RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE!!
"Annie rafiki yangu nimekukosea nini mimi?" Viktoria aliuliza huku akilia kwa uchungu.
"hujanikosea kitu ila mdogo wako kapenda nilipopenda ndiyo kosa lake linalokufanya uteseke, pia tabia ya kupiga makelele humu haitakiwi na nikisikia unagoma kula nakata pua hiyo. Chukua chakula na ule upesi sasa hivi" Annie aliongea kwa ukali na Viktoria akasogea hadi kwenye meza iliyopo humo chumbani akachukua chakula akaanza kula.
"nilimuahidi Moses maumivu ya kibao alichonipiga nitashare na mtu mwingine ndiyo maana nimekupa kipigo wewe, tena mdogo wako asipomuacha Mosea nitakuua halafu nitamteka mama yako pia nitamuua. Sitaki nimteke yeye sababu nitamkosa Moses moja kwa moja" Annie aliongea kwa hasira sana.
****
"Annie hivi wewe na Moses mna uhusiano mpaka useme hivyo, si ulimuona baada ya kuletwa na mdogo wangu nyumbani. Isitoshe wewe umetembea na mjomba wake Moses Tasu mara nyingi sana tena mlikuwa kwenye mapenzi mazito sana" Victoria alilalamika huku akilia kwa uchungu kwa kuonewa bila sababu yoyote.
"Kelele! Wewe hivi unajua maana ya kupenda wewe? Hata kama nilikuwa na mahusiano na mjomba wake na ameuchezea mwili wangu vya kutosha it doesn't matter, Tasu alikuwa mpenzi wangu na si mpenzi wangu hadi sasa. Pia wa kwanza kumpenda Moses kati yangu na Beatrice haijalishi chochote kwangu, ninachokijali kwa sasa ni Moses kuwa mikononi mwangu na si vinginevyo tena ikibidi hata kumuondoa Beatrice duniani kama itawezekana lakini si kumkosa Moses mwanaume ninayempenda" Annie aliongea kwa ukali kisha akashusha pumzi akamuangalia Victoria kwa dakika kadhaa halafu akasema, "Siwezi kumuua mdogo wako kwa sasa kwasababu nitachukiwa na Moses na pia sitokuachia wewe mpaka vitu viwili vitimie ambavyo ni vifuatavyo, cha kwanza ni Moses awe mikononi mwangu na cha pili ni Moses afute tape ya ngono aliyonikashifu ambayo ana mpango wa kuisambaza mitandaoni. Visipotimia hivyo utaanza kufa wewe atafuata mama yako na kisha baba yako yaani vita haitaisha mpaka Moses awe katika mikono yangu. Upo hapo bibi? Haya kula chakula upesi na kiishe"
Maneno hayo yalimfanya Victoria azidi kulia huku akiwa na chakula mdomoni, hakika hakutegemea wala kutarajia kama rafiki yake kipenzi wa siku nyingi atakuja kumfanyia kitu kama hicho na hata kutaka kuiua familia yake kisa anapenda asipopendwa.
"Tena uoge maana unanuka jasho tangu uletwe humu hujaoga na vipodozi vyote unavyotumia ukiwa kwenu vipo pale kwenye dressing table na nguo size yako zipo pale kwenye kabati ubadili hizo ukioga sitaki mtu mchafu kwenye chumba kisafi kama hiki, Umesikiaa! Sasa leta jeuri au kiburi nikupeleke selo ya basement ya jengo hili haja uwe unamalizia kwenye ndoo utajuta na huko utakuwa mke wa vijana wangu yaani kila siku kazi yako ni kuwaburudisha kimwili" Annie aliongea kwa ukali sana hadi victoria akaogopa maana hakuwahi kumuona rafiki yake akiwa katika ukali namna hiyo.
"Sa.....sawa" Victoria aliitikia kwa kubabaika kutokana na kumuogopa sana Annie baada ya kumfahamu upande wa pili alivyo, alimzoea Annie yule ambaye hakuwa ameyaficha makucha yake na sasa anakutana naye akiwa Ameyakunjua makucha yake yaliyomjaza hofu moyoni mwake. Hakuwa anajua kama ana urafiki na chui mwenye njaa ya kutaka asicho na haki nacho ambaye nje amejivika ngozi ya kondooo ili awahadae kondoo wengine kwamba ni mwenzao jambo ambalo siyo kweli, sasa chui huyo ameivua ngozi ya kondoo aliyoivaa na kumfanya aonekane na ngozi yake halisi. Hofu zaidi ya hofu juu ya hofu ndiyo ilitanda katika moyo wa Viktoria kwa jambo ambalo hakulitarajia na sasa limemjia, hana pakukimbilia na akileta ujanja balaa zaidi atajiletea.
Usiku wa siku hiyo Annie aliondoka kurudi kwao akimuacha rafiki aliyekuwa mpendwa akiwa yupo ndani ya chumba kizuri ambacho kilikuwa ni zaidi ya jela.
****
Siku iliyofuata Moses aliamua kuwasiliana na Allen na alipompata alimuomba kuonana naye katika hoteli ya Mangrove, majira ya saa nne asubuhi katika sehemu ya viti maalum ya hoteli hiyo walionekana vijana watatu ambapo mmoja wao alionekana kuwazidi umri wengine wakiwa wamekaa kwenye meza iliyojitenga ndani hoteli hiyo. Vijana hao walikuwa ni Moses, Hillary na Allen ambao ndiyo waliadiana kuwepo eneo hilo.
"ndiyo madogo nawasikiliza" Allen aliongea akiwa ameshika bilauri ya kinywani mkononi mwake.
"Kaka mkubwa tumekuita hapa ili tupate ushirikiano wako wa mali au hata mawazo katika jambo hili, nadhani unatambua juu ya jambo lililomkuta Victoria" Moses aliongea
"ndiyo natambua ila kwa sasa hiyo taarifa hainihusu na siwezi nikajishughulisha nayo" Allen aliongea kwa msisitizo.
"Broda tunatambua Viktoria alikuwa mpenzi wako huoni kama hutendi haki isitoshe alikuwa anakupenda na wazazi tu ndiyo waliwatenganisha" Hillary alimwambia Allen.
"hata kama siwezi kumsaidia yule mzee aliyenitesa mpaka nikaondolewa kwenye nchi hii niliyozaliwa nikakulia kisa tu nina uhusiano na mtoto wake, sina matumaini ya kuwa na Vicky tena ndiyo maana sitasaidia chochote katika hili labda mkamuambie yule kahaba mwenye urafiki nae" Allen aliongea kwa hasira.
"bro wanadamu hatuendi hivyo hebu weka utu kidogo kwa mtu aliyekupenda na hakuwahi kukusaliti hata siku moja, huoni kama ni jambo jema kufanya hivyo. Pia hatuwezi kumtegemea Annie maana ni adui yetu" Moses aliongea kwa ustarabu.
"hivi nyie madogo mnaongea nini aliyonifanyia baba yake wanadamu ndiyo wanaenda vile? Isitoshe katuma askari wamekuja kunizoa home wakanipeleka kisa Vicky kutekwa. Yaani narudi nchi hii niliyozaliwa nikijua nitakuwa na amani sasa na matokeo yake hata nusu mwaka sifiki naanza kukumbwa na vibweka vya huyo mzee wa kihaya. Kiufupi ni kwamba sipo tayari muache huyo mzee ahangaike hadi alie kama akishindwa" Allen aliongea kwa hasira kisha akainuka kwenye kitu alichokaa akaondoka.
"Dah! Kazi ipo hapa" Moses aliongea akionekana kusononeshwa na maneno ya Allen kisha akainamisha kichwa chini ya meza
"mtu wangu hapa haina jinsi maana jamaa ndiyo huyo kakutolea nje katika kumtafuta Vicky, tusubiri tu uchunguzi wa polisi na si vinginevyo" Hillary alimwambia Moses huku akimshika bega, maneno ya Hilary yalimfanya Moses ainue kichwa chake kisha akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akasema, "sipo tayari kusubiria polisi bali nipo tayari kuona furaha ya Beatrice na si huzuni".
"Moses unamaanisha nini kusema hivyo" Hilary alimuuliza.
"kiufupi ni hivi nitamtafuta Vicky kwa mikono yangu mwenyewe nahakikisha kabla nekta haijaanza Vicky kashapatikana. Sitaki Beatrice afeli kisa jambo hili na sitaki Beatrice awe na huzuni kisa jambo hili" Moses aliongea kwa hisia kali.
"Moses huoni hiyo kitu ni too dangerous, buddy utaingia matatani maana huwajui hao watu waliomteka Vicky ni wa aina gani" Hilaty alizidi kumshauri Moses.
"Hilary napenda kuona furaha katika uso wa Beatrice hivyo basi kama na wewe unapenda kuona furahs ya Shem wako nadhani utaniunga mkono na kama hupendi hutaniunga mkono, upo pamoja na mimi?" Moses aliongea na mwisho wa maneno yake akaliza swali lililhitaji ushirikiano na jibu kutoka kwa Hilary.
"Tupo pamoja Moses wewe ni rafiki yangu wa siku nyingi siwezi kukusaliti hata siku moja" Hilary aliongea hiku akimpa mkono Moses.
"sasa tuianze hii kazi haraka iwezekanavyo nifuate" Moses aliongea akainuka kwenye kiti akaondoka na Hilary naye akaminuka kwenye kitu akamfuata
****
BUNJU
DAR ES SALAAM
Binti aliyevalia mavazi ya kampuni ya usambazaji maji jijini Dar es salaam maarufu kama Dawasco alionekana alifika kwenye nyumba ambayo ndiyo yalikuwa makazi ya vijana wa Brian akabonyeza kengele ya getini mara moja, mlango wa nyumba hiyo ulifunguliwa na mwanamke aliyejifunga kitenge kuanzia kifuani na kichwani alikuwa na taulo .
"Habari za hapa?" Binti huyo mfanyakazi wa kampuni ya usambazaji ya Dawasco alisalimia.
"Salama, sijui nikusaidie nini?" Yule mwanamke aliitikia salamu akamuuliza.
"Naitwa Debora Kaimuzi ni mfanyakazi wa Dawasco nimekuja kusoma mita ya maji nadhani taarifa za ujio wetu zinajulikana tangu wiki iliyopita" Debors aliongea
"mwenzangu sisi ndiyo kwanza tunahamia majuzi tu na taarifa nimezipata leo asubuhi tu. Karibu ndani dada" Mwanamke huyo aliongea kisha akamkaribisha Debora ndani ya nyumba hiyo, Debora aliingia ndani ya hiyo nyumba huku akikagua kila sehemu ya nyumba hiyo kwa kuzungusha macho yake kwa tahadhari. Alienda hadi sehemu yenye mita akafungua mfuniko wa plastiki uliyoifunika mita akasoma halafu akaandika kikaratasi kidogo akampatia yule mwanamke huku akimwambia, "hiyo ndiyo bili yenu nadhani umenielewa".
"Sawa dada hamna shida akija mume wangu nitampatia" Yule mwanamke aliongea huku akiipokea bili ya maji kutoka kwa Debora.
"haya dada nashukuru nilijua nikija nitawakuta wale wazungu niliowazoea kumbe tayari wamehama, wacha niende nikawahi kumalizia kufanya kazi ofisini" Debora aliaga.
"haya karibu tena dada" Mwanamkehuyo alimuaga kisha akafunga geti baada ya Debora kutoka nje.
Debora alipotoka nje ya geti alisimamusha pikipiki iliyokuwa ikipita akapanda akamtajia dereva wa pikipiki mahali alipokuwa anakwenda na pikipiki ikaondolewa kwa mwendo wa kasi.
Baada ya dakika mbili tu tangu Debora aondoke katika nyumba hiyo gari la kampuni ya Dawasco aina ya double cabin Toyota hilux lilifika kwenye geti la nyumba hiyo likasimama, Debora akiwa na mavazi yaleyale alishuka ndani ya gari akaenda kubonyeza kengele ya nyumba ile mara moja. Geti lilifunguliwa na yule yule mwanamke wa awali ambaye alimuambia, " anhaaa dada umerudi tena karibu".
"habari yako dada, nimekuja kukupatia taarifa ya kwamba maji ndani ya nyumba hii yamelipiwa bili ya miaka miwili hivyo akija mfanyakazi yoyotewa kampuni yetu usikubali asome mita na akuandikie bili. Utatumia hii risiti kumuonesha" Debora aliongea kwa msisitizo, sauti ya Debora ndiyo ilizidi kumchanganya huyu mama kwani ilikuwa tofauti na awali.
"Wewe si Debora na umekuja hapa muda si mrefu kusoma mita na umeniachia bili hii hapa hata ndani sijaingia nayo tangu uniachie" Yule mwanamke aliongea akamkabidhi ile bili Debora ambaye aliipitia kwa macho na akajikuta akishangaa.
"samahani dada unaona mimi ndiyo nafika sasa hivi na wenzangu wengine wapo ndani ya gari, huyo aliyekupa hii bili sio mimi na huu mwandiko siyo wangu bili hii ni ya kampuni yetu" Debora aliongea maneno ambayo yalizidi kumshangaza yule mwanamke, alipoona mwanamke yule hakuridhika na maelezo yake aliwaita wenzake waliokuwa wamo ndani ya gari wakaja kuthibitisha hilo.
"Dada inabidi uwe makini sana maana matapeli ni wengi sana hapa jijini hasa kwa watu wageni kama nyinyi, hii nyumba ishalipiwa kila kitu na hilo suala wenyewe walisahau kuwaambia ndiyo maana nikaja kukuambia" Debors alimwambia yule mwanamke kisha akamuaga akaondoka.
MUDA MFUPI ULIOPITA
Baada ya Debora wa kwanza kutoka ndani ya nyumba ambayo ilikuwa inatumiwa kana kituo cha vijana wa Brian alipanda pikipiki iliyomchukua mpaka maeneo ya jirani na Tegeta na aliposhuka alimlipa dereva wa pikipiki. Alitembea hadi ilipoegeshwa gari aina ya Suzuki escudo ya rangi nyekundu yenye vioo vya giza akafungua mlango akaingia upande wa kiti kilichokuwa kipo pembeni ya dereva, kwenye usukani wa gari hiyo alikuwa yupo Norbert Kaila ambaye alikuwa amekilaza kiti cha dereva. Debora huyo wa kwanza alitoa wigi akilovaa kichwani kisha akachukua mafuta akajipaka usoni halafu akashika kidevu chake akakivuta kwa juu na kupelekea ngozi ya usoni utoke taratibu na mwishowe akalitoa plastiki lenye sura ya Debora na akabakibna sura yake halisi.
Hakuwa mwingine bali ni Hilda ndiyo aliyekuwa amevaa sura ya bandia iliyomfanya afanane na Debora, aliweka vitu vyote kwenye kiti cha nyuma kisha akamrukia Norbert akambusu mdomoni kwa muda mrefu halafu akamlalia kifuani.
"kwanza nipe ripoti ya huko utokapo" Norbert alimuambia Hilda huku akichezea nywele zake.
"Wameshashtuka mchezo kuwa wanafuatiliwa na wamehama tayari na nyumba ile kuna watu wanaishi" Hilda alimwambia Norbert.
"sasa mwali hapo tuna haja ya kutumia plan B uliyoitaja hapo awali ikiwa plan A imefeli na ikishindikana nayo tutatumia plan B plus yenye kuleta matokeo haraka au unaonaje?" Norbert aliongea huku akinyanyua kiti cha dereva pamoja na kumuinua Hilda kifuani mwake.
"Plan B nadhani itafanya kazi zaidi.na hatutahitaji hiyo plan B plus kwa jambo dogo kama hili. Kazi ya huku imeisha tusanzuke fasta" Hilda aliongea na Norbert aliwasha gari akaliingiza barabarani akaelekea barabara iendayo katikati ya jiji.
****
Majira ya saa kumi alasiri tayari taarifa ya kuonekana kwa mwanamke aliyejitambulisha kama mfanyakazi wa dawasco ilifika katika mikono ya Brian ambaye alikuwa yupo na vijana wake pamoja kibaraka wake Tasu boy au Kennedy kwa jina halisi. Wote kwa pamoja walikuwa wamejichimbia kwenye maskani yao mpya iliyopo Kibada baada ya awali kuingia dosari kwa kuvamiwa na Norbert ambaye hakujulikana hadi muda huo yupo wapi baada ya kuwatoroka kule kwenye msitu wa Sao hill Iringa.
"vijana nadhani mmeelewa maana yangu nilipowaambia ile nyumba tuikodishe maana nilijua kama yule Kaila yupo hapa jijini basi atatuma watu waje kupeleleza pale kama alivyotumwa huyo mwanamke mliyemsikia kupitia kwa Kimaro niliyempangisha ile nyumba. Hivyo basi napenda mtambue kwamba Norbert Kaila si mwandishi wa habari pekee bali ana mafunzo ya ujasusi maana mtu wa kawaida ni vigumu sana kutoroka kule na kufanya maafa kama aliyofanya yeye" Brian aliongea.
"Don hapo nimekupata vilivyo uliposema vile hakika ulipatia vilevile, sasa cha msingi tufanye kazi yetu wewe utapata majibu tu" Obren alipendekeza.
"siyo mfanye peke yenu tu mimi nitahusika vile vile maana kwa alichokifanya Kaila kinanipa tahadhari ya kwamba ni yeye pia aliyesababisha mauaji ya Campbel na Christian sasa nguvu inahitajika kwani huyu si mtu wa kawaida. Also Tasu ni muda muafaka huu wa kuplay your part katika mission hii" Brian aliongea
"Don napendekeza huyu mpwa wangu tumtie nguvuni siku atakayomaliza mtihani tu kwa muda huu mchache wacha nifanye mazoea ya kutoka out naye ili hata siku nitakayomtia nguvuni iwe kwa gia hii hii ya kwenda naye matembezi" Tasu alieleza mbinu yake.
"mbinu nzuri sana hiyo Tasu na hapo ndipo tutakapokamilisha kazj yetu na kuiachia Tanzania maafa makubwa kisha bara la Ulaya na Amerika yanafuata" Calvin aliongea.
"Nadhani kila kitu kipo ndani ya mpango na wajibu wangu as a teacher nao utatusaidia kwa sana katika kumsogeza karibu na ikiwezekana hata mimi naweza kutumika kama chambo ya kumnasa" Jameson naye alichangua.
"Okay sasa ni hivi Tasu na Jameson ndiyo chambo mnaostahiki kumnasa huyu kijana ili atuoneshe ilipo maabara ya siri ya marehemu baba yake, yoyote kati yenu atakayepata nafasi ya kumnasa kuanzia siku atakayomaliza mtihani afanye hivyo. Hili ni hitimisho hakuna la zaidi. Tumeelewana?!" Brian aliongea kwa msisitizo.
"Don!" Wote waliitikia kutii amri hiyo iliyotoka kwa Brian kama mkuu wao; walitawanyika papo hapo baada ya hitimisho hilo la Brian kuendelea na kazi nyingine.
****
Wakati Brian na vijana wake wakiweka hitimisho la kazi yao Moses na Hilary walikuwa wapo chumbani kwa Moses wakipanga mikakati mipya kabisa ya kazi ambayo Moses alitakiwa kuifanya ili kuirudisha furaha ya mpenzi, kumtafuta Victoria ndiyo ilikuwa kazi kuu ambayo Moses alijitosa kuifanya na hakujali uhatari bali alijali furaha ya mpenzi wake ya kuonekana kwa dada yake. Vitendea kazi muhimu vya kazi yao tayari vilikuwa vipo ndani ya chumba hicho na kilichobaki ilikuwa ni utekelezaji wa jambo lililoazimiwa na Moses, silaha ya kisasa iliyotengeneza nchini Marekani bastola iitwayo smith & wasson model 500 pamoja na vitu vingine muhimu vya kufanyia kazi.
"Mose kila kitu kipo tayari ila bado nina wasiwasi na hii mission" Hilary alimuambia Moses.
"Worry out buddy wewe utakuwa ukikaa home ukiwasiliana na mimi na kuniongoza kwenye tatizo lolote,hiki kinasa sauti nitakachokiweka ndani ya sikio ndiyo kitakachokujulisha nilipo kupitia GPS iliyomo ndani yake..Hata nikipatwa na tatizo utajua" Moses alimtoa hofu Hilary.
"ok buddy nipo pamoja nitatumia utundu wangu wa computer katika kukusaidia" Hilary aliongea huku akimpa mkono Moses.
"sasa wewe nenda na vitu kwa ajili ya kazi hapo nyumbani kwenu, mimi nitajifanya nimelala mapema mlango nafunga halafu napitia basement iliyopo humu chumbani kwangu ambayo mtu yoyote haijui nikaanze kazi yangu" Moses aliongea huku akiichomeka bastola kiunoni, Hilary naye akakusanya kila alichohitajika kuondoka nacho akamuaga Moses akasema, "gari ya kazi ipo pale kwenye nguzo mtaa wa Warioba ni range rover ya zamani kidogo ina rangi nyeusi. Funguo hizi hapa".
"Poa" Moses aliitikia huku akizipokea funguo za gari, Hilary aliondoka akimuacha Moses akimaliza kujiandaa.
Moses alivaa nguo nyeusi ambazo zilimkaa vyema na alivaa kofia kubwa iliyomfunika sehemu kubwa ya uso wake kisha akafungua kabati la nguo akatawanya nguo, mlango mwingine ulionekana ambao pia aliufungua akaingia kisha akafunga mlango wa kabati kama ulivyokuwa awali na kurudishia nguo kama zilivyo. Aliufunga mlango wa pili pia baada ya kuingia ndani kabisa. Alishuka kwenye ngazi zilizopo humo ndani ya kabati hadi chini kabisa ambapo taa zilikuwa zinawaka zilimsaidia kuongoza njia aliyokuwa anaelekea.
*Moses ajitosa
*Ndiyo kwanza mwanzo
TUKUTANE TENA KESHO PANAPO UHAI NA AFYA NJEMA
MWENYE KUIHITAJI RIWAYA HII HADI MWISHO ANAWEZA KUWASILIANA NA MTUNZI
KUPITIA NAMBA ZAKE HAPO JUU KWA NJIA YA UJUMBE MFUPI TU WA MANENO NA SI
KUPIGA. HUKO UTAIPATA YOTE.
KWA RIWAYA ZAIDI LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK AMBAO NI:
No comments:
Post a Comment