Saturday, November 26, 2016

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA KUMI NA TATU






RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________





    SEHEMU YA KUMI NA TATU!!

             "Yuko wapi Dokta Hilary" Afisa mteule huyo alimuuliza mfanyakazi huyo ambaye alianza kutetemeka kwa uoga.

             "ni mimi niwasaidie nini?" Sauti kutoka ndani ya nyumba  hiyo ilisikika na hapo wanajeshi wote wakaingia wakimsukuma msichana huyo wa kazi, waliingia ndani wakamkuta Dokta Hilary akiwa kasimama na mkewe Irene akiwa na mavazi ya  kulalia.

             "Moses yupo wapi"Afisa mteule huyo daraja la pili ambaye alijulikana kutokana na kuvaa cheo mkononi kilicho na umbo kama la saa yenye alama ya mwenge alimuuliza Dokta Hilary huku wenzake wakimnyooshea bunduki kwa tahadhari.



             "Sijui alipo" Dokta Hilary alijibu kwa kujiamini.

             "Ok, mkamateni yeye mpaka atakapojileta Moses" Afisa mteule  huyo aliongea kuwapa amri wenzake, askari hao walisogea mbele ili wamtie nguvuni Dokta Hilary lakini walisita baada ya kusikika amri nyingine.

             "SUBIRI!" Afisa mteule ambaye ndiye kiongozi wap alipaza sauti.


****



      Wanajeshi wote walisitisha zoezi hilo lakini hawakusitisha kuwawekea bunduki Dokta Hilary na Irene, walitega sikio kwa mara ya pili wasubiri amri ya Afisa mteule daraja la pili aliyekuwa yupo nyuma yao.

              "Hapana msimkamate Dokta Hilary kwani huyo hatashawishi Moses kujitokeza, mnajua njia rahisi ya kumshawishi Moses kujitokeza ni ipi?" Afisa Mteule daraja la pili aliongea kisha akauliza swali ambalo halikujibiwa na wanajeshi waliopo chini yake, alikuwa akimtazama Dokta Hilary kwa tabasamu mithili ya mtu aliyekuja kiamani.

      Tabasamu lake lilikuwa linaongeza hofu katika moyo wa Dokta Hilary kwani lilikuwa ni tabasamu lililofuatana na fikra chanya, fikra hizo hazikutambuliwa na yeyote hadi pale Afisa huyo alipoziweka wazi.

              "Mkamteni mke wake" Afisa huyo alisema huku akitabasamu.

             "Nini? No! No! No! Nikamateni mimi mke wangu muacheni jamani" Dokta Hilary aliongea huku akisogeza mke wake mgongoni mwake kumkinga.

             "Nikamateni mimi!" Dokta Hilaty alipaza sauti huku akirudi nyuma akiwa amemkinga mke wake, mlio wa bunduki ikikokiwa baada ya kuondolewa usalama kutoka kwa mmoja wa wanajeshi hao ulisikika papo hapo. Mwanajeshi mmoja aliyeishika bunduki yake aina ya SMG ambayo kitako chake alikiweka begani ili kuzuia isitikisike wakati anapiga; alikuwa tayari ameweka shabaha kwenye mwili wa Dokta Hilary.

            "Tufumue ubongo wako na ubongo umwagike kisha tumchukue mke wako akataabike au tumchukue mke wako tuweze kumpata tunayemtaka. Haaaaa! Dokta Hilary chaguo ni lako hapo au nikuchagulie ukiwa upo hivyo hivyo umemficha mke wako mgongoni mwake" Afisa mteule daraja la pili aliongea.

      Maneno hayo yalimfanya Dokta Hilary amtoe mke wake nyuma ya mgongo wake, uamuzi uliokuwa ukitaka kuchukuliwa na wanajeshi ulikuwa ni mbaya zaidi hata ya huo anaotaka kuufanya. Mwanajeshi mmoja alisogea mbele zaidi akamchukua Irene kwa nguvu, alimuacha Dokta Hilary akiwa hana cha kufanya zaidi ya kubaki akitazama mke anavyokamatwa na wanajeshi hao.

              "Noooo! Hilary fanya kitu mume wangu usiwaruhusu wanichukue" Irene alilalamika huku akijaribu kujitoa mikononi mwa mwanajeshi aliyemdaka, Dokta Hilary alijikuta  akipiga hatua  zaidi mbele baada ya uchungu za sauti ya mke kumuumiza moyoni mwake. Hatua zake hizo zilizuiwa kwa mara moja na bunduki nyingine kutoka kwa mwanajeshi mwingine ilimuelekea, alisitisha ghafla kupiga hatua nyingine kutokana na kuhofia bunduki hiyo isije ikatoa kikohozi cha ghafla kitachoutwaa uhai wake papo hapo.

              "Lala chini, naona unajifanya mjuaji wewe" Afisa mteule huyo aliongea, Dokta Hilary alilala chini bila ya kupenda na wanajeshi hao walitoka mmoja baada ya mmoja.

    Afisa mteule ndiye aliyekuwa wa mwisho kutoka nje na alitoka na ufunguo wa mlango mkubwa kisha akaufunga kwa nje, sauti ya gari ikiondoka ilisikika na ilizidi kumchanganya zaidi Dokta Hilary. Alikimbia hadi mlangoni kisha akanyonga kitasa akiwa ametokwa na kumbukumbu ya kufungwa kwa mlango na mwanajeshi yule, alinyonga kitasa bila mafanikio ndipo akakumbuka kuchungulia kwenye tundu la funguo. Hakuweza kuona nje kwa muda huo wa alfajiri kutokana na tundu la kitasa hicho kuzuiwa na ufunguo, aligeuka nyuma akiwa amechanganyikiwa akawaona wafanyakazi wake wakiwa wanamshangaa kwa kile anachokufanya muda huo.

               "Hey! Mnashangaa nini nyinyi kaleteni  funguo za akiba sasa hivi, mkichelewa sekunde mbili kazi hamna!" Dokta Hilary aliwafokea wafanyakazi wake akiwa amechanganyikiwa kabiaa, aliweka mikono kichwani kisha akakaa chini bila ya kupenda akajikunyata mithili ya kinda la ndege lilikosa joto la mama yake kipindi cha baridi.

                "Aaaaaaaargh! Mke wangu mimi jamani" Dokta Hilary alitoa ukeleleea uchungu pamoja na malalamishi ambayo hayakuwa na mhusika wa kumlalamikia, kulia alitamani lakini kulia huko alishindwa kutokana na roho ya kiume  aliyonayo.

    Macho yake yaligeuka rangi na kuwa mekundu kutokana na uchungu alioupata baada ya kutekwa kwa mke wake, sehemu ya moyo wake alihisi ikikandamizwa na kitu chenye ncha kutokana na kutiwa nguvuni kwa kipenzi chake anayemhusudu. Kutoka pale alipoikunja miguu kwa kujikunyata aliinyoosha kisha akaanza kuichezesha kwa fujo mithili ya mtoto aliyekuwa amenyimwa hela ya kununua pipi, makelele ya uchungu ndiyo yalifuata huku akiweka mikono kwenye kichwa chake.

     Alidumu akipiga kelele hizo kwa muda hadi psle alipoguswa begani akatulia ghafla akamuangalia aliyemgusa uso wake ulitua kwenye funguo za mlangoni zilizokuwa zikining'nizwa na mkono wa kike  kuashiria alitakiwa azichukue. Alipomuangalia mtu  aliyeshika funguo hizo aligundua ni mmoja wa wafanyakazi wa nyumba yake, hapo ndipo akili yake ikarudi kawaida akakumbuka kwamba aliwatuma kuleta funguo hizo.

    Kuletewa  kwa funguo hakukumfurahisha na ndiyo kwanza kulizidi kumtia hasira zaidi, alimtazama mfanyakazi huyo kwa  jicho lake jekundu lenye kutangsza hasira za wsziwazi. Wekundu wa jicho hilo ulizidi kuleta hofu kwa mfanyajazi huyo, mfanyakazi huyo hakuuona utofauti wa rangi uliopo katika jicho hilo na nyanya ambazo amezoea kuzikatakata kutengeneza mboga. Tofauti ya wekundu huu ulikuwa ukimtisha na wa nyanya haukuwa ukimtisha, Dokta Hilary naye aliendelea kumtazama mfanyakazi wake huyo wa kike kwa muda wa sekunde kadhaa kisha akaachia msonyo mzito sana.

              "Bloody fool! Sasa unanionesha funguo katika uso wangu ili iweje? Kuna tundu la funguo uweze kufungua mlango, haya utie kwenye tundu la pua ufungue mlango" Dokta Hilary aliongea kwa hasira huku akimtanulia tundu la pua mfanyakazi wake autie ufunguo huo, mfanyakazi alizidi kutetemeka kwa uoga akawatazama wenzake ambao walikuwa sebuleni hapo kwa uoga.

     Wenzake walimuashiria akaufungue mlango mkubwa kwa haraka naye alifanya hivyo akiwa anatetemeka sana, aliufungua mlango huo kwa hofu kubwa sana kwa kukosea kutumbukiza funguo kwa zaidi ya mara nne.

     Mara ya tano mlango ulipofunguka aljikuta akienda chini baada ya kukumbwa na kukumbo kizito kutoka kwa Dokta Hilary hadi akaanguka chini, gauni fupi alilovaa liliweka mambo hadharani kwa wafanyakazi wenzake ambao ni jinsia moja na yeye pamoja  kadamnasi ya samani iliyopo sebuleni. Wafanyakazi wenzake walienda kumsaidia kumuinua haraka kisha wakakimbilia nje alipokimbilia bosi wao baada kumkumba kikumbo, walimkuta Dokta Hilary akiwa anayaangalia magari yake ambayo hayakuwa na upepo kwenye matairi hadi muda huo kutokana na kutobolewa matairi.

       Dokta Hilary alikaa chini  akiwa anapiga makelele kwa hasira sana huku akiwa amechanganyikiwa, alikuja kuguswa begani tena na mfanyakazi wake mwingine.

                 "Bo...bosi Professa Gawaza anapiga simu" Mfanyakazi huyo alimuambia Dokta Hilary huku akibabaika kutokana na hasira alizomuona nazo, simu hiyo kwa mara nyingine ilimrudisha Dokta Hilary katika hali ya kawaida. Aliipoikea simu hiyo  kutoka kwenye mikono ya mfanyakazi wake, aliiweka sikioni kisha akaanza mashambulizi ya makombora bila hata kushambuliwa yeye.

                  "Moses you are an idiot (Moses wewe ni mjinga)!  Kwa ujinga wako mke wangu ametekwa na wanajeshi na kwa upumbavu wako wewe nabaki nataabika........ nikusikilize kwa lipi Moses nitakalokuelewa.......nini? Ngoja" Dokta Hilary aliongea kwa hasira kisha akaikata simu akairudisha mikononi mwa mfanyakazi wake.

                  "Asitoke mtu" Alisema kisha akatimua mbio pekupeku mpaka getini, alimuamuru mlinzi amfungulie geti na ye alitii akamfungulia.


****


 MWANZO WA ALFAJIRI.
  
       Wanajeshi wa jeshi la wananchi (JWTZ) wakati wanapanga mikakati yao juu ya kumtia mikononi Moses hawakujua kama idara ya usalama wa taifa iliyopo chini ya Moses ilikuwa ina vibaraka katika sehemu zote za nchi hii. Ndani ya jeshi hilo pia vibaraka wa usalama wa taifa katika kulinda usalama wa nchi kwa kutoa taarifa muhimu walikuwepo bila ya wanejeshi wenyewe kujua, wakati mpango huo ukipangwa mwanajeshi mmoja mwenye cheo cha Koplo anayeaminika sana kwa ulengaji shabaha alihusishwa kutokana kuhitajika  sehemu kama hiyo.

     Hawakujua kama mwanajeshi huyo alikuwa yupo katika idara ya usalama wa taifa  na amepachikwa jeshini hapo kwa kazi maalum kama hizo, wakati mkutano ukiendelea Koplo huyo aliipiga namba ya Moses kisha akaiacha hewani bila wenzake kujua. Wakati wakiendelea mazungumzo tayari  mpango wao wote ulifika kwa Mosea bila wao kujua, katika mpango huo Afisa mteule daraja la pili aliyeongoza kumkamata Irene alimuita Koplo huyo kibaraka wa TISS na kumuambia juu ya kiini cha mpango huo ni kumteka Irene mke wa Dokta Hilary.

     Wakati wanaondoka kulekea nyumbani kwa Dokta Hilary tayari Moses alishafika jirani na maeneo ya nyumbani kwa Dokta Hilary, wakati wanaingia ndani ya nyumba hiyo Moses alikuwa ameshawaona na tayari aliandaa mtego mwingine utakaomuwezesha kumtoa Irene. Makazi ya Dokta Hilary yalikuwa yapo mtaa wa Flamingo huko Mbezi  beach na njia waliyoitumia wanajeshi hao kufika hapo tayari Moses aliijua na alienda kuwawekea mtego, wakati wanajeshi hao wanatoka walitumia nia ilele waliyokuwa wamekuja nayo.

     Walipita kwenye mtaa wa Busara  kisha wakafuata mtaa wa Hekima wakawa wanaelekea  kwenye barabara ya Mbaraka Mwinshehe, hawakutambua mitaa kadhaa hapo mbele yao Moses alikuwa akiwangojea kwa hamu sana na walipofika kwenye anga za Moses ghafla mipira ya matairi ya gari lao ilipasuka yote. Hapo walisimamisha gari wakashuka kwenda kuangalia kile kilichotokea hadi matairi yao yakapasuka, hawakutambua kama kushuka kwao walikuwa wamefanya kosa kubwa jingine zaidi hata ya kosa kuliko kosa la awali la kupita katika njia hiyo.

     Kitendo cha wao kushuka chupa nne zenye umbile kama chupa ya dawa ya mbu zilitupwa, hawakuwa wamezutambua kwa haraka zile chupa zilikuwa za nini kutokana na ufinyu wa mwangaza wa Alfajiri na hata walipokuja kuzitambua tayari walikuwa wamechelewa.

     Moshi mzito wenye kemikali uliwavamia kwenye macho yao pamoja na kwenye pua zao wakabaki wakikohoa sana huku macho yakiwawasha, waliishiwa nguvu kwa kukohoa huko kutokana na gesi nzito iliyokuwa imevamia, ulipokuja kuondoka moshi huo tayari Irene hakuwa katika mikono yao na  hapo ndipo wakauona ubao wenye misumari uliokuwa umetegeshwa barabarani ambao ndiyo uliotoboa matairi yote ya gari. Walibaki wakijilaumu tu kutokana na kushindwa kutekeleza kazi na wakawa na hofu sana juu ya uzembe huo, walipojitazama idadi yao ndiyo walizidi kuchanganyikiwa kwani yule Koplo kibaraka wa usalama wa taifa hakuwepo kati yao.







       (2)UTEPE

   Mapambazuko ya siku mpya ya jumamosi tayari yalishashika nafasi yake kwa kuvizishwa kwa mpango wa kutaka kumtia mbaroni Moses, baada ya jua kuchomoza kwa upande mwingine katika hoteli ya New Avon Norbert alitoka akiwa na Jospehine wakaenda kupata kifungua kinywa  wakiwa pamoja. Majira ya  saa tano asubuhi yalipotimu Josephine alimuaga Norbert akimuacha hapo kwenye mgahawa akaondoka, alitumia usafiri wa teksi akapotea kwenye upeo wa macho ya Norbert huku akimuacha Norbert akiwa na mengi yaliyomfanya aendelee kuketi hapo kwenye mgahawa.

     Hapo aliamua  kuitoa simu yake na akaweka sauti zilizojirekodi akazisikiliza kwa umakini hadi akazimaliza, fikra ya utambuzi juu ya jambo jingine ndiyo zilifuata na hakuona umuhimu wa yeye kubaki hapo. Alinyayuka kitini kwenye mgahawa huo akarudi alipoliacha gari lake kwenye maegesho jirani na hoteli ya New Avon, hakutaka kupoteza ilimbidi aondoke eneo hilo kwa haraka sana.

     Aliingia ndani ya gari lake na kabla hajawasha kioo cha gari lake kiligongwa na ikamlazimu kushusha baada ya kumuona msichana mrembo aliyevaa kisasa zaidi, kioo kilipmalizika kushushwa alipokelewa na tabasamu pana zaidi kutoka kwa msichana huyo mwenye umbo matata na mrefu. Norbert alijikuta akimtazama msichana huyo kwa kiusanifu zaidi kisha akatingisha kichwa akiwa na tabasamu, alipomtazama msichana huyo mwenye sura inayofanana kwa kiasi kikubwa na wasichana kutoka nchi  ya Rwanda alijikuta akimkumbuka jasusi mwenzake Hilda Alphonce waliyefanya naye kazi kwenye JINAMIZI na SHUJAA pamoja na visa vingine.

    Alitoa tabasamu lililomfanya hata binti huyo amshangae kwani hakuwa akimuelewa, alibaki akimtazama kisha  akatazama pembeni kuonesha kuwa ana aibu lakini kimtazamo wa Norbert aliona kuwa ilikuwa ni aibu geresha.

                 "Habari yako kaka yangu" Alimsabahi Norbert.

                "safi mdada za kwako?" Norbert aliitikia.

                "safi tu, samahani kaka yangu sijui unaelekea wapi?" Aliuliza huku akiabza kujiumauma

                "Naelekea Keko mdada" Norbert alimjibu.

               "samahani kwa usumbufu kaka yangu" Alisema.

               "bila samahani mrembo" Norbert alimuambia

               "nahitaji nifike hapo Sofia House Keko nimesahau handbag yenye pesa yangu kwenye appartment niliyopanga" Alisema.

              "si vibaya nikakusogeza mdada , ingia kwenye gari" Norbert alimuambia, binti huyo bila kuchelewa aliingia kwenye gari akiacha sehemu zake za nyuma zikifanya fujo  ambayo ilionekana wazi kwa Norbert. Huo ulikuwa ugonjwa wake wa kupenda wanawake wenye maumbo tata pamoja na wenye sura nzuri, lakini kwa binti huyo kila akilitazama umbo lake vinyweleo vyote vilimsisimka.

     Suruali  ya kahawia yenye  kubana iliyombana kisawasawa binti huyo hadi nguo ya ndani ikaonekana bado haikumletea mvuto Norbert kwani moyo wake ulisita kabisa kuvutika naye. koti la suti akilolivaa kwa juu ambalo lilkuwa limeifunika shati ya kubana aliyoiachia sehemu ya kifuani wazi bado haikuwa imemletea mwenyekiti wa mwili wa Norbert usumbufu. Norbert alijihisi yupo tofauti na siku zote kwani hakuwa amevutiwa na mwili huo wa msichana mrembo, ushawishi wa matamanio yake  juu ya mrembo hayakuwepo kabisa. Hadi muda huo tayari mrembo huyo alishaketi ndani na alifunga mkanda, Norbert aliwasha gari kisha akaliingiza barabarani.

                   "Janet, nani mwenzangu" Binti huyo alijitambulisha huku akimpatia mkono Norbert.

                   "Kaila au Norbe.."

                   "ohoo! Norbert Kaila ndiyo wewe, mwndishi wa habari maarufu wa kujitegemea"

                   "Hujakosea"

                  "Basi nafurahi kukufahamu ila nahitaji kukufahamu zaidi"

                 "kiaje yaani sijakuelewa"

                "Kama hivi ujitambulishe  vizuri mbele ya rafiki" Janet alipoongea hivyo Norbert alihisi akiguswa na kitu cha baridi sehemu ya kwenye mbavu wakati mikono yake ikiwa kwenye usukani, alipoangalia eneo hilo aliiona bastola isiyo na kiwambo cha kuzuia sauti ikiwa imegusa sehemu ya mbavu.

               "IMI DESERT EAGLE original kutoka kwa Israel ndiyo hii siyo  ile ya Marekani, ukileta ujinga kidogo tu nacharanga mbavu zako hadi kwenye moyo hii" Janet alimuambia Norbert huku akiwa ameweka uso wa tabasamu.

               "Pandisha vioo tafadhali usihitaji nikumalize mapema watu wakipata faida kutoka kwetu"  Janet alimuambia Norbert ambaye alitii bila kupenda akapandisha  vioo, Norbert alijua alikuwa amekamatika kwani hakuwa na uwezo aa kumfanya chochote Janet.

      Aliwaza aongeze  mwendo halafu akanyage breki kwa ghafla lakini hiyo isingesaidia kitu, Janet alikuwa amejifunga mkanda hivyo angekanyaga breki za gari kwa ghafla mkanda ungenasa kumzuia asiende hivyo asingemfanya chochote na ingekuwa ni nafasi tosha kwa Janet kufumua mbavu zake kwa bastola hiyo yenye uwezo mkubwa.

      Alikuwa akiitambua  IMI Desert eagle uwezo wake hivyo hakutaka kuleta ubishi hata kidogo kuepuka kuleta makuu, alishikilia mikono yake kwenye usukani wa gari akijua amekamatika kabisa na hakupata nafasi yoyote ambayo angeitumia kama kosa la kuweza kumuokoa.

                "Nenda Mwembeyanga moja kwa moja"  Janet alimuambia Norbert kisha akaanza kuutembea mkono wake wa pili katika  eneo la zipu ya Norbert. Alipapasa eneo hilo kwa tararibu sana kwa mikono yake huku akimtazama Norbert, hakuridhika na hapo akafungua zipu ya suruali yake akatia mkono ndani juu ya nguo ya ndani akazidi kumpapasa hadi mwenyekiti akaleta fujo hafifu kutokana na mawazo ya Norbert kuwaza umauti tu ndiyo ulikuwa unamkabili.

               "Kumbe na wewe muoga sana mbona huyu aliyenitamani siku ile tulipokutana klabu Bilicanas hadi ukanitongoza kwenye parking ya magari leo hii mnyonge" Janet aliongea  huku akimtazama Norbert ambaye akili yake iliwaza kujiokoa tu na siyo suala jingine ndiyo maana mwenyekiti aligoma kujitambulisha kiufasaha ndani ya suruali yake, hapo alipoambiwa maneno hayo na Janet ndiyo kumbukumbu za siku nyingi zilizopita hata kabla mabalaa hayo hayajaanza alipokutana binti aliyemvutia sana akamtongoza kwenye maegesho ya magari klabu ya usiku ya Bilicanas.

               "Dorene" Norbert aliongea kwa taratibu huku  akimtazama Janet kwa jicho la kuibia.

               "Ulinifahamu kwa jina hilo lisilo halisi na leo umenifahamu kwa jina jingine lisilo halisi, kiuhalisi niite Leopard Queen  member of Cats Kingdom" Kwa mara ya kwanza alijitambulisha jina lake analolitumia ambalo lilimfanya Norbert arudishe mawazo siku ile aliyokuwa ametekwa na Cats kingdom wakiwa chini ya Panthers, alilikumbuka umbile la mwanamke aliyekuwa amevaa kinyago cha paka na hapo akabaini ndiye huyu aliyekuwa anaongea  naye. Moyoni alijilaumu kwa kuchelewa kumkumbuka hadi anaingia kwenye mtego wake, aliitukana tusi halmashauri ya kumbukumbu kwa kushindwa kumbukumbu haraka hadi amenasa kwenye mtego.

              "Kama nilivyokuambia leo tutafahamiana vizuri zaidi, nilikuwa nangojea nafasi hii adimu tangu unaingia na malaya wako pale mgahawani. Ngoja tufike tutafahamiana zaidi then Quantanise itakuondoa kama ilivyowaondoa wengine, nataka ujue hakuna wa kutuzuia hata N001 mpelelezi wa daraja la kwanza tunayemsaka tumuangamize kabla hajaanza yeye"  Leopard Queen aliongea kwa dharau  pasipo kutambua N001 anayemzungumzia ndiyo huyo yupo aliyemtia nguvuni, alikuwa akimtambua Norbert kama mwandishi wa habari mjanja anayelindwa na wanausalama  lakini hakumtambua kama huyo ndiyo mpelelezi wa hatari wanayemsaka kabla hajaanza kazi.

               "Hongereni" Norbert aliwapongeza huku akiachia tabasamu mithili  ya mtu aliyepo kwenye eneo lenye amani.

              "Norbert Kaila wewe mfu tayari tuone zile ngumi zako ulizojifunza ili ujilinde kwa ufichuzi wako utazitumia mbele ya Leopard Queen ukiwa umetoka kumtumia huyu bwana kwa yule mfanyakazi wa bandari" Leopard Queen huku akimchezea mwenyekiti wa mwili wa Norbert kwa madah, hazikupita dakika kumi na tano mwenyekiti huyo aliamka usingizini akainyanyua nguo ya ndani  ya Norbert akiomba afunguliwe.

             "Wooow! Kaamka leo namdunga Quantanise yeye" Leopard Queen aliongea na muda huo tayari walikuwa wameshaingia Mwembeyanga Temeke, alimuelekeza Norbert aende hadi kwenye geti la Ghala moja lenye maandishi yalisomeka 'Nourhern brothers warehouse'. Hapo aliamriwa apige honi na alipiga honi geti likafunguliwa, Norbert aliingiza gari ndani na geti likafungwa tena na mwanaume mwenye mwili wa  kimazoezi.

             "Shusha kioo" Leopard Queen alimuambia, Norbert alishusha kioo na hapo mdomo wa bunduki ukapenya ndani ya gari ukagusa kichwa chake.

      Leopard Queen alishuka ndani ya gari akazunguka upande wa dereva dirishani akamnyooshea bastola Norbert huku mwenye bunduki akiishusha chini akasogea pembeni, Leorpard Queen alimuamuru Norbert ashuke lakini alisita baada ya kusikia honi ya pikipiki kwa nje.

                "Gasper ni nani huyo anayepiga honi" Leopard Queen alimuuliza yule mwaneume aliyewafungulia geti ambaye alikuwa peke yake ndani.

                      "Madam ni mleta tenki nafikiri una habari ya kuletwa kwa tank mpya ya maji kwani ile ya zamani imetoboka" Gasper aliongea.

                      "Ok ficha silaha umfungulie aingize tenki upande wa kushoto kwenye parking ya malori" Leopard alimuambia Gasper ambaye alikimbia upesi akaenda kufungua geti, muda huo Leopard Queen alikuwa amemuwekea bastola Norbert akijua amemdhibiti kumbe tayari walishafanya kosa.

                       "Golden chance" Norbert alijisemea moyoni huku akitazama kwa jicho la kuibia kwenye kioo cha pembeni akaiona pikipiki aina ya Toyo yenye matairi matatu ikiwa imebeba tenki kubwa la kuhifadhia maji la lita 2000, muda huo gari ya Norbert ambalo amepewa kwa kazi hizo lilikuwa limewekwa mfumo wa automatic(moja kwa moja) na gia yake ipo herufi D (drive). Ushindi wa kukwepa mdomo wa mamba aliuona unakuja na hapo akaachia breki za gari makusudi, gari yake ilisogea mbele na kusababisha Leopard Queen amkazie macho kwa hasira.

                     "We! We! We! Weka gia hiyo kwenye  P parking haraka" Leopard Queen  alimuamrisha kuweka parking  pasipo kutambua kuwa alikuwa anafanya kosa kubwa sana kumuambia afanye hivyo, mfumo wa automatic wa gari upo mpangilio P-R-N-D-2-L.

       Mfumo huo huwezi kuweka P ambayo ni parking bila kuivuka  R ambayo ni  reverse yaani gia ya kurudi nyuma, Norbert alipoona geti lililofunguluwa lipo usawa wake alirudisha gia kama anaipeleka parking na alivyofika R alifanya kitu ambacho Leopard Queen hakutarajia kama anaweka kukifanya kwa muda huo . Kwa kasi ya ajabu alikanyaga mafuta akaachia breki akarudisha gari nyuma kwa nguvu sana akamuacha Leopard Queen akipiga risasi zilizoishia kwenye kioo chake cha gari kisichoingia risasi, alienda kuigonga ile pikipiki matairi matatu akaitoa hadi nje kutoka pale getini ikarushwa umbali wa mita kadhaa kutoka geti liliopo na hapo akaweza kutoka nje ya geti hilo.



*Mfyuuuu! Toka lini simba akanaswa na mtego wa panya

*Kaila katika ubora wake kaudhihirisha



JUMAPILI     NAYO SIKU TUKUTANE TENA PANAPO UHAI




HAIRUHUSIWI KUNAKILI RIWAYA HII KWA NAMNA YOYOTE PASIPO RIDHAA
YA MTUNZI





No comments:

Post a Comment