RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
ILIPOISHIA
"ooh! My daughter please forgive me(ooh binti yangu tafadhali nisamehe) ni kazi tu ilinihitaji na ndio inayotulisha na kutuvesha wote. I know it was your birthday, that's why I bought gift for you. You have to smile and give hug to daddy so as to get your gift(najua ni ilikuwa ni aiku yako ya kuzaliwa, ndio maana nimenunua zawadi kwa ajili yako. Unatakiwa utabasamu na umkumbatie baba ili upate zawadi yako) Mzee Bernard aliongea kuonesha upendo kwa binti yake, Beatrice alitabasamu kisha akaenda kumkumbatia baba yake huku akisema, "I love you daddy(nakupenda baba)".
ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI YAKE
SEHEMU YA KUMI NA TANO!!
"I love you too my daughter(nakupenda pia mwanangu)" Mzee Bernard aliongea.
"ok, I want my gift now(sawa, ninataka zawadi yangu sasa)" Beatrice aliongea kwa sauti ya kudeka.
"first close your eyes( kwanza fumba macho yako)" Mzee Bernard aliongea huku akiziba macho ya binti yake kwa kiganja chake cha mkono, alimuongoza hadi nje kwenye maegesho ya magari akifuatiwa na mke wake pamoja na Victoria. Walipofika eneo hilo la maegesho alitoa kiganja chake usoni mwa Beatrice kisha akasema, "suprise!!". Mama Beatrice pamoja na Victoria waliishia kutabasamu huku wakipiga makofi kwa furaha, Beatrice aliishia kutoa tabasamu lenye mchanganyiko wa machozi kutokana na zawadi hiyo iliyokuwa mbele yake muda huo. Usafiri alionunuliwa kama zawadi na baba yake ndiyo ulifanya awe katika hali hiyo, ni gari aina ya range rover sport ya rangi nyeupe.
"Dady! Dady! Thanks so much, I love you(Baba! Baba! Asante sana, nakupenda sana)" Beatrice aliongea huku akimkumbatia baba yake, Victoria na Mama Beatrice walikuwa wamejawa na uso wenye tabasamu kutokana na kumpenda sana Beatrice.
****
Mapambazuko ya siku mpya ni ya jumatatu yalikuwani kwa ajili ya kazi na watu huanza pilika zao za kila siku baada ya mapumziko ya mwisho wa wiki, ilikuwa ni jumatatu tulivu na yenye amani. Siku hii ndiyo siku ambayo Norbert akiwa kama mwandishi wa habari wa kujitegemea, alitakiwa kuandika ripoti ya kielimu katika jarida la Afrika ya mashariki linalohusisha habari zinazokusanywa na waandishi kutoka nchi tano za Afrika ya mashariki. Ndani ya siku hii Norbert alitakiwa kuandika ripoti hiyo kwa kupita katika shule mbalimbali za kibinafsi na kiserikali, mlolongo wa ripoti hiyo ulitakiwa katika shule ya Neema trust na Al-mutazir, Azania, Jangwani, Mchikichini na Jitegemee. Saa moja kamili ya asubuhi ilipotimu tayari alikuwa yupo ndani ya shule ya Neema trust na muda huo alionana na uongozi wa shule pamoja na walimu, utambulisho wake kwa idara mbalimbali za shule ndiyo ulifuatia ili kujulikana na walimu wa shule hiyo. Norbert aliongozwa kwa msaada wa mkuu wa shule hiyo katika utambulisho wake kwa idara mbalimbali za shule hiyo, hadi utambulisho wote unaisha tayari Norbert alikuwa ameshapata mshangao mwingine ambao aliuficha katika macho yake ili usijulikane. Sura ya mwalimu mmojawapo wa shule hiyo haikuwa ngeni katika macho yake, mwalimu huyo ambaye ni mwalimu wa idara ya sayansi katika shule hiyo na mwenye asili ya ulaya. Alipojaribu kukumbuka mahali alipomuona ndipo alipopatwa na hamasa zaidi ya kuredelea kufuatilia suala alilolianza siku mbili zilizopita kutokana na kuhakikisha juu ya mtu huyo, kumbukumbu zake zilimpa kila kitu anachokihitaji juu ya mtu huyo. Dokta Jameson ndiye mtu aliyemuona na akamtambua sehemu aliyowahi kukutana nae kwa mara ya kwanza, mzungu huyo alimtambua kama ni mmojawapo kati ya wazungu sita aliwaona Biharamulo pia akapewa taarifa zao na Norene. Muda wa kukaa mstarini ulipowadia katika shule hiyo, Norbert alitambulishwa kwa wanafunzi wote pamoja kuhimizwa wanafunzi wampe ushirikiano katika kazi yake iliyomleta hapo shuleni. Ulipofika muda wa vipindi Norbert aliingia madarasa mbalimbali kufanya ufafiti wake uliomleta shuleni hapo, siku hiyo kila mwanafunzi alikuwa yuko makini katika masomo kutokana na tahadhari waliyopewa na walimu juu ya ripoti hiyo ambayo ingeweza kuipa sifa mbaya shule hiyo ikiwa wanafunzi watafanya ujinga.
****
SAMAKI SAMAKI
MLIMANI CITY
Wakati utafiti wa Norbert ukiwa unaendelea katika madarasa mbalimbali katika shule ya Neema trust, Annie na Tasu boy walikuwa wapo ndani ya eneo la mlimani city katika mgahawa wa Samaki samaki kwa miadi waliyoahidiana usiku uliopita. Wapenzi hawa walioachana muda mrefu waliamua wakutane kwa mara ya kwanza toka walivyoachana, kila mmoja alimuona mpya mwenzake ndani ya siku hiyi ingawa hawakuwa wapo kimapenzi katika miadi hiyo. Tasu alimuona Annie ni msichana aliyebadilika vilevile Annie alimuona Tasu ni mtu aliyebadilika ingawa hakutaka kuwa nae tena kutokana na moyo wake kuvutwa na sumaku yenye nguvu kuliko ya Tasu, Moses ndiyo sumaku yenye nguvu ambayo ilikuwa ikiuvuta moyo wake na kufanya asiwe anampenda tena Tasu boy.
"Annie naona leo umenikumbuka, vipi kuna jipya?" Tasu aliuliza baada ya salamu na maongezi ya muda mfupi yaliyodumu baina yao.
"jipya lipo ndiyo maana nikakuita hapa my ex" Annie aliongea.
"haya nipe data zote basi juu ya hilo jipya" Tasu aliongea huku akimtaza Annie kwa umakini.
"kuna dili nataka nikupatie na uwatumie vijana wako na nipo tayari kulipa kiasi chochote cha pesa" Annie aliongea.
"mmmh! Leo umekuja na dili wewe haya hebu liweke mezani" Tasu aliongea huku akiweka tabasamu usoni mwake, Annie alifungua mkoba wake kisha akatoa picha mbili zenye sura za watu wenye jinsia tofauti halafu akampatia Tasu bila kusema lolote. Tasu alipoziangalia picha hizo alijikuta akishtuka sana ingawa aliuficha mshtuko alionao kwa Annie. "wote wanasoma Neema trust high school Mbezi, inahitajika watengane kwa namna yoyote ili Andrew aweze kumpata msichana huyo" Annie aliongea.
"hilo tu, kazi rahisi sana kwangu" Tasu aliongea kwa dharau.
"kiasi gani mnataka ili kukamilisha kazi hiyo?" Annie aliuliza.
"sitahitaji kiasi chochote kutoka kwako katika kazi hii, kiufupi nitakufanyia bure" Tasu aliongea akiwa ametabasamu.
"Tasu stop joking, hii kazi si rahisi niambie tuelewane dili la kibiashara. Usilete mapenzi hapa" Annie aliongea baada ya kushangazwa na maneno ya Tasu boy.
" No! No! No! Annie sileti mapenzi hapa, the boy in this picture is a part of our don's deal(mvulana kwenye hii picha ni sehemu ya mpango wa bosi wetu)" Tasu aliongea kwa msisitizo.
"kivipi unajua sijakuelewa we mwanaume" Annie alihitaji ufafanuzi wa maneno aliyoyaongea Tasu.
"huyo dogo namjua anaitwa Moses Lawrence Gawaza ni mtoto wa aliyekuwa mwanasayansi maarufu Prof Lawrence Gawaza ambaye nafikiri unamfahamu kwani anajulikana sana hapo chuoni kwenu" Tasu aliongea maneno ambayo yalizidi kumshangaza Annie kutokana na kutojua kuwa Mosea ni mtoto wa professa Gawaza, alitambua jina la Gawaza la Moses na hakutambua kama ni mtoto wa mwanasayansi aliyekuwa ana pesa sana.
"kwahiyo ndiyo sababu ya kunifanyia kazi yangu bure?" Annie aliuliza baada ya kushusha pumzi ndefu kwa nguvu kutokana na maelezo ya Tasu.
"kazi uliyoniletea ndiyo mwangaza kwetu katika kukipata kitu tunachokihitaji ambacho huyo dogo anacho. Hapo hamuhitajiki kunilipa ni saidia na mimi nikusaidie, yaani kusaidiana." Tasu alimweleza. Annie aliafiki maelezo ya Tasu kwa kichwa kisha akasema, "ok hamna shida nafikiri niwape uhuru wa kufanya kazi yenu".
"ndiyo linalotakiwa hilo na ikiwa utahitajika basi mimi na wenzangu tutakuita" Tasu aliongea.
"ok tumemaliza, wacha mimi niwahi chuo nina kipindi saa tatu" Annie aliongea huku akinyanyuka kwenye kiti cha samani za kiasili alichokalia, alikumbatiana na Tasu halafu akaondoka.
****
Muda wa mapumziko ulipowadia tayari Moses na Beatrice walikuwa wapo kwenye meza wanayoitumia kila siku wakiwa wapo pamoja na Hilary na Irene, siku hiyo kila mmoja wao alitawaliwa na furaha na hakuna hata mmoja aliyetawaliwa na chembe ya huzuni katika moyo wake. Uwepo wa wenza wao katika meza hiyo, ndiyo ilikuwa sababu ya wao kuwa na furaha. Maongezi yasiyochosha na yenye kufurahisha yaliendelea baina yao huku utani ukiwa umetawala sehemu kubwa ya mazungumzo, vifungua kinywa vilikuwa vikinyweka katika meza hiyo kwa taratibu na vikifurahiwa na watumiaji wake. Mazungumzo yakiwa yamepamba moto baina yao katika meza hiyo, msichana wa kidato cha tatu alifika mezani hapo kisha akawasabahi wote.
"Moses nakuomba mara moja" aliongea msichana huyo
"wa nini?! Kwa.." Beatrice aliuliza kwa sauti yenye ukali lakini Moses akamfinya ili asiendelee kuongea.
"mdogo wangu kwani huwezi kuongea hapahapa" Mosea alinwambia yule msichana.
"yule mwandishi mwandishi anayefanya utafiti anakuhitaji" Msichana huyo aliongea na kupelekea Beatrice aingiwe na aibu kutokana na wivu aliokuwa nao ambao haukuwa na maana yoyote. Moses aliinuka kwejye kiti alichokalia kisha akamwambia Beatrice, "bibie wivu umezidisha sasa".
"yaani naona wivu hata ukiwa mbali nami kwa sekunde kadhaa kwa jinsi ninavyokupenda, si unajua abiria huchunga chake" Beatrice aliongea huku Hilary na Irene wakicheka sana kutokana na kauli hiyo.
"Shem huo wivu ukizidi basi hata kivuli chake utakionea wivu" Hilary aliongea huku akicheka.
"oyaa we boyaa unazingua sasa" Aliongea Moses akiwa kasimama huku akisikiliza maongezi hayo.
"we mwanga hebu wahi ukamsikilize Kaila ili urudi umpunguze bibie wahka" Hilary aliongea na kupelekea Moses aondoke haraka huku akicheka.
"Bite unajisikiaje Moses kuondoka," Irene alimuuliza Beatrice.
"yaani kama nimepungukiwa na kiungo changu cha muhimu" Beatrice aliongea akiwa ameinamisha uso wake.
"he! Heee! Kupenda ugonjwa kweli" Irene aliongea huku akiachia kicheko cha kike.
"Shem usijali utazoea tu hata huyu anakucheka alikuwa hivyohivyo yaani alikuwa na wivu huyu" Hilary aliongea maneno yaliyomlenga Irene.
"jamaniii! Hilary naona sasa wanianika" Irene akiongea huku akimuegemea Hilary halafu akampiga kibao cha kifua kisichoumiza. Hilary alicheka sana kisha akasema, "nyani haoni kundule sio". Sauti ya kengele ya kuingia darasani ilisikika na hapo ndiyo ukawa mwisho wa wao kukaa hapo na huzuni kwa Beatrice kutokana na kutomuona Moses hadi muda huo, alijikuta anakosa amani kwa kutomuona wake mwandani.
"Bite twende class" Irene alimwambia Beatrice.
"hapana Irene I can't bila kumuona Moses" Beatrice aliongea kinyonge.
"Bite utamuona wakati wa kutoka usijali" Irene alimbembeleza huku akimuinua kitini lakini Beatrice akagoma huku akiangalia sehemu ya kuingia kantini walipo, wote kwa pamoja waligeuka kuangalia alipoangalia Beatrice kisha wakatabasamu baada ya kumuona Moses akirejea.
"yaani shem ni afadhali ulivyokuja mana aligoma kwenda class kisa hajakuona" Irene huku akimtazama Moses, Beatrice alijikuta akiingiwa na aibu ya ghafla pamoja na kicheko cha chinichini kutokana na maneno ya Irene. Moses alipokaribia eneo walilopo alimkimbilia kisha akamkumbatia kwa nguvu pasipo kujali uwepo wa wahudumu wa hapo kantini, Moses naye alimpokea Beatrice kwa moyo mmoja.
"usihofu mi ni wako tu" Moses alimuambia kisha akamgeukia Hilary baada ya kuachiana na Beatrice, alimwambia "we mwanga Kusega ndio anaelekea class, si unajua ni Bios sasa hivi".
"jamani si tunaingia kama vipi baadae" Hilary aliongea kuwaaga Irene na Beatrice kwa kuwakumbatia, Moses naye aliwaaga hivyo hivyo kisha wakaondoka kuelekea darasani.
****
Baada ya masaa kadhaa Moses na Hilary walikuwa wapo ndani ya gari wakirudi nyumbani kwao, siku hiyo hakufuatana na mpenzi wake kutokana kupitiwa na baba yake hivyo akaondoka akiwa pamoja na Irene. Siku hiyo Hilary ndiye aliyekuwa dereva wa gari na kwakuwa alikuja na gari ya kwao, safari ya kurudi nyumbani ilitawaliwa na soga la ujana wanalopenda kuongea marafiki hawa walioshibana. Vicheko na utani vilitawala ndani ya gari hilo kuanzia walipotoka shuleni hadi jirani na mataa ya Mwenge, vicheko vyao vilikatika ghafla baada ya wao kupatwa na tukio lilillotishia uhai usalama wao. Sauti ya kishindo ilisikika nyuma yao baada ya Hilary kupunguza mwendo kutokana na uwepo wa daladala inayopakia mbele yao, mshtuko huo uliwashtua wote ingawa walibaki salama kutokana na kufunga mikanda ya gari. Walipoangalia kioo cha nyuma walikuta kimevunjika na chenga za chupa zikiwa zimeanguka nyuma kwenye kochi la nyuma, gari aina ya landcruiser ya mkonga yenye rangi nyeusi ikiwa imeigonga gari yao. Wote walishuka kwa jazba wakaenda hadi kwenye gari ya nyuma, walimkuta dereva wa landcruiser akiwa amekaa kwenye kiti chake akiwa hana wasiwasi hata kidogo. Kimuonekano dereva huyo alikuwa ana mwili mpana sana na wenye kuogopesha kwa mtu wa kawaida, laiti kama ingekuwa ni mtu mwingine mwenye mwili wa kimazoezi wa wastani kama ilivyo kwa Moses lazima angeogopa ingawa kwa Moses hakuthubutu kuogopa. Hilary alipomuona dereva huyo mwenyewe alinywea kama kamwagiwa maji ya baridi na hakuthubutu kuongea chochote, Moses alisogea hadi kwenye dirisha la dereva halafu akaufungua mlango wa dereva kwa nguvu kisha akamvuta nje yule dereva kwa nguvu. Yule dereva alianguka chini kama mzigo kutokana na kutotarajia kufanyiwa kitendo kama kile, alipojiinua alikutana na teke zito kutoka kwa Moses lililompata la mdomo hadi damu zikawa zimeanza kumtoka.
"mtoto mdogo unakimbilia mali usizoziweza, Beatrice ni wa mkuu wetu" Yule dereva aliongea kwa dharau ingawa kapigwa mdomoni hadi jino likawa limemtoka, Moses alipandwa zaidi na hasira na akaachia teke ambalo lilionwa vizuri na yule dereva. Dereva wa landcruiser alimzoa Moses kwa ngwara ya chini kisha akasimama sawasawa akimsubiri Moses asimame, Moses alisimama haraka huku akimtazama Dereva kwa hasira. Ngumi za nipige nikupige ndiyo zilifuatia kwa muda huo huku eneo la ajali likiwa limezungukwa na umati mkubwa wa watu, polisi hadi muda huo walikuwa hawajawasili ingawa simu ilishapigwa kituoni muda mrefu. Ugomvi huo uliendelea hadi pale wasamaria wema walipowaamua wakiwa wamechoka wote ingawa bado yule dereva alikuwa ana dharau.
"na bado wewe hadi umuache Beatrice ndiyo utaishi kwa amani" Aliongea yule dereva huku akiondoka eneo la tukio bila kusubiri askari wa barabarani kuja kupima ajali, Moses naye hakutaka kusubiri eneo hilo. Yeye pamoja na Hilary waliingia kwenye gari kisha wakaondoka eneo hilo, Moses alikuwa kapasuka sehemu nyingi za mwili wake hasa usoni kutokana na makonde mazito ya yule dereva ingawa naye alimjeruhi mtu kwa makonde aliyoyashusha.
****
JIONI
MAISHA CLUB
JIJINI DAR ES SALAAM
Andrew pamoja na kundi lake waliokuja kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Beatrice walikuwa wapo katika eneo lenye giza, mbele yao kulikuwa kuna yule dereva wa land cruiser aliyegonga gari ya Hilary kwa nyuma akiwa ana plasta kadhaa usoni. Andrew pamoja na wenzake walizidi kushangaa hali aliyokuwa nayo dereva huyo, walitegemea kazi yao ya kumtisha Moses ili amuache Beatrice ingefanikiwa. Kujeruhiwa kwa mtu waliyemtuma ndiko kuliwashangaza sana.
"Kwahiyo imekuaje ulivyoenda huko?" Andrew aliuliza kwa mshangao.
"dogo yule ni sumu kabisa yaani hafai, nadhani mnaniona nilivyo" Yule dereva aliongea.
"kwahiyo yule fala ndiyo kakufanya wewe hivi?" Rafiki mmojawapo wa Andrew alimuuliza.
"unauliza majibu, madogo sikieni kwa umakini. Kama kazi yenu ndiyo hiyo basi tena, yaani dogo hana ufundi wa kupigana ila balaa nimelipata. Mi kazi yenu basi na hela yenu ndiyo hii imenitibu na nyingine nitasogezea maisha na siwezi kuirudisha" Aliongea yule dereva kisha akanyanyuka kwenye akaondoka akiwaacha waliompa kazi wakiwa wanashangaa.
"oyaa Andrew ushauri wa sista wako naona unafaa kuliko hii njia unayotumia" Rafiki mwingine wa Andrew alimshauri kuhusiana na suala hilo.
"man unajua nini, plan ya sista anamtaka yule fala na mimi sitaki ampate sista hata kama sista kamaindi mi barida tu niko radhi amkose na jamaa atoswe na Bite" Andrew aliongea.
"hivi we unampenda Bite kweli na unamtakia sista wako mema" Mwingine alimuuliza.
"ndiyo nampenda Bite na namtakia mema sista" Andrew alijibu
"basi fuata ushauri wa sista wako kwani kuchukuliwa na huyo lofa ni kiti gani, yeye si mwanamke pia na anapenda" Alishauriwa na rafiki yake aliyemuuliza swali, Andrew alitaka kuongea lakini mlio wa kuita katika simu yake ulimkatisha na ikamlazimu apokee baada ya kujua ni dada yake.
"sema sista" Andrew alisema kisha akatulia kimya akiwa amekunja uso akisikiliza maneno yanayotolewa na dada yake ambaye alisikika akiongea kwa ukali hata kwa wenzake, simu ilipokatika Andrew alishusha pumzi kisha akasema, "oyaa janga jingine hili, sista kashtuka mchezo wetu. Jamaa kumbe naye kaumia na alikuwa hospitali".
"umeona sasa mwana si msala huo, unafikiri atakusaidia umpate Bite wakati umecheza karata chafu dhidi ya anayempenda" Lawama iilianza kumshukia Andrew kutoka kwa rafiki yake aliyekuwa anamshauri.
"si muda wa kulaumiana mshkaji huu, kwanza hapa tusepeni maana naona hakunifai tena" Andrew aliongea huku akisimama kwa ajili ya kuondoka eneo hilo, wenzake nao walimfuata pasipo kusema chochote.
ITAENDELEA!
No comments:
Post a Comment