Tuesday, December 1, 2015

KOSA SEHEMU YA KUMI NA NNE

   KOSA


MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



 ILIPOISHIA

Furaha ilidhihirika machoni mwetu kwa kufanikiwa kukivuka kikwazo kile lakini furaha hii haikudumu kwani dosari kubwa iliingilia furaha hii, tukiwa tupo katikati ya pori usiku majira ya saa sita milio ya risasi ilianza kusikika na vioo vya  gari letu vikaanza  kupasuka.Yule askari ambaye ndiye aliyekuwa dereva wetu alitoa ukelele wa maumivu akiachia usukani wa  gari
 na gari likaingia pembeni ya barabara nusura ligonge mti baada ya  yeye kuwahi kukanyaga breki ya gari.




ENDELEA NA MKASA HUU WENYE KUELIMISHA NA KUSISIMUA




SEHEMU YA KUMI NA NNE!!
Milio ya risasi iliendelea kurindima mithili ya ngoma kwenye sherehe ya kikabila, vioo vya gari letu vilitobolewa na matundu ya risasi ambazo zilikuwa zinatokea upande wa pili wa barabara. Muda huo mimi nilikuwa nimesharuka nje ya gari baada ya kuona kuwa ni hatari ndiyo ipo mbele yetu, Nurulayt naye alikuwa amesharuka nje ya gari kisha akajilaza chini kwenye miti mita kadhaa  kutoka barabarani. Hali ilikuwa ngumu kwa yule askari wa uhamiaji aliyekodiwa na Nurulayt atuvushe mpakani kwani alipojaribu kutoka kupitia mlango wa kushoto ambao alikuwepo Nurulayt kutokana na mlango wa kwake kutokuwa salama kuutumia risasi ilitua mgongoni mwake na kumfanya ageuke nyuma ili aweze kumshambulia aliyemtupia risasi, yule askari alipogeuka aliinua kichwa  ili aone vizuri kwani alikuwa amelala kifudifudi kutokana na risasi iliyompata mgongoni. Nikiwa nimejibanza kwenye mti mnene uliopo mita kadhaa kutoka barabarani, nilimshuhudia yule askari akitobolewa kichwa chake na risasi baada ya kuinua kichwa ili atazame upande anaotokea adui yake. Askari yule hakutoa hata neno la mwisho baada ya risasi hiyo ya masafa marefu  kutoboa kichwa kisha kuendelea na safari hadi kwenye shina mti nililosimama ikapita juu kidogo ya kichwa changu kisha ikaendeleana safari.
"Abdul lala chini haraka utakufa huoni risasi imekukosa hiyo"  Nurulayt aliniambia kwa sauti huku akiweka sawa bunduki aina ya short gun  aliyopewa na yule askari, nililala chini kwa haraka sana na macho nikawa nayaelekeza kwenye gari  letu ambalo bado lilikuwa linanguruma hadi muda huo kutokana na kutozimwa na taa bado zilikuwa zinawaka kuanzia ya ndani hadi za nje. Mlango mbele wa gari letu upande wa kiti cha kushoto cha dereva ulikuwa wazi baada ya yule askari kuufungua akijaribu kutoka nje hivyo ikawa njia  rahisi sana kwa mlengaji  kumuua kwani gari hii mlango mmoja ukiwa wazi basi taa ya ndani inawaka hivyo mtu wa nje anakuona kirahisi. Tukio hili ni tukio jingine linalonifanya nimshukuru Mungu katika maisha yangu kwani nafsi yangu ilinisihi nifungue kioo cha dirisha nililokaa baada tu ya kuvuka mpakani, Nurulayt naye alifanya hivyohivyo na dereva wa gari ambaye ndiye yule askari wa uhamiaji nchini Botswana wala hakufanya hivyo yeye aliendelea kuacha kioo kimepandishwa. Ndiyo maana hata kioo kilipovunjwa ni risasi iliyolengwa na ikampata begani kisha nyingine zikafuata
Tukiwa bado tumelala chini huku bunduki zetu tukiziweka tayari kwa lolote tuliwaona watu wasiopungua kumi wakiwa na bunduki aina ya AK47 karibia wote kasoro mmoa alikuwa ana bunduki aina ya sniper rifle, walikuwa wakitokea katika pori lililopo upande wa pili wa barabara.
"huyu mwenye bunduki ya wadunguaji ndiye aliyempiga dereva wetu risasi ya mgongo na ya kichwa, hivyo tunahitajika kuwamaliza wote ili tuendelee na safari la si  hivyo tutakwamia hapa" Nurulayt aliongea kwa sauti ya chini huku akiweka bunduki yake sawa.
"Hatuhitaji shambulizi la risasi wapo wengi wale tunahitajika tufanye kitu cha ziada" Nilimwambia Nurulayt huku nikiishusha bunduki yake chini kwani alionekana anataka kuitumia.
"come on Abdul kitu kipi hicho zaidi ya risasi kuwamaliza" Nurulayt aliniambia akionekana hajanielewa.
"una visu hapo?" Nilimuuliza
"ndiyo ninavyo hivi hapa" Nurulayt alijibu huku akifungua sare ya askari wa uhamiaji aliyoivaa akatoa visu vinne akanipatia.
"kuwa mtazamaji mama wa mtoto wangu" Nilimuambia huku nikichukua visu, Nurulayt  aliishia kutabasamu tu kisha akanikonyeza halafu akasema, " good luck ingawa sitaweza kukuona ili niwe mtazamaji". Nilitabasamu kisha nikaviweka visu mafichoni halafu nikaanza kujiburuta kama nilivyofundishwa na jeshi la jeshi la kujenga taifa kipindi namaliza kidato cha sita kwa mafunzo miezi mitatu, nilitambaa kwa umbali mrefu kidogo bila hata kujulikana na wale watu waliopo barabarani. Nilipokaribia eneo lenye nyasi ndefu niliokota kipande cha jiwe nikakirusha mbele yangu kiasi cha mita kadhaa huku nikiwatazama wale watu waliopo barabarani. Risasi zilimiminika kuelekwa upande niliorusha jiwe bila hata kuangalia kama kuna adui wanayemlenga, walipoacha kupiga risasi  nilimuona yule mwenye bunduki aina ya Sniper rifle akiwalaumu waliokuwa wanapiga  risasi kisha akawaamrisha waende kuangalia kuna nini. Amri hiyo waliyopewa ilinifanya nitabasamu tu kisha nikachukua majani mengi nikavijivisha mwilini mwangu kuanzia kwenye viatu hadi kwenye kofia ya sare niliyoivaa,  wale watu walikuja sita upande niliokuwepo kwa kasi bila umakini na walikuwa wanapita sehemu niliyopo mimi kwani ni sehemu yenye njia ya kuelekea upande niliorusha jiwe. Walikuwa wakitembea wawili wawili kwa haraka kuwahi eneo lenye majani mengi bila hata kuonekana kama wanafuata tahadhari yoyote, walipofika usawa wangu ndipo walipojuta kuja mbio bila uangalifu kwani wawili wa nyuma niliwazoa mtama na walipoanguka nilikuwa tayari nimesharukia nikawapiga magoti ya kwenye koo kila mmojs wakatulia kama maji mtungini. Wawili wa kati niliwarushia visu vya kwenye shingo kwa haraka walipotaka kugeuka nyuma kuangalia kilichowapata wenzao, nilipomaliza hayo nilijitupa pembeni kwenye vichaka haraka sana na hata wale wawili waliokuwa mbele walipogeuka waliona miili ya wenzao isiyo na uhai ikiwa ipo njiani.
" Oooh! Shit!" Aliongea mmoja kwa sauti huku akihangaika kuchomoa simu ya upepo iliyopo kiunoni mwake bila hata kuangalia usalama wa eneo hilo kutokana na kuchanganyika na vifo vya wenzao vilivyotokea ndani ya muda usiozidi dakika moja, hakutambua kama kufanya hivyo ni uzembe mkubwa katika eneo lisilo na usalama kama hilo. Vichwa vyao tayari vilikuwa vimevurugwa na tukio la kufa wenzao na hapo ndipo nilipopata nafasi ya kufanya shambulizi jingine la kimya kimya na la ghafla, niliachia visu viwili vilivyobakia ambavyo vilitua katika shingo zao nikilenga sehemu ya shingo ambayo ni mwanzo wa koromeo. Walidondoka kama mizigo kutokana shambulizi hilo kisha wakatulia bila hata kuonekana kufurukuta wakati roho zao zikiachana na mwili, hapo ndipo nilipojiuliza kwanini hawa watu wanakufa hivi bila hata kuonesha purukushani zozote kipindi wanaiaga dunia. Maswali yangu niliona hayana mtu wa kunipa  majibu hivyo sikutaka kupoteza muda eneo hilo hata kidogo, nilichukua bunduki nne zenye mikanda nikafunga usalama wa bunduki zote kisha nikazivaa mgongoni  na nilichukua vibebea visasi vilivyojaa kisha nikaanza kusogea upande wa barabarani kwa kujivuta taratibu mithili ya chatu aliyemmeza mnyama ambaye hajamshibisha kisawasawa. Nilipokaribia nililitazama eneo kwa umakini kisha nikachukua bunduki moja aina ya AK47 niliyoichukua kutoka kwa wale watu niliowaua, niliiangalia nikatoa uaalama wake nikaiweka tayari kuanza shambulizi huku nikiwatazama wale watu ambao sasa hivi wamebaki wanne tu. Sikutaka kusubiri tena nilianza kuwalenga kwa mfululizo wawili wakasalimiana na ardhi wakiwa wameshaacha roho za mikononi mwa malaika mtoa roho, waliobaki ni yule mwenye bunduki ya Sniper rifle na wengine wawili wenye AK47 kila mmoja.Walikuwa wamegusana migongo yao huku bunduki zao wakiwa wamezielekeza mithili ya pembe mshabaha, kila mmoja alikuwa akilinda usalama wa wenzake kwa nyuma yake. Walikuwa wakizunguka kula upande  ili wajihami kwani bunduki ile iliyowaua wenzao hawakujua imetokea wapi, walikuwa wakizunguka kuangalia pande tofauti wakionekana wamechanganywa na vifo vya wenzao. Yule mwenye sniper rifle alipoelekea upande aliopo Nurulayt wakati mwenzake akiwa nyuma yake akimlinda nilisikia mlio uliokaribiana na mzinga na wote wawili wakatupwa umbali wa mita moja toka pale waliposimama na damu ilikuwa imeanza kutoka katika vichwa vyao. Mlio huo ulipotoka na wale walipoanguka sikuona dalili za mtu yoyote kuja barabarani ingawa sauti hiyo ilikuwa ni ya bunduki aina ya shortgun, niliamua kutamba hadi nilipomuacha Nurulayt ili kuhakikisha kama ni yeye aliyepiga kwani bunduki kama iliyowapiga wale watu anayo mikononi mwake. Nilimshukuru Mungu nilipomkuta wa mama mtoto wangu salama akiwa amelala kifudifudi akiwa ameelekeza bunduki barabarani, nilimsogelea  Nurulayt karibu na nilipomfikia alishtuka  akanielekezea bunduki usoni kwa haraka sana akiwa amejigeuza akalala chali kwa haraka sana.
"hey ni mimi" Nilimwambia huku nikishtuka kutokana na uso wangu kutazamana na midomo miwili ya bunduki.
"muda mwingine uwe makini unapokuja kwani hiyo mijani uliyoivaa ningekutambua vipi, utakufa wewe mwanaume" Nurulayt aliniambia
"ok nimekuelewa, ile kazi ni ya mkono wako?" Nilimuuliza kuhusu wale watu wawili waliouawa na risasi moja niliyoisikia ikitokea upande aliopo.
"ndiyo, na wale watatu ni kazi ya mkono wako?" Alikiri ndiye aliyepiga ile risasi kisha akaniuliza swali.
"ndiyo, tena nina nyongeza mama" Nilimjibu huku nikiushuaha ule  mzigo wa risasi mgongoni.
"vizuri nadhani wale wengine umewazima" Nurulayt aliongea
"kabisa nimetumia vile visu hata sauti hawajatoa" Nilimpa uhakika wa kumalizika kwa kazi.
"kwa sumu iliyokuwa kwenye vile visu hata maji hawaombi kama vimetua shingoni mwao, twende zetu" Nurulayt huku akijiinua kutoka pale chini alipokuwepo  kisha akaanza kutembea huku akiwa ameinama na amakunja magoti kidogo. Nilimfuata kwa mwendo huo huo aliokuwa anatembea yeye hadi kwenye gari  letu, Nurulayt aliuvuta mwili wa yule askari wa uhamiaji aliyekusaidia kutuvusha hadi nje ya gari kisha akaokota silaha zote za wale watu waliotuvamia akazitia ndani ya gari. Tulilikagua gari letu.kwenye matairi tukakuta ni zima halina tatizo lolote, baada ya kuona tuna uwezo wa  kuendelea na safari hatukuwa na muda wa kusubiri zaidi ya kuingia ndani ya gari na safari ikaendelea kama kawaida ili  tulivuke pori hilo. Hadi tunalipita pori hilo tayari ilikuwa ni saa nane usiku na sasa tulikuwa tumeingia katika mji mdogo ambao sikuujua jina lake unaitwaje, mji ulitawaliwa na ukimya kutokana na wakazi wake kuwa wamepumzika muda huo wa usiku.  Nurulayt naye alizidi kubadili gia za gari akilipita eneo hilo ambalo  hakunitajia  linaitwaje hadi leo hii, alizidi kuwa makini na barabara huku akiwa kimya kabisa na alionekana hakutaka kuongea kabisa. Nilimuacha aendelee kuchezea usukani na mimi nikanyoosha kiti nikajilaza taratibu na usingizi ukachukua nafasi yake, nilikuja kushtuka usingizini baada ya kusikia napigwa kibao . Nilipofumbua macho nilimuona Nutulayt akiniashiria niinuke na mimi nikainuka, nilipotazama pembeni nje niliona giza bado lipo.
"vipi mbona umesimamisha gari hapa?" Nilimuuliza huku nikiangalia njia na nikagundua tupo sehemu yenye miti mingi.
"hebu vua hayo magwanda ya askariwa uhamiaji wa Botswana ni hatari kwetu" Nurulayt aliniambia huku akivua  magwanda yake pamoja na viatu, nami nilivua  magwanda yangu nikavaa nguo za kawaida nilizokuwa nimezivaa hapo awali. Nurulayt naye alivaa nguo zake za mwanzo na safari ikaendelea huku nikiuchapa usingizi kama kawaida. Niliamshwa kwa mara ya pili na Nurulayt tukiwa tupo katika eneo lenye mji mdogo uliochangamka ambao sikuutambua unaitwaje, kwa makadirio ilikuwa ni saa nne asubuhi kutokana na kuangalia upande ambao jua lipo tangu lilipoanza kuchomoza.
"hapa ni wapi?"Nilimuuliza huku nikipiga miayo kutokana na uchovu niliokuwa nao.
"hebu kwanza funga mdomo huo usije ukanimeza bure, hapa ni Runde hebu shuka tukapate stafustahi" Nurulayt aliniongea huku akinifunga mdomo  nilipokuwa napiga miayo, nilishuka kwenye gari na Nurulayt naye alishuka kisha tukaingia kwenye  mgahawa  uliopo pembezoni mwa barabara. Tulipata stafustahi tukarudi kwenye gari tukaendelea na safari kama kawaida, muda huo mimi ndiye niliyekuwa dereva wa gari na ikawa zamu yake Nurulayt kulala. Hadi inatimu saa tisa alasiri tayari nilikuwa nimeshafika katika kijiji ambacho sikukijua kinaitwaje kilichopakana na msitu mkubwa sana, nilipofika hapo nilimuamsha Nurulayt ambaye alishtuka kisha akaanza kutazama mazingira ya eneo tulilopo kisha akanitazama kwa mshangao sana.
"vipi mbona hivyo?" Nilimuliza baada ya kumuona ananishangaa sana.
"Abdul naona sasa tunataka kuuana" Nurulayt aliongea kwa kulalamika.
"kivipi?"Nilimuuliza.
"mwendo gani umeutumia hadi sasa hivi uwe umefika hapa kwenye hichi kijiji jirani na msitu huu wa Chirinda" Nurulayt aliongea akionekana ameshangazwa na mwendo nilioutumua hadi nimefika hapo.
" wa kifo" Nilimjibu
"sikupi uendeshe tena utaniua we mwanaume unafikiri hii formula one" Nurulayt aliongea.
"wewe ulivyokuwa unaendesha kule Kalahari ulikuwa huoni kama utaua mtu, tema unabahati ulilala yaani ungekuwa hujalala ungekufa kwa uoga" Nilimwambia huku nikishuka ndani ya gari, Nurulayt naye alishuka kwenye kisha akaniambia, " funga milango ya gari na unifuate". Nilifunga milango nikamfuata kuelekea katikati ya kijiji ambacho pia sikukitambua kinaitwaje hadi leo hii, Nurulayt aliniongoza hadi katika mlango wa nyumba ambayo inaonekana ni ya siku nyingi ingawa ina kila dalili za kufanyiwa marekebisho. Aligonga mlango  mara moja kisha akatulia kumya, mlango wa nyumba hiyo ulifunguliwa na mwanamke aliyejitanda vitenge vya kizaire ambaye hakuongea chochote zaidi ya kutuashiria tuingie ndani tu ndiye aliyefungua mlango. Sote wawili tuliingia ndani na mwanamke huyo akafunga mlango kwa makomeo kisha akatuuliza, " za safari?".
"Salama lakini sio salama sana" Nurulayt alijibu huku akimfuata yule mwanamke ambaye alikuwa anaingia katika chumba kimojawapo katika nyumba hiyo, nami niliwafuata bila hata kuambiwa niwafuate hadi ndani ya chumba hicho. Mandhari pana ya chumba chenye mitambo mbalimbali ya tarakilishi ndiyo ilionekana ipo ndani ya chumba hicho, upande mmoja kulikuwa kuna kitanda kipana cha kulala.
"jamani karibuni tena" Alituambia tena yule mwanamke.
"tushakaribia nadhani ni muda  muafaka wa kujua tusichokijua Madam Rhoda" Nurulayt alimwambia yule mwanamke kisha akanigeukia mimi akaniambia "Abdul huyu anaitwa Madam Rhoda kama ulivyosikia nikimuita, alikuwa ni msaidizi wa kaka yangu Sabir ambaye aliuliwa na Faiz kama nilivyokueleza hapo awali na ndiyo yeye aliyenipa mwongozo wa kazi hii ya kumtafuta mwanangu kwa kunipatia vifaa vya  kazi vya kusnzia".
Nilitabasamu baada ya kupokea utambupisho huo wa mwanamke aliyetupokea, yule mwanamke naye alitabasamu baada ya mimi kutabasamu.
"Madam huyu ni Abdul baba yake Ilham na nipo naye  kwenye kazi hii" Nurulayt alimpa utambulisho wangu yule mwanamke.
"ok, sasa tuanze kueleweshana" Yule mwanamke aliongea huku akibonyeza vitufe vya tarakilishi ya mapakato iliyopo humo ndani. Kwenye tarakilishi zilikuja picha mbalimbali za kambi ambayo ilionekana ilikuwa ipo katikati ya msitu, kambi hii ilikuwa imezungukwa na minara mbalimbali yenye vibanda kwa juu ambavyo hutumiwa na walinzi wa kambi hiyo.
"jamani hii ndiyo kambi ya kundi la Gorilla katika msitu wa chirinda, ipo kilomita mbili kusini mashariki mwa barabara ipitayo  katikati ya msitu huo, kambi hii ipo ni mali ya Scorpio nadhani Nuru unamfahamu" Yule meanamke alitoa maelezo halafu akamuuliza Nurulayt.
"Scorpio?! Hapana simfahamu" Nurulayt aliongea huku akivuta kumbukumbu katika halmshauri kuu ya mwili wake kama anaweza kumkumbuka lakini halmashauri kuu ambayo ni ubongo ilionesha kutolikumbuka jina hilo, hivyo yeye pia alikataa  kutolikumbuka jina hilo.
"ngoja nikuoneshe picha yake labda unaweza kumkumbuka maana sikuwahi kulijua jina lake halisi zaidi ya hilo la Scorpio" Madam Rhoda aliongea kisha akafungua faili moja lililopo kwenye tarakilishi  yake lililokuwa na picha ambayo sote tuliitambua kwa jina jingine kabisa.
"Faiz!" Nilisema kwa mshangao sana.
"sasa huyu ndiye mmliki wa hilo kundi ingawa kwa sasa hayupo nchi hii na hajulikani wapi alipo, Nurulayt nadhani unamfahamu." Madam Rhoda aliongea.
"muuaji aliyeutoa uhai wa kaka yangu nitamsahsu vipi? Kumbe bado yupo hai wale waasi  wa Kongo tumewalipa hela nyingi wamuue wamemuacha" Nurulayt aliongea kwa uchungu sana.
"haya jamani tuendeleeni na kilichowaleta" Madam Rhoda alisema huku akifungua picha za msitu wa Chirinda  sehemu ya kambi ya Gorilla boys halafu akasema, "kambi hii ina tower zisizopungua ishirini ambazo zina masniper zote sasa ukiingia bila tahadhari umeisha. Kushoto kwake ndani kuna majengo makubwa mawili ya ghorofa yenye makao makuu  ya kambi hiyo, upande wa kusini mwa makao makuu hiyo ndipo kwenye  ghala lenye vito vya thamani na madini mbalimbali waliyowahi kuyateka hawa watu".
ramani hii hapa itawasaidia kupata mwongozo mzuri tena inabidi muwe na bunduki aina sniper rifle kila mmoja kama mnataka muingie bila kugunduliwa kwani wale walinzi wa juu kwenye zile tower mnatakiwa muwaue mkiwa mbali ili wasiwaone wakawatungua, kumbuka wao ni sniper na ndiyo wenye kibarua kikuu cha kuilinda hiyo kambi. Je mna sniper rifle katika silaha zenu?" Madam Rhoda alieleza mwisho akatuuliza juu ya bunduki hiyo kama tunayo.
"ndiyo tunayo moja tuliyoipata kama ngawira" Nurulayt alijibu
"mnatakiwa muwe na ya pili kwani kutungua masniper ishirini sio mchezo hivyo kila mmoja anatakiwa awe na yake" Madam Rhoda alitusisitiza,  kusikia suala hilo wote tuliinama chini kutokana na kutokuwa na namna ya kuipata hiyo silaha.
"hilo msijali nitawasaidia mtimize wajibu wenu, Nuru hebu lete briefscafe mbili zipo chumba ninacholala" Madam Rhoda alimuamuru Nurulayt ambaye alitoka haraka aliposikia amri hiyo kisha akarejea akiwa mikoba miwili ya kufunga kwa namba akampatia Madam Rhoda.


*kesho kutwa nayo siku uhai na afya vinahitajika kulijua KOSA.

No comments:

Post a Comment