Saturday, December 12, 2015

SHUJAA SEHEMU YA NANE

RIWAYA: SHUJAA


MTUNZI: Hassan O Mambosasa


SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



ILIPOISHIA
"nafurahi kukufahamu" Norbert alimwambia Scott huku wakipeana mikono ,kitendo cha Norbert
kumuona Scott haikuwa mara ya kwanza. Alijaribu kuvuta picha ni wapi alipomuona lakini kumbukumbu zilikuja na kutoka, alipofikiria mara kwa mara ya pili ndipo kumbukumbu zake zilipompa jibu sahihi na
hapo ndipo akatambua mahali alipomuona Scott. Hakika alibaini ni mmoja wa watu aliowapiga picha
kule Biharamulo usiku wa kuamkia Ijumaa ingawa alikuwa ana muonekano tofauti, sasa hapo ndipo vita
ya maswali ilipoushambulia ubongo wake ingawa alionekana hakuwa na wazo lolote zito. Kiherehere
cha kutaka kupata majibu ya maswali yake kilishampanda na hapo alikuwa akisaka majibu kwa
kutumia dhana jambo lilimjia tofauri, alivyotambulishwa na ujio wa mtu huyo vilikuwa vitu viwili tofauti.



ENDELEA NAYO ILI KUPATA UHONDO ULIOMO NDANI YAKE


SEHEMU YA NANE!!
Hadi muda hamasa ya udodosaji wa undani wa Scott ndiyo iliyomfurukuta nafsini mwake, wazo la kuwepo uwezekano wa kuwa anaonana uso kwa uso na mtu mbaya ndio lilitawala akili yake kiasi kikubwa. Zote zilikuwa dhana tu juu ya Scott ambazo zilihitaji ushahidi wa kuzifanya vionekane ni ukweli ndani ya tarakilishi ya ubongo  wake, mawazo hayo yalitawala ubongo wake ndani ya sekunde kadhaa pasipo kujulikana na waliopo mbele yake kama yupo nje ya eneo hilo kimawazo.
"hivyo ofisa huyu nadhani ameingia siku..." Dkt Mbungu alijikuta akiwa haijui siku aliyoingia Scott  ndani ya nchi hii kutokana  na kutotajiwa na Scott na ikamlazimu  amuangalie mhusika kwa namna ya kutaka atajiwe.

"juzi na ndege ya shirika la Uswisi nikitokea likizo nyumbani Uswisi" Scott alimtajia akiwa anajiamini sana pasipo kuonesha chembe yoyote ya ubabaikaji, akili zake zilimwambia kuwa amefanikiwa kuwadanganya watu hao. Hakutambua kama alikuwa anadanganya mtu mmoja na mwingine hakuwa akimdanganya, akiwa kama hinadamu hakuweza kusoma mawazo yaliyomo katika ubongo wa binadamu yoyote. Ndio maana fikra zake zilimuambia kama alifanikiwa kudanganya kumbe alikuwa anajidanganya yeye mwenyewe.

"ndio bwana Scott nafurahi kuupata ujio wa mtu kama wewe kutoka kwenye asasi kubwa za kimataifa kama umoja wa mataifa hivyo titarajie mazuri katika safari yako ya kuja huku nchini kwetu" Norbert aliongea kwa kumuhadaa Scott huku Dkt Mbungu akitikisa kichwa kukubaliana na  maneno aliyoyaongea Norbert.

"ndiyo maana yake nafikiri itakuwa chachu ya taifa hili kuongeza juhudi za kupambana na wanasayansi haramu kupitia kazi yangu iliyonileta hapa Tanzania" Scott aliongea kwa namna ya kujivunia  kama amekujaTanzania kwa ajili ya kazi hiyo.

"sasa jamani mimi ninawahi sehemu mara moja, inabidi niondoke hivi sasa" Norbert aliongea huku akipeana mikono na Dkt Mbungu pamoja na Scott.

"haya bwana Kaila tuonane jumatatu ofisini kwa ajili ya kazi nyingine kuhusu mimea hii ukipata nafasi ya kufanya hivyo"  Dkt Mbungu alimwambia Norbert ambaye tayari alikuwa ameshaanza kuondoka. Nafsi ya Norbert muda huo ilimwambia anatakiwa kufanya jambo la upesi sana na jambo hilo litafanyika tu ikiwa atawahi kuondoka mapema kabla ya mgeni wa Dkt Mbungu hajaondoka, ndiyo maana aliaga kuwa anawahi sehemu jambo ambalo sio la ukweli. Kiherehere cha kudadisi mambo juu ya Scott ndio kilikuwa kikimchachafya katika mwili wake na ikamlazimu atangulie ili jambo analotaka kulifanya lisiharibike.



****


Usingizi ulimpaa mapema na ndoto alizokuwa akiziota juu ya  kipenzi cha moyo ambaye bado hajafsnikiwa kufangua naye ukurasa mpya zilipotea, alipofungua macho alikutana na miale ya jua ambayo imepenya kutoka kwenye  mwanya mdogo ulioachwa na pazia baada ya kutofunikwa vizuri. Moses aliulaani mwanga huo kwa kuingia ndani na pia aliilaani mpambazuko wa siku  hiyo mpya, aliinuka kisha akaenda kufunika vizuri pazia halafu akarejea kitandani na akajifunika tena shuka kama ilivyokuwa awali. Alifumba macho kisha akahamisha mawazo yote katika kuuvuta usingizi ambao uligoma kuja kutokana na mazoea yake ya kuamka mapema, lengo la kuuvuta usingizi huo kwa mara ya pili ilikuwa aweze kuota tena ndoto juu ya kipenzi cha moyo wake wanayependana. Hakika kupenda kwa mara ya kwanza kulimchanganya na kukamfanya awe kama mwendawazimu kutokana na kitendo cha kulala kwa lengo la kumuota Bratrice kwa mara ya pili, ni  mawazo ya kujenga nyumba  hewani ndoiyo yalimjia kutokana  na kutokuwepo wala kuwahi kutokea mtu kujipangia ndoto ya kuota pindi alalapo. Aliamua kuamka kisha akaenda kusafisha kinywa chake akiwa na ana tabasamu lisilofutika katika uso wake, alijikuta akiimba nyimbo mbalimbali za mapenzi za kingereza kila muda. Hali hii ilimshangaza sana mjomba wake baada ya kumuona maana haikuwa kawaida yake, udadisi wa kutaka kumuuliza kipi kinamsumbua ndio uliomvaa mjomba wake.
"anko kuna nini mbona leo tabasamu halikubanduki usoni" Kennedy alimuuliza Moses ili kubaini kinachomfanya mpwa wake huyo atabasamu muda wote.

"hamna kitu anko ni furaha ya kuiona siku nyingine ya mapumziko ya mwisho wa wiki" Moses aliamua kutumia uongo ili kuficha chimbuko ka furaha iliyomo nafsini mwake.

"mmh! Anko  inamaana tumeanza  kufichana siku hizi?" Kennedy alimuuliza Moses.

"hapana anko sijakuficha kitu chochote nina furaha ya kuiona siku ya mapumziko tu" Moses aliongea.

"Mmmh! Yote sawa basi, kapate kifungua kinywa kwanza" Kennedy alimwambia Moses kisha akaelekea chumbani kwake. Moses aliekea sehemu yenye ukumbi wa kula chakula kwa ajili ya kupata kifungua kinywa, alikuta kila kitu kimeandaliwa na kinamsubiri yeye ili aweze kuvitendea haki vitafunwa vya asubuhi hiyo.


****



Beatrice naye usingizi uliwahi kumuacha akiwa bado anauhitaji na alipoulazimisha bado uligoma kuja hivyo ikamlazimu kuamka kwani kulikuwa tayari kushapambazuka, aliinyoosha kivivu baada ya kuamka huku miayo ikiwa imetawala kinywa chake kisha akainuka kitandani hadi kwenye meza ndogo ya kuwekea vipodozi halafu akakaa kwenye stuli ndogo iliyopo kwenye meza hiyo yenye kioo kilichojengwa kisasa. Shajara yake ilikuwa ipo juu ya meza hiyo ya vipodozi ikiwa imefungwa kama akivyoiacha, hicho ndicho kitu cha kwanza alichoweza kukikumbuka asubuhi hiyo kuliko hata suala la kusafisha kinywa chake. Aliifungua Shajara hiyo hadi alipoibandika picha ndogo ya Moses kisha akaibusu huku akitabasamu, aliinyanyua Shajara hiyo kisha akaikumbatia. Ama kweli  penzi ni uchizi ukikuvaa  hautibiki kwa daktari yoyote yule mwenye   uzoefu wa kutibu magonjwa ya akili, tiba ya penzi ni kumpata yule aliyekuletea ugonjwa ili  awe tiba kwako na ukimkosa jua ndio itasababisha ugonjwa kabisa. Ndio hivyohivyo kwa binti huyu ambaye anasumbuliwa na ugonjwa huu na anahitaji dawa haraka iwezekanavyo  na dawa yenyewe ni chimbuko la ugonjwa huo yaani mtu aiesababisha akawa na hali hiyo, hakika Moses ndiyo tiba sahihi ya ugonjwa wake na anamuhitaji zaidi ya mgonjwa anavyomuhitaji daktari wa ugonjwa wake. Bado aliendelea kukaa kwenye kijistuli  kidogo kilichopo katika meza ndogo ya kuweka vipodozi  ambayo wenye lugha yao hii kila kukicha.huwa tunaipapatikia kuliko lugha yetu wanapenda kuita meza hiyo  kwa jina la 'Dressing table', tabasamu lisilokauka mithili ya chemchem itokanayo na mwamba uliopo ardhini ndio iliujaza uso wake na kumfanya aonekane mrembo zaidi.
"crazy lover hujambo" aliisikia sauti ya dada yake Victoria akimuita jina linakoendana na  jinsi alivyo.

"mmmh dada, sijambo"  Beatrice aliongea .

"yaani huyo mkaka atakutia wazimu kabisa huko unapoelekea" Victoria alimwambia.

"jana umesema nipo right kuwa hivi kwasababu ya huyu handsome boy, sasa leo mbona unaniambia atanitia wazimu?" Beatrice aliuliza kwa sauti iliyojaa deko.

"young sis tatizo umezidi au ni mara ya kwanza kupenda?" Victoria alimwambia huku akimfuata hadi kwenye meza hiyo ya kuwekea vipodozi halafu akamkumbatia kwa nyuma kisha akamwambia, "feelings juu yake zikikuzidi namna hiyo utafanya Dady ajue na iwe kama the thing happen to my first boyfriend".

"mmh! Unanitisha dada" Beatrice aliongea.

"sio kama nakutisha Dady ni mkali sana kuhusu hayo mambo nadhani unamkumbuka Allen my first boyfriend ambaye alilala nyuma ya nondo kisa kujulikana kwa uhusiano wangu na yeye " Victoria alimwambia  Beatrice.

"yeah! Namkumbuka dada" Beatrice alikubali kumkumbuka mtu aliyetajiwa na dada yake.

"you suppose to be careful otherwise utakuwa umemuingiza kijana wa watu matatizoni kama ilivyokuwa kwa Allen ambaye nampenda na nitaendelea kumpenda ingawa hayupo ndani ya nchi hii kutokana na  balaa la our Dady" Victoria alimwambia Beatrice huku machozi yakiwa yanamlenga katika macho yake, alisimama pembeni ya mdogo wake kisha akamwambia "napenda kuiona furaha yako mdogo wangu na sipendi kuiona huzuni yako katika siku hii ya leo ambayo ni ya furaha kwako sitaki yakupate kama yalinipata mimi, najua umemualika katika sherehe hii ya kuzaliwa kwako. Sasa basi kuwa makini ili  wapambe wa dady wasijue lolote kuhusu hisia zako juu yake, la si hivyo jua dady akirudi safari furaha yako itageuka shubiri".

"ok sis nimekuelewa please don't cry nitakuwa makini" Beatrica alimwambia dada yake kisha akainuka halafu akamkumbatia.

"usijali mdogo wangu, jiandae twende shoping kwa ajili ya sherehe jioni ya leo" Victoria alimwambia mdogo wake huku akifuta machozi yaliyoanza kumtoka alipokuwa akimkumbusha jambo lililotonesha kidonda chake cha kutenganishwa na mpenzi wake wa kwanza anayempenda  kuliko kitu chochote. Beatrice alimuachia dada yake kisha akaelekea katika mlango wa bafu lililopo humo chumbani mwake, aliingia ndani ya bafu hilo akimuacha dada yake akiwa akiwa yupo chumbani mwake.


****



Baada ya kutoka nyumbani kwa Dkt Mbungu  aliamua kufanya jambo ambalo hakutakiwa achelewe kulifanya, Norbett aliingia kwenye mgahawa uliopo jirani na nyumba ya Dkt Mbungu kisha akakaa katika kiti kilichopo mkabala na lango la nyumba hiyo kilichozibwa na maua yalipambwa pembeni ya mgahawa huo. Kiti hicho alichokaa ilikuwa ni rahisi kwa mtu wa ndani kumuona wa nje na vigumu kwa mtu wa nje kumuona wa ndani kutokana na maua yaliyozunguka mgahawa huo. Aliagiza kinywaji kisicho na kilevi ili kupoteza muda wa kuwepo eneo hilo, subira yake ndiyo aliyoihitaji ili kufanya jambo alilolikusudia kulifanya kwa muda huo na uvumilivu wa kusubiri muda muafaka wa kutekeleza jambo hilo ufike ndio kitu peke alichokilazimisha kiutawale moyo wake kwa muda huo. Wazo la kuegesha gari jirani na mgahawa huo ndio lilimfanya mpango wake huo uwe upo vizuri kwa kutotambulika kama alikuja na usafiri ndani ya nyumba hiyo, aliendelea kunywa kinywaji chake taratibu huku akili ikiwa ipo makini katika kuangalia lango kuu la kuingilia nyumbani kwa Dkt Mbungu. Wahenga wanasema subira huvuta heri na haraka haraka haina baraka, usemi huo ulijidhihirisha wazi kutokana na subira aliyoiweka Norbert katika kusubiri muda mahususi wa kufanya kazi yake kwani subira yake ilizaa matunda baada ya gari aina ya range rover yenye rangi ya fedha ilipotoka ndani ya nyumba ya Dkt Mbungu ikiwa na dereva mwenye asili ya kiafrika na mzungu aliyekaa kiti kilichopo pembeni ya dereva. Upeo mkali wa macho ya Norbert uliweza kumtambua mzungu huyo ambaye ndiye aliyekuwa amefanya akae katika mgahawa huo, sasa alihitaji jambo ambalo alilipanga kulifanya na ikamlazimu kusubiri hapo mgahawani. Kinywaji chake alikiona hakina maana tena zaidi ya kufanya jambo lilimuweka hapo, alisubiri gari hilo lilipoondoka kwa umbali wa mita kadhaa kisha akalipa kinywaji chake halafu akaenda hadi alipoegesha gari yake.  Aliingia kwa haraka kisha akaliwasha halafu akaliingiza barabarani kufuata uelekeo ambao ile range rover imepita kwa mwendo wa kasi, baada ya mwendo mfupi aliikuta ikiwa ipo katika mwendo wa kasi baada ya barabara ya eneo la Msasani kuwa tupu.









ITAENDELEA!!


RUKSA KUSHARE RIWAYA HII KOKOTE UPENDAPO, ILA USINAKILIA KWA NAMNA YEYTE ILE BILA RIDHAA YA MTUNZI

No comments:

Post a Comment