Sunday, December 13, 2015

SHUJAA SEHEMU YA TISA


RIWAYA: SHUJAA


MTUNZI: Hassan O Mambosasa

SIMU:+255713776843
+255762219759


WHATSAPP:+255713776843


FACEBOOK PAGE LINK:  www.riwayamaridhawa.blogspot.com







SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE


ILIPOISHIA
Upeo mkali wa macho ya Norbert uliweza kumtambua mzungu huyo ambaye ndiye aliyekuwa
amefanya akae katika mgahawa huo, sasa alihitaji jambo ambalo alilipanga kulifanya na ikamlazimu
kusubiri hapo mgahawani. Kinywaji chake alikiona hakina maana tena zaidi ya kufanya jambo
lilimuweka hapo, alisubiri gari hilo lilipoondoka kwa umbali wa mita kadhaa kisha akalipa kinywaji chake
halafu akaenda hadi alipoegesha gari yake. Aliingia kwa haraka kisha akaliwasha halafu akaliingiza
barabarani kufuata uelekeo ambao ile range rover imepita kwa mwendo wa kasi, baada ya mwendo
mfupi aliikuta ikiwa ipo katika mwendo wa kasi baada ya barabara ya eneo la Msasani kuwa tupu.





ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI YAKE




 SEHEMU YA TISA!!
Bado walikuwa wapo mtaa wa Mahando ambao ndio mtaa wenye makazi ya Dkt Mbungu, Norbert aliifuatilia gari ya Scott kwa namna ambayo ni ngumu kujulikana kama anamfuatilia. Akiwa ameacha umbali wa mita nyingi ambao ulimsaidia kufanya Scott na dereva wake wasimuhisi chochote, mwendo alioutumia ulikuwa ni wa wastani ulikuwa haushindi mwendo wa gari ya mbele yake. Utumiaji wa mwendo wa namna hii ulisababisha Norbert asiweze kuikaribia gari ya mbele yake, umakini wake katika kulifuatilia gari la mbele yake ulizidi kuwa mkubwa. Gari alilomo Scott liliingia kulia lilipofika mtaa wa Tosamaganga kuifuata barabara inayoenda kwenye barabara ya Haile Selassie, lilienda kwa mwendo mfupi kisha likakata kona kuingia kushoto katika barabara ya Haile Selasie kisha likaongeza mwendokasi wake. Norbert naye alikuwa analiungia mkia kwa namna ya kipekee na gari hilo lilipoingia barabara ya Haile Selasie yeye alikuwa nyuma kwa umbali wa mitaa kadha akiwa ameyaacha magari mawili yakiwa yametangulia mbele ya gari hilo, aliongeza mwendokasi wa gari akiwa yupo makini sana na muelekeo wa gari hilo. Walipofika mgahawa wa Gastro Garden magari mawili yaliyopo mbele ya gari ya Norbert yaliingia hapo na kumfanya Norbert awe nyuma ya gari ya akina Scott kwa umbali wa mita kadhaa, hapo Norbert alihisi upo uwezekano watu waliomo ndani ya gari hiyo ya mbele  kuhisi kama wanafuatiliwa. Hivyo alihitajika afanye jambo kuwapoteza akili watu na wahisi hali ya kutofuatiliwa, akiwa nafikiria jambo la kufanya tayari walikuwa wamefika Shopers plaza iliyopo kando ya barabara ya Haile Selassie. Norbert akikata kona kuingia Shopers plaza halafu akaelekea yalipo megesho ya magari.  Alisimamisha gari katika maegesho hayo kisha akatoa simu yake ya kiganjani , alibonyeza baadhi ya vitufe vya simu hiyo kisha akaiweka sikioni.

"hey Simion tukutane pale pa siku zote na uje na gari yako" aliongea kisha akakata simu kisha akaiweka, aliwasha gari kisha akatoka eneo la Shorpers plaza. Aliingia tena katika barabara ya Haile Selasie kwa kuelekea upande wa kushoto kisha akaongeza kufuata ili aliwahi gari alilokuwa analifuatilia, baada ya mwendo mfupi alilikuta gari la akina Scott likivuka makutano ya barabara ya Haile Selassie na ile iendayo mtaa wa Mwaya. Gari hiyo iliendelea kufuata barabara ya Haile Selasie kwa mwendo wa kasi huku Norbert akiwa bado yupo nyuma yake, ilipokuwa ikikaribia barabara ya hiyo na ya kaole Norbert aliongeza mwendo kisha akapandisha vioo vya gari yake ambavyo ni vya giza.Aliipita gari hiyo kwa mwendo mkali kisha akawa yupo mbele yake huku taa ya njano ya upande wa kushoto kuashiria anaingia  kushoto ikiwa imewashwa, alikata kona kuingia  kushoto katika mtaa wa Lincolin kwa kuitumia barabara ya Kaole kisha akaenda mbele kwa umbali mfupi na kupelekea atokee katika barabara iliyopo upande wa kulia. Barabara hiyo ambayo inaelekea katikati ya mtaa wa Lincoln ilikuwa pembeni yake kwa muda huo, likata kona kuingia kulia kisha akatembea kwa umbali mfupi halafu akaegesha gari pembeni ya barabara mbele ya toyota harrier ya rangi nyeusi yenye vioo vya giza. Norbert kwa haraka kisha akatembea hadi kwenye mlango wa dereva wa toyote harrier, aliufungua mlango wa dereva wa gari hiyo ambayo dereva wake alikuwa ndani yake.

"Simion ingia kwenye gari yangu halafu unifuate" alimwambia dereva gari hiyo ambaye alitii mara moja.  Simion aliingia ndani ya gari ya Norbert na Norbert akaingia kwenye gati yake kisha safari ikaanza. Wote kwa pamoja walielekea barabara hiyo moja kwa moja kisha wakakata kulia walipofika katika barabara ya Chole wakielekea yalipo makutano ya barabara hiyo na ya Haile Selasie, walikata kona kuingia kushoto kisha wakaongeza mwendo wa magari ya yao.


****



Amani ndani ya moyo wa Scott ilipotea muda mfupi tu tangu alipoliona gari aina ya suzuki ya rangi nyekundu ikiwa nyuma yake tangu alipoiona kwenye mtaa wa Tosamaganga ikimfuatilia. Wakati wapo barabara ya Haile Selasie ndipo alipozidi kuitilia shaka gari hiyo kutokana na kuonekana inamfuatilia kwa mbinu za hali ya juu za kiusalama. Kijana huyu mwenye mafunzo ya kijasusi aliijua mbinu hiyo ya kufuatiliwa ambayo  isingejulikana na mtu wa kawaida, gari hilo lilipoingia  Shopers plaza aliliona na akajiridhisha kwamba halimfuatilii yeye. Amani katika moyo wake ilirudi ingawa haikudumu kwa muda mrefu, amani hiyi iliondoka tena baada ya kuliona gari lililokuwa likimfuatilia likiwa nyuma yake. Hapo aligeuka nyuma kisha akaitazama vizuri lakini hakufanikiwa kumuona dereva wa gari hiyo.

"hii gari huko nyuma nina wasiwasi nayo" Scott alimwambia dereva.

"usijali bosi ngoja tuingie Ally hassan mwinyi road halafu  nitajua nishughulike naye vipi" Dereva alimtoa wasiwasi  huku akiangalia kwa umakini kwenye vioo vya pembeni halafu akasema "huyo hapo anatupita". Scott alipoangalia upande wa dereva aliiona ile gari ikiwapita kisha ikawasha taa kiashiria ya upande wa kushoto kuashiria inaingia kushoto, gari ile iliingia katika barabara ya Kaole kwa mwendo wa wastani.

"nadhani tumeweka dhana mbaya" Dereva aliongea.

"si dhana mbaya ila kujihami muhimu maana huenda nikawa najulikana na mtu yoyote" Scott alimwambia.

"nadhani hakuna anayekujua bosi maana ndio kwanza una siku mbili" Dereva alimwambia.

" tusijiaminishe kitu tusichokijua namna hiyo" Scott alimwambia. Hawakuiona ile gari tena hadi wanaingia mtaa wa Chabruma kwenye makutano ya barabara ya Haile selassie na barabara ya Alli Hassan Mwinyi ndipo walipoiona ikiwa ipo nyuma ya toyota harrier ya rangi nyeusi . Walipoingia barabara ya Ally Hassan Mwinyi waliiona ikiwa ipo nyuma ya toyota harrier, dereva wa Scott aliitazama ile gari vizuri kisha akatoa simu yaken Alibonyeza baadhi ya vitufe kisha akaiweka sikioni.

"nataka niwakute kwenye mataa ya mtaa wa Morocco kisha muifuatilie gari aina ya suzuki escudo ya rangi nyekundu ambayo ipo nyuma yangu ikiwa imeacha gari moja mbele. Nataka mumpe utamu derevs wake". alikata simu kisha akamtazama Scott halafu akamwambia "kazi imeisha sisi turudi maskani tu".  Scott alitabasamu kisha akakubali kwa kutikisa kichwa chake, furaha yao ilizidi pale walipokuwa wanayavuka mataa ya Morocco  wakiingia barabara ya Bagamoyo baada ya kuwaona vijana wao wa kazi wakiwa wameegesha gari yao pembeni.

"vijana wa kazi hao hapo si tuwe na amani tu" Dereva alimwambia Scott akiwa ametabasamu. Wakiwa wanaendelea na safari yao ile gari ya vijana wao ilikuwa ipo nyuma ya suzuki ya Norbert inayoendeshwa na Simion. Hadi wanawasili mataa ya Mwenge tayari walikuwa wana uhakika kuwa ile gari inawafuatilia, kwenye mataa ya Mwenge walikuta taa za upande wao zimewaka nyekundu hali iliyowalazimu kusimama kutii sheria. Wakiwa hapo macho yao yote yalikuwa kwenye suzuki waliotilia shaka ambayo sasa ilikuwa imeingia kwenye barabara ya Sam nujoma ikiwaacha hapo kwenye mataa wakisubiri waingie njia ya Bagamoyo. Hadi muda huo hawakuwa wameitilia shaka toyota harrier iliyokuwa ipo nyuma yao kwenye foleni hiyo ya mataa, waliwaachia kazi vijana wao waitekeleze wao wakawa  wamekaa kiamani.


****


                   MLIMANI CITY
                 DAR ES SALAAM



Gari aina ya toyota altezza ya rangi ya njano iliegeshwa kwenye maegesho ya magari ya mlimani city kisha milango ya gari hiyo ikafunguliwa, miguu ya rangi ang'avu inayoelekea kuitwa meupe ilitangulia kugusa ardhi ya eneo la Mlimani city kisha viatu virefu vya rangi nyekundu vikaifanya miguu hiyo ionekane  ipo ghorofani. Mabinti wawili wenye uzuri wa asili walionekana wakishuka ndani ya gari hiyo, kimuonekano tu kwa kuwatazama walionekana walikuwa ni ndugu. Magauni ya kufanana waliyoyavaa yaliwafanya waonekane ni mapacha kutokana na kufanana kwao, macho ya vijana wakware ambao wapo hapo kwa ajili ya kuonekana na macho ya warembo yalinasa upande walioshuka mabinti hao. Victoria na mdogo wake Beatrice ndio hao mabinti walioingia , waliingia moja kwa moja ndani ya
 mlango ulioandikwa game wakiacha mjadala nyuma yao ukiendelea.  Pembeni ya mlango walioingia mabinti hawa kulikuwa kuna kundi wavulana waliokuwa wamevaa mavazi ya kileo.

"wana hizo totoz mmezisoma" mmoja wa wavulana hao aliongea.

"dah! Aisee mungu kajua kuumba, watoto kama mlango wa msalani hawaujui"  Mwingine akaongea kuwasifia.

"naona hamjipendi nyinyi" mmoja mwingine aliwaambia.

"Kevi acha uoga wewe, kwani wake za watu wale" aliyesimama karibu na kijana aliyeitwa Kevi aliongea.

"mnamjua Bernard Mutashobya" Kevi akawauliza

"daah yule mzee mkuda aliyemtupa mwanafunzi wa UD ndani kisa anamkaa mtoto wake" Kijana aliyekuwa anawasifia Beatrice na Victoria aliongea.

"sasa hawa ndio watoto wake na huyo mmoja anaeonekana ni mrefu kuliko mwenzie ndiye huyo demu aliyesababisha jamaa akalala ndani na baadaye akaihama nchi. Sasa kama hamjitaki nyinyi vamieni msala huo" Kevi aliwapa onyo kisha akaanza kutembea kuelekea mahali lilipo geti la kuingilia.

"wana kama ndio hao watoto wake basi mi najipenda sana" kijana aliyeanza kuwaonesha wenzake wakina beatrice aliongea kisha akaongoka kumfuata Kevi huku wenzake wakiwa nyuma.


****

Safari ya Scott na dereva wake iliishia kwenye nyumba ya kifaharii iliyopo maeneo ya Bunju, muda wote huo Norbert alikuwa nyuma yao na hata walipoingia pembeni ya barabara kisha wakaenda kwenye nyumba hiyo iliyojitenga na makazi ya watu tayari aliwaona na ikamlazimu kupita sehemu hiyo  kwa umbali mrefu kisha akaenda kupumzika katika sheli iliyopo Bunju huku akijaza mafuta ya gari hiyo, alipomaliza aliondoka kurejea alipotoka baada ya kuwa na uhakika wa kuwapumbaza Scott na dereva wake kwa chenga ya mwili aliyowapiga. Hakuwa na wasiwasi na Simion ambaye alijua kama anafuatiliwa, Norbert anamtambua Simion kama mtu mjanja kupitiliza na aliwahi kuponyoka katika mikono ya hatari kwa kucheza  na akili zake tu.


***



Baada ya kuingia barabara ya Sam nujoma Simon aliitazama gari ya vijana waliotumwa na dereva wa Scott kisha akatabasamu, alikanyaga mwendo kuifuata barabara ya Sam nujoma huku akicheka mwenyewe. Aliuvuka mzunguko wa barabara uliopo jirani na Mlimani city kisha akaifuata barabara ya Sam nujoma hadi kwenye makutano ya barabara hiyo na barabara ya Igesa inayoelekea Sinza makaburini ambapo aliiacha barabara ya Sam nujoma kisha akaingia barabara ya Igesa. Aliifuata barabara moja kwa moja kisha akakata kona ya pili iliyopo upande wa kulia ambayo ilimpeleka hadi kwenye nyumba moja ya ghorofa yenye geti jeusi, alipiga honi mara moja na kupelekea geti lifunguliwe kisha akaingiza gari ndani akiangalia nyuma kupitia vioovya pembeni. Watu waliotumwa kumfuatilia walipitiliza moja kwa moja baada ya kujua eneo ilipoingia hiyo gari, Simion aliingiza ndani hadi kwenye maegesho ambapo alipokelewa na binti mmoja mrembo.

"bibie jiandae kuna watu nimewaingiza choo cha kike, kwahiyo tarajia ugeni leo wa wageni wanaohitaji sebene"  Simion alimwambia binti huyo huku akifunga milango ya gari.

"dah sijacheza siku nyingi sebene sasa tarajia wageni hao watapata dansa la nguvu" Binti huyo alijibu kimafumbo kama alivyosemeshwa na Simion.




****


               JIONI

           MIKOCHENI
       DAR ES SALAAM


Sauti ya muziki mlaini ndiyo iliyokuwa ikiwaliwaza watu wachache waliopo katika viti vilivyopambwa vizuri katika bustani nzuri ya majani, mbele ya viti hivyo kulikuwa kuna meza kubwa iliyopambwa kwa namna ya kuvutia ikiwa ina viti vitatu vilivyonakshiwa na mapambo ya vitambaa vyenye rangi taofauti. Nje ya geti la nyumba hiyo kulikuwa na walinzi waliovalia suruali nyeusi pamoja na shati jeupe lenye tai ya kipepeo inayoning'inia shingoni mwao, mandishi mbalimbali yakumtakia Beatrice sikukuu njema ya kuzaliwa ndiyo yalikuwa katika mabango mbalimbali yaliyomo humo ndani.

ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment