Sunday, December 20, 2015

SHUJAA SEHEMU YA KUMI NA SITA





MTUNZI: Hassan O Mambosasa

SIMU:+255713776843
+255762219759



WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



            ILIPOISHIA

"ndiyo nampenda Bite na namtakia mema sista" Andrew alijibu
"basi fuata ushauri wa sista wako kwani kuchukuliwa na huyo lofa ni kiti gani, yeye si mwanamke pia na anapenda" Alishauriwa na rafiki yake aliyemuuliza swali, Andrew alitaka kuongea lakini mlio wa kuita katika simu yake ulimkatisha na ikamlazimu apokee baada ya kujua ni dada yake.
"sema sista" Andrew alisema kisha akatulia kimya akiwa amekunja uso akisikiliza maneno yanayotolewa na dada yake ambaye alisikika akiongea kwa ukali hata kwa wenzake, simu ilipokatika Andrew alishusha pumzi
kisha akasema, "oyaa janga jingine hili, sista kashtuka mchezo wetu. Jamaa kumbe naye kaumia na alikuwa hospitali".
"umeona sasa mwana si msala huo, unafikiri atakusaidia umpate Bite wakati umecheza karata chafu dhidi ya anayempenda" Lawama iilianza kumshukia Andrew kutoka kwa rafiki yake aliyekuwa anamshauri.
"si muda wa kulaumiana mshkaji huu, kwanza hapa tusepeni maana naona hakunifai tena" Andrew aliongea huku akisimama kwa ajili ya kuondoka eneo hilo,  wenzake nao walimfuata pasipo kusema chochote.




ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI YAKE



SEHEMU YA KUMI NA SITA!!


****

              MAKAO MAKUU
   EAST AFRICA SECURITY AGENCY
                (E.A.S.A)
               DODOMA.


Taarifa za uwepo wa gaidi kutoka Ulaya ndani ya Ukanda wa Afrika ya mashariki ndiyo ziliingia katika  ofisi za makao makuu ya EASA jijini Dodoma, mawasiliano ya EASA  na mashirika ya kijasusi kama KGB, MOSSAD na M16 ndiyo yalifanikisha taarifa hii ifike katika meza ya mkurugenzi  wa EASA  katika makao makuu hayo ya Dodoma. Mashirika hayo yalikuwa yapo radhi kuleta majasusi wao katika ukanda huu ili wasaidiane katika upelelezi lakini EASA ikaamua kulivalia njuga suala hili baada ya kupata ushahidi unaonesha kutumika kwa akaunti ya Brown Mcdonald  ya benki ya Barclays katika nchi tofauti za ukanda huu. Hakika ilikuwa ni habari ambayo ilitakiwa kuchukuliwa hatua ndani ya muda mfupi ili iweze kutatuliwa, kikao cha dharura kiliitishwa baina ya wakuu wa matawi mbalimbali wa shirika hilo katika kila nchi. Nchini Tanzania Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo makao makuu jijini Dodoma, aliwaita  CE  wa matawi yote nchini Tanzania kisha kikao kizito baina yao kikaendeshwa kwa muda wa masaa mawili hadi wakaafikiana wampe kazi hiyo mpelelezi mmoja wa kitengo cha SECRET SERVICE ndani ya shirika hilo. Namba kadhaa za majina ya wapelelezi hao yalipendekezwa na mwishowe uteuzi wa wapelelezi hao kutokana na ubora na uzoefu wao ukafuata. Hadi muda kikao kinaisha tayari mpelelezi aliyetakiwa kupewa kazi hiyo alishajulikana na ikawa inasubiriwa akabidhiwe majukumu hayo tu aweze kuyatekeleza kama shirika lilivyomtaka ili aweze kulinda na kuihami Afrika ya mashariki. Mpelelezi ambaye yupo chini ya CE wa Dar es salaam ndiye aliyeteuliwa hivyo kazi ya kumtafuta gaidi huyo ikawa ipo chini yake kwa muda huo.

****

 Andrew alipowasili nyumbani kwao tu alipokelewa na hali ya kununa ya dada yake na hata alipomsalimia salamu haikuitikiwa, kisirani cha waziwazi ndicho kilionekana kwa dada yake ingawa haikujikana mbele ya mama yao. Kitendo alichomfanyia Moses ndicho kilisababisha yote hayo ingawa hakutambua dada yake aliambiwa na nani taarifa hiyo ambayo kwake ilikuwa ni siri kati yake na marafiki zake, jambo lilikomjia kichwani kwa muda huo ilikuwa ni kuweka mambo sawa kwa kuongea na dada yake  ili awe na amani.  Muda huo Annie alikuwa chumbani kwake na ikamlazimu Andrew amfuate ili aweze kuweka mambo sawa, ilimbidi ajikaze na ajivike ujasiri ili aende kwani alimtambua dada yake ni mtu wa jazba sana akiwa amekasirishwa. Alienda hadi chumbani kwa dada yake kisha akagonga mlango kwa taratibu lakini hakuitikiwa, aliponyonga kitasa kuufungua mlango alikuta mlango haujafungwa hivyo ikamlazimu aingie ndani.
"Andrew unataka nini? Toka kabla haujanichefua" Annie alimwambi kwa ukali baada ya Andrew  kuingia ndani.
"sista nisikilize kwanza" Andrew aliongea kwa upole.
"nikusikilize kwa lipi wewe usiyetaka kusikia, nimekuambia hilo suala uniachie mimi lakini hukutaka kusikia na ukaamua umtumie ampige Moses wakati unajua yeye ni kila kitu kwangu" Annie aliongea kwa ukali.
" Sista una uhakika gani  kama ni mimi niliyemtuma huyo mtu, hivi huoni kama unanituhumu kwa kosa ambalo sijalifanya. Umepiga simu na ukaanza kunishambulia kwa maneno tu bila hata kunipa nafasi ya kuongea ndiyo nini hii" Andrew aliamua kujitetea kwa kutumia uongo ambao kidogo ulionekana kumuingia Annie.
"Kwahiyo unataka kuniambia itatokea mtu tu aje agonge gari lake kimakusudi bila ya kutumwa na kama katumwa ni nani mwenye ugomvi na Moses kama siyo wewe" Annie aliongea akiwa kapunguza ukali.
"nitajuaje labda ana ugomvi na mtu mwingine" Andrew aliongea.
"hivi mtoto wa Professa Lawarence Gawaza  unamjua?" Annie alimuuliza.
"namsikia tu ila sijawahi kumuona, kwa sifa ni mtu asiye na ugomvi na mtu  na haijawahi kutokea akagombana na mtu" Andrew aliongea.
"sasa basi inabidi utambue huyo mtu unayemtaja ni Moses na mtu wa kwanza kugombana naye ni wewe. Sijui una jingine la kuniongopea?"Annie aliongea akiwa ameukunja uso wake, baada ya kusikia maneno hayo Andrew aliishia kushtuka kisha akainamisha uso wake chini akakaa kimya.
"sasa umesema hajawahi kugombana na mtu, sasa niambie mwenye chuki na Moses Lawrence Gawaza ni nani?"Annie aliuliza akiwa amekunja sura.
"Sista sorry ni chuki ya kutotaka kuona  Moses ninayemchukia ninamuita shemeji kwa dada yangu kipenzi. Nisamehe dada" Andrew alijikuta akikiri kosa lake mwenyewe.
" Andrew hivi nishawahi kumchukia mtu anayenifanya nikose penzi langu ambaye ndiye kipenzi kwako mpaka nikafikia hatua nimtumie mtu? Yaani kuheshimu upendo wako kwa Beatrice umeona haitoshi mpaka ukamtumie mtu kipenzi changu" Annie alilalamika.
"Sista nisamehe nimekosa sitarudia" Andrew aliongea huku akipiga magoti mbele ya dada yake.
"Nikishakusamehe ndiyo itabadilisha kuwa hujatenda kosa sio?" Annie aliuliza kwa ukali.
"haibadilishi ila ndiyo itanifanya niwe na amani moyoni mwangu" Andrew aliongea.
"hayo ya amani ya moyoni mwako utayajua mwenyewe na kuanzia sasa sitaki unishirikishe katika suala la kutafuta penzi la Beatrice utajijua wewe mweyewe, get out" Annie aliongea kwa ukali akionesha kwa kidole mlango ulipo.
"Sista nisikilize kwanza usifanye hivyo" Andrew aliongea aliongea akiwa amepiga magoti vilevile huku Annie akimuonesha kwa ishara atoke nje. Andrew alizidi kumuhimiza dada yake lakini haikufua dafu zaidi ya kuzidisha hasira kwa dada yake.
"Andrew nadhani unanijua nikiwa nina hasira, sasa wewe baki hapa kama sijakupiga ile flat screen ya kichwa" Annie aliongea akimuonesha Andrew mahali kilipo kioo bapa cha tarakilishi, kisha akainuka halafu akasema " nadhani umenisahau sasa ngoja nikukumbuahe jinsi nilivyo". Alienda hadi kwenye meza ndogo ya tarakilishi kwa haraka huku Andrew akitimua mbio kutoka nje ya chumba cha Annie baada ya kuona dada yake alikuwa akimaanisha kile anachokisema. Andrew alimtambua dada yake kama mtu asiye na masihara akiwa na hasira na angeweza kumuweka alama usoni  kama angempiga na kioo hicho, tukio la kuunguzwa msichana wa kazi na dada yake kwa kutumia mafuta ya moto kipindi cha nyuma ndiyo lilimpa tahadhari juu ya hasira za dada yake. Kitendo cha Andrew kutoka nje ya chumba cha dada yake alisindikizwa na msonyo mkali kisha mlango ukabamizwa na Annie kwa nguvu.

****

Baada ya kufika nyumbani tangu atoke hospitali kufungwa vidonda, Moses alitembelewa na Irene, Beatrice pamoja na Victoria walioletwa na Hilary  hapo nyumbani kwao Moses. Beatrice hakuwa na amanj ya moyo kila akitazama plasta zilizopo usoni mwa Moses ingawa alitolewa hofu kwa kuambiwa yupo sawa kidogo. Irene na Victoria nao walihuzunika hivyohivyo kila walipomtazama Moses alivyo tena katika nyumba pweke kama hiyo.
"hivi ilikuwaje?" Victoria aliuliza.
"aisee chanzo ni ajali ndiyo jamaa yangu akazichapa na baunsa  aliyeligonga gari letu kwa nyuma" Hilary alieleza kwa kifupi.
"Honey si ungemuacha tu, umeona sasa umejiletea matatizo" Beatrice alimwambia Moses akiwa amepakata kichwa chake katika mapaja yake.
"Baby hivi kama angetuua  yule halafu alifanya makusudi ndiyo maana kanitia hasira" Moses aliongea taratibu kutokana na maumivu aliyokuwa anayasikia katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
"ila jamaa naye kaipata maana ana manundu kibao, shem nikupe big up maana una mume ana ngumi nzito kama Tyson"  Hilary aliongea huku akitia utani kidogo katika maongezi na kusababisha wote wacheke, wakiwa wanaendelea na mazungumzo mlio wa gari nje ulisikika ukitokea getini kuelekea  kwenye maegesho. Baada ya muda mlio wa gari uliisha baada ya gari kuzimwa kisha wakasikia sauti za viatu vya mtu akija sebuleni.
"Anko wako huyo, umemuambia juu ya balaa lililokupata?" Hilary aliuliza huku Moses akikataa kwa kutikisa kichwa. Kennedy alitokea sebuleni hapo akiwa na kashika koti la suti pamoja na mkoba wa ofisini, alikutana na ugeni wa watu anaowajua na wengine asiowajua pamoja na kustushwa na hali aliyokutana nayo mpwa wake. Alipokea salamu za wote pamoja na utambuliaho wa kila mmoja sebuleni hapo huku akimtazama Victoria kwa umakini halafu akampa ishara ambayo haikujulikana na mtu yoyote.
"ehee! Mbona uko hivyo?" Kennedy aliuliza baada ya kuitikia salamu, Moses alimsimulia mkasa mzima wa tukio lililomkuta.
"mna namba za hilo gari?" Kennedy aliuliza.
"hizi hapa" Hilary aliongea huku akitia kikaratasi kidogo mfukoni mwake kisha akampatia Kennedy wakati huo wote wapo kimya wakimuangalia Kennedy ambaye uso wake ulikuwa umebadilika na ukionekana una ghadhabu za waziwazi.
"haaa! Hilary weka begi langu ndani, nitarudi baadaye kidogo" Kennedy aliongea huku akitoka nje kwa kasi akiwa ameacha koti la suti na mkoba wake wa ofisini hapo sebuleni. Sauti ya kuwashwa gari ilisikika kisha huku geti nalo likisikika likifunguliaa, gari aliyoingia nayo Kennedy iliondoka kwa kasi hadi makelele yakawa yanasikika.
"Mmmh! Kimeshanuka tayari" Moses aliongea kwa sauti ya chini.
"oyaa ujue anko wako sijamuelewa" Hilary alionesha kutoelewa mambo yaliyokuwa yanafanywa na Kennedy.
"jamaa huyo ni mkorofi sana nyie subirini tu kama akiwahi kurudi au  akichelewa nitawahadithia" Moses aliongea kwa  sauti ya chini.
"kwahiyo kaenda kumtafuta aliyekufanyia hivi? " Irene aliuliza.
"nyie subirini hapa mtajua" Moses aliongea, mlio wa ujumbe mfupi ulisikika kwenye simu ya Victoria, Victoria  aliufungua ujumbe huo kisha akaguna baada ya kuusoma. Wote walimtazama lakini akaonesha tabasamu la uongo baada ya kuusoma ujumbe huo, jina la mtuma ujumbe lilikuwa ni Tasu boy ambaye alikuwa ni shemeji yake kwa rafiki yake Annie.
"vipi shem kwema?" Moses alimuuliza Victoria.
"kwema tu" Victoria alijibu.

****

   Gari aina ya range rover ilifika kwenye lango la gereji moja iliyopo maeneo ya Tegeta kisha ikapiga honi kwa fujo, lango hilo lilifunguliwa kisha gari hiyo ikaingia kwa kasi ndani hadi jirani na landucruiser ya mkonga  yenye rangi nyeusi. Gari hiyo ilipisimama Kennedy alishuka akiwa na kaja kishari akamuendea aliyemfungulia geti halafu akampiga ngumi mfululizo huku akitukana matusi.
"aliyekodi Land cruiser ile pale ni nani?!" Alimuuliza kwa ukali kisha kamuongeza mtama.
"ni Mponjo" Yule mfungua geti alijibu huku akiwa anatoa mguno wa maumivu, Kennedy aliachia tusi zito  la nguoni kisha akafungua mlango mdogo wa geti akatoka. Alielekea hadi ilipo baa ndogo iliyopo jirani na gereji hiyo kwa mwendo wa kasi, alipofika kwenye baa hiyo alienda hadi upande wenye kutumiwa na wacheza kamari ambao ulikuwa una kelele sana muda huo. Alipoingia eneo la kuchezea kamari akiwa na sura yenye ghadhabu kelele zote za wacheza kamari zilitulia huku kila mmoja akiwa anamtazama kwa wasiwasi. Kennedy alitembeza macho yake ndani humo kwa kila mmoja, alipomuona yule dereva wa land cruiser aliyetumwa na Andrew alimnyooshea kidole kisha akafoka, "Mponjo ku****** njoo mwenyewe".
"bro Tasu kwema?" Mponjo alijikuta akitetemeka baada ya kugundua anayetafutwa na Kennedy(Tasu) ni yeye.
" we fala nikikufuata utaitwa marehemu" Kennedy aliongea kwa ukali, Mponjo alijikuta akienda mwenyewe  huku wenzake wakimsikitia kutokana kumjua balaa la Kennedy vizuri. Eneo la gereji hiyo aliyofika Kennedy wanamtambua kama ni mtu mkorofi pia ni mmoja wa watu makatili. Mponjo alipomfikia Kennedy alisukumwa kwa kofi la shingo huku akiambiwa, "choko we ongoza njia". Mponjo alitoka na alipofika nje ya baa hiyo alipigwa teke la mgongo hadi akaanguka kisha kichapo kizito kikamshukia huku akiwa anapelekwa gereji, alipoingizwa ndani ya gereji ndipo alipopewa kipigo mfululizo huku akiwa hajaambiwa kosa alilolifanya ni lipi.
"Bro Tasu mbona unanionea nimekufanyia nini?" Mponjo aliuliza akiwa anatema damu mdomoni kwa kipigo alichopata.
"Nakuoneaeh! Sikuwahi kukuambia nina mtoto wa dada yangu anayetakiwa anipatie kitu kinachohitajika na don na nikaonya huyo mtoto nampenda sana ingawa siwezi kusaliti amri za Don. Sasa wewe kipi kimekutuma ukampige" Kennedy alifoka kwa hasira sana kisha akamwambia , "ingia kwenye gari haraka".  Hadi hapo tayari Mponjo alitambua kosa alilolitenda na akaingia kwenye gari aliyokuja Kennedy kwa upole. Kennedy alimuru geti lifunguliwe kisha akaitoa gari kwa kaai kuondoka eneo hilo.

****

Moses, Beatrice, Hilary, Irene na Victoria walikuwa bado wapo sebuleni kwa akina Moses wakiongea ,maongezi yao yalikatishwa na sauti ya kurudi la Kennedy kwa kasi hapo baada ya kupita saa moja tangu aondoke.
"Moses! Moses!" Sauti ya Kennedy ilisikika kutoka nje ikimuita Moses na kupelekea wote kwa pamoja watoke nje. Huko walimkuta Kennedy akiwa anampiga mtu mwenye mwili mkubwa wa kimazoezi, wote walibaki na mahangao walipomuona mtu aliye na plasta usoni  na majeraha kadhaa usoni.
"ndiye huyu aliyekuvamia na akagonga gari yenu?" Kennedy aliuliza huku akimuinua uso Mponjo ili Moses amuone, hapo ndipo Moses alipomtambua mtu huyo.
"ndiye huyo" Moses alijibu na kupelekea yule mtu apigwe teke la uso na Kennedy.
"pumbavu wewe nakwambia utanieleza ni nani aliyekutuma umpige mpwa wangu" Kennedy aliongea kwa hasira huku akishusha kichapo kizito kwa Mponjo hadi wasichana wote wakaziba macho yao kwa huruma na uoga wa kuogopa kushudia mtu akipigwa. Kipigo hicho kizito kilienda kwa muda wa dakika kadhaa pasipo huruma yoyote, Kennedy alimrudisha tena Mponjo kwenye gari tena muda huu akimuweka sehemu ya kuwekea mizigo halafu akasema, "ngoja aende kufunzwa adabu huyu".
"Anko Kenne usiue tu" Moses alimwambia Kennedy.
"usijali kuhusu hilo" Kennedy alijibu huku akiingia kwenye gari kisha akaondoka tena kwa mwendo wa kasi, muda huo wote Irene, Beatrice na Victoria pamoja Hilary walikuwa kimya hadi Kennedy anaondoka.
"Baby anko wako nimeanza kumuogopa" Beatrice alimwambia Moses kwa kudeka.
"Shem hata mimi nimeanza kumuogopa mwenzangu, anko wako mkali" Irene naye aliongea
"ondoeni hofu ni mtetezi wangu tu nisionewe ila hana neno yule" Moses aliongea.
"Shem hivi yule mko vipi naye?" Victoria aliuliza.
"ni kaka mdogo wa marehemu mama" Moses alijibu kisha akaendelea, "ni rafiki yangu, msela wetu mimi na Hilary kiufupi ndiyo mtu wangu wa karibu kwa sasa".
"ok wacha sisi tuwahi maana saa tatu hii watoto wa kike kuwa mbali na nyumbani si vizuri ingawa tumeaga" Victoria aliaga kutokana na muda kuwa umeenda, Beatrice naye alimuaga mpenzi wake kwa kumkumbatia kisha akamuaga Hilary huku Irene akifanya hivyo hivyo. Wote kwa pamoja waliondoka wakiwaacha Hilary na Moses nyumbani hapo.

****

 
  Majuto siku zote huja baada ya kutenda jambo ambalo hukulijua matokeo yake na wala hukuweza kufikiri kama litakuja kutokea kwa namna ambayo hukuitarajia, haya ndiyo yalimjia Andrew baada ya kutuma mtu akampige Moses ili amtishe aachane na Beatrice na matokeo yake ni huyo  mtu kujeruhiwa naye na jambo hilo kugundulika na dada yake. Hakuwaa anatambua kama alikuwa analazimisha maji yapande badala ya kuyawekea mteremko ili yashuke, kupuuza mbinu ya dada yake na kuitumia mbinu yake mwenyewe katika  kumpata Beatrice ndiyo ilichangia. Yote haya ni kwa sababu alikuwa akimchukia Moses na hakutaka kuona kuna ukaribu baina yake ndiyo maana hakutaka awe shemeji yake, sasa dada yake amenuna na hataki hata kuongea naye na moyoni amejawa na majuto tu.


No comments:

Post a Comment