Wednesday, December 9, 2015

SHUJAA SEHEMU YA TANO

RIWAYA: SHUJAA

MTUNZI: Hassan O Mambosasa

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE

ANGALIZO: UANDISHI WA SEHEMU HII YA TANO UMETUMIA LUGHA KIGENI KWENYE BAADHI YA SEHEMU HASA KATIKA UELEZAJI WA MTAALA WA KEMIA KWA KIDATO CHA SITA KUTOKANA NA UGUMU WA KUFASIRI LUGHA YA SAYANSI

ILIPOISHIA
Alitembea
kwa tahadhari hadi katikati ya miti iliyo jirani na
eneo hilo akiwa na kamera yake ya kipelelezi tofauti
na kamera yake ya kawaida. Ajibanza
hapo hadi aliposhudia ujio wa boti mfano wa
nyambizi iliyofika hadi ukingoni, hadi hapo aliweza
kupiga
picha kila anachokiona kwa msaada wa mwangaza
uliotoka katika taa ya helikopta na taa ya boti. Hadi
watu sita wanashuka kwenye boti ile alikuwa
amewaona na amewapiga picha, boti hiyo pia
alikuwa ameiona na ameipiga picha pia na helikopta
aliipiga vizuri akilenga namba zake zilizopo ubavuni.
Alipomaliza alibaki palepale hadi walipoingia ndani
ya helikopta kuondoka, na ile boti ilipozama chini.
Hapo alirudi kwenye hema kisha akajilaza pembeni
ya msimamizi wake kama ilivyokuwa awali. Hadi
asubuhi inaingia alikuwa macho na jua
lilipochomoza alikusanya vitu vyake kisha
akaondoka porini hapo akiwa na msaidizi aliyepewa

ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI
YAKE

SEHEMU YA TANO
Alifika kisha akakabidhi kila kitu alichokabidhiwa na
ofisi za pori hilo halafu akakodi gari ya kumpeleka
bukoba mjini, uzuri wa hifadhi ya Biharamulo ilikuwa
ina magari ya kukodiwa maalum kwa ajili ya wateja
wao. Norbert alipata gari aina ya landcruiser yenye
mkonga ambayo iliwekwa hapo mahususi kwa
ajili ya kukodiwa, alielewana bei na dereva wa gari
hilo kutoka hapo hadi Bukoba mjini. Baada ya
makubaliano kufikiwa alipanda gari hiyo kisha safari
ikaanza, kwa kuelekea barabara iendayo kaskazini
mwa Biharamulo ili kuisaka Bukoba, ubora wa gari
aliyoikodi kwa masafa marefu ulimfanya awe na
uhakika wa kuwasili Bukoba ndani ya masaa kadhaa.
Pia dereva wa gari naye alijua sana kucheza na
usukani wa gari pamoja na kupangua gia, uhodari
wa dereva huyu ulimfanya Norbert atabasamu na
akijipongeza kwa chaguo lake bora miongoni mwa
madereva wengi aliowakuta jirani na ofisi za hifadhi
ya Biharamulo, walitumia masaa kadhaa wakawa
wameshafika mwanzo wa barabara ya Uganda
inayoeleiea Bukoba mjini. Dereva wa gari hilo alipita
kushoto ili azunguke mzunguko unaounganisha
barabara anatoka na barabara iendayo Bukoba mjini,
aliingia kushoto kuishika barabara hiyo kwa
mwendo wa wastani kisha akaongeza mwendo
baada ya kuingia rasmi katika barabara ya Uganda.
Hakika alimpata dereva aijuaye barabara za mkoa
huo kiundani zaidi kutokana na kuwa mwenyeji wa
mkoa huo. Dereva huyu alinyoosha barabara hiyo ya
Uganda hadi alipofika mwanzo wa barabara ya
Kawawa kisha akangia kushoto kuifuata barabara ya
Kawawa kuelekea mtaa wa Biashara kwenye
barabara ya biashara, aliingia katika barabara ya
Biashara kwa mwendo hadi katika kona ya barabara
iendayo makutano ya barabara ya sokoine ,hapo
alikata kona upande wa kulia kuelekea yalipo
makutano ya barabara hiyo na ya Sokoine. Alipofika
makutano ya barabara za Sokoine na Jamhuri
alinyoosha moja kwa moja kuifuata barabara ya
Jamhuri kwa mwendo wa kasi hadi yalipo makutano
ya Barabara ya Barongo na Jamhuri, hapo
alipunguza mwendo kisha akavuka makutano hayo
kwa mwendo wa wastani halafu akanyoosha moja
kwa moja kuifuata tena barabara ya Jamhuri hadi
zilipo ofisi za CCM hapo aliegesha gari kisha
akateremka akimuacha Norbert ndani ya gari .
Alirudi baada ya dakika kadhaa akiwa na pakiti ya
konyagi akiinywa mdomoni kisha akapanda kwa ajili
ya kuliondoa gari eneo hilo.

"kaka hiyo si pombe na unaendesha gari, hivi si
hatari hiyo?" Norbert alimuuliza

"usijali kaka kuhusu hii kwani bila hii mimi siwezi
kuendeshagari vizuri" Dereva alijibu huku akiweka
gia kuingia barabarani

"ok ni sawa tu tuendelee na safari" Norbert aliongea
kwa mara ya mwisho kisha akakaa kimya kumuacha
dereva aendelee na kazi yake . Dereva aliendelea na
makeke yake ya kuendesha gari huku mkono mmoja
akinywa kipakiti cha konyagi hadi akakimaliza,
alinyoosha barabara ya Jamhuri hadi katika
makutano ya barabara hiyo na barabara ya
Aerodrome.
Alinyoosha barabara hiyo hadi karibu na uwanja wa
ndege wa bukoba kisha akaweka gari pembeni
baada ya kupokea amri kutoka kwa Norbert, Norbert
alishuka hapo kisha akampatia malipo dereva huyo
kama walivyokubaliana. Dereva wa gari aligeuza
kisha akaondoka eneo hilo na Norbert akaelekea katika
ofisi za uwanja wa ndege wa Bukoba kwa miguu.
Baada ya muda mfupi alifika ofisi za uwanja wa
ndege huo kisha akaenda hadi mapokezi. Hapo
mapokezi alimkuta msichana aliyekuwa akiongea na
mgeni, alisubiri hadi alipomaliza kuongea na mgeni
ambaye alionekana ni mteja kisha akamfuata katika
dawati la mapokezi. Alimshika kidevu kwa namna ya
uchokozi.

"we mwanaume wewe naona umetoka kwa mke
mwenzangu" Msichana wa mapokezi alianza
kumtania Norbert pasipo salamu baada ya
kuchezewa kidevu

"aah! bibie mi kijana sasa ulitaka niende wapi"
Nobert aliongea kwa sauti ndogo huku akiwa
ameegemea meza.

"khaa! Yaani umeniacha mimi unaenda kwa bibi
mwingine, muone hutulii kama jogoo" Msichana wa
mapokezi akiongea huku akiwa ameuvuta mdomo
kwa namna ya kudeka.

"bibie usinune basi utasababisha na mimi ninune,
kumbuka ukitabasamu na mimi ndiyo nitatabasamu.
Nilikuwa kikazi zaidi mama" Norbert aliongea ili
kumfanya msichana huyo atabasamu, msichana
huyo alipotabasamu alimwambia "Frida nipe basi
niwahi maana muda ndio huu". Frida aliingiza
mikono chini ya meza ya mapokezi baada ya
kuambiwa hivyo, alitoa tikiti moja ya ndege ya
fastjet kisha akampatia Norbert.

"watu wameshaanza kuingia Nor, hebu wahi" Fridah
alimwambia Norbert

"haya bibie nikirudi jiandae maana nitapeleka posa
kwenu" Norbert aliongea akiwa anaelekea ndani ya
uwanja.

"nyooo lione vile na ukapera umwachie nani" Fridah
alimsindikiza na maneno hayo huku akiwa
amebinua mdomo.

****

 
SHULE YA NEEMA TRUST
"Soil Colloids, the colloidal state refers to a two-
phase system in
which one material in a very finely divided state is
dispersed through second phase.
The examples are:
Solid in liquid - Clay in water (dispersion of clay in
water)
Liquid in gas -Fog or clouds in atmosphere
The clay fraction of the soil contains particles less
than 0.002 mm in size. Particles less than 0.001
mm size possess colloidal properties and are
known as soil colloids. There are ten properties of
soil colloids, anyone can mention them?" Dkt
Jameson alitiririka katika kufundisha katika darasa la
kombi ya PCB kidato cha sita kwa mara ya kwanza toka
alipotambulishwa kwa wanafunzi asubuhi ya siku
hiyo, aliuliza swali na kupelekea darasa zima libaki
na mwanafunzi mmoja tu ndiye aliyenyoosha
mkono.

" your name please(jina lsko tafadhali)" Dkt
Jamesom alimwambia mwanafunzi huyo.

"Moses Gawaza" Mwanafunzi huyo alitaja jina lake.

"ok you can continue(sawa unaweza ukaendelea)
Dkt Jameson alimwambia

"The properties of Soil colloids are size, surface
area, surface charges, absorption cation, absorption
of water,cohesion,adhesion,swelling and shrinkage,
dispersion and floculation, brownian movement and
non permeabilitiy" Moses alitiririka kisha akaketi
kwenye meza yake alipomaliza.

"very good, clap your hands for him(vizuri
sana,mpigieni makofi )" Dkt Jameson aliongea akiwa
na tabasamu pana usoni mwake na kupelekea wanafunzi wote wapige makofi

"Iam hope you know the general properties of Soil
colloids through Mr Gawaza, lets continue in details (natumai
mnajua sifa kuu za Soil colloids kupitia kwa bwana Gawaza tuendelee kiupana).
Size: The most important common property of
inorganic and organic colloids is their extremely
small size. They are too small to be seen with an
ordinary light microscope. Only with an electron
microscope they can be seen. Most are smaller
than 2 micrometers in diameter...." Dkt Jameson
aliendelea kutiririka ili wanafunzi wake wamuelewe.
Hadi kipindi kinaisha tayari muda wa kutoka
shuleni hapo ulikuwa unakaribia, wanafunzi wote
walifurahia sana kipindi cha Dkt Jameson
kilichowafanya waelewe mambo mengi katika somo
la Kemia. Dkt Jameson alimuita Moses baada ya
kumaliza kufundisha kisha akaelekea ofisini, Moses
alitoka kwenda kuelekea ofisini alipoitwa na Dkt
Jameson.

"kaa kwenye kiti Gawaza" DKt Jameson alimwambia
Moses alipoingia ofisini kisha akainuka akiwa
ameshika faili akielekea kwenye makabati ya mafaili
halafu. Aliweka faili kwenye kabati halafu akarejea.

"ndio mwalimu" Moses aliitikia wito.

"unaweza ukaniita kakaJameson kwani mimi ni
kijana kama wewe tu isipokuwa nimekuzidi kielimu
tu" Dkt Jameson alikataa kuitwa kwawadhifa
aliostahiki.

"ndii kaka Jameson" Moses akasema.

"Gawaza najua wewe ni mwanafunzi mwerevu sana
na unajua vitu vingi ambavyo baadhi ya wenzako
hawavijui, sasa kwanini usiwe unawaelekeza
iliwaelewe kama wewe"

"ujue mimi najua kidogo tu na katika hicho kidogo
huwa namfanya mwenzangu atakaye kukijua ili
akijue. Hivyo suala la mimi kuwaelekeza wenzangu
najitahidi ingawa kuna wengine hawataki
kuelekezwa".

"vizuri sana hivi huwa unasoma masomi ya ziada
sehemu? kama unasoma basi hakikisha na wenzako
wanapajua ili wakasome"

"sisomi masomo ya ziada popote ila nilikuwa
ninafundishwa na baba yangu mzazi ambaye kwa
sasa ni marehemu".

"ooh! Pole sana kwa hilo, je baba yako naye alikuwa
mwalimu?"

"hapana hakuwa mwalimu bali alikuwa ni
mwanasayansi maarufu"

"mwanasayansi?! Nawajua wanasayansi wa karibia
bara zima la Africa,jina lake ni nani?"

" Professa Lawrence Gawaza"

"sawa nishamtambua, alikuwa ni mmoja wa
maprofessa wa chuo cha Havard na aliacha kazi
akarejea Tanzania kuendelea na shughuli zake
binafsi. Unaonekana una kipawa kama cha baba
yako, jitahidi utakuwa kama yeye. Ni hayo tu
unawezaa ukarudi darasani".

"sawa kaka asante"

Moses alinyanyuka kwenye halafu akapeana mkono
na Dkt Jameson kisha akaondoka kuelekea darasani.
Muda wa kutoka ulipofika Beatrice alikuja darasani kwa akina Moses
akiwa na bahasha mkononi mwake, alienda hadi
alipo Moses kisha akachukua kiti kilicho jirani
akaketi.

"mambo" alimsabahi Moses

"poa, za masomo" Moses aliitikia salamu akiwa
ametabasamu.

"safi tu, niambie msongolisti wangu" Beatrice
alitumbukiza utani

"nikuambie nini mlimbwende cha zaidi, au nikutolee
mambo ya electric potential sasa hivi" Mosea
alitumbukiza utani na kupelekea Beatrice acheke.

"unataka kunipasua kichwa nini yaani hiyo History ni
janga kwangu" Beatrice alisema huku akimpatia
bahasha Moses halafu akamwambia "ni kadi hii
kesho njoo nyumbani tafadhali ni sherehe yangu ya
kuzaliwa".

"usijali nitakuja maana si jumamosi, tarajia ugeni
wangu Bite"

"sawa leo ninaondoka na gari ya dady maana
amenifuata yupo nje, inabidi nikuage kwa namna
ninayopenda kama hutojali"

"ok niage basi upendevyo Bite".

"waao! simama basi".

Moses alisimama akijua anaagwa kwa namna ya
kawaida tu, akiwa amesimama alishtuka akiwa
amekumbatiwa na Beatrice. Ulaini wa mwili wa
Beatrice na joto lake ulimfanya ajihisi amepigwa
shoti ya ajabu mwilini mwake, Beatrice alimbusu
Moses shavuni kisha akaondoka huku akisema "bye
bye".
Moses alibaki ameduwaa akimtazama Beatrice
aliyekuwa akiondoka, Bratrice alipopotea katika upeo
wa macho yake alibaki akiwa ameduwaa kwa
kilichotokea.

"we boya bisha tena nikuone,changamkia tenda
hiyo" Sauti ya Hillary ilisikika kutoka nyuma yake na
kupelekea akurupuke kwenye mawazo.

"yaani mtoto anajilenga mwenyewe we unashindwa
kumaliza" Hillary aliendelea kumlaumu Moses.

"naona leo umeamua uniaibishe" Moses alimwambia

"nikuaibishe kwa lipi wakati wote wamesepa" Hillary
alimwambia Moses. Moses aliangalia darasa zima
na kukuta darasa lote ni tupu na wao wawili tu ndio
waliobaki.

"daah! Nilijua kuna wanga wananichora" Moses
aliongea huku akichukua begi lake la vitabu.

"wacha uoga wewe ,naona kakupatia barua kabisa"
Hillary alimwambia

"ni kadi tu ya mwaliko"

"poa tusepe kama vipi".

Walitoka humo darasani wakiwa wanaongea mambo
yao mbalimbali, utani kwa marafiki hawa ilikuwa ni
kitu cha kawaida sana.




ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment