Wednesday, December 23, 2015
Tuesday, December 22, 2015
Monday, December 21, 2015
Sunday, December 20, 2015
Saturday, December 19, 2015
Friday, December 18, 2015
Thursday, December 17, 2015
Wednesday, December 16, 2015
SHUJAA SEHEMU YA KUMI NA MBILI
RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
ILIPOISHIA
"Hakika mimi ni kitwana mtoa burudani kwako Malkia ninayekuhusudu zaidi ya nafsi yangu, jukumu la kukupa burudani ewe malkia wangu uliye pekee ni langu na nitalifanya pasipo kungoja shukrani zaidi ya hifadhi ya moyo wangu katika Kasri la upendo wako. Nanena yatokayo moyoni yanayothibitika hata machoni, I love you Beatrice " Moses aliamua kuweka hisia zake wazi kwa Beatrice huku mapigo yake ya moyo yakiwa juu kama ameshtuliwa na ndoto ya kutisha usingizini. Maneno hayo yalisababisha moyo wa Beatrice mshtuko wa furaha, kitendo cha yeye kutamkiwa neno hilo na kijana aliyempenda ilikuwa ni furaha kwake ingawa alikosa la kuongea kwa muda huo. Hata alipotaka kuongea alikatishwa na sauti ya mama yake.
Tuesday, December 15, 2015
SHUJAA SEHEMU YA KUMI NA MOJA
RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
ILIPOISHIA
Muimbaji wa nyimbo hiyo alipomaliza kuimba beti za mwisho za nyimbo hiyo, watu waliomzunguka walitawanyika na kufanya sura yake ionekane kwa Beatrice huku watu wakipiga makofi kwa shangwe. Beatrice aliishia kutabasamu baada ya kumuona muimbaji akiwa ni Moses, hakujua ratiba ya ile sherehe ilipangwaje maana ni jambo lilikuwa la kushtukiza kwake na lililomfurahisha.
Monday, December 14, 2015
SHUJAA SEHEMU YA KUMI
RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
ILIPOISHIA
JIONI
MIKOCHENI
DAR ES SALAAM
Sauti ya muziki mlaini ndiyo iliyokuwa ikiwaliwaza watu wachache waliopo katika viti vilivyopambwa
vizuri katika bustani nzuri ya majani, mbele ya viti hivyo kulikuwa kuna meza kubwa iliyopambwa kwa
namna ya kuvutia ikiwa ina viti vitatu vilivyonakshiwa na mapambo ya vitambaa vyenye
rangi taofauti. Nje ya geti la nyumba hiyo kulikuwa na walinzi waliovalia suruali nyeusi pamoja na shati
jeupe lenye tai ya kipepeo inayoning'inia shingoni mwao, mandishi mbalimbali yakumtakia Beatrice
sikukuu njema ya kuzaliwa ndiyo yalikuwa katikati mabango mbalimbali yaliyomo humo ndani.
Sunday, December 13, 2015
SHUJAA SEHEMU YA TISA
RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
FACEBOOK PAGE LINK: www.riwayamaridhawa.blogspot.com
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
ILIPOISHIA
Upeo mkali wa macho ya Norbert uliweza kumtambua mzungu huyo ambaye ndiye aliyekuwa
amefanya akae katika mgahawa huo, sasa alihitaji jambo ambalo alilipanga kulifanya na ikamlazimu
kusubiri hapo mgahawani. Kinywaji chake alikiona hakina maana tena zaidi ya kufanya jambo
lilimuweka hapo, alisubiri gari hilo lilipoondoka kwa umbali wa mita kadhaa kisha akalipa kinywaji chake
halafu akaenda hadi alipoegesha gari yake. Aliingia kwa haraka kisha akaliwasha halafu akaliingiza
barabarani kufuata uelekeo ambao ile range rover imepita kwa mwendo wa kasi, baada ya mwendo
mfupi aliikuta ikiwa ipo katika mwendo wa kasi baada ya barabara ya eneo la Msasani kuwa tupu.
ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI YAKE
SEHEMU YA TISA!!
Bado walikuwa wapo mtaa wa Mahando ambao ndio mtaa wenye makazi ya Dkt Mbungu, Norbert aliifuatilia gari ya Scott kwa namna ambayo ni ngumu kujulikana kama anamfuatilia. Akiwa ameacha umbali wa mita nyingi ambao ulimsaidia kufanya Scott na dereva wake wasimuhisi chochote, mwendo alioutumia ulikuwa ni wa wastani ulikuwa haushindi mwendo wa gari ya mbele yake. Utumiaji wa mwendo wa namna hii ulisababisha Norbert asiweze kuikaribia gari ya mbele yake, umakini wake katika kulifuatilia gari la mbele yake ulizidi kuwa mkubwa. Gari alilomo Scott liliingia kulia lilipofika mtaa wa Tosamaganga kuifuata barabara inayoenda kwenye barabara ya Haile Selassie, lilienda kwa mwendo mfupi kisha likakata kona kuingia kushoto katika barabara ya Haile Selasie kisha likaongeza mwendokasi wake. Norbert naye alikuwa analiungia mkia kwa namna ya kipekee na gari hilo lilipoingia barabara ya Haile Selasie yeye alikuwa nyuma kwa umbali wa mitaa kadha akiwa ameyaacha magari mawili yakiwa yametangulia mbele ya gari hilo, aliongeza mwendokasi wa gari akiwa yupo makini sana na muelekeo wa gari hilo. Walipofika mgahawa wa Gastro Garden magari mawili yaliyopo mbele ya gari ya Norbert yaliingia hapo na kumfanya Norbert awe nyuma ya gari ya akina Scott kwa umbali wa mita kadhaa, hapo Norbert alihisi upo uwezekano watu waliomo ndani ya gari hiyo ya mbele kuhisi kama wanafuatiliwa. Hivyo alihitajika afanye jambo kuwapoteza akili watu na wahisi hali ya kutofuatiliwa, akiwa nafikiria jambo la kufanya tayari walikuwa wamefika Shopers plaza iliyopo kando ya barabara ya Haile Selassie. Norbert akikata kona kuingia Shopers plaza halafu akaelekea yalipo megesho ya magari. Alisimamisha gari katika maegesho hayo kisha akatoa simu yake ya kiganjani , alibonyeza baadhi ya vitufe vya simu hiyo kisha akaiweka sikioni.
"hey Simion tukutane pale pa siku zote na uje na gari yako" aliongea kisha akakata simu kisha akaiweka, aliwasha gari kisha akatoka eneo la Shorpers plaza. Aliingia tena katika barabara ya Haile Selasie kwa kuelekea upande wa kushoto kisha akaongeza kufuata ili aliwahi gari alilokuwa analifuatilia, baada ya mwendo mfupi alilikuta gari la akina Scott likivuka makutano ya barabara ya Haile Selassie na ile iendayo mtaa wa Mwaya. Gari hiyo iliendelea kufuata barabara ya Haile Selasie kwa mwendo wa kasi huku Norbert akiwa bado yupo nyuma yake, ilipokuwa ikikaribia barabara ya hiyo na ya kaole Norbert aliongeza mwendo kisha akapandisha vioo vya gari yake ambavyo ni vya giza.Aliipita gari hiyo kwa mwendo mkali kisha akawa yupo mbele yake huku taa ya njano ya upande wa kushoto kuashiria anaingia kushoto ikiwa imewashwa, alikata kona kuingia kushoto katika mtaa wa Lincolin kwa kuitumia barabara ya Kaole kisha akaenda mbele kwa umbali mfupi na kupelekea atokee katika barabara iliyopo upande wa kulia. Barabara hiyo ambayo inaelekea katikati ya mtaa wa Lincoln ilikuwa pembeni yake kwa muda huo, likata kona kuingia kulia kisha akatembea kwa umbali mfupi halafu akaegesha gari pembeni ya barabara mbele ya toyota harrier ya rangi nyeusi yenye vioo vya giza. Norbert kwa haraka kisha akatembea hadi kwenye mlango wa dereva wa toyote harrier, aliufungua mlango wa dereva wa gari hiyo ambayo dereva wake alikuwa ndani yake.
"Simion ingia kwenye gari yangu halafu unifuate" alimwambia dereva gari hiyo ambaye alitii mara moja. Simion aliingia ndani ya gari ya Norbert na Norbert akaingia kwenye gati yake kisha safari ikaanza. Wote kwa pamoja walielekea barabara hiyo moja kwa moja kisha wakakata kulia walipofika katika barabara ya Chole wakielekea yalipo makutano ya barabara hiyo na ya Haile Selasie, walikata kona kuingia kushoto kisha wakaongeza mwendo wa magari ya yao.
****
Amani ndani ya moyo wa Scott ilipotea muda mfupi tu tangu alipoliona gari aina ya suzuki ya rangi nyekundu ikiwa nyuma yake tangu alipoiona kwenye mtaa wa Tosamaganga ikimfuatilia. Wakati wapo barabara ya Haile Selasie ndipo alipozidi kuitilia shaka gari hiyo kutokana na kuonekana inamfuatilia kwa mbinu za hali ya juu za kiusalama. Kijana huyu mwenye mafunzo ya kijasusi aliijua mbinu hiyo ya kufuatiliwa ambayo isingejulikana na mtu wa kawaida, gari hilo lilipoingia Shopers plaza aliliona na akajiridhisha kwamba halimfuatilii yeye. Amani katika moyo wake ilirudi ingawa haikudumu kwa muda mrefu, amani hiyi iliondoka tena baada ya kuliona gari lililokuwa likimfuatilia likiwa nyuma yake. Hapo aligeuka nyuma kisha akaitazama vizuri lakini hakufanikiwa kumuona dereva wa gari hiyo.
"hii gari huko nyuma nina wasiwasi nayo" Scott alimwambia dereva.
"usijali bosi ngoja tuingie Ally hassan mwinyi road halafu nitajua nishughulike naye vipi" Dereva alimtoa wasiwasi huku akiangalia kwa umakini kwenye vioo vya pembeni halafu akasema "huyo hapo anatupita". Scott alipoangalia upande wa dereva aliiona ile gari ikiwapita kisha ikawasha taa kiashiria ya upande wa kushoto kuashiria inaingia kushoto, gari ile iliingia katika barabara ya Kaole kwa mwendo wa wastani.
"nadhani tumeweka dhana mbaya" Dereva aliongea.
"si dhana mbaya ila kujihami muhimu maana huenda nikawa najulikana na mtu yoyote" Scott alimwambia.
"nadhani hakuna anayekujua bosi maana ndio kwanza una siku mbili" Dereva alimwambia.
" tusijiaminishe kitu tusichokijua namna hiyo" Scott alimwambia. Hawakuiona ile gari tena hadi wanaingia mtaa wa Chabruma kwenye makutano ya barabara ya Haile selassie na barabara ya Alli Hassan Mwinyi ndipo walipoiona ikiwa ipo nyuma ya toyota harrier ya rangi nyeusi . Walipoingia barabara ya Ally Hassan Mwinyi waliiona ikiwa ipo nyuma ya toyota harrier, dereva wa Scott aliitazama ile gari vizuri kisha akatoa simu yaken Alibonyeza baadhi ya vitufe kisha akaiweka sikioni.
"nataka niwakute kwenye mataa ya mtaa wa Morocco kisha muifuatilie gari aina ya suzuki escudo ya rangi nyekundu ambayo ipo nyuma yangu ikiwa imeacha gari moja mbele. Nataka mumpe utamu derevs wake". alikata simu kisha akamtazama Scott halafu akamwambia "kazi imeisha sisi turudi maskani tu". Scott alitabasamu kisha akakubali kwa kutikisa kichwa chake, furaha yao ilizidi pale walipokuwa wanayavuka mataa ya Morocco wakiingia barabara ya Bagamoyo baada ya kuwaona vijana wao wa kazi wakiwa wameegesha gari yao pembeni.
"vijana wa kazi hao hapo si tuwe na amani tu" Dereva alimwambia Scott akiwa ametabasamu. Wakiwa wanaendelea na safari yao ile gari ya vijana wao ilikuwa ipo nyuma ya suzuki ya Norbert inayoendeshwa na Simion. Hadi wanawasili mataa ya Mwenge tayari walikuwa wana uhakika kuwa ile gari inawafuatilia, kwenye mataa ya Mwenge walikuta taa za upande wao zimewaka nyekundu hali iliyowalazimu kusimama kutii sheria. Wakiwa hapo macho yao yote yalikuwa kwenye suzuki waliotilia shaka ambayo sasa ilikuwa imeingia kwenye barabara ya Sam nujoma ikiwaacha hapo kwenye mataa wakisubiri waingie njia ya Bagamoyo. Hadi muda huo hawakuwa wameitilia shaka toyota harrier iliyokuwa ipo nyuma yao kwenye foleni hiyo ya mataa, waliwaachia kazi vijana wao waitekeleze wao wakawa wamekaa kiamani.
****
MLIMANI CITY
DAR ES SALAAM
Gari aina ya toyota altezza ya rangi ya njano iliegeshwa kwenye maegesho ya magari ya mlimani city kisha milango ya gari hiyo ikafunguliwa, miguu ya rangi ang'avu inayoelekea kuitwa meupe ilitangulia kugusa ardhi ya eneo la Mlimani city kisha viatu virefu vya rangi nyekundu vikaifanya miguu hiyo ionekane ipo ghorofani. Mabinti wawili wenye uzuri wa asili walionekana wakishuka ndani ya gari hiyo, kimuonekano tu kwa kuwatazama walionekana walikuwa ni ndugu. Magauni ya kufanana waliyoyavaa yaliwafanya waonekane ni mapacha kutokana na kufanana kwao, macho ya vijana wakware ambao wapo hapo kwa ajili ya kuonekana na macho ya warembo yalinasa upande walioshuka mabinti hao. Victoria na mdogo wake Beatrice ndio hao mabinti walioingia , waliingia moja kwa moja ndani ya
mlango ulioandikwa game wakiacha mjadala nyuma yao ukiendelea. Pembeni ya mlango walioingia mabinti hawa kulikuwa kuna kundi wavulana waliokuwa wamevaa mavazi ya kileo.
"wana hizo totoz mmezisoma" mmoja wa wavulana hao aliongea.
"dah! Aisee mungu kajua kuumba, watoto kama mlango wa msalani hawaujui" Mwingine akaongea kuwasifia.
"naona hamjipendi nyinyi" mmoja mwingine aliwaambia.
"Kevi acha uoga wewe, kwani wake za watu wale" aliyesimama karibu na kijana aliyeitwa Kevi aliongea.
"mnamjua Bernard Mutashobya" Kevi akawauliza
"daah yule mzee mkuda aliyemtupa mwanafunzi wa UD ndani kisa anamkaa mtoto wake" Kijana aliyekuwa anawasifia Beatrice na Victoria aliongea.
"sasa hawa ndio watoto wake na huyo mmoja anaeonekana ni mrefu kuliko mwenzie ndiye huyo demu aliyesababisha jamaa akalala ndani na baadaye akaihama nchi. Sasa kama hamjitaki nyinyi vamieni msala huo" Kevi aliwapa onyo kisha akaanza kutembea kuelekea mahali lilipo geti la kuingilia.
"wana kama ndio hao watoto wake basi mi najipenda sana" kijana aliyeanza kuwaonesha wenzake wakina beatrice aliongea kisha akaongoka kumfuata Kevi huku wenzake wakiwa nyuma.
****
Safari ya Scott na dereva wake iliishia kwenye nyumba ya kifaharii iliyopo maeneo ya Bunju, muda wote huo Norbert alikuwa nyuma yao na hata walipoingia pembeni ya barabara kisha wakaenda kwenye nyumba hiyo iliyojitenga na makazi ya watu tayari aliwaona na ikamlazimu kupita sehemu hiyo kwa umbali mrefu kisha akaenda kupumzika katika sheli iliyopo Bunju huku akijaza mafuta ya gari hiyo, alipomaliza aliondoka kurejea alipotoka baada ya kuwa na uhakika wa kuwapumbaza Scott na dereva wake kwa chenga ya mwili aliyowapiga. Hakuwa na wasiwasi na Simion ambaye alijua kama anafuatiliwa, Norbert anamtambua Simion kama mtu mjanja kupitiliza na aliwahi kuponyoka katika mikono ya hatari kwa kucheza na akili zake tu.
***
Baada ya kuingia barabara ya Sam nujoma Simon aliitazama gari ya vijana waliotumwa na dereva wa Scott kisha akatabasamu, alikanyaga mwendo kuifuata barabara ya Sam nujoma huku akicheka mwenyewe. Aliuvuka mzunguko wa barabara uliopo jirani na Mlimani city kisha akaifuata barabara ya Sam nujoma hadi kwenye makutano ya barabara hiyo na barabara ya Igesa inayoelekea Sinza makaburini ambapo aliiacha barabara ya Sam nujoma kisha akaingia barabara ya Igesa. Aliifuata barabara moja kwa moja kisha akakata kona ya pili iliyopo upande wa kulia ambayo ilimpeleka hadi kwenye nyumba moja ya ghorofa yenye geti jeusi, alipiga honi mara moja na kupelekea geti lifunguliwe kisha akaingiza gari ndani akiangalia nyuma kupitia vioovya pembeni. Watu waliotumwa kumfuatilia walipitiliza moja kwa moja baada ya kujua eneo ilipoingia hiyo gari, Simion aliingiza ndani hadi kwenye maegesho ambapo alipokelewa na binti mmoja mrembo.
"bibie jiandae kuna watu nimewaingiza choo cha kike, kwahiyo tarajia ugeni leo wa wageni wanaohitaji sebene" Simion alimwambia binti huyo huku akifunga milango ya gari.
"dah sijacheza siku nyingi sebene sasa tarajia wageni hao watapata dansa la nguvu" Binti huyo alijibu kimafumbo kama alivyosemeshwa na Simion.
****
JIONI
MIKOCHENI
DAR ES SALAAM
Sauti ya muziki mlaini ndiyo iliyokuwa ikiwaliwaza watu wachache waliopo katika viti vilivyopambwa vizuri katika bustani nzuri ya majani, mbele ya viti hivyo kulikuwa kuna meza kubwa iliyopambwa kwa namna ya kuvutia ikiwa ina viti vitatu vilivyonakshiwa na mapambo ya vitambaa vyenye rangi taofauti. Nje ya geti la nyumba hiyo kulikuwa na walinzi waliovalia suruali nyeusi pamoja na shati jeupe lenye tai ya kipepeo inayoning'inia shingoni mwao, mandishi mbalimbali yakumtakia Beatrice sikukuu njema ya kuzaliwa ndiyo yalikuwa katika mabango mbalimbali yaliyomo humo ndani.
ITAENDELEA!!
Saturday, December 12, 2015
SHUJAA SEHEMU YA NANE
RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
ILIPOISHIA
"nafurahi kukufahamu" Norbert alimwambia Scott huku wakipeana mikono ,kitendo cha Norbert
kumuona Scott haikuwa mara ya kwanza. Alijaribu kuvuta picha ni wapi alipomuona lakini kumbukumbu zilikuja na kutoka, alipofikiria mara kwa mara ya pili ndipo kumbukumbu zake zilipompa jibu sahihi na
hapo ndipo akatambua mahali alipomuona Scott. Hakika alibaini ni mmoja wa watu aliowapiga picha
kule Biharamulo usiku wa kuamkia Ijumaa ingawa alikuwa ana muonekano tofauti, sasa hapo ndipo vita
ya maswali ilipoushambulia ubongo wake ingawa alionekana hakuwa na wazo lolote zito. Kiherehere
cha kutaka kupata majibu ya maswali yake kilishampanda na hapo alikuwa akisaka majibu kwa
kutumia dhana jambo lilimjia tofauri, alivyotambulishwa na ujio wa mtu huyo vilikuwa vitu viwili tofauti.
ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI YAKE
SEHEMU YA NANE!!
Hadi muda hamasa ya udodosaji wa undani wa Scott ndiyo iliyomfurukuta nafsini mwake, wazo la kuwepo uwezekano wa kuwa anaonana uso kwa uso na mtu mbaya ndio lilitawala akili yake kiasi kikubwa. Zote zilikuwa dhana tu juu ya Scott ambazo zilihitaji ushahidi wa kuzifanya vionekane ni ukweli ndani ya tarakilishi ya ubongo wake, mawazo hayo yalitawala ubongo wake ndani ya sekunde kadhaa pasipo kujulikana na waliopo mbele yake kama yupo nje ya eneo hilo kimawazo.
"hivyo ofisa huyu nadhani ameingia siku..." Dkt Mbungu alijikuta akiwa haijui siku aliyoingia Scott ndani ya nchi hii kutokana na kutotajiwa na Scott na ikamlazimu amuangalie mhusika kwa namna ya kutaka atajiwe.
"juzi na ndege ya shirika la Uswisi nikitokea likizo nyumbani Uswisi" Scott alimtajia akiwa anajiamini sana pasipo kuonesha chembe yoyote ya ubabaikaji, akili zake zilimwambia kuwa amefanikiwa kuwadanganya watu hao. Hakutambua kama alikuwa anadanganya mtu mmoja na mwingine hakuwa akimdanganya, akiwa kama hinadamu hakuweza kusoma mawazo yaliyomo katika ubongo wa binadamu yoyote. Ndio maana fikra zake zilimuambia kama alifanikiwa kudanganya kumbe alikuwa anajidanganya yeye mwenyewe.
"ndio bwana Scott nafurahi kuupata ujio wa mtu kama wewe kutoka kwenye asasi kubwa za kimataifa kama umoja wa mataifa hivyo titarajie mazuri katika safari yako ya kuja huku nchini kwetu" Norbert aliongea kwa kumuhadaa Scott huku Dkt Mbungu akitikisa kichwa kukubaliana na maneno aliyoyaongea Norbert.
"ndiyo maana yake nafikiri itakuwa chachu ya taifa hili kuongeza juhudi za kupambana na wanasayansi haramu kupitia kazi yangu iliyonileta hapa Tanzania" Scott aliongea kwa namna ya kujivunia kama amekujaTanzania kwa ajili ya kazi hiyo.
"sasa jamani mimi ninawahi sehemu mara moja, inabidi niondoke hivi sasa" Norbert aliongea huku akipeana mikono na Dkt Mbungu pamoja na Scott.
"haya bwana Kaila tuonane jumatatu ofisini kwa ajili ya kazi nyingine kuhusu mimea hii ukipata nafasi ya kufanya hivyo" Dkt Mbungu alimwambia Norbert ambaye tayari alikuwa ameshaanza kuondoka. Nafsi ya Norbert muda huo ilimwambia anatakiwa kufanya jambo la upesi sana na jambo hilo litafanyika tu ikiwa atawahi kuondoka mapema kabla ya mgeni wa Dkt Mbungu hajaondoka, ndiyo maana aliaga kuwa anawahi sehemu jambo ambalo sio la ukweli. Kiherehere cha kudadisi mambo juu ya Scott ndio kilikuwa kikimchachafya katika mwili wake na ikamlazimu atangulie ili jambo analotaka kulifanya lisiharibike.
****
Usingizi ulimpaa mapema na ndoto alizokuwa akiziota juu ya kipenzi cha moyo ambaye bado hajafsnikiwa kufangua naye ukurasa mpya zilipotea, alipofungua macho alikutana na miale ya jua ambayo imepenya kutoka kwenye mwanya mdogo ulioachwa na pazia baada ya kutofunikwa vizuri. Moses aliulaani mwanga huo kwa kuingia ndani na pia aliilaani mpambazuko wa siku hiyo mpya, aliinuka kisha akaenda kufunika vizuri pazia halafu akarejea kitandani na akajifunika tena shuka kama ilivyokuwa awali. Alifumba macho kisha akahamisha mawazo yote katika kuuvuta usingizi ambao uligoma kuja kutokana na mazoea yake ya kuamka mapema, lengo la kuuvuta usingizi huo kwa mara ya pili ilikuwa aweze kuota tena ndoto juu ya kipenzi cha moyo wake wanayependana. Hakika kupenda kwa mara ya kwanza kulimchanganya na kukamfanya awe kama mwendawazimu kutokana na kitendo cha kulala kwa lengo la kumuota Bratrice kwa mara ya pili, ni mawazo ya kujenga nyumba hewani ndoiyo yalimjia kutokana na kutokuwepo wala kuwahi kutokea mtu kujipangia ndoto ya kuota pindi alalapo. Aliamua kuamka kisha akaenda kusafisha kinywa chake akiwa na ana tabasamu lisilofutika katika uso wake, alijikuta akiimba nyimbo mbalimbali za mapenzi za kingereza kila muda. Hali hii ilimshangaza sana mjomba wake baada ya kumuona maana haikuwa kawaida yake, udadisi wa kutaka kumuuliza kipi kinamsumbua ndio uliomvaa mjomba wake.
"anko kuna nini mbona leo tabasamu halikubanduki usoni" Kennedy alimuuliza Moses ili kubaini kinachomfanya mpwa wake huyo atabasamu muda wote.
"hamna kitu anko ni furaha ya kuiona siku nyingine ya mapumziko ya mwisho wa wiki" Moses aliamua kutumia uongo ili kuficha chimbuko ka furaha iliyomo nafsini mwake.
"mmh! Anko inamaana tumeanza kufichana siku hizi?" Kennedy alimuuliza Moses.
"hapana anko sijakuficha kitu chochote nina furaha ya kuiona siku ya mapumziko tu" Moses aliongea.
"Mmmh! Yote sawa basi, kapate kifungua kinywa kwanza" Kennedy alimwambia Moses kisha akaelekea chumbani kwake. Moses aliekea sehemu yenye ukumbi wa kula chakula kwa ajili ya kupata kifungua kinywa, alikuta kila kitu kimeandaliwa na kinamsubiri yeye ili aweze kuvitendea haki vitafunwa vya asubuhi hiyo.
****
Beatrice naye usingizi uliwahi kumuacha akiwa bado anauhitaji na alipoulazimisha bado uligoma kuja hivyo ikamlazimu kuamka kwani kulikuwa tayari kushapambazuka, aliinyoosha kivivu baada ya kuamka huku miayo ikiwa imetawala kinywa chake kisha akainuka kitandani hadi kwenye meza ndogo ya kuwekea vipodozi halafu akakaa kwenye stuli ndogo iliyopo kwenye meza hiyo yenye kioo kilichojengwa kisasa. Shajara yake ilikuwa ipo juu ya meza hiyo ya vipodozi ikiwa imefungwa kama akivyoiacha, hicho ndicho kitu cha kwanza alichoweza kukikumbuka asubuhi hiyo kuliko hata suala la kusafisha kinywa chake. Aliifungua Shajara hiyo hadi alipoibandika picha ndogo ya Moses kisha akaibusu huku akitabasamu, aliinyanyua Shajara hiyo kisha akaikumbatia. Ama kweli penzi ni uchizi ukikuvaa hautibiki kwa daktari yoyote yule mwenye uzoefu wa kutibu magonjwa ya akili, tiba ya penzi ni kumpata yule aliyekuletea ugonjwa ili awe tiba kwako na ukimkosa jua ndio itasababisha ugonjwa kabisa. Ndio hivyohivyo kwa binti huyu ambaye anasumbuliwa na ugonjwa huu na anahitaji dawa haraka iwezekanavyo na dawa yenyewe ni chimbuko la ugonjwa huo yaani mtu aiesababisha akawa na hali hiyo, hakika Moses ndiyo tiba sahihi ya ugonjwa wake na anamuhitaji zaidi ya mgonjwa anavyomuhitaji daktari wa ugonjwa wake. Bado aliendelea kukaa kwenye kijistuli kidogo kilichopo katika meza ndogo ya kuweka vipodozi ambayo wenye lugha yao hii kila kukicha.huwa tunaipapatikia kuliko lugha yetu wanapenda kuita meza hiyo kwa jina la 'Dressing table', tabasamu lisilokauka mithili ya chemchem itokanayo na mwamba uliopo ardhini ndio iliujaza uso wake na kumfanya aonekane mrembo zaidi.
"crazy lover hujambo" aliisikia sauti ya dada yake Victoria akimuita jina linakoendana na jinsi alivyo.
"mmmh dada, sijambo" Beatrice aliongea .
"yaani huyo mkaka atakutia wazimu kabisa huko unapoelekea" Victoria alimwambia.
"jana umesema nipo right kuwa hivi kwasababu ya huyu handsome boy, sasa leo mbona unaniambia atanitia wazimu?" Beatrice aliuliza kwa sauti iliyojaa deko.
"young sis tatizo umezidi au ni mara ya kwanza kupenda?" Victoria alimwambia huku akimfuata hadi kwenye meza hiyo ya kuwekea vipodozi halafu akamkumbatia kwa nyuma kisha akamwambia, "feelings juu yake zikikuzidi namna hiyo utafanya Dady ajue na iwe kama the thing happen to my first boyfriend".
"mmh! Unanitisha dada" Beatrice aliongea.
"sio kama nakutisha Dady ni mkali sana kuhusu hayo mambo nadhani unamkumbuka Allen my first boyfriend ambaye alilala nyuma ya nondo kisa kujulikana kwa uhusiano wangu na yeye " Victoria alimwambia Beatrice.
"yeah! Namkumbuka dada" Beatrice alikubali kumkumbuka mtu aliyetajiwa na dada yake.
"you suppose to be careful otherwise utakuwa umemuingiza kijana wa watu matatizoni kama ilivyokuwa kwa Allen ambaye nampenda na nitaendelea kumpenda ingawa hayupo ndani ya nchi hii kutokana na balaa la our Dady" Victoria alimwambia Beatrice huku machozi yakiwa yanamlenga katika macho yake, alisimama pembeni ya mdogo wake kisha akamwambia "napenda kuiona furaha yako mdogo wangu na sipendi kuiona huzuni yako katika siku hii ya leo ambayo ni ya furaha kwako sitaki yakupate kama yalinipata mimi, najua umemualika katika sherehe hii ya kuzaliwa kwako. Sasa basi kuwa makini ili wapambe wa dady wasijue lolote kuhusu hisia zako juu yake, la si hivyo jua dady akirudi safari furaha yako itageuka shubiri".
"ok sis nimekuelewa please don't cry nitakuwa makini" Beatrica alimwambia dada yake kisha akainuka halafu akamkumbatia.
"usijali mdogo wangu, jiandae twende shoping kwa ajili ya sherehe jioni ya leo" Victoria alimwambia mdogo wake huku akifuta machozi yaliyoanza kumtoka alipokuwa akimkumbusha jambo lililotonesha kidonda chake cha kutenganishwa na mpenzi wake wa kwanza anayempenda kuliko kitu chochote. Beatrice alimuachia dada yake kisha akaelekea katika mlango wa bafu lililopo humo chumbani mwake, aliingia ndani ya bafu hilo akimuacha dada yake akiwa akiwa yupo chumbani mwake.
****
Baada ya kutoka nyumbani kwa Dkt Mbungu aliamua kufanya jambo ambalo hakutakiwa achelewe kulifanya, Norbett aliingia kwenye mgahawa uliopo jirani na nyumba ya Dkt Mbungu kisha akakaa katika kiti kilichopo mkabala na lango la nyumba hiyo kilichozibwa na maua yalipambwa pembeni ya mgahawa huo. Kiti hicho alichokaa ilikuwa ni rahisi kwa mtu wa ndani kumuona wa nje na vigumu kwa mtu wa nje kumuona wa ndani kutokana na maua yaliyozunguka mgahawa huo. Aliagiza kinywaji kisicho na kilevi ili kupoteza muda wa kuwepo eneo hilo, subira yake ndiyo aliyoihitaji ili kufanya jambo alilolikusudia kulifanya kwa muda huo na uvumilivu wa kusubiri muda muafaka wa kutekeleza jambo hilo ufike ndio kitu peke alichokilazimisha kiutawale moyo wake kwa muda huo. Wazo la kuegesha gari jirani na mgahawa huo ndio lilimfanya mpango wake huo uwe upo vizuri kwa kutotambulika kama alikuja na usafiri ndani ya nyumba hiyo, aliendelea kunywa kinywaji chake taratibu huku akili ikiwa ipo makini katika kuangalia lango kuu la kuingilia nyumbani kwa Dkt Mbungu. Wahenga wanasema subira huvuta heri na haraka haraka haina baraka, usemi huo ulijidhihirisha wazi kutokana na subira aliyoiweka Norbert katika kusubiri muda mahususi wa kufanya kazi yake kwani subira yake ilizaa matunda baada ya gari aina ya range rover yenye rangi ya fedha ilipotoka ndani ya nyumba ya Dkt Mbungu ikiwa na dereva mwenye asili ya kiafrika na mzungu aliyekaa kiti kilichopo pembeni ya dereva. Upeo mkali wa macho ya Norbert uliweza kumtambua mzungu huyo ambaye ndiye aliyekuwa amefanya akae katika mgahawa huo, sasa alihitaji jambo ambalo alilipanga kulifanya na ikamlazimu kusubiri hapo mgahawani. Kinywaji chake alikiona hakina maana tena zaidi ya kufanya jambo lilimuweka hapo, alisubiri gari hilo lilipoondoka kwa umbali wa mita kadhaa kisha akalipa kinywaji chake halafu akaenda hadi alipoegesha gari yake. Aliingia kwa haraka kisha akaliwasha halafu akaliingiza barabarani kufuata uelekeo ambao ile range rover imepita kwa mwendo wa kasi, baada ya mwendo mfupi aliikuta ikiwa ipo katika mwendo wa kasi baada ya barabara ya eneo la Msasani kuwa tupu.
ITAENDELEA!!
RUKSA KUSHARE RIWAYA HII KOKOTE UPENDAPO, ILA USINAKILIA KWA NAMNA YEYTE ILE BILA RIDHAA YA MTUNZI

Friday, December 11, 2015
SHUJAA SEHEMU YA SABA
RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
ILIPOISHIA
.
"kwa kweli huyu mtoto kuwa HKL ni haki yake
maana huu mwandiko ni mkali balaa.. Mh! Hebu
ngoja" aliongea peke kisha akawa kama amegundua
kitu, aliinuka hadi kwenye begi lake la shule kisha
akachomoa bahasha nyingine halafu akarejea
kitandani halafu akaifungua bahasha hiyo. Aliitoa
kadi ya mapenzi ambayo alitumiwa na msichana
anayejiita Dream girl kisha akaifungua halafu
akaiweka sambamba na kadi ya mwaliko wa sherehe
ya kuzaliwa ya Beatrice. Alitazama miandiko ya kike
iliyomo kwenye kadi hiyo kwa umakini kisha
akaguna kuashiria amegundua kitu, alirudia tena
kuitazama miandiko hiyo halafu akatabasamu.
"Ha! Hai! Ha! Ha! Dream girl sasa nimekujua"
alisema baada ya kuona miandiko inafanana katika
kadi hizo, hakika aliweza kumbaini Beatrice kama
msichana aliyemsumbua kwa wiki kadhaa.
"huyu Hilary nahisi ni mwanga maana aliyoniambia
juu ya Beatrice ni ukweli mtupu" alizidi kuongea
peke yake haea alipokumbuka kauli ya Hilary juu ya
Beatrice
Thursday, December 10, 2015
SHUJAA SEHEMU YA SITA
RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
ILIPOISHIA
Moses alibaki ameduwaa akimtazama Beatrice
aliyekuwa akiondoka, Bratrice alipopotea katika upeo
wa macho yake alibaki akiwa ameduwaa kwa
kilichotokea.
"we boya bisha tena nikuone,changamkia tenda
hiyo" Sauti ya Hillary ilisikika kutoka nyuma yake na
kupelekea akurupuke kwenye mawazo.

Wednesday, December 9, 2015
SHUJAA SEHEMU YA TANO
RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
ANGALIZO: UANDISHI WA SEHEMU HII YA TANO UMETUMIA LUGHA KIGENI KWENYE BAADHI YA SEHEMU HASA KATIKA UELEZAJI WA MTAALA WA KEMIA KWA KIDATO CHA SITA KUTOKANA NA UGUMU WA KUFASIRI LUGHA YA SAYANSI
ILIPOISHIA
Alitembea
kwa tahadhari hadi katikati ya miti iliyo jirani na
eneo hilo akiwa na kamera yake ya kipelelezi tofauti
na kamera yake ya kawaida. Ajibanza
hapo hadi aliposhudia ujio wa boti mfano wa
nyambizi iliyofika hadi ukingoni, hadi hapo aliweza
kupiga
picha kila anachokiona kwa msaada wa mwangaza
uliotoka katika taa ya helikopta na taa ya boti. Hadi
watu sita wanashuka kwenye boti ile alikuwa
amewaona na amewapiga picha, boti hiyo pia
alikuwa ameiona na ameipiga picha pia na helikopta
aliipiga vizuri akilenga namba zake zilizopo ubavuni.
Alipomaliza alibaki palepale hadi walipoingia ndani
ya helikopta kuondoka, na ile boti ilipozama chini.
Hapo alirudi kwenye hema kisha akajilaza pembeni
ya msimamizi wake kama ilivyokuwa awali. Hadi
asubuhi inaingia alikuwa macho na jua
lilipochomoza alikusanya vitu vyake kisha
akaondoka porini hapo akiwa na msaidizi aliyepewa
ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI
YAKE
SEHEMU YA TANO
Alifika kisha akakabidhi kila kitu alichokabidhiwa na
ofisi za pori hilo halafu akakodi gari ya kumpeleka
bukoba mjini, uzuri wa hifadhi ya Biharamulo ilikuwa
ina magari ya kukodiwa maalum kwa ajili ya wateja
wao. Norbert alipata gari aina ya landcruiser yenye
mkonga ambayo iliwekwa hapo mahususi kwa
ajili ya kukodiwa, alielewana bei na dereva wa gari
hilo kutoka hapo hadi Bukoba mjini. Baada ya
makubaliano kufikiwa alipanda gari hiyo kisha safari
ikaanza, kwa kuelekea barabara iendayo kaskazini
mwa Biharamulo ili kuisaka Bukoba, ubora wa gari
aliyoikodi kwa masafa marefu ulimfanya awe na
uhakika wa kuwasili Bukoba ndani ya masaa kadhaa.
Pia dereva wa gari naye alijua sana kucheza na
usukani wa gari pamoja na kupangua gia, uhodari
wa dereva huyu ulimfanya Norbert atabasamu na
akijipongeza kwa chaguo lake bora miongoni mwa
madereva wengi aliowakuta jirani na ofisi za hifadhi
ya Biharamulo, walitumia masaa kadhaa wakawa
wameshafika mwanzo wa barabara ya Uganda
inayoeleiea Bukoba mjini. Dereva wa gari hilo alipita
kushoto ili azunguke mzunguko unaounganisha
barabara anatoka na barabara iendayo Bukoba mjini,
aliingia kushoto kuishika barabara hiyo kwa
mwendo wa wastani kisha akaongeza mwendo
baada ya kuingia rasmi katika barabara ya Uganda.
Hakika alimpata dereva aijuaye barabara za mkoa
huo kiundani zaidi kutokana na kuwa mwenyeji wa
mkoa huo. Dereva huyu alinyoosha barabara hiyo ya
Uganda hadi alipofika mwanzo wa barabara ya
Kawawa kisha akangia kushoto kuifuata barabara ya
Kawawa kuelekea mtaa wa Biashara kwenye
barabara ya biashara, aliingia katika barabara ya
Biashara kwa mwendo hadi katika kona ya barabara
iendayo makutano ya barabara ya sokoine ,hapo
alikata kona upande wa kulia kuelekea yalipo
makutano ya barabara hiyo na ya Sokoine. Alipofika
makutano ya barabara za Sokoine na Jamhuri
alinyoosha moja kwa moja kuifuata barabara ya
Jamhuri kwa mwendo wa kasi hadi yalipo makutano
ya Barabara ya Barongo na Jamhuri, hapo
alipunguza mwendo kisha akavuka makutano hayo
kwa mwendo wa wastani halafu akanyoosha moja
kwa moja kuifuata tena barabara ya Jamhuri hadi
zilipo ofisi za CCM hapo aliegesha gari kisha
akateremka akimuacha Norbert ndani ya gari .
Alirudi baada ya dakika kadhaa akiwa na pakiti ya
konyagi akiinywa mdomoni kisha akapanda kwa ajili
ya kuliondoa gari eneo hilo.
"kaka hiyo si pombe na unaendesha gari, hivi si
hatari hiyo?" Norbert alimuuliza
"usijali kaka kuhusu hii kwani bila hii mimi siwezi
kuendeshagari vizuri" Dereva alijibu huku akiweka
gia kuingia barabarani
"ok ni sawa tu tuendelee na safari" Norbert aliongea
kwa mara ya mwisho kisha akakaa kimya kumuacha
dereva aendelee na kazi yake . Dereva aliendelea na
makeke yake ya kuendesha gari huku mkono mmoja
akinywa kipakiti cha konyagi hadi akakimaliza,
alinyoosha barabara ya Jamhuri hadi katika
makutano ya barabara hiyo na barabara ya
Aerodrome.
Alinyoosha barabara hiyo hadi karibu na uwanja wa
ndege wa bukoba kisha akaweka gari pembeni
baada ya kupokea amri kutoka kwa Norbert, Norbert
alishuka hapo kisha akampatia malipo dereva huyo
kama walivyokubaliana. Dereva wa gari aligeuza
kisha akaondoka eneo hilo na Norbert akaelekea katika
ofisi za uwanja wa ndege wa Bukoba kwa miguu.
Baada ya muda mfupi alifika ofisi za uwanja wa
ndege huo kisha akaenda hadi mapokezi. Hapo
mapokezi alimkuta msichana aliyekuwa akiongea na
mgeni, alisubiri hadi alipomaliza kuongea na mgeni
ambaye alionekana ni mteja kisha akamfuata katika
dawati la mapokezi. Alimshika kidevu kwa namna ya
uchokozi.
"we mwanaume wewe naona umetoka kwa mke
mwenzangu" Msichana wa mapokezi alianza
kumtania Norbert pasipo salamu baada ya
kuchezewa kidevu
"aah! bibie mi kijana sasa ulitaka niende wapi"
Nobert aliongea kwa sauti ndogo huku akiwa
ameegemea meza.
"khaa! Yaani umeniacha mimi unaenda kwa bibi
mwingine, muone hutulii kama jogoo" Msichana wa
mapokezi akiongea huku akiwa ameuvuta mdomo
kwa namna ya kudeka.
"bibie usinune basi utasababisha na mimi ninune,
kumbuka ukitabasamu na mimi ndiyo nitatabasamu.
Nilikuwa kikazi zaidi mama" Norbert aliongea ili
kumfanya msichana huyo atabasamu, msichana
huyo alipotabasamu alimwambia "Frida nipe basi
niwahi maana muda ndio huu". Frida aliingiza
mikono chini ya meza ya mapokezi baada ya
kuambiwa hivyo, alitoa tikiti moja ya ndege ya
fastjet kisha akampatia Norbert.
"watu wameshaanza kuingia Nor, hebu wahi" Fridah
alimwambia Norbert
"haya bibie nikirudi jiandae maana nitapeleka posa
kwenu" Norbert aliongea akiwa anaelekea ndani ya
uwanja.
"nyooo lione vile na ukapera umwachie nani" Fridah
alimsindikiza na maneno hayo huku akiwa
amebinua mdomo.
****
SHULE YA NEEMA TRUST
"Soil Colloids, the colloidal state refers to a two-
phase system in
which one material in a very finely divided state is
dispersed through second phase.
The examples are:
Solid in liquid - Clay in water (dispersion of clay in
water)
Liquid in gas -Fog or clouds in atmosphere
The clay fraction of the soil contains particles less
than 0.002 mm in size. Particles less than 0.001
mm size possess colloidal properties and are
known as soil colloids. There are ten properties of
soil colloids, anyone can mention them?" Dkt
Jameson alitiririka katika kufundisha katika darasa la
kombi ya PCB kidato cha sita kwa mara ya kwanza toka
alipotambulishwa kwa wanafunzi asubuhi ya siku
hiyo, aliuliza swali na kupelekea darasa zima libaki
na mwanafunzi mmoja tu ndiye aliyenyoosha
mkono.
" your name please(jina lsko tafadhali)" Dkt
Jamesom alimwambia mwanafunzi huyo.
"Moses Gawaza" Mwanafunzi huyo alitaja jina lake.
"ok you can continue(sawa unaweza ukaendelea)
Dkt Jameson alimwambia
"The properties of Soil colloids are size, surface
area, surface charges, absorption cation, absorption
of water,cohesion,adhesion,sw elling and shrinkage,
dispersion and floculation, brownian movement and
non permeabilitiy" Moses alitiririka kisha akaketi
kwenye meza yake alipomaliza.
"very good, clap your hands for him(vizuri
sana,mpigieni makofi )" Dkt Jameson aliongea akiwa
na tabasamu pana usoni mwake na kupelekea wanafunzi wote wapige makofi
"Iam hope you know the general properties of Soil
colloids through Mr Gawaza, lets continue in details (natumai
mnajua sifa kuu za Soil colloids kupitia kwa bwana Gawaza tuendelee kiupana).
Size: The most important common property of
inorganic and organic colloids is their extremely
small size. They are too small to be seen with an
ordinary light microscope. Only with an electron
microscope they can be seen. Most are smaller
than 2 micrometers in diameter...." Dkt Jameson
aliendelea kutiririka ili wanafunzi wake wamuelewe.
Hadi kipindi kinaisha tayari muda wa kutoka
shuleni hapo ulikuwa unakaribia, wanafunzi wote
walifurahia sana kipindi cha Dkt Jameson
kilichowafanya waelewe mambo mengi katika somo
la Kemia. Dkt Jameson alimuita Moses baada ya
kumaliza kufundisha kisha akaelekea ofisini, Moses
alitoka kwenda kuelekea ofisini alipoitwa na Dkt
Jameson.
"kaa kwenye kiti Gawaza" DKt Jameson alimwambia
Moses alipoingia ofisini kisha akainuka akiwa
ameshika faili akielekea kwenye makabati ya mafaili
halafu. Aliweka faili kwenye kabati halafu akarejea.
"ndio mwalimu" Moses aliitikia wito.
"unaweza ukaniita kakaJameson kwani mimi ni
kijana kama wewe tu isipokuwa nimekuzidi kielimu
tu" Dkt Jameson alikataa kuitwa kwawadhifa
aliostahiki.
"ndii kaka Jameson" Moses akasema.
"Gawaza najua wewe ni mwanafunzi mwerevu sana
na unajua vitu vingi ambavyo baadhi ya wenzako
hawavijui, sasa kwanini usiwe unawaelekeza
iliwaelewe kama wewe"
"ujue mimi najua kidogo tu na katika hicho kidogo
huwa namfanya mwenzangu atakaye kukijua ili
akijue. Hivyo suala la mimi kuwaelekeza wenzangu
najitahidi ingawa kuna wengine hawataki
kuelekezwa".
"vizuri sana hivi huwa unasoma masomi ya ziada
sehemu? kama unasoma basi hakikisha na wenzako
wanapajua ili wakasome"
"sisomi masomo ya ziada popote ila nilikuwa
ninafundishwa na baba yangu mzazi ambaye kwa
sasa ni marehemu".
"ooh! Pole sana kwa hilo, je baba yako naye alikuwa
mwalimu?"
"hapana hakuwa mwalimu bali alikuwa ni
mwanasayansi maarufu"
"mwanasayansi?! Nawajua wanasayansi wa karibia
bara zima la Africa,jina lake ni nani?"
" Professa Lawrence Gawaza"
"sawa nishamtambua, alikuwa ni mmoja wa
maprofessa wa chuo cha Havard na aliacha kazi
akarejea Tanzania kuendelea na shughuli zake
binafsi. Unaonekana una kipawa kama cha baba
yako, jitahidi utakuwa kama yeye. Ni hayo tu
unawezaa ukarudi darasani".
"sawa kaka asante"
Moses alinyanyuka kwenye halafu akapeana mkono
na Dkt Jameson kisha akaondoka kuelekea darasani.
Muda wa kutoka ulipofika Beatrice alikuja darasani kwa akina Moses
akiwa na bahasha mkononi mwake, alienda hadi
alipo Moses kisha akachukua kiti kilicho jirani
akaketi.
"mambo" alimsabahi Moses
"poa, za masomo" Moses aliitikia salamu akiwa
ametabasamu.
"safi tu, niambie msongolisti wangu" Beatrice
alitumbukiza utani
"nikuambie nini mlimbwende cha zaidi, au nikutolee
mambo ya electric potential sasa hivi" Mosea
alitumbukiza utani na kupelekea Beatrice acheke.
"unataka kunipasua kichwa nini yaani hiyo History ni
janga kwangu" Beatrice alisema huku akimpatia
bahasha Moses halafu akamwambia "ni kadi hii
kesho njoo nyumbani tafadhali ni sherehe yangu ya
kuzaliwa".
"usijali nitakuja maana si jumamosi, tarajia ugeni
wangu Bite"
"sawa leo ninaondoka na gari ya dady maana
amenifuata yupo nje, inabidi nikuage kwa namna
ninayopenda kama hutojali"
"ok niage basi upendevyo Bite".
"waao! simama basi".
Moses alisimama akijua anaagwa kwa namna ya
kawaida tu, akiwa amesimama alishtuka akiwa
amekumbatiwa na Beatrice. Ulaini wa mwili wa
Beatrice na joto lake ulimfanya ajihisi amepigwa
shoti ya ajabu mwilini mwake, Beatrice alimbusu
Moses shavuni kisha akaondoka huku akisema "bye
bye".
Moses alibaki ameduwaa akimtazama Beatrice
aliyekuwa akiondoka, Bratrice alipopotea katika upeo
wa macho yake alibaki akiwa ameduwaa kwa
kilichotokea.
"we boya bisha tena nikuone,changamkia tenda
hiyo" Sauti ya Hillary ilisikika kutoka nyuma yake na
kupelekea akurupuke kwenye mawazo.
"yaani mtoto anajilenga mwenyewe we unashindwa
kumaliza" Hillary aliendelea kumlaumu Moses.
"naona leo umeamua uniaibishe" Moses alimwambia
"nikuaibishe kwa lipi wakati wote wamesepa" Hillary
alimwambia Moses. Moses aliangalia darasa zima
na kukuta darasa lote ni tupu na wao wawili tu ndio
waliobaki.
"daah! Nilijua kuna wanga wananichora" Moses
aliongea huku akichukua begi lake la vitabu.
"wacha uoga wewe ,naona kakupatia barua kabisa"
Hillary alimwambia
"ni kadi tu ya mwaliko"
"poa tusepe kama vipi".
Walitoka humo darasani wakiwa wanaongea mambo
yao mbalimbali, utani kwa marafiki hawa ilikuwa ni
kitu cha kawaida sana.

of water,cohesion,adhesion,sw

Tuesday, December 8, 2015
SHUJAA SEHEMU YA NNE
RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843...
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGI

MASAA MAWILI BAADAE
KWENYE MBUGA YA KENYA WILD IMPALA
Mbuga hii iliyo jirani iliyo jirani na ziwa Victoria
kulikuwa na na handaki kubwa sana lililochimbwa
kilomita mbili kutoka ziwani, ndani ya Handaki hilo
kulikuwa na kundi la watu takribani sita wenye asili
ya barani Ulaya. Watu hao walikuwa wameizunguka
meza kubwa ya duara iliyotengenezwa kwa chuma,
meza hiyo ilikuwana urefu uliowafikia kiunoni mwao,
katikati ya meza hiyo kulikuwa na karatasi kubwa
lilioenea karibu meza nzima.
"nafikiri tutumie boti yenye uwezo wa kuzama kama
ilivyo Nyambizi" aliongea Obren ambaye alikuwa ni
mmoja kati ya watu waliokuwa wapo eneo hilo.
"ni njia sana nzuri, sasa tukatokee sehemu gani
iliyokuwa salama" aliongea mzungu mwingine kisha
akauliza swali.
" Calvin mbona rahisi hiyo, tutapita chini kwa chini
hadi katika pori la Rubondo lililopo katika kisiwa cha
Rubondo kisha hapo tutafanya mapumziko ya muda
kisha tutaendelea hadi Kagera" Campbel alijibu swali
hilo huku akielekeza kwenye ramani sehemu
wanazopitia.
"njia nzuri hiyo nadhani ramani itatusaidia kufika"
alisema Calvin
"ndio inasaidia na tukifika huko tutachukuliwa na
helikopta hadi kibaha halafu hapo tutakutana na
Tasi" aliongea Campbel.
"Obren, Calvin, Scott , Jameson na Christian
nadhani tupo pamoja sasa team mambas tuingie.
kazi!" alihitimisha Campbel kisha akanyoosha ngumi
mbele na kupelekea wenzake wote wanyooshe
ngumi na kukutanisha ngumi ya Campbel.
"kazii!" wote waliitikia kwa pamoja kisha wakatoka
kwenda kuchukua vitu vyao vya muhimu
ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI
YAKE
SEHEMU YA NNE
Baada ya dakika kadhaa wote walirejea wakiwa
wamevaa mabegi ya mgongoni yenye rangi ya kahawia,
wote walielekea kwenye ngazi zilizopo ndani ya
handaki hilo zilizowapeleka mpaka sehemu yenye
bwawa kubwa lililotengenezwa kwa namna ya
kuvutia. Ndani ya bwawa hilo kulikuwa kuna boti ya
kisasa yenye rangi ya kijani ikiwa imeegeshwa
pembezoni mwa bwawa hilo, hadi muda huo tayari
walikuwa wameshafika jirani na boti hiyo ili
kujiandaa kuingia ndani yake. Waliingia kwa pamoja
ndani ya boti hiyo kisha wakaenda kuketi kwenye
viti vilivyomo humo ndani.
"anza safari" Campbel alimwambia nahodha wa boti
hiyo aliyekuwa yupo katika usukani mbele yao.
Nahodha wa boti hiyo alibonyeza kimojawao
miongoni mwa vitufe vingi vilivyopo mbele yake na
kupelekea boti hiyo ijifunike huku umbo lake likiwa
kama yai , alibonyeza tena kitufe kingine kisha
akashikilia usukani wa boti hiyo kwa mikono miwili. Boti
ilizama ndani ya bwawa hilo kuelekea chini kabisa
hadi lilipofika usawa wa bomba kubwa la duara
lenye uwezo wa kupitisha boti hiyo ambayo sasa ipo
katika umbile la nyambizi ya kivita ingawa ina umbo
dogo. Walipita ndani ya bomba hilo hadi kwenye mlango
wa kioo kuashiria ni mwisho wa bomba hilo. Hapo
nahodha alichukua simu ya kijeshi kisha akasema
"Captain B45 hapa. Tupo kwenye mlango, ninahitaji
ufunguliwe tupite". Alipomaliza kuongea alirudisha
simu sehemu yake kisha akashika kwa mkono
mmoja kwa nguvu huku mkono mwingine ukiwa
umeshika chuma kilicho na umbo kama gia ya gari.
Mlango wa kioo uliokuwa mbele yao ulifunguka
kupelekea maji yaingie huku nyuma ya boti hiyo
kukitokea kioo kingine kama cha awali kuzuia maji
yasiingie kwenye handaki, yule nahodha alisukuma
kile chuma kilicho na umbo kama gia ya gari na
kupelekea boti hiyo ianze kwenda kwa mwendo wa
kasi. Akiwa anatumia ramani iliyopo kwenye kioo
kilichopo chini ya usukani pamoja na dira iliyopo
mbele yake, aliweza kukiongoza chombo kuelekea
kusini magharibi mwa eneo walilolopo. Mwendokasi
wa boti hiyo uliwafanya wote waliomo humo ndani
watulie kutokana na kona kali zilizokuwa zikikatwa
na nahodha ili kukwepa miamba iliyomo ziwani.
Nahodha ilimbidi afanye kazi ya ziada katika
kucheza na usukani wa boti hiyo, hadi wanafika
kisiwa cha Rubondo tayari ilikuwa usiku wa manane
hivyo iliwalazimu kuinua boti juu ili wapumzike kwa
muda mfupi kisha waendelee.Waliifungua boti hiyi
ikawa wazi baada ya kuinua juu.
"kwanini tusiende kwenye kingo ya ziwa ile pale
tuka tukapumzike" aliongea Calvin huku akisimama
kwenye kiti chake baada ya kufungua mkanda
"unataka ufanywe kitoweo sio?" aliuliza Nahodha wa
boti hiyo.
"kivipi nahodha?" Calvin naye aliuliza
"hii sio bahari rafiki bali ni ziwa na kuna mamba
pembezoni mwake, sasa ukienda kule unajitafutia
kifo kwani wanakaa pembezoni" Nahodha wa
chombo chao alifafanua
"aaah! nafikiri ni kiumbe kidogo na hakitaweza
kushindana nguvu na mimi" Calvin aliongea kwa
dharau.
"rafiki ukae ukijua mamba wa pale ni wakubwa na
wenye uzito mkubwa sana, sasa suala kushindana
nao nguvu usijidanganye kabisa" Nahodha
alimwambia
"huyo hajui mamba zaidi ya kuwaona kwenye zoo
kawazoea kenge wa majini" Obren aliongea
kimasihara huku akicheka.
"ujue mamba wa humu ziwani wanafika urefu mita
sita na uzito wa tani moja, sasa kama unaweza
kushindana nao nguvu nikupe boti ndogo ya kujaza
na upepo uende" Nahodha alisema.
"aisee hao mamba wa Afrika kama ndio wapo hivyo
basi siendi, tupumzike hapahapa" Calvin kwa upole
huku akirudi kwenye kiti chake baada ya kusimama
kwa muda mrefu.
"sio mamba wa Afrika tu ndio wapo hivyo hata wa
dunia nzima ni wakubwa na uliowaona wewe ni
watoto, ushawahi kusikia ukubwa wa mamba aitwae
Lolong wa Ufilipino?" aliyepo jirani yake alimwambia
"ujue Scott yule mamba waliomkamata Wafilipino
nilijua ni wa uongo" Calvin alimwambia Scott
"sasa ndiyo ujue kuwa yule mamba ni wa ukweli na
haikuwahi kuonekana mamba mkubwa namna ile
kwa mujibu wa watafiti wa mambo ya wanyama"
Campbel naye alimwambia Calvin.
Walipumzika kwa
muda wa nusu saa huku
wakijadiliana mambo mabalimbali, mapumziko
yalipoisha nahodha alibonyeza kitufe na kupelekea
boti ijifunge kama awali kisha akawageukia wakina
Campbel.
"mikanda ni muhimu jamani" aliwaambia kisha
akabonyeza kitufe kingine na kupelekea boti hiyo
ianze kuzama taratibu, alikipeleka mbele kile chuma
kilicho na umbo kama gia ya gari. Boti ilianza
kwenda kwa mwendo mkubwa kama awali na
nahodha wake alizidi kuongeza umakini kuliko awali,
eneo lenye mawe mengi ndani ya ziwa hilo ndio
waliloingia na kupelekea nahodha akate kona kila
mara kuyakwepa mawe hayo. Hadi saa tisa usiku
inaingia tayari walikuwa wameshawasili Kagera
katika hifadhi ya Biharamulo iliyopo pembezoni mwa
ziwa Viktoria, kwa umbali wa mita kadhaa toka
kwenye kingo ya ziwa hilo kulikuwa na helikopta
kubwa ya kisasa aina ya AW139SAR ikiwa
imeegeshwa sehemu tambarare. Boti hiyo iliibuka
juu ya maji pembezoni mwa ziwa kisha ikajifuungua
halafu ikasogea hadi kando kabisa jirani na nchi
kavu, Campbel,Obren,Calvin,James
Christian
ndiyo walioruka hadi nchi kavu kwa ukakamavu
huku nahodha akiwa amebaki ndani ya boti.
Kikosi hiki cha watu sita kilikimbia hadi ilipo
helikopta kisha kikaingia ndani pamoja na mizigo
yao, nahodha wa boti aliishia hapo kama wajibu
wake ulivyomtaka. Aliifunika boti halafu akaizamisha
ndani ya maji kama awali kisha akaondoka eneo
hilo, eneo ambalo boti hiyo iliibuka lilibaki tulivu
kama hakuna jambo lolote lilitokea.
"fungeni mikanda tafadhali" Rubani wa helikopta
aliwaambia vijana wa kazi aliotumwa kuja
kuwachukua ambao nao walitii bila kuweka walakini
wowote. Rubani alikinyanyua chombo chake kama
alivyotakiwa kufanya kisha akakiongoza kuelekea
mahali kilipotakiwa kuelekea, njiani watu wote
walikuwa kimya kusubiri mwisho wa safari ili
washuke. Mnamo alfajiri saa kumi na moja kasoro
helikopta hiyo iliwasili katika uwanja wa mpira
uliopo jirani na shule ya msingi iliyopo maeneo ya
kibaha, pembezoni mwa uwanja huo kulikuwa kuna
gari aina ya AUDI Q8 ikiwa imeegeshwa kwenye
kivuli cha mti wa mwembe. Pembeni ya mwembe
huo kulikuwa na range rover ya rangi ya kijivu.
Helikopta hiyo ilitua katika uwanja huo kisha milango
yake ikafunguliwa baada ya upanga wake kuacha
kuzunguka toka ilipozimwa, vijana sita wa kazi
walishuka wakakutana na Tasi akiwa amesimama
katika uwanja huo akiwasubiri
"karibuni" Tasi aliwaambia huku akiwapa mkono kila
mmoja.
"tushakaribia" Calvin aliongea kwa niaba ya
wenzake. Wote waliondoka hadi yalipoegeshwa
magari yaliyo jirani na uwanja huo kisha wakaingia
kwenye magari hayo, Tasi aliingia kwenye gari aina
ya AUDI Q8 akiwa na Campbel, Obren na Calvin
huku Jameson, Christian na Scott wakiingia kwenye
range rover wakiwa pamoja na dereva aliyekuja na
Tasi.
Msafara wa magari hayo mawili uliondoka uwanjani
hapo baada ya Helikopta iliyotua hapo uwanjani
kuondoka, msafara huu uliingia barabara ya
Morogoro kwa mwendo wa kasi ukielekea katikati ya
jiji.
****
Mnamo saa kumi na moja na nusu alfajiri Moses
alishtuka usingizini kama ilivyo kawaida yake,
aliinuka kitandani halafu akaelekea kwenye mahali
ilipo maliwato ndani ya chumba chake. Huko
alijisafisha vizuri kisha akatoka halafu akafanya
maandalizi kwa ajili ya shule, alipomaliza alitoka
hadi nje kwenye eneo la maegesho ya magari.
Aliingia kwenye gari analotumia kila siku kisha
akaliwasha, aliweka gia taratibu kisha akaachia breki
na kupelekea gari lianze kujongea kuelekea geti ambapo mlinzi tayari alikuwa ameshafungua geti ili
kuruhusu gari, akiwa amesimama pembeni ya geti
kama ilivyo kawaida yake.
"niaje kaka?" Moses alimsabahi mlinzi baada ya
kusimamisha gari alipofika usawa wa getini.
"poa dogo, za asubuhi?" Mlinzi aliitikia salamu huku
akimjulia hali.
"salama tu, hivi anko Kenne katoka saa ngapi
maana nimeona gari moja halipo"
"ametoka mida ya saa kumi alfajiri" Mlinzi alijibu.
"hakukwambia anapoenda"
"ameniambia anaelekea kazini kapata dharura"
"sawa kaka, wacha mi niwahi shule"
"poa dogo".
Moses aliondoa gari kwa mwendo wa kasi akielekea
barabara iendayo mtaa wa Warioba baada ya
kuagana na mlinzi wa nyumbani kwao..
****
Saa moja na nusu asubuhi walimu na wanafunzi wote wa shule ya Neema trust
walikuwa wamekusanyika katika eneo maalum la
kukusanyika wanafunzi kila siku asubuhi, haikuwa
kawaida kwa walimu wote kukusanyika hapo ifikapo
muda wa mstarini zaidi ya walimu wa zamu tu. Siku
hiyo shule nzuma ilikuwepo hapo kuashiria kuna
jambo muhimu na mkuu wa shule alikuwepo pia,
ratiba ya kila siku ya mstarini ilianza kisha mkuu wa
shule akasimama kuzunguka na wanafunzi wote.
"habari za asubuhi wanafunzi......natumaini wote
mmeamka salama na mpo na afya njema kama ilivyo
kawaida, dhumuni la kuwaita hapa ni kuwajulisha
juu ya ujio wa mwalimu mpya wa masomo ya Kemia
katika shule mwenye utaalamu wa hali ya juu katika
ufundishaji kutoka nchini Uingereza. Mwalimu huyu
atakuwa pamoja nanyi katika masomo hayo kwa
vidato vya nne, tano na sita kwa muda huu ambao
mwalimu wenu wa Kemia atakuwa likizo baada ya
kupata matatizo ya kifamilia. Napenda nimkaribishe
kwenu Dokta Jameson Share" alihitimisha mkuu wa
shule huku Dkt Jameson akisogea kusalimiana na
wanafunzi.
"habari za asubuhi wanafunzi na vijana wenzangu
kama mimi...........naitwa Dkt Jameson Share
nitakuwa nanyi katika masomo ya kemia katika
kidato vilivyotajwa na mkuu wa shule, hivyo
naombeni ushirikiano wenu kama wanafunzi" Dkt
Jameson alihitimisha na kupeleka shule nzima ipige
makofi.
Wanafunzi wote walitawanyika baada ya taratibu
zingine za hapo mstarini kuisha, waliingia
madarasani moja kwa moja kusubiri vipindi vianze.
****
Norbert Kaila ni mwandishi mashuhuri wa habari wa
nchini Tanzania pia ni mpelelezi wa shirika la EASA
(East Africa Security Agency) la Afrika ya mashariki,
kijana huyu alikuwa yupo katika pori la Hifadhi ya
Biharamulo kwa siku tatu zilizopita akifanya utafiti
kama mwandishi wa habari juu ya pori hilo. Kwa
muda wa siku tatu hizo alikuwa anaishi ndani ya
hema akiwa na askari mmoja aliyepewa na ofisi za
wanyama pori zilizo jirani na Hifadhi hiyo. Usiku uliopita
akiwa amelala katika hema lake alishtuliwa na ujio
wa helikopta katika pori hilo, ujio wa helikopta hiyo
ulimpa hamasa ya kutaka kujua ni nini kinaendelea.
Hivyo alitoka katika lake lilipo umbali wa mita
takribani mia tatu toka ilipo helikopta hiyo. Alitembea
kwa tahadhari hadi katikati ya miti iliyo jirani na
eneo hilo akiwa na kamera yake ya kipelelezi tofauti
na kamera yake ya kawaida. Ajibanza
hapo hadi aliposhudia ujio wa boti mfano wa
nyambizi iliyofika hadi ukingoni, hadi hapo aliweza kuoiga
picha kila anachokiona kwa msaada wa mwangaza
uliotoka katika taa ya helikopta na taa ya boti. Hadi
watu sita wanashuka kwenye boti ile alikuwa
amewaona na amewapiga picha, boti hiyo pia
alikuwa ameiona na ameipiga picha pia na helikopta
aliipiga vizuri akilenga namba zake zilizopo ubavuni.
Alipomaliza alibaki palepale hadi walipoingia ndani
ya helikopta kuondoka, na ile boti ilipozama chini.
Hapo alirudi kwenye hema kisha akajilaza pembeni
ya msimamizi wake kama ilivyokuwa awali. Hadi
asubuhi inaingia alikuwa macho na jua
lilipochomoza alikusanya vitu vyake kisha
akaondoka porini hapo akiwa na msaidizi aliyepewa.
MZEE WA KAZI KAZINI
ITAENDELEA!!
Monday, December 7, 2015
SHUJAA SEHEMU YA TATU
RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII KWA MARA NYINGINE
ANGALIZO: KAZI YA RIWAYA HII YA KISWAHILI NI KUELIMISHA NA KUENDELEZA KISWAHILI. NDIO MAANA NIMETUMIA KISWAHILI SEHEMU WANAPOZUNGUMZA WAGENI ILI NIENDANE NA JAMII WANAYOSOMA, BAADHI YA MANENO YA KINGEREZA YAMETUMIKA KUAKISI JAMII YA SASA ISIVYOTHAMINI LUGHA YA TAIFA
ILIPOISHIA
Siku iliyofuata Beatrice aliwahi kantini baada ya tu
ya kusikia kengele ya mapumziko, alikaa katika kiti
kilicho mkabala na kiti anachokalia Moses kila siku .
Baada ya muda Moses alifika hapo kantini akiwa
amebeba vitabu mkononi, alienda hadi kwenye kiti
anachokitumia siku na kumkuta Beatrice akiwa
tayari keshawasili eneo hilo. Aliweka vitabu na
kumsabahi
"mambo Bite" ha lafu akavuta kiti na kuketi, Beatrice
alimjibu, "safi tu upo poa?". Alivuta kiti na kuketi
kisha akasema "nipo poa, naona leo umeniwahi" ,
kauli hiyo
ilimfanya Beatrice atabasamu pasipo kusema lolote
huku akimtazama Moses.
ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI
YAKE
SEHEMU YA TATU
Moses aliinuka na kwenda kuagiza kifungua kinywa
kisha akarejea kitini, alimtazama Beatrice na
kumuambia, "mbona leo mtulivu hivyo kuliko
kawaida?". Beatrice akamwambia, "walaa nipo
kawaida siku zote ila sitaki kuongea sana kama kila
siku".
Moses akauliza, "mmmh! kwanini?"
"we unataka nipaliwe kama jana" Beatrice akaongea
kwa sauti yenye mchanganyiko wa deko na
kusababusha Moses acheke. Hakika kiliwazo kingine
kwa Beatrice baada ya kumuona mvulana
anayempenda akicheka, alitokea kupenda karibu kila
kitu cha Moses kasoro huzuni yake.
"na wewe umezidi" Moses aliongea huku akicheka
"na wewe bwana hebu acha hayo, hivi jana ulitaka
kuniambia nini?"
"ohoo! Halafu nilitaka nisahau"
"tell me now(niambie sasa)"
Moses alimuashiria Beatrice angoje kwanza muda
huo alikuwa na anatafuna kitafunwa mdomoni,
alimeza kisha akapika funda moja la chai.
Alipolimeza akasema, "Beatrice najua umejua
umetokea kuwa rafiki yangu mkubwa kwa muda
mfupi tu toka tulipoanza kuwa marafiki", aliposema
hivyo akajiweka vizuri kwenye kiti kisha akaendelea,
"sasa basi nataka unisaidie jambo moja tu kama
utaweza".
"Jambo gani hilo Mose?"
"relax Bite ndio ninakwambia sasa"
"sawa Iam listening you(ninakusikiliza)"
"najua unajua ni kiasi gani nimekuwa nikisumbuliwa
na mdada mwenye kujiita Dream girl, sasa nataka
unisaidie katika kumpata huyu mdada maana
nimechoshwa na tabia yake ya usumbufu"
"sasa hapo how can i help(nitawezaje kusaidia) maana hata huyo mdada
hata mimi simjui"
"I know its hard but try (najua ni ngumu lakini jaribu)ikiwa unanipenda
unanipenda mimi kama rafiki yako"
"mmh! Kusema kweli unanipa majaribu"
"unapenda kuniona nikiwa nina furaha"
"Yeah! Napenda kukuona ukiona ukiwa na furaha"
"please help me(please help me) kama unapenda kuniona nina furaha".
Beatrice allijifikiria kwa muda kisha akasema, "ok I
will try(saa nitajaribu)". Kauli hiyo ikimfanya Moses atabasamu
huku akisema "ukifanikiwa nitakupa zawadi yoyote
uitakayo". Waliendelea kunywa chai hadi muda
wakamaliza kabla ya muda wa mapumziko
haujaisha, waliendelea kuongea mambo mengine ya
kawaida huku Beatrice akiwa ni mwenye furaha
muda wote kama ilivyo kawaida yake. Hatimaye
kengele ya kurudi darasani ikagongwa, wote
walinyanyuka na kuondoka kurudi darasani.
Walitembea hadi sehemu ambayo kila mtu
anatakiwa kuelekea mahali yalipo madarasa yao ,
hapo Beatrice akamwambia Moses, "tuonane muda
wa kutoka kama hutakuwa na nafasi". Moses
alimuonesha ishara ya dole gumba ya kukubaliana
na jambo alilolisema, Moses akiwa na vitabu vyake
mkononi aliamua kuelekea darasani kwao moja kwa
moja. Siku hiyo Moses alijikuta akiwa na hisia za
ghafla juu ya Janet, kila akimfikiria alitamani kuwa
naye karibu zaidi. Akiwa darasani baada ya kipindi
cha kwanza baada ya mapumziko kuisha alijikuta
akimuuliza rafiki yake kipenzi humo darasani kwao,
" Hilary umemuona yule demu niliyekuwa nae
kantini?"
"ndiyo si Beatrice au kuna mwingine?" Hilary alijibu
na kuuliza swali papo hapo.
"unamuonaje?" Moses alimuuliza Hilary.
"aisee yupo poa sana, tena kazama kwako au
hujashtuka?"
"wala hamna kitu kama hicho"
"Mose wa wapi wewe yaani kukaa naye huko kote
bado hujajua"
"hamna hicho kitu wewe punguza fikra zako"
"ok tuache hayo, kwanini umeniuliza hivyo?"
"uongo dhambi ndugu, nahisi kumuhitaji baada ya
necta kuisha?"
"aisee leo umekuwa vipi? maana sio kawaida yako"
"Acha udaku we mwanga, mengine yakaushie tu".
Kauli hiyo ilimfanya Hillary acheke sana huku
akisema, "maajabu ya daunia msongolisti kanasa
leo". Moses naye alijikuta akicheka kwa kauli ya
utani aliyoitoa Hilary.
"haya msongolisti mgoni tupige msuli sasa nahisi
ticha haingii huyu" Moses naye akatumbukiza utani
huku akifungua daftari lake lililopo juu ya meza.
Muda wa kutoka ulipofika Moses na Beatrice
walikutana pale walipoachana awali, siku hiyo
Beatrice alitaka waondoke pamoha na Moses. Moses
akiwa na usafiri wake aliokuja nao alikubali pasipo
kuweka walakini wa aina yoyore, alimfungulia
mlango wa gari na kumruhusu kama malkia wake.
"mmh na wewe bwana kwa mbwembwe" aliongea
Beatrice baada ya kuona Moses amemfungulia
mlango kama kijakazi afanyavyo kwa malkia.
"sasa mgeni akiingia kwenye mali ya mwenyeji
lazima anyenyekewe" Moses alitetea kitendo chake
cha kumfungulia mlango Beatrice. Baada ya Beatrice
kuingia ndani ya gari naye alizunguka upande wa
dereva kisha akamuuliza Beatrice, "nikuache wapi?".
Beatrice akajibu pasipo kumuangalia Moses
"mikocheni kama unaelekea huko". Kauli hiyo
ilimfanya Moses atabasamu baada ya kubaini
wanaelekea sehemu moja, aliwasha gari kisha akaendesha kuelekea getini kisha akatoka na kuingia
barabarani kisha akaliondoa kwa mwendo wa kasi.
Baada ya dakika takribani thelathini walikuwa
wamefika mikocheni katika mtaa wa Warioba
sehemu ambapo kuna barabara iendayo mtaa wa
mazinde, Beatrice aliomba kushushwa
njiani, "kwanini nisikupeleke hadi kwenu?" Moses
aliuliza.
"usijali hapa panatosha tu" Beatrice aliongea akiwa
tayari ameshafungua mlango wa gari baada ya
Moses kusimamisha gari.
"Moses usijali nimefuatwa na gari na dereva yule
pale" Bearice aliongea huku akionesha kwa kidole
upande wa pili wa barabara jirani na waliposimama.
Moses alipotazama pembeni ya barabara aliona gari
aina ya Toyota landcruiser V8 ikiwa imeegeshwa
pembezoni mwa barabara mkabala na alipoegesha
gari lake. Hadi muda huo Beatrice alikuwa tayari
ameshashuka garini na sasa alikuwa akivuka
barabara huku akimpungia mkono Moses, baada ya
Beatrice kuingia katika gari lililomfuata Moses
aliondoa mguu wake kwenye breki kisha akakanyaga mwendo
na kupelekea gari ianze kuondoka taratibu. Allikata
kona kuingia njia iendayo mtaa wa Mazinde ambapo
ndio anaishi, alinyoosha barabara moja kwa moja hiyo moja
mwa umbali mrefu kiasi kisha akakata kushoto
kuingia mtaa wa mazinde halafu akaelekea moja
kwa moja hadi kwenye geti la nyumbani kwao
****
JIJINI KISUMU
NCHINI KENYA
Ndani ya klabu ya hoteli ya Sunset pembezoni mwa
mji huo upande wa magharibi wa nchi hiyo, ndani
ya hoteli hiyo ya nyota tatu kulikuwa na mkutano
mkubwa wa watu wenye maslahi ya aina moja.
Brian, kundi la wazungu wenzake ndio wahudhuriaji
wa mkutano huo wenye. Msemaji wa kikao hicho
alikuwa ni Brian ambaye alifungua kikao hicho kwa
kusema, "habari za jioni ,natumai kila mmoja wetu ni
mzima wa afya na ameitikia wito wa mkutano huu
wa siri wa umoja wetu kwa kujua lengo la mkutano
huu. Pia nadhani ni muda muafaka kwa sisi
tuunyamzishe umoja wa Ulaya ambao umekuwa
kikwazo katika biashara yetu inayotuweka mjini na
inayotuwezesha sisi kuendesha biashara zetu
nyingine, nadhani nyote mnajua kwamba tulimtuma
Tasi akachukue virusi kwa namna yoyote baada ya Professa
kugoma kufanya biashara nami" alinyamaza kwa
muda kisha akanyanyua bilauri ya pombe iliyopo mezani
halafu akapiga funda moja.
"Professa huyu aligoma baada ya kusikia kuwa nina
mpango wa kuvijaribu nchini Tanzania kwenye
makazi yake na ambapo anapatikana mwanae
kipenzi, kutokana na ukaidi sisi tukamwambia
atumie mbinu mbadala ili aweze kutupatia bure
maana mwanzo aligoma kutupatia kwa malipo. Tasu
alifanikiwa kumchoma Professa sindano ya sumu
inayoua taratibu ambayo hadi inamuua hakuwa
ametupatia virusi hao, dawa ya sumu hiyo tulikuwa
tunayo na ikatulazimu tumwambie atapata dawa
kama akileta virusi mikononi mwetu. Yote hayo
bado Professa alikaidi na akaishia kusema ipo
mikononi kwa mtu wake anaemuamini na
hatutowapata, hivyo basi hayo ndio maneno
aliyotuchia yenye ukaidi. Sasa nataka nisikilize
mawazo yenu kila mmoja ili tuweze kupata njia
mbadala" alihitimisha kisha akawatazama
wahudhuriaji wa mkutano huo kila mmoja. Mmoja
wa wazungu alinyoosha mkono na kupelekea Brian
asema , "ndio Obren tunakusikiliza"
"Bosi mi naona tumuache Tasi aendelee na kazi
yake na kama akishindwa tutamuongezea nguvu ili
atuwezeshe kupatikana kwa huyo wa kumuaminiwa
na Professa apatikane haraka iwezekanyo" aliongea
Obren kisha akakaa kwenye kiti chake. Mzungu
mwingine alinyoosha mkono na kupelekea Brian
aseme ,"ndio Campbel tunakusikiliza"
"bosi mimi sikubaliani kabisa na Mr Obren kwa
jambo alilolizungumza, nashauri sis ndio tuingie
kazini na huyo Tasi tumtumie kivingine ila si
kwenye kazi hii" Campel aliongea na kupelekea watu
wote waafiki kwa kutikisa vichwa kuashiria
wamekubaliana na rai ya Campbel. Brian aliinuka
kwenye kiti chake kisha akasema "je kuna mwenye
la ziada juu ya hili? nadhani nyote mmekubalia na
ushauri wa Campbel, sasa kikosi chenu wenyewe
kiingie kazini kuanzia muda huu hamna la ziada".
Brian alihitimisha kisha akainuka kwenye kiti chake
halafu akaondoka.Wote waliobaki walitazamana kila
mmoja huku ukimya ukimya ukiwa umetawala,
Cambel aliuvunja ukimya huo kwa kusema, "jamani
tukutane kambini kwetu kule kwenye mbuga" halafu
akainuka kisha akaondoka eneo hilo.
****
MASAA MAWILI BAADAE
KWENYE MBUGA YA KENYA WILD IMPALA
Mbuga hii iliyo jirani iliyo jirani na ziwa Victoria
kulikuwa na na handaki kubwa sana lililochimbwa
kilomita mbili kutoka ziwani, ndani ya Handaki hilo
kulikuwa na kundi la watu takribani sita wenye asili
ya barani Ulaya. Watu hao walikuwa wameizunguka
meza kubwa ya duara iliyotengenezwa kwa chuma,
meza hiyo ilikuwana urefu uliowafikia kiunoni mwao,
katikati ya meza hiyo kulikuwa na karatasi kubwa
lilioenea karibu meza nzima.
"nafikiri tutumie boti yenye uwezo wa kuzama kama
ilivyo Nyambizi" aliongea Obren ambaye alikuwa ni
mmoja kati ya watu waliokuwa wapo eneo hilo.
"ni njia sana nzuri, sasa tukatokee sehemu gani
iliyokuwa salama" aliongea mzungu mwingine kisha
akauliza swali.
" Calvin mbona rahisi hiyo, tutapita chini kwa chini
hadi katika pori la Rubondo lililopo katika kisiwa cha
Rubondo kisha hapo tutafanya mapumziko ya muda
kisha tutaendelea hadi Kagera" Campbel alijibu swali
hilo huku akielekeza kwenye ramani sehemu
wanazopitia.
"njia nzuri hiyo nadhani ramani itatusaidia kufika"
alisema Calvin
"ndio inasaidia na tukifika huko tutachukuliwa na
helikopta hadi kibaha halafu hapo tutakutana na
Tasi" aliongea Campbel.
"Obren, Calvin, Scott , Jameson na Christian
nadhani tupo pamoja sasa team mambas tuingie.
kazi!" alihitimisha Campbel kisha akanyoosha ngumi
mbele na kupelekea wenzake wote wanyooshe
ngumi na kukutanisha ngumi ya Campbel.
"kazii!" wote waliitikia kwa pamoja kisha wakatoka
kwenda kuchukua vitu vyao vya muhimu
ITAENDELEA!!
Sunday, December 6, 2015
SHUJAA SEHEMU YA PILI
SHUJAA
MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA
SEHEMU YA PILI
Kujipitisha kwake katika madarasa ya sayansi hakukuzaa matunda yoyote, alijitahidi kumsalimja kwa uchangamfu ili awezs angalau kuzoeana naye. Salamu yake ilijibiwa kawaida na kila akitaka kujiweka karibu naye alishindwa kutokana na umakini wa kijana huyo kwenye masomo uliomfanya awe hapendi na mabinti. Baada ya jitihada zote kushindikana kushindikana sasa alibuni mbinu mbadala ya kumfikishia ujumbe kijana huyo, kila siku alikuwa akiwahi shule mapema kabla ya watu wote hawajafika. Muda huo wa asubuhi inayoifukuza alfajiri alikuwa akiweka kadi mbalimbali za mapenzi katika meza ya kijana huyo, mchezo huu ulimchanganya sana Moses hadi akawa anawauliza wanafunzi wenzake kama anamjua. Kila akijaribu kuwauliza wenzake juu ya jambo hilo aliambulia patupu pasipo kumpata anayemchezea mchezo huo, hali hiyo iliendelea kila siku huku mtumaji akiwa anajiita dream girl. Hali hiyo ilizidi kuendelea kila siku anapoingia darasani asubuhi, "be a man(kuwa mwanaume) Mose vitu hivyo havilaziwi damu hata siku moja" mmoja wa wanafunzi alimwambia Moses baada ya kumuona kila siku akilalamika juu ya tukio la kuletewa kadi na mtu msichana asiyemtambua. Hali hii ilizidi kuendelea na sasa akawa akikaa kantini muda wa mapumziko analetewa kadi na watu mbambali, kila kadi anayoifungua inatoka kwa yule yule msichana anayejiita dream girl. Hayo yalizidi kumchanganya sana Moses na akawa na shauku ya kumjua huyo
Saturday, December 5, 2015
SHUJAA SEHEMU YA KWANZA
SHUJAA
MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP: +255713776843
ANZA SASA
Huzuni ilikuwa imemtawala usoni kijana Moses na
kumfanya aonekane mtu mzima tofauti na
muonekano wake ulivyo, kila akijaribu kuhangaika
kwenda na baba yake katika hospitali tofauti ndani
ya jiji la Dae es salaam juhudi zake zilikuwa
zinagonga mwamba katika kutafuta tabibu awezaye
kumtibu baba yake aliyeugua ghafla pasipo
kujulikana chanzo kuugua huko. "mwanangu najua
unahangaika sana katika kuhakikisha.......ninapona
na ninarudi katika hali ya kawaida ila....." alikatisha
kuongea na kuanza kukohoa mfululizo huku
akimtazama mwanae kwa huruma kisha akaendelea
kusema "sitopona mwanangu ujue najua hujui
chanzo cha kuugua kwangu.." alihema kwa nguvu
huku akimtazama mwanae kwa jicho la huruma sana
kutokana na huzuni iliyomgubika kijana Moses. Baba
Moses akaendelea kusema "nimekuwa nikitumia
muda wa maisha yangu kwa miaka mingi katika
kugundua vitu mbalimbali katika sayansi pasipo
kujua mwisho wa kazi yangu hii , nimekuwa
nikitumiwa na watu matajiri ili niweze kupata fedha
kwa kuitumia kazi yangu vibaya. Sasa haya ndiyo
matokeo ya kazi yangu hii" alisitisha kuzungumza
kisha akamtuma Moses akamletee mkoba wake
anaoutumia kuhifadhi nyaraka zake muhimu.
Hakuwa mwingine bali ni professa Lawrence Gawaza
mwanasayansi wa siku nyingi na bingwa wa
kutengeneza kemikali hatari kwa maisha ya viumbe
hai, sasa yupo kitandani akiwa anaumwa ugonjwa
ulioshindwa kujulikana chanzo chake na matabibu
wa hospitali tofauti alizoenda kufafutiwa tiba. Moses
kijana wa miaka kumi na nane ndio kijana pekee wa
Prof Gawaza,hakuwa na mtu mwingine isipokuwa
mwanae huyo aliyekuwa anampenda sana. Mke
wake kipenzi alifariki siku aliyomzaa Moses, hivyo
hakuwa na mtu wa karibu hapo nyumbani zaidi ya
mwanae huyo.
Moses alimpelekea mkoba baba yake pale kitandani
anapomuuguzia,aliamriwa afungue kwa namba za
siri alizotajiwa na baba yake. Alipofungua alikutana
na makabrasha mengi pqmoja na funguo ndogo
sana, "umeiona hiyo funguo?" Prof Gawaza aliuliza
kwa tabu kutokana na kuzidiwa kwake. "huo pamoja
na hayo makabrasha naomba uwe mtunzaji wake na
usimkabidhi yoyote yule" Prof Gawaza alimwambia
mtoto wake huyo kwa sauti yenye kutoka kwa shida.
Moses naye aliitikia kwa kichwa huku machozi
yakimtoka kutokana na hali ya baba yake ilivyo, "we
ni mwanaume sasa haina haja ya kulia kwani
haisa......idii kitu chochote, kazania masomo yako
halafu....."alishindwa kumalizia kauli hiyo baada ya
kikohozi kumbana. Alikohoa kwa nguvu sana kisha
akaomba maji. Moses alikimbia kutoka chumbani
anapomuuguza baba yake hadi kwenye cha kulia
chakula kwenye jokofu la kupooza maji. Alichukua
bilau moja ndefu akaiweka usawa wa koki ya jokofu,
kisha akafungua koki ya jokofu kuruhusu maji
yaliyopo kwenye chupa kubwa juh ya jokofu hilo
yashuke kwa kasi, Alivyoijaza alirudi kwa kasi hadi
chumbani alipo baba yake, alipofika alimkuta kalalĂ¡
mithili ya mtu aliye ndani ya usingizi mzito. "baba
amka unywe maji" alimuita huku akimtingisha
mkono,cha ajabu hakuamka wala kuonesha dalili
zozote za kuamka. Moses alimtingisha baba yake
huyo kwa nguvu lakini hakuamka, aliita kwa sauti
kubwa lakini sauti yake haikuzaa jitihada zozote za
kumuamsha Prof Gawaza katika usingizi wa milele
aliolala. Moses alichanganyikiwa sana na hali
aliyomkuta nayo baba yak baada ya kumletea maji, "
baba! baba! baba! baba! babaaaa!" alipiga kelele
kwa nguvu baada ya kubaini baba yake hakuamka.
"Mose vipi mbona hivyo, kuna nini?" ilisikika sauti
ya mlinziwa nyumba hiyo pale mlangoni kisha
akaonekana mlinzi akivuka kizingiti cha chumba
hiko kwa kasi, kilio cha kwikwi cha Moses ndicho
kilimkaribisha humo chumbani na utulivu wa Prof
Gawaza ambaye alikuwa amelaliwa na Moses kifuani.
Alimnyanyua Moses kisha akaweka mkono katika
upande uliopo moyo katika kifua cha profesa,
hakuridhika akaweka na sikio kabisa kifuani mwa
bosi wake. Alipoinua uso wake ulikuwa umejaa
huzuni sana na alimshika mkono Moses kisha
akaenda naye nje, alipofika akamkalisha kwenye
baraza la nyumba. "yakupasa ujikaze dogo kwani
wewe ni mwanaume, kumbuka wewe ndio msimamizi
wa mali hizi na baba wa baadaye. Dogo jikaze najua
unasikia uchungu" Mlinzi alianza kumpa nasaha
Moses juu ya tatizo lililomfika. Pia akazidi
kumueleza "kumbuka binadamu hatuwezi kuwa
pamoja milele hata siku moja kwani ipo siku
tutatengana, ndio kama hivi mzee kakutoka ingawa
bado tunamuhitaji. Mose kutengana na mtu wako wa
karibu ni mojawapo ya changamoto za maisha na
kipimo cha ukomavu wako, sasa basi inabidi
ujioneshe upo mkomavu kiasi gani kwa kujikaza
katika suala kama hili. Baada ya mlinzi kumpa
Moses maneno ya kumtia moyo aliamua kwenda
kutoa taarifa kwa majirani pamoja na kuwapigia watu
wa karibu na Prof Gawaza.
***************************************
Brown Mcdonald ni mzungu mwenye mtandao
mkubwa dunia unohusiana na uhalifu wa kila aina,
umri wake na utajiri alionao ni vitu viwili tofauti.
Akiwa na vibaraka karibia kila nchi aliowaamini sana
katika biashara zake, hakika hakuna alitakalo
lifanyike katika biashara zake likashindikana. Kijana
huyu ambaye ni mwanajeshi aliyeasi amri katika
kikosi cha Uingereza na mtuhumiwa nambari moja
wa uhalifu barani ulaya aliamua kuja Afrika akiwa na
kundi kubwa la vijana wake baada ya msako wake
kuwa mkali barani Ulaya. Akiwa amevaa sura ya
bandia na alama za vidole mwake aliweza kuficha
muonekano wake pamoja na kupata passport mpya
ya kusafiria kwa njia ya kawaida tu pasipo
kugundulika na wanausalama wa dunia ambao
wanamsaka. Sasa ameingia ukanda wa Afrika ya
mashariki akiwa kama mfanyabiashara mwenye
viwanda vya kusindika katika nchi zote za Afrika ya
mashariki, ndani ya muda mfupi toka aingie katika
ukanda huu amejizolea umaarufu kutokana na ubora
wa bishaa zake. Akiwa anatambulika kama Brian
Stockman aliweza kuwa mfanyabiashara mwenye
ushawishi mkubwa katika soko la kimataifa, viwanda
vyake vilikuwa kama mwamvuli wa kuficha biashara
yake haramu anayoifanya ya kuuza dawa za kulevya
na nyara mbalimbali za serikali. Uongo
alioidanganya dunia ullikuwa umefanikiwa na sasa
alikuwa anajihisi mtu huru katika biashara zake,
aliweza kusafirisha bidhaa haramu pasipo kikwazo
chochote. Akiwa ametimiza mwaka mmoja tu toka
aanze kujulikana na wakazi wa kandahii ya Afrika ya
mashariki, alipata habari ya kugunduliwa kwa hatari
na mwanasayansi wa kitanzania. Taarifa hiyo
ilimvutia sana na akafanya jitihada za kuonanan na
mwanasayansi huyo, aliomba kuonana na
mwanasayansi huyo. Alipokubaliwa alipanga mahali
pa kukutana nae, hilo liliafikiwa na mwanasayansi
huyo.
Baada ya siku mbili walikutana katika mgahawa
uliomo hoteli ya Serena jijini Dar es salaam katika
sehemu iliyojitenga, kila mmoja akiwa na kinywaji
chake na amekaa kwenye kiti kilicho mkabala na
mwenzake. Baada ya kusalimiana Brian(Brown)
alianza kuongea kwa kiswahili kisicho fasaha chenye
maneno ya kingereza "sina mengi za kukuweka hapa
bana Gawaza, nahitaji tufanye bussiness".
"what kind of bussiness(biashata ya aina gani")
aliuliza Gawaza.
"no ipoo ongea na mswahili professa onesha jinsi
gani unatukuza swahili bana" Brian alimuumbua Prof
Gawaza baada kuona anajali sana kingereza kuliko
lugha yake ya taifa.
"ok mr Brian biashara ya aina gani?" prof Gawaza
aliuliza huku akitabasamu.
"i know you are scientist(najua wewe ni
mwanasayansi) na umegundua virus ambao
ninawahitaji kwa ajili ya kasi yangu binafsi" Brian
alieleza kiini cha kukutana.
"virus wale ni hatari sana Mr Brian na bado sijatafuta
dawa yake, huoni kama ni hatari kwako if you
release them(kama utawaachia)" Prof Gawaza
alimwambia Brian huku akipiga funda moja la
mvinyo ulio katika bilauri.
"I don't care about that(sijali kuhusu hilo) Professa
ninachohitaji ni virus na jaribio ndani ya nchi hii"
Brian alisema maneno hayo akiwa na uso wenye
dharau.
"no sipo tayari kwa hilo mr Brian kama unataka
biashara yoyote ya virus nitakupa ila si kujaribu
ndani ya nchi yangu yenye damu yangu...thats all"
Prof Gawaza alinyanyuka kwa hasira na kuondoka
eneo hilo. "we will meet again(tutakutana tena)"
Brian alimwambia kwa sauti kisha akaendelea
kunywa kinywaji chake kwa taratibu. Alipomaliza
alinyanyuka kwenye kiti alichokaa akiwa na hasira
maradufu, "I'll show him (nitamuonesha)" Brian
aliropoka kwa hasira kisha akanyanyuka kuelekea
ulipo mlangi wa kutokea katika mgahawa wa hoteli
hiyo. Alitoka na kuondoka kwa mwendo wa haraka
hadi alipoegesha, aliingia ndani na kuliwasha kisha
akatoweka katika eneo hilo.
**************************************
Maelfu ya watu walihudhuria katika msiba katika
msiba wa Professa Gawaza uliokuwepo nyumbani
kwake maeneo ya mikocheni jijini Dar es salaam,
wengi wakiwa ni ndugu,jamaa na marafiki wa
mwanasayansi huyo maarufu ndani ya jiji la Dar es
salaam. Uwanja wa nyumba hiyo ulifurika watu wa
rika zote wakiwa na mavazi meusi huku wale watu
wa karibu wa marehemu wakiwa wamevalia nguo
nyeusi chini na fulana nyeupe yenye picha ya
marehemu sehemu ya kifuani. Turubai kubwa
lilifungwa nje ya nyumba hiyo pamoja na viti vyenye
rangi moja vilivyokaliwa na wahudhuriaji wa msiba
huo, mtoto pekee wa marehemu ambaye ni Moses
alikuwa kakaa ndani muda wote huku kilio kikiwa
ndiyo kiliwazo chake. Siku iliyofuata mwili wa
marehemu uliagwa katika eneo hilo la nyumbani
kwake kisha msafara wa magari kutoka kwa
wahudhuriaji wa msiba huo uliondoka msibani hapo
kuelekea yalipo makaburi ya kinondoni maeno ya
kinondoni kwa ajili ya kuupeleka mwili wa marehemu
katika nyumba ya milele . Mazishi yalifanyika katika
makburi hayo kisha watu wakatawanyika kuelekewa
makwao na wengine kurudi msibani.
Baada ya siku takribani saba ndugu wote wa
marehemu waliondoka ndani ya nyumba hiyo na
kupelekea Moses mjomba wake ambaye alijitolea
kuishi naye na mlinzi wawe watu pekee waliobaki
katika nyumba hiyo. Maisha bila ya baba yake ndio
yaliyofuata baada ya msiba wake, pesa alizoziacha
baba yake pamoja na msaada wa rafiki mkubwa wa
baba yake aitwae Dk Mbungu ulioweza kumsaidia
katika vitu mbalimbali ndio uliopelekea aweze
kujimudu katika mahitaji yake muhimu ikiwemo
ulipaji wa ada shuleni. Hadi muda huo Moses
alikuwa anasoma kidato cha tano katika shule ya
Neema trust iliyopo mbezi jijjnj Dar es salaam,
aliamua kujiendeleza kielimu kielimu na kutoshika
mambo yoyote yasiyohusiana na elimu ili aweze
kujijenga. Umakini wake katika masomo ulimfanya
awe mwanafunzi bora katika shule yao, hadi muhula
wa kidato unakwisha mnamo mwezi mei mwaka
uliofuata, tayari alikuwa anaongoza shule nzima kwa
kupata alsma za juu kuliko mtu yoyote katika kombi
za sayansi zote. Akiwa likizo alitumia muda wake
mwingi kujisomea na akawa hajishughulishi na
mambo ya anasa, mnamo mwezi wa saba muhula
mpya wa kidato cha sita ukaanza kama ilivyo ratiba
ya nchi nzina ya Tanzania. Ulikuwa muhula wa
masomo ambapo wsnafunzi wengi walizinduka
kutoka kwenye usingizi baada ya kutokuwa makini
katika masomo yao ya kidato cha tano, katika kombi
ya PCB ambayo Moses alikuwa anasoma tayari
umakini wa wanafunzi ulizidi maradufu ingawa
hawakufua dafu mbele ya uwezo wa Moses
aliyezinduka mapema kabla yao.
**************************************
Beatrice Bernard ni binti wa familia yenye uwezo
anayesoma katika shule ya Neema Trust, ni
mojawapo ya wasichana warembo na wenye kuvutia
katika shule hiyo iliyosheheni watoto wa matajiri
kutoka sehemu mbalimbali ndani ya Afrika ya
mashariki. Umbo lake la asili ya asili ndio lilimfanya
avutie kwa kila anayemtazama, mchanganyiko wa
wazazi kutoka makabila tofauti ndio ulimfanya avutie
maradufu. Baba yake mzee Bernard alikuwa ni
muhaya na mama yake akiwa ni mrangi, hakika
alikuwa na umbo tata lililozua maswali na
minong'ono kila apitapo. Yote hayo pamoja na sifa
zote alizozipata na kusumbuliwa na watu kutoka
sehemu mbalimbali, alikuwa ni msichama aliyezama
katika penzi zito la mtu asiyemjali wala kuthamini
upendo wake. Utanashati wa huyo kijana ndio
uliomvutia sana na kufanya awe kiliwazo cha macho
yake, ustarabu na upole wake ndio uliomfanya
apende kuwa nae.maishani mwake. Kijana huyo
hakuwa mwingine ila ni Moses Gawaza kijana
mpenda masomo kuliko anasa kama ilivyo vijana wa
umri wake. Beatrice akiwa anasoma madarasa ya
arts katika kombi ya HKL alijitahido kujenga ukaribu
na kijana wa madarasa ya sayansi bila ya mafanikio,
hii haikumkatisha tamaa Beatrice zaidi ya kupenda
kuwa karibuIRI na Moses kutokana na misimamo
aliyonayo huyo kijana kamaJ mwanaume..
ITAENDELEA!!
Subscribe to:
Posts (Atom)