Wednesday, November 16, 2016

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA TATU



     

 RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

       SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




     SEHEMU YA TATU!!

           "nafikiri tu..." Moses aliongea lakini alishindwa kumalizia kauli yake baada ya simu ya Norbert kuita, Norbert alizuia Moses asiongee kisha akapokea simu akasikiliza bila kusema kitu hadi ikakatwa.

     Aliirudisha aliweka simu yake kisha katikitisa kichwa chake  halafu akavuta pumzi kwa nguvu akaiachia akmtazma Moses.



      "kuna nini?" Moses aliuliza

       "Mufti mkuu wa Dar es salaam amekutwa amefariki ofisini kwake na mwili ni kama wa Askofu Edson" Norbert aliongea kisha akanyanyua macho juu kutazama dari la ofisi.

       "Shit!" Moses alisema huku akipiga ngumi mezani kwa nguvu


****

    Kwa mara ya kwanza alianza kuufikiria uamuzi wake wa kutoa dawa ya Quantanise hapo ndipo akabaini kwamba alifanya kosa, ilikuwa imeshatokea na hana muda wa kurekebisha ili isitokee na alitamani hata muda urudi nyuma aweze kurekebisha pale alipokosea. Kumpa Askofu Edson zile kemikali lilikuwa ni kosa kubwa ambalo anaona amelifanya na alizidi kujuta zaidi kwa kumpatia kemikali, kwani isingetokea yeye kumpatia hiyo dawa hayo yasingetokea.

    Hakuhisi kabisa kama mtumishi yule wa mungu angeweza kuwa na uhusika na watu wanaofanya mauaji hayo kwa kutumia kemikali hizo, kilichomjia ndani ya fikra zake ni kwamba Askofu Edson alifanyiwa mchezo mchafu wa kunyang'anywa kemikali hizo na watu hao wanaofanya mauaji kisha akauawa kwa kutumia kemikali hizo ambazo zilikuwa katika mikono yake. Majuto yake yalikuwa zaidi katika kumpatia kemikali hizo usiku kwani alibaini ndiyo kosa pekee aliloweza kulifanya, alitamamni muda urudi nyuma ili amzuie afuate asubuhi kwani aliamini angekuwa ameweza kumuokoa na mambo mengi na hata kuokoa balaa ililokuwa lipo mbioni kumkaribia la kutumika kitu kilivumbuliwa na mikono yake kwa kupoteza uhai wa watu wengine wasio na hatia kabisa.

    Moses aliwaza sana na kuwazua juu ya suiala hilo kwani lilikuwa likiekea kumchafulia jina lake na heshima yake ambayo amejijengea Tanzania kutokana na kazi zake ambazo anazifanya kwa ajili ya Taifa lake, aliona kuna jambo la hatari ambalo lilikuwa likimjia kwa muda huo yey na familia yake ijayo hivyo alihitaji kufanya kitu kwa manufaa ya familia pia aepushe balaa ambalo lionaelekea kumkumba ndani ya muda huo.

    Alipozidi kulifikiria suala hilo alijikuta akiinuka kwenye kiti alichokuwa ameketi akaelekea dirishani ambapo aliangaza macho nje huku mikono akiwa akiwa ameshika kiuno chake, hali aliyokuwa nayo Moses kwa muda huo ilimfanya hata Norbert amtazame sana kwani alihisi kuna jambo zaidi linamtatiza ukiachana na hilo la vifo vinavyotokea.

          "Dogo vipi mbona una mawazo sana au hii ishu imekutachi sana?" Norbert alimuuliza Moses kutokana na hali aliyokuwa nayo baada ya kupokea taarifa hiyo ya kufa kiongozi wa dini ya kiislamu.

           "hii ishu itachukua sura mpya zaidi tofauti hata unavyoifikiria kaka, nahisi itamletea matatizo hata mke wangu kwani ni mjamzito sasa hivi" Moes alimuambia Norbert huku akitazama dirishani na hakujighulisha kumtazama kwani mawazo aliyokuwa nayo ndiyo yalimfanya ashindwe hata kuangalia nyuma alipo Norbert.

           "Dogo nafikiri tuingie kazini tuweze kuwapata hawa wahusika tu haina haja ya kuhofia namalna hiyo" Norbert alimuambia Moses.

           "Hapana broda ujue hii kitu inalenga kunichafua mimi ndani ya jamii hii ninayoheshimika, hebu fikiria mauaji hayo yanayotokea kutoka kwa viongozi wa dini tofauti kwa kutumia kemikali ambayo ni sumu niliyoitengeneza mwenyewe kwa mikono yangu ikijulikana na wanachi itakuwa vipi? Kama si kudhani mimi ndiyo nahusika na mpango huu wote na hapo hasira zote za waumini wa dini zote zitanigeukia mimi, fikiria mke wangu atakuwa kwenye hali gani kaka na watu watatuchukulia hatua gani?" Moses aliongea kwa hisia sana huku akigeuka akimtazama Norbert machozi yakiwa yanaanza kumlenga katika macho yake lakini hayakutiririka kudhihirika wazi ionekane kama ni yupo ndani ya kilio kutokana na suala hilo.

             "mojawapo ya sheria ya kijasusi inasema, usiruhusu hisia za moyo wako zikutawale katika mambo kama haya Moses. Kumbuka wewe intelligence hivyo akili zinatakiwa ziwe nyingi kuliko hisia za moyu mdogo wangu. ukifuatisha hisia ni mwanzo wa kuharibu na pia kujiharibia na hata kuhatarisha maisha ya wengine na maisha ya Beatrice. Unatakiwa umlinde kwa akili zako za kijasusi na siyo ufuate hisia mdogo, wewe ni mtu mwenye akili sana na ndiyo maana ulistahiki kuitwa shujaa ulipoharibu mipango ya Browan Stockman alipotaka kuiletea maafa Tanzania na sifa hiyo imekufanya uwe ndani ya kazi hii" Norbert alimsihi Moses kutokana na kutaka kutenda kosa ambalo ni kinyume cha kanuni za kijasusi, ushauri huo ulimrudisha Moses kwenye hali yake ya kiwaida kabisa baada ya kushusha pumzi ndefu akionesha kuwa ushauri ule ameuafiki.

               "Asante, nafikiri ni muda wa kucheza na akili zaidi" Moses aliongea.

              "Tuanze kupunguza hofu zako kwanza then,  mengine yatafuata dogo" Norbert aliongea.

               "hilo nalo ni la muhimu ngoja nifanye mpango wa ghafla wa kupunguza hofu yangu tukitoka hapa, halafu kuna kingine cha ziada inabidi tukijue" Moses aliongea huku akikuna kichwa kama ilivyo kawaida yake akifikiria mawazo chanya.

               "sema tuanze kazi mara moja, ari ishanijia " Norbert alimuambia huku akitabasamu.

              "cha kwanza kabisa inabidi twende kwenye bandari ndogo ya boti zinazoenda Zanzibar kuna kitu kimenijia kichwani" Moses alisema kisha akamuashiria Norbert waondoke.

              "Ok twende na wazo lako halafu nitakuambia wazo langu nadhani linaweza kuwa endelezo la wazo kama likiwa chanya na pia linaweza kuwa ni jipya kabisa kama wazo lako lisipokuwa chanya, uaminifu kwa mwingine hakuna" Norbert alisema huku akielekea mlangoni.

               "hakika" Moses aliafikiana na maelezo yake hukui akimfuata nyuma.


****


      BANDARINI
    DAR ES SALAAM

     Robo saa tangu Norbert na Moses watoke kwenye ofisi ya Norbert maeneo ya bandarini upande wenye boti ziendazo Zanzibar walionekana watu wawili wenye asili ya kisomali wakiwa wamevaa kinadhifu wakiingia mahala hapo, walielekea hadi wenye uongozi wa bandari hapo wakajitambulisha kam maofisa wa Interpol(INTERNATIONAL POLICE) waliopo hapo kwa kazi maalum. Maofisa hao walijitambulisha pia kwa kiongozi husika waliomkuta kisha wakaeleza shida yao iliyowapeleka hapo, walieleza umuhimu wa kitu wanachokitafuta ndiyo maana wakafika hapo kwa ajili ya usalama wa Taifa hili kwani limevamiwa tayari.

          "Kusema kweli jana usiku kuanzia saa mbili hakukuwa na boti ya kampuni yoyote iliyotoka hapa bandarini na wala hakukuwa na boti yoyote iliyoingia muda huo hapa bandarini, siku ya jana boti zote zilifanya safari mapema tu tofauti na siku nyingine kwa hofu ya machafuko ya bahari wakati wa usiku kama ilivyotangazwa na mamlaka ya hali ya hewa. Uongozio wa bandari ulichukua tahadhari mapema sana kwa kuzuia makampuni yote yenye kumiliki Boti za safari kwa bahari ya hindi zisifanye safari zake kuepusha ajali zenye kuweza kuepukika" Kiongozi husika waliyemkuta hapo kwenye uongozi wa bandari aliwapa maelezo.

            "Ok, je tunaweza kuziona rekodi zinazoonesha juu ya suala hilo" Mmoja wa maofisa wa Interpol aliuliza.

             "bila shaka mnaweza kuziona ngoja niagize kitabu chenye rekodi hizo kiletwe" Kiongozi huyo aliongea kisha akanyanyua mkonga wa simu uliopo mezani kwakole akabonyeza tarakimu mbili kwenye simu hiyo akaongea,"leta record book ya safari za jana"
Alirudisha simu mahala pake na muda huohuo aliingia binti mrembo ofisini humo akakabidhi kitabu hicho kwa huyo kiongozi husika halafu akatoka nje huku akisindikizwa kwa macho na mmoja w maofisa wa     Interpol ambaye alionesha kumuangalia sana huyo binti hasa umbo lake la kuvutia. Afisa huyo aliacha kusindikiza binti huyo pale tu alipopotea katika upeo wa macho yake baada ya mlango kufungwa.

             "nadhani mjionee mwenyewe" Yule kiongozi alisema kisha akawasogezea kitabu hicho ambapo kilitazamwa na maofisa hao kwa umakini mkubwa sana halafu wakakirudisha kwa kiongozi huyo.

            "sawa tunashukuru kwa ushirikiano wako, tukikuhitaji hatutasita kukutafuta tena. Nafikiri utatupa msaada zaidi kama huuu ulitupatia leo' Mmoja wa maofisa wa Interpol alisema

            "Hofu ondoeni kuhusu hilo, karibuni tena" kiongozi huyo aliwaaga kwa ukarimu na maofisa hao walitoka katika ofisi hizo za uongozi wakelekea walipoacha gari lao, waliondoa gari lao wakawa wanelekea usawa wa posta ya zamani na walipofika aktika jengo la benki ya taifa ya biashara(NBC) wakaingia kwenye barabara iendayo Posta mpya.

     Walienda kwa mwendo wa wastani kutokana na wingi wa magri hadi kwenye mzunguko wa barabarani wenye sanamu la askari waliuzunguka mzunguko huo wakaingia upande wa kushoto wakafuata barabara ya Samora ambayo iliwapeleka hadi kwenye mtaa wa Ohio ambapo waloinyoosha barabara hadi mtaa wa Mirambo jirani na ubalozi wa Finland na Sweden kisha wakaingia kushoto kushoto. Safari yao iliendelea akwa kuizunguka mitaa ya eneo hilo wakiwa hawana uelekeo maaalum na hatimaye wakaeleka ilipo maabara ya umoja wa mataifa. Waloshuka hapo wakaingia ndani ya ofisi za maabara hiyo wakajitambulisha wakaeleza shida yao iliyowaleta hapo, walipelekwa kwa kiongozi wa ulinzi wa maabara hiyo wakapewa kile walichokuwa wakikihitaji na hapo ndipo alama ya taa ndani ya vichwa vyao iliwajia kutokana na mwangaza walioupata kutokana na kile walichokuwa wakikitafuta.

      Baada ya kukamilisha kila kitu walichokuwa wakikihitaji walichukua sehemu ya ushahidi wakaondoka nayo humo baada ya kutoa shukrani kwa wenyeji wao, walitoka hadi kwenye maegesho ya magari hapo kwenye eneo la maabara hiyo na wakaingia ndani ya gari walilokuja wakaondoka eneo hilo wakiwa na mwaqngaza wa kile walichojkuwa wakikitafuta.


       Jambo ambalo halikujulikana na maofisa hao wa Interpol ni kwamba walikuwa wakicheza na mtu anayejua kucheza mchezo waliokuwa wakiucheza, walipokuwa wanaingia Bandarini na kujitambulisha hakika hawakuwa wamebaini pale kulikuwa na sehemu ya mkono wa mtu wanayecheza naye huo mchezo, hadi wanatoka pale wanaelekea ilipo Maabara ya umoja wa mataifa kwa kuzunguka kwenye mitaa ili wapoteze lengo hawakujua kama walikuwa wnafuatiliwa baada ya sehemu ya mkono wa mhusika wanaomtafuta kutoa taarifa kwenye mwili kupitia mshipa wa fahamu uliounganisha sehemu ya hiyo ya mkono wake iliyopo kwenye ofisi za Bandari na mwili  mzima uliopo mahala pasipojulikana.

       Walipoingia ndani ya maabara hiyo ndipo waliokuwa wanawafuatlia waliwafanyia kitu kingine kwa kupitia kutegeshea vitu kwenye gari lao.

       Maofisa hao walipotoka ndani ya maabara hiyo tayari walikuwa wanafuatwa na kivuli kisichoonekana bila ya wao kujua, gari ya maofisa hao ilienda barabarani kwa mwendo mzuri hadi ilipofika katika mtaa wa Shaaban Robert ndipo mambo yalipobadilika kwani ilianza kuyumba na hatimaye ikagonga sehemu ya uzio wa chuo cha IFM ikatoa Moshi mbele na hakukuonekana dalili ya mtu kutoka ndanio yake.

      Muda huohuo gari aina ford ilifika kwa kasi eneo kisha watu wawili wenye miili iliyojengeka kimazoezi wakashuka haraka sna, walienda kwenye milango  ya gari ya maofisa wa Interpol wakafungua milango wakiwa na uhakika wa kile wanachokifanya na walijua mpango wao. Kila mmoja alizunguka mlango wa upande wake kuifungua kwa upesi na hapo ndipo walipokutana  na kisanga kingine kilichotoka ndani ya gari hiyo, kitendo cha kuifungua milango ya gari hiyo kila mmoja alisalimiana na soli ya kiatu ya pua iliyowayumbisha hadi wakakaribia kuanguka.

     Walipokaa sawa waliwaoana wale maoofisa wawili wa Interpol wenye asili ya kisomali ambao walitofautiana kwa vimo tu wakiwa wamesimama huku wakiwatazama, kitendo cha kuwaona maafisa hao wakiwa na fahamu zao ilikuwa ni jambo la ajabu sana kwao na hapo ndipo walipobaioni kuwa sehemu ya mpango wao haikuwa imefanikiwa.

    Wale maafisa wawili wa Interpol walitaka kuwavamia wote kwa pamoja wawapige lakini walipowatazma wapinzani wao walitambua fika hawakuwa na upinzani wa kutisha kwao hivyo  afisa mmoja ambaye alikuwa amezidiwa urefu na mwenzake ndiyo aliwasogelea  wale watu waliokuja na gari aina ya Ford akiwa hata hajakaa kimapigano, wale watu walimvamia kwa pamoja afisa huyo lakini walijikuta wakisalimiana na ardhi baada  kupigwa mateke mawili ya karate  yaliyopigwa kwa mpigo kutoka kwa Afisa huyo.

    Walijiinua kwa haraka baada ya kubaini wananchi walishaanza kujaa na kama wangepigwa ingekuwa ni aibu, wqalimfuata kwa pamoja kwa mapigo ya karate ili waende nae sambamba lakini waligonga mwamba tena baada ya afisa yule kuja na mapigo ya kininja tofauti na mapigo ya awali. Mapigo hayo yalimvunja mmoja mguu papo hapo akawa hawezi tena kupigana na mwingine aliyebakia akajipa ujasiri akaja kwa kasi bila hata ya kuwa na tahadhari, alipopiga hatua kumfikia yule Afisa alipewa pigo la karate lililompata kwenye pua yake ambalo lilimchanganya hadi akawa hamuoni adui yake na hapo ndiyo ikawa nafasi nzuri kwa yule Afisa kuachia teke liitwalo YOKO GERI KEKOMI(teke hili hupigwa kwa sehemu ya pembeni ya mguu kwa kutumia nguvu nyingikatika kupiga), teke hilo lilitua katika mbavu na hapo ndiyo ikawa mwisho wa yule mtu kupigana na afisa Interpol.

    Muda huohuo ving'ora vya gari la polisi vilisikika na hapo maafisa hao wote kwa pmoja walipiga sarakasi kuruka uzio wa Chuo cha IFM wakazunguka nyuma ya jengo lilloandikwa BLOCK A.

    Baada ya dakika moja  tangu maafisa wale waingie ndani ya uzio  nyuma ya jengo lile Norbert na Moses walionekana na wakitoka katika lango kuu la chuo wakipishana na maaskari waliokuwa wakiingia ndani ya chuo hicho kwa kasi sana, Norbert na Moses walitoka nje wakajichanganya na raia ambao walikuwa wameshajaa eneo hilo wakaondoka bila kujulikana.


   MUDA MFUPI KABLA

    Baada ya Norbert na Moses kutoka katika ofisi za WAHANGA walikuwa wamevaa sura za bandia kisomali pamoja suti nadhifu zenye vitambulisho feki vya Interpol , walielekea hadi bandarini ambapo walikuwa wakifuatilia juu ya suala la linalotaka kumkumba Moses. Walipopata taarifa muhimu wote kwa pamoja walielekea katika maabara ya Umoja wa mataifa anayofanya kazi Moses huko walichukua mkanda uliorekodi tukio zima la usiku uliopita wakati Askofu Edson anakuja kuchukua huo mzigo wa kemikali zenye sumu, walipopata mkanda huo waliondoka wakarudi maegesho kwenye gari yao ambapo wakati wqnaingia ndani ya gari Norbert aliuipindisha mguu chini ya kiti cha dereva wakati anaketi na akahisi kugusa kitu. Aliingiza mkono chini ya kiti hicho akatoa chupa ndogo kama ya manukato ikwa imebandikwa kitu mfano wa saa kilichokuwa kikihesabu dakika.

           "Klorofomu hii, ndani ya gari letu kulitembelewa na wajinga wanojifanya wajanja ngoja na sisi tuwaoneshe ujanja, fungua hapo utoe kitamba viwili kimoja nipatie kingine chukua" Norbert aliongea na Moses akafanya kama alivyoambiwa. Walichuua na chupa ya maji enye maji  iliyopo ndani ya gari yao wakaifungua wakaiacha wazi makusudi.

             "sasa tuone kama klorofomu inaweza kufanya kazi mbele ya maji na hapo ndiyo wageni wetu watakapokujua nina imani wanafutuatilia" Norbert alisema huku akiwasha gari, kauli hiyo ilimfanya Moses atabasamu tu.

     Walizunguka kwa gari makusudi ili kusubiri dakika za kile kifaa mfano wa saa ziishe, walipokuwa wamefika usawa wa chuo cha Maliasili na utalii ndiyo dakika ziliisha na ile chupa ikapasuka hewa nzito ikatanda ndani ya gari. Norbert na Moses waliweka vitamba midomoni mwao ili hewa ile isiwadhuru, Norbert aliligongesha gari makusudi  alipofika kwenye ukuta wa IFM na hapo ndipo wapinzani wao wakjua wamefanikiwa kumbe ulikuwa ni mtego kwao baada ya mtego wao kubainika.




****



    JENGO LA PENSHENI LA BENJAMINI MKAPA
             MTAA WA AZIKIWE

     Ndani ya idara ya sheria ya jengo hili iliyopo ghhorofa ya kumi na tano Beatrice ambaye alikuwa ni wakili wa shirika la mfuko wa hifadhi ya jamii alikuwa akifanya kazi zake za ofisini kama kawaida baada ya kutoka mahakamani kwenda kufuatilia kesi ya shirika lake lililoishtaki shirika jingine kwa kushindwa kuleta michango kama waliyoandikishiana mikataba. Akiwa hana wala lile simu ya mezani iliyopo katika meza yake iliita, aliipokea simu hiyo akaiweka sikioni kisha akaisikiliza  akasema, "ndiyo bosi....ok nakuja".

    Alieleka moja kwa moja kwa mkuu wa idara ya sheria ambaye ndiye bosi aliyempigia simu, aliruhusiwa kuingia na aliijgia ndani akamkuta mkuu wa idara ya sheria akiwa katika kusubiri ujio wake.

         "ndiyo bosi" Beatrice aliongea baada ya kuketi kwenye kiti kilichotenganisha kiti cha mkuu wa idara na kiti chake.

         "Mrs Gawaza nimekuita hapa, nimepokea simu kwa mkurugenzi mkuu kuwa unahitajika uende kwenye semina ya sheria Uingereza itakayoanza kesho kutwa hivyo kesho inabidi ujiandae kusafiri" Mkuu wa idara ya sheria alimueleza.

        "lakini bosi mbona ghafla hivyo?" Beatrice aliuliza akiwa anashangazwa na jinsi safari hiyo alivyoshtukizwa.

        "hata mimi nimeletewa ghafla na Mkurugenzi ambaye naye ameletewa ghafla na ngazi za juu" Mkuu wa idara ya sheria alieleza, Beatrice aliposikia maneno hayo alishusha pumzi tu kwani hakutarajia na hakuwa na uwezo wa kupinga safari hiyo pasipo kupoteza kibarua chake jambo ambalo hakutaka litokee ingawa mumewe alikuwa na pesa nyingi.

        "Sawa bosi nimekuelewa" Beatrice alikubali

        "vizuri Mrs Gawaza, kila kitu kipo tayari kilichobaki ni wewe kujiandaa tu. Unaachiwa muda huu mpaka kesho ukapumzike kwa ajili ya safari hiyo" Mkuu wa idara alimueleza

        "sawa bosi nashukuru" Beatrice alikubali hilo suala ingawa moyoni mwake alikuwa na simanzi kubwa ya kumuacha mume wake kipenzi kwa ghafla.

        "vizuri, tiketi hii hapa ya ndege na taratibu nyingine zote zipo tayari, nakutakia safari njema ukatuwakilishe vizuri huko Ulaya zaidi hata ya unavyotuwakilisha  hapa nchini sehemu mbalimbali"  Mkuu wa idaraya sheria aliongea huku akimpatia mkono wa kumuaga Beatrice,  mkono huo ulipokelewa na Beatrice kisha akatoka ofisini kwake na hapo sura isiyo na furaha ikauvaa moyo wake kwani hakutaka hata kidogo kukaa mbali na mumewe.

    Alienda kuwaaga wafanyakazi wenzake akiwa na  furaha ya bandia ambayo aliiweka usoni mwake lakini moyoni alikuwa na huzuni kuu ambayo  ilibaki ikimtafuna ndani kwa ndani, kila alipolifikiria suala la kukaa mbali na Moses kiasi cha bara tofauti ambayo haijawahi kutokea tangu walipoanza mahusiano aliona ni suala ambalo ni gumu sana kukubaliana nalo kwani moyo ulikuwa unauma sana akifikiria suala hilo.

    Mapenzi mazito aliyonayo kwa mume wake ndiyo yalimfanya awe na hali hiyo ambayo ilimbidi apigane nayo ili aweze kuizoea ikiwa tu mume wake ataridhia kuondoka kwake kwenda nje ya nchi akiwa na kiumbe tumboni mwake. Aliondoka kazini kwake baada ya kumuaga kila mtu anayefahamiana naye hapo ofisini kisha akaelekea nyumbani kwake akisubiri ujio wa mume wake jioni ya siku hiyo aweze kumpa taarifa hiyo yenye simanzi ambayo kwake ni zaidi ya msiba.


****


     MAKAO MAKUU
   USALAMA WA TAIFA
     DAR ES SALAAM


     Wakati Beatrice akipokea taarifa ya safari mume wake alikuwa katika ofisi yake ya usalama wa taifa baada kuaagana na Norbert tangu walipoanza hatua ya awali katika kazi yao ya kutegua kitendawili ambacho kilikuwa kipo katika anga zao, mbele ya ofisi yake iliyojaa samani za kisasa kulikuwa kuna mwanaume anayekaribia kuitwa mtu mzima ambaye kium,ri alikuwa analingana na marehemu Kennedy aliyekuwa mjomba wake Moses ingawa kicheo ndani ya usalama wa taifa alikuwa yupo chini ya Moses hivyo alikuwa akimheshimu sana. Mwanume huyo alikuwa ni msaidizi wa Moses katika idara ya usalama wa taifa pia ni mkurugenzi wa shirirka la mfuko wa hifahdi ya jamii ambalo ndilo sjirika analofanyi kazi mke wa Moses.

             "Ndiyo Mr Mabina niambie kazi niliyokupatia imeendaje?" Moses alimuuliza msaidizi wake huyo akiwa sura isiyo na mzaha hata kidogo.

             "Imefanikiwa Mkuu kwa asilimia zote kwani nimeweza kumchomeka katika safari ya kwenda Uingereza ambayo ilikuwa ikihusisha mawakili wanne wa shirika la mfuko wahifadhi ya jamii" Mabina alijibu akiwa  ana sura ya umakini kama ilivyo mkuu wake.

            "vizuri sana na umefanya kazi nzuri kwani hofu yangu ipo kwake tu, sasa inabidi uwe makini wasikujue kama wewe ni msaidizi wangu kwani itakucost Mr Mabina. Waache wanaojulikana wansongoza idara hii ndiyo hao hao wajulikane lakini si uongozi halisi wa Idara hii kwani hiyo itakuwa ni hatari sana kwako pia......Unaeza ukaenda" Moses aliongea kisha akamruhusu msaidizi wake aonde akaendelee na kazi nyingine, kisha yeye akamalizia kazi muhimu katika ofisi yake akaondoka kuelekea nyumbnai.


****

     Wakati Moses akiwa anaongea na msaidizi ilikuwa tayari ni mida ya saa tisa na nusu ambao ni muda kutoka kazini kwa baadhi ya wafanyakzi wa mashirika mbalimbali, Norbert muda huo alikuwa yupo ndani ya gari yake aina ya suzuki Escudo akiwa ameegesha kando ya barabara akionekana alikuwa navuta subira ya jambo ambalo lilimfanya awepo hapo.

      Alikuwa yupo jirani na bandari inayotumiwa na na boti ndogo zinazosafiri kwenda zanzibar, baada ya dakika takribani kumi yule binti aliyeleta kitabu cha rekodi walipokuja hapo kuulizia kuhusu boti zilizoondoka jana alionekana akitoka ndani ya geti, alikuwa akielekea barabarani akitembea kwa mwendo wa uchovu sana ingawa mapambo yake aliyojaliwa yalikuwa yakitikisiika na kuzidi kumchanganya Norbhert.

          "Moyo wee! Usikome mjini hamna mwenye chake" Moyo aliongea kwa sauti ya chini huku akiachia breki ya gari akimfuata binti huyo.   

                                                       ITAENDELEA!!




HAIRUHUSIWI KUNAKILI RIWAYA HII KWA NAMNA  YOYOTE PASIPO RIDHAA YA MTUNZI