RIWAYA: KOSA
MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
ILIPOISHIA
"ndiyo tunayo moja tuliyoipata kama ngawira" Nurulayt alijibu
"mnatakiwa muwe na ya pili kwani kutungua masniper ishirini sio mchezo hivyo kila mmoja anatakiwa awe na yake" Madam Rhoda alitusisitiza, kusikia suala hilo wote tuliinama chini kutokana na kutokuwa na namna ya kuipata hiyo silaha.
"hilo msijali nitawasaidia mtimize wajibu wenu, Nuru hebu lete briefscafe mbili zipo chumba ninacholala" Madam Rhoda alimuamuru Nurulayt ambaye alitoka haraka aliposikia amri hiyo kisha akarejea akiwa mikoba miwili ya kufunga kwa namba akampatia Madam Rhoda.
ENDELEA NA MKASA HUU WA KUSISIMUA WENYE KUFUNDIDHA
SEHEMU YA KUMI NA TANO!!
Nurulayt alimkabidhi mikoba hiyo Madam Rhoda ambaye aliipokea kisha akaufungua mmojawapo
akatuonesha kilichopo ndani yake, bunduki aina ya sniper rifle ya kisasa ndiyo tuliyoiona ikiwa imefunguliwa na imegawamywa vipisi.
"bunduki ni hizi hapa moja mmeiona nyingine ipo kwenye hii briefscafe ambayo haijafunguliwa" Madam Rhoda aliongea kisha akaanza kuifunga taratibu hadi ilipokamilika, alipoikamilisha bunduki hiyo alitutazama kama tupo pamoja nae nasi tulitikisa vichwa kuashiria tupo pamoja nae. Aliporidhika kuwa tumeelewa namna ya ufungaji bunduki ile aliinama chini ya meza akatoa makasha mwili madogo akayaweka mezani, alipoyafungua macho yangu yalikutana na risasi ndefu ambazo mara nyingi hutumiwa katika bunduki za masafa marefu kama sniper rifle.
"risasi hizi hapa nadhani mnaelewa jinsi ya kuziweka na kuzitumia" Madam Rhoda aliongea
"hilo lisikupe tabu tunaelewa namna ya kutumia" Nurulayt alimwambia Madam Rhoda.
"ok mkishawamaliza hawa masniper wa kambi hii, mvuke uzio kwa umakini na mtumie bunduki isiyo na sauti humo ndani au iliyowekwa kiwambo cha kuzuia sauri ili vijana wa kundi hili la Gorrila wasishtuke mapema itakuwa ni hatari kwenu ikiwa watawagundua mapema. Mkifanikiwa kuwapunguza bila kugundulika mtakuwa mmepunguza idadi kubwa ya maadui kwenu, sidhani kama itakuwa ngumu kwenu" Madam Rhoda alitueleza huku akituelekeza kupitia ramani iliyopo kwenye tarakilishi yake ya mapakato, alipofikia hapo aliifunga tarakilishi yake kisha akasema, " nawatakieni kazi njema". Sote tulitabssamu baada ya kusikia hivyo kisha tukapeana naye mikono huku tukiwa tayari tumepokea makasha yenye risasi kwa ajili ya bunduki tulizopewa, tuliyaweka yale makasha kwenye mikoba tuliyokabidhiwa kisha tukatoka humo ndani tukiwa tumeongozana na madam Rhoda hadi sebuleni.
"napenda niwaage hapahapa mimi si mtokaji nje kwani natafutwa na wabaya wangu, namba ya hizo briefscafe ni 1789. Kila la heri" Madam Rhoda aliongea huku akinipatia mkono halaf akakumbatiana na Nurulayt kwa uchangamfu hafifu kisha akatufungulia mlango, tulitoka tukampungia mkono kisha tukaanza kuondoka kwa mwendo wa haraka tukiwa makini sana. Tulipita njia ileile tuliyopita awali hadi tulipoliacha gari letu ambalo lilikuwa salama, nilifungua milango nikaweka mkoba ndani na Nurulayt naye akaweka mkoba wake halafu akaniambia, "nisubiri hapahapa narudi sasa hivi". Alishuka kwenye akaingia mitaani na alirejea baada ya dakika kumi akiwa na mfuko mweusi ambao aliujaza vitu, aliingia ndani ya gari akautupa mfuko huo kiti cha nyuma halafu akasema "tuondoke fuata barabara inayoingia msituni". Nilipopata maelekezo yake niliwasha gari nikaliingiza barabarani nikaliondoa kwa mwendo wa wastani hadi nilipokiacha kijiji kisha nikaendesha mwendo niliokuwa nauendesha wakati Nurulayr akiwa amelala, niliweka gia namba tano kisha nikakanyaga mafuta hadi Nurulayt akawa ananishangaa na aliwahi kufunga mkanda wa gari kwa tahadhari ya usalama wake.
"Abdul tunakomoana siyo" Aliniambia kwa mshangao kutokana na mwenfo kasi ninaoutumia.
"kulichokutuma ukaniachia gari ni nini wakati ulisema huniachii tena, sasa leo mpaka utapike kwa mwendo huu" Nilimwambia huku macho yangu yakiwa mbele ili nisipoteze umakini kwani tulikuwa tumeingia katika eneo la msitu wa Chirinda tayari.
"haya baba Ilham we tumia mwendo huo wakati njia huijui subiri upitilize utajijua mwenyewe" Nurulayt aliniambia hivyo ili nipunguze mwenfo lakini sikupunguza na nilizidi kukanyaga mafuta huku niliwasha taa kutokana na mazingira ya msitu kuonekana kuwa giza tulipofika katikati ya msitu huo. Baada ya mwendo mrefu niliiona njia iliyoonekana kama ni njia za miguu mbili ambayo kabisa nilijua ilitokana na upitishwaji wa gari sehemu yenye majani mengi na kupelekea majani yaliyokanyagwa yakauke kabisa yakatengeza njia mbili zenye ukubwa sana na njia ya watembea kwa miguu porini. Hapo ndipo nilipopunguza mwendo kidogo kisha nikaingia katika njia hiyo nikikata kona kali hadi Nurulayt akayumba ila mkanda aliouvaa ulimsaidia, Nurulayt alinitazama kwa mshangao ambao sikuujali kabisa zaidi ya kuzidi kukanyaga mafuta ya gari nilipoingia kwenye njia hiyo. Niliendesha gari kwa umbali wa wastani kisha nikakata kona kwa kasi nikaitumbukiza gari kwenye kichaka ambacho kilikuwa kimefungamana miti, upande niloupitia kulikuwa kumevunjwa baadhi ya miti na gari hili ingawa sikuiharibu gari. Niliizima gari pamoja na taa zote kisha nikashuka nikaenda kuchukua majani nikaziba njia niliyoingilia pamoja na kulifunika gari kwa matawi ya miti, Nurulayt hadi muda huo alikuwa akihema kutokana na kona ya ghafla niliyoikata na alikuwa bado yupo ndani ya gari. Nilipohakikisha usalama wa kutosha wa gari nilirudi ndani ya gari nikaingia sehemu ya dereva nikalaza kiti nikatulia.
"Abdul hivi hii njia mpaka tunafika huku umeijuaje wakati wewe siyo mwenyeji?" Nurulayt aliniuliza.
"ramani ya madam Rhoda ndiyo imeniongoza hadi nikafika hapa, wakati tunaelekezwa mimi nilishaikariri" Nilimjibu huku nikimtazama usoni, Nurulayt naye alikinyoosha kiti chake kama nilivyonyoosha mimi akawa amegeuza shingo akawa ananitazama.
"wewe mwanaume sikuwezi hata kidogo yaani umeniweka roho juu sana" Nurulayt aliniambia huku akiniangalia kwa macho malegevu.
"mmmh! Wewe je?" Nilimuuliza.
"Abdul kuna kitu nataka nikuambie" Nurulayr aliongea jambo jingine kabisa akiacha mada tuliyokuwa tunaongea hapo awali.
"sema nakusikiliza" Nilimwambia huku nikiwa tayari kusikiliza ingawa nilihisi kitu katika macho yake, baada ya kumuambia Nurulayt hivyo aliamua kujisogeza karibu yangu akitaka kuleta mdomo karibu na kinywa changu huku macho yake akiwa kayalegeza yanaelekea kama anataka kusinzia. Alipokaribia kugusa kinywa changu nilimzuia kwani sikutaka jambo hilo litokee kwa muda huo, Nurulayt alionekana kushangaa kwa kitendo hicho kisha akawa na sura yenye masononeko ghafla.
"sio muda wake huu Nuru" Nilimwambia Nurulayt.
"Abdul please kidogo tu" Nurulayt aliniambia huku akijaribu kuleta kinywa chake kwangu na ikanibidi nimzuie tena kwani sikutaka jambo hilo litokee kwa muda huu.
"Nuru tupo kwenye kazi sasa habari hizi weka kando kabisa" Nilimwambia Nurulayt huku nikiweka sura ambayo ilimaanisha ninachokiongea.
"basi busu refu tu Abdul nipatie" Nurulayt aliendelea kunisihi nifanye anachokitaka lakini sikutaka kumuelewa.
"natambua kinachoamsha hisia zako ni busu sasa nikikupa busu yatakuwa mengine hayo Nuru, elewa tupo kazini hapa" Nilimwambia Nurulayt naye akarudi sehemu yake akatulia, ilinibidi nifanye hivyo kwani sikuwa tayari kumsaliti Sarina hata kidogo kutokana na ahadi tulizowekeana naye. Kutembea na Nurulayt kwa muda huo kwangu niliona hatia ndiyo maana nikaamua nitafute kisingizio cha uwepo wa kazi yetu, tulipumzika hapo kwa muda mfupi kisha baadae tukaanza kuaandaa silaha na tulimaliza kabla hata giza halijaingia. Giza lilipoingia kabisa tulikula chakula ambacho kilikuwa katika mfuko mweusi aliokuja nao Nurulayt halafu tukaamua kulala ili kupumzika zaidi kwa ajili ya kazi nzito ambayo tunaenda kuikabili masaa kadhaa yajayo, baada ya masaa kadhaa niliamka na nikamuamsha na Nurulayt ili tujiandae kwa ajili ya safari yetu. Tulikuwa tupo ndani ya giza nene lililozidi kutisha kutokana na miti mingi iliyopo katika msitu huo, tulibeba silaha zetu ambazo zilikuwa ni mzigo kwetu tukaelekea upande wa kusini mashariki tukiwa tunatembea kwa umakini pia kwa mwendo wa taratibu kutokana na silaha tulizozibeba kuwa nzito. Baada ya kutembea mwendo mrefu tulianza kuona waya ukiwa umekatiza katika eneo ambalo lilikuwa linaonekana kutokana na mwanga wa mwezi kupita katika eneo hilo ambalo lilionekana kukatwa baadhi ya miti, nilimuonesha Nurulayt huo waya ambao ni mwembamba wenye rangi ya fedha ambao niliuona kutokana na mng'ao wake baada ta kupigwa na mwanga wa Mwezi.
"kuwa makini nao huo ni mtego yaani ukiusukuma au ukiukanyaga hslafu ukauachia basi jua unalipuwa vipande vipande na bomu lililounganishwa na huu waya" Nurulayt aliniambia na ikanibidi niuruke lakini nilipouruka niliweka mguu pabaya nikajikuta nimezolewa kama mzigo na nipo kichwa chini miguu juu nikining'inia huku mguu wangu mmoja ukiwa umefungwa kamba juu ya mti, nilikuwa nimenaswa na mtego ambao hutumia kamba inayowekwa kitanzi chini na matawi ya miti. Ikiwa utakanyaga kwenye kitanzi kilichotegeshwa jua kuna tawi la mti ambayo liliinamishwa kwa nguvu litaifyatua ile kamba na kitanzi kitabana mguu wako. Haya ndiyo yaliyonikuta mimi na nilipomtazama Nurulayt alionekana kushtuka na alitaka kunipa kisu ili niikate lakini nilimzuia kisha nikaishika ile kamba na nikaipanda hadi juu ingawa ilikuwa ikiniumiza mikono, nilipofika mwisho wa ile kamba nilikaa kwenye tawi la mti nikatazama mbele upande tuliokuwa tunaelekea na nikavutika nizidi kuangalia kutokana na nilichokiona huko mbele. Kambi ya Gorrila boys ndiyo ilikuwa mbele ya macho yangu ikiwa ipo kwenye eneo lililokaa kama bonde lenye umbo la duara, juu ya bonde hilo kulikuwa na minara yenye vibanda ambayo tuliiona kwenye tarakilishi ya Madam Rhoda ikiwa na taa kubwa ambayo ilikuwa ikizungushwa na mtu aliyekuwa kwenye kila mnara ili kumulika maeneo ya kando ya kambi kwa ajili ya usalama wa kambi. Nilipooona mszingura yote niliifungua ile kamba mguuni na nikashuka kwenye mti huo upesi hadi chini nilipomuacha Nurulayt akiwa ananitazama pamoja na kutazama mazingira ya eneo hilo.
"kambi ipo karibu pita kushoto na mimu nipite kulia kisha tuanze kutungua masniper wote mpaka waishe, tutakutana kwenye mlango wa ghala lao wanapotunza vito na madini" Nilimwambia Nurulayt ambaye alitii na akapita kushoto na mimi nikapita kulia nikafuata mlima ambao upo jirani na kambi hiyo, hapo nikawa nipo peke yangu na niliomba Mungu nikutane na Nurulayt kwenye mlango wa lile ghala.
Nilitembea hadi kwenye ncha ya jabali lililopo kwenye kilima ambacho upande wa pili kuna kambi ya Gorilla boys, hapo nilitua silaha zangu kisha nikaichukua bunduki aina ya sniper rifle ambayo tulipatiwa na Madam Rhoda nikaiweka visimamio vyake na na nikaikagua darubini yake nikaona inafaa kisha nikaanza kupitia vibanda mbalimbali vya vinara yenye wadunguaji ishirini. Kibanda cha kwanza niliona kitupu na nilipokagua niliona mtu kalala chini, nilipokagua kibanda cha pili niliona mdunguaji wa pili akishtuka na kuanguka, hapo ndipo nikatambua kama Nurulayt ameanza kuwatungua wale wadunguaji wa kambi hii kama anatungua maembe kwenye shamba lisilo lake kwa wizi. Nami nilianza kwa kupitia kibanda ambacho taa inazungushwa nikamtungua mdunguaji wa pale na nilifanya hivyo hadi vibanda vyote vilipokuwa vitupu kutokana na Nurulayt naye kupitisha mkono katika udunguaji, nilipoona wameisha nilianza kuwalenga walinzi waliokuwawapo peke yao hadi wakaisha. Nilipoona wameisha nilibeba silaha zangu nikaanza kuteremka bondeni kuifuata kambi hiyo kwa mwendo wa kasi na wa kimya kimya hadi jirani na uzio wa kambi, niliweka baadhi ya silaha zangu chini na nikazificha kwenye kichaka kilicho jirani na eneo nililosimsma. Nilichukua bunduki aina ya UZI mbili zenye viwambo vya kuzuia sauti, Shotgun moja ya bomba mbili na MP5 moja pamoja vibebea risasi kadhaa, Shotgun pamoja na MP5 nilizivaa mgongoni huku UZI mbili zenye viwambo vya kuzuia sauti nikizishika mikononi mwangu. Bunduki hizi nilizozichagua niliwahi kusikia sifa zake kwenye mitandao na uwezo wake na hii Shotgun ya bomba mbili usiku wa siku iliyopita nilishuhudia mwenyewe ikiua watu wawili kwa risasi moja tu, hivyo niliona zinafaa kwa kazi yangu sikuwa na shaka nazo.
Niliamua kwenda mbele ya kambi hiyo kwa kupitia vichakani hadi nilipofikia lango kuu la kuingilia ndani, kwenye geti hilo kulikuwa kuna walinzi sita ambao walikuwa wapo makini kuangalia pande zote. Walinzi hapo walikuwa wamejipanga mbalimbali hivyo ikanibidi nipige hesabu za jinsi ya kuwavaa hadi nikapata mbinu, nilimpiga risasi aliyekuwa wa mwisho upande wa kushoto akaanguka chini na kupelekea walinzi wote waelekeze bunduki zao kule wakijua nipo upande ule. Walifanya kosa kubwa sana na likawagharimu maisha yao kwani niliwamiminia risasi wote wakafa papo hapo, nilitembea hadi getini haraka haraka nikaangalia sikukuta mtu na nikaamua kuingia ndani nikitembea kwa umakini na nilijibanza kwenye kingo za mahema ambapo nilisikia minong'ono ya watu ikitokea ndani kuashiria kuna kundi la watu walikuwa wanazungumza. Nilipobaini uwepo wa watu mule ndani niliamua kuzunguka nyuma nikiona ni jambo sahihi kumbe nilikuwa nimefanya kosa kubwa, nilipofika huko nyuma ya hema hilo nilisikia mlio wa kengele ndogo ikilia kwa nguvu kisha kengele ya hatari ikafuata na kupelekea eneo nililokaa libadilike liwake taa nyekundu na nilipoangalia juu ya eneo nililosimama niliona kamera ya ulinzi ikiwa inawaka taa nyekundu huku kengele ya hatari ya kambi nzima ikisikika. Nilianza kusikia vishindo vya watu wakikimbia hata hili hema nililokuwa nipo nyuma yake nilianza kusikia watu wakitoka na ikanibidi nitoe kisu nichane hema na nikaingia ndani ili nipate usalama. Nilitokea katika eneo lenye vitanda mbalimbali vya kubebana na ina meza kubwa iliyo na mabomu kadhaa ya kurusha, hema hili lilionekana kuwa na vyumba viwili hivyo ilinibidi nikague vyote na nilipoona hamna mtu nilibeba mabomu kumi ya kurusha kisha nikanyata kufuata mlango wa kutokea nikiwa na mabomu matatu mkononi na saba mfukoni. Nilipofika karibu na mlango nilijibana pembeni nikachungulia nje ambapo nilioona kundi kubwa la watu wakiwa wamechuchumaa wakimzunguka mtu mmoja ambaye alionekana kuwapa maelekezo.
"wakasalimie babu zao kuzimu hawa" Nilijisemea kisha nikachomoa pini za mabomu matatu kwa mpigo nikayarusha kwa nguvu hadi katikati yao, kishindo kikubwa kilitokea huku yakusikika mayowe ya maumivu ambayo niliyapuuzia. Nilipohakikisha hajapona hata mmoja nilitoka nikawa nakimbia kuelekea lilipo ghala lao, namshukuru Mungu nilifanikiwa kufika salama na nikamkuta Nurulayt akiwa yupo mlangoni akiningoja na aliponiona aliingia ndani nami nikaingia halafu mlango akaufunga. "Abdul unataka kuharibu kazi?" Nurulayt aliniuliza baada ya kumaliza kufunga mlango.
"ni bahati mbaya sikujua kama kuna kamera za ulinzi hapa" Nilimwambia huku nikihema sana kutokana na matukio niliyoyafanya nilihisi yanataka kunichanganya kichwa changu kwani suala la kuua sio jambo dogo.
"humu kuna kamera za ulinzi automatic ambazo si lazima ziwe na msimamizi kwenye chumba chake, zina taa juu yake hiyo kamera ikimuona mlinzi au mtu yoyote wa humu ndani inawaka kijani na ikimuona asiyehusika inawaka nyekundu na inatoa alarm ndogo itakayosababisha alarm kuu ya humu ndani iwake na ndiyo maana alarm imelia, twende tukamalizie kazi" Nurulayt alinipa maelezo kuhusu kamera yenye uwezo ambao sikuwahi kuusikia.
Tulitembea ndani ya ghala hadi tulipona ngazi zinaingia kuelekea chini ambazo tulizifuata na tukakuta kote kupo kimya, tuliingia chini ya ardhi kabisa hadi katika eneo lenye madini tofauti yaliyopangwa vizuri katika viberenge mbalimbali vilivyopo kwenye reli maalum zinazopita kwenye mashimo maalum yaliyochongwa vizuri. Kila madini yaliandikwa uzito wake na ikatufanya tuone viberenge viwili vyenye kuunganishwa vilivyosheheni almasi vikiwa vimeandikwa kilo 600 katika kasha la madini lililopo juu ya viberenge hivyo, tulipokiona viberenge hicho tulikisukuma hadi kwenye reli zilizopo humo na tukapnda baada ya viberenge kukolea mwendo. Viberenge hivyo vilipita sehemu yenye mteremko mkali na kupelekea mwendo uongezeke, baada ya muda mfupi tulifika mwisho wa reli hizo kukiwa na uwanja mdogo wenye helikopta kubwa, pembeni kuna mashine ndogo ya kubebea mizigo yenye gia nyingi za mkono kwa ajili ya kuiongoza. Eneo hilo nalo lilikuwa tupu kabisa na halikuwa na mtu hivyo kazi yetu ikafanyika kwa urahisi kabisa, Nurulayt aliunyanyua ule mzigo wote kwa kutumia ile mashine ya kubebea mizigo akauingiza ndani ya helikopta kisha akaingia ndani akakaa sehrmu ya rubani akaniambia, "panda twende".
" unaweza kuendesha helikopta?" Nilimuuliza.
"hebu wacha maswali yako panda bwana wanakuja hao" Nurulayt aliniambia na muda huo huo tukasnza mtikisiko ambo unatokea ikipita treni, nilipanda kwenye helikopta haraka sana nikiwa nimekaa mlangoni kwa tahadhari. Nurulayt aliwasha helikopta na aliipandisha juu baada ya kuanza kuchanganya huku akiiongoza kuelekea mashariki ili aiache kambi hiyo. Helikopta ilipokuwa juu kabisa wale watu walikuwa wameshafika pale kwenye uwanja ilipokuwa imeegeshwa, walianza kutupa risasi lakini Nurulayt aliongeza mwendo akawaacha.
*tamati ya KOSA ileee, tukutane panapo uhai kulihitimisha hili kosa.

No comments:
Post a Comment