KIONJO KWA WALE WAPENZI WA RIWAYA ZA KICHAWI
DAR MPAKA SONGEA
“Shenzi kabisa nyinyi si wabishi sasa tune kama mtafika” Bibi yake Nyoni alisema huku akiweka macho yake kwenye maji yaliyopo ndani ya chungu.
Kutikisika kwa maji kulipotulia tu, alipuliza kwa mdomo wake ndani ya chungu hiko na mambo yakaanza tena namna hiyo. Tena alitoa pulizo mara mbili kwa nguvu mno, maji yalicheza haswa huku picha ya chombo kile cha angani ikitikisika.
Alicheka kwa ngnvu, na maji yalipoanza kutuliza alitazama pembeni kwa haraka. Macho yake yalitua kwenye kipande kidogo cha gazeti kilichokunjwa. Alikitwaa kwa haraka kisha akakifungua, ndani yake kulionekana unga wa rangi ya kijani ambao aliumimina ndani ya maji.
Aliukoroga kwa haraka kisha akayatazama jinsi kimiminika kile kilivyokuwa kikizunguka humo ndani. Kukiona namna hiyo alisonya kwa nguvu, cheko lile lilimuondoka kabisa.. Akabaki ni mwenye kununa huku akitazama taswira ile ambayo bado haijandoka pamoja na kutia unga ule. Wingu jeupe alilokuwa akiliona hapo, lilibadilika na kuwa jeusi kupindukia baada ya maji kukolezwa na kitu alichokiweka.
Safari hii Ndege ilionekana ikizunguka kutoka upande mmoja kwenda mwingine, mithili ya upanga wa feni. Kuona hivyo yeye alivuta mdomo kabisa na kuupeleka kulia na kushoto, uso ulimbadilika na kuonekana ni mwenye na hasira.
Baada ya kuzungusha namna hiyo hatimaye alifungua kinywa chake, kufanya hivyo alitokwa na mate mdomoni ambayo aliyatema humo chunguni. Afanalek! Kufanya hivyo, radi moja ya nguvu ilionekana ikipiga pale kiasi cha kuifanya ndege ile ibinuke mara moja na kisha ikakaa sawa.
SHILINGI 4000 YAKO TU NDIYO UNAWEZA KUIPATA BURUDANI NZIMA ILIYOMO HUMO NDANI, HUJACHELEWA BADO. UTAIPATA NA UTAISOMA HUKU FACEBOOK NA KWENYE EMAIL.
ULIPAJI
TUMA MALIPO KWENYE NAMBA ZIFUATAZO;
TIGOPESA O713 776843-HASSAN MAMBOSASA
MPESA 0762 219759-HASSAN O MAMBOPSASA
AIRTEL MONEY 0788 602793- HASSAN MAMBOSASA
MUHIMU: UKILIPA UTUME JINA ULILOLIPIA AU NAMBA ZA MUAMALA KWEND INBOX YA RIWAYA MARIDHAWA LINK http://m.me/riwayamaridhawa IKIWA WEWE NI MTUMIAJI WA FACEBOOK,ILI TUIJUE AKAUNTI YAKO UNAYOPASWA KUTUMIWA RIWAYA.
WALE WA EMAIL HAKIKISHA UNALIPA NA KUTUTUMIA EMAIL YAKO KWA NJIA YA SMS.
NI HAYO TU, JUMAPILI NJEMA KWENU NYOTE
No comments:
Post a Comment