Sunday, December 6, 2015

SHUJAA SEHEMU YA PILI





  SHUJAA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA



SEHEMU YA PILI
Kujipitisha kwake katika madarasa ya sayansi hakukuzaa matunda yoyote, alijitahidi kumsalimja kwa uchangamfu ili awezs angalau kuzoeana naye. Salamu yake ilijibiwa kawaida na kila akitaka kujiweka karibu naye alishindwa  kutokana na umakini wa kijana huyo kwenye masomo uliomfanya awe hapendi na mabinti. Baada ya jitihada zote kushindikana kushindikana sasa alibuni mbinu mbadala ya kumfikishia ujumbe kijana huyo,  kila siku alikuwa akiwahi shule mapema kabla ya watu wote hawajafika. Muda huo wa asubuhi inayoifukuza alfajiri alikuwa  akiweka kadi mbalimbali za mapenzi katika meza ya kijana huyo, mchezo huu ulimchanganya sana Moses hadi akawa anawauliza wanafunzi wenzake kama anamjua. Kila akijaribu kuwauliza wenzake juu ya jambo hilo aliambulia patupu pasipo kumpata anayemchezea mchezo huo, hali hiyo iliendelea kila siku huku mtumaji akiwa anajiita dream girl.  Hali hiyo ilizidi kuendelea kila siku  anapoingia darasani asubuhi, "be a man(kuwa mwanaume) Mose vitu hivyo havilaziwi damu hata siku moja" mmoja wa wanafunzi alimwambia Moses  baada ya kumuona kila siku akilalamika juu ya tukio la kuletewa kadi na mtu msichana asiyemtambua.  Hali hii ilizidi kuendelea na sasa akawa akikaa kantini muda wa mapumziko analetewa kadi na watu mbambali, kila kadi anayoifungua inatoka kwa yule yule msichana anayejiita dream girl. Hayo yalizidi kumchanganya sana Moses na akawa na shauku ya kumjua huyo
msichana anayemchanganya kila siku.
 Siku moja akiwa ameinama katika meza ya kantini baada ya kupokea kadi kutoka kwa dream girl, aliguswa begani na mkono laini sana. Hakuhitaji kufikiria sana juu ya mtu aliyemgusa, kwani alishajua ni mwanamke.
"mambo Mose" alipewa salamu baada ya kuinua uso wake kumtazama aliyemgusa begani.
"safi tu za kwako" Moses alijibu salamu hiyo  kivivu huku akijiweka sawa.
"safi tu,  mbona umekuwa mnyonge sana leo?" msichana aliyemsalimia Moses aliuliza.
"dah! we acha tu kuna mtu ananichanganya"  Moses alijibu kinyonge sana.
"nani tena huyo anayekusumbua kijana makini kama wewe,  anataka akutibulie masomo yako nini?"  msichana huyo alimwambia Moses ili kumvuta aendelee kuongea.  Moses naye badala ya kujibu swali alitoa kadi aliyopewa akaiweka mezani kumuonesha yule msichana.
"jamanii hivi huyu mdada anayekutumia kadi amechanganyikiwa nini mbona simuelewi"

"hata mimi nashangaa yaani  mtu hajui kama hii ni shule na sio sehemu ya mapenzi"

"labda umemchanganya sana ndio anaogopa kukukosa kijana handsome kama wewe"

"hamna kitu kama hicho mdada wazuri wangapi  ndio anione mimi tu"

"usiusemee moyo wake labda ndio kikichompendeza.

Kengele ya kuingia darasani iligongwa na huo ndio ukawa mwisho wa maongezi yao, "naona muda wa kutimiza kilichotuleta umewadia sasa wacha nikuage dada nani?!"  Moses aliongea huku akiwa amesimama huku akimpa mkono tayari kwa kwenda darasani kuendekea na masomo.
"Beatrice au Bite" msichana huyu naye aliongea huku akipokea mkono wa Moses kwa uchangamfu. Moses aliondoka eneo hilo na kumuacha Beatrice akimsindikiza kwa macho akiwa na tabasamu mwanana usoni mwake. Hakika ilikuwa nj faraja tosha kwake kuweza kuongea na Moses hata kushika kiganja chake,  alijiona ameshukiwa na nyota ya jaa kutoka mbinguni.  Siku hiyo yote alishinda akiwa na furaha isiyo na kifani, alikuwa ni mtu mwenye tabasamu muda wote  hata marafiki zake wakawa wanamshangaa. Alipotoka shule alipita katika duka la linalouzwa kisha akanunua kadi zingine kwa ajili ya kuendelea na mchezo wake wa kumtumia Moses, alirudi nyumbani kwao akiwa anachekacheka njia nzima huku akiubusu mkono wake wa kulia alioshikana na Moses.

****

  Brian anajikuta akiingia kwenye kashfa kubwa kutokana na viwanda vyake kusambaza siagi yenye kemikali nyingi kwa watanzania, uchunguzi ulipofanywa inabainika ni kiwanda chake kilichopo Tanga ndicho kilichosababisha hayo yote. Tuhuma hizi  zinapelekea viwanda vyake vifungwe na kusababisha baadhi ya biadhara zake haramu ndani ya nchi ya Tanzania zikwame. Akiwa amebakiwa na viwanda katika nchi zingine  za Afrika ya mashariki aliendelea na uzalishaji kama kawaida, alijiapiza kuja kuishikisha adabu Tanzania kwa hasara waliyompa ya kufungiwa viwanda vyake vya nchini humo. Gaidi huyu wa kimataifa aliamua kuanza kuitafuta virusi hatari hatari vilivyotengenezwa na marehemu Prof Gawaza, alimtumia kijana wake anayejulikana kama Tasi boy ili kufanikisha shughuli hiyo.  "If I get them, I will try them in Tanzania  (kama nitawapata nitawajaribu ndani ya Tanzania)" alijisemea Brian akiwa.amekaa katika moja ya nyumba zake iliyopo Kisumu nchini Kenya jirani kabisa na Ziwa Viktoria.

****

 Siku iliyofuata Beatrice aliwahi mapema shuleni kama ilivyo kawaida yake, alienda darasani kwa akina Moses kwa mwendo wa tahadhari kisha akaweka kadi za mapenzi katika mtoto wa meza ya Moses. Alipomaliza alitoka ndani ya darasa hilo huku akihakikisha hakuna anayemwona, alirudi darasani kwake  kuendelea na masomo yake kama kawaida.  Muda wa mapumziko ulipofika alimpa kadi mmoja wa rafiki zake ampelekee Moses kantini kisha yeye akatangulia kantini. Alipofika kantini alimkuta Moses akiwa amefika tayari akiwa anapata kifungua kinywa,  alienda kuketi kiti kilicho mkabala na kiti alichoketi Moses katika meza moja.
"Mambo Mose" alimsabahi kwa tabasamu lililochanua kama ua.

"safi Bite, mzima wewe?" Moses aliitikia salamu ya Beatrice na kumuuliza hali yake.

 "mi mzima wa afya khofu kwako tu"

 "namshukuru mungu nami ni mzima"

Waliendelea kuongea mambo mbalimbali huku wakipata kifungua kinywa, muda wote huo Beatrice alikuwa ni mwenye tabasamu pana kuliko hata katika maneno yasiyohitaji kuleta tabasamu.  Uchangamfu aliounesha Beatrice pamoja na mambo ya kufurahisha yalimfanya Moses atabasamu kwa muda huo, tabasamu lake lilikuja kufifia mithili ya taa iliyokosa umeme baada ya binti wa madarasa ya sanaa kumletea bahasha nyeupe.  Msichana aliiweka mezani bahasha kisha akasema "samahani kaka yangu nimetumwa nikuletee na mdada mmoja  anayejulikana kama dream girl. Uso wa Moses tayari ulibadilika na kuwa wenye kuonesha kukereka na jambo hilo, yule msichana aliondoka hapo kantini  baada ya ujumbe aliotumwa kufika kwa mlengwa.  Moses alimuangalia Beatrice kwa muda kisha akasema "Iam so tored with this game(nimechoja sana na huu mchezo(  unaweza kunisaidia kitu kama hutojali".  Muda huo Beatrice alikuwa ameinua kikombe cha chai akawa anakunywa madaha, wakati Moses anamwambia hivyo alijikuta amepaliwa na  chai kutokana na mshtuko alioupata baada ya kusikia kauli ya Moses. Alianza kukohoa huku akiwa ameshika kifua hali iliyomlazimu Moses kuinuka na kwenda kumshika bega  akimpiga mgongoni kwa namna isiyoumiza, alichukua kipande cha tishu na kumpatia kisha akamwambia,  "pole sana Bite,chukua tishu ujifute maana naona chai imekulowanisha". Beateice alipokea tishu akajifuta katika sketi yake, muda huo huo kengele ya kurudi darasani inagongwa na kupelekea Moses anyanyuke na kumuambia Beatrice "tutaongea kesho vizuri Bite ngoja niwahi darasani". Aliondoka eneo hilo kuelekea darasani baada ya kumuaga, Beatrice alibaki anatasamu na mwili ukimsisimka kila akikumbuka alivyoguswa mgongo wake na Moses wakati alipopaliwa.   "Iam going to be crazy for this boy,  ooh Beatrice Iam in love(ninaelekea kuwa kichaa kwa  huyu mvulana, Beatrice nipo katika mapenzi" alijisemea moyoni huku akiwa amefumbata mikono yake kifuani.   Alinyanyuka kwenye kiti na kuelekea darasani kwa ajili ya kuendelea na vipindi.

****

   Majira ya jioni Moses alikuwa tayari amesharejea nyumbani kwao anapoishi na mjomba wake Kennedy, mlinzi na msichana ambaye ni msaidizi wa kazi ndio waliokuwa  watu wengine walioongezeka ndani ya nyumba hiyo. Uchangamfu wao na ushirikiano ndio uliofanya wawe na furaha ingawa ni wachache , vitu alivyoachiwa na baba yake hakuwahi kuvigusa wala kuvichunguza. Akiwa mpenzi wa majaribio ya kisayansi na kujua vitu mbalimbali,  alikuwa akishinda katika maabara ndogo ya baba yake iliyopo katika nyumbani hapo. Uzoefu wake katika mambo mbalimbali na ukiongeza na vitu mbalimbali alivyofundishwa na baba yake, aliweza kufanya majaribio kwa kufuata sheria na kanuni za maabara hiyo. Jioni ya siku nayo aliamua kuingua maabara ili kuendelea kufanya majaribio, ndani ya maabara hiyo iliyo chini ya nyumva alimkuta mjomba wake akiwa anapekua  moha ya mafaili ya baba yake.
 "anko Kenne vipi?" alimuuliza

 "anko kuna karatasi nilikuwa nimeishika wakati jana naingia humu kuangalia unavyofanya majaribio, cha ajabu siioni na nilipoangalia kila sehemu humu ndani sikuipata hivyo nimeamua nije kuangalia humu" alijibu Kennedy huku mboni zake za macho zikiwa hazitulii

"ungeniuliza mimi anko  ndiye najua kila kitu cha humu na kinachohusiana na humu, karatasi hiyo ipoje?" Moses akamwambia

"ni nyaraka ya benki"

"kuna karatasi nimeziona kwenye kiti cha nyuma cha gari ndogo hebu kaangalie kama ukikosa hapo"

  Kennedy alipekua mafaili kisha akaacha na kutoka humo ndani, Moses aliendelea na majaribio kama kawaida pasipo kumtilia maanani mjomba wake. Baada ya muda mjomba wake alirudi akiwa na karatasi mkononi mwake.  "anko nimeipata tayari" alimwambia Moses ambaye macho yake alikuwa ameyaelekeza katika  matundu mawili ya hadubini. Moses alimjibu pasipo kuinua kichwa chake, "sawa anko", Kennedy aliondoka eneo hilo pasipo kutia neno jingine.  Baada ya Moses kumaliza kufanya majaribio alifunga mlango wa maabara bila ya kutumia funguo, alienda hadi katika chumba cha kulia chakula kwa ajilibya kupata chakula cha usiku. Tayari saa mbili usiku ilishawadia, alipomaliza kula alienda kujisomea kama ilivyo kawaida yake ili aende sawa na mtaala wa kidato cha sita.




****

Siku iliyofuata  Beatrice aliwahi kantini baada ya tu ya kusikia kengele ya mapumziko, alikaa  katika kiti kilicho mkabala na kiti anachokalia Moses kila siku . Baada ya muda Moses alifika hapo kantini akiwa amebeba vitabu mkononi, alienda hadi kwenye kiti anachokitumia siku na kumkuta Beatrice akiwa tayari keshawasili eneo hilo. Aliweka vitabu na kumsabahi "mambo Bite"  ha lafu akavuta kiti na kuketi, Beatrice alimjibu, "safi tu upo poa?". Alivuta kiti na kuketi kisha akasema "naona leo umeniwahi" , kauli hiyo ilimfanya Beatrice atabasamu pasipo kusema lolote huku akimtazama Moses.



ITAENDELEA

No comments:

Post a Comment