Monday, December 14, 2015

SHUJAA SEHEMU YA KUMI


RIWAYA: SHUJAA


MTUNZI: Hassan O Mambosasa

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



ILIPOISHIA

              JIONI
          MIKOCHENI
     DAR ES SALAAM

Sauti ya muziki mlaini ndiyo iliyokuwa ikiwaliwaza watu wachache waliopo katika viti vilivyopambwa
vizuri katika bustani nzuri ya majani, mbele ya viti hivyo kulikuwa kuna meza kubwa iliyopambwa kwa
namna ya kuvutia ikiwa ina viti vitatu vilivyonakshiwa na mapambo ya vitambaa vyenye
rangi taofauti. Nje ya geti la nyumba hiyo kulikuwa na walinzi waliovalia suruali nyeusi pamoja na shati
jeupe lenye tai ya kipepeo inayoning'inia shingoni mwao, mandishi mbalimbali yakumtakia Beatrice
sikukuu njema ya kuzaliwa ndiyo yalikuwa katikati mabango mbalimbali yaliyomo humo ndani.





ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO








         SEHEMU YA KUMI!!
Eneo la maegesho la nyumba hilo lilianza kujaa magari ya aina mbalimbali ya waalikwa wa sherehe hiyo, asilimia kubwa ya wageni waliopo ndani ya sherehe hiyo walikuwa ni vijana kutokana na sherehe hiyo ilikuwa inamuhusu kijana  wa kike. Wavulana watanashati na wenye kunukia uturi wa kila namna ndio walionekana, wasichana wenye mavazi ya kisasa pamoja viatu vya gharama nao waliifanya sherehe hiyo ionekane ni yenye kuvutia. Hadi muda huo Beatrice alikuwa yupo katika chumba anacholala akiwa amezungukwa na marafiki zake na wa marafiki wa dada yake, mavazi ya kisasa na yenye kupendeza ndio yaliyoonekana kupamba miili ya marafiki hao pamoja na mhusika wa sherehe hiyo. Beatrice alipendeza mithili ya malaika aliyeremka ndani ya siku hiyo, gauni fupi lililoishia kwenye mwanzo wa mapaja yake lilikuwa limemkaa sawia, mtindo wa nywele alioutengeneza mchana wa siku hiyo alipokuwa saluni nao ulimpa kigezo cha kuwa msichana mrembo. Kiatu kirefu cha rangi nyekundu ambacho kiliubeba mguu wake wa wastani na wenye kuvutia, rangi ya nyekundu ya gauni lililoishia kwenye mabega yake lilimfanya aonekane ni  msichana aliyeshushwa na si kutoka katika kifuko cha uzazi cha mwanamke. Kupendeza kwa binti huyu hakukuweza kuelezeka kwa maandidhi wala kwa maneno ukapamaliza, mimi mwandishi wa simulizu hii nimechukua vipengele hafifu vya kuelezea kupendeza kwa Beatrice ndani ya siku hiyo na laiti ningelieleza kwa kirefu ningaliweza kumaliza makaratasi saba ya maandishi.

"Shosti leo lazima huyo Mose anase hapa maana mtoto unalipa sana" Mmoja wa marafiki wa marafiki wa Beatrice aliongea kumsifia kutokana na kupendeza huko.

"nakwambia leo shem wangu lazima adate akikuona tu" Irene ambaye ni msichana wa Hilary aliongea.

"He! Heee! Angalia angalie asidate yeye Bite kachizika kwake" Msichana mwingine aliongea na kumfanya Beatrice amtazame huku akicheka.

"mmh! Marry unanianika sasa" Beatrice  aliongea kwa  kunung'unika. Muda huo wote wakati Beatrice na mashoga zake wanaongea kuhusu huyo kupendeza kwake, Victoria na marafiki zake wawili ambao majina yao ni Lailat na Annie walikuwa wskiwasikiliza huku wakitabasamu.

"Bite kwani huyo Mose yupoje maana umekuwa crazy lover" Lailat aliuliza baada ya kuona Beatrice akiwa na kila dalili ya kumpenda kijana huyo anaezungumziwa tena kuliko kawaida.

"yaani shosti namsubiri kwa hamu nimemuona huyo anaedrive moyo  wa mdogo wangu leo, picha hainitoshi kumpa alama za mvuto kwake" Victoria naye aliongea.

"mmmh! Sis nawe unazidi sasa" Beatrice aliongea kwa sauti ya deko.

"sio nazidi ila umekuwa crazy lover kwa ajili yake, nitajudge hadhi yake na muonekane wake unafanana na wewe  na wewe kuwa hivi" Victoria aliongea zaidi.

"shosti hebu leo  tumuone huyo handsome boy akiingia" Annie ambaye ni rafiki wa Victoria naye alidakia kisha akageuza shingo kuangalia mlangoni baada ya kitasa cha mlango huo kuzungushwa.

"jamani wote mpo huku bado nusu saa tu sherehe ianze, kwanini msishuke sitting room ili mjiandae kuingia eneo husika" likuwa sauti ya mama yake Beatrice kisha akaonekana  akiwa amesimama mlangoni.

"Mammy! We are coming(mama tunakuja)" Victoria alimwambia mama yake.

"do hurry my daughters thirteen minutes remaining(fanyeni upesi mabinti zangu dakika thelathini zimebaki) Mama Beatrice aliongea kisha akafunga mlango.

***

Wakati  Mama Beatrice akiwaambia Beatrice na dada yake pamoja na rafiki zake wafanye haraka, Moses na Hilary walikuwa wapo getini ndani ya gari aina ya BMW ya kisasa. Muda huo walikuwa wanawaonesha walinzi kadi za  mualiko kisha wakaingia ndani baada ya kufunguliwa geti, Moses ndiye alikuwa dereva kwa muda huo, walipofika kwenye maegesho Hilary alitoa simu kisha akampigia Irene na aliiweka sikioni baada ya simu kuanza kuita.

"honey tumefika tayari......yes baby tupo eneo la parking kwenye BMW nyekundu.....ok we are waiting for you" Hilary aliongea na Irene kwenye simu kisha akakata baada ya kumaliza kuongea nae. Alimkamata bega Moses kisha akamuambia "jombaa Irene anakuja sa subiri aje ndio tuingie nae, au unasemaje?!"

"haina mbaya jombaa tusubiri hiyo sketi" Moses alijibu kisha akamuambia Hilary, "we mwanga vipi kwa viwalo mtoto atanataje?".

"aisee mwana kwa hivyo viwalo leo umetupia wacha nikupe sifa, ila angalia usije ukawa kipendezo cha madada leo"  Hilary alimwambia Moses. Baada ya muda mfupi Irene alifika eneo la maegesho ya magari akiwa na muonekano ambao ni mvuto kwa Hilary, wote walipomuona waliishuka garini  na kufanya mavazi waliyovaa yaonekane vizuri. Hilary alikuwa amevaa shati ya rangi ya bluu yenye kuteleza na suruali ya rangi ya maziwa pamoja na kiatu cheupe, Moses alikuwa kavaa shati ya rangi nyekundu iliyomuonesha umbile lake la kimazoezi na suruali nyeusi yenye kitambaa cha kuteleza pamoja na kiatu cheusi. Irene alimkimbilia Hilary na kumkumbatia kwa furaha huku mabusu motomoto wakawa wanashushiana, wapenzi hawa walimsahau Moses aliyekuwa amesimama pembeni yao.

"mmh! Mmmh!" Moses aliguna ili awashtue hawa wapenzi hawa na akafanikiwa kuwashtua wakarudi katika hali ya kawaida.

"Heee! Shem mambo?!" Irene alisabahi Moses kwa kumkumbatia.

"poa tu, za hapa" Mosea aliitikia salamu.

"safi tu, jamani hebu twendeni hivi kwnza kisha ndio tuingie eneo la party"  Irene aliwaambia huku akiuvuta mkono wa Hilary kuelekea kwenye mlango wa nyumba ya ghorofa ambayo ndiyo makazi ya akina Beatrice, Irene aliwaongoza hadi mlangoni kisha akafungua akiwaambia, "karibuni". Mandhari ya sebule pana ndiyo iliyowapokea na viti vilivyokaliwa na mabinti wa rika tofauti ndiyo  walipamba sebule hiyo kwa kukaa juu ya makochi ya kisasa yaliyopo, mabinti waliokuwepo sebuleni hapo walimtazama Moses kutokana na uzuri wa sura yake pamoja na muonekano wake. Beatrice alikuwa kaupa mgongo upande aliokuwepo Moses na hakuwa na taarifa za ujio wa Moses, ule uzuri ambao unanishinda mimi mwandishi kuumaliza kuuelezea ndiyo ulimfanya Moses aduwae. Kitendo cha yeye kupewa mgongo na  Beatrice kilimfanya Moses apate fursa ya kukitazama kiuno cha Beatrice pamoja na fungashio lililopo chini ya kiuno lililofunikwa na gauni iliyomkaa vema,  Beatrice hakuwa amegeuka hadi muda huo. Irene ndiye alimfanya ageuke baada ya kumuambia, "Bite suprise for you".

"Waooooow! Moses" Beatrice aliongea baada ya kugeuka huku akimkimbilia Moses kisha akamkumbatia kwa hisia kali, joto la binti huyu lilipenya katika maungio ya Moses. Moses alijjkuta akimkumbatia Beatrice kwa hisia.

"khaa! Hiyo salamu inatosha, tusalimie na wengine handsome boy" Victoria aliropoka baada ya kuona mdogo wake amekumbatiwa kwa muda mrefu. Beatrice alimuachia Moses huku akimwambia dada yake, " mmmh! Sis".  Moses alianza kuwasalimia wote kwa uchangamfu huku Hilary akiwa nyuma yake akiwasalamia kama alivyofanya mwenzake. Msichana wa mwisho kumsalimia alikuwa ni Annie rafiki wa Victoria, hapo Moses alianza kuhisi jambo kutokana na kituko alichokionesha huyo msichana ambaye ni mkubwa kwake kiumri na hata kidaraja la kielimu. Annie aliutekenya mkono wa Moses pale alipopeana naye mkono kisha akamkonyeza kwa haraka, baada ya kuwasalimia wote Moses alimfuata Batrice kisha akamwambia "Ikiwa  kwa muonekano huu ungekuwa unaonekana kila siku mithili ya nyota iliyopo angani, basi anga lote lingeonekana kama mchana kwa muda wa usiku ambao ungejitokeza kwa sababu unang'aa. Bite now I'm seeing angel in front of me me(Bite sasa ninaona Malaika mbele yako), siwezi kusema upo kama malaika bali wewe ni malaika mbele ya macho yangu. Umependeza sana". Maneno hayo aliyatamka akiwa kasimama akiangaliana naye uso kwa uso,  wasichana wote waliopo eneo hilo walipiga makofi huku Hilary akiishia kutabasamu.

" oooh! Nilitaka nisahau sasa, Happy birthday" Moses alikumbuka kumtakia furaha ya sikukuu ya kuzaliwa Beatrice. Hilary alibaki akimshangaa Moses ndani ya siku hiyo kutokana na kutokuwa na aibu mbele ya mabinti kama ilivyo kawaida yake, hakujua rafiki yake huyo alipatwa na siku hiyo ya leo hata asiwe na aibu. Beatrice alimkumbatia Moses kwa mara ya pili huku wengine wakiwa wanwatazama kama hadhira ya  igizo la jukwaani, Moses alikuwa ni burudani tosha kwa waliopo kwa mabinti hao.

"halafu we mdog wangu ndio nini hata kutambulishana ni vigumu, ameishia kutusalimia tu hata hatujamjua  wala hajatujua sisi ni wakina nani. Bite ndio kupagawa huko" Victoria alimwambia Beatrice kwa kuonesha lawama za magizo.

"mmh! Sis, ok ngoja niwatambulishe this guy is Moses Lawrence Gawaza. Ni zaidi ya rafiki kwangu, yule ni rafiki yake anaitwa Hilary Wilson. Moses yule pale muongeaji sana ni dada yangu  anaitwa Victoria na wale wawili ni marafiki zake, yule pale ni Annie na yul nj Lailat. Nadhani hawa wengine unawafahamu"  Beatrice alitoa utambulisho wa watu waliopo sebuleni hapo akiwa ameweka mkono katika bega la Moses.

"jamani sie tupo hapo ukumbini" Hilary alisema huku akiwa ameshika kiuno cha Irene.  Hilary na Moses walitoka nje ya nyumba hiyo kwa pamoja wakiwa na Irene, nyuma ilibaki minong'ono juu ya wavulana hao walionekana watanashati mbele ya macho ya wasichana hao.

****

  Watu wa kuaminika waliotumwa na dereva wake Scott majira ya saa moja jioni walikuwa wapo nje ya nyumba ambayo Simion aliingiza gari la Norbert, ilipotimu saa moja na robo jioni waliuruka uzio wa nyumba hiyo kwa lengo la kumuangamiza Simion baada a kuwa na uhakika ya uwepo wake ndani ya nyumba hiyo. Vijana hawa wapo sita wenye bastola ziitwazo FN 5.7 za nchini Ubelgiji zenye uwezo kupiga risasi umbali wa mita 1510, viwambo vya kuzuia sauti ndiyo vilikuwa vipo mbele ya bastola zao ili kuzuia zisitoe sauti. Walijigawa kwa makundi mawili walipoikaribia mlangovwa nyumba hiyo, watatu walibaki mbele na watatu walizunguka mlango wa nyuma ya nyumba hiyo. Kiongozi wa vijana hao alizunguka mlango wa mbele akiwa na vijana wawili na msaidizi wake alizunguka mlango wa nyuma akiwa na vijana wengine wawili. Wote kwa pamoja walifanikiwa kuingia ndani ya nyumba hiyo ambayo ilionekana ni haina dalili ya uwepo wa mtu, walikuwa wakiwasiliana kupitia simu zao ndogo walizopachika ndani ya sikio.

" Eddy pako clear huku sijui kwako" Kiongozi wa hao vijana alimuuliza msaidizi wake kwa sauti ya chini kupitia simu zao za mawasiliano.

"Joe ni clear kwa upande wa jikoni naona hakuna dalili za kuwepo mtu"  Eddy ambayo ndiye msaudizi wa kikoai hiko alijibu. Wote walikutana katikati ya sebule ya nyumba hiyo na hawakuona dalili ya uwepo wa mtu, hapo  ndipo walipoanza kuangalia picha zilizopo hapo sebuleni kwenye ukuta.

"tumekwisha jamani tukichelewa kutoka humu ndani" Joe aliongea huku akiangalia picha ya mwanamke iliyopo ukutani katika nyumba hiyo, alianza kutembea kuelekea mlangoni.

"Joe kuna nini mbona sikuelewi?" Eddy aliuliza.

"kama hii nyumba ni ya Luteni kanali wa JWTZ ambaye ni komandoo wa kuaminika  unafikiri tukikaa hapa tutakuwa hapa si tutajisogeza karibu na kifo" Joe aliongea.

"nini?" Eddy aliuliza.

"huyo malaya kwenye hiyo picha ni komandoo wa JWTZ na ni hatari kama tuki...." Joe alishindwa kumalizia kauli yake baada ya umeme wa ndani ya nyumba hiyo kuzimika, giza lilichukua nafasi yake hadi wakawa hawaonani. Vishindo vya kupigwa mtu vilisikika kisha mmojammoja akaanza kutoa ukelele wa maumivu kisha ananyamaza, Joe na Eddy ndio watu pekee  waliosalia bila ya kusikika sauti ya maumivu ikitoka midomoni mwao.

"Frank!.... Elius!....Ramso!.....Dick! Mpo wap..." Joe alijikuta akiropoka lakinj hakumalizia baada ya kusikia ngumi ikitua katika mdomo wake kisha bastola yake ikapigwa teke, Eddy naye alijikuta akipigwa teke mkono alioushika bastola hadi bastola ikaruka pembeni.Taa za umeme ziliwaka na kilichopo eneo hilo kikawa kinaonekana dhahiri, yule binti aliyempokea Simion mchana wakati anaingia hapo ndani ndiye aliyeonekana na ndiye sura yake ilikuwa kwenye picha hapo ukutani. Simion naye alikuwepo eneo hilo upande wa ukutani jirani na swichi kuu ya umeme, yeye ndiye aliyezima umeme wa nyumba hiyo.

"wageni mnataka disko la aina gani labda" Yule binti aliwauliza Joel na Eddy ambao walikuwa kimya na hawana ujanja kutokana na  kuingia katika anga za mtu wasiyemuweza.

"Belinda ngoja niwachagulie maana naona wamepagawa na personality na mcheza shoo aliyepo mbele yao" Simion aliongea. Joe alitambua wazi kama ameingia anga za mtu mwenye uwezo kuliko wa kawaida lakini hakutaka kukubali kushindwa kirahisi namna hiyo, neno mwanamke kumshinda kijinga aliona ni tusi zito zaidu ya kuambiwa amelawitiwa.
Ili ajithibitishe ni kidume hataki kuwa kifo cha kikondoo mbele ya mbwa mwitu mmoja, alikunja ngumi huku akimfuata Belinda kwa mapigo ya karate ya nguvu. Mapigo yote yalikosa lengo baada ya Belinda kuyakwepa kwa kupiga sarakasi iliyompeleka pembeni ya eneo alilosimama awali lililopo jirani na sehemu aliyopo Eddy, Eddy naye aliamua kujiunga kwenye mpambano huo kwa kupiga teke la kuzunguka ambalo lilipita hewani bila kumpata mlengwa huku mguu wake aliosimamia ukichotwa na Belinda aliyeinama chini kukwepa teke lake. Eddy alijikuta akianguka kwenye meza ya kioo iliyopo sebuleni hapo, huo ndio ukawa mwisho wake baada ya kisogo chake kupigiza kwenye meza hiyo. Joe naye alikuja na mateke mfululizo yaliyorudishwa na  pigo la mateke mawili kutoka kwa  Belinda hadi akaanguka jirani na ilipo bastola mojawapo iliyopigwa teke awali na Belinda. Kitendo cha yeye kuiona bastola hiyo alijua ni nafasi yake ya mwisho kummaliza Belinda, aliiokota kisha akamnyoosha kwa lengo la kumlenga Belinda lakini alijikuta akiachia ukelele wa maumivu huku bastola akiiachia ikaanguka. Alipoangalia mkononi mwake aliona kisu kikiwa kimezama kiganjani mwake na ndicho kilimfanya aachie bastola aliyoishika.

"nina kawaida ya kutembea na kisu kiunoni kama tahadhari, ndiyo ambacho nilichokuchoma mkononi ili usisambaratishe ubongo wa malkia wangu"  Simion aliongea baada ya kumrushia  kilichomchoma Joe mkononi kisha akamgeukia Belinda halafu akamwambia, "bibie mchezeshee mtindo wa hardcore ili aipate burudani".  Baada ya Belinda kuambiwa hivyo aliachia mateke mfululizo ambayo yalimpata Joe kifuani kisha akaivunja shingo ya Joe kwa mapigo ya kombati ya shingo, huo ndiyo ukawa mwisho wa Joe kuwepo duniani.


*****

 Saa mbili kamili ilipowadia sherehe ya kuzaliwa kwa Beatrice ilianza kwa kumkaribisha Beatrice eneo la sherehe kwa muziki wa taratibu ulioimbwa na Conway Twitty wa marekani ndio uliokuwa unaimbwa na mmoja wa mtu aliyekuwa hapo kwenye sherehe. Watu walipiga makofi kufuatisha mdundo wa mziki huo huku mwimbaji akiwa anasikika sauti tu, 'happy birthday darlin' ndio jina la nyimbo uliokuwa ukiimbwa na mtu mwenye sauti ya kuvutia. Hadi Beatrice anaketi kwenye  kiti alichoandaliwa wimbo huo uliendelea kuimbwa na muimbaji alikuwa yupo katikati ya kundi la watu waliomzunguka wakati akiingia mahali hapo, watu hao waliomzunguka ni miongoni mwa waalikwa wa sherehe hiyo.

" Well you can say why he didn't give me anything
but he sure took a lotta things away
     Happy birthday darlin'...
      Happy birthday darlin'...
       Happy birthday darlin"

Muimbaji wa nyimbo hiyo alipomaliza kuimba beti za mwisho za nyimbo hiyo, watu waliomzunguka walitawanyika na kufanya sura yake ionekane kwa Beatrice huku watu wakipiga makofi kwa shangwe. Beatrice aliishia kutabasamu baada ya kumuona muimbaji akiwa ni Moses, hakujua ratiba ya ile sherehe ilipangwaje maana ni jambo lilikuwa la kushtukiza kwake na lililomfurahisha.



ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment