Wednesday, December 23, 2015

SHUJAA SEHEMU YA KUMI NA TISA








RIWAYA: SHUJAA


MTUNZI: Hassan O Mambosasa

SIMU:+255713776843
+255762219759



WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE


SEHEMU YA KUMI NA TISA!!

Moses alishuka kwenye lifti kisha akafuata ukumbi mwembamba uliompeleka mpaka kwenye mlango ambao hauna kitasa zaidi ya sehemu ya kuweka alama za mkono. Moses aliweka kiganja cha mkono kama karatasi hiyo ilivyomtaka na mlango wa eneo hilo utoa kengele halafu ukafunguka.
"mmmh! Maajabu haya" Moses aliishia kuongea peke yake baada ya kuona mandhari uliyopo mbele yake.

****

Moses aliona maabara ya kisasa ikiwa ipo kwenye mazingira haya ya hoteli hii tena katika sehemu ambayo haijulikani na mtu mwingine yoyote, ilikuwa ni maabara yenye kila kitendea kazi cha kisasa zaidi kuliko hata maabara anayoitumia akiwa nyumbani kwao ambayo ina milango inayofungwa kwa vitasa tu. Maabara hii ya kisasa ilikuwa na milango inayofungwa na kufunguliwa na mashine tena yenye sehemu ya kuweka alama ya vidole kwenye mlango wa mkuu, Moses aliingia ndani ya maabara hiyo akiwa anashangaa mandhari yake na vifaa vya kisasa vilivyomo ndani yake. Ni mfano kati ya maabara bora alizowahi kuziona kwenye televisheni tu na hakuwahi kuziona kwingineko, vioo mbalimbali vya tarakilishi vilikuwa vipo humo ndani katika sehemu mbalimbali za maabara hiyo ambavyo ni mahsusi kwa ajili ya uchunguzi wa kisayansi utakaofanyika ndani ya maabara hiyo. Moses alijikuta akitembea huku akishangaa mazingira ya maabara  hadi katika mlango wenye maandishi yaliyosomeka PRIVATE, pembeni ya mlango huo aliona sehemu ya kuweka alama za kiganja cha mkono kama ilivyokuwa kwa mlango mkubwa wa kuingilia humo ndani. Moses aliutazama ule mlango kwa muda wa sekunde kadhaa kisha akaweka kiganja chake kama alivyofanya kwenye mlango mkubwa wa kuingia ndani ya maabara. Mlango ulifunguka kwa taratibu baada ya kengele maalum iliyopo mlangoni kulia, mandhari nyingine ya kuvutu ilionekana ikiwa imepambwa na taa zenye rangi ya kijani na kulifanya eneo hilo liwe na mwanga hafifu sana. Majokofu mbalimbali ya vioo yenye vitu mbalimbali vya maabara zikiwemo kemikali yalikuwa yamepangwa kwa mpangilio maalum wenye kuvutia, kila mbele ya jokofu kulikuwa na karatasi yenye kutoa maelezo na tahadhari juu ya kilichopo humo ndani. Moses alipata wasaa mwingine wa kujua kemikali mbalimbali za kisayansi ambazo alikuwa hazijui ingawa alikuwa mwanafunzi wa masomo ya sayansi, madhara mbalimbali ya kemikali hizo alizijua na akawa anachukua tahadhari kubwa sana kila anapopita. Majokofu kadhaa aliyapitia na mwishowe akafika kwenye kabati la vioo lenye  mlango unaofunguliwa kwa kutumia alama za mkono kama mlango mkuu wa kuingilia hapo, Moses alitaka kufungua mlango huo lakini akasita baada ya kuona faili lililochomekwa pembeni ya kabati hilo ambalo lilimvutia hadi akalichukua akalisoma. Faili hilo lilimfanya aweke katika kulisoma huku moyo wake ukimuenda mbio kwa kila alichokisoma kuhusu kabati hilo, alikuwa anasoma huku akiliangalia kabati hilo lenye vioo visivyoonesha nje. Baada ya kumaliza kulisoma faili hilo alilirudisha sehemu yake kisha akashusha pumzi ndefu halafu akaweka kiganja cha mkono katika eneo la kufungulia mlango huo kwa kutumia alama ya mkono, mlango wa kabati ulifunguka huku hewa ikitoka ndani ya kabati hilo na kengele maalum ikilia. Ndani ya kabati hilo Moses alikuta chupa mbili ndogo za vioo zenye vimiminika vyenye rangi tofauti, chupa moja ilikuwa na kimininika chenye rangi nyekundu na nyingine ilikuwa na kimininika chenye rangi ya kijani. Chupa moja iliandikwa maandishi yaliyosomeka 'DO NOT SHAKE THIS CONTAINER OTHERWISE  ROTAN VIRUS WILL BUST THIS CONTAINER(USITINGISHE HICHI CHOMBO VINGINEVYO VIRUSI ROTAN WATAPASUA CHOMBO HICHI), kwenye kasha la chupa hiyo kulikuwa na ala yenye kuonesha hatari. Chupa hiyo ilikuwa na kimiminikacha kijani ambacho Moses alikuwa na hofu nacho kila akikitazama, chupa ya pembeni yenye kimiminika chenye rangi nyekundu ilikuwa na maandishi yaliyoandikwa 'UNFINISHED WORK(KAZI ISIYOMALIZIWA))' . Moses aliichukua chupa hiyo kisha akafunga mlango wa kabati hilo kama alivyoukuta halafu akaendelea kuangalia maeneo mengine ya maabara hiyo, baada ya muda  alirudi pale kwenye eneo la kufanyia majaribio  akiwa na chupa kadhaa za kemikali.
"ikiwa baba yangu alishindwa kuikamilisha kazi hii basi mimi leo naikamilisha" Moses aliongea kwa ari huku akivaa koti mojawapo la kitabibu lilipo humo maabara, alivaa mipira mkononi pamoja na miwani maalum ya maabara kisha akachukua vitendea kazi na kazi akaianza mara moja.

****
   
 Muda wa kuondoka nyumbani ulipofika wanafunzi  wote wa shule ya sekondari ya Neema trust wasiokaa bweni waliondoka kurudi nyumbani kwao, Beatrice naye alikuwa miongoni mwa wanafunzi hao akiwa  pamoja na Irene na Hilary. Walitoka kwa pamoja hadi kwenye maegesho ya magari kwakuwa wote walipanga kuondoka kwa kutumia gari la alilokuja nalo Hilary, siku hiyo wote walipanga kwenda kwa akina Moses kumjulia ndiyo maana walitumia gari moja. Eneo la maegesho ya magari jirani na gari yao kulikuwa na gari aina ya landcruiser tatu zenye rangi nyeusi, walipokaribia gari yao milango ya land cruiser mojawapo ilifunguliwa na kijana aliyevaa suti nyeupe pamoja na kofia aina ya  Hat alionekana akishuka huku milango mingine ya gatri hilo ikifunguliwa. Wote kwa pamoja walisimama wakawa wanamuangalia kijana huyo aliyesimama na wapambe wawili wenye suti nyeusi, kijana huyo alivua kofia na kupelekea wote waione sura yake ambayo hawapendi kuiona.
"nyinyi mnaweza mkamsubiri Beatrice kwenye gari nahitaji kuongea naye peke yake" Kijana yule aliongea na kupelekea  Hilary na Irene waanze kuondoka,  Beatrice aliwazuia wasiondoke huku akisema "wakiondoka na mimi naondoka, unaweza kuongea hapahapa kama una maongezi na mimi na hawa wakiwa wapo. Andrew ongea shida yako sina muda wa kukaa hapa naenda kumuona my hubby". Maneno hayo yslimfanya Andrew ashushe pumzi huku akiangalia chini kutokana na kuumizwa nayo kuyasikia kutoka kwenye kinywa cha Beatrice, alihisi mwili wake ukianza kumchemka ghafla na dalili ya kutokwa na jasho ikawa inaonekana. Maneno ya kuongea yalimuisha hapohapo na akawa amebaki akiwa ameduwa kama kapigwa shoti ya umeme ya ghafla, alipowaangalia Hilary na Irene usoni aliona wazi wanamuonesha matabasamu ya kejeli.
"Hey! Don't waste my time(Hey! Usipoteze muda wangu) niambie kile kilichokufanya ujitutumue na hao wapambe wako mpaka unisimamishe njiani, hey naenda nyumbani kwa mpenzi wangu  sasa usinicheleweshe" Beatrice aliongea huku akiwa anamtazama Andrew kwa dharau.
"Shem tuwahi muda unaenda si unajua unahitajika kurudi nyumbani kwenu mapema" Hilary aliongea huku akimshika mkono Irene, Irene naye alimshika mkono Beatrice akawa anamvuta ili waondoke eneo hilo.
"You can't go like that(huwezi kuondoka kama hivyo) Beatrice" Andrew alitamka huku akiushika mkono  wa Beatrice kwa nguvu hadi akawa anamuumiza, Beatrice alitoa ukelele wa maumivu huku akiutoa mkono wake mwingine ulioshikwa na Irene.
"oyaa wacha ufala wewe usilazimishe mtu hataki wewe" Hilary alimpayukia Andrew kwa kitendo chake cha kuukamata mkono wa Beatrice kwa nguvu, Andrew aliendelea kung'ang'ania mkono wa Beatrice huku akimtazama Andrew kwa jicho la pembeni kutokana na tusi alilomtukana.
"we kenge kaa kim.." Andrew alitaka kumpa onyo Hilary lakini kofi zito la mkono wa kulia wa Beatrice lilitua kwenye shavu lake jirani na jicho, alijikuta akiuachia mkono wa Beatrice bila ya kupenda.
"you are bastard Andrew(wewe ni mwanaharamu Andrew) siku nyingine ujifunze kuwa usipopendwa hapakufai" Beatrice aliongea kwa hasira kisha akaondoka pamoja na wenzake kwenda kupanda gari la Hilary, hadi gari alilopanda Beatrice linaondoka Andrew aliendelea kubaki palepale akiwa amekumbwa na fadhaa ya ghafla kwa kofi alilopigwa. Aliwatazama wapambe aliokuja nao kisha akawaashiria waondoke, aliingia ndani ya gari akiwa ameinamisha kichwa chini kwa kitendo cha aibu kilichomkuta. Magari matatu ya msafara wake aliyoingia nayo hapo eneo la maegesho yaliondoka taratibu kuelekea getini kisha yakafuata njia ambayo Hilary  aliitumia.

****

Moses alifanikiwa kufika salama nyumbani kwao akitokea kule maabara , aliegesha gari kwenye eneo la maegesho. Alipojiandaa kushuka alisikia mlio wa gari nyingine ikija eneo la mapokezi hapo nyumbani kwao ambalo alilitambua kama ni la Hilary, Moses alishuka akiwa anatembea taratibu taratibu hadi kwenye mlango wa dereva  wa gari la Hilary akijua kaja mwenyewe. Milango ya gari mitatu ambapo miwili ya mbele na mmoja wa nyuma ilipofunguliwa ndipo alipotambua kama Hilary hakuja peke yake.
"wooow! My love" Sauti ya ilisikika kisha akaonekana Beatrice akishuka akienda upande aliopo Moses, Moses alighairi kwenda upande wa dereva na akamfuta alipo Beatrice akamkumbatia huku mvua ya mabusu ikishushwa kwenye papi za midomo ya Beatrice.
"unaendeleaje sweetie?!"Beatrice aliuliza.
"naendelea  vizuri baby  vipi za shule?" Moses alimuuliza Beatrice.
"safi tu, nimekumis sana mpenzi" Beatrice aliongea akiwa kamuegemea Moses.
"yaani hunishindi mimi mpenzi" Moses aliongea huku akimbusu Beatrice mdomoni.
"oyaa we mwanga yaani umeuona usingizi wako ila sisi hujatuona" Hilary aliropoka baada ya Moses kutumia muda mrefu akiwa anasalimiana na Beatrice bila ya kuwasilimia.
"aah! Wa wapi wewe, si unajua kabisa bila ya huu usingizi mimi sina amani so wacha niupate kwanza. Vipi mko poa lakini nyinyi lover birds" Moses aliongea kuwaambia Hilary na Irene kisha akawafuata akawasilimu wore wawili.
"mambo si hayo sasa, si kila muda umegandana na huo usingizi" Hilary aliongea kwa masihara na kupelekea wote wacheke.
"shem nawe una maneno wewe" Beatrice aliongea huku akicheka kutokana na maneno ya masihara ya Hilary, wakiwa wamesimama hapo getini kulianza kusikika mzozo kati ya mlinzi na watu asiowajua. Sauti ya geti kufunguliwa kwa nguvu ilisikika kisha milio ya matairi ya magari ikasikika ikija kwa kasi, gari tatu  aina ya land cruiser ambazo zilikuja shule ya Neema trust ziliingia hapo kwa kasi hadi jirani na eneo la maegesho walipokuwa wamesimama Moses, Beatrice, Hilary na Irene. Andrew alishuka kwenye gari iliyokuwa ipo mbele yao akiwa na alama ya vidole shavuni mwake, macho yake yalikuwa mekundu kama nyanya mbivu iliyoiva sana, magari yaliyosalia nayo yalishusha  watu kumi waliovaa suruali nyeusi na fulana nyeusi zilizowabana miili yao.
"nashkuru kwa kuniongoza hadi sehemu anayoiahi huyu mbwa"Andrew aliongea kimadharau huku akicheka kifedhuli.
"we koma we!  Mbwa mwenyewe mfuata vya watu" Beatrice aliongea kwa hasira.
"we unasemaje wewe?!" Andrew aliongea kwa hasira huku akimfuata Beatrice, alipomfikia alijaribu kumshika mkono na hapo akajikuta ameenda chini kama gogo baada ya Moses kuachia ngumi nzito iliyompata kwenye paji la uso.
"mbwa dada yake anaenitaka hadi akanitongoza" Moses aliongea kwa hasira huku mikono ikimtetemeka akimuangalia Andrew aliyeanguka chini baada ya ngumi yake kumpata sawia, Beatrice alibaki mdomo wazi kwa kusikia Annie alimtongoza Moses. Wapambe wa Andrew ambao wapo chini ya mshirika wake walipotaka kuingilia Andrew aliwazuia huku akisema, "hili ni pambano langu nyie kaeni pembeni namtandika mwenyewe. Mosea aliposikia hivyo hakujali hali yake na alimsogeza Beatrice nyuma ili akabiliane na Andrew, Beatrice alijikuta akimng'ang'ania ili aache kupigana lakini Moses alimtuliza kwa kumpa busu refu la kifaransa halafu akamwambia "usiwe na hofu juu yangu".  Busu hilo lilizidi kumuongeza hasira Andrew na akajikuta akitukana matusi mbalimbali ili asababishe Moses amuachie Beatrics, jambo hilo lilifanikiwa na Moses akamuacha Beatrice jirani na Hilary kisha akajiweka sawa kupigana na Andrew. Mpambano ulianza kwa Andrew kurusha ngumi mfululizo kutokana na hasira alizokuwa nazo huku matusi yakiwa yanamtoka mdomoni kwake mithili ya maji yanavyomwagika kwenye koki mbovu ya bomba, ngumi zote alizozirusha ziliishia kupiga hewa tu huku masumbwi mazito yakimshukia mfululizo kutoka kwa Moses. Ndani ya dakika tano uso wa Andrew ulikuwa umechafuka kwa damu na akawa hajiwezi hata kuinuka, Moses alimuongozea mateke ya mbavu hadi wapambe wa Andrew wakaingilia wakataka kumpiga.
"stop! Msimguse huyo atazilipia mwenyewe hizi damu zinazonitoka usoni.............Moses huu ni mwanzo tu na ukae ukijua umewasha moto utakaokuwakia mwenyewe" Andrew aliongea huku akinyanyuliwa kwa msaada  wa wapambe wake kupelekwa kwenye gari, aliingia ndani ya gari pamoja na wapambe halafu wakaondoka kwa kasi.
"mwana over Tyson vile maana umempa mabomba ya maana kama yule baunsa wa jana" Hilary alianza kuongea kwa masihara baada ya msafara wa Andrew kuondoka.
"halafu na wewe" Moses aliongea huku akimrushia ngumi ya kimasihara Hilary akiwa anacheka, Hilary alikimbia kuingia ndani na wote wakamfuata.

****

    BUNJU
  DAR ES SALAAM

Mlango wa geti la nyumba wanayoishi Scott na wenzake uligongwa badala ya kuminywa  kwa kengele iliyopo getini, mlinzi alipofungua alikutana na kijana wa makamo akiwa amevaa mavazi yanayomuonesha kwamba anaishi katika maisha duni sana. Mlinzi alipoiona sura ya kijana huyo alitabasamu kisha akamuambia, "kumbe ni wewe boya, niaje?".
"muzu, habari ni gani aisee?" Yule kijana alijibu kisha akaingia ndani.
"vipi hapo wapo?"Yule kijana aliuliza.
"yupo bosi Christian na Campbel tu, wengine wameenda town kuongea na Don" Mlinzi alimjibu na yule kijana akaingia ndani moja kwa moja kupitia mlango uliopo uani, alienda hadi sebuleni akawakuta Chiristian na Campbel wakiongea.
"ahaa! Boyka umekuja, mzigo upo tayari ne.." Christian aliongea kwa kiswahili  fasaha lakini alishindwa kumalizia baada ya kichwa chake kutobolewa na risasi, Campbel alishtuka na akakimbilia kutoa bastola lakini Boyka akaiwahi kwa kupiga risasi mkono alioshika bastola akatulia akiwa hana la kufanya.
"tulia hivyo usilete ujinga hata kidogo, twende mlipoweka mzigo" Boyka alimuambia Cambel huku akimpeleka hadi kwenye chumba  chenye mzigo mkubwa wa madawa ya kulevya, alitoa kamera na akamuamuru Campbel aupige  picha naye akatii amri.
"nani mkubwa wenu?" Boyka alimuuliza huku akimuelekezea bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti, Cambel alijifanya jeuri na akakaa kimya hakujibu na hapo ndipo Boyka aliyapiga risasi magoti yake yote. Kilichofuata hapo ilikuwa ni maumivu kwa Campbel kwani alivunjwa goti yote kwa kipigo kutoka kwa Boyka.
"hutaki kusema sio" Boyka alimuliza huku akiinyonga miguu ya Campbel iliyovunjika, Campbel alipoona kazidiwa alitoa kidani cha mkufu wake wa shingoni akanyonya kama pipi akafa hapohapo.
"Shit! Kajiua huyu" Boyka alisema kwa hasira kisha akaipekua maiti ya Campbel ambapo alikuta kadi ndogo ya kutunza kumbukumbu ya simu pamoja flash ya taratikilishi. Vyote alivichukua kisha akaondoka na mfuko mtupu wa kuwekea madawa ya kulevya hadi sebuleni, aliichukua tarakilishi ya mapakato aliyoikuta hapo sebuleni akaitia kwenye mfuko mtupu halafu akaondoka kama hajafanya tukio.



****


 Wakati Boyka ambaye ni msambazaji wa madawa wa kuaminika akiwamaliza wazungu wawili kati ya sita waliotumwa na Brian, nyumbani kwa akina Moses kulikuwa kuna mambo mengine kabisa. Baada ya wote kuingia ndani Hilary na Irene aliingia katika chumba cha wageni na Moses pamoja na Beatrice waliingia katika chumba cha kulala cha Moses, Beatrice aliingia kwa kusita na hatimaye akaingia moja kwa moja hadi kitandani akaketi. Moses alipoingia tu aliuficha ule mkoba wa baba yake aliondoka nao halafu akaenda kukaa kitandani na Beatrice.
"ooh! Joto sana" Beatrice aliongea huku akifungua vifungo vitatu vya shule na kusababisha sidiria laini aliyoivaa ndani ionekane, Moses alibaki akimuangalia Beatrice chini ya shingo hadi kifuani.





ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment