Monday, March 20, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE



WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com





SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA!!
Kitendo hicho ilikuwa ni mpango kabambe uliokuwa umesukwa na ukasukika, wote walibaki wakitabasamu kwa kuweza kumtia nguvuni kwani tayari sifa zake walikuwa wameshazisikia kama alikuwa ni mjanja sana. Mwenyeji wake alinyanyuka pale kitini alipokuwa amekaa na alijongea hadi eneo ambalo Norbert alikuwa ameangukia, alimpiga teke la kumsukuma na kupelekea ageuke chali kwani alikuwa yupo kifudifudi.

"Simba hachezewi sharubu hata siku moja, sasa kakuparua na kucha"  ALiongea huku akimtazama mateka wake kwa dharau kuu.





________________________TIRIRIKA NAYO


           ILIVYOKUWA
   Homa ya matumbo ya kuhara aliyokuwa ameachia baadhi ya wale waliokuwa kwenye mtandao wa ufisadi katika siku iliyopita, ndiyo ilifanya Kamishna aweze kukutana na wenzao ambao walikuwa mtandao mmoja aliokuwa akiwajua. Walikuwa wamebaki wawili tu ambapo mmoja alikuwa ni huyo Katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi na mwingine alikuwa  ni Kardinali Michael, wote waliambiwa ikiwa ataingia kwenye eneo lao lazima wamuweke kwenye mtego akamatwe. Hilo ndiyo lilikuwa limefanyika bila ya Norbert mwenyewe kujua wala Waheshimiwa kuambiwa kwani haikuwa na umuhimu wa kuwaambia mtu huyo awe amewekwa nguvuni, Norbert alipoingia kwenye eneo la ofisi ambayo ilikuwa na mtego uliomnasa. Hakujua kabisa kuwa  tayari kulikuwa na mpango ambao ulikuwa umeundwa, alichojua ni lazima wale waliokuwa amewapitia jana watakuwa wamechnganyikiwa sana kiasi cha kushindwa kufukiria jambo jingine lolote. Hakujua mmmoja wao kati ya aliokuwa amewatembelea jana bado akili yake ilikuwa ipo sawa, ndiyo huyo aliyefanya mipango ya kila namna afute aibu aliyokuwa nayo.


  Alipofika kwnye ofisi ya Katibu Mukhtasi na kumuambia kuwa alikuwa akitaka kuonana na Katibu mkuu, hakujua kabisa kuwa kupewa taarifa Mhusika juu ya kuonana naye ilikuwa ni kama alikuwaa amempa muda wa kusuka mpango. Muda aliokuwa ameambiwa asubiri hapo nje, Mhusika mkuu huko ndani alikuwa akiwasiliana na mmoja wa kijana wao kuja kutekeleza kazi, Kijana huyo alikuwa ni yule Fundi aliyekuwa ameingia ofisini humo. Norbert bila ya kujua aliingia na hapo Fundi huyo aliyekuwa amejibana kwenye mlango alichukua kifaa muhimu sana miongoni mwa vifaa alivyokuwa amekuja navyo. Ilikuwa ni spana kubwa sana itumikayo kufungua koki za maji ndiyo alikuwa ameishika, windo lao lilipoingia kwenye anga zao kilichofuata ni ile spana ambayo ilishuka kwenye kisogo chake na kumpoteza fahamu zote.


****


    Haikupia muda mrefu tangu Norbert aanguke, Katibu Mukhatsi aliagizwa na bosi wake mahali na hapo akawa ametoka kwenye eneo lake la kazi. Yule Fundi aliitumia nafasi hiyo iliyokuwa imepangwa na Katibu mkuu kumchukua Teka lao na kisha akaondoka nalo katika eneo hilo, ilikuwa ni hila iliyokuwa imepangwa ya kumtoa yule binti mahali alipokuwa ili waweze kumtoa Norbert ofisini humo na ilifanikiwa.  Yule Fundi mhalifu alimshusha Norbert kwenye ngazi za dharura za ghorofa hiyo hadi chini, alimpakia kwenye gari lake alilokuja nalo hapo akiwa na mwenzake humo ndani.

 Baada ya kuingizwa tu humo ndani ya gari alifungwa kamba na kisha, akashikliwa barabara. Safari ya kuondoka hapo wizarani ndiyo ilianza baada ya kazi hiyo kukamilika, ilikuwa ni kitendo ambacho kilikuwa kimefanywa kwa kimyakimya na hakikujulikana na mtu yeyote hyule adi wanaondoka kwenye eneo hilo baada ya kukamilisha kazi yao iliyokuwa imewaleta hapo.



*****



   Fahamu zilikuja kumrudia Norbert akajikuta yupo ndani ya chumba ambacho kilikuwa na giza sana, alikuwa kafungwa kwenye nguzo moja ndefu sana mithili ya mtu aliyekuwa amesulubiwa msalabani. Mkononi ma miguuni kwenye nguzo hiyo alikuwa amefungwa kamba ngumu sana ambayo ilimuumiza mikono kutokana na kukazwa sana, alipoangaza ndani ya chumba hiko bado hakuwa ameujua alikuwa yupo wapi. Akili ilipokuja kumkaa vizuri alikuja kujua kuwa alikuwa yupo ndani ya chumba ambacho kilikuwa na giza sana, alijua kabisa kuwa alikuwa aameingia mtegoni katika siku ambayo hakutarajia kabisa kuwa angeweza kuingia mtegoni kinamna ile.

  Moyoni alijilaumu sana kwa kufanya kosa la kujiamini kupita kiasi alipoingia ndani ya ofisi hiyo, aliona laiti asingejiamini namna ile basi hayo yasingemkuta kabisa na angeweza hata kujikomboa kutoka kwenye balaa ambalo limempata tayari. Alikuwa yupo ndani ya chumba hicho ambacho kilikuwa hakina dirisha hata moja na kufanya humo ndani kuwe na joto kali sana, giza la humo ndani alipolizoea alikuwa kujua kuwa ilikuwa ni sehemu ya ghala au chumba kimojawao ndani ya kiwanda ambako hakukijua ni kipi. Alikaa ndani ya  chumba hicho kwa muda ambao hakuujua kabisa, alikuja kujua kuwa muda ulikuwa umekwenda sana baada ya njaa kuanza kumsumbua kwenye tumbo lake lakini hakujali kabisa.  Aliendelea kukaa kwenye mazingira hayo huku nguvu tayari zikiwa zimeanza kumuishia, ulikuja kufunguliwa mlango katika muda ambao hakuujua na hapo alibaini kuwa giza lilikuwa tayari limeingia kutokana na kuonekana hakukuwa na dalili ya mwanga huko nje. Alijua kabisa kuwa chumba hiko alichokuwa amefungiwa kuwa mlango wake haukuwa ndani ya kabisa baada kusikia mlio wa magari ukisikika nje, mlango huo ulipofunguliwa aliona kundi la watu wale waliokuwa wamepatwa na homa ya kuhara aliyokuwa ameisambaza wakiingia humo ndani wakiwa wameongozana na Kamishna. Bi Kishimba,Kaitbu Mkuu waizara ya nishati na madini, Bwana Mushi na yule Katibu mkuu wa wazara ya uchukuzi walipomuona tu walitoa matabasamu yao tu.

"Kaila umeona matokeo ya ukaidi wako sasa, siku nzima upo humu ndani na hujala chochote" Kamishana aliongea huku akimsogolea karibu.

"Na hutokula humu ndani uishiwe nguvu na ufe hapohapo, hatutaki kukuua na mikono yetu sisi, yote kwa ubishi wako tu yaani ungekubali hata upokee hongo yetu na uachane na huo upuuzi wako ungekuwa upo mtaani sasa hivi unadunda" Bwana Mushi naye alimsema

"Sawasawa handsome mwenye mvuto, dawa ya mabinti leo hii utaishia hapo kwenye nguzo kwa ukaidi wako wa kijinga tu. Eti unakataa hela kisa uzalendo wewe, wazalndo na walikuwa kina Hayati Sokoine kijana wangu na nataka ufe huku ukijifunza kuwa upekuzi si mzuri" Mrs Kishimba aliongea


"Yaani wewe hujui kitu wewe kuhusu hii nchi unajifanya wewe mjuaji sana yaani, tumesoma kwa shida kwenye udogo wetu huku tukishuhudia ulanguzi uliotupa tabu sisi wa chini. Sasa tumeipata nafasi kwanini tusijivunie  wewe, nataka ujue uzalendo hakuna sasa hii nipesa tu" Katibu Mkuu wa wizara ya  uchukuzi aliongea, muda huohuo yule Katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini aliyetaka kumpiga risasi alisogelea karibu huku akicheka sana.

"Niambie Jet li wangu, si wewe jana uliyeipiga bastola yangu teke na kisha ukaruka pembeni kama unacheza The bodyguaard. Kiko wapi sasa, unaishia kufa kwa upumbavu wako tu. Yaani wenzako waliokuwa wakikaa kimya ulikuwa unawaona wajinga siyo sasa huo upelelezi wako na uandishi wakowa habari ni kwishinei" Katibu wa wizara ya nishati na madini aliongea kwa kejeli.


"Sijakataa nitakufa ndiyo ila inabidi mfikirie kwa umakini sana juu yenu, nani atapona hapo mnafikiri kuwa ndiyo mtapona hapo. Laptop zote tano zipo mikononi mwa Jama wa Majama. Mtu pkee aliyebakia kati ya watu waliofanya utafiti wakajua kuhusu ufisadi wenu, na anayo ile yenye ripoti kamili. Mkumbuke ni  yeye tu anayeweza kuchambua lile neno siri sasa kazi kwenu" Norbert alionge maneno ambayo yaliwafanya wote waliokuwa humo ndani wakae kimya ghafla na wakaanza kutazamana kila mmoja kutokana na habari hiyo iliyiwaletea homa tena.


"Mimi na wenzangu tulipoitwa Wahanga hamkuwa mkijua maana yake sasa ndiyo hii, sisi ni waandishi tulio tayari kufa  na kwajili ya kuongea ukweli tu. Najua nitakufa  tu hapa nikifika kesho kwa  vidonda vya tumbo na njaa hii ila hilo mkubali kabisa mmekwisha nyinyi, ule ushahidi wenu mkiniomba rushwa upo kamili kwa wenzangu" Norbert aliongea huku akitia chumvi katika maneno yake, hakuwa ni mgonjwa ila aliamua awahadae kwani  wangekuwa wapo makini na yeye na hapo ndipo angeweza kuwazidi akili wote.

"Tunaondoka Kaila ila tutarudi na dawa yako" Kamishna alisema akiwa ameanza kubabaika na kisha alitoka ndani ya chumnba hicho, alifuatiwa na wenzake wote waliokuwa wameanza kuingiwa na unyonge kutokana na maneno ahyo waliyokuwa wameambiwa na Norbert aliyekuwa yupo tayari kwa lolote


****


   Ziliopita siku mbili hakuwa  amepata chakula na alikuwa akilalamika sana kuwa tuombo likimuuma, hakuwa aliyemsikiliza humo ndani. Baada ya kupiga kelele kwa muda mrefu sana hatimaye majira ya alasiri Norbert alionekana akiwa ametulia tu, walinzi waliokuw wapo eneo hilo walikuja kumuangalia na kuangalia pumzi zake hawakuona dalili ya kupumua kwake. Hilo lilifanya wote kwa pamoja wamshushe hapo alipokuwa amefungwa, walikuwa wakidhani kuwa alikuwa ameaga dunia tayari kumbe ilikuwa ni hila tu. Hakuwa na vidonda vya tumbo wala  vya utumbo, walipomuweka chini alianza kizaazaa ingawa hakuwa na nguvu vizuri kutokana na kutokula kwa siku mbili. Alianza kuwachota wote wawili kwa miguu yake aliyozingusha kama feni, walipanguka aliwawahi kila mmoja katika shingo zao.


  Mmoja alimbana na miguu na mwingine alimkamata na mikono yake, ingawa hakuwa kabisa na nguvu  hakutaka kabisa kuachia shingo zao hao watu hadi pale walipotulia kuashiria hawakuwa na uhai. Hapo alijinua huku akimpekua mmoja na kuchukua funguo za humo, alifanikiwa kutoka nje ambapo alijikuta akiwa yupo ndani ya ghala ambayo alikuwa akiijua vymea. Ilikuwa ni ghala ambayo ilikuwa ipo maeneo ya Mwembeyanga, kule ambako Josephine alijaribu kumtia nguvuni kwenye kisa cha WAKALA WA GIZA akashindwa. Norbert alipotoka nje tu ya ghala hiyo kwenye sehemu ambayo alikuwa amefungiwa aliuendea uzio wa nyumba hiyo kwenye upande ambao ulikuwa upo karibu na paa la kibanda kidogo kilichokuwa kipo nyuma ya Ghala hiyo. Alipanda hicho kibanda na kisha akashika ukuta na kutoka nje akiwa yupo  na uchafu mwingi sana, hapo alijikongoja kwa taratibu sana kwani hakukuwa na umbali mkubwa kutoka pale alipokuwa akiishi ingawa hakuwa akijulikana kama alikuwa na nyumba  maeneo hayo. Alifanikiwa kufika Temeke alipokuwa akiishi  na aliingia ndani ya nyumba yake, baada ya kuingia  ndani kwake alishusha pumzi kwa kuweza kutoroka kule ambako alikuwa amewekwa mateka.



****


  Ndani ya siku ilikuwa ni siku ya jumatano ambapo siku mbili tu zilikuwa zimebaki katika muda aliokuwa amepewa Norbert, pia ilikuwa ni siku ambayo Rais Zuber kwa mara ya mwsiho atalala nje ya Tanzania kabla hajarejea nchini siku inyofuata. Ndani ya siku hii agizo jingine lilitoka kwa Rais akiwa yupo nje kabla hajarudi nchini. Agiza hilo lilikuwa ni kuzuia hati zote za kusafiria wa watumishi wa umma mpaka atakaporudi, agiza hilo lilitangazwa kwenye vyombo vya habari jambo ambalo lilizdi kuwashangaza wengi hasa wale waliokuwa watumishi wa umma.


  Kikundi cha watu ambao walikuwa wamejiandaa waondoke nje ya chi mambo yakiwa mabay ilishindikana kabisa, siku ya Jumamosi kulitarajiwa  kulikuwa na ziara ya Rais wa marekani nchini hivyo hiyo ilikuwa imewekwa kuwa sababu kuu ya kuweza kuzuia. Watumishi wote wa umma walitakiwa waanze maandalizi mapema sana ya kuampokeaa Rais huyo ambaye mwenyeji wake alikuwa akitangulia siku inayofuata.

 Hilo lilikuwa ni suala ambalo lilipokewa vizuri kwa wafujaji uchumi ndani ya nchi hii, waliamini kabisa kuwa bajeti maalum ingetengwa kwa ajili ya ziara hiyo jambo ambalo walikuwa wakilisubiria kwa hamu sana waweze kuzifuja pesa kwa mara nyingine kabisa. Wengine wale waliokuwa wakihusika walikuwa wameshateuliwa haraka sana na Makamu wa rais, hao waliambiwa kabisa kuwa Rais Zuber akifika tu mapema asubuhi ya siku inayofuata alikuwa akitaka sana kuongea nao  baada ya kupumzika na uchovu wa safari.


  Ilikuwa ni neema kabisa kwa wafujaji hao kwani waliona walikuwa wakifuja kwa mara ya mwisho kabla ya kutoroka, waliamini kabisa siku yeyote bomu walilokuwa wakilizuia lisilipuke lingelipuka kutoka na kuwa lilikuwa lipo mikononi mwa watu mwingine kabisa. Walikuwa wakikaa na furaha wakiingojea kwa hamu sana hiyo siku ya kuja huyo kiongozi mwenye jina kubwa duniani ili waweze kujichumia kupitia ujio wake. Waliamini kabisa kuwa serikali ingetenga bajeti kubwa sana kwa ujio wake huyo kwa shughuli mbalimbali na kwakuwa walikuwa wameaminiwa wao waliona ni nafasi yao.



****




  Majira ya jioni Norbert alikuwa amesharudiwa na nguvu zake ambazo hazikuwepo hapo awali kutokana na kukosa mlo, alikuwa ameshapata mlo stahiki ambao ulirudisha nguvu zake zilizokuwa zimepotea. Alikuwa pia amehsajisafisha mwili wake kutokana na kuka siku mbili bila kujisafisha, baada ya hapo alitoka na kwenda kule ambako alikuwa amemuacha Jama Wa Majama akiwa amejificha kuwa muda huo ambao hali ya hewa ya usalama wake ilikuwa imetibuka. Alimkuta akiwa yupo kama alivyomuacha, walipoonana kitu cha kwanza kuulizwa iikuwa ni kutoonekana kwake. Jambo hilon diyo alikimbilia kuulizwa kutokana na kuadimika sana, Norbert ilimbidi atumie wasaa huo kumueleza kila kitu ambacho kilikuwa kimemkuta hadi akawa namna hiyo.

"Ule ni mtandao mpana Kaila uujue hivyo na hawaingiliwi tu" Jama alimueleza

"Kujiamini sana huondoa umakini naamini sitolifanya kosa hili tena" Norbert aliongea

"Sasa mpango upo vipi maana Mheshimiwa anateseka tu bila ya hatia yeyote ile"

"Kuwa na subira Jama mpango kila kitu ni kesho kutwa leo hii wewe pumzika mimi ninaenda kuimaliza kazi"

"Ok ila majamaa hawajakufinya wale"

"Hawajanigusa hata eti walitaka nife kwaa njaa nikawa natafuta golden ndiyo hiyo nimeipata"

"Uwe makini sana"

"Hilo usihofu kabisa ndugu nipo makini sana" Baada ya kuongea maneno hayo Norbert alinyanyuka na kisha akasema, "nina kiporo cha kuifanya hapa, baadaye panapo majaliwa ndugu"

"Hamna shida ndugu"

   Baada ya kuagana hapo alitoka hadi nje ya nyumba hiyo akiwa hajatumia usaifri wowote ule, hesabu yake yote ilikuwa ni kwenda kuichukua ile Pikipiki yake ambayo alikuwa ameiacha kule wizarani katika muda huo kwani aliamini kabisa haitokuwa imeondolewa eneo lile kutokana na ulinzi ambao inao.


****


"Jamani mambo magumu huko" Kamishna aliongea majira ya jioni kwenye kikao walichokuwa wameitana kwenye chumba cha hoteli

"Kuna nini Kamishna?" Bi Kishimba aliuliza akiwa hajaelewa kabisa, swali hilo lilifanya wengine nao waulize kwani alionekana kuwa na uso ambao umechachawa kabisa.

"Kaila ametoroka kule na kaua walinzi wawili" Aliwajibu wote huku akionekana kachanganyikiwa sana

"Ooooh! Sasa atatuvua nguo huyu jamani" Bwana Msuhi aliongea akionekan kuchoka kabla hajachoshwa kwaa taarifa hiyo aliyopewa hapo

"Mushi come down  bado muda upo, tujue jinsi gani tunaweza tukaokoka hapa na pia tumnyamazishe huyu" Katibu wa wizara ya uchukuzi aliongea

"Enhee  Shija umeongea hapo si muda wakukata tamaa huu, bado tuna nafasi ya kumshikisha adabu huyu mtoto tusimuhofie kisa yeye ni Mpelelezi wa daraja la juu. Tunaye Askofu naye ni dawa tosha kwake" Kamishna aliongea


ITAENDELEA!!
   

No comments:

Post a Comment