Friday, December 11, 2015

SHUJAA SEHEMU YA SABA





RIWAYA: SHUJAA


MTUNZI: Hassan O Mambosasa

SIMU:+255713776843
+255762219759


WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



                        ILIPOISHIA
.
"kwa kweli huyu mtoto kuwa HKL ni haki yake
maana huu mwandiko ni mkali balaa.. Mh! Hebu
ngoja" aliongea peke kisha akawa kama amegundua
kitu, aliinuka hadi kwenye begi lake la shule kisha
akachomoa bahasha nyingine halafu akarejea
kitandani halafu akaifungua bahasha hiyo. Aliitoa
kadi ya mapenzi ambayo alitumiwa na msichana
anayejiita Dream girl kisha akaifungua halafu
akaiweka sambamba na kadi ya mwaliko wa sherehe
ya kuzaliwa ya Beatrice. Alitazama miandiko ya kike
iliyomo kwenye kadi hiyo kwa umakini kisha
akaguna kuashiria amegundua kitu, alirudia tena
kuitazama miandiko hiyo halafu akatabasamu.

"Ha! Hai! Ha! Ha! Dream girl sasa nimekujua"
alisema baada ya kuona miandiko inafanana katika
kadi hizo, hakika aliweza kumbaini Beatrice kama
msichana aliyemsumbua kwa wiki kadhaa.

"huyu Hilary nahisi ni mwanga maana aliyoniambia
juu ya Beatrice ni ukweli mtupu" alizidi kuongea
peke yake haea alipokumbuka kauli ya Hilary juu ya
Beatrice



ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO


        SEHEMU YA SABA
Sasa amefanikiwa kumjua dream girl aliyekuwa  akimsumbua kila siku, uzuri wa dream girl mwenyewe kweli ulikuwa ni sahihi na jinsi anavyojiita. Hakukosea kujiita hivyo katika kuficha  utambulisho wake, binti aliyetokea kumvutia hata yeye mwenyewe tangu alipoanza mazoea naye. Moses alijiona ni mwenye bahati  kwa kujua anapendwa na msichana aliyeanza kumpenda baada ya muda mfupi tu toka wazoeane. Hakika aliyaamini maneno ya rafiki yake kipenzi mwenye uzoefu katika masuala hayo,

"najihisi kutaka kuvunja ahadi niliyojiwekea kwa huyu maana yake ni ana ushawishi mtupu" alijisemea kisha akavuta shuka lililopo jirani yake kuutafuta usingizi wa usiku huo. Usingizi ulichelewa kumvamia kijana huyu kutokana na mawazo juu ya binti aliyepata ushawishi wa ghafla wa kumpenda, hakika macho yakitamani na moyo utahitaji na macho yasipotamani basi katu moyo hauwezi kuhitaji. Macho ya Moses yametamani uzuri wote alionao binti huyo na ndio maana moyo wake ukamuhitaji kuwa na zaidi ya ukaribu naye, ukaribu wa kipekee ndio uliohitajika na moyo wa  Moses ili binti huyu awe zaidi ya rafiki kwake katika maisha yake.

"sasa mpaka usubiri umuweke ndani keshakuwa wa
mwenzako huyo" maneno ya Hilary aliyomuambia wakati wanarejea nyumbani yalimjia kichwani mwake na kumfanya awe na haraka ya kumpata binti huyo aliyetokea kumvutia sana. Papara za ujana ziliuvaa moyo wake kwa kuhofia kuwahiwa na mtu mwingine katika kumpata msichana huyo, alijihisi na hali tofauti mwilini mwake kila alimpomfikiria  binti huyo mwenye uzuri wa kipekee katika macho yake.

"aisee hapa nimenasa kabisa" aliongea peke yake huku akivuta shuka vizuri katika kuusaka usingizi ambao ulionekana kumpaa ingawa alikuwa na uchovu wa alipokuwa anajisomea. Hitaji linalokuja moyoni mwako kwa kujihisi unahitaji kuwa na zadi ya ukaribu na mtu au kitu fulani katika maisha yako ya kila siku, haya ndio  mapenzi na yameuteka moyo wa kijana huyu kwa ghafla tofauti na ilivyokuwa awali. Hadi usingizi unampata tayari alishatawaliwa na mawazo juu ya Beatrice na alikuwa yupo katika ulimwengu mwingine wa ndoto juu ya binti anayemhusudu ndani ya nafsi yake.



****


   Hali ilikuwa hivyohivyo kwa Beatrice kwa usiku huo kutokana na penzi zito alilonalo kwa Moses kijana mtanashati mwenye kuyajali masomo yake, hadi muda huo wa usiku alikuwa yupo kitandani akiangalia picha iliyomo ndani ya Shajara(diary) yake. Alijikuta akitabasamu kila alipoitazama picha aliyoiomba kwa mwenyewe walipokuwa  wakipata kifungua kinywa asubuhi ya siku hiyo kipindi cha mapumziko baada ya vipindi viwili vya kwanza kuisha, kimtazamo kwa jinsi anavyotabasamu unaweza kusema kaanza kurukwa na akili kumbe alichanganywa na penzi zito alilonalo kwa Moses.

"Moses kuna kitu nataka nikuombe kama hutojali"

"nakusikiliza ni kitu gani hicho?"

"nimeona picha yako ndogo kwenye pochi yako ya hela, je unaweza ukanipatia ili niwe nayo kama ukumbusho"

"mh!"

"mh! what remember Iam your friend and I will your best friend(mmh nini kumbuka mimi ni rafiki yako na nitakuwa rafiki bora)"

"ok hii hapa chukua tu" aliyakumbuka maneno ya siku hiyo asubuhi alipomuomba picha Moses wakipata kifungua kichwa muda wa mapumziko. Upendo alionao kwa kijana huyu ulimtia hadi akafikia hatua ya kusema, "Iam going to be crazy(ninaelekea kuwa kichaa)" kisha akaikumbatia Shajara yake aliyoibandika picha ya Moses huku uso wenye tabasamu linaloelekea kuwa kicheko ukiwa umemtawala.

"we Bite ushakuwa kichaa siku hizi" ilikuwa ni sauti ya dada  yake iliyomshtua katika  mawazo juu ya Moses. Beatrice alikuwa anapenda kulala chumba kimoja na dada yake aitwae  Victoria katika vitanda tofauti ingawa alipewa chumba chake kingine chenye kila kitu, muda huo dada yake alikuwa ameshtuka usingizini akiwa na gauni ya kulalia baada ya kulifunua shuka alilojifunika.

"mbona unacheka peke yako" dada yake alizidi kumuuliza kutokana na jinsi alivyomuona wakati anaamka.

"nothing sis" Beatrice alijibu huku akiifunika Shajara yake.

"mdogo wangu naona tumeanza kufichana siku hizi"

"hapana dada"Beatrice alikanusha huku akinyanyuka kuelekea alipo dada yake, alipofika alimuwekea mkono wa kushoto begani kisha akaulalia mkono wake huo.

"Iam in love sis(nipo katika mapenzi dada)" alimwambia dada yake kisha akamuegemea kwa namna ya kudeka, kisha akaifungua Shajara halafu akamuonesha picha ya Moses.

"ndio nani huyu hebu nitambulishe kwa picha tu" Dada yake alimuuliza.

"the boy whom I love(mvulana ambaye nampenda) Beatrice alijibu kwa sauti ya kudeka.

"una haki ya kuwa hivi mdogo wangu kwa ajili ya huyu mvulana, ni mzuri haswa" Dada yako alimwambia kisha akamshuka kidevu chake halafu akamwambia, "time to sleep muda wa kulala, unajua kesho ni maandalizi ya  sherehe yako mdogo wangu". Beatrice aliitikia kwa kutikisa kichwa kisha akarudi kitandani kwake halafu akalala.


****

 Rafiki kipenzi wa marehemu Professa Gawaza aitwae Dokta Mbungu alipata ugeni ambao hakuutarajia asubuhi ya siku ya jumamosi, mgeni huyo ambaye hakuwa na miadi naye  alifika nyumbani kwake maeneo ya Msasani. Rangi ya ngozi ya mgeni huyo ndiyo kitu pekee kilichopelekea mwanasayansi huyu amkaribishe ingawa hakuwa na miadi naye siku hiyo ambayo kwake ni ya mapumziko. Hakika bado alikuwa na ule ushamba wa kumuhusudu mzungu kuliko mtu mweusi katika mambo  yake, ndiyo maana alimkaribisha mgeni huyo tofauti na ilivyo kwa watu wengine wasio na miadi naye anaoishia kukataa kuonana na hata kumpa ruhusa mlinzi wake awaruhusu. Utanashati wa mgeni huyu ndiyo chanzo kingine kilichofanya mgeni huyo aruhusiwe, kwa ukarimu wa hali ya juu alimkaribisha katika viti vilivyopo katika bustani ya kuvutia iliyopo nyumbani kwake. Kinywaji cha kisasa kabisa alimuagizia halafu akamkaribishakwa namna ya kipekee.
"naam bwana Scott nakusikiliza mgeni wangu" Dkt Mbungu alimwmbia mgeni wake.

"kama nilivyokuambia awali mimi ni mgeni ambaye nimekuja hapa kwa ajili ya kujadiliana jinsi ya kupambana na wanasayansi hatari ambao wanatumia taaluma kwa kutengeneza virusi hatari kwa maisha ya binadamu. Nikiwa kama mmoja wa maofisa wa shirika la umoja wa mataifa(WHO) nimeamua kuja kwako ili nipate msaada katika kufanikisha kupatikana kwa wanasayansi wa aina hii" Scott alijieleza huku akitoa kitambulisho kumuonesha Dkt Mbungu kwa mara ya pili.

"kwa kweli wanasayansi wenye kutengeneza virusi ndani ya Tanzania hawapo kwa sasa, sema kuna virusi ambavyo vilitengenezwa kwa bahati mbaya na marehemu Professa Gawaza ambavyo alishindwa kuviua na hata dawa ya kuvizuia alishindwa kuipata. Kutokana na hilo aliamua  kuvificha mahali pake pa siri kisha faili lenye kanuni ya kutengeneza virusi hao alilifungia hukohuko na funguo akampatia mtu wake mwenye kumuamini" Dkt Mbungu alimueleza.

"Dokta unajua vitu kama hivyo inahitaji vizuiliwe na hao virusi kwa bahati mbaya wakafikiwa na watu wabaya unafikiri itakuwaje? Vitu kama hivi inahitaji kudhibitiwa" Scott alimwambia.

"bwana Scott ujue unaongea ukweli kabisa ila tatizo ni kuipata hiyo dawa au kemikali inayoweza kuua hao virusi maana mwenyewe aliyewatengeneza amethibitisha hatari yake maana alivijaribu kwa panya ambao walikuwa walitoka mapele makubwa huku wakivuja damu mdomoni ndani ya kuda mfupi tu. Panya hao aliwaunguza moto hadi wakawa majivu na ameyapima majivu yao ameyakuta  bado yana chembembe za seli za virusi hao. Pia amejaribu  kuwatilia kemikali tofauti za kuua vijidudu ili awauwe lakini ameshindwa, hivyo ameamua kuwafungia huko mahala pake  pa siri ili wasifikiwe na watu"

"sawa nimekuelewa Dokta, hivi unadhani tukikutanisha nguvu zenu na za wanasayansi wa umoja wa matifa kitengo cha shirika la afya tutakosa dawa kweli?"

"eeee nadhani tutapata dawa maana wengi  wenye umoja wana nguvu"

"sasa inabidi hao virus tuwapeleke makao makuu ili wakafanyiwe na wewe ukusanye jopo lako ili muende nalo huko mkaungane na wenzenu"

"hilo ni wazo zuri sana, tatizo sipajui alipowaficha na mtu muaminifu aliyempa funguo za huko simjui pia"

"hili nalo ni tatizo kubwa, sasa kimtazamo wako anaweza akawa ni nani anayemuamini"

"kusema kweli Gawaza alikuwa na watu wawili aliowaamini ambao ni shemeji yake ambaye anafanya kazi TANAPA na mwanae wa pekee aitwae Moses Lawrence Gawaza. Hao ndio anaowaamini na mwenye ukaribu nao na hakuwahi kuniamini mimi kama anavyowaamini hao"

"je unafikiri tutawapata wapi hao watu?"

"huyo shemeji yake kwa sasa anaishi nyumbani kwake kutokana na upweke alionao mtoto wa marehemu".
Scott alitaka kuuliza swali tena lakini akakatishwa na ujio wa mlinzi aliyeouja hapo ghafla.

"Wangoko kuna tatizo?" Dkt Mbungu alimuuliza mlinzi wake

"kuna mgeni mzee" Mlinzi alisema

"ni nani?" Dkt Mbungu aliuliza

"Norbert Kaila" Mlinzi alijibu

"ohoo! Kumbe ni huyo, mruhusu na umuelekeze nilipo" Dkt Mbungu alitoa amri kisha akamgeukia Scott halafu akamwambia "huyu anayeingia sasa ni mmoja wa waandishi wa habari hodari na nilimuagiza aniangalizie majani ya miti ya miti alipokuwa ziarani huko Kagera kwa ajili ya kutengeneza dawa, nadhani sasa ndio kaniletea".  Norbert alifika hapo bustanini akamkuta Dk Mbungu akiwa na mgeni wake  wakiongea.

"Norbert karibu sana" Dk Mbungu alimkaribisha Norbert huku akisimama kwenye kiti alichokalia

"asante mzee, shikamoo.  Habari yako" aliitikia ukaribisho wa mwenyeji wake kisha akamsabahi Scott.

"safi" Scott aliitikia kisha akawa amekaa kimya, Dk Mbungu alianza kumwambia Norbert,  " marhaba, vipi kijana umefanikiwa kupata hata mfano wa mmea niliokutuma?".

"ndio Dokta nimefanikiwa kuupata na ndio huu hapa" Norbert alijibu kisha akatoa mfuko mdogo wa plastiki kisha akampatia Dk Mbungu.

"vizuri sana ndio huu mmea ninaouhitaji, ohoo halafu nimesahau kukutambulisha. Kutana na bwana Scott kutoka shirika la afya  duniani WHO yupo nchini kwa kazi maalum" Dk Mbungu alimtambuliaha mgeni wake kwa Norbert ambaye alionekana kumjua mgeni huyo.

"nafurahi kukufahamu" Norbert alimwambia Scott huku wakipeana mikono ,kitendo cha Norbert kumuona Scott haikuwa mara ya kwanza. Alijaribu kuvuta picha ni wapi alipomuona lakini kumbukumbu zilikuja na kutoka, alipofikiria mara kwa mara ya pili ndipo kumbukumbu zake zilipompa jibu sahihi na hapo ndipo akatambua mahali alipomuona Scott. Hakika alibaini ni mmoja wa watu aliowapiga picha kule Biharamulo usiku wa kuamkia Ijumaa ingawa alikuwa ana muonekano tofauti, sasa hapo ndipo vita ya maswali ilipoushambulia ubongo wake ingawa alionekana hakuwa na wazo lolote zito. Kiherehere cha kutaka kupata majibu ya maswali yake kilishampanda na  hapo alikuwa akisaka majibu kwa kutumia dhana jambo lilimjia  tofauri, alivyotambulishwa na ujio wa mtu huyo vilikuwa vitu viwili tofauti.



ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment