Saturday, December 5, 2015

SHUJAA SEHEMU YA KWANZA





 SHUJAA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP: +255713776843


ANZA SASA
Huzuni ilikuwa imemtawala usoni kijana Moses na
kumfanya aonekane mtu mzima tofauti na
muonekano wake ulivyo, kila akijaribu kuhangaika
kwenda na baba yake katika hospitali tofauti ndani
ya jiji la Dae es salaam juhudi zake zilikuwa
zinagonga mwamba katika kutafuta tabibu awezaye
kumtibu baba yake aliyeugua ghafla pasipo
kujulikana chanzo kuugua huko. "mwanangu najua
unahangaika sana katika kuhakikisha.......ninapona
na ninarudi katika hali ya kawaida ila....." alikatisha
kuongea na kuanza kukohoa mfululizo huku
akimtazama mwanae kwa huruma kisha akaendelea
kusema "sitopona mwanangu ujue najua hujui
chanzo cha kuugua kwangu.." alihema kwa nguvu
huku akimtazama mwanae kwa jicho la huruma sana
kutokana na huzuni iliyomgubika kijana Moses. Baba
Moses akaendelea kusema "nimekuwa nikitumia
muda wa maisha yangu kwa miaka mingi katika
kugundua vitu mbalimbali katika sayansi pasipo
kujua mwisho wa kazi yangu hii , nimekuwa
nikitumiwa na watu matajiri ili niweze kupata fedha
kwa kuitumia kazi yangu vibaya. Sasa haya ndiyo
matokeo ya kazi yangu hii" alisitisha kuzungumza
kisha akamtuma Moses akamletee mkoba wake
anaoutumia kuhifadhi nyaraka zake muhimu.
Hakuwa mwingine bali ni professa Lawrence Gawaza
mwanasayansi wa siku nyingi na bingwa wa
kutengeneza kemikali hatari kwa maisha ya viumbe
hai, sasa yupo kitandani akiwa anaumwa ugonjwa
ulioshindwa kujulikana chanzo chake na matabibu
wa hospitali tofauti alizoenda kufafutiwa tiba. Moses
kijana wa miaka kumi na nane ndio kijana pekee wa
Prof Gawaza,hakuwa na mtu mwingine isipokuwa
mwanae huyo aliyekuwa anampenda sana. Mke
wake kipenzi alifariki siku aliyomzaa Moses, hivyo
hakuwa na mtu wa karibu hapo nyumbani zaidi ya
mwanae huyo.
Moses alimpelekea mkoba baba yake pale kitandani
anapomuuguzia,aliamriwa afungue kwa namba za
siri alizotajiwa na baba yake. Alipofungua alikutana
na makabrasha mengi pqmoja na funguo ndogo
sana, "umeiona hiyo funguo?" Prof Gawaza aliuliza
kwa tabu kutokana na kuzidiwa kwake. "huo pamoja
na hayo makabrasha naomba uwe mtunzaji wake na
usimkabidhi yoyote yule" Prof Gawaza alimwambia
mtoto wake huyo kwa sauti yenye kutoka kwa shida.
Moses naye aliitikia kwa kichwa huku machozi
yakimtoka kutokana na hali ya baba yake ilivyo, "we
ni mwanaume sasa haina haja ya kulia kwani
haisa......idii kitu chochote, kazania masomo yako
halafu....."alishindwa kumalizia kauli hiyo baada ya
kikohozi kumbana. Alikohoa kwa nguvu sana kisha
akaomba maji. Moses alikimbia kutoka chumbani
anapomuuguza baba yake hadi kwenye cha kulia
chakula kwenye jokofu la kupooza maji. Alichukua
bilau moja ndefu akaiweka usawa wa koki ya jokofu,
kisha akafungua koki ya jokofu kuruhusu maji
yaliyopo kwenye chupa kubwa juh ya jokofu hilo
yashuke kwa kasi, Alivyoijaza alirudi kwa kasi hadi
chumbani alipo baba yake, alipofika alimkuta kalalá
mithili ya mtu aliye ndani ya usingizi mzito. "baba
amka unywe maji" alimuita huku akimtingisha
mkono,cha ajabu hakuamka wala kuonesha dalili
zozote za kuamka. Moses alimtingisha baba yake
huyo kwa nguvu lakini hakuamka, aliita kwa sauti
kubwa lakini sauti yake haikuzaa jitihada zozote za
kumuamsha Prof Gawaza katika usingizi wa milele
aliolala. Moses alichanganyikiwa sana na hali
aliyomkuta nayo baba yak baada ya kumletea maji, "
baba! baba! baba! baba! babaaaa!" alipiga kelele
kwa nguvu baada ya kubaini baba yake hakuamka.
"Mose vipi mbona hivyo, kuna nini?" ilisikika sauti
ya mlinziwa nyumba hiyo pale mlangoni kisha
akaonekana mlinzi akivuka kizingiti cha chumba
hiko kwa kasi, kilio cha kwikwi cha Moses ndicho
kilimkaribisha humo chumbani na utulivu wa Prof
Gawaza ambaye alikuwa amelaliwa na Moses kifuani.
Alimnyanyua Moses kisha akaweka mkono katika
upande uliopo moyo katika kifua cha profesa,
hakuridhika akaweka na sikio kabisa kifuani mwa
bosi wake. Alipoinua uso wake ulikuwa umejaa
huzuni sana na alimshika mkono Moses kisha
akaenda naye nje, alipofika akamkalisha kwenye
baraza la nyumba. "yakupasa ujikaze dogo kwani
wewe ni mwanaume, kumbuka wewe ndio msimamizi
wa mali hizi na baba wa baadaye. Dogo jikaze najua
unasikia uchungu" Mlinzi alianza kumpa nasaha
Moses juu ya tatizo lililomfika. Pia akazidi
kumueleza "kumbuka binadamu hatuwezi kuwa
pamoja milele hata siku moja kwani ipo siku
tutatengana, ndio kama hivi mzee kakutoka ingawa
bado tunamuhitaji. Mose kutengana na mtu wako wa
karibu ni mojawapo ya changamoto za maisha na
kipimo cha ukomavu wako, sasa basi inabidi
ujioneshe upo mkomavu kiasi gani kwa kujikaza
katika suala kama hili. Baada ya mlinzi kumpa
Moses maneno ya kumtia moyo aliamua kwenda
kutoa taarifa kwa majirani pamoja na kuwapigia watu
wa karibu na Prof Gawaza.


***************************************

Brown Mcdonald ni mzungu mwenye mtandao
mkubwa dunia unohusiana na uhalifu wa kila aina,
umri wake na utajiri alionao ni vitu viwili tofauti.
Akiwa na vibaraka karibia kila nchi aliowaamini sana
katika biashara zake, hakika hakuna alitakalo
lifanyike katika biashara zake likashindikana. Kijana
huyu ambaye ni mwanajeshi aliyeasi amri katika
kikosi cha Uingereza na mtuhumiwa nambari moja
wa uhalifu barani ulaya aliamua kuja Afrika akiwa na
kundi kubwa la vijana wake baada ya msako wake
kuwa mkali barani Ulaya. Akiwa amevaa sura ya
bandia na alama za vidole mwake aliweza kuficha
muonekano wake pamoja na kupata passport mpya
ya kusafiria kwa njia ya kawaida tu pasipo
kugundulika na wanausalama wa dunia ambao
wanamsaka. Sasa ameingia ukanda wa Afrika ya
mashariki akiwa kama mfanyabiashara mwenye
viwanda vya kusindika katika nchi zote za Afrika ya
mashariki, ndani ya muda mfupi toka aingie katika
ukanda huu amejizolea umaarufu kutokana na ubora
wa bishaa zake. Akiwa anatambulika kama Brian
Stockman aliweza kuwa mfanyabiashara mwenye
ushawishi mkubwa katika soko la kimataifa, viwanda
vyake vilikuwa kama mwamvuli wa kuficha biashara
yake haramu anayoifanya ya kuuza dawa za kulevya
na nyara mbalimbali za serikali. Uongo
alioidanganya dunia ullikuwa umefanikiwa na sasa
alikuwa anajihisi mtu huru katika biashara zake,
aliweza kusafirisha bidhaa haramu pasipo kikwazo
chochote. Akiwa ametimiza mwaka mmoja tu toka
aanze kujulikana na wakazi wa kandahii ya Afrika ya
mashariki, alipata habari ya kugunduliwa kwa hatari
na mwanasayansi wa kitanzania. Taarifa hiyo
ilimvutia sana na akafanya jitihada za kuonanan na
mwanasayansi huyo, aliomba kuonana na
mwanasayansi huyo. Alipokubaliwa alipanga mahali
pa kukutana nae, hilo liliafikiwa na mwanasayansi
huyo.
Baada ya siku mbili walikutana katika mgahawa
uliomo hoteli ya Serena jijini Dar es salaam katika
sehemu iliyojitenga, kila mmoja akiwa na kinywaji
chake na amekaa kwenye kiti kilicho mkabala na
mwenzake. Baada ya kusalimiana Brian(Brown)
alianza kuongea kwa kiswahili kisicho fasaha chenye
maneno ya kingereza "sina mengi za kukuweka hapa
bana Gawaza, nahitaji tufanye bussiness".
"what kind of bussiness(biashata ya aina gani")
aliuliza Gawaza.
"no ipoo ongea na mswahili professa onesha jinsi
gani unatukuza swahili bana" Brian alimuumbua Prof
Gawaza baada kuona anajali sana kingereza kuliko
lugha yake ya taifa.
"ok mr Brian biashara ya aina gani?" prof Gawaza
aliuliza huku akitabasamu.
"i know you are scientist(najua wewe ni
mwanasayansi) na umegundua virus ambao
ninawahitaji kwa ajili ya kasi yangu binafsi" Brian
alieleza kiini cha kukutana.
"virus wale ni hatari sana Mr Brian na bado sijatafuta
dawa yake, huoni kama ni hatari kwako if you
release them(kama utawaachia)" Prof Gawaza
alimwambia Brian huku akipiga funda moja la
mvinyo ulio katika bilauri.
"I don't care about that(sijali kuhusu hilo) Professa
ninachohitaji ni virus na jaribio ndani ya nchi hii"
Brian alisema maneno hayo akiwa na uso wenye
dharau.
"no sipo tayari kwa hilo mr Brian kama unataka
biashara yoyote ya virus nitakupa ila si kujaribu
ndani ya nchi yangu yenye damu yangu...thats all"
Prof Gawaza alinyanyuka kwa hasira na kuondoka
eneo hilo. "we will meet again(tutakutana tena)"
Brian alimwambia kwa sauti kisha akaendelea
kunywa kinywaji chake kwa taratibu. Alipomaliza
alinyanyuka kwenye kiti alichokaa akiwa na hasira
maradufu, "I'll show him (nitamuonesha)" Brian
aliropoka kwa hasira kisha akanyanyuka kuelekea
ulipo mlangi wa kutokea katika mgahawa wa hoteli
hiyo. Alitoka na kuondoka kwa mwendo wa haraka
hadi alipoegesha, aliingia ndani na kuliwasha kisha
akatoweka katika eneo hilo.


**************************************


Maelfu ya watu walihudhuria katika msiba katika
msiba wa Professa Gawaza uliokuwepo nyumbani
kwake maeneo ya mikocheni jijini Dar es salaam,
wengi wakiwa ni ndugu,jamaa na marafiki wa
mwanasayansi huyo maarufu ndani ya jiji la Dar es
salaam. Uwanja wa nyumba hiyo ulifurika watu wa
rika zote wakiwa na mavazi meusi huku wale watu
wa karibu wa marehemu wakiwa wamevalia nguo
nyeusi chini na fulana nyeupe yenye picha ya
marehemu sehemu ya kifuani. Turubai kubwa
lilifungwa nje ya nyumba hiyo pamoja na viti vyenye
rangi moja vilivyokaliwa na wahudhuriaji wa msiba
huo, mtoto pekee wa marehemu ambaye ni Moses
alikuwa kakaa ndani muda wote huku kilio kikiwa
ndiyo kiliwazo chake. Siku iliyofuata mwili wa
marehemu uliagwa katika eneo hilo la nyumbani
kwake kisha msafara wa magari kutoka kwa
wahudhuriaji wa msiba huo uliondoka msibani hapo
kuelekea yalipo makaburi ya kinondoni maeno ya
kinondoni kwa ajili ya kuupeleka mwili wa marehemu
katika nyumba ya milele . Mazishi yalifanyika katika
makburi hayo kisha watu wakatawanyika kuelekewa
makwao na wengine kurudi msibani.
Baada ya siku takribani saba ndugu wote wa
marehemu waliondoka ndani ya nyumba hiyo na
kupelekea Moses mjomba wake ambaye alijitolea
kuishi naye na mlinzi wawe watu pekee waliobaki
katika nyumba hiyo. Maisha bila ya baba yake ndio
yaliyofuata baada ya msiba wake, pesa alizoziacha
baba yake pamoja na msaada wa rafiki mkubwa wa
baba yake aitwae Dk Mbungu ulioweza kumsaidia
katika vitu mbalimbali ndio uliopelekea aweze
kujimudu katika mahitaji yake muhimu ikiwemo
ulipaji wa ada shuleni. Hadi muda huo Moses
alikuwa anasoma kidato cha tano katika shule ya
Neema trust iliyopo mbezi jijjnj Dar es salaam,
aliamua kujiendeleza kielimu kielimu na kutoshika
mambo yoyote yasiyohusiana na elimu ili aweze
kujijenga. Umakini wake katika masomo ulimfanya
awe mwanafunzi bora katika shule yao, hadi muhula
wa kidato unakwisha mnamo mwezi mei mwaka
uliofuata, tayari alikuwa anaongoza shule nzima kwa
kupata alsma za juu kuliko mtu yoyote katika kombi
za sayansi zote. Akiwa likizo alitumia muda wake
mwingi kujisomea na akawa hajishughulishi na
mambo ya anasa, mnamo mwezi wa saba muhula
mpya wa kidato cha sita ukaanza kama ilivyo ratiba
ya nchi nzina ya Tanzania. Ulikuwa muhula wa
masomo ambapo wsnafunzi wengi walizinduka
kutoka kwenye usingizi baada ya kutokuwa makini
katika masomo yao ya kidato cha tano, katika kombi
ya PCB ambayo Moses alikuwa anasoma tayari
umakini wa wanafunzi ulizidi maradufu ingawa
hawakufua dafu mbele ya uwezo wa Moses
aliyezinduka mapema kabla yao.


**************************************

Beatrice Bernard ni binti wa familia yenye uwezo
anayesoma katika shule ya Neema Trust, ni
mojawapo ya wasichana warembo na wenye kuvutia
katika shule hiyo iliyosheheni watoto wa matajiri
kutoka sehemu mbalimbali ndani ya Afrika ya
mashariki. Umbo lake la asili ya asili ndio lilimfanya
avutie kwa kila anayemtazama, mchanganyiko wa
wazazi kutoka makabila tofauti ndio ulimfanya avutie
maradufu. Baba yake mzee Bernard alikuwa ni
muhaya na mama yake akiwa ni mrangi, hakika
alikuwa na umbo tata lililozua maswali na
minong'ono kila apitapo. Yote hayo pamoja na sifa
zote alizozipata na kusumbuliwa na watu kutoka
sehemu mbalimbali, alikuwa ni msichama aliyezama
katika penzi zito la mtu asiyemjali wala kuthamini
upendo wake. Utanashati wa huyo kijana ndio
uliomvutia sana na kufanya awe kiliwazo cha macho
yake, ustarabu na upole wake ndio uliomfanya
apende kuwa nae.maishani mwake. Kijana huyo
hakuwa mwingine ila ni Moses Gawaza kijana
mpenda masomo kuliko anasa kama ilivyo vijana wa
umri wake. Beatrice akiwa anasoma madarasa ya
arts katika kombi ya HKL alijitahido kujenga ukaribu
na kijana wa madarasa ya sayansi bila ya mafanikio,
hii haikumkatisha tamaa Beatrice zaidi ya kupenda
kuwa karibuIRI na Moses kutokana na misimamo
aliyonayo huyo kijana kamaJ mwanaume..

ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment