Tuesday, December 15, 2015

SHUJAA SEHEMU YA KUMI NA MOJA







RIWAYA: SHUJAA


MTUNZI: Hassan O Mambosasa

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



            ILIPOISHIA

Muimbaji wa nyimbo hiyo alipomaliza kuimba beti za mwisho za nyimbo hiyo, watu waliomzunguka walitawanyika na kufanya sura yake ionekane kwa Beatrice huku watu wakipiga makofi kwa shangwe. Beatrice aliishia kutabasamu baada ya kumuona muimbaji akiwa ni Moses, hakujua ratiba ya ile sherehe ilipangwaje maana ni jambo lilikuwa la kushtukiza kwake na lililomfurahisha.



ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI YAKE



SEHEMU YA KUMI NA MOJA!!
Mapigo ya moyo wake yalikuwa yakimuenda mbio kutokana na kushtukiwa na tukio lenyewe, machozi yasiyoashiria kilio yalikuwa yakimtoka Beatrice mashavuni mwake  kwa furaha aliyokuwa nayo. Alimkimbilia Moses kisha akamkumbatia huku akitabasamu kutokana na mshtukizo aliomfanyia kisha akamuachia, Moses alikabidhi kipaza sauti kwa mshereheshaji kisha akarudi kuketi katika kiti chake kilichopo mbele kabisa jirani na viti walivyokalia Irene na Hilary.

"makofi kwake Moses kwa mara nyingine kwa kuweza kutupa burudani pamoja na kumfurahisha mlengwa wa sherehe yetu ya leo" Mshereheshaji aliongea na kupelekea watu wapige makofi, burudani ya aina yake aliyoitoa Moses  ilimfanya hata mama yake Beatrice afurahi kutokana na uhodari wa kuimba alionao. Sauti nzuri aliyotumbuiza nayo ilimfanya ashindwe hata kugeuka kuangalia pembeni kutokana na kutazamwa na macho ya wakina dada wengi waliohudhuria sherehe hiyo. Hadi muda huo hakuwa amemwambia rafiki yake juu ya kituko alichofanyiwa na Annie baada ya kumpa mkono walipokuwa ndani, ratiba ya sherehe iliendelea kama ilivyopangwa na muda huu keki mahususi kwa ajili ya sherehe hiyo ilisogezwa  karibu na eneo alilopo Beatrice ikiwa na mishumaa inayowaka na maandishi ya kumtakia Beatrice sikukuu njema ya kuzaliwa. Keki hiyo iliyotengenezwa kwa namna ya kipekee iliwafanya wahudhuriaji waikodolee macho kwa huku wengine wakitoa pongezi kwa mtengenezaji wake.
"happy birthday to you,
 happy birthday to you,
 happy birthday happy birthday,
 happy bitthday to you"
Wahudhuriaji wote waliimbia huku wakipiga makofi wakati Beatrice akijiandaa kupuliza mishumaa iliyopo juu ya keki, alipoipuliza watu wote walipiga makofi kwa nguvu.

"mabibi na mabwana sasa umefika ule muda wa kitoto chetu kilichozaliwa kuchagua mvulana atakayempa company katika sherehe akakae nae mbele pembeni yake" Mshereheshaji aliongea baada ya zoezi la kuzima mshumaa kuisha, safari hii alifungua kikaratasi alichokishika mkononi halafu akakiangalia kisha akasema, "ukisikia jina lako unakuja mbele tafadhali eh...................Richard Godwin, Moses Gawaza, Andrew Kabaita na Rished Amur". Majina ya wavulana waliotajwa yaliitikiwa na walengwa kisha wakatoka mbele wakasimama katika mstari mmoja, watu walishangilia na kupiga makofi kila jina la mmojawapo lilipotajwa. Kundi la vijana waliokaa nyuma  katika meza moja ndio lilishangilia kwa nguvu baada ya kusikia jina la Andrew Kabaita likiitwa. Wavulana wote walioteuliwa hapo mbele walikuwa ni watanashati wote na waliovaa mavazi ya kuvutia na yenye gharama, Andrew peke yake ndiye aliongeza kikolombwezo cha mikufu ya dhahabu shingoni iliyomfanya apendeze kuliko wengine.

"sasa ni muda wa Beatrice kuchagua partiner wake katika sherehe hii ambaye atakuwa naye bega kwa bega mpaka sherehe inaisha" Mshereheshaji aliongea huku akimuashiria Beatrice kwa mkono asogee mbele kwa ajili ya kuchagua mtu wa kuwa naye katika sherehe hiyo.

"sasa wavulana mlioteuliwa unaombwa unyooshe mkono wako mbele kama unaomba kwenda kudance na bibie" Mshereheshaji aliwaambia wavulana watanashati waliopo mbele wakiwa wamejipanfa safu moja, Beatrice alianza kupita kwa Richard ambaye alikuwa wa mwanzo kisha akamshika kiganja  chake na kupelekea watu wote washangilie kwa nguvu wakijua ndiyo kachagua. Beatrice aliuachia mkono wa Richard na kupelekea watu waseme, "aaaaaaaaah!",  alisogea hatua moja hadi eneo alilokuwepo Rished kisha akamshika kama alivyomshika  Richard halafu akamwachia na kupelekea baadhi ya watu waseme, "aaaaaaaaah!". Alimsogelea Andrew na akashika mkono wake ambao  ulikamatwa na Adrew kisha mkono mwingine wa kijana huyu ukawa upo kiunoni mwa binti huyu,  DJ wa sherehe hiyo alipiga mziki wa taratibu na Andrew akalazimisha kucheza na Beatrice huku wenzake wakishangilia kwa nguvu. Jambo hilo lilimuhuzunisha Moses na akajiona amepasuliwa moyo wake na kisu kibutu chenye kutu, alijikaza kiume ingawa aliamini moyoni mwake alikuwa amekosa nafasi adimu kama hiyo. Andrew alikuwa anacheza muziki huo na Beatrice akiwa yupo nusu hatua mbele ya Moses, Mosea alizidi kuumia kwa jambo hilo na akageuka kuwapa mgongo ili arudi kwenye kiti chake akaketi moyoni akijua amekosa nafasi hiyo ya kuwa karibu na Beatrice katika sherehe hiyo. Alipotaka kupiga hatua ili aondoke mziki ulizimwa ghafla na akajikuta ameshindwa kuondoka kurudi kitini, Andrew alimtazama DJ wa sherehe hiyo  kuashiria kutofurahishwa na uamuzi wake wa kuzima muziki. Muda huo Victoria,Hilary,Irene na Mama Beatrice walipiga makofi kwa nguvu kisha baadhi ya waalikwa nao wakapiga makofi pia, hicho ndicho kilisababisha Andrew aangalie upande wa waalikwa ambao walikuwa nyuma yake na ikapelekea aone kitu kilichosababisha amuachie Beatrice mkono. Alichokiona ni mkono mmoja wa Beatrice ukiwa umeukamata mkono wa Moses kumzuia asiondoke, hii ndio sababu iliyomfanya Moses ashindwe kuondoka kurudi kitini na akabaki amempa mgongo Beatrice akiwa ameinamisha uso wake chini. Andrew alijikuta akiingiwa na aibu ya ghafla na akajiona ni mtu aliyeaibika kwa kitu alichofanyiwa na Beatrice, alisimama akiwa amepigwa na butwaa na aibu juu akishuhudia Moses akiwa amekumbatiwa na Beatrice kwa muda huo na mziki mwembamba ukiwa umeanza kupigwa taratibu kisha Moses na Beatrice wakarudi mbele kwenye kiti cha watu wawili walichoandaliwa.

"watanashati na vijana wenye mvuto walikuwa wakicheza kamari ya kugombea kukaa karibu na rose flower na bahati ikamuongukia mtanashati mwingine kama walivyo wao, brothers mmependeza na mnavutia kwa macho za totoz za hali yoyote ingawa mwenzenu kaangukiwa na bahati ya kuchaguliwa na mlengwa wa sherehe. Asanteni kwa kujitokeza na kuonesha utanashati wenye mvuto" Mshereshaji aliwaambia Richard, Andrew na Rished huku watu wakishangilia. Washiriki waliokosa bahati hiyo walipoondoka Mshereheshaji alimgeukia Moses, "jamaa uko Benet na dada hapo kama umeoa, ohoo mwisho sherehe hii tu". Ulikuwa ni utani amba uliwafanya watu wacheke na Moses mwenyewe akaishia kutabasamu.

****

Kitendo cha Beatrice kumkubalia Moses awe mtu wake katika sherehe hiyo ilikuwa ni mwiba mkalii uliuchoma moyo wake  kwa mshtukizo na kumfanya abaki na maumivu makali sana. Andrew ingawa ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona Beatrice kwa macho yake tangu alipokuwa akioneshwa picha na  dada yake, alitokea kumpenda sana binti huyo huyo, pia yeye katika shindano hilo ni mipango ya dada yake ambaye ni rafiki kipenzi wa Victoria. Annie ndiye dada yake na ndiye aliyemfanyia mpango wa kumuwezesha kukaa karibu na Beatrice, mpango huo ulifanikiwa ingawa ulimuumiza moyo kwa kutokuwa chaguo la msichana anayempenda. Andrew aliwasili katika meza anayokaa akakutana na sura za wenzake zikimtazama kwa huruma, alikaa kwenye kiti chake kinyonge na alijitahidi kuwa na uso wenye uchangamfu ingawa moyoni amejeruhiwa na silaha asiyoidhania.

"sasa inakuaje huyu demu amchague yule mpolipoli na mshamba tu kwetu" Mmmoja wa marafiki wa Andrew alisema.

"yaani nashangaa kabisa, kamuacha mshkaji wetu anayeng'aa shingoni kwa madini halafu anamfuata yule" Mwingine akadakia. Muda huo  Annie aliwasili hadi jirani na Andrew kisha akamshika bega kwa upole, Andrew aliinua macho kumtazama dada yake kwa upole uliojaa huzuni.

"njoo mara moja" Annie alimwambia kisha akaanza kutoka kuelekea pembeni mwa eneo lenye sherehe karibu na bwawa la kuogelea, Annie alikaa kwenye kiti kinatumiwa na watu wakati wanapumzika wakiwa wanaogelea na mdogo wake akakaa karibu yake.

"pole kwa yaliyokukuta young bro" Annie alimpa pole mdogo wake.

"sister siwezi nikapoa mpaka kiu yangu itulie, kiu yangu ni kumpata Beatrice sasa kama nikimkosa ni kidonda kwangu" Andrew aliongea kwa huzuni.

"najua hilo ndio maana nikakuita hapa" Annie aliongea kisha akatazama pande zote halafu akasema, "kuna njia moja nataka tuicheze na ikifanikiwa basi wewe utampata Beatrice kiulaini".

"really?!" Andrew aliuliza kwa mshangao.

"yeah! Young bro kuna kitu nakitaka na kukipata basi na wewe utampata Beatrice" Annie alimwambia.

"Sis hivi rafiki yako Victoria hawezi kukusaidia kwa hili maana yeye ni mtu wa karibu kwa Beatrice, nampenda dada hebu jaribu kunisaidia kwa kumtumia yeye" Andrew aliongea.

"ni vigumu sana kumtumia kwa mambo hayo kwani hataki hata kidogo, Andrew hivi unapenda mimi dada yako niwe na furaha" Annie aliongea.

"ndiyo dada" Andrew alijibu.

"basi hii njia nitakayokupa ya kumpata Beatrice ndiyo furaha yangu pia itapatikana, kama unanipenda mimi dada yako basi naomba tushirikine katika kuipata furaha yangu" Annie aliongea huku akiwa ameshika kiganja cha Andrew.

"ok" Andrew alikubali.

"that's why I love you my young bro(hiyo ndiyo sababu nakupenda mdogo wangu), turudi basi" Annie aliongea huku akisimama na Andrew naye akasimama kisha wakaanza kutembea kurudi katika eneo la sherehe.


****


 Wakati sherehe ya Beatrice ikipamba moto na ikiwa yenye furaha, eneo jingine la jiji la Dar es salaam kulikuwa na sherehe ya watu wawili ambayo ilihitajika kuanza ndani ya muda mfupi tu wahusika wa sherehe hiyo watakapomaliza kazi ndogo ya kueleweshana kuhusu jambo linalowahusu. Sherehe iliyopangwa kusherekewa na wawili tu ndiyo iliyokuwa inangojewa kwa hamu na mmojawapo kati yao, utofauti wa jinsia zao ndiyo chanzo pekee cha sherehe hiyo iliyomo ndani ya nyumba ya kawaida iliyopo maeneo Tabata. Wote wawili walikuwa wapo katika uwanja wa sherehe ulio na urefu wa futi sita kila upande, mavazi waliyovaa yaliashiria kujitayarisha kwa ajili ya sherehe hiyo. Norbert na Norene ndiyo wahusika wa sherehe hiyo na sasa wapo katika mavazi ya chumbani tu, walikuwa wamelala kifudifudi kuiangalia tarakilishi ya mapakato iliyopo mbele yao katika kitanda. Picha alizotumiwa Norene ndiyo zilionekana kwenye kioo tarakilishi hiyo zikiwa na maelezo mengi yakiwa chini yake, Norene alianza kumuelezea mambo mengi kuhusu hizo picha.

"Vijana ulionitumia picha zao ni wahalifu wa genge hatari la gaidi kutoka Ulaya ambaye anatafutwa kwa udi na uvumba na wanausalama wa umoja wa Ulaya kutokana na uhalifu alioufanya, hawa ndio vijana wake ingawa kwa majina bado sikufanikiwa kuwajua" Norene alimueleza Norbert ambaye alikuwa akimsikiliza huku akifanya uchokozi katika mwili wake, alipopumzika kueleza Norbert alianza kutembeza papi za midomo yake kwenye mgongo wake ulio wazi kutokana na kuvaa gauni fupi la kulalia.

"Nor bwanaa tumalizie kwanza ndio mengine yafuate, please acha bwana unanisisimua mwenzio" Norene alilalamika huku akiwa amefumba macho kwa hisia.

"Haya mama tumalizie tuanze kazi nyingine inayohitaji kuelekezana wote" Norbert aliongea huku akilala sawasawa kama alivyokuwa awali.

"hii boti uliyoipiga picha ni mali ya shirika la KGB la Urusi na iliibiwa baada ya  gaidi aitwae Brown Macdonald kufanikiwa kumuua kachero wa KGB katika mapambano na wauza unga, helikopta uliyoipiga ni mali ya shirika la hifadhi za taifa TANAPA kwa mujibu wa namba zilizopo ubavuni mwake. Ni hayo tu" Norene alihitimisha kisha akamuangalia Norbert kwa macho malegevu.

"unajua kuna la nyongeza ambalo ambalo linahitajika kusaidiana wote wawili" Norbert alimwambia huku akimtazama usoni.

"lipi hilo?" Norene aliuliza huku macho yake yakiashiria kuhitaji jambo ambalo alishindwa kulitamka.

"ni hili hapa" Norbert alisema kisha akagusa papi zake za mdomo na za Norene kwa ghafla bila kutarajiwa, Norene alipokea papi hizo na kupelekea uwe mwanzo wa sherehe yao waliyokuwa wakiingojea baada ya kumaliza jambo lililokuwa mbele yao.



****


"mabibi na mabwana sasa umefika ule muda wa Beatrice kukata keki, Beatrice unaombwa usogee mbele kwenye keki ili uweze kukamilisha zoezi la kukata keki kisha uanze kuwalisha wapendwa wa sherehe hii" Mshereheshaji wa sherehe hiyo aliongea baada ya kuitazama karatasi ya ratiba iliyopo mkononi mwake. Beatrice alisogea hadi ilipo keki kisha akashika kisu maalum kwa ajili ya kukatia keki,  alikata keki hiyo  vipande vidogo kisha akamuangalia Mshereheshaji baada ya kumaliza.

"sasa Moses unaombwa usogee karibu na Beatrice kisha ulishwe keki na yeye akulishe halafu wengine wafuate" Mshereheshaji aliongea huku baadhi ya watu wakipiga makofi hasa Hilary,Irene na Victoria. Beatrice alichukua uma kisha akaichoma keki halafu akaunyanyua ums ukiwa na keki, alimlisha Moses huku miale ya kamera ikiwamulika. Moses naye alinyanyua uma wenye kipande cha keki kisha akamlisha Beatrice huku nderemo na vifijo vikiwasindikiza na miale ya kamera ikifanya kazi yake ya kuwamulika. Waalikwa wengine nao walifuatia baada ya watu wa karibu na ndugu wa Beatrice walipomaliza katika kulishwa keki, walipomaliza kulishwa wote keki tayari muda wa kuingia chakula kwa mujibu wa ratiba ya sherehe ulikuwa umewadia na watu wakajipanga kwa ajili ya chakula. Moses na Beatrice walipelekwa kwenye meza ya vinne na wakawa wameungana na Hilary pamoja na Irene katika meza moja kwa ajili ya kupata chakuka, furaha na vicheko vilitawala meza hiyo na huzuni na wivu vilikuwa vimeitawala meza ya tatu kutoka pale walipo iliyotumiwa na Annie pamoja na mdogo wake. Beatrice na Moses walipomaliza kula walibaki hapo wakiongea mambo mbalimbali na marafiki zao waliopo katika uhusiano wa kimapenzi.

"Mose nakuomba mara moja" Beatrice alisema akanyanyuka kisha akaelekea pembeni eneo ambalo halina mtu, Moses alinyanyuka akamfuata eneo alilosimama. Walitazamana kwa sura zenye tabasamu pasipo kusema jambo lolote kwa takribani kwa sekunde kadhaa, uliingia ukimya uliopo ndani ya nafsi zao kwa ghafla na kila mmoja akahitaji kusema jambo kwa mwenzake lakini waliishia kutazamana. Moses alihitaji kusema jambo lakini nafsi yake ikamwambia awe na subira na asikilize jambo aliloitiwa.

"Yaani nakosa la kusema kwa furaha uliyonipatia leo, asante ni jambo lisilotosha kwa furaha uliuonipa leo katika sherehe ya kuzaliwa kwangu hasa ulipotumia sauti yako nzuri na tabasamu  lako linalonipendeza kila ninapoliona. Kiukweli naona nikisema asante nitakuwa sijafikia furaha uliyonipatia siku ya leo" Beatrice aliongea.

"asante ni jambo linaloweza kulipiza firaha niliyokuletea katika siku ya leo kwako ikiwa ni kama rafiki, pia ni jambo linazidi kulipizwa ikiwa kuna kuna jambo jingine zaidi" Moses aliongea.

"kivipi?" Beatrice aliuliza kutokana na kutoelewa kauli ya Moses.

"Hakika mimi ni kitwana mtoa burudani kwako Malkia ninayekuhusudu zaidi ya nafsi yangu, jukumu la kukupa burudani ewe malkia wangu uliye pekee ni langu na nitalifanya pasipo kungoja shukrani zaidi ya hifadhi ya moyo wangu katika Kasri la upendo wako. Nanena yatokayo moyoni yanayothibitika hata machoni, I love you Beatrice "  Moses aliamua kuweka hisia zake wazi kwa Beatrice huku mapigo yake ya moyo yakiwa juu kama ameshtuliwa na ndoto ya kutisha usingizini. Maneno hayo yalisababisha moyo wa Beatrice mshtuko wa furaha, kitendo cha yeye kutamkiwa neno hilo na kijana aliyempenda ilikuwa ni furaha kwake ingawa alikosa la kuongea kwa muda huo. Hata alipotaka kuongea  alikatishwa na sauti ya mama yake.

"Beatrice njoo upige picha mara moja" Mama Beatrice alimuita Beatrice akiwa umbali mfupi toka pale alipo. Beatrice alianza kumfuta mama yake huku Moses akiwa amesimama palepale.

"Moses baba na wewe njoo pia" Mams Beatrice alimuita Moses pia katika suala la kupiga picha. Moses aliitiiia wito huo kisha akamfuata Mama Beatrice alipo kwa ajili ya zoezi la kupiga picha.




ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment