Thursday, December 10, 2015

SHUJAA SEHEMU YA SITA

RIWAYA: SHUJAA

MTUNZI: Hassan O Mambosasa

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
 

ILIPOISHIA

Moses alibaki ameduwaa akimtazama Beatrice
aliyekuwa akiondoka, Bratrice alipopotea katika upeo
wa macho yake alibaki akiwa ameduwaa kwa
kilichotokea.

"we boya bisha tena nikuone,changamkia tenda
hiyo" Sauti ya Hillary ilisikika kutoka nyuma yake na
kupelekea akurupuke kwenye mawazo.

"yaani mtoto anajilenga mwenyewe we unashindwa
kumaliza" Hillary aliendelea kumlaumu Moses.

"naona leo umeamua uniaibishe" Moses alimwambia

"nikuaibishe kwa lipi wakati wote wamesepa" Hillary
alimwambia Moses. Moses aliangalia darasa zima
na kukuta darasa lote ni tupu na wao wawili tu ndio
waliobaki.

"daah! Nilijua kuna wanga wananichora" Moses
aliongea huku akichukua begi lake la vitabu.

"wacha uoga wewe ,naona kakupatia barua kabisa"
Hillary alimwambia

"ni kadi tu ya mwaliko"

"poa tusepe kama vipi".

Walitoka humo darasani wakiwa wanaongea mambo
yao mbalimbali, utani kwa marafiki hawa ilikuwa ni
kitu cha kawaida sana.


ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI YAKE



SEHEMU YA SITA
Ilikuwa ni kawaida kwa marafiki hawa kuondoka pamoja kila ifikapo muda wa kutoka  na ikitokea mmoja ana jambo lingemfanya asiondoke na mwenzake lazina atoe taarifa kwa mwenzake, ndio maana hata siku ile Moses alipoondoka na Beatrice basi Hilary alikuwa na taarifa juu ya jambo hilo. Wote walikuwa wanatoka katika familia zenye uwezo na wote walikuwa na uwezo wa kuja shule na usafiri, uwezo huu wa kifedha wa familia zao haukuwa sababu ya wao kutoondoka pamoja. Ilikuwa Moses akija na usafiri basi Hilary hatokuja nao na Hilary akija na usafiri basi Moses hatokuja nao,  yote haya yalifanywa ili kuwawezesha waondoke pamoja ingawa walikuwa wanakaa mitaa tofauti ya sehemu moja. Siku hiyo ya ijumaa Moses ndiye aliyekuja na usafiri na Hilary hakuwa amekuja na usafiri, walitoka pamoja hadi katika maegesho ya magari kisha wakaingia kwenye gari la Moses.
"we mwanga siku juzi nimepanda teksi kwasababu ya ile sketi" Hilary alimwambia Moses walipokuwa ndani ya gari.

"we mgoni uligoma sasa mimi nifanyeje" Moses alisema huku akiwa anafunga mkanda wa gari.

"yaani mzee mi nilitaka uue mchezo ila we umeremba" Hilary aliongea huku naye akifunga mkanda wa gari.

"muda wa hilo bado nasubiri wakati waje"

"wacha zako wewe utamkosa yule"

"kama nilipangiwa nimpate nitampata na kama sikupangiwa ujue sitampata"

"tatizo wewe ni mjanja wa mjini anayeelekea kuwa mgoroko, yaani mtoto anakukumbatia kabisa kisha anakupiga busu karibia na mdomo halafu unamuacha"

"mambo mazuri hayahitaji papara we mgoni".

"alaa! kwahiyo unasubiri umuweke ndani".

"ndio mpango mzima huo".

"sasa mpaka usubiri umuweke ndani keshakuwa wa mwenzako huyo".

"hebu zima hiy kitu, hivi huyu ticha wa leo unamchukuliaje jinsi alivyoishuka ile soil colloids kwenye kemia leo".

"mwana yule ni bonge la ticha tena kijana anayeendana na itikadi zetu,yaani tukiendelea naye jua lile somo tunaua siku ya necta".

"daah! Hapo umeongea kweli , kumbe muda mwingine huwa unaongea vya maana . Sasa kwanini unapenda kuongelea uzinzi tu"

"ili nikupe ujanja uache kuwa domozege"

"wewe mwanga nini? Domozege nani au unataka nimchukue  Irene ndio uamini mimi sio domozege. Mimi nipo na mipango yangu ya kitabu ndio maana"

"yaani demu wangu humuwezi kabisa ingawa unapendwa na mtoto mkali zaidi yake, ukitaka nisikuone domozege anza na huyo Bite"

"alaa kumbe ngoja sasa, kesho utaona kama utakuwepo kwenye birthday yake"

"aisee Irene kaalikwa jua na mimi nimealikwa pia, kesho nipo ndugu"
Maneno ya Hilary  katika mazungumzo hayo yalilenga kumfamya Moses amtongoze Beatrice, hakika kwa mtazamo wake aliona yamefanikiwa kumshawishi Moses. Siku hiyo Moses aliamua kumpeleka rafiki yake hadi nyumbani kwao katika mtaa wa Msikitini kisha na yeye akarudi nyumbani kwao, walikaa eneo moja isipokuwa mitaa tofauti na ikiwa mkoja atakuja na usafiri basi lazima ampeleke mwenzake hadi kwao kama kawaida yao.

****

 Norbert alifanikiwa kufika salama nyumbani kwake maeneo ya Temeke jijini Dar es salaam, tukio la kuwaona watu katika hifadhi ya Biharamulo lilimjia kichwani mwake hadi muda huo wa usiku. Hapo alitoa kamera ya ke aliyofanikisha kuwapiga picha watu wale akaiwasha, aliamua kuzipitia zile picha kwa umakini kabisa huku nafsi yake ikimtuma kuwafuatilia zaidi wazungu hao aliowapiga picha.

"ujio wa watu hawa unanipa ari ya kuwajua zaidi" alizidi kujifikiria zaidi na kujiuliza maswali zaidi juu ya watu hao. Alitaka kujua watu hao ni wakina nani hasa na kwanini waingie kinyemela ndani ya nchi, alitaka kufahamu ni kwanini watumie   boti ya kivita kuje eneo alilowakuta.  Miili ya watu hawa pamoja na mizigo waliyokuwa wamebeba ni sababu nyingine iliyompa shaka sana. Alijifikiria sana juu ya watu hao na mwisho akaamua akaamua kuiwasha tarakilishi  ya mapajani yenye muundo wa kisasa, aliunganisha mawasoliano ya ana kwa ana katika tarakilishi hiyo kisha akasubiri baqda ya kuona memo 'please wait'  katika kioo cha tarakilishi yake.  Neno hilo lilipoondoka ilionekana sura ya binti mrembo katika kioo chq tarakilishi hiyo,  Norbert alimuonesha ishara ya busu binti huyo anayewasiliana naye ana kwa ana kisha akatabasamu.
"loh! Mwanaume wewe leo umenikumbuka kwa lipi?" Binti huyo alisikika akiongea baada ya Norbert kumuonesha ishara ya busu.

"nimekumbuka kwa kile unachonipatia siku zote mke wa mimi"  Norbert aliongea.

"loh! Nani mkeo?"  Yule binti aliuliza kwa jicho la kusuta

"ni wewe Norene kwani kuna mwingine?" Nobert akamwambia.

"akaa! Babu wee mimi mke wa mtu" Binti aliyetajwa kwa iina la Norene alikana kwa namna ya kimasihara.

"kwani kuna mke wa punda duniani" Norbert alingea kimasihara hadi Norene akacheka

"Nor tuachane na hayo ujue nina hamu na wewe" Norene alisema akiwa na uso wenye aibu.

"usijali mama nipo kwa ajili yako ndio maana nimerejea jijini ili nikufaidishe wewe" Norbert alibembeleza.

"mmh! Haya kesho nakungoja ofisini, kuna lipi jipya?"

"Norene kuna picha za watu nimezipata nilipokuwa Kagera, unaweza kunisaidie kuwaperuzi niwajue kwa njia ya mtandao wa kampuni yetu"

"hebu zitume nizione"
Baada ya kuambiwa hivyo Norbert alichomeka waya kwa kuziunganisha tarakilishi na kamera na kupelekea picha za ndani ya kamera yaoe zionekane kwenye tarakilishi, alizituma piicha zote kwenda kwa Norene kisha akamwambia "hizo happ hebu zicheki na uzifanyie kazi kesho nitakuja kuchukua ulichokibaini".

"haya mpenzi usiku mwema,uniote" Norene alisema.

"malaika wa ndoto   kagoma siku hizi kuniotesha ndoto hizo" Norbert aliondea kimasihara

"nyoo lione" Norene aliongea huku kavuta mdomo.

"haya mama nitakuota"

Walimaliza kuongea kwa muda huo
Norbert aliamua kwenda kujipumzisha kutokana na uchovu wa safari.

  Norene ni binti wa kimbulu mwenye sura nzuri na umbo lenye utata kwa wanaume wakware wenye uchu, binti huyu ni mtaalamu wa tarakilishu aliyehitimu mafunzo ya computer science katika chuo cha Oxford cha Uingereza. Mbali na elimu hiyo pia binti huyu mhitimu wa mafunzo ya ujasusi aliyoyapata nchini Urusi  ambapo alipelekwa na kampuni ya EASA baada ya kuona ujuzi wake katika masuala ya Tarakilishi na baadaye alipewa kazi kama katibu mukhtasi wa CE ambaye ndiye mkuu wa Norbert kikazi. Binti huyu alikutana na Norbert Kaila kwa mara ya kwanza katika mpango wa kuzuia ulipuaji wa silaha nzito  uliokuwa unataka kufanyika  ndani ya nchi  hii, kazi ya kutoa maelekezo juu ya mambo muhimu katika mpango huo  aliifanya huku Norbert akiwani msikilizaji wa maelekezo hayo. Baada ya hapo walianzisha  ukarbu baina yao na hatimaye wakaja kuwa wapenzi waliodumu kwa muda mfupi kisha wakaachana ingawa bado huwa wanjikumbusha enzi za penzi lao kama wakiwa wana hamu ya kufanya hivyo. Hadi muda huo walikuwa ni wapenzi wasio rasmi na ukaribu wao mara nyingi upo kwenye kazi tu, huyo ndiye Norene ambaye alikuwa anaongea na  Noebert kupitia mawasiliano ya ana kwa ana ya Tarakilishi.


****

                 BUNJU
            DAR ES SALAAM


Jameson, Csmpbel,Calvin,Obren,Christian na Scott walikuwa wapo ndani ya nyumba ya kifahari inayomilikiwa na Kitoza, walikuwa wakijadili juu ya mpango wao uliowaleta nchini Tanzania. Kazi hiyo waliyotumwa na bosi wao Brian iliyotakiwa iishe kwa haraka na kitu walichotumwa walitakiwa wawe wamekipata kama bosi wao alivyoagiza, vijana hawa ni watu waliojaa ukatili na wasio na roho ya huruma linapokuja suala la kazi inayowabidi kufanya hivyo. Ukatili wao huo ulikuwa sio kitu kwa  bosi wao ambaye aliwatuma kufanya kazi hiyo ndani ya siku walizokabidhiwa, wote walimuogopa Brian kama ebola kutokana na ukatili wake pamoja na uwezo wake wa kupigana.

"jamani mchezo ushaanza kama  tulivyopanga  hivyo tutarajie mazuri zaidi" Jameson alianza kuwaambia wenzake waliookuwa wameweka kikao cha pamoja.

"hebu tupe muelekeo kazi ya leo huko" Obren alihitaji taarifa kamili juu ya kazi yao.

"Kupitia mpango aliouandaa Kimwaga  nimefanikiwa kuingia ndani ya shule ile na kupitia elimu yangu niliyonayo katika masuala ya sayansi nimefanikiwa  kujenga ukaribu na kijana wa Gawaza kwa kiasi fulani" Jameson aliwaelezea.

"vizuri kwa hatua uliyofikia sasa kilichobaki ni kumtafuta mtu aliyekuwa  anaaminiwa na Professa naona ndiye atakayekuwa msaada kwetu" Scott aliongea

"nadhani tuongeze umakini kwa katika kumfuatilia huyu kijana tu" Jameson alishauri.

"kuwa mtu wa karibu wa mtu haimaanishi ndiyo unaaminiwa sana, nafikiri kila mtu atafutek kwa njia anayoifahamu na mwisho siku tuwe tunakutana kama hivi kuelezana juu ya tafiti zetu.  Au wenzangu  mnasemaje" Campbel alishauri

"mi naungana na hoja ya aliyoitoa Campbel, nadhani kila mtu afanye kazi kwa dhana yake halafu mwisho wa siku tunaunganisha matokeo ya kazi ili kupata ufumbuzi" Christian alikubaliana na ushauri wa Campbel. Wenginewaoiobaki waliangaliana kisha wakatikisa vichwa vyao kuashiria wamekubaliana na ushauri huo, walipanga mambo mengine ya kawaida yanayohusu mstakabali wao wa kuwepo ndani ya nchi  hii.


****

           MIKOCHENI
        DAR ES SALAAM


 Moses akiwa amekaa chumbani kwake baada ya kujisomea aliamua kuifungua kadi ya mwaliko aliyopewa na Beatrice kwa mara ya kwanza, harufu nzuri ya manukato ndio aliyokutana nayo baada ya kufungua bahasha ya kadi hiyo. Kadi nzuri iliyopambwa kwa namna ya kuvutia ndiyo aliyoiona pamoja na maandishi yalioandikwa kwa kalamu za wino zenye rangi mchanganyiko ndio zilizoashiria jina lake kwa mwandiko wa kike wenye kuvutia. Uzuri wa mwandiko uliokutwa ndani ya kadi hiyo ulimvutia kiasi cha cha kumfanya atumie dakika kadhaa kuutazama mwandiko huo.
"kwa kweli huyu mtoto kuwa HKL ni haki yake maana huu mwandiko ni mkali balaa.. Mh! Hebu ngoja" aliongea peke kisha akawa kama amegundua kitu, aliinuka hadi kwenye begi lake la shule kisha akachomoa bahasha nyingine halafu akarejea kitandani halafu akaifungua bahasha hiyo. Aliitoa kadi ya mapenzi ambayo alitumiwa na msichana anayejiita Dream girl kisha akaifungua halafu akaiweka sambamba na kadi ya mwaliko wa sherehe ya kuzaliwa ya Beatrice. Alitazama miandiko ya kike iliyomo kwenye kadi hiyo kwa umakini kisha akaguna kuashiria amegundua kitu, alirudia tena kuitazama miandiko hiyo halafu akatabasamu.
"Ha! Hai! Ha! Ha! Dream girl sasa nimekujua" alisema baada ya kuona miandiko inafanana katika kadi hizo, hakika  aliweza kumbaini Beatrice kama msichana aliyemsumbua kwa wiki kadhaa.

"huyu Hilary nahisi ni mwanga maana aliyoniambia juu  ya Beatrice ni ukweli mtupu" alizidi kuongea  peke yake haea alipokumbuka kauli ya Hilary juu ya Beatrice

No comments:

Post a Comment