Monday, December 7, 2015

SHUJAA SEHEMU YA TATU







RIWAYA: SHUJAA

MTUNZI: Hassan O Mambosasa

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII KWA MARA NYINGINE

ANGALIZO: KAZI YA RIWAYA HII YA KISWAHILI NI KUELIMISHA NA KUENDELEZA KISWAHILI. NDIO MAANA NIMETUMIA KISWAHILI SEHEMU WANAPOZUNGUMZA WAGENI ILI NIENDANE NA JAMII WANAYOSOMA, BAADHI YA MANENO YA KINGEREZA YAMETUMIKA KUAKISI JAMII YA SASA ISIVYOTHAMINI LUGHA YA TAIFA

ILIPOISHIA
Siku iliyofuata Beatrice aliwahi kantini baada ya tu
ya kusikia kengele ya mapumziko, alikaa katika kiti
kilicho mkabala na kiti anachokalia Moses kila siku .
Baada ya muda Moses alifika hapo kantini akiwa
amebeba vitabu mkononi, alienda hadi kwenye kiti
anachokitumia siku na kumkuta Beatrice akiwa
tayari keshawasili eneo hilo. Aliweka vitabu na
kumsabahi
"mambo Bite" ha lafu akavuta kiti na kuketi, Beatrice
alimjibu, "safi tu upo poa?". Alivuta kiti na kuketi
kisha akasema "nipo poa, naona leo umeniwahi" ,
kauli hiyo
ilimfanya Beatrice atabasamu pasipo kusema lolote
huku akimtazama Moses.

ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI
YAKE

SEHEMU YA TATU
Moses aliinuka na kwenda kuagiza kifungua kinywa
kisha akarejea kitini, alimtazama Beatrice na
kumuambia, "mbona leo mtulivu hivyo kuliko
kawaida?". Beatrice akamwambia, "walaa nipo
kawaida siku zote ila sitaki kuongea sana kama kila
siku".

Moses akauliza, "mmmh! kwanini?"

"we unataka nipaliwe kama jana" Beatrice akaongea
kwa sauti yenye mchanganyiko wa deko na
kusababusha Moses acheke. Hakika kiliwazo kingine
kwa Beatrice baada ya kumuona mvulana
anayempenda akicheka, alitokea kupenda karibu kila
kitu cha Moses kasoro huzuni yake.

"na wewe umezidi" Moses aliongea huku akicheka

"na wewe bwana hebu acha hayo, hivi jana ulitaka
kuniambia nini?"

"ohoo! Halafu nilitaka nisahau"

"tell me now(niambie sasa)"
Moses alimuashiria Beatrice angoje kwanza muda
huo alikuwa na anatafuna kitafunwa mdomoni,
alimeza kisha akapika funda moja la chai.
Alipolimeza akasema, "Beatrice najua umejua
umetokea kuwa rafiki yangu mkubwa kwa muda
mfupi tu toka tulipoanza kuwa marafiki", aliposema
hivyo akajiweka vizuri kwenye kiti kisha akaendelea,
"sasa basi nataka unisaidie jambo moja tu kama
utaweza".

"Jambo gani hilo Mose?"

"relax Bite ndio ninakwambia sasa"

"sawa Iam listening you(ninakusikiliza)"

"najua unajua ni kiasi gani nimekuwa nikisumbuliwa
na mdada mwenye kujiita Dream girl, sasa nataka
unisaidie katika kumpata huyu mdada maana
nimechoshwa na tabia yake ya usumbufu"

"sasa hapo how can i help(nitawezaje kusaidia) maana hata huyo mdada
hata mimi simjui"

"I know its hard but try (najua ni ngumu lakini jaribu)ikiwa unanipenda
unanipenda mimi kama rafiki yako"

"mmh! Kusema kweli unanipa majaribu"

"unapenda kuniona nikiwa nina furaha"
"Yeah! Napenda kukuona ukiona ukiwa na furaha"

"please help me(please help me) kama unapenda kuniona nina furaha".

Beatrice allijifikiria kwa muda kisha akasema, "ok I
will try(saa nitajaribu)". Kauli hiyo ikimfanya Moses atabasamu
huku akisema "ukifanikiwa nitakupa zawadi yoyote
uitakayo". Waliendelea kunywa chai hadi muda
wakamaliza kabla ya muda wa mapumziko
haujaisha, waliendelea kuongea mambo mengine ya
kawaida huku Beatrice akiwa ni mwenye furaha
muda wote kama ilivyo kawaida yake. Hatimaye
kengele ya kurudi darasani ikagongwa, wote
walinyanyuka na kuondoka kurudi darasani.
Walitembea hadi sehemu ambayo kila mtu
anatakiwa kuelekea mahali yalipo madarasa yao ,
hapo Beatrice akamwambia Moses, "tuonane muda
wa kutoka kama hutakuwa na nafasi". Moses
alimuonesha ishara ya dole gumba ya kukubaliana
na jambo alilolisema, Moses akiwa na vitabu vyake
mkononi aliamua kuelekea darasani kwao moja kwa
moja. Siku hiyo Moses alijikuta akiwa na hisia za
ghafla juu ya Janet, kila akimfikiria alitamani kuwa
naye karibu zaidi. Akiwa darasani baada ya kipindi
cha kwanza baada ya mapumziko kuisha alijikuta
akimuuliza rafiki yake kipenzi humo darasani kwao,

" Hilary umemuona yule demu niliyekuwa nae
kantini?"

"ndiyo si Beatrice au kuna mwingine?" Hilary alijibu
na kuuliza swali papo hapo.

"unamuonaje?" Moses alimuuliza Hilary.

"aisee yupo poa sana, tena kazama kwako au
hujashtuka?"

"wala hamna kitu kama hicho"

"Mose wa wapi wewe yaani kukaa naye huko kote
bado hujajua"

"hamna hicho kitu wewe punguza fikra zako"

"ok tuache hayo, kwanini umeniuliza hivyo?"

"uongo dhambi ndugu, nahisi kumuhitaji baada ya
necta kuisha?"

"aisee leo umekuwa vipi? maana sio kawaida yako"

"Acha udaku we mwanga, mengine yakaushie tu".
Kauli hiyo ilimfanya Hillary acheke sana huku
akisema, "maajabu ya daunia msongolisti kanasa
leo". Moses naye alijikuta akicheka kwa kauli ya
utani aliyoitoa Hilary.

"haya msongolisti mgoni tupige msuli sasa nahisi
ticha haingii huyu" Moses naye akatumbukiza utani
huku akifungua daftari lake lililopo juu ya meza.
Muda wa kutoka ulipofika Moses na Beatrice
walikutana pale walipoachana awali, siku hiyo
Beatrice alitaka waondoke pamoha na Moses. Moses
akiwa na usafiri wake aliokuja nao alikubali pasipo
kuweka walakini wa aina yoyore, alimfungulia
mlango wa gari na kumruhusu kama malkia wake.

"mmh na wewe bwana kwa mbwembwe" aliongea
Beatrice baada ya kuona Moses amemfungulia
mlango kama kijakazi afanyavyo kwa malkia.

"sasa mgeni akiingia kwenye mali ya mwenyeji
lazima anyenyekewe" Moses alitetea kitendo chake
cha kumfungulia mlango Beatrice. Baada ya Beatrice
kuingia ndani ya gari naye alizunguka upande wa
dereva kisha akamuuliza Beatrice, "nikuache wapi?".
Beatrice akajibu pasipo kumuangalia Moses
"mikocheni kama unaelekea huko". Kauli hiyo
ilimfanya Moses atabasamu baada ya kubaini
wanaelekea sehemu moja, aliwasha gari kisha akaendesha kuelekea getini kisha akatoka na kuingia
barabarani kisha akaliondoa kwa mwendo wa kasi.
Baada ya dakika takribani thelathini walikuwa
wamefika mikocheni katika mtaa wa Warioba
sehemu ambapo kuna barabara iendayo mtaa wa
mazinde, Beatrice aliomba kushushwa
njiani, "kwanini nisikupeleke hadi kwenu?" Moses
aliuliza.

"usijali hapa panatosha tu" Beatrice aliongea akiwa
tayari ameshafungua mlango wa gari baada ya
Moses kusimamisha gari.

"Moses usijali nimefuatwa na gari na dereva yule
pale" Bearice aliongea huku akionesha kwa kidole
upande wa pili wa barabara jirani na waliposimama.
Moses alipotazama pembeni ya barabara aliona gari
aina ya Toyota landcruiser V8 ikiwa imeegeshwa
pembezoni mwa barabara mkabala na alipoegesha
gari lake. Hadi muda huo Beatrice alikuwa tayari
ameshashuka garini na sasa alikuwa akivuka
barabara huku akimpungia mkono Moses, baada ya
Beatrice kuingia katika gari lililomfuata Moses
aliondoa mguu wake kwenye breki kisha akakanyaga mwendo
na kupelekea gari ianze kuondoka taratibu. Allikata
kona kuingia njia iendayo mtaa wa Mazinde ambapo
ndio anaishi, alinyoosha barabara moja kwa moja hiyo moja
mwa umbali mrefu kiasi kisha akakata kushoto
kuingia mtaa wa mazinde halafu akaelekea moja
kwa moja hadi kwenye geti la nyumbani kwao


****

JIJINI KISUMU
NCHINI KENYA
Ndani ya klabu ya hoteli ya Sunset pembezoni mwa
mji huo upande wa magharibi wa nchi hiyo, ndani
ya hoteli hiyo ya nyota tatu kulikuwa na mkutano
mkubwa wa watu wenye maslahi ya aina moja.
Brian, kundi la wazungu wenzake ndio wahudhuriaji
wa mkutano huo wenye. Msemaji wa kikao hicho
alikuwa ni Brian ambaye alifungua kikao hicho kwa
kusema, "habari za jioni ,natumai kila mmoja wetu ni
mzima wa afya na ameitikia wito wa mkutano huu
wa siri wa umoja wetu kwa kujua lengo la mkutano
huu. Pia nadhani ni muda muafaka kwa sisi
tuunyamzishe umoja wa Ulaya ambao umekuwa
kikwazo katika biashara yetu inayotuweka mjini na
inayotuwezesha sisi kuendesha biashara zetu
nyingine, nadhani nyote mnajua kwamba tulimtuma
Tasi akachukue virusi kwa namna yoyote baada ya Professa
kugoma kufanya biashara nami" alinyamaza kwa
muda kisha akanyanyua bilauri ya pombe iliyopo mezani
halafu akapiga funda moja.

"Professa huyu aligoma baada ya kusikia kuwa nina
mpango wa kuvijaribu nchini Tanzania kwenye
makazi yake na ambapo anapatikana mwanae
kipenzi, kutokana na ukaidi sisi tukamwambia
atumie mbinu mbadala ili aweze kutupatia bure
maana mwanzo aligoma kutupatia kwa malipo. Tasu
alifanikiwa kumchoma Professa sindano ya sumu
inayoua taratibu ambayo hadi inamuua hakuwa
ametupatia virusi hao, dawa ya sumu hiyo tulikuwa
tunayo na ikatulazimu tumwambie atapata dawa
kama akileta virusi mikononi mwetu. Yote hayo
bado Professa alikaidi na akaishia kusema ipo
mikononi kwa mtu wake anaemuamini na
hatutowapata, hivyo basi hayo ndio maneno
aliyotuchia yenye ukaidi. Sasa nataka nisikilize
mawazo yenu kila mmoja ili tuweze kupata njia
mbadala" alihitimisha kisha akawatazama
wahudhuriaji wa mkutano huo kila mmoja. Mmoja
wa wazungu alinyoosha mkono na kupelekea Brian
asema , "ndio Obren tunakusikiliza"

"Bosi mi naona tumuache Tasi aendelee na kazi
yake na kama akishindwa tutamuongezea nguvu ili
atuwezeshe kupatikana kwa huyo wa kumuaminiwa
na Professa apatikane haraka iwezekanyo" aliongea
Obren kisha akakaa kwenye kiti chake. Mzungu
mwingine alinyoosha mkono na kupelekea Brian
aseme ,"ndio Campbel tunakusikiliza"

"bosi mimi sikubaliani kabisa na Mr Obren kwa
jambo alilolizungumza, nashauri sis ndio tuingie
kazini na huyo Tasi tumtumie kivingine ila si
kwenye kazi hii" Campel aliongea na kupelekea watu
wote waafiki kwa kutikisa vichwa kuashiria
wamekubaliana na rai ya Campbel. Brian aliinuka
kwenye kiti chake kisha akasema "je kuna mwenye
la ziada juu ya hili? nadhani nyote mmekubalia na
ushauri wa Campbel, sasa kikosi chenu wenyewe
kiingie kazini kuanzia muda huu hamna la ziada".
Brian alihitimisha kisha akainuka kwenye kiti chake
halafu akaondoka.Wote waliobaki walitazamana kila
mmoja huku ukimya ukimya ukiwa umetawala,
Cambel aliuvunja ukimya huo kwa kusema, "jamani
tukutane kambini kwetu kule kwenye mbuga" halafu
akainuka kisha akaondoka eneo hilo.


****


MASAA MAWILI BAADAE
KWENYE MBUGA YA KENYA WILD IMPALA
Mbuga hii iliyo jirani iliyo jirani na ziwa Victoria
kulikuwa na na handaki kubwa sana lililochimbwa
kilomita mbili kutoka ziwani, ndani ya Handaki hilo
kulikuwa na kundi la watu takribani sita wenye asili
ya barani Ulaya. Watu hao walikuwa wameizunguka
meza kubwa ya duara iliyotengenezwa kwa chuma,
meza hiyo ilikuwana urefu uliowafikia kiunoni mwao,
katikati ya meza hiyo kulikuwa na karatasi kubwa
lilioenea karibu meza nzima.

"nafikiri tutumie boti yenye uwezo wa kuzama kama
ilivyo Nyambizi" aliongea Obren ambaye alikuwa ni
mmoja kati ya watu waliokuwa wapo eneo hilo.

"ni njia sana nzuri, sasa tukatokee sehemu gani
iliyokuwa salama" aliongea mzungu mwingine kisha
akauliza swali.

" Calvin mbona rahisi hiyo, tutapita chini kwa chini
hadi katika pori la Rubondo lililopo katika kisiwa cha
Rubondo kisha hapo tutafanya mapumziko ya muda
kisha tutaendelea hadi Kagera" Campbel alijibu swali
hilo huku akielekeza kwenye ramani sehemu
wanazopitia.

"njia nzuri hiyo nadhani ramani itatusaidia kufika"
alisema Calvin

"ndio inasaidia na tukifika huko tutachukuliwa na
helikopta hadi kibaha halafu hapo tutakutana na
Tasi" aliongea Campbel.

"Obren, Calvin, Scott , Jameson na Christian
nadhani tupo pamoja sasa team mambas tuingie.
kazi!" alihitimisha Campbel kisha akanyoosha ngumi
mbele na kupelekea wenzake wote wanyooshe
ngumi na kukutanisha ngumi ya Campbel.

"kazii!" wote waliitikia kwa pamoja kisha wakatoka
kwenda kuchukua vitu vyao vya muhimu



ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment