Tuesday, November 15, 2016

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA PILI





 RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA



    SEHEMU YA PILI!!

     Mzee huyu ulipofunguliwa mlango alionesha kutojali ndiyo alijigeuza upande wa ukutani wa godoro alilolalia akionesha ni kiburi sana. Jambo hilo lilimuudhi sana askari aliyefungua mlango hadi akmfuata akampiga rungu la kwenye paja lilomfanya mzee huyo augulie maumivu kisha akamvuta kwa nguvu.

           "Pumbavu wewe unadhani hapa ni ikulu ulipoingia kwa kumwaga damu ya wenzako" Askari alimfokea huku akimsukuma nje mzee huyo ambaye alikuwa ameshika sehemu ya paja liyopigwa runmgu.

            "tena ongoza njia kabla sijakuongeza rungu la pili fisadi wa nchi wewe" Askari alimuambia kwaukali huku akimsukuma atangulie mbele.


****
 
     Mzee huyo  aliongoza njia huku akiwa anatembea kwa kuchechemea kutokana na maumivu aliyoyapata baada ya kupigwa rungu la paja, maumivu yalizidi kuongezeka zaidi baada ya hofu kubwa kuugubika moyo wake  alipofikiria jambo aliloitiwa na askari wa gereza hilo kutokana na kuchukiwa sana. Jambo hilo hakuhitaji litokee ndani ya muda huo kwani hakuna kiumbe anayevuta pumzi atakuwa tayari  kuona jambo hilo likitokea kwake hasa mwenye ndoto zake ambazo zinaishi ndani ya halmashauri ya kichwa chake, upande wa pili alijipa moyo kwani alidhani huenda  kuna ugeni ulikuwa umekuja kumtembelea baada ya kupita mwezi mmoja hakutembelewa na mtu yoyote yule.

      Wasiwasi wa kutokea kwa jambo asilolitaka litokee akiwa ana malengo yake ambayo yanaishi ulizidi ndani ya ubongo wake kiasi cha kuzidi uzito upande wa matumaini yake, kwa wasiwasi aliokuwa nao alijikuta akigeuka nyuma kumtazama yule askari anayemsindikiza na hapo ndipo akaibua jambo jingine kabisa.

      Macho yake yalipotazama uso wa askari yule yalizidisha chuki aliyonayo askari yule kwake na hapo ndipo akaibua jambo jingine likatokea baada ya kurudisha shingo yake kutazama mbele, lilikuwa ni kofi zito la mkono mgumu na wenye sugu  wa askari huyo ambalo lilimfanya hadi ahisi kiwewe kilichomyumbisha na alipokaa sawa alisonga mbele na hakuthubutu kutazama tena nyuma.

            "Ukigeuza shingo yake nakuongeza rungu la kichogoni kenge wee! Unafikiri kuna mtu anayetaka atazamwe humu na macho yako ya kishetani hayo, tena ongeza mwendo tusikupunguzie muda sisi" Yule askari alifoka huku akizidi kumsogelea karibu zaidi kwa mwendo wa kasi na kusababisha mzee huyo atembee kwa haraka zaidi, hakika aliogopa kupigwa kofi la pli na yule askari kutokana na kofi la kwanza kumletea maumivu makubwa.

      Ujasiri wote aliokuwa kipindi yupo uraiani ulikuwa umemuisha kabisa na hapo uoga ndiyo ulitawala moyo wake kwani hakuwa na ujanja, ama kweli yamemfika asiyoyatarajia kama yatamfika katika maisha  yake.

     Aliongozwa na yule askari anayeongozwa naye kwa chuki hadi katika eneo maalum la kuonana na wageni katika gereza hilo na hapo ndipp nafsi yake ikapata ahueni baada ya  kumuona ndugu yake akiwa yupo upande wa pili akimsubiria na simu ya mkonga ilikuwa ipo sikioni mwake. Naye aliweka mkonga wa simu sikioni mwake kisha akasema, "mdogo wangu vipi mradi unaenda sawa?".

           "unaenda sawa kaka sasa hivi umefikia pazuri na ndugu zako uliotuachia tutanufaika nao, hatua ya kwanza ya ukuaji imeanza tunatarajia hatua ya pili itafuatia mpaka zitimie hatua zote tano ndiyo matunda ya mradi tuyaone" Ndugu yake aliongea akiachia tabasamu pana na kusababisha mzee yule naye  aachie tabasamu kisha akaongea neno la lugha ya kimasai lililomfanya ndugu yake atoe hofu naye akamjibu kwa kimasai mzee yule naye akarudisha tabasamu kwa ndugu yake.

          "Sasa hakikisha mradi unafikia malengo mdogo wangu  si unajua familia inanitegemea kwa sasa sina njia ya kutimiza mahitaji yao ila hiyo ndiyo njia pekee" Yule mzee aliongea kisha akaweka mkonga wa simu chini halafu akamtazama ndugu yake kwa tabasamu ambapo naye aliridisha tabasamu lile, alimuonesha ndugu ya  ishara ya kumuaga  akawa amesimama palepale.

     Ndugu yake alianza kuondoka taratibu sana akiwa aanatazamwa na mzee huyo hadi alipopotea katika upeo wa macho ya mzee huyo akiwa hamuoni tena katika eneo alllokuwa amekaa ndugu yake akiposimama hapo awali, mzee huyo alibaki papo hapo akimtazama upande wa pili wa kioo kwenye eneo maalum ambalo wageni wakija kuwatembelea wafungwa husimama akiwa anawaza kitu ndani ya kichwa chake hadi muda waliopewa uliopoisha akawa bado amesimama pale mpaka alipokuja kukumbushwa na askari aliyomleta kwa namna asiyoipendelea kabisa kukumbushwa nayo.

      Kofi la kisogoni na kuvutwa kwa ukosi wa vazi lake la kifungwa ndiyonamna aliyokumbushwa na askari huyo wa gereza na akajikuta akiingia tena kwenye maumivu aliyokuwa akiyakwepa awali alipokuwa akihusiwa kazane na askari yule wakatia kimleta eneo hilo. Alitolea eneo hilo na kupelekwa ndani ya chumba chake cha gerezani humo kwa namna ambayo ilitumiwa wakati analetwa katika chumba cha kuzungumzwa na mgeni.



****



     YOMBO
  DAR ES SALAAM

     Amani ya eneo la Yombo tayari ilisjakuwa imepotea kwa tukio lililofanywa na mzee wa kqnisa ambaye ni mgeni katika mtaa huo, amani ya eneo hilo ilibidi irudi kwa kutumia nguvu ya polisi kwani mapigano yalishazuka baada ya tukio hilo, upande wa dini zote ulikuwa ukiwatetea wenzao na hapo ndipo baadhi ya raia wa eneo wakijikuta wakikatishwa maisha yao kutokana ugomvi huo.

     Hali ilipozidi kuwa tete mabomu ya machozi yalihusika katika kuwatawanya wanadini hao walioingia dosari katika kutetea waumini wenzao katika kila dini, askari wakutuliza ghasia walikuwa wameenea katika eneo hilo wakiwa na kazi ya kutuliza ugomvi huo kwa kutumia kila mbinu ikiwemo kupiga raia wabishi na hata kurusha mabomu ya machozi. Juhudi za askari hao ziligonga mwamba na hapo magari yenye maji yanayowasha yakaingia eneo hilo na kuanza kumwaga maji hayo kwa wananchi ambalo walikuwa wakipigana wenyewe, ahueni ya vurugu hizo zilionekana ingawa kuna baadhi ya raia bado walikuwa wabishi kuacha kupigana hata kwa maji hayo na ikawabidi askari wakutuliza ghasia wabadili mbinu ili kumaliza tatizo hilo.

     Risasi za mpira ndiyo mbinu iliyofuata baada ya mbinu ya awali kushindikana walifyatua risasi hizo kwa raia waliopo mbele yao ambayo iliwafanya raia hao wache ugomvi mara moja baada ya kuona wenzao wakirushwa na bunduki hizo baada ya kuwapata, dhana ya kwamba wenzao walikuwa wamepigwa risasi za moto ndiyo iliowajia raia katika vichwa na kukimbia ili kuokoa masiha yao mkutokana risasi hizo walizodhani za moto ndiyo jambo waliloliona linafaa kuliko kukaa katika eneo hilo.

     Ndani ya dakika tano tayari eneo hilo lilikuwa tulivu baada ya kutumika kwa risasi za mpira katika kutawanya watu na wale walioangushwa na risasi za mpira waliiingia katika mikono ya askari  baada ya kuwahiwa na kutiwa nguvuni, ndani ya dakika nyingine tano tayari magari ya wagonjwa  yalifika eneo hilo na mengine ya kubeba miili yalikuwa tayari yamefika katika eneo. Waandishi wa habari kutoka vituo mbalimbali vya habari nao tayari walikuwa wamefika eneo hilo wakitafuta habari ili waweze kuwafikishia hadhira ya watanzania waliookuwa nje ya eneo hilo.

    Upelelezi wa kiini cha tukio nao ulianza mara moja ili kubaini chanzo chake kupitis kuwahoji wale watu waliokuwa wametiwa nguvuni na maaskari, chanzo kilipobainiwa maaskari hao waliingia kazini katika kumtafuta aliyesababisha tukio zima hilo na hapo ndipo wakabaki na mshtuko baaada ya kubaini jambo jingine lililo zidi kuwashangaza wale maaskari kuhusu mtu kiiini cha tukio hilo.

    Mzee wa kanisa ambaye ndiye kiini  cha tukio hilo hakupatikana yeye wala familia yake na hata alipoulizwa mwenye nyumba ambayo mzee huyo wa kanisa alipangisha mwezi mmoja uliopita tangu ahamie mtaa huo alitoa jibu ambalo lilizidi kuwashngaza sana maaskari hao.

     Mvurugo, mkanganyhiko, machanganyo ndiyo ulikuwa umevamia vichwa vya maaskari waliokuwa na ari ya kufanya kazi tangu alipoingia rais mpya anayewajali ndiyo ulikuwa umevamia vichwa vyao na kuwafanya wabaki wakikuna bongo zao watafute mahali pa kuanzia kwa upande mwingine kutokana na kukosekana kile walichokuwa wakikihitaji kutokana na majibu waliyopewa na mwenye nyumba iliyokuwa anatumia na mzee wa kanisa huyo.

      Maaskari hao waliafikiana waende  kwenye kanisa ambalo lilikuwa likiomgozwa na Mzee Kimaro kama mzee wa kanisa  ili kupata walau kitu kitakachowapa mwanga katika jambo wanalolitafuta, walifanya upesi na wakaenda kanisani hapo lakini napo waliambulia patupu wakabaki wakikuna bongo zao kwa mara nyingine juu ya tukio hilo linalowachanganya vichwa vyao hadi muda huo.

     Akili zao walizifikirisha kinyume na kufikiria kwa kawaida juu ya tukio hilo lakini napo ilikuwa ni kazi bure kwani haikuleta matunda ya kuvuta fikra zao zaidi, walitumia mbinu mbalimbali za kiaskari lakini mwisho wake ikawabidi waliweke hilo suala kiporo walianze baadaye kidogo kwa kutumia mbinu nyingine tofauti naya awali waliyokuwa wanaitumia.



****



     Jioni ilipofika vituo mbalimbali vya habari vilikuwa vinarusha taarifa ya tukio zima lilotokea Yombo na ikawa ndiyo habari kuu kwa baadhi ya vituo vya televisheni nchini, saa mbili  usiku ilipowadia vituo vikubwa vya habari navyo vilirusha juu ya tukio hilo kutokana na kuchukua sura mpya ndani ya nchi yenye amani Tanzania.

     Taarifa hiyo ya habari ilikuwa ikiangaliwa na Moses pamoja na mkewe Beatrice wakiwa  wameegemeana subeleni katika nyumba ya Moses Mikocheni ambapo Beatrice alikuwa amelaza kichwa chake kwenye mapaja ya Moses huku akuelekeza macho kwenye luninga, taarifa hiyo pamoja na umwagaji damu wa eneo uliotokea ulionekana kumsikitisha sana Moses na Beatrice  wakiwa wameelekza macho yao kwenye luninga iliyopo sebuleni hapo.

      Zilipoonekna damu zilizokuwa zimemwagika eneo hilo Beatrice alijikuta akigeuza uso pembeni na hakutaka hata kuangalia hadi pale habari hiyo ilipoisha na ikafuata habri nyingine ndiyo akarudisha macho yake yatazame kioo cha luninga kwa mara nyingine. Moyo mwepesi alionao Beatrice ndiyo ulimfanya Beatrice aangalie pembeni na hakutaka kulitazama tukio hilo hata kidogo, kwa Moses  aliona kawaida kutazama habari hiyo hadi inaisha.

         "Loh! Yaani nchi hii sijui inaelekea wapi kwa kweli" Beatrice aliongea baada ya habari hiyo kuisha.

          "usiseme nchi hii sema raia wa nchii hii because nchi haina kosa mke wangu" Moses alimrekebisha Bratrice kauli yake.

           "mmh haya vyovyote"  Beatrice aliongea huku akijiweka vizuri kwenye mapaja ya Moses, muda huo Moses alitaka kuongea neno lakini  alisitisha baada ya simu yake ya kiganjani iliyopo kwenye kochi kuita.

      Aliitupia macho yake yote mawili simu ile ambayo hakuweza kuifuta bila ya kumnyanyua Beatrice katika mapaja yake alipokuwa amegemeza kichwa chake, kikwazo chake cha kutoweza kuifuata simu hiyo kiligunduliwa mapema na Beatrice ambaye aliisogeza simu kwa mguu wake hadi ilipofika usawa wqa mikono yake kisha akainyanyua ile simu akaitazama kwenye kioo kuona jina la mpigaji na alipoliona  alisema,"Honey askofu Edson huyo anakupigia"

     Moses aliposikia hivyo aliichukua simu kwa haraka kisha akaipokea na kuiweka sikioni akasikiliza upande wa pili wa simu hiyo halfu akasema,"amen Bwana Yesu asifiwe baba.....si mgekuja kesho asubuhi kuufuata tu huo mzigo baba....sawa hamna tabu ngoja niwataarifu vijana waliopo shift ya usiku kazini wawapatie huo mzigo..amen asante baba".

     Simu ilikatwa kisha akabonyeza namba kadhaa kwenye simu yake akaiweka sikioni akaongea,"Benson askofu Edson anakuja hapo kazini mpatie ule mzigo uliotengwa wa chupa za dawa Quntanise kwani zintakiwa zisafirishwe usiku huu kwa boti hadi Zanzibar walipo wawakilishi waliozihitaji ili ziweze kuondoka Italy siku inayofuata". Alipomaliza alikata simu kisha akarudisha macho yake kwenye kioo cha televisheni akagundua ulikuwa ni muda wa  matangazo baada ya habari za kitaifa kuisha, aliipoona hivyo aliinamisha kichwa chake na akambusu mke wake mdomoni kwa ghafla na kusababisha mke wake aachie tabasamu.

         "Honey time ya kula hii" Moses alimuambia Beatrice baada ya kuangalia katika meza ya chakula chakula kilikuwa kikimaliziwa kutengwa na msichana wa kazi, Beatrice aliposikia alijifanya kusononeka akionekana hataki kutoa kichwa chake katika m iguu ya Moses. Alibaki vile vile akiwa anatabasamu usoni huku akimuangalia Moses ambaye alibaki akimtazama tu baada ya kumuambia kuhusu muda wa kula, Moses alipoona kimya aliamua kupenyeza mkono wake mmoja kwenye uvungu wa mapaja ya Beatrice kisha mkono mwingine akashika kwenye shingo.

    Alimyanyua kwa kushtukiza na kusababisha acheke kwa furaha huku mikono akiwa ameizungusha shingoni mwa Moses, alibebwa hivyo hadi mezani kisha wote kwa pamoja wakakutanisha ndimi zao halafu Beatrice akashushwa jirani na kiti kimojawapo kilichopo kwenye meza ya chakula akakaa. Walianza muda wa kuweka matumbo yao sawa kwa pamoja huku wakilishana kama ilivyo kawaida yao kutokana na jinsi walivyo na furaha wakiwa pamoja, Beatrice aliendelea na mtindo wake wa kudeka kila mahali ambapo Moses yupo karibu.
Baada ya chakula wote kwa pamoja walirudi kwenyye luninga kisha baadaye walielekea chumbani kwao.




    
    ASUBUHI ILIYOFUATA

      Simu ya Moses iliita kwa fujo majira ya ssa kumi na mbili asubuhi muda mchache kabla ya kengele ya kumuamsha kulia, simu hiyo ilimfanya usingizi wake ausitishe kisha akaipokea kwa haraka hiyo simu na kuiweka.

            "What(nini)?" Aliongea kwa nguvu baada ya kupokea taarifa kwa njia ya simu ambayo ilimfanya atoke kitandani hapohapo kwa haraka hadi Beatrice naye akaamka kutokana na papara aliyokuwa nayo mumewe.

             "Mume wangu kuna nini mbona mapema hivyo?" Beatrice aliuliza huku akifikicha macho yake kutokana na usingizi alionao, alipokaa kitandani alimuona Moses akiwa anavaa mavazi maalum anayoyatumia kwenda nayo bafuni kuoga.

             "kuna dharura imetokea inabidi niwahi sasa hivi nyumbani kwa Askofu Edson nimepigiwa simu na Kaila yupo huko ananisubiri ili nikafanye uchunguzi wa kina wa tatizo lililotokea" Moses aliongea akionekana anawahi bafuni.

            "Baby mbona sikuelewi kuna nini?" Beatrice aliuliza wakati Moses akiwa ameshaingia kwenye kizingiti cha bafuni,Moses aliposikia swali la mke wake alirudisha kichwa chake  nyuma akawa anachungulia mahali alipo Beatrice akasema,"Bishop Edson is dead(Askofu Edson amefariki)".

           "What?" Beatrice aliuliza kwa mshngao lakini swali lilkosa kujibiwa kwani Moses tayari alikuwa ameshaingia kwenye mlango wa bafuni kwa haraka sana, Beatrice naye taarifa hiyo ikamtoa uchovu wote kwani alijua kuwa kazi aliyoitiwa mume wake akiwa kama mwanasaynsi pia ni hufanya uchunguzi wa vipimo mbalimbali vya miili ya watu waliyokufa kwa utata.

    Aliamka kitandani akatoa nguo za mume wake kwa ajili ya kutumia siku hiyo pamoja na viatu ambavyo tayari vilikuwa vimeng'arishwa na dawa, baada ya dakika tano Moses alitoka akiwa tayari ameshajifuta maji na taulo lililopo bafuni na alijiandaa haraka sana na baada ya kuwa tayari Beatrice alimkabidhi mkoba wake wa muhimu wa kiofisi kisha alimbusu mke wake na akamkumbatia akachukua funguo ya gari.

         "My love utatumia gari nyingine kwenda kazini acha niwahi" Moses alimuambia Beatrice akatoka upesi sana akawa anaelekea mlangoni.

         "Take care(kuwa mwangalifu)" Beatrice alimuambiwa kwa sauti na kusababisha Moses ageuke amtazame akiwa na tabasamu kisha akasema,"I will".

     Alifunga mlango akatoka nje akimuacha Beatrice akiwa amerudi kitandani akakaa kitako, baada dakika takribani mbili  mlio wa gari analolitumia Moses ulisikika kuashiria kuwa ndiyo alikuwa anatoka



****

 
   NUSU SAA BAADAYE,
      MBEZI BEACH

      Gari aina ya Bmw yenye rangi nyekundu ilionekana ikiingia ndani ya nyumba moja yenye geti kubwa baada geti kufunguliwa, gari hiyo ilipitiliza moja kwa moja hadi sehemu ya maegesho ambapo kulikuwa kuna gari tatu za polisi na mbili za kiraia. Moses alionekana akishuka ndani ya gari hiyo aina ya BMW baada tu ya gari hiyo kuegeshwa. Alipokelewa na msaidizi wa hapo ndani ambaye alimpeleka hadi mlangoni ambapo alikuta utepe umezungushwa eneo hilo, alivuka utepe akaingia ndani akakutana na baadhi ya maaskari,Norbert pamoja Dokta Hilary kutoka hospitali ya taifa .

       Ilikuwa ni ndani ya eneo la sebule ambako mwili ulionekana kufunikwa shuka jeupe, maasakri walipomuona Moses ambaye wanamtambua kama mwansayansi mashuhuri tu walimkaribisha kisha wakamsimulia kila kitu na ripoti yao ilivyo.

         "mwili vipi mmeshaanza kuchunguza?" Moses aliuliza baada ya kupewa taarifa hiyo

         "hapana bado ndiyo Dokta Hilary alikuwa anakusubiri wewe kwani kuna kitu amekibaini" Askari mmoja alijibu.

         "vizuri' Moses alipongeza kisha kamfuata Dokta Hilary akasalimiana kwani ni rafiki yake wa siku nyingi tangu kipindi yupo shuleni.

         "vipi Bite hajambo?" Dokta Hilary aliuliza

         "Ndiyo hajambo, vipi Irene naye?" Moses alimuleleza kuhusu hali ya Irene kisha kamuulizia kuhusu hali ya Beatrice

         "hajambo,afadhali umefika njoo uone nilichokibaini katika mwili huu" Hilary alimuambia Moses huku akimpatia mipira ya kuuvaa mikononi, Moses alivaa mipira hiyo na kwa pamoja wakuendea mwili uliokuwa umefunika shuka wakaufunua. Ulikuwa ni mwili wa Askofu Edson ambao tayari ulikuwa kuwa mwekundu tofauti na miili mingine  inavyokuwa baada ya kuondokwa na uhai.

         "Shit! Waambie Wauguziaskari waupeleke hospitali tukachukue vipimo" Moses alisema huku akisimama akawa anavua mipira ya mkononi aliyovaa halafu akampa ishara Norbert kisha akasogea mahali ambapo hapakuwa na mtu, Norbert alimfuata hadi mahala hapo akawa anamtazama kumuashiria aongee.

         'Quantanise ipo ndani ya mwili wake na ndiyo chanzo cha kumuua, hivyo kauawa hisia zangu zinanipa jibu hilo  na nitakupa jibu sahihi zaidi" Moses aliongea pasipo kujali kama Norbert kamsikiliza au hakumsiliza na aliondoka eneo hilo akatoka hadi nje akarudi kwenye gari lake akaingia ndani, alitoa simu yake ya mkononi akabonyeza baadhi ya namba halafu akaiweka sikioni
"Moses Gawaza mkurugenzi mkuu TISS,naomba alama za vidole zitakazochukuliwa katika eneo la tukio la kifo cha Askofu ziletwe ofisini kwangu haraka sana" Aliomgea baada ya simu kupokelewa kisha akakata akashuka kwenye gari lake.


****


     Upande mwingine wa jiji la Dar es salaam katika nyumba iliyopo  maeneo ya Ilala, kulikuwa kuna kikao cha watu watano ambao walionekana kufurahi sana kwani mpango wao ulikuwa umefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuufanya. Watu hao walikuwa wameweka duara na mbele yao kulikuwa na boksi kubwa lenye alama ya nembo ya maabara ya umoja wa mataifa ambayo alikuwa akifanya kazi Moses.

    Wawili kati ya hao watu walikuwa ni viongozi wakubwa wa kiimani nchini, wawili walikuwa ni  vijana wa makamo wanaokaribia utuzima ambao walikuwa mapacha na mmoja alikuwa kijana anayekaribia utuzima mwenye muonekano wa kitanshati sana.

           "Yaani nyinyi Panthers nimeamini kuwa sikuwaleta hapa kwa kazi bure kwani umuhimu wenu tumeuona jana maana Edson angetuchomesha yule" Yule kijana aliongea huku akitabasamu tu akiwaambia wale mapacha wanaokaribia utuzima.

           "unajua uliposema kwamba Askofu Edson ameenda huku akiwa kavaa lile vazi la kiaskofi kupeleka ile barua nilijua tu tayari alikuwa amekosea na uliponieleza kuwa yule jamaa ni  Mkurugenzi wa usalama wa taifa basi nilijua inabidi tupoteze ushahidi kabisa ili mambo yasiwe mabaya. Kumbuka haitakiwi kuvaa vazi lile nje ya kanisa angevaa suti yake na shati lake la zambarau linalomtambulisha kama askofu' Mmoja wa wale mapacha alisema.

           "hata mimi nilikuwa nina wasiwasi maana nilimsisitiza asivae ila yeye kavaa halafu anakuja kutuambia alitaka kumteka akili zaidi" Kiongozi wa dini ya kikristo aliongea.

           "Ok siyo ishu tena hiyo sasa tuanze na mkakati mwingine nafikiri ni zamu ya Young Panther utekeleza" Yule kijana aliwaambia kisha wakaanza kupanga mikakati mipya ya mpango wao ambao laiti ingejulikana mapema basi serikali pamoja na wanachi wangeweza kuondokwa mabalaa ambayo yalikuwa yankuja kuikumba nchi yenye amani na upendo Tanzania, usiri wa mpango wao ndiyo umefanya jamii isitambue azma ya watu hawa.


****


     Baada ya   masaa kadhaa  mpango mwingine usukwe tayari majibu ya uchunguzi wa     Mwili wa Askofu Edson yalikuwa yameshatoka na nakala moja ilikuwa imeshawasilishwa polisi na nakala nyingine ilikuwa ipo mikononi mwa Moses ambaye muda huo alikuwa akiijadili na Norbert katika ofisi ya wahanga iliyopo katikati ya jiji la Dar es salaam. Kile alichokifikiria Moses juu ya kilichosababisha kifo cha Askofu Edson ndiyo hicho hicho kilikuwa kwenye majibu hayo, mwili wa  Askofu Edson ulikutwa na kiwango kidogo cha dawa ya Qyantanise ambayo hutumika kuua wadudu kwenye mimea pia alama za vidole zilikuwa zimekutwa katika eneo hilo tayri zilikuwepo hapo mbele yao ambayo bado haikujikana muhusika ni yupi hadi muda huo.

         "Dogo aliyefanya haya mauaji si mtanzania kabisa" Norbert baada ya kuyapitia majibu hayo kwa mara ya aliongea .

         "hata mimi hilo nimelibaini mapema tu kwani kila mtanzania mwenye umri kuanzia miaka kumi na nane alama yake ya mkono ipo kwenye kitambulisho cha kupiga kura au kitambulisho cha taifa, hivyo kila mtanzania fingerprint yake imeingia kwenye database ya serikali. Kutokana na serikali kuvitilia mkazo vitambulisho hivi kila mtu amejisajili sasa kama angekuwa mtanzania angekuwa kashajulikana sura hadi picha kwani vipo kwenye mitambo ya serikali" Moses alikubaliana na maneno ya Norbert kisha akatoa ufafanuzi zaidi.

           "wajibu wa kumjua mhusika wa hili suala ni wetu, inabidi ajulikane tulinde heshima ya nchi na rais wetu' Norbert aliongea

            "nafikiri tu..." Moses aliongea lakini alishindwa kumalizia kauli yake baada ya simu ya Norbert kuita, Norbert alizuia Moses asiongee kisha akapokea simu akasikiliza bila kusema kitu hadi ikakatwa.

      Aliirudisha aliweka simu yake kisha katikitisa kichwa chake  halafu akavuta pumzi kwa nguvu akaiachia akmtazma Moses.

            "kuna nini?" Moses aliuliza

           "Mufti mkuu wa Dar es salaam amekutwa amefariki ofisini kwake na mwili ni kama wa Askofu Edson" Norbert aliongea kisha akanyanyua macho juu kutazama dari la ofisi.

           "Shit!" Moses alisema huku akipiga ngumi mezani kwa nguvu

ITAENDELEA!!


HAIRUHUSIWI KUNAKILI RIWAYA HII KWA NAMNA YOYOTE PASIPO RIDHAA
YA MTUNZI





UKIIHITAJI YOTE KWA MALIPO, BASI WASILIANA NASI KUPITIA UJUMBE MFUPI WA MANENO KWENDA NAMBA 0762 219759