Thursday, December 3, 2015

KOSA SEHEMU YA MWISHO







HASSAN O MAMBOSASA

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



 ILIPOISHIA
Nurulayt aliunyanyua ule mzigo wote kwa kutumia ile mashine ya kubebea mizigo akauingiza ndani ya helikopta kisha akaingia ndani  akakaa sehrmu ya rubani akaniambia, "panda twende".
" unaweza kuendesha helikopta?" Nilimuuliza.
"hebu wacha maswali yako panda bwana wanakuja hao"  Nurulayt aliniambia na muda huo huo tukasnza mtikisiko ambo unatokea ikipita treni, nilipanda kwenye helikopta haraka sana nikiwa nimekaa mlangoni kwa tahadhari. Nurulayt aliwasha helikopta na aliipandisha juu baada ya kuanza kuchanganya huku akiiongoza kuelekea mashariki ili aiache kambi hiyo. Helikopta ilipokuwa juu kabisa wale watu walikuwa wameshafika pale kwenye uwanja  ilipokuwa imeegeshwa, walianza kutupa risasi lakini Nurulayt aliongeza mwendo akawaacha.


MALIZIA MKASA HUU WA KUSISIMUA WENYE KUFUNDISHA


SEHEMU YA MWISHO!!
Baada ya kukivuka kikwazo hicho kwa mara nyingine nilijikuta nikimshukuru Mungu kwa kunifanya niwe mzima hadi muda huo tangu nilipojiweka katika mdomo wa mamba katika kambi ile, siiutarajia kama nitaweza kutoka na kuiba katika kambi ile yenye ulinzi na wapiganaji hodari sana wanaotumia silaha. Nilipomtazama Nurulayt kule mbele nilimuona yupo makini sana kuiongoza helikopta kwa mwendo wa kasi, tulikuwa tumeshaiacha  kambi kwa umbali mkubwa hata ukitumia darubini utaiona kwa mbali sana na hatukuwa na wasiwasi na wale vijana wa Gorilla zaidi ya kusonga mbele.
"GRIIIIIIIII!   GRIIIIIIIIIIIII!  GRIIIIIIIIII! "  Mlio wa  simu ulisikika katika mfuko wa suruali yangu ambao ulinishtua sana kwani nilishasahau kama nilikuwa nimebeba simu kabisa katika tangu mara ya mwisho kuitumia siku ile niliyokutana na Nurulayt tangu tupoteane miaka mitano iliyopita, mlio huo pia ulimshtua Nurulayt na kumfanya atazame nyuma kwa mshangao.
"Abdul umekuja na  simu tena ipo loud, huoni kama ingekuwa ni hatari kwako" Nurulayt aliniambia huku akitazama mbele kwa umakini.
"sikujua kama nina simu kwani nilishasahau kabisa" Nilimwambia huku niitoa ile simu nikaiangalia kwenye kioo na nikakuta mpigaji ni yule yule anayenipa kazi za ajabu tangu nijikute nipo Namibia.
"ipokee basi au kama hutaki izime" Nurulayt aliniambia akionekana kukerwa sana na simu niliyonayo jinsi inavyoita kwa fujo, sikuwa na jinsi kwani nisingeipokea ingekuwa ni hasara yangu na kama ningeipokea ingekuwa ni afadhali kwani sikujua huyu mtu anayejiita F.A.Z anataka kuniambia nini. Niliipokea nikaiweka sikioni bila ya kusema chochote ili nimsikilize yeye.
"Napenda niwapongeze kwa kufanikiwa kuiba almasi niliyowatuma pia naomba nikupongeze kwa kufanikiwa kutolewa hardware zangu mgongoni mwako na huyo malaya wako mkijua sitajua upo wapi  ilihali unayo simu  niliyokupatia mimi mwenyewe yenye Global positioning system yaani GPS, sasa basi hujaweza kunifanya nisijue uliopo Abdul hiyo GPS ya kwenye hiyo simu imeunganidhwa huku nilipo katika kompyuta zangu sasa nitajua ulipo hata uhame bara hili. Kwanza tuachane na hayo kwenye hii simu kuna ramani inayokuelekeza sehemu ya kupeleka mzigo huo sasa mpe huyo malaya alete mzigo unapohitajika, pia kumbukeni helikopta hiyo ina mafuta pungufu sasa  mkijifanya mnazunguka sana jua imekula kwenu na ninahitaji mzigo huo haraka sana" Yule mtu alinipa maelekezo kisha simu ikakatwa, sikuwa na jinsi ikabidi nimuoneshe ramani hiyo Nurulayt na nimuelekeze kila kitu Nurulayt nilichoambiwa. Nurulayt alitii maelezo na safari ya kurudi sehemu iliyooneshwa ndiyo ikaanza kwa mwendo wa kasi ili tuwahi kufika eneo hilo, baada ya saa moja nilihisi helikopta ikianza kushuka taratibu na nilipoangalia chini nikaona alama ya H ya rangi nyeupe ikiwa ipo juu ya ghorofa mojawapo katika mji nadhifu sana ambao sikuujua unaitwaje hadi muda huo.
"Nuru hapa ni wapi?" Nilijikuta nikimuuliza Nurulayt.
"ni Widhoek hapo  au umepasahau kabisa" Nurulayt alinitajia sehemu hiyo ambayo ndiyo mji mkuu wa Namibia tuliouacha hapo awali, sikuweza kuutambua kutokana na muonekano wake  kwa juu kwani ulikuwa ni tofauti sana. Nurulayt aliishusha helikopta hadi ikatua katika alama ile ya H iliyokuwa juu ya ghorofa mojawapo ambalo niliwaona watu wengi walioshika silaha zao wakiwa wapo hapo, Nurulayt alipozima Helikopta tulishuka na kisha tukasimama mbele ya mmoja wa watu tulipwakuta hapo ambaye alitusogelea akaanza kutupekua nguo zetu achukua silaha zetu zote.
"why( kwanini)?" Nilimuuliza yule mtu aliyetupekua
"you are going to meet our Boss,  weapon are not allowed. Follow me (mnaenda kukutana na bosi wetu, silaha haziruhusiwi. Nifuateni)" Yule alituambia kisha akaelekea pembeni ya eneo hilo ambalo kulikuwa na tundu kubwa kama mlango lenye ngazi zinazoingia ndani ya ghorofa hilo, tulimfuata tukiwa tumefuatwa nyuma na vijana wawili wenye silaha nzito sana. Tulishuka ngazi hizo hadi chini kisha tukaufuata ukumbi mwembamba uliotupeleka hadi kwenye mlango wenye kamera kwa juu yenye taa juu yake kama ile ya kule kambini kwa vijana wa gorilla, yule mtu aliyetukagua aliisogelea ile kamera kisha akasema "they are here Boss( wapo hapa Bosi)". Aliposema hivyo alinivuta mkono na kunisogeza karibu na ile kamera  huku akiniambia "your face ( sura yako), niliinua uso  wangu nikaitazama ile kamera huku kengele maalum ikilia na mlango ukafunguka. Tuliingia ndani tukiwa tumeongozana na wale watu na tukatokea katika ofisi pana yenye mandhari ya kuvutia pamoja na milango minne tofauti, mbele yetu  kama mita sita kulikuwa kuna meza yenye mafaili kadhaa pamoja na kiti cha kuzunguka kilichotupa mgongo.
"kaeni kwenye makochi hapo" Sauti ile iiliyokuwa ikinipa kazi nisizozipenda ilitoa  amri ikitokea katika kiti kile cha kuzunguka kilichotupa mgongo, tulikaa katika makochi yaliyopo jirani nasi yakiwa mita sita kutoka pale alipo.
"Abdul, Nurulayt hatimaye tunakutana leo hii" Aliongea yule mtu huku akuzungusha kiti kuangalia tulipo na hapo ndipo nilipoibaini sura yake halisi na nikajikuta nikishtuka sana, Nurulayt naye alishtuka sana kwani alibaini yupo ndani ya himaya  ya hatari.
"FAIZ ni wewe kweli" Niliongea huku nikinyanyuka nikataka kumfuata lakini nulishtushwa na milio ya kukokiwa  bunduki  na  nilipoangalia pembeni nilitazama na bunduki mbili aina ya SPAS-12  kutoka kwa wale  watu tuliyoingia nao, sikuwa na jinsi niliishia kukaa tu palepale huku tayari nikiwa najua kilichonifanya niwe pale.
"kinachowashangaza ni kipi nyinyi? Faiz kuwa hai sio? Mlidhani atakufa kwa hila zenu mlizozifanya nyie wasomali. Abdul yaani uko radhi kujaribu kumuua rafiki yako kipenzi kisa mwanamke ambaye hakupendi mwenye mapenzi na rafiki yako kisa una pesa tu, kakwambia nani pesa inaleta mapenzi mpaka ufanye haya. Ilivyopita miaka kumi ulidhani limeisha sio?" Nilikaripiwa na nikajikuta nikiinama chini baada ya kushindwa kumtazama kutokana na maneno makali aliyokuwa anayatoa hadi machozi yakawa yanamtoka.
"Faiz nisamehe rafiki yangu" Nilijikuta nikiomba msamaha.
"wa kuniomba msamaha ni mimi kwani, muombe Faiz mwenye huruma ya kusamehe ila mimi huwa sisamehi" Yule mtu ambaye nilijua ni Faiz alitoa kauli inayoonesha kukana kama yeye siyo Faiz.
"wewe kama si Faiz ni nani?" Nilimuuliza.
"mimi ni Fauz  Ally Zaid kifupi F.A.Z  au Scorpio pacha wa Faiz Ally Zaid  niliyeikimbia nchi yangu nikiwa na mdogo wangu Khalid na nikazamia Afrika ya kusini kutafuta maisha na nikayapata kama haya niliyokuwa nayo kwa tabu na dhiki nikiwa nina uhakika wa kuja kuipa maisha bora familia yangu lakini wewe ukaivuruga familia hiyo kwa jeuri ya pesa zako ambazo hujui zinatafutwa vipi. Pesa hizo za ulizorithi umeona ni bora uwalipe wale waasi wa Kongo wamteke Fauz halafu wawambie familia yetu walete nusu tani ya almasi  kutoka katika himaya yangu mwenyewe iliyo chini vijana wangu Gorrila boys, unajua matokeo yake ni nini?...........Baba yangu Mzee Ally Zaid aliyekuwa ni mwanajeshi mstaafu akaamua kwenda kujaribu kuiba hiyo almasi akajikuta anauawa kikatili huku nikiwa sijui kama vijana wangu wamemuua bsba yangu mzazi alipokuwa ana harakati za kumkomboa mwanae,   Abdul............Abdul nilijiapiza lazima ulipie kwa kukuonesha hiyo pesa inatafutwaje kama ulivyotembea na wale wanawake  ili kupata dola milioni moja za kimarekani na kuiba hizo almasi ili mfe kama mlivyosababisha baba yangu afe lakini mmepona kwasababu Mungu bado anawahitaji nyinyi mashetani" Aliongea huku machozi yakimtoka  na mwili ikimtetemeka kwa hasira, alipoacha kuongea mlango mmojawapo ukafunguliwa na akaingia mtu aliyetokea kuwa rafiki yangu mkubwa na pia meneja wa makampuni. Khalid Zaid ambaye yule niliyemshuhudia akiwaeleza  waandishi wa habari kuwa nipo masomoni ndiye aliyeingia huku akitoa tabasamu pana sana, nilibaki nikishangaa sana kwani sikutarajia kabisa kama nitakutana naye huku kutokana na kumuamini sana.
"Khalid na wewe pia?" Nilijikuta nikiongea kwa mshangao.
"huyo anaitwa Khalid Ally Zaid na unamfahamu kama kama Khalid Zaid  kwani huwa hatumii jina la kati na Faiz hatumii jina  lake la mwisho, nilimtuma kwa ajili ya kukamilisha kazi hii na ukamuamini bila ya kutambua unamuamini Nyoka" Fauz aliongea huku Khalid akitabasamu.
"huyu ndiye aliyekuwa anakupeleleza na hata siku ile uliyochukua binti ambaye ni mfuasi wangu uliyeamini ni changudoa yeye ndiye aliyeusuka mpango ule mpaka ukanyonya matiti ya yule binti anayeitwa Angel aliyoyapakaa madawa ya kulevya ukalala. Pia huyuhuyu ndiye aliyekupasua mgongoni akakufunga hardware ukiwa hujitambui baada ya kunusishwa Klorofomu ukatupwa kwenye kisiwa katika bahari ya Antlantiki siku nne baadaye na ya tano ukajikuta  umelala ufukweni" Fauz aliongea  tena kunifahamisha juu ya Khalid, muda huohuo mlango mwingine ulifunguliwa na akaingia mtu aliyekuwa anaendeshwa kwenye kiti cha matairi  na msichana ambaye sikuweza kumtambua kabisa. Walifika hadi eneo aliposimama Khalid wakiwa wamevaa kofia zilizoziba nyuso zao kwa sehemu kubwa.
"Abdul umefanya kosa lililozaa maafa mengine bila ya kujijua kwa kutumia jeuri ya pesa zako na wewe ndiyo cha huyu mtu aliyekaa kwenye kiti cha matairi ashindwe kutembea tangu nampata, nadhani huyu hujamtambua ni nani ngoja umuone" Fauz alisema kisha akamfunua kofia yule aliyekaa  kwenye kiti cha matairi.
"Faiz!" Niliropoka baada ya kuiona sura ya Faiz kwa mara nyingine baada ya miaka kumi kupita, Faiz alikuwa ananitazama kwa uso uliojaa na hasira sana huku akiachia tabasamu lisiloashiria furaha katika uso wake.
"unashangaa kuniona nipo hai sio fedhuli mkubwa we?" Faiz aliongea akiwa na hasira sana kisha akamgeukia kaka yake akamuambia, "Kaka ulipokimbia nyumbani ukiwa na mdogo wetu nilikuona huna maana ndiyo maana hata chuo na shuleni nilisema nimezaliwa peke yangu kumbe nina pacha wangu, nimeingia chuo nikapata rafiki nikamuona ana maana kumbe hana maana kwani ametumia watu waniteke na wamenichoma sindano ya sumu ambayo inanifanya niwe katika kiti cha matairi hadi leo hii. Ama kweli umdhaniaye ndiye kumbe siye, huyu baradhuri nilimuona  anafaa kumbe hafai na nikakuona wewe hufai kumbe ndiye unafaa, Fauz huyu mtu namchukia sana" Faiz aliongea huku akitokwa na machozi, mimi mwenyewe machozi yalianza kunitoka kutokana na kujuta sana kutokana na mambo niliyomtendea rafiki yangu tukiwa chuo ingawa machozi hayakuweza kubadilisha ukweli wa jambo hilo liwe halijatokea.
"Faiz nisamehe rafiki yangu nimekosa" Nilimuomba msamaha Faiz  huku nikinyanyuka ili walau nikapige magoti mbele yake anielewe lakini nilishindwa kwenda kutokana na kuwekewa bunduki kwa mara nyingine nilipotaka kwenda. Nilirudi nikakaa chini nikamtazama Nurulayt ambaye alionekana pia kujuta kwa kile alichomfanyia Faiz.
"Abdul tafadhali sana naomba usiniite rafiki yako na ukitaka nikusamehe mlete Huwaida hapa  kwani nilimtumia email nilipokombolewa na anajua juu ya uovu wako na kama huwezi  sitakusamehe, namtaka mpenzi wangu tu kwani sijui umemficha wapi hadi sasa" Faiz aliongea huku uso wake ukiwa umetawaliwa na hasira, nilipisikia hilo suala ikabidi nimtazame Nurulayt kisha nikasema, " Faiz haiwezekani jambo hilo kwani Huwaida niliyempenda na aliyekupenda wewe tayari ni marehemu kwa sasa".
"What! Hapanaaaa" Faiz aliongea kwa uchungu kisha akaanza kulia kwa uchungu huku mishipa ya damu ya kichwa ikiwa imemtoka, nilimuonea huruma saba ingawa chanzo cha yote nilikuwa ni mimi.
"Abdul  kama Huwaida kafa basi mwnao lazima afe kwa namna yoyote" Faiz aliongea kwa uchungu.
"Kifo cha Huwaida ni mimi ndiye mhusika  na si Abdul wala  mtoto wetu Ilham na kama unataka kuniadhibu niadhibu ila kaka yako Fauz lazima pia naye alipe kwa kumuua Sabir kaka yangu aliyekuwa rafiki yake na mshirika na kuhusika kwangu katika kutekwa kwako nilikuwa nalenga Fauz na sio wewe" Nurulayt kwa mara ya kwanza aliingilia kutokana na kusikia suala la kutaka kuuliwa Ilham, maneno hayo yalimfanya Fauz atabasamu.
"Alaa kwahiyo umemfanya kaka yangu awe mtu wa kutembea kwa baiskeli kisa mimi kumuua Sabir na ukadhani yeye ni Fauz, sikulaumu sana  najua umekosea kufananisha kwa jinsi tunavyofanana......Sabir alikuwa ni rafiki yangu sana ila amenigeuka  kwa kuuwa watu wangu pia kutaka kumuua mdogo wangu kwa bomu, hivi ungekuwa wewe mtu kama huyu utamfanyaje?" Fauz aliongea na mwisho akamuuliza swali Nurulayt lililomfanya ashindwe kujibu na pia akajiona  ana hatia sana kwa kufanya kile anachokifanya, Faiz alipoona Nurulayt ameshindwa kujibu swali lake alitoa ishara moja ambayo sikuielewa. Mlinzi mmoja mwenye bunduki alisogea mbele baada ya kutolewa ishara ile kisha akampatia bunduki Faiz, Faiz naye aliishika ile bunduki akaelekeza tulipo kisha akaifyatua ikatoa mlio niliousikia. Kuusikia mlio wa bunduki nilitambua haijanipiga mimi kwani bunduki ikikupiga husikii mlio wowote, nilipomuangalia Nurulayt niliona sindano yenye manyoya kama mshale wa mchezo wa dart ikiwa imemchoma begani mwake. Nurulayt aliutia ule mshale kisha akautupa chini na akabaki akiugulia maumivu, nilipomtazama Faiz nilimuona akitabasamu kisha akanielekezea bunduki mimi akiwa makini sana. Hapo mapigo yalianza kwenda mbio na ikanibidi nifumbe macho tu nikusubiria nitandikwe , mlio wa bunduki niliusikia kwa mara ya pili nikafumbua macho nikamuona Faiz akitabasamu.
"Abdul sioni kosa lako lolote lililobakia kwani umejifunza vya kutosha ila huyo mwanamke ana kosa ndiyo maana nimemuadhibu, kosa lako kubwa ilikuwa ni kutoa pesa katika mpango wa huyu mwanamke hivyo umepata funzo hiyo pesa ya urithi uliyoitoa katika mpango huo inatafutwaje" Faiz aliongea huku akinitazama halafu akamegukia Nurulayt akamuambia "Nuru hiyo ndiyo ulistahiki kwa kuhukumu watu bila kujua kama upo sahihi au haupo, sindano zilizo ndani ya bunduki hii zina sumu ambayo ikiingia kwenye damu huponi na itakuua taratibu kuanzia kiungo  kimoja baada ya kingine hadi unakata roho". Faiz alipomaliza kuongea hivyo nilijikuta nikilia baada ya kusikia Nurulayt kachomwa sindano ya sumu na nikamkumbatia ingawa yeye hakuonesha kuhuzunika hata kidogo. Baada ya kusema maneno hayo Faiz alimgeukia Fauz akamwambia, " hii inawatosha wape vitu vyao", Fauz naye alitii na akamuita kijana wake mmoja akampa mkoba ambao alikuja kunipatia. Niliupokea  mkoba huo nikaufungua   nikakuta hati za mali zangu zote pamoja na kadi zangu za benki, niliufunga mkoba huo kisha nikatulia nikawa nawatazama ndugu wale watatu.
"Niliwaambia waandishi kuwa upo masomoni nadhani sasa muda wa masomo umeisha na umepata funzo sasa upo huru, tupatie kila tulichokupatia" Khalid aliongea huku akitabasamu, nilipoambiwa hivyo nilitoa simu nikamrushia naye akaidaka.
"Abdul natambua kama wewe ni binadamu unakosea kwani hakuna aliyemkamilifu, hivyo nimekusamehe wewe na mwenzako.....Nurulayt naomba unisamehe sana sikuwa na jibsi zaidi ya kufanya hivyo nilivyokufanyia na napenda mtambue mtoto wenu yupo nyumbani kwa Sarina mama yake wa kambo, guards take them to the room" Faiz aliongea
Walinzi walituchukua wakatutoa nje ya chumba hicho wakatupeleka chumba kingine kilicho na nguo tofauti za kike na za kiume, huko tulioga na tukabadilisha nguo kisha tukashuka hadi chini na tukachukua teksi iliyotupeleka hadi nyumbani kwa Nurulayt ambapo tulipanda gari yangu nilipewa tukaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa Sarina. Tulifanikiwa  kufika na tukashuka tukaingia ndani ya uzio kisha tukagonga mlango wa mbele tukasubiri kufunguliwa, baada ya dakika kadhaa Sarina alifungua mlango na alinikumbatia kwa furaha baada ya kuniona nimerejea nikiwa mzima. Nurulayt alikaribishwa ndani na hapo tukamsimulia kila kitu hasa juu ya Ilham kuwa ni mwanangu. "Waar is Ilham?( Yuko wapi amelala)" Nurulayt aliuliza akiwa na shauku ya kumuona Ilham
" lê(amelala)" Sarina alimjibu lakini Nurulayt alitaka amuone Ilham tu kwani hakuwa amemuona kwa miaka mitano, ilimbidi Sarina amuelekeze chumba kilipo na Nurulayt akaenda akituacha tukiongea . Aliporejea alikuwa amembeba Ilham ambaye tayari alikuwa ameamka, huku akionekana kuwa ana furaha kwa kumuona mtoto wake kwa mara nyingine.
"Anko umerudi?" Ilham aliongea aliponiona nikiwa nimejea.
"wewe sio anko yule ni baba, umesikia? Haya nenda kamsalimie  baba " Nurulayt alimuambia Ilham
"ok mummy" Ilham alijibu halafu akaja kunikumbatia akiwa na furaha na mimu nikiwa na furaha kwa kumjua mwanangu.
"Sarina...dankie(Sarina......asante) Nurulayt alimshukuru Sarina kwa kumtunzia Ilham, Sarina alitabasamu kuonesha amekubali  shukrani ya Nurulayt.

Nilikaa kwa Sarina kwa siku kadhaa kisha nikaenda hadi Walvis kwa rafiki yangu Jonas nikamchukua hadi nyumbani kwa Sarina, baada ya wiki mbili nilikuwa nipo Tanzania nikiwa na Sarina, Ilham, Nurulayt pamoja na Jonas ambaye nilimpatia nyumba na mtaji kama shukrani kwa msaada wake kwangu nilipokuwa nina shida aliponiokota ufukweni. Miezi miwili iliyofuata nilifunga ndoa na Sarina hapahapa Dar es salaam iliyohudhuriwa na watu mbalimbali na sherehe kubwa ikafanyika katika moja ya hoteli ninazozimiliki, furaha yangu ya kuwa na mwanamke ninayempenda  katika ndoa  ilitimia kuanzia siku hiyo.
Baada ya miezi mitatu tangu nifunge ndoa na Sarina hali ya kuafya ya Nurylayt ilianza kubadilika kwa baadhi ya viungo kushindwa kufanya kazi na  akipolekwa hospitali ilibainika tumechelewa kwani sumu ilishasambaa mwilini kote na hakukuwa na tiba ya kumuokoa, Nurulayt aliugua kitandani kwa muda mrefu sana hadi Sarina anapata ujauzito yeye alikuwa bado ni wa kitandani. Sarina alipojifungua watoto mapacha wa kiume ambao niliwaita Haasan na Hussein yeye bado alikuwa kitandani, baada ya miaka mitatu  tangu aanze kuugua Nurulayt aliaga dunia katika muda wa alasiri na  akatuachia huzuni na majonzi yaliyobaki moyoni mwangu na kunipelekea nitokwe na machozi kipindi naandika mkasa huu ulionikumba. Mungu amlaze pema mama wa mtoto wangu wa kwanza na binti yangu mkubwa kati ya watoto sita niliojaliwa na Muumba, nakumbuka mazishi ya Nurulayt niliteuliwa niingie kaburini kuipokea maiti lakini nilishindwa kutokana na kulia sana hasa nikimkumbuka katika kipindi chote nilichokuwa naye.

****

Walipomaliza ukurasa wa mwisho wa shajara hiyo Hassan na Hussein wote walijikuta wakitokwa na mschozi baada ya kujua mkasa uliomkumba baba yao pamoja na mama yao wa kambo ambaye kamzaa dada yao mkubwa.
"aisee mi Mariam simtaki tena hapa nimepata funzo tosha" Hassan aliongea huku akijifuta machozi.
"kweli pesa haileti mapenzi na pesa ibilisi" Hussein aliongea huku naye akijifuta machozi.
"wanawake wapo wengi nitatafuta mwingine ngoja nimuache jamaa awe naye ili niepuke kufanya kosa kwani alichokifanya baba kimenipa funzo tosha" Hassan aliongea huku akimtazams Hussein.
"kaka hapo umeamua na umefanya busara kubwa sana, tafuta mwingine wazuri wapo wengi sana ndani ya dunia hii. Huwezi jua Mungu amekupangia  nani baada ya Mariam kuchukuliwa na jamaa cha msingi badili direction ya moyo wako tu" Hussein alimshauri Hassan.
"kweli kabisa hii diary imenifunza mengi kabisa, cheki time maana nasikia tumbo linanisokota kwa njaa" Hassan alimwambia Hussein. Hussein alichukua simu yake ya mkononi akaangalia saa na alijikuta akipigwa na mshangao baada ya kuangalia saaa.
"Ebwanaeh! Time imeenda sana saa kumi hii, hebu twende tukale kwanza" Hussein aliongea kisha akasimama akaelekea mlangoni ili aelekee sebuleni, Hassan naye alimfuata kwa nyuma.
Walipofika sebuleni walikutana na wazazi wao wakawasalimia kisha wakataka kwenda kwenye meza ya chakula lakini baba yao aliwaita na akawaambia wakae kwenye kochi.
"Hussein, Hasaan" Mzee Abdul aliita majina yao.
"naam Baba" wote waliitikia kwa pamoja.
"najua mmemaliza kusoma diary yangu wanangu, je Hassan bado unataka kufanya ulichodhamiria?" Mzee Abdul aliuliza
"hapana sitafanya nimejifunza pesa si lolote katika mapenzi" Hassan alijibu.
"vizuri, niliamua kuwaacha mjue maisha yangu nyuma ili mjifunze na nyinyi wanangu. Nafurahi mmejifunza na naomba mfuate hayo mliyojifunza, ukiona umekataliwa jua kuna kizuri unaandaliwa mwanangu sasa utafute anayekupenda ili uje kuwa kama mimi Abdul na mama yenu hapa Sarina" Mzee Abdul aliongea huku Bi Sarina akitabasamu.
"sawa baba tumekuelewa" walijibu kwa pamoja.
"nendeni mkale" Mzee Abdul aliwaruhusu watoto wake, Hassan na Hussein walielekea kwenye meza ya chakula wakiwaacha wazazi wao wakiongea.
"ujue mwanzo sikuliafiki suala la wewe kuwapa watoto ile diary wasome ila sasa naona upo sahihi kabisa Mume wangu" Bi Sarina aliongea kwa sauti ya chini kumuambia mume wake.
"unajua katika suala la kuwafunza watoto inabidi muda mwingine tuwe wawazi kwao ili wajue hasara za jambo hilo mke wangu" Mzee Abdul alimwambia mke wake.
"hakika mume wangu wewe ni baba bora kwa watoto wako" Bi Sarina alimwambia mume wake.
"hata wewe ni mama bora kwa watoto, nakupenda sana" Mzee Abdul aliongea.
"nakupenda pia mume wangu" Bi Sarina aliongea huku akitabasamu.
Tangu siku hiyo Hassan aliachana na habari za kutaka kumdhuru rafiki yake na akawa na urafiki naye.

   MWISHO!!

natumaini umejifunza mengi sana, maoni yako tafadhali kwa mtunzi wa riwaya hii

NDUGU MSOMAJI INABIDI UTAMBUE KUWA LIKE
YAKO NDIYO INIPAYO NGUVU YA KUANDIKA RIWAYA
HII, HIVYO LIKE ILI KAMA UPO PAMOJA NAMI.
COMMENT KAMA UNA USHAURI AU MAONI. USIPIGE SIMU KATIKA NAMBA HIZO HAPO JUU, UJUMBE MFUPI WA MANENO UNATOSHA


No comments:

Post a Comment