Monday, January 2, 2017

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI





RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________


SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI!
Kamishna Wilfred alikuwa hajatambua kitu hicho kilikuwa nini na alipeleka mkono kukigusa lakini kitu hicho kilimkandamiza haswa, alijikuta akiongeza mwendo na kisha kufunga breki kwa ghafla baada ya kutambua kuwa alikuwa amewekewa bastola kisogoni mwake.  Gari yake ilisimama kwwa nguvu sana lakini yule aliyekuwa amemshikilia hiyo bastola hakutetereka hata kidogo, bastola hiyo iliendelea kutulia palepale kisogoni mwake vilevile.
              "Nimefunga mkanda kamishna unafikiri nitaaanguka kwa hiyo breki na bastola inidondoke" Alisikia sauti isiyokuwa ngeni ikimuambia



_________
___________
_____________TIRIRIKA NAYO
___________
_________

   Kauli hiyo ilimfanya Kamishna Wilfred ashindwe hata kuendelea kuendesha gari baada ya kulisimamisha kwa ghafla akitegemea mtu aliyekuwa amekaa kiti cha nyuma angeyumba na bastola aliyokuwa amemuwekea imponyoke lakini haikuwa hivyo, kufunga mkanda kwa huyo mtu aliyemuwekea bastola kulimzuia kuyumba huko kwani mkanda ulishika barabara baada ya kupata mshtuko kwa jinsi gari ilivyosimamishwa kwa kasi kubwa na Kamishna Wilfred. Moyoni alilaani kabisa hiyo teknolojia ya magari kwa kuweka mtindo wa mikanda kunasa ikipata mshtuko kumzuia mtu asiyumbe au kujigonga, teknolojia hii yenye manufaa na kuweza hata umuepusha mtumiaji wa gari asiumie sana yeye aliiona haifai hata kidogo kwani imemfanya azidi kuwa katika kuti kavu badala ya kumuweka kwenye kuti bichi ajinusuru mbele ya adui yake aliyekuwa yumo ndani ya gari yake amedhibiti vilivyo. Alitulia tu kimya hakuwa na la kufanya kwani mbinu zote zilikuwa zimemuisha kabisa kwa muda huo, hakujua alikuwa ameweka kitimoto na mtu gani ambaye alikuwa yupo ndani ya gari tangu anaingia ndani ya nyumba ya Wilson   hadi anatoka kwani hakuwa amesimamisha gari mahala mpaka aseme adui huo alikuwa amepanda gari njiani.
                     "yaani tunajivunia tuna kamishna wa umri wa wastani katika nchi yetu ambaye anaonekana mzalendo kumbe mnafiki tu" Mtu huyo aliyekuwa amemuwekea bastola alimuambia, Kamishna Wilfred aliposikia sauti hiyo ambayo siyo ngeni katika masikio yake alitamani kugeuka lakini bastola aliyokuwa ameelekezewa ilimkandamiza shingoni akabaki akiwa mpole asifanye chochote
                      "Tulia hivyohivyo kamishna utanijua tu muda ukifika na hapo utaeleza kwanini unashirikiana na wasaliti wa taifa hili, kwa sasa endesha gari uelekeo wa bank club kurasini upesi sana" Mtu huyo aliongea huku akiutoa usalama wa bunduki, Kamishna Wilfred hakuwa na ubishi alitii kama alivyoelekezwa na akaendesha gari akielekea huko alipoelekezwa na mtu huyo aliyekuwa ameshikilia hatima yake kwa muda huo na nageweza kumfanyia chochote kibaya kwake.
                   "Tena endesha kwa kasi tuwahi kufika kamishana mapema si unajua jioni hii kuna foleni" Alimuamuru, Kamishna Wilfred aliendesha kama alivyokuwa ameagizwa na mtu huyo ambaye alikuwa hajamjua ni nani hadi muda huo ili kuepuka kuyapoteza maisha yake wakati bado ana malengo mengi sana ndani ya dunia hii akiwa bado hajayatimiza.

    Ilibidi awe mpole tu kwani alikuwa akifanya usaliti kwa lengo la kupata pesa na pia kwa maslahi yake mengine binafsi, sasa angeleta ukaidi wowote malengo hayo yasingetimia kamwe na ungekuwa ni mwanzo wa kuwa na hasara kwa kushiriki mpango ambao haukumpa manufaa hadi anaaga dunia. Hilo jambo hakulitaka litokee hata kidogo kwake, tayari yupo ndani ya kuti kavu na moyoni alibaki tu akijilaani kwa kutolikagua gari lake tangu anatoka nyumbani na hadi aliposimama njiani kununua vocha dukani. Aliamini kabisa kuwa adui yake alikuwa akimfuatilia na ndiyo alipanda gari lake muda huo pasipo yeye kujua. Alijiona amefanya uzembe wa hali ya juu wa kubamiza tu milango pasipo kuiweka vibanio vyake alipokimbia mara moja kwenye duka lilopo pembezoni mwa barabara alipokuwa akihitaji vocha baada ya kuishiwa kifurushi chake cha mtandao katika muda ambao hakutarajia kama kingemuishia.
             "Kamishna leo ndiyo utajua kama wanausalama tuna ukorofi sana" Mtu huyo alimuambia wakiwa wanazidi kumaliza mitaa kueleka kurasini.
              "we ni nani kwani Norbert siyo?!" Kamishan alijipa ujasiri akauliza kibabe  ingawa moyoni anajua ubabe wake huo usingemsaidia chochote katika hali hiyo
               "Shida yako kunijua tu utanijua tukifika Kamishna, nimekuwa nikifuatilia nyendo zako kwa ukaribu sana"  Mtu huyo aliongea, Kamishna alisonya  huku akipiga usukani wa gari lake akizidi kujilaumu sana.
                "shida yako nini wewe  niambie unataka kiasi gani usiendelee kunisumbua" Kamishna alijikuta akiropoka tu.
                "Ha! Ha! Ha! Unadhani mimi ni askari mla rushwa kama wewe, mimi ni askari safi wa jeshi la polisi ninachohitaji ni wewe tu kufika mahali unapostahiki kwa usaliti wako" Mtu huyo aliongea maneno ambayo yalimfanya Kamishna Wilfred azidi kufikiria juu yake zaidi  hasa alipotaja yupo ndani ya jeshi la polisi, alimfikiria zaidi mtu huyo na alizidi kufikiri zaidi  na hatimaye akawa amemshuku jina mmoja wa maafisa aliyepo chini yake kuwa ndiyo huyo aliyekuwa nyuma yake.
                 "We John unataka nini haswa kwa mkuu wako wa kazi" Kamishan aliuliza akibahatisha kulitaja jina la huyo aliyekuwa amedhibiti humo ndani ya gari.
                   "Ha! Ha! Ha! Ha! Vizuri kwa kulijua jina langu bila kukutambulisha, ndiyo mimi DCP John Faustin nipo nyuma yake kwa sasa" DCP John aliongea huku akicheka bastola ikiwa imemueleka mkuu wake wa kazi, huyu ni mmoja wa wapelelezi wa shirika la EASA ambalo ndiyo Norbert yupo lakini yeye alikuwa ni normal service kama alivyo Moses na si secret service kama kina Norbert, Hilda na Allison.

     Ndani ya kazi hii ya kuwaumbua wasaliti kwa mara nyingine tena akiwa yupo upande wa wazalendo kama kawaida yake, DCP John alikuwa ameingia ndani ya kazi hiyo baada ya kuhisi jeshi hilo la polisi lilikuwa na msaliti ndani yake. Alianza uchunguzi wake  kwa askari wote waliopo chini yake na hata waliopo juu yake baada ya kuhisi uwepo wa msaliti tangu kilipomalizika kikao cha dharura na mheshimiwa rais yalipotokea mauaji Yombo, hakujua msaliti kwamba alikuwa ni miongoni mwa wakubwa zake ambao alikuwa akiwaheshimu kutokana na vyeo vyao. Alipopata habari za kutumwa kwa special forces wa jeshi la polisi kwenda nyumbani kwa Moses na M.J Belinda kwenda kuwangamiza alipatwa na wasiwasi kikosi hicho kilikuwa kimetumwa na kamishana yeyote ndani ya jeshi la polisi miongoni mwa makamishna waliopo ndani ya jiji la Dar es salaam.

    Hapo alianza kuwafuatilia makamishna mmoja baada ya mwingine. Kamishna wa tatu katika kumpeleleza alikuwa ndiyo huyo Kamishna Wifred na sasa alikuwa amemnasa akiwa ndiyo msaliti haswa aliyekuwa akimtafuta ndani ya makamishna wa jeshi la polisi, alikuwa ni kibaraka wa EASA asiyefahamika kabisa kama yumo ndani ya jeshi la polisi kwa  askari yoyote zaidi ya kufahamika na wenzake wa EASA. DCP John ni mpelelezi ambaye ameshirikiana na Norbert ndani ya jeshi la polisi kwa kazi tofauti ikiwemo ndani ya kisa cha JINAMIZI wakati akiwa na cheo cha ASP (assistant superintendent police/mrakibu msaidizi wa polisi), ndani ya kisa hicho yeye ndiye alimtorosha Norbert maeneo ya Segera Tanga baada ya kuangusha kitambulisho chake akageuziwa kesi na Briton wa usalama wa taifa kipindi cha utawala wa mzee Ole. Pia ameshirikiana naye katika kisa cha SHUJAA ambapo ni yeye aliyemsaidia Norbert kuwarudisha Moses, Beatrice, Dokta Hilary pamoja na Irene kipindi wakiwa kidato ch asia baada ya kuvamiwa na wahalifu na komredi pamoja na wale wa Annie.
    Amerudi tena ndani ya kazi yake akiwa ameshughulika na msaliti ndani ya jeshi la polisi pasipo kumuambia yeyote hadi amempata, yupo njiani akiwa naye anampeleka kurasini ambapo ndipo mahala alipoona panafaa kumpeleka msaliti kama huyo. Ndani ya muda huo tayari ilikuwa imepita nusu saa na sasa wapo katika barabara ya Kilwa maeneo ya Mivinjeni, bastola bado ilikuwa imeelekea shingoni mwa Kamishna Wilfred ambaye alikuwa ametii amri ya DCP John ya kwenda wanapolekea. Aliendesha gari hadi Mtoni kwa Azizi Ally ambapo aliamriwa akate kona kuingia njia inayoeleka Kurasini aachane na barabara ya Kilwa, walienda na barabra hiyo hadi Kurasini mta wa Bank club kwenye nyumba kubwa iliyokuwa na uzio mrefu sana. Hapo aliamriwa apige honi ambapo kijana mwenye mwili mkubwa mazoezi alitoka nje hadi ilipo gari, kijana huyo alisogea kwenye dirisha la dereva akijua mhusika wa hapo ndiyo yupo mbele.

    Kioo cha nyum ya dereva kilifunguka ndipo kijaa huyo akasogea nyuma akamuona DCP John ambaye alimpa amri ya kufungua geti gari hiyo iingie ndani, kijana huyo alikimbia na kufungua geti kwa haraka gari hiyo ikaingia ndani hadi kwenye eneo maalum ambalo Kamishan Wilfred aliamriwa aegeshe gari. Aliegesha gari bila kupinga wala kuleta usumbufu wowote kwa hao waliokuwa wameushikilia uhai wake kwa muda huo, aliamriwa azime gari naye alitii vilevile hakuleta ubishi wa aina yoyote kwa  wapinzani wake ambao hakuwajua kama upinzani wao ulikuwa ukimlenga yeye pia. Aliamriwa ashuke naye alitii akashuka ndani ya gari hiyo akakutana na yule kijana aliyekuwa amefungua get akiwa tayari ameshalifunga  aada ya gari kuingia na ameshika bastola naye baada ya kumuona DCP John akiwa ameshika bastola , bastola ya yule kijana nayo ilichukua uelekeo wa mahali alipo Kamishna Wilfred. DCP John alishuka ndani ya gari naye akamuelezea bastola Kamishna Wilfred kama alivyokuwa amefanya huyo kijana.
             "Kamishna karibu sana ndani ya nyumba ya EASA na utegemee mawili kuingia ndani ya nyumba hii ukiwa na makosa au siyo mhusika wa humu, la kwanza ni kupona ila makazi yako yatakuwa ni gerezani milele ukitoka humu na la pili ni kufa tu ukiwa umeleta  ubishi usiofaa" DCP John aliongea huku akimuashiria kwa bastola yake mahali ulipo mlango wa kuingilia katika nyumba hiyo ya siri ya kampuni ya EASA, Kamishna Wilfred ujasiri wote ulimuisha alipooona kuwa alikuwa akitazamana na mdomo wa bastola  ya DCP John kwa mara nyingine ambaye alikuwa akitabasamu tu ingawa hakuwa na faraj wala furaha iliyomfanya atabsamu kwa muda huo.
               "Kamishnaaa! Afrika ya mashariki haichezewi na wasaliti kama nyinyi ikiwa wanausalama wake wapo kazini" DCP John alimuambia huku akiwa nyuma yake akimuangoza Kamishna Wilfrd kulekea ndani ya nyumba hiyo, yule kijana alifanya ya kufungua mlango katika kila eneo walilokuwa wakipita hadi walipoingia katika vyumba vya chini ya ardhi.

     Kamishna Wilfred alipoyaona mazingira ya eneo hilo alikuwa ameshakata tamaa ya kuishi kwani aliona uwezekano wa kutoroka humo ndani ulikuwa ni mgumu sana, moyoni alijiwa na roho iliyokuwa ikimlaumu sana tamaa yake ya pesa ndiyo ilikuwa imemponza sana hadi akaingia katika eneo hilo lenye ugumu wa kutoka kwa mtu kama yeye. Upande mwingine wa nafsi yake  ulikuwa ukimpa moyo ni sehemu ya maisha kuwa na matatizo kama hayo apige moyo konde tu anaweza kusalimika, alijipa moyo wa kusalimika akiamini kuwa aliyemsaidia akawa hajashikwa siku zote alizokuwa akifanya uhalifu atamsaidia na hapo aweze kutoka. Kamishna huyu aliyekuwa amepewa cheo kikubwa na kuaminiwa sana katika jeshi la polisi alikuwa ameshasahau kabisa kwamba anayemtegea ataweza kumnusuru eneo hilo alikuwa amemkosea kwa kiasi kikubwa sana,habari ya kuwapa viongozi wa dini pesa ili wamuasi huyo anayemtegea  kwake hakuwa nazo ila yeye alikuwa akitegemea tu kukolewa na huyo anayemuamini atakuwa ni mwokozi wake ndani ya balaa hilo zito ambalo lipo mbele yake kwa usiku huo. Usiku ambao ni usiku mmoja kati ya usiku miwili iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu iishe ili waweze kuyachukua madaraka makuu ya nchi ya Tanzania.

    Moyoni kabisa alikuwa akimtegemea Mungu  wakati walikuwa walikuwa wana mpango wakuhalalisha kile ambacho muumba alikuwa amekikataza kisihalalishwe, yote hayo aliyasahau na alikuwa akimuomba Mugnu atoke hapo salama ili asiwe amefanya kazi bure tu kuisaliti kazi yake aliyokula kiapo akitumia kitabu kitakatifu cha dini yake. Dhambi kubwa yote aliyofanya ikiwemo kuvunja kiapo kizito alichokula kipindi anajiunga na jeshi la polisi sasa ilikuwa imeanza kumtafuna yeye mwenyewe kuanzia siku hiyo,dhambi ya pili ya kutaka kuhalalisha kile alichokuwa amekipinga Mungu sasa ilikuwa ikimtafuna pia ingawa alikuwa akimuomba Mwenyezi kwa dhati ndani ya moyo wake aweze kutoka ndani ya eneo hilo.

   Ama kweli alimuona Muumba ni asiyeona huo uongo wake aliokuwa akiidanganya ndani ya nafsi yake, alikuwa akimuomba akombolewe muda huo wakati alikuwa azimia kwenda kufanya jambo baya  akitoka hapo la kwenda kushiriki kuhakikisha ule mpango wake ulikuwa unatimia vilivyo. Kamishna Wilfed usiku huo ndiyo anajikuta akijuta tangu aanze kushiriki mpango huo kwa kulipa kisasi cha ndugu yake ambaye anaamini kabisa alikuwa ameuliwa na  EASA  hata kabla hajaambiwa na Mzee Ole juu ya muuaji halisi wa ndugu yake masaa machache yaliyopita, siku zote hizo alikuwa akishiriki katika kukomoa shirika hilo pamoja na wote waliohusika katika kumuondosha Mzee Ole madarakani na kupelekea kuuawa kwa ndugu yake Reginald Kitoza aliyekuwa mtu wa karibu sana kwa Mzee Ole kama ilivyo Moses kwa Rais Zuber.
     Akiwa ametangulizwa mbele ya DCP John na nyuma ya yule kijana wa aliyewafungulia geti kwa mita takribani tatu, Rias Ole aliongozwa hadi ulipo mlango mzito wa chuma ndani ya vyumba vya chini ya ardhi ndani ya nyumba hiyo. Kijana yule alifungua mlango ule wa chuma ambao ulimhitaji kubonyeza namba maalum ukutani, ulipofunguka chumba hicho kiliwaka taa na kijana yule akaingia ndani kisha Kmaishna Wilfred akafuatia. Kamishna Wilfred alipoingia ndani ya chumba hiko aliamini kabisa uwezo wa kutoka humo ndani ulikuwa mdogo hasa baada ya kumshuhudia mtu aliyekuwa akiaminika ni mtu hatari akiwa yupo amefungwa minyororo mikononi na miguuni, mtu yule aliyekuwa akiamnika kuwa ni komando hivi sana aliamuona akiwa amepungukiwa mwili wake ule wa kimazoezi na akiwa na vidonda kadha mwilini mwake.

    Moyo wake uliingiwa na ganzi pia alimuona kijana wa special force aliyekuwa ni mmojawapo kati ya vijana aliokuwa amewatuma kumkomboa Lion kule ofisini kwa Norbert baada ya mzee yule kutotoka tangu alipoingia ndani ya ofisi ile ambayo baadaye Norbert aliacha kuitumia, alimshuhudia kijana huyo akimtazama sana kwa huruma alipofika katikati ya chumba hicho akiwa amewekewa bastola kisogoni kwake. Kamishna Wilfred alishindwa kabisa kumtazama askari wake yule waspeciala forced kutokana na matatizo aliyokuwa amemsababishia kwa kumpa amri zisizo na baraka  la jeshi la polisi lote, pia alishindwa kumtazama yule Komandoo wa kizungu aliyetiwa mikononi na Moses nyumbani kwa M.J Belinda walipotumwa kwenda kumuua mwenye nyumba ambaye ni kikwazo kwao. Kamishna Wilfred alienda kufungwa moja kwa moja kwenye kiti cha mateso ambacho kilikuwa humo  ndani ambapo kila mateka mpya anayeingia humo  lazima apitie hapo kwenye kti hicho ndiyo aende kufungwa minyororo kama wengine aliowakuta humo ndani. Baada ya kufungiwa barabraa kwenye kiti hicho cha mateso ndiyo DCP John alirudisha bastola yake kwenye pochi maalum aliyokuwa ameiweka kwapani kisha akasogea hadi karibu kabisa na kiti alichofungiwa Kamishna Wilfred, alimtazama mkuu wake wa kazi huyo kwa sekunde kadhaa huku akitabasamu halafu akasikitika sana kwa ujinga aliokuwa  akiufanya.
                  "Kamishna unafikiri nchi hii ulinzi wake ni mdogo sana hadi muweze kufanya mlitakalo, mtizame huyo mzungu aliyekuwa ni mpiganaji mzuri mkamtuma kwenda kumuua Meja jenrali Belinda alivyo, ohooo! Kiti hicho ullichokalia wewe ndiyo kimemfanya akawa vile tena kwa taarifa yako ametapika siri zenu zote.  Alikuwa mbishi sana akabanikwa korodani zake hadi akaongea ukweli na sasa hivi huo ubishi wake ushampa utasa kabisa hataweza kuzalisha hata kama akitoka humu mzima, sasa Kamishna jindae na wewe mtesaji anakuja ikifika zamu yako" DCP John alionga huku akimtazama Kmaishna Wilfred, aliacha kumtazama bada ya kumalizakuongea maneno hayo kisha akayahamisha macho kwa yule kijana wa special force.
                  "Mtazame huyo kijana wa special force katika jeshi la polisi ambaye kaumia kawa kibogoyo yote kwa ajili tu ya kufuata amri zako wewe msaliti akiwa hana uwezo wa kupinga maana wewe ni mkubwa wake, sasa hivi yupo humu akiwa ameshakata tamaa kabisa ya kuendelea kuishi Kamishna yote kwa ajili yako tu wewe ukitumia madaraka hayo uliyopewa vibaya. Kaheshimu amri zako ndiyo maana akazitii lakini leo ndiyo zimemuweka humu" DCP John aliongea huku akimtazama yule askari wa special force ambapo maneno hayo yalimfanya atokwe na mchozi baada ya kuona ameharibikiwa na maisha tu kwa ajili ya Kamishna Wilfred.
                   "Mkuu nilikuheshimu na kufuata amri zako lakini sasa nimeharibikiwa na maisha yangu tu yote kwa ajili yako wewe tu, onaaa! Nimemuacha mke wangu mjamzito nyumbani hadi leo hajui kama nimekufa au la.

     Unafikiri ataishi kwenye hali gani Kamishna ikiwa wewe umeharibu maisha yangu. Kamishna mama yangu ni mgonjwa nimemtoa shamba nimemleta mjini ili aweze kupatiwa matibabu nikitegemea kazi hii ndiyo itakayomtibu fikiria atakuwa yupo kwenye hali gani mimi nikiwa hapa, wenzangu pia wameuawa nyumbani kwa Meja jenerali yote kufuata amri zako tu fikiria wewe unayekaaa na mkeo pamoja na familia yako kwa raha ukila chakula kitamu ambacho hata tulipokuwa kazini hatukumdu kukipata. Aaaaaaargh! Kamishna umeangamiza maisha yangu ingawa bado napumua" Askari yule wa special force alilalamika huku akilia kwa uchungu akimtazam Kamishna Wilfrwd pale kwenye alipokuwa amefungwa, maneno hayo yalikuwa yamemuingia vilivyo Kamishna Wilfred akajikuta akiinamisha uso wake chini kutokana na uzito wa maneno hayo ambayo yalikuwa yamatolewa na mtu mwenye uchungu sana.
                "Angalia sasa unaona hata aibu kumtazama sajenti Ismu kwa uovu  wako, eti unataka kumlipia kisasi Kitoza huyu msaliti aliyeshiriki mauaji ya makomandoo wa jeshi siyo. Yaani ulivyo na moyo mwepesi hadi unaona aibu kumtazama Ismu hukufaa kufanya hayo kabisa, subiri na wewe familia yako isote baada kuonja joto ya jiwe iliyowapata hawa wenzako waliofungwa hapa" DCP John aliongea huku akimtazama Kamishna Wilfred kwa masikitiko sana, Kamishna Wilfred kwa siku hiyo alijikuta akikumbuka maneno ya mkewe ambayo ambayo alimuambia siku chache baada ya kupokea habari za kifo cha Reginald Kitoza binamu yake aiyekuwa akimpenda kama ndugu yake wa damu.
                 "mume wangu naomba umuachie Mungu tu visasi  havikufai na cheo chako hiko"
                 "hapana sikubali lazima aliyemuua alipie kwa gharama yoyote ile"
                 "kumbuka alikuwa ana hatia yule na kauawa akiwa hatiani"
                 "we mwanamke ishia hapohapo nishasema nitalipa kisasi cha ndugu yangu wazazi wetu ni damu moja hivyo namuona kama ndugu yangu wa damu yule"
                 "ohooo! Sawa siishi nyumba moja na wasaliti , naenda kwetu
      (siku  mke wa Kamishna Wilfred alipoongea maneno hayo alikuwa ni ana cheo cha SP {super intendent police}, ilikuwa ni majira ya usiku ambapo mke wake aliaga kururdi kwao akipakia nguo zake kwenye begi. Kutokana na mapenzi mazito aliyonayo kwa mke wake na kuhofia kuvuja kwa adhma yake alijikuta akilegeza msimamo kimaigizo ndipo mke wake akabaki na aliamua kufanya adhma hiyo kisiri na sasa usaliti wa kusema uongo kwa mke wake pia unamtafuna leo hii).

*JOHN FAUSTIN AKIWA CHEO CHA KAMISHNA MSAIDIZI KWA MARA NYINGINE TENA DANI YA WAKALA WA GIZA, WASOMAJI WAJINAMIZI INAYOENDELEA KWENYE GROUP LA KULIPIA NA INBOX KWA MALIPO NAFIKIRI MTAITAMBUA KAZI ALIYOIFANYA HUYU KUMUOKOA NORBERT

"KAMISHNA WILFRED KAPATIKANA, USALITI UNAMTAFUNA TARATIBU

USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI NA TATU KUJUA  KILICHOWAPATA WATU HAWA










No comments:

Post a Comment