Saturday, December 19, 2015

MJUE ANICETI KITEREZA

Aniceti Kitereza

                  ANICETI KITEREZA

     Natambua wengi wenu mtakuwa hammumfahamu huyu mwanfasihi wetu mkongwe kabisa ambaye kwa sasa hatunaye duniani, ni mwanafasihi ambaye katika historia ya fasihi nchini Tanzania hatokaa asahaulike kabisa kutokana na kazi zake za awali alizokuwa ameziandika.


     Huyu mmojawapo kati ya waandishi wa riwaya wa mwanzo kabisa nchini Tanzania, alizaliwa mwaka 1896 Ukerewe nchini Tanganyika ambayo kwa sasa inafahamika kama Tanzania. Aniceti Kitereza alizaliwa kwa Muchuma na mume wake Mulindima.Pia alikuwa ni mjukuu wa mtemi Machunda wa wa ukoo wa Silanga katika kisiwa cha Ukerewe.  Kitereza alipokuwa na umri wa miaka mitano  tu mnamo mwaka 1901, baba yake mzazi alifariki dunia kwa ugonjwa wa Ndui, kuanzia hapo Kitereza alilelewa na mama yake na kiongozi wa mahakama ya Omukama aitwae Mukaka ambaye alimlea kama mwanae wa kumzaa.


    Mukaka baadaye kabisa aliwapelekea watoto wake wote na watoto wa ndugu zake kwenda kusoma katika shule ya kikatoliki karibu na kijiji cha Kangunguli, Kitereza alianza kusoma shule ya kikatoliki hiyo mnamo 1905 ambapo alibatizwa jina na kupewa jina la kikristo la Aniceti.



    Miaka miwili baadaye 1907 Mukaka alifariki dania na nafasi yake kiuongozi ikachukuliwa na mtoto wake Ruhumbika, ambaye alimshawishi Kitereza kuondoka Kangunguli kwenda kuendelea na elimu zaidi  katika shule ya kidini ya Rubya ndani ya eneo liitwalo Rubya ambalo leo hii lipo ndani ya mkoa wa Kagera. Kitereza alisoma kwa muda wa miaka kumi  ambapo alihamishiwa katika ngazi ya watu wazima ndani ya shule hiyo. Hapo alifanikiwa kukimudu kilatini ambayo ilikuwa ni ni lugha ya kufundishia katika shule za kidini za kiroma..

   Kitereza alisoma kigiriki , kijerumani  pia katika kipindi hicho cha ukoloni na lugha ya kiswahili vilevile, baada ya wajerumani kushindwa vita kuu ya kwanza ya dunia.Kitereza alisoma somo la imani ya Mungu na asili dini (Theology) na filosofia kama sehemu ya mafunzo ya utawa katika seminari ya kiroma.

 Kitereza ameandika kitabu marufu sana ambacho kinaitwa Myombekere na Bugonoka na Ntulanalwo na Bulihwali  kwa lugha yake mama ya Kikerewe .

Alifariki dunia mnano mwaka 1981 akiwa na umri wa miaka 85 .


NAAM HUYU NDIYE MWANAFASIHI WETU WA SIKU YA LEO, TUKUTANE WIKI IJAYO SIKU KAMA YA LEO KUMJUA MWANFASIHI MWINGINE NDANI YA NCHI YA TANZANIA.






TUNAPENDA KUWAOMBA RADHI SANA KWA KUKATISHA MUENDELEZO WA HISTORIA ZA WANAFASIHI WETU KWA WIKI KADHAA ZILIZOPITA KUTOKA NA SABABU ZILIZOPO NJE YA UWEZO WETU. SASA TUWE PAMOJA WIKI IJAYO TENA PANAPO MAJALIWA

No comments:

Post a Comment