jarusi akimtazama mwanume wa ndoto zake siku ya harusi, aliingiza mkono mfukoni na hapo milio ya kuondolewa usalama kwa bastola ikasikika.
                "usifanye ujanja wowote Norbert utakufa kabla hujatimiza ndoto zako zakuwepo duniani" Santos alimkoromea huku akimtazama kwa hasira, Norbert aliutoa mkono aliouingiza ndani ya koti haraka ukiwa na kiboksi cha peremende za kutafuna bila kumeza za batoock.
                "Hey ni big G tu hizi" Norbert aliwaambia huku akiwaonesha, alifungua kiboksi hicho bila wasiwasi wowote kisha akachomoa kikaratsi kidogo akakifungua huku akitabasamu alitoa premende hiyo ya kutafuna tu kisha akaitia mdomoni mwake akaanza kuitafuna huku akitabasamu kama kawaida yake.
                "dustbin hamna hapa, sasa nitaweka hizi karatasi za hii big G?" Norbert aliuliza akiwatazama watu wale waliokuwa wakimtazama kwa hasira.
                "usilete porojo wewe kwanza jibu maswali yetu kabla hujawafuata wafu" L.J Ibrahim aliongea kwa kufoka huku akigusa kifyatulio cha bastola kwa lengo la kumtisha Norbert lakini Norbert hakutishika hata kidogo ndiyo kwanza alizidikutoa tabsamu lililokuwa linakribia na kicheko.
                 "sasa hizi karatasi za Big G kwahiyo nizitupe kwenye tiles hapa haya" Norbert aliongea pasipo kuonesha kuwa anawatilia maanani na akazitupa karatasi hizo kwenye sakafu ya marumaru huku akiwatazama maadui zake.

    Maneno hayo yalimuudhi sana Benson akaona alikuwa akidharauliwa yeye na wenzake, kwa hasira zake alimuelekezea bastola Norbert kisha akafyatua risasi kwa lengo la kumuua lakini Thomas aliiwahi risasi hiyo akaielekezo chini. Risasi hiyo ilitoa mlipuko mkubwa sana baada ya kupiga marumaru na iliingia ndani ya marumaru kiasi cha nusu inchi, tukio hilo lilikuwa ni lenye kushtua kwa Norbert lakini hakuonesha mshtuko wowote yeye aliendelea kutabasamu tu kama aliona  jambo la kusuuza moyo wake.
               "Thomas ungeacha nimmalize huyu mshenzi dharau hizi" Benson aliongea kwa hasira.
              "Benson cool down buddy, huyu hahitajiki kufa mapema namna hii" Thommas alimuambia
              "Uniue kama ulivyomuua General Kulika ili muweze kupata kueneza ushenzi wenu"Norbert aliongea maneno ambayo yalizidi kuwachoma watu hao. Tan alizidi kupigilia msumari katika maelezo hayo, "Au mnafikiri sijui mkamuua mufti na Askofu Edson aliyekuwa mwenzenu, mnadhani sitambui kama mmetumwa na Askofu shoga anayeitwa Achim Valdermar alimaarufu kama Jack Shaw tena alipokuja Tanzania Benson ulionana naye kaika hoteli ya Kempiski".
     Maneno hayo yalizidi kumvuruga kila mmoja hapo wakabaki wakipandwa na hasira sana, walijua tayari Norbert alikuwa akijua siri zao nyingi na ilikuwa ni hatari sana kwao kama angetoka mzima eneo hilo. L.J Ibrahim ndiyo alipandwa na hasira zaidi akaelekeza bastola kwenye upande aliofungwa yule mtu aliyekuwa amejawa na damu usoni, alifyatua risasi tatu ambazo zilimpata yule kwenye paaji la uso na kifuani kisha akairudisha bastola katika usawa alipo Norbert.
                 "Ndiyo unajua mengi tuone sasa kama utatoka hapa ukiwa mzima, hii siri itabaki miongoni mwetu tu.  Tumeanza na huyu mwandishi wa habari mwenzako aliyekupigia simu uje huku hadi ukaingia mtegoni" L.J Ibrahim aliongea kwa kujiamini.
                   "Ok hata mimi naona ndiyo maana mkabandika matangazo yenye nembo za televisheni kwenye magari ili muweze kuninasa mimi siyo" Norbert alizidi kupoteza muda kwa kuongea maneno yenye kuudhi, aliponyamaza kimya saa yake ya mkononi ililia ambapo alibonyeza kitufe ikazima.
                    "sorry saa ilikuwa na automatic alarm" Norbert alisema huku akiwa hajali vitisho alivyopewa, aliwatazama maadui zake ambapo kila mmoja alikuwa akiiiweka sawa risasi kuashiria yupo tayari kufyatua risasi.
                   "Hatuna mjadala na wewe fyatueni risasi tumalize kazi" L.J Ibrahim aliwaambia wenzake, kila mmoja alijiweka tayari kufyatuia risasi lakini walijikuta wakisita baada ya Norbert kuwaonesha ishara ya mkono wasubiri.
                    "Ok mpo tayari kuniua lakini hampo tayari kuishi nyinyi" Norbert aliongea huku akileegeza tai aliyoivaa, tai hiyo ilionekana tofauti na tai nyingine zilizoeleka baada ya Norbert kuilegeza, sehemu ya kupita shingoni ilionekana kuwa ina waya wa umeme. Norbert akipowageuzia tai hiyo waione kwa nyuma wote kwa pamoja walijikuta akishtuka wakishtuka, yeye ndiyo alizidi kutabasamu kwani aliona ilikuwa ni njia pekee ya kujikomboa katika eneo hilo
                   "Ohh! No" Thomas alisema huku akishusha bastola baada ya kuona klekilichokuwa kipo nyuma ya tai hiyo, lilikuwa ni bomu la kutegwa   lilibanwa nyuma ya tai likiwa linazidi kupungua dakika zake. Wenzake nao walishusha silaha zao wenyewe na hawakuwa na ujanja tena baada ya kuona hilo bomu, Benson naye aliishiwa mbinu na akateremsha silaha kama walivyofanya wenzake na wote wakamtazama Norbert kwa umakini wasijue alikuwa amedhamirira kufanya nini baada ya kuwaonesha bomu hilo.
                    "kufa kwangu siyo hasara sana bali kufa kwenu ndiyo hasara, hamtapata hata nusu ya malipo ya kazi mliyokuwa mnaifanya na lengo la kuifanya kazi hiyo ilikuwa ni kupata hela. Fikirieni kwa mara mbili ndani ya dakika kadhaa mtakuwa mmetawanyika viungo vyenu vyote mkiwa hamjapata chochote ilihali hamfanyi kazi hii kizalendo mseme mmekufa kishujaa, nikifa mimi shirika zima na ukanda huu wote utanitukuza N001 kafa kishujaa kwa kufa pamoaj na madhlimu" Norbert aliwapa somo lisilohitaji mtaala ambalo liliwaingia hadi kwenye mioyo yao maadui zake wakabaki hawana la kusema.
                    "saa yangu ilipotoa mlio wa Alarm niliwaambia kwamba hiyo ni automatic alarm, si kweli bali ilinitaka niactivate hili bomu na mimi nikabonyeza ili kuactivate. Hii ndiyo remote ya hili bomu" Norbert aliwaambia huku akiwaonesha saa yake, maadui zake mbinu zote waliishiwa wakajikuta wakihema kwa kihoro cha kuogopa kufa.
                    "ndani ya dakika hizo wote tutakuwa marehemu humu ndani, mkitaka tupone wote basi muambieni, Huyo askari aliyekuwa yupo nyuma yangu afungue mlango anipishe nitoke.Pia napenda mtambue kama mkinipiga risasi hakuna atakayeweza  kulitegua bomu lenye huu waya ulio na mawasiliano na mishipa ya neva zangu. Mkiniua tu nalo linalipuka na litateguka lenyewe nikifika umbali wa kilomita mbili kutoka hapa, sasa uchaguzi wenu msuke au mnyoe" Norbert alizidi kuwatangulia kujanja.
                      "Hisani hebu mfungulie mlango huyo" L.J Ibrahim alijikuta akitii masharti ya Norbert na yule mwanajeshi aliyemleta Norbert alipiga saluti akafungua mlango, Norbeet alipoona mlango umefunguliwa alivua saa yake ya mkononi akawarushia maadui zake ambapo saa hiyo ilidakwa na Santos akaitazama akakuta ikihesabu dakika kama za kwenye bomu.
                   "Saa hiyo ni remote kwa ajili ya kutega na kutegua tu na siyo remote kwa ajili ya kulipua, hivyo msijidanganye kama mnaweza kuniua nayo. Pia inaweza kutegua bomu hili ikifika nusu ya dakika zilizowekwa lilipuke" Norbert aliongea huku akigeuka nyuma, alitembea hadi mlangoni akiwa na tabasamu la ushindi baada ya kuwazidi maadui zake ujanja.
    Alipofika mlangoni alichomoa ufunguo akatoka kisha akawafungia mlango kwa nje maadui zake, alienda hadi kwenye gari lake na akaingia akaliwasha akaweka gia akaondoka kuelekea getini ambapo mlinzi alimruhusu bila kipingamizi chochote. Norbert alitoka ndani ya ya nyumba ya L.J Ibrahim akaingia barabarani kwa kasi kuhofia wasije maadui zake wakampuuza na kuanza kumfuatilia, kuendesha kwake kwa kasi kituo cha kwanza ilikuwa ni makumbusho ambapo  alitoa koleo kisha akakata waya mmojawapo wa bomu hilo halafu akaivua ile tai akaiweka kando. Aliendelea kuendesha gari kwa kasi huku akiwa  akipitia njia za panya nyingi kuliko barabara kuu kuhofia kufuatiliwa, alizunguka mitaa tofauti ya jiji la Dar es hadi pale alipohakikisha yupo kwenye amani ndipo akaelekea kwenye nyumba ya kampuni yake.

****

    Baada ya Norbert kuondoka huku nyuma wote kwa pamoja ndiyo hasira ziliwarejea wakaona kama wamevuliwa nguo kwa jinsi walivyomkosa Norbert, walibaki wakiwa wamechoka pasipo kufanya kazi ngumu yoyote  ambayo ingewafanya wachoke. Kila mmoja alikuwa akiugulia kivyake hasira zilizokuwa zikimfurukuta ndani ya moyo wake baada ya kuzidiwa ujanja na bingwa wa ujanja, uchungu dhidi ya kuzidiwa ujanja ulikuwa mkubwa sana kwa Benson hadi akajikuta akilia akiona Mungu alikuwa akimyima fursa ya kulipiza kisasi cha kuuawa pacha wake na Norbert.
    Alijikuta akiufuata ule mwili wa rafuiki yake Norbert ambaye ni mwandishi wa habari akaupiga mateke mfululizo, alipochoka alitoa bastola akaanza kuuumiminia risasi hadi bastola ilipofyatuka chuma kilichopo nje  ya bomba kurudi nyuma baada ya risasi kuisha. Alipiga kelele kwa nguvu kama kichaa na akarudia tena kuupiga mateke mwili wa yule mwandishi wa habari waliyemtumia kumnasa Norbert, aliona haridhiki  na  kuupiga huko mwili huo akaufungua kamba ngumu walizokuwa wamemfunga kisha akaulaza chini. Aliutazama mwili huo huku akihema kama kama nyoka aina ya kobra akiwa anajianda  kumkabili adui, aliukanyaga tena mwili ule hadi ukawa unatoa majimaji mdomoni lakini bado hasira zake za kumkosa Norbert hazikumuisha hata kidogo. Aliwatazama wenzake ambao walikuwa wakimtazama kwa masikitiko sana kwa jinsi alivyokuwa na hasira sana, walikuwa wamemuacha aupigwe huo mwili anavyotaka na alipoacha kuupiga huo mwili wakajua  tayari alikuwa kumbe bado hasira zilikuwa zipo ndani ya nfsi yake.
    Benson alipoacha kuwatazama wenzake alirudisha macho yake kwenye mwili wa mwandishi wa habari rafiki yake Norbert ambao ulikuwa hautambuliki na wala haufai kutazamika kwa macho ya kawaida, alipoutazama ule mwili alikuwa kama ndiyo anamuona Norbert  ambaye ndiye adui yake mkubwa. Hasira zake zilizidi mara dufu hasa baada ya taswira ya maiti ya pacha yake kumjia kichwani , alijkuta akijisachi kiunoni akatoa kisu cha  kufungua na kujifunga kisha akawa anauinamia ule mwili akiwa ameshika kisu akikielekeza upande wa nchi yake chini. Alikuwa tayari ameingiwa na roho yenye zaidi ya unyama na ukatili zaidi hata wa Simba anaporarua mawindo yake. Alikuwa akidhamiria kufanya jambo baya zaidi katrika mwili huo ambalo kwa binadamu wa kawaida halimpasi kufanya, jambo halikuwezekana kufanyika kwani Thomas alimuwahi kwa kumpokonya kisu akakitupa kutoka sebule hiyo hadi sebule ndogo ya kulia chakula ambayo nayo samani zilikuwa zimetolewa.  Wilson naye alimuwahi kwa haraka akamshika madhubuti asiendelee kufanya ukatili ambao haukuwa na tija yoyote kwa maiti hiyo, Benson  aliishia kufurukuta akirusharusha miguu lakini Wilson hakuwa tayari kumuachia.
                  "nasema niachie mimi huyu mshenzi nimtie adabu" Benson aliongea kwa hasira huku akilia.
                  "Come on Benson huyu reporter ana kosa gani?!" Thomas alimuuliza kwa sauti ya juu, muda huo huo saa ya Norbert iliyokuwa ipo mikononi mwa Santos ilitoa mlio kisha ikawaka taa kwenye kioo, Santos alipotazama kwenye kioo alikutana na  taswira ya mkono wa binadamu ikiwa umeonesha alama ya dole la kati apamoja na maandishi yaliyoandikwa 'LOSER'
                   "Damn Norbert!" Santos aliongea kwa hasira huku akiibamiza saa hiyo kwenye marumaru.

*WAJANJA WAMEJANJIWA
*MAMBO YAZIDI KUWA MABAYA KWA MABAYA KWA UPANDE WA MAADUI WA TAIFA
*MCHEZO BADO MBICHI KWAO

USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA KUJUA WACHIMBA KISIMA WAMEFANIKIWA KUTOKA AU NDIYO WANADIDIMIA NDANI YAKE.



*Mtafutanoo

No comments:

Post a Comment