Tuesday, December 22, 2015

SHUJAA SEHEMU YA KUMI NA NANE







RIWAYA: SHUJAA


MTUNZI: Hassan O Mambosasa

SIMU:+255713776843
+255762219759



WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE


SEHEMU YA KUMI NA NANE!!
"mzigo wako huo hapo nyuma ya kiti" Norene aliongea huku macho yakiwa kwenye kioo cha tarakilishi, Norbert alichukua sanduku aliloelekezwa kisha akamtekenya Norene halafu akambusu shavuni. Alichukua begi dogo lenye umbo kama mkoba wa kuhifadhia pesa halafu akaanza kuondoka ofisini humo.
"Nor" Norene alimuita na kumfanya asimame kumsikiliza, Norbert alirudi hadi pale alipo Norene kisha akamtazama Norene.
"kazi njema ila ukae utambue nakupenda" Norene alimuambia Norbert kisha akabadilishana naye shurubati ya kinywani mwake kwa dakika nzima.
"kila la heri" Norene alimuambia Norbert kisha akaendelea na kazi zingine, Norbert aliondoka bila kusema chochote zaidi ya kutabasamu.


****


Asubuhi ya siku iliyofuata ilkuwa ni siku ya pilika pilika kwa kila mtu mwenye wajibu, ilikuwa ni siku ya jumanne ambayo ndiyo siku ya pili ya mwanzo wa wiki. Siku hii wanafunzi wote walikwenda shuleni kwa ajili na aliyebaki nyumbani basi alikuwa mtoro au mgonjwa, siku hii ilikuwa ni siku ya kukaa nyumbani kwa Moses kwani hali yake haikumruhusu kwenda shule kama ilivyo kawaida yake. Ugomvi wake na baunsa Mponjo ndiyo ulisababisha abaki nyumbani kutokana kuumia sehemu mbalimbali za mwili wake. Upweke wa nyumbani kwao uliotokana na ukosefu wa watu ndani ya nyumba hiyo, ulimfanya ajione anaishi kwenye gofu ambalo alikuwa kama mateka.Ingawa nyumbani kwao kulikuwa na watu wawili waliosalia ambao ni msaidizi wa kazi na mlinzi, bado alikuwa na upweke kutokana na kutokuwa na mazoea nao hao wafanyakazi wa nyumba hiyo zaidi ya kuongea nao pale inapobidi. Siku hiyo aliamua aipitishe kwa kuangalia filamu baada ya kumaliza kusoma masomo yake, alichagua kati ya filamu anayoipenda inayoitwa district B13 ya mapigano isiyochosha kuiangalia. Moses aliangalia filamu hiyo hadi ikaisha kisha akaamua kutoka nje kupunga upepo kwenye bustani nzuri iliyopo pembezoni mwa  nyumba ndani ya uzio, alipofika hapo kwenye bustani aliamuagiza msichana wao wa kazi amletee shurubati ya parachichi ambayo ndiyo kinywaji pekee akipendacho akiwa nyumbani kwao, kinywaji kililetwa  akawa anapiga funda moja huku akiperuzi kwa kutumia simu yake ya mkononi. Hazikupita hata dakika kumi tangu akae hapo kwenye kiti cha kuning'inia kwenye bustani ya nyumbani kwao, simu yake iliita kwa kutetemeka kutokana kuitoa mlio jina lilionekana kwenye kioo ni Gate man. Moses aliipokea kisha akasema, "kwema kaka....mwanamke au mwanaume?....amesema anaitwa nani?........hajakuambia jina?......yupoje?........mh! Hebu mruhusu aingie mwambie nipo kwenye buatani......ok! Hamna shida". Moses alipomaliza kuongea na simu alibadilika  akawa na uso usio na furaha kwa alichokisikia kwenye simu alipoongea na mlinzi wa getini, macho yake  yote yalikuwa sehemu ambayo mtu akiwa na anatokea getini unamuona kutokana na taarifa aliyoipata kupitia simu. Baada ya dakika takribani moja mlinzi wa getini aliingia akiwa ameongozana na msichana ambaye Moses hakumtambua kwa haraka, alikuwa ni msichana aliyevaa gauni ya rangi ya waridi pamoja na kofia ya rangi urujuani. Msichana huyu chini alivaa viatu vya rangi ya urujuani kama ilivyo kofia yake ya kichwani ambayo wazungu hupenda kuiita Ladies Formal Hats, msichana huyu alipendeza haswa kutokana na umbo lake matata la wastani lisilokuwa na unene wa sana wala wembamba wa kupitiliza. Moses alibaki akimshangaa huyo msichana na alshindwa hata kumtambua kutokana na kofia aliyovaa. Uturi aliojipuliza msichana huyu ulikuwa ukizishambulia pua zake kwa muda huo, alibaki akimshangaa huyo msichana asijue aliwahi kumuona wapi.
"dogo mgeni  wako huyu hapa nimeamua nimlete kwani huku bustanini hakujui" Mlinzi alimuambia Moses baada ya kufika eneo alilopo akiwa yupo na mgeni wa Moses.
"poa kaka haina shida, mgeni karibu" Moses aliongea kumuambia mlinzi kisha akamkaribisha mgeni wake ambaye hakumtambua hadi muda huo, msichana huyo alikaa jirani na Moses kwenye kiti kirefu cha kuning'inia alichokaa Moses. Msichana huyo alipokaa alimtazama Moses huku macho yake yakiwa hayaonekani dhahiri kwa Moses kutokana na kofia aliyoivaa kufunika sehemu kubwa ya uso wake, Moses aliishia kuona papi za midomo ya msichana huyo iliyopakwa rangi mdomo iliyompendeza sana. Moses alibaki akimtazama msichana huyo kwa umakinl pasipo kutia neno lolote, yule msichana alipoanza kuivua kofia aliyovaa kichwani umakini wa Moses katika kumtazama uliongezeka kuliko kawaida akiwa amepambwa  na shauku kuu ya kutaka kuuuona uso wa mrembo huyo. Msichana alipomaliza kuvua kofia aliyoivaa ndiyo Moses naye uso wake ukabadilika kutokana na kuishuhudia sura ambayo si ngeni kwake, ni sura ya msichana ambaye ni mrembo na mwenye kila sifa ya kuitwa mrembo aliyekuwa ni karaha kwa Moses kila akimuona.
"wewe!" Moses aliishia kuongea huku uso wake ukionekana kutopendezwa na ujio wa msichana huyo, msichana huyo alikaa kimya huku akimtazama Moses kwa huruma.
"Annie unataka nini?" Moses aliongea huku akimkazia macho Annie aliyekuwa akimtazama kwa huruma kutokana na plasta kadhaa zilizopo usoni mwake.
"nakutaka wewe Moses na si kingine chochote ndiyo maana nipo hapa" Annie aliongea huku akimshika Moses kiganja cha mkono.
"ili mkanimalize sio? Mdogo wako jana ametuma mtu anifanyie hivi na wewe unitake kwa lipi" Moses aliongea huku akiutoa mkono wa Annie.
"Moses please nielewe nakupenda ndiyo maana nipo hapa kwa ajili yako na si vinginevyo, nimegombana na mdogo wangu kwa ajili yako. Nipo upande wako naomba unielewe" Annie alilalamika huku uso wake ukiwa unalengwa na machozi.
"Annie hivi wewe ni mwanamke wa aina gani usiyeelewa,wewe ni kama dada yangu kiumri na hata kielimu sasa suala kuwa na mimi kimapenzi sahau kabisa. Na hata kama jana hukuhusika na mchezo wa mdogo wako lakini huwezi kubadilisha moyo wangu nampenda Beatrice na vinginevyo" Moses aliongea huku akiwa anamaanisha kile anachokiongea kwa kutumia macho yake na hata mwili wake. Annie aliposikia maneno hayo alishusha pumzi kisha akauliza, "hivi unachokipenda kwa Beatrice ni kipi?", gauni aliyovaa Annie ilikuwa inamfikia kwenye mapaja juu ya magoti na alipouliza swali hilo alianza kuipandisha juu kwa kujitikisa mapaja yake. Alikuwa akimtazama Moses usoni huku akifanya kitendo hicho kwa madaha na macho akiwa ameyalegeza, hali hiyo ilizidi kumpa Moses wakati mgumu sana kwakuwa ni mwanaume rijali aliyetimia kwa kila kitu. Siku zote mwanamke kwa mwanaume ni kama mtego hivyo usipokuwa makini lazima unaswe na huwezi kusema kwamba unaweza ukaepuka kwa kutoweka umakini juu yake, hakuna mwanaume mwenye uwezo wa kujizuia lazima uukwepe kwa kuondoka. Hata nabii wa Mungu Yussuf alipowekewa mtego na mke wa waziri uzalendo ulimshinda ndiyo maana akaamua kukimbia kanzu yake ikavutwa ikachanwa kwa nyuma, laiti kama angekaa pale basi angekuwa ni miongoni mwa wapotevu. Mwanamke ni mtego tena zaidi ya mtego wa simba na ukiingia njia ya kuutoka ni kuukimbia, hata Moses uzalendo ulishaanza kumshinda hasa baada ya kuona mapaja ya Annie meupe yaliyojazia pamoja na nguo ya ndani yenye kuonesha.
"Annie please behave yourself, we ni kama dada yangu" Mosea aliongea huku akinyanyuka kwenye kiti huku uso wake akiwa ameangalia pembeni kumkwepa  Annie.
"ni kama lakini siyo dada yako na ninaweza kuwa na wewe  kama mpenzi wangu, hivi Beatrice ana kitu gajn nisichokuwacho mimi kama uzuri ninao na kila kitu ninacho. Nifanye nini ili unielewe Moses kama nakupenda, yaani nimeamua kuweka maungo yangu wazi mbele yako lakini hutaki kunielewa" Annie alizidi kulalamika kwa Moses.
"when eyes are not admire heart does not desire(wakati macho hayakutamani moyo hautahitaji) ndiyo una kila kitu alichonacho mwanamke lakini kama Beatrice lakini moyo wangu haupo kwako bali upo kwake. Mapenzi si kunifunulia miguu ndiyo nikupende Annie ni kufunuliana moyo kwa kila mmoja. Beatrice amenifunulia moyo wake na mimi nimemfunulia wangu, sasa basi moyo wangu umefunuka kwake ila si kwako. Jaribu kuwa kuelewa Annie" Moses aliongea huku akijikaza kisabuni akiwa amesimama amempa mgongo Annie asione maungo yake aliyoyaacha wazi, maneno hayo yalimuingia sana Annie na yakawa yamemgusa kwenye mtima wake hadi akajifunika vizuri miguu yake. Aliinuka pale alipokuwa amekaa akaenda kumkumbatia Moses kwa nyuma huku akihema sana.
"Nakupenda Moses naomba unielewe" Annie alilalamika huku machozi yakimtoka. Moses aliitoa mikono ya Annie kwa nguvu kisha akamwambia, " huwezi kulazimisha maji yapande mlima Annie, ninaye ninayempenda na sihitaji mwingine zaidi yake". Annie alibaki akitokwa na machozi kwa ajili ya Moses aliye na mtu anayempenda, Moses hakuonesha kumjali sana na badala yake alitoa simu yake kisha akabonyeza baadhi ya namba akaweka simu sikioni huku akisema, "niletee funguo ya Audi ". Alipokata simu alisubiri kwa dakika kadhaa ambapo aliletewa ufunguo wa gari na msichana wa kazi,
"kaka Moses si umeambiwa usiendeshe gari mpaka upone" Msichana alimuambia Moses.
"Dada si kazi yako unaweza ukaenda" Moses alimuambia dada wa kazi na aliingia ndani ya nyumba yao kwa dakika kadhaa kisha akatoka akiwa na mkoba wa marehemu baba yake aliopatiwa hadi pale bustanini.
"nadhani umekuja na usafiri wako na upo hapo nje kwaheri mimi natoka" Moses alimwambia Annie ambaye alionekana kutokuwa na dalili ya kuondoka na uso wake ukiwa umejaa majonzi. Annie aliposikia kauli hiyo alisimama kwenye kiti halafu akasema, "Moses machozi yangu hayapotei hivihivi bali yatalipwa tu", alipomaliza kuongea maneno hayo akiwa na hasira aliondoka akimuacha Moses akiwa hamuelewi alichomaanisha. Moses aliyafikiria maneno ya Annie kwa muda mfupi kisha akayapuuzia halafu akaelekea kwenye banda la gari ili aweze kuitoa gari mojawapo ambayo haipo kwenye maegesho ya magari.


****

Wakati Moses akiwa anataka kutoka ndani ya nyumba yao, sehemu nyingine ya jiji la Dar es salaam kulikuwa kuna mazingira yenye utulivu sana kutokana na ukimya wa eneo hilo. Eneo hilo ambalo ni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam katika wilaya ya Kinondoni, Bunju ndiyo jina la eneo hilo lenye ukimya na utulivu sana. Moja ya mtaa wa eneo hilo alionekana mzee wa makamo mwenye nywele za mvi akiwa na mavazi ambayo yalionekana kukosa maji kwa muda mrefu sana, mzee huyu alikuwa kabeba gunia kubwa lenye chupa tupu  za maji ambazo zilifika nusu ya gunia hilo. Kimtazamo tu kwa kumuangalia ungemjua kama ni muokota chupa tupu za plastiki kwa ajili ya kuziuza ili kujipatia kipato chake, alikuwa ni mzee aliyezoeleka hapo mtaani kwa kila mtu na hata kwenye nyumba za watu wenye uwezo  wa juu kifedha kutokana na kuwasaidia kupunguza uchafu wa chupa za plastiki majumbani mwao. Siku hii alipita kama kawaida yake katika nyumba mbalimbali iliajipatie chupa hizo kwa ajili ya kwenda kuuza, alipita katika nyumba tofauti na mwisho wake  akafika kwenye nyumba kubwa yenye ukimya mkubwa ndani yake. Alibonyeza kengele ya nyumba hiyo iliyopo getini mara moja na geti likafunguliwa na mlinzi wa nyumba hiyo ambaye alimtambua mzee huyo kwa kazi yake.
"anhaaa! Mzee Kitwisho shikamoo" Mlinzi alimchangamkia mzee huyo.
"marahaba kijana, vipi mzigo wangu upo tayari?" Mzee Kitwisho aliuliza.
"ndiyo mzee wangu upo tayari, pita pale karibu na bomba ukauchukue" Mlinzi alimwambia mzee Kitwisho huku akimfungulia mlango mdogo wa geti, mzee Kitwisho alienda kuchukua mzigo wake ambao ni rundo la chupa za maji zikiwa zimewekwa sehemu maalumu. Macho ya mzee huyu yalikuwa makini sana katika kuutazama mazingira ya nyumba hiyo huku akitembea kidhaifu kutokana na gunia alilolibeba mgongoni, alipofika jirani na bomba alichukua gunia jingine dogo lililosheheni chupa za maji huku mboni za macho yake yakiwa yanazunguka kutazama eneo lote la humo ndani.
"we can't kidnap him we have to find another way(hatuwezi kumteka tunatakiwa tutafute njia nyingine)" ilisikika sauti ya watu wakibishana ndani ya nyumba kisha mlango ukafunguliwa na wazungu wawili wakaonekana wakiwa wanatoka nje kwenye mlango unaotazamana na eneo ambalo bomba la maji lipo.
"who is this guy(huyu jamaa ni nani?)" Mmoja wa wale wazungu aliuliza.
"He is poor old  man who collects empty plastic bottles(ni mzee masikinj ambaye hukusanya chupa tupu za plastiki)" Mwenzake alijibu swali.
"how can you trust him like that, he is in our secret place(mtawezaje kumuamini kama hivi, yupo ndani ya sehemu yetu ya siri )" Yule mwenzake alilaumu.
"don't worry about him Christian, he doesn't understand any thing even our language(uaiwe na wasiwasi kuhusu yeye Christian, huwa haelewi chochote hata lugha yetu)" Yule mzungu alimtoa mwenzake wasiwasi kuhusu mzee Kitwisho, muda huo wazungu hawa wakiwa wanaongea mzee Kitwisho alionekana kutokuwa na habari nao kabisa kwani alikuwa akimalizia kushindilia chupa za plastiki kwenye gunia alilokuja nalo.
"muzee Twisho bari yako" Yule mzungu aliyekuwa akimtoa wasiwasi mwenzake alimsabahi mzee Kitwishi kwa kiswahili cha kubahatisha.
"salama tu Campbell, za asubuhi?" Mzee Kitwisho aliitikia salamu huku akinyanyua gunia lake akiwa anataka kuondoka.
"salama muzee haya  karibu tena" Campbel alimwambia Kitwisho aliyekuwa anaelekea getini.
"asante kijana" Mzee Kitwisho aliitikia salamu huku akitoka nje ya geti halafu mlinzi akafunga . Baada ya mlinzi kufunga geti  alipotoka nje mzee Kitwisho alitembea kwa mwendo hadi kwenye kibanda chake kilichopo katikati ya shamba maeneo hayohayo ya Bunju, aliweka mzigo nje kisha akaingia hadi ndani kwenye kibanda chake. Alipoingia tu ndani akakaribishwa na sauti iliyomuambia, "vipi mjomba umerudi salama?"
"salama tu mzee wangu" Mzee Kitwisho alijibu akiwa na sauti ya kijana tofauti na ya awali, aliufunga mlango kisha akaingia ndani ya chumba kidogo cha kibanda hicho. Huko alikutwa mzee mwingine aliyefanana kila kitu na mzee Kitwisho akiwa kajilaza kwenye kitanda, kimtazamo mtu wa kawaida atasema mapacha lakini haikuwa hivyo. Yule mzee Kitwisho aliyeingia ndani akitoka kuokota chupa aliishika sura yake kisha akaivuta na kupelekea sura hiyo ivulike kama nguo, ndani  ya sura hiyo ya bandia alionekana Norbert Kaila badala ya mzee Kitwisho wa awali.
"nadhani kazi yangu imeishia hapa mjomba" Mzee Kitwisho aliyekuwa ndani alimuambia Norbert huku akijiinua kitandani.
"hapana mjomba bado kazi ipo na nitakuwa nawe hapa ili niikamilishe kwani kazi haijaisha" Norbert aliongea huku akiketi jirani na mzee Kitwisho ambaye ni mjomba wake.
"sawa mjomba haina shida" Mzee Kitwisho alikubali.

****

Safari ya Moses iliishia kwenye hoteli ya Mangroove ambayo ni moja kati ya hoteli tano alizoachiwa na baba yake, akiwa na karatasi aliyoipata kwenye mkoba wa baba yake yenye ramani . Alienda moja kwa moja ndani ya hoteli hiyo kwa kutumia mlango ambao ulikuwa haujulikani na watu wa kawaida na kuufikia ilikuwa lazima utumie karatasi hiyo. Aliingia kwenye mlango huo kwa mujibu wa karatasi hiyo ambao ulimpeleka hadi sehemu yenye lifti ya kizamani ambayo hakuwahi kuiona tangu aanze kuingia ndani ya hoteli, karatasi hiyo ilimuelekeza apande lfti hiyo naye akati kisha akapanda lifti hiyo ambayo ilianza kushuka chini kwa kasi hadi sehemu yenye mataa ambayo yalijiwasha baada ya lifti hiyo kufika. Moses alishuka kwenye lifti kisha akafuata ukumbi mwembamba uliompeleka mpaka kwenye mlango ambao hauna kitasa zaidi ya sehemu ya kuweka alama za mkono. Moses aliweka kiganja cha mkono kama karatasi hiyo ilivyomtaka na mlango wa eneo hilo utoa kengele halafu ukafunguka.
"mmmh! Maajabu haya" Moses aliishia kuongea peke yake baada ya kuona mandhari uliyopo mbele yake.




ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment