RIWAYA: WAKALA WA GIZA
MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA
SIMU: +255713776843
+255762219759
WHATSAPP: +255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA
______________+18__________________
SEHEMU YA ISHIRINI
Ilikuwa ni siku maalum ya kukutana na Josphine tangu alipoagana naye kwa mara ya mwisho siku ya jumamosi, pia zilikuwa zimebaki siku tatu na masaa mawili nchi ya Tanzania iingie katika mikono ya kijeshi chini ya Luteni Jenerali Ibrahim.
Siku hiyo Norbert aliamua aende katika nyumba anayoishi Josephine akiwa na akili nusu hofu nusu amani, alitumia dakika shirini akawa tayari yupo ndani ya eneo la Keko Michungwani. Hapo alimpigia simu Josephine aje amfuate katika muda huo wa usiku kisha akatulia amsubiei Jospine aje baada ya kumpa taarifa.
****
Baada ya dakika takribani tatu mlango wa pembeni ya kiri cha dereva wa gari hiyo ulifunguliwa, Joseohine aliingia ndani ya gari hiyo akiwa amevaa kaptula fupi ya kitambaa kigumu(kadeti) ambayo ilikuwa ya rangi ya kahawia. Alikuwa kavaa na vesti nyeupe kwa juu iliyofanya matiti yake machanga yaonekane vyema, umbo lake la kibantu lilikuwa limeonekana vyema na nguo hizo alizovaa ambalo lilimfanya Norbert asiache kumtazama hadi alipoketi kwenye kiti ambapo mzigo wake wa nyuma ulitawanyika katika kiti hicho ukafanya umbo lililojengeka chini ya kiuno chake sehemu ya mapaja lionekane pana sana kutokana na kaptula aliyovaa kumbana sana.
Ilikuwa ni kaptula iliyoishia katika eneo la chini ya goti ambayo ilifanya mguu wake uliojaa uonekane vyema kwa Norbert ambaye alikuwa anatabasamu akimtazama tu, Norbert muda huo macho yake yalitua sehemu za kati ya mapaja kisha akayashusha mapajani akaweka mikononi katika mapaja hayo ambapo alimfanya Josephine amtazame kwa macho yenye aibu malegevu sana. Kitendo cha Josephine kumtazama Norbert kwa macho malegevu ilikuwa ni nafasi tosha ya Norbert kupeleka kinywa chake kwenye kinywa cha Norbert ambapo kilipokewa vizuri, walibadilisha shurubati ya kinywa a uchu humo ndani ya gari hali ambayo iliwafanya wadumu kwa muda mrefu hadi pale Josephine alimpomtoa Norbert kwa kumrudisha nyuma kifua chake kwa mikono yake laini.
Norbert aliporudishwa hivyo nyuma aliamua kuleta kinywa chake kikafanikiwa akaendelea kubadilisha shurubati hiyo ya kichwa kwa muda mfupi kisha akautoa mdomo wake akuhamiaha jirani na sikio la Josephine, alilibusu kwa busu la muda mrefu sikio hilo sehemu ya juu ambayo ilimfanya Josephine ajihisi hali tofauti iliyomlazimu amrudishe tena Norbert nyuma kwa kutumia mikono yake laini ya kirembo.
"Nor bwana si tunaenda kwangu hebu acha" Josephine alilalamika kwa sauti inayotoka puani, Norbert naye akisitisha zoezi hilo ambalo lingefanya gari hiyo ibebe vurumai lao muda mfupi ujao. Aliwasha gari kisha akaliingiza barabarani akaendesha kwa kufuata maelekezo ya Josephine, safari yao iliishia kwenye nyumba ya kawaida ambayo ilikuwa na uzio wa matofali uliokuwa umechakaa kuoneaha ulikuwa umejengwa siku nyingi sana. Norbert alisimamisha gari katika lango la nyumba hiyo lililojengwa kwa namna ya kisasa ingawa uzio ulikuwa wa kizamani, Josephine alishuka ndani ya gari akaenda kwenye lango hilo ambalo alilifungua kwa ufunguo alioutoa mfukoni mwake.
Alilifungua lango lote na Norbert akaingiza gari hadi ndani katika mandhari nzuri yenye maua, ilikuwa ni ndani ya nyumba ya kawaida ambayo ilikarabatiwa ikaonekana ni yenye kupendeza. Norbert alipeleka gari hadi kwenye maegesho ya nyumba hiyo kisha akalizima, alishuka ndani ya gari akafunga milango akamkuta tayari Josephine alikuwa amemalizia kufunga geti na yupo nyuma ya gari akimsubiri ashuke.
"Karibu sana mpenzi hapa ndiyo kwangu" Josephine alimkaribisha Norbert ambaye alizungusha macho katika mazingira ya nyumba hiyo kisha akatabasamu.
"asante mpenzi umejitahidi sana" Norbert aliongea kisha akajisogeza karibu ya Josephine zaidi akawa anatazamana naye usoni, aliweka mikono kiunoni mwa Josephine lakini ilitolewa kwa kimadaha na Josephine ambaye aligeuka nyuma akaanza kupiga hatua kuelekea kilipo kibaraza cha nyumba yake.
Norbert hakulitilia maanani suala hilo ingawa alishagundua hali tofauti tangu wapo ndani ya gari yake Josephine alimpomfuata, alimfuata Josephine kwa nyuma hadi kwenye kibaraza cha nyumba hiyo. Josephine alitoa ufunguo ndani ya mfuko wa kaptula yake akafungua mlango wa nyumba hiyo, alimuashiria Norbert akaribie ndani akiwa na tabasamu pana usoni mwake.
Norbert alipokaribishwa alichungulia ndani eneo la sebuleni kisha akasita kuingia hali iliyomshangaza nwenyeji wake, mshangao wa Josephine katika kumshangaa huko yeye aliutumia kama nafasi nyingine akampiga busu refu sana linalohusisha kukutanisha kwa ndimi vinywani. Josephine hakutarajia busu hilo la ghafla na alibaki anashangaa zaidi hata alipoachiwa mapigo yalimuenda mbio sana akabaki anatazama Norbert kwa jinsi alivyotumia nafasi ile, Norbert yeye alibaki anatabasamu tu alipofanya kitendo hicho kisha akachuchumaa kwa kuugemea mguu mmoja.
"Ni nyumba ya mke wangu yenye mandhari safi hivyo sipaswi kuingia na viatu" Norbert aliongea huku akianza kufungua kamba za viatu, Josephine alimzuia kisha akainama akafunga ile kamba ya kiatu ambayo Norbert rayari aliifungua.
Alimshika mkono kisha akaingia naye ndani wakatokea kwenye sebule pana yenye makochi ya kisasa, ilikuwa ni sebule pia yenye madirisha yaliyobeba mapazia yenye mtindo wa kisasa wa kuwekwa vyuma. Mandhari hiyo ilipendeza zaidi na Norbert alibaki akiishangaa tu hadi pale Josephine alipomvuta aende kuketi kwenye kochi la kuketi mtu mmoja, Norbert aligoma kwenda kuketi kwenye kochi hilo la mtu mmoja kisha akalitazama kochi jingine linalotazamana na kochi lile.
"nafasi ya kukaa karibu na wewe nitaipata wapi ikiwa nitakaa kwenye kochi hilo, ngoja nikaketi kwenye kochi lile pale" Norbert alisema kisha akaenda kuketi kwenye kochi kubwa lilipo mkabala na kochi la mtu mmoja pia lipo mkabala na mlango.
Kochi hilo liililokuwa lipo mbele ya dirisha lililofungwa na pazia zito kwa umbali wa sentimita kadhaa ndiyo lilimshawishi Norbert akae alipoingia ndani ya sebule ya nyumba hiyo.
"nikuletee kinywaji gani laazizi?" Josephine aliuliza.
"Chochote ukipendacho wewe na mimi nitapenda" Norbert alijibu.
"Basi mimi napenda pegi za gongo sijui utakunywa" Josephine alitania.
"mh!" Norbert aliguna na Josephine alicheka kwa nguvu sana.
"mwaya nakutania ngoja nikuletee wine nafikiri utaipenda" Josephine aliongea.
"Yap ninaipenda tena kwakuwa hiyo ndiyo uliyoichagua" Norbert aliongea huku akitabasamu na Josephine alitoka akaelekea katika ukumbi mefu uliopo jirani na sebule na aliporudi alikuwa kabeba sahani kubwa aliyofunikwa pamoja na chupa ya mvinyo iliyowekwa bilauri kwa juu ili iwe rahisi kubebwa pamoja.
Aliviweka vitu hivyo kwenye meza ya kioo ya kisasa ambayo ilikuwa ipo jirani na Norbert ambaye alibaki anatabasamu tu, aliisogeza meza jirani na Norbert huku akitingishika sehemu zake za mapambo. Josephine alifunua mfuniko wa sahani ambayo alikuja nayo na hapo ndizi zilizokaangwa vizuri pamoja na nyama za kukaanga zikaonekana, pembeni kulikuwa kuna kisu na uma pamoja na kachumbari iliyotayarishwa vizuri.
Josephine alipovitenga hivyo vitu alinyanyuka tena akaelekea jikoni ambapo alirejea akiwa na jagi la maji lililowekwa kwenye beseni dogo, jagi hilo alimmiminia Norbert maji ili anawe mikono kisha akakinga beseni chini yake maji yamwagikie.
"Karibu mume wangu mtarajiwa" Josephine alimkaribisha Norbert ambaye aliishia kutabasamu tu kisha akafungua chupa ya mvinyo akaumimina kwenye bilauri, Norbert hakutaka kufanya ajizi alichukua kisu akazikata ndizi vipande halafu akachukua uma akachoma kipande kimoja cha ndizi kisha akakitia kachumbari.
Alikipeleka mdomoni akasita kisha akamuita Josephine ambaye alijongea akaketi jirani naye, Norbert alimtazama Josephine kwa tabasamu kisha akautazama uma ambao ulikuwa umebeba kipande cha ndizi ambacho kingemtoa mate mtu yoyote kutokana na kachumbari iliyopo juu yake.
"Ikiwa kwa sasa tumefanikiwa kuwa pamoja basi chakula hiki yatupasa kuonja pamoja, mwanamke mpishi mzuri kuliko wote huwa anaonja chakula chake akiwa mbele ya mpenzi wake" Norbert alimuambia Josephine huku akimpelekea uma wenye ndizi mdomoni, Josephine aliushika mkono wa Norbert kumzuia huku akimlegezea macho.
"Kwa ajili yako baby haina haja ya kuonja kwani najiamini nimeandaa kitu special for you, nikionja mbele yako means sijiamini na pishi langu" Josephine aliongea.
"siyo hivyo baby maisha nikushare kila kitu kasoro mavazi tu hivyo chakula tunashare pamoja, kula please" Norbert alimuambia huku akimsogezea uma wenye ndizi jirani na mdomo huku akimtazama Josephine kwa macho makini, mboni za macho ya Josphine zilikuwa zisizotulia hata kidogo na zilikuwa zinachezacheza kama mbegu ya sufi ikiwa inapulizwa na upepo mwingi.
Alizidi kumsogezea uma karibu na mdomo wa Josephine ambaye alikuwa amefumba mdomo hakufungua, alipofikisha uma ule kiasi cha nusu sentimita kutoka zilipo papi za midomo ya Josephine alihisi kitu cha baridi kikugusa kichwa chake mbele ya sikio.
"Welcome Kaila(Karibu Kaila)" Norbert alisikia ikitoka upande ulipo pazia na alipopeleka jicho pembeni aliona bastola ndefu ikiwa imegusa kichwani, pazia lilifunguliwa na Benjamin akaonekana akiwa yupo nyuma ya pazia .
Muda huo Josephine aliutoa mkono wa Norbert kwa taratibu uliokuwa umeshika umma ili kumlisha akaushusha chini huku akitabasamu, aliinuka akamtazama Norbert ambaye alikuwa alikuwa anahema kwa nguvu sana. Josephine aliachia kicheko cha nguvu sana kisha akamtazama Norbert kwa dharau sana, Norbert aliinua macho ya mshangao kumtazama Josephine ambaye ndiyo kakolewa na kicheko.
"Josephine ni wewe kweli?" Norbert aliuliza kwa macho yanayoonesha kutoamini kwa kile kilichotokea.
"Ndiyo mimi Josephine ukipenda niite Leopard Queen nafikiri unanitambua Norbert Kaila wa East Africa Security Agency kwa kifupi EASA, siku zote ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu Norbert. Jumamosi ulinikimbia lakini leo nimekutia nguvuni huna ujanja wa kunikimbia sasa lazima ufe ka.." Josephine aliongea kwa majigambo na alikatishwa na Norbert aliyedakia maneno yake.
"Kama ulivyowaua wanajeshi waliyokuwa wanalinda nyumba yA General kule Muhimbili" Norbert alidakia akamshangaza Josephine, aliupuuzia mshangao wa Josephine kisha akaendelea "Ulifikiri mchezo wenu wa kitoto sitaujua Josephine, wakati naingia humu ndani uliponifungulia nilichungulia kisha nikarudi nikashika kamba za viatu nikaanzaa kufungua nivue viatu. Sikutaka kuvua viatu Josephine bali nilizuga kwa chungulia mazingira ya humu ndani yakoje ndiyo nikaingia" Norbert aliongea huku akitabasamu tofauti na alivyokuwa na uoga hapo awali.
"Tena nimechungulia kupitia tundu la pazia kutumbukiza chuma niliweza kumuona huyu bwana kupitia kofia aliyovaa kujitokeza sehemu hiyo, bado nilivyoingia ndani ukanipeleka nikakae pale kwenye kochi la mtu mmoja lakini niliamua kuja kukaa hapa si kama nimepapenda bali ili nipachunguze kwani najua kwenye pazia kuna mtu. Nilipoinuka kwenye kochi lile kuja hapa niliona kochi hili lipo mbele ya pazi kiasi cha sentimita kadhaa tena limeburuzwa muda si mrefu na alama za kuburuzwa kwake nikaziona kwenye tiles" Norbett aliongea maneno ambayo yalizidi kumshangaza sana Josephine, alipoangalia pembeni mwa kochi alilokaa Norbert aliona kweli alama za kuburuzwa.
Alibaki akimtazama Norbert aliyekuwa anatabasamu usoni mwake ingawa alikuwa amewekewa bastola kichwani na Benjamin, alijilazimisha kutabasamu lakini bado mshangao wake juu ya akili za Norbert ulibaki palepale hakutegemea kama anagekuwa na uwezo wa kufikiria kiasi kile.
"Nesi aliyekuona ukitoka pale wodini baada ya wewe kuua wale wanajeshi alituambia sifa zako zote zilivyo nikakuchora nikaipata sura yako kamili, ulidhani nitadanganyika nilipokuwa nawe" Norbert alizidi kuongea huku akimtazama Josephine kwa dharau.
"Hey! You talked too much but today you will die , thanks my love for your help. Now eat your food( Hey! Umeongea sana lakini leo utakufa, asante mpenzi wangu kwa msaada wako. Sasa kula chakula chako" Benjamin aliongea huku akimtazama Josephine kwa sekunde kadhaa alimpompa shukran, alitoa usalama wa bastola kisha akamuamrisha Norbert ale chakula alichoekewa.
Norbert aliposikia amri hiyo alimtazama Josepbine ambaye alikuwa anamtazama kwa tabasamu la kejeli kisha akanyanyua ule uma aliouchoma ndizi, Norbert aliunyanyua ule uma akaupeleka kinywani mwake taratibu na akazidi kumuona Josephine akitabasamu. Alipoufikisha karibu na kinywa chake alisita kisha akausogeza kando ya mdomo, alitoa tabasamu pana huku akimtazama Josephine ambaye ndiye aliyemleta katika mdomo wa kifo.
"Wait, your love and my love too. Oooh! Our lover(Subiri, mpenzi wako na mpenzi wangu pia. Oooh! Mpenzi wetu)" Norbert aliongea huku akitabasamu kama kawaida yake.
"Stop talking nonsense Norbert eat your food (acha kuongea yasiyo na maana Norbert kula chakula chako)" Benjamin aliongea huku akimkandamiza Norbert na mdomo wa bastola ambao umetengenezwa kwa chuma.
"Siyo nonsense Benson mpenzi wangu kwakuwa nimelala naye na wewe ni mpenzi wako kwakuwa umelala naye, au Josephine naongopa?" Norbert alizidi kuongea maneno mengi yaliyowazubaisha maadui zake, moyo wa Josephine uliposikia maneno hayo ulipiga kwa nguvu kama ulikuwa unapasuka kwani Norbert alikuwa ameanika mengine mbele ya mpenzi wake ambaye hakumruhusu kulala na Norbert ili awekewe mtego.
Maneno hayo yaliibadilisha sura ya Benjamin akawa ni mwenye hasira alipoyasikia kwani hakutegemea kama Josephine atafanya hivyo, macho yake yalikazika kutokana na matuta kujitokeza katikati ya nyusi zake.
"Benjamin usimsikilize huyo muue anapoteza muda tu" Josephine aliongea kwa kubabaika kwani alijua Norbert tayari alikuwa amevuruga mambo.
"Ohooo! Kumbe Benjamin na siyo Benson, mapacha nyinyi inaonekana. Sasa muulize mpenzi wako ijumaa alilala wapi?" Norbert alizidi kupigilia msumari katika hasira ambazo tayari zilikuwa zimepanda kichwani mwa Benson, maneno hayo yalimfanya Josephine azidi kushtuka akaanza kurudi nyuma akawa anaelekea eneo ambalo kuna kabati iliyowekwa luninga na video ya santuri.
"Bitch! You slept with him! ( Malaya! Umelala naye!)" Benjamin aliongea kwa hasira kisha akaihamisha bastola kutoka kichwani mwa Norbert akamuelekezea Josephine akiwa ameweka kidole sehemu ya kufyatulia, ilikuwa ni nafasi ambayo Norbert alikuwa akiisubiri kwa hamu sana aweze kujinasua kwenye mtego ule.
Nafasi hiyo hakutaka kuichezea kabisa aliamua kuitumia vile ipasavyo kwa mtu mwenye silaha ambaye angekuwa hatari kwake akimuachia, Benjamin aliponyoosha mkono wenye bastola kumuelekea Josephine alifyatua risasi kwa haraka sana ambayo alilenga kumpiga nayo huyo binti huyo kwenye paji la uso lakini ilimpata ya bega baada ya Norbert kuudaka mkono huo akiwa na lengo la kumzuia. Norbert alipoudaka mkono wa Benjamin kwa kasi ya ajabu alimuinua juu kwa mtindo wa judo kisha akamwangusha juu ya meza ya kioo iliyokuwa ipo mbele yake, lilikuwa ni pigo ambalo lilimnyamazisha Benjamin papo hapo baads ya kukatwa na vioo na kichwa chake kupigizwa kwenye kioo kigumu.
Norbert alimtazama Benjamin ambaye alikuwa anavuja damu kisha akachukua bastola yake ambayo bado ilikuwa na risasi, alimsogelea Josephine ambaye alikuwa ameanguka chuni baada ya kupigwa risasu huku akimnyooshea bastola.
"Norbert usiniue tafadhali" Josephine aliongea huku akijishika jeraha lililojeruhiwa na risasi ilitofayatuliwa na Benjamin ambayo ilikuwa impate kichwani.
"Laiti ningetaka ufe basi ningemuacha huyo bwana wako aumwage ubongo wako" Norbert aliongea huku akikichuchumaa mbele ya Josephine akawa anamtazama kwa huruma, aliitazama na bastola ya Benjamin yenye kiwambo cha kuzuia sauti kisha akashika Josephine nyuma ya shingo.
"Ukawape salamu kuwa N001 hakamatwi kijinga namna hiyo" Norbert alimuambia Josephine ambaye alishtuka baada baada ya kusikia namba ya mpelelezi hatari wa EASA ambaye hakuwa anamjua kwa sura, mshangao wake huyo ulizimwa na busu zitO lisiloashiria upendo kutoka kwa Norbert ambalo Josephine alilipokea bila kupenda. Norbert alipomaliza kumpiga busu hilo alimuongeza na kitako cha bastola cha kisogoni, Josephine alizirai papo hapo.
Norbert alimpekua Josephine mifukoni mwake akatoa simu ambayo alipekua kwenye ujumbe wa maneno hadi alipopata namba ambayo aliitilia shaka, aliipiga namba hiyo na aliiweka simu sikioni ilipoanza kuita.
"Siyo Leopard Queen ni N001 hapa nimepita nyumbani kwa Leopard Queen na Benjamin njoo uchukue masalia" Aliongea baada ya simu kupokelewa kisha akakata pasipo kusikiliza upande wa pili ulikuwa unssemaje, alipomaliza alichukua funguo za mlango na geti kisha akatoa kitambaa akafuta sehemu zote ambayo alikuwa amegusa kwa mikono yake.
Aliondoka ndani ya eneo hilo akiwacha wenyeji wake katika hali tofauti na jinsi walivyompokea, alitoka nje ya nyumba hiyo na alifungua geti kisha akatoa gari nje halafu akalifunga geti kama zilivyo funguo akazitupa ndani ya uzio.
Aliondoka eneo hilo la Keko kwa kasi sana akiwa na uhakika tayari simu yake ilikuwa imefika mahali husika, tabasamu pana lilikuwa limechanua usomi mwake baada ya kupiga hatua katika kazi yake ya hatari.
****
Simu hiyo aliyopiga Norbert ilipokelewa na Wilson akiwa katika mapumziko kitandani, alikuwa amelala baada ya kufanya jimai na mwenza ambaye alimchukua siku hiyo. Taarifa alizozipokea zilimfanya ashtuke hadi mwenza aliyekuwa naye ambaye alikuwa amelala kifudifudi bila nguo akageuka, mwenza huyo alikuwa ni binti mdogo sana wa miaka chini ya ishirini na tano. Alikuwa ni binti mchanga kabisa ambapo kifua chake kilionekana dhahiri kutokana na kutokuwa na nguo, binti huyo alimtazama Wilson jinsi alivyoshtuka kisha akamshika mabegani mwake kwa upendo baada ya Norbert kukata simu.
"Baby kuna nini jamani mbona hivyo?" Binti huyo alimuuliza Wilson kwa upendo mkubwa huku akilegeza sauti.
"Matatizo ya kibiashara tu Farida, inabidi nitoke nikaonane na washirika wangu ili tuyaweke sawa usiku huu huu" Wilson aliongea huku akinyanyija kitandani.
"Jamani mpenzi kwahiyo itakuwaje?" Farida aliuliza.
"Usiwe na hofu Farida tutakutana siku nyingine ngoja nikupe ya matumizi, asubuhi wewe nenda chuo tu ukaendelea na masomo" Wilson aliongea huku akivaa nguo zake, alipomaliza aliingiza mkono mfukoni akatoa kitita cha pesa ambacho alimpatia Farida kisha akambusu mdomoni binti huyo ambaye angeweza hata kuwa mpwa wake.
Wilson hakutaka kupoteza .muda alichukua funguo zake za gari akatoka chumbani humo usiku huohuo, alitembea kwa haraka hadi yalipo maegesho ya magari akaingia ndani ya gari yake akaiwasha akaiondoa eneo hilo
TUKUTANE TENA JUMAPILI PANAPO UHAI NA AFYA NJEMA
HAIRUHUSIWI KUNAKILI RIWAYA HII KWA NAMNA YOYOTE PASIPO RIDHAA
YA MTUNZI
No comments:
Post a Comment